Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Mtu Adimu Kupatikana Katika Jamii Yako.

$
0
0
Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri katika maisha yako. Hongera kwa siku hii nzuri sana katika maisha yako, kwani ni zawadi ya kipekee sana ambayo ukiitumia vizuri itakuletea mafanikio makubwa sana katika maisha yako.
 

Ndugu mpendwa, nipende kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia katika darasa letu la leo. Hivyo basi, nakusihi sana tuweze kusafiri kimawazo hadi pale tamati ya kipindi chetu cha leo, hivyo karibu sana ndugu msomaji wangu.

Rafiki, katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza mtu adimu kupatikana katika jamii yako. Kwanini nasema mtu adimu kupatikana katika jamii yako? Kwa sababu siyo mtu wa kawaida ndiyo nasema adimu yaani kupatikana kwake ni shida. Kitu chochote ambacho kinakuwa adimu kupatikana basi kina thamani kubwa ndiyo maana siyo rahisi kupatikana kila wakati au kirahisi.

Kama unasoma mtandao huu kila siku, basi hapana shaka kuwa umeshakutana na makala nyingi zinazohusiana na muda au wakati. Muda ndiyo kila kitu katika maisha yetu ndiyo unatibu na kutupatia yale tunayoyafanya au tunayotazamia kuyafanya kila siku. Kumbe basi, muda ndiyo rasilimali muhimu sana katika maisha ya muda kwani hata siku zetu za kuishi hapa duniani ziko katika muda siku yako ikifika utaondoka ndiyo maana huwa ninasisitiza kila siku napo kuwa naandika makala hapa Amka Mtanzania lakini pia katika mtandao wa Kessy Deo.

SOMA; Hivi Ndivyo Vitu Vinavyo Kupotezea Muda Sana Katika Maisha Yako.

Ni kawaida katika jamii kutojua thamani ya muda na kama hujajitambua huwezi kuona kama muda ndiyo una thamani sana lakini kuna wengine wanaona pesa ndiyo ina thamani zaidi kuliko muda. Kama huna muda ni wazi kabisa huwezi kupata pesa na tunafundishwa kila siku kuwa ukipoteza muda huwezi kuupata lakini ukipoteza pesa unaweza kuitafuta. Mtu anayetambua thamani ya muda kamwe hawezi kuchezea muda wake hata kidogo.

Ndugu msomaji, baada ya utangulizi huo hapo juu sasa tuangalie nini shabaha au lengo letu la leo kupitia makala hii? Jibu ni kwamba tunataka kumjua mtu adimu kupatikana katika jamii yetu ni yupi? Huenda unajiuliza je katika jamii yangu hivi kuna mtu adimu kupatikana? Na kama yupo je ni mtu wa namna gani? Karibu sasa uweze kupata jawabu lako kupitia darasa hili.

Mpenzi msomaji, mtu adimu kupatikana katika jamii yako siyo mtu mwingine bali ni bahili wa muda. Ndiyo, mtu adimu kupatikana katika jamii yako basi ni bahili wa muda kwani umeshawahi kusikia watu ni mabahili kweli wa hela lakini hata siku moja kusikia mtu ni bahili wa muda ni adimu sana katika jamii yako. Au jiulize tokea unakuwa umeshawahi kusikia watu hawa au mtu ni bahili kweli wa muda? Lakini bahili wa hela umelisikia sana katika maisha yako.

SOMA; Sehemu 7 Ambazo Unatumia Kupoteza Rasilimali Muda Wako

Watu wengi wamekuwa ni watu wanaouza sana muda wao bila wao wenyewe kujua, mtu yuko radhi utumie hata masaa mawili lakini siyo pesa yake, anaweza kuwa bahili kweli wa pesa lakini kwenye muda mtumie vile unavyoweza. Mtu anayejua thamani ya muda lazima awe bahili wa muda kwani anajua fika muda ndiyo unazalisha pesa atakayo na wala si vinginevyo. Unatakiwa kuwa bahili wa muda kweli kweli kuliko maelezo, usikubali kupatikana kirahisi katika maisha yao kwani kupatikana kirahishi ni sawa sawa na bidhaa ambayo haina thamani.

Mpendwa rafiki, tunatakiwa sasa tubadilishe nadharia iliyozoeleka katika jamii yetu ya kuwa tu mabahili wa pesa badala yake tuwe mahili wa muda. Hata mabilioni ya Bill Gates hayawezi kununua hata dakika moja ya muda, kwahiyo, muda ni kitu cha thamani sana katika maisha yetu. Unatakiwa kuwa bahili sana wa muda wako, bora watu wakuone mbaya lakini utumie muda wako vizuri kwani kuna watu wengine bado hawajatambua thamani yao au kusudi la maisha yao hapa duniani.

Watu wanasau kuwa hata maisha yetu ni muda jinsi unavyotumia muda wako ndivyo unavyoishi kwahiyo kila siku unatakiwa kuishi vizuri yaani utumie muda wako vizuri vilivyo. 

Usikubali mtu aje akupotezee muda wako kwa habari hasi ambazo hazikusaidii kitu katika maisha yako. Unatakiwa kuwa mtu wa kusema hapana ili muda wako utumie vizuri kwani kuna vitu vingi vya kusema hapana vinavyokula muda wako.

Hatua ya kuchukua leo, ukitaka kuwa mtu adimu katika jamii yako basi kuwa bahili wa muda. Usikubali kuwa mtu wa ndiyo kwenye kila jambo kwani itakusababishia kula muda wako. Watu ambao ni bahili wa muda huwa ni watu makini sana na wenye thamani kubwa. 

Ukitaka kuwa na thamani kuwa bahili wa muda.

Mwisho, tunaalikwa kuwa bahili wa muda katika maisha yetu kwani ni watu ambao wamekuwa adimu sana kupatikana katika karni hii ya ishirini na moja. Ukiwa na nidhamu ya kutawala muda wako utaokoa vitu vingi kwenye maisha yako.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kujifunza kila siku. Asante sana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>