Kushindwa Unapoiga.
Tumekuwa tunaona kila mara, mtu anaanzisha kitu, anakuja na ubunifu wa tofauti, na tunaona ni kitu kizuri. Ghafla wengi wanaiga ubunifu ule, lakini wengi wanaishia njiani. Pamoja na wengi kuiga na kuonekana kuna ushindani mkali, bado wale walioanzisha huwa wanadumu na wale wanaoiga wanapotea kabisa.
Swali kubwa ambalo wengi wamekuwa wanajiuliza ni kwa nini wengi wanaoiga huwa hawafanikiwi?
Na kwa wale wanaoiga kuna kitu ambacho huwa wanakiona na kinawashangaza. Wakati unawaona wengine wanafanya, ulikuwa unafurahia na kuona ni kitu kizuri. Lakini unapokuja kufanya wewe, hufurahii na ule uzuri huuoni tena. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa kuelewa nini kinasababisha haya.
Leo kupitia makala hii nakwenda kukuonesha kwa nini wanaoiga huwa hawafanikiwi na ufanye nini kufanikiwa kama inabidi uige.
Kwa nini wanaoiga huwa hawafanikiwi?
SOMA; Sometimes You Win, Sometimes You Learn. (Somo Kubwa Unaloweza Kujifunza UCHAMBUZI Kupitia Makosa Yako).
Siyo kila kitu unachoona wengi wanafanya na ukafurahia, wewe ukifanya pia utafurahia. Hili ndiyo kosa kubwa sana ambalo wengi wamekuwa wakifanya na kuishia kuanguka pale wanapoiga. Wanachofurahia wengine, na hata wanachoweza kufanya vizuri, siyo uhakika kwamba na wewe unaweza kufurahia na kufanya vizuri.
Kosa jingine kubwa watu wanafanya ni kufikiri kwa sababu watu wanafanya kitu basi wanakifurahia muda wote, au kila siku kwao ni mafanikio. Hivyo wanapoiga kwa mtazamo huo, na kuanza kufanya, wanakutana na uhalisia kwamba kuna ugumu na changamoto kubwa, ndipo wanaposhindwa kuendelea na kuacha.
Katika kitu chochote ambacho unafanya, siku ya kwanza huwa siku ya furaha, kwa sababu unafanya kitu kipya, ambacho una matumaini makubwa kitaleta matokeo bora. Kadiri siku zinavyokwenda ile hamasa ya mwanzo huwa inapotea na uhalisia wa kitu unaanza kuonekana, ugumu unaanza kuonekana na changamoto zinaanza kujitokeza. Hapa ndipo wale waliojitoa kweli kufanya wanaendelea kufanya, wakati wale walioiga juu juu tu wanashindwa kuendelea.
Hawakujua kumbe ndani mambo yanaweza kuwa magumu kiasi kile.
SOMA; Unawezaje Kuepuka Hofu Ya Kushindwa Unapotaka Kufanya Jambo Jipya?
Siyo kila unayemwona anafanya kitu kwa kufurahia anapata matokeo mazuri muda wote, wengi wanafurahia kwa sababu ndiyo kitu wamechagua kufanya. Wanajua ni mchango gani wanatoa kwa wengine, na zile changamoto wanazopitia ndiyo zinawahamasisha zaidi.
Hivyo, kuangalia jambo lolote kwa nje, na kulipenda kisha kuingia kufanya, ni njia ya uhakika ya kwenda kushindwa, kwa sababu yapo mengi ya ndani ambayo huwezi kuyajua mpaka utakapoingia kufanya.
Je unawezaje kufanikiwa kwa kitu cha kuiga?
Japo ni vigumu lakini inawezekana, kama umejitoa kweli na unataka kufanikiwa.
Kwanza amua kukomaa mpaka pale utakapofanikiwa. Unapoona wengine wanafanya, na kuvutiwa kufanya, usifikirie kwamba ni rahisi na njia ya haraka ya kufanikiwa. Jua kwamba zipo changamoto kubwa utakazokutana nazo, utakwama, utakutana na matatizo. Lazima uweze kuvuka yote hayo kama kweli unataka kufanikiwa. Tofauti na hapo hutaweza kufika mbali, kwa sababu mambo siyo rahisi kama yanavyoonekana kwa nje.
Pili, jipe sababu kuu ya kwa nini unafanya. Licha ya kuona kwa nje wengine wanafanya, jipe sababu kuu kwa nini unafanya. Angalia ni mchango gani unatoa kwa wengine, angalia ni namna gani inakusukuma wewe mbele. Unapokuwa na sababu kubwa ya kufanya, unasukumwa kufanya zaidi kuliko kukosa sababu. Unapokaribia kukata tamaa, ukikumbuka ile sababu kubwa, unapata nguvu ya kuendelea kufanya. Sababu itakupa nguvu hata pale unapoona mambo hayawezekani tena.
SOMA; Hizi Ndizo Aina Tatu (3) Za Kushindwa Katika Maisha Na Kazi.
Tatu, tengeneza maono makubwa kwa kile unachofanya. Hata kama umeiga kwa kuona nje, kaa chini na tengeneza maono yako. Angalia utakuwa wapi miaka mingi ijayo kupitia kile unachofanya. Usiishie tu kuangalia leo unafanya nini, bali angalia miaka mitano, kumi, ishirini na hata hamsini ijayo utakuwa wapi. Kadiri unavyoona mbali, ndivyo unavyokuwa tayari kupambana hata kama mambo ni magumu. Kwa sababu haijalishi leo ni ngumu kiasi gani, kesho inakuwa na mwanga zaidi kama utakuwa na maono.
Nne, endelea kuboresha zaidi. Tatizo la wengi wanaoiga ni kwamba wanaiga kila kitu halafu hakuna chochote wanaboresha au kubadili. Kwa namna hii safari inakuwa ngumu kwao kwa sababu mengi wanayofanya hawayajui vizuri. Unapoiga kitu, angalia namna ya kukiboresha zaidi ili kiendane na hali yako wewe. Na kila siku endelea kuboresha, endelea kujifunza zaidi na endelea kujaribu mambo mapya, hayo yatakuwezesha kujitofautisha na wale ambao umewaiga.
Hayo ni mambo muhimu kabisa ambayo unahitaji kuyazingatia iwapo utaiga kile ambacho umependa wengine wanavyofanya. Kamwe usibebwe na mwonekano wa nje na kushindwa kuona changamoto za ndani. Chochote unachoamua kufanya, jua changamoto utakutana nazo nyingi. Jiandae kupambana nazo, kuwa na sababu ya kufanya na tengeneza maono makubwa ya wapi unataka kufika. Kila siku weka juhudi na endelea kuwa bora zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.