Habari rafiki yangu?
Kama unaangalia hapa, najua unatumia mtandao wa intaneti na unatumia mitandao ya kijamii. Najua upo kwenye makundi mbalimbali kwenye mitandao hii, pengine unajifunza, pengine hakuna unachojifunza. Huenda kuna manufaa umeyapata mpaka sasa, au huenda unalalamika kwamba inakupotezea muda lakini huwezi kuachana nayo.
Mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, ni fursa mpya na ya kipekee ambayo tunakutana nayo sasa. Ni vitu ambavyo havikuwepo kwa siku nyingi, hivyo wengi ndiyo tunakutana nayo sasa na kuanza kuitumia. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna mtu anayetufundisha matumizi sahihi ya mitandao hii. Sisi tunapata vifaa na kuanza kuitumia.
Kutokana na ukosefu huu wa elimu sahihi, watu wamekuwa wanafanya mambo ya ajabu sana kwenye mitandao hii. Wamekuwa wanapoteza muda kufuatilia mambo ya wengine. Wapo ambao wamekuwa wanazusha mambo yasiyo ya kweli, na wengine wanayasambaza bila ya kujua kama ni ukweli au la.
Ukiacha tu matumizi ya kawaida, nakuja na swali kwako, je katika matumizi haya ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, umewahi kulipwa na yeyote? Je umewahi kufanya chochote kupitia mitandao hii na mtu akakulipa? Kama jibu ni hapana, basi unapoteza fursa nzuri mno kwako. Unayo nafasi nzuri ya kulipwa kupitia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii.
Kwenye somo la leo nimezungumzia matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. Nimekushirikisha mambo matatu muhimu ya kuzingatia kwenye matumizi yako ya mitandao ya kijamii ili uweze kunufaika sana. Chukua muda wako na angalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya, ili uweze kujua matumizi sahihi ya mtandao wa intaneti.
Kama kifaa chako kinaruhusu, unaweza kuliangalia somo hilo hapo chini.
Kama hulioni basi bonyeza maandishi haya na utakwenda moja kwa moja kuangalia.
Jifunze matumizi sahihi ya mtandao wa intaneti na kisha anza kuitumia kwa usahihi. Unaweza kuanzisha na kukuza biashara yako kwenye mitandao hii, au pia kukuza biashara yako uliyonayo sasa kupitia mitandao hii.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.