Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Sheria Sita (6) Za Mafanikio Ambazo Watu Wa Mafanikio Wanazitumia Sana.

$
0
0
Kuishi maisha ya mafanikio sio ajali. Zipo taratibu na kanuni ambazo karibu watu wote wenye mafanikio wanazitumia kanuni au sheria hizo hadi kuweza kufikia mafanikio makubwa karibu kila wakati.
Ukifatilia kwa makini watu wenye mafanikio wanaishi kwa sheria. Je, unajua sheria hizo ni zipi? Hebu twende kwa pamoja tujifunze baadhi ya sheria ambazo zinatumiwa sana na watu wa mafanikio.
1. Kufanya kwa ubora.
Watu wenye mafanikio kwa chochorte wanachokifanya wamechagua kufanya kwa ubora kila siku. Hakuna ambacho wanachokifanya mikononi mwao halafu wakachagua kulipua au kukifanya hovyo.
Hii ni sheria ambayo wanaitumia sana karibu katika maisha yao yote. Chochote wanachokifanya hata ikiwa ndio kwa mara ya kwanz, huamua  kukifanya kwa ubora zaidi ili kuweza kuhakikisha ndoto zao zinatimia.

Zijue vyema sheria za mafanikio ili ufanikiwe.
2. Kusikiliza kwa makini.
Watu wenye mafanikio hawaishii tu kufanya kwa ubora, bali pia huwa makini sana na kusikiliza wengine wanasema nini juu ya kile wanachoambiwa na kuamua kukitekeleza kwa ufasaha.
Watu wenye mafanikio wao wanaona bila kufanya hivyo kuna mambo mengi ambayo watakuwa wanakwenda nayo kinyume na mwisho wa siku watashindwa kutimiza malengo yale waliyokusudia.
3. Kutokuogopa kitu.
Sheria nyingine ambayo watu wenye mafanikio wanaishi nayo ni kule kutokuchagua kuogopa kitu. Mara nyingi ni watu wasiogopa kitu, utashangaa wanafanya jambo hili au lile bila wasiwasi.
Kutokana na ujasiri huu ndio unaowafanya waweze kufanya mambo mengi na hatimae kuweza kufanikiwa kwa viwango va juu. Kwa hiyo kutokuogopa wanaitumia ni kama sheria ya kuwasaidia kufanikiwa.
4. Kuwa na malengo makubwa.
Maisha ya watu wenye mafanikio yapo kwenye karatasi. Ninaposema maisha yao yapo kwenye karatasi nikiwa na maana kwamba ni watu wa kuishi kwa malengo, ni watu wa kuishi kwa mipango.
Kwa sababu mara nyingi wanakuwa ni watu wa malengo hiyo huwavuta na kuwapa nguvu na hamasa ya kufikia mafanikio yao. Kwa sababu kila siku wanakuwa wana kitu ambacho wanakifatilia mpaka kuweza kutimia.
5. Kuweka vipaumbele.
Huwezi kupata mafanikio, kama hauna vipaumble ulivyojiwekea. Watu wenye mafanikio wanaishi kwenye sheria hii ya kujiwewekea vipaumbele karibu kwenye maisha yao yote. Hakuna amabacho hawaweki vipaumbele.
Ni watu ambao wanachagua jambo moja na kuamua kulifanya na kulipa uzito wa hali ya juu sana hadi kuweza kufanikiwa. Ni sheria ambayo inafanya kazi vyema hata leo hii ukiaamua na wewe kuitumia itakufanikisha.
6. Kufanya maisha ya wengine kuwa bora pia.
Watu wenye mafanikio, si tu wanakazana kufanya maisha yao yawe bora, ila pia hujitahidi sana kufanya na maisha ya wengine yawe bora. Hutoa kila wanachoweza ili kuwasaidia wengine pia.
Ukichunguza, utagundua haya ndiyo maisha yao. Ni watu wakusaidia watu, na kwa sababu ya sheria hiyo wanayoitumia sana mwisho wa siku na hata wao wenyewe hujikuta wapo kwenye mafanikio makubwa.
Kwa kuzitumia sheria hizo na kuamua kuzifanyia kazi, ni njia mojawapo bora ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Kwa makala nyingine nzuri za maisha na mafanikio, tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kuweza kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,



Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles