Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Mambo Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawafanyi Tena Kwenye Maisha Yao

$
0
0
Kwa kawaida tunapotaka kufanya jambo fulani la kimafanikio kwa wengi wetu huwa tuna tabia ya kuangalia hasa watu wenye mafanikio ni kitu gani ambacho walikifanya hadi kufikia mafanikio hayo. Kwa lugha rahisi tunakuwa tunahamasika sana kwa kuona yale mambo ambayo watu wenye mafanikio waliyafanya na hadi kufanikiwa.
Leo nataka nikubadilishe mtazamo kidogo. Ni hivi, pamoja na mazuri mengi ambayo watu wenye mafanikio wanayafanya, lakini pia wanafanya makosa. Tofauti kubwa inayojitokeza ni kwamba wao wanajifunza sana kutokana na makosa yao na hawafanyi tena makosa hayo. Watu hawa wenye mafanikio hawakati tamaa wakikosea, ila hawarudii makosa yao.
Unaweza ukajifunza sana pia kupitia mambo ambayo watu wenye mafanikio hawayafanyi tena katika maisha yao mara baada ya kufanya makosa hayo kwa mara kwanza. Yafuatayo ni mambo  ambayo watu wenye mafanikio hawafanyi tena.
1 – Kubadilika kwa sababu ya wengine
Watu wenye mafanikio ni watu ambao hawana kasumba hii. Ni watu ambao hawabadilishwi kwa sababu ya watu fulani wamesema hivi au wamesema vile juu ya maisha yao. Kila wakati ni watu wanaoamini kile wanachokijua kwamba ndicho kinawasidia.
Kuna wakati Steve Jobs mwanzilishi wa kampuni ya ‘apple’ alitaniwa sana na wachora katuni kwa sababu ya kuvaa nguo za aina moja kwa muda mrefu. Hilo halikumshtua Stebve Jobs na aliendelea na maisa yake. Mara nyingi watu wenye mafanikio ndivyo walivyo, hawaendeshwi na upepo.
.2 – Kukaa kwenye uhusiano mbovu
Haijalishi ni uhusianao wa kimapenzi au uhusuiano wa kibiashara lakini watu wenye mafanikio hawafanyi kosa la kuendelea kukaa kwenye uhusiano mbovu au uhusiano ambao hauwasaidiii kuweza kupiga hatua za kimafanikio.
Hebe jiulize ni mara ngapi watu wengi hujikuta tupo kwenye uhusiano ambao hauna mbele wala nyuma eti kwa sababu ni jamaa zetu. Lakini watu wenye mafanikio hawawezi kuendekeza hilo. Kila aina ya uhusiano mbovu hawawezi kuendelea nao maana utawarudisha nyuma.
3 – Kuamini wengine ni bora kuliko wewe
Mara nyingi ni kama asili ya binadamu kuweza kuamini kwamba watu wengine wanaweza wakawa bora kuliko wewe.  Watu wenye mafanikio hawafanyi kosa sana la kuweza kuamini kwamba wengine ndio bora kuliko wao. Kila wakati wanaamini sana ule ubora ulio ndani mwao.
Kwa msingi huo wa kuamini ubora uliondani mwao hujikuta wakifanya mambo yao kwa kjiamini sana na mwisho wa siku hujikuta wakifikia mafanikio makubwa sana ambayo wengi hawawezi kuyafikia kiurahisi.
4 – Kuacha kuweka malengo ya muda mrefu.
Karibia watu watu wote wenye mafanikio wanaelewa umuhimu wa kuweka malengo ya muda mrefu ili kufikia mafanikio yao. Ni watu ambao wanakuwa makini sana na hawapotezwi na kujiwekea malengo ya muda mfupi tu peke yake ambayo yanakuwa mchango mkubwa kwa malengo ya muda mrefu.
Kwa hiyo katika hili watu wenye mafanikio ukiangalia utaratibu wao wa kujiwekea malengo wanayo ratiba ya kujiwekea malengo ya muda mrefu ambayo kiuhalisia huwafikisha katika mafanikio makubwa ambapo kama wasingeweza kuweka wasingefika mbali sana kimafanikio.
5 – Kushindwa kuweka malengo
Si kitu cha ajabu kuona watu ambao hawana mafanikio kushindwa kuweka malengo ya kimafanikio. Watu wenye nia ya mafanikio siku zote wanaaangalia mbele na kwa msingi huo malengo yao ni lazima wanakuwa wanayaweka na hadi kuyafanikisha.
Watu hawa wanakuwa wanajua ni kipi wafanye wapi na wakati gani na pia wanakuwa wanajua hakuna mafanikio ambayo yanaweza kupatikana kama hakuna malengo yoyote ambayo yamewekwa. Hivyo malengo kwao ni lazima na hawafanyi kosa la kutojiwekea malengo au kujua kule wanakotaka kufika.
 6 – Kuipoteza hamasa
Watu wenye mafanikio  wanajua sana kwamba siri mojawapo pekee ya kukufikisha kwenye mafanikio ni muhimu sana kwa wewe kuwa na hamasa karibu kila siku. Wanatambua hamasa ndio kichocheo kimojawapo kikubwa ambacho kinaweza kukufikisha kwenye mafanikio.
Kwa kulijua hilo wanahakikisha kila siku ndani mwao wanakuwa wanahamasa kubwa ambayo inawasukuma kufanya na kufanya tena hadi kufikia mafaniki yao. Wanajua bila hamasa hakuna mafanikio makubwa ambayo yanaweza kupatikana.
Kwa kuangalia kwa haraka haraka hayo ndiyo mambo ambayo karibu watu wengi wenye mafanikio hawafanyi tena kwenye maisha yao.
Kwa makala nyingine za mafanikio, endelea kujifunza pia kupitia DIRA YA MAFANIKIOkila siku.
Tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>