Habari za leo rafiki yangu?
Kila mtu anapenda kufanikiwa, mafanikio ni kitu ambacho kinazungumzwa na kutamaniwa na wengi, lakini wachache sana ndiyo wanaoweza kuyafikia mafanikio. Licha ya wengi kupenda, wachache ndiyo wanayapata hasa yale mafanikio wanayotaka.
Hapa ndipo watu wanashawishika kwamba huenda kuna watu wana bahati ya mafanikio kuliko wengine. Au wapo watu ambao walizaliwa kufanikiwa na wengine walizaliwa ili wawepo tu.
Mimi nimekuwa nakataa hilo mara zote, kwa sababu kila siku naona tofauti kubwa iliyopo kati ya wale wanaofanikiwa na wale wanaoendelea kuwa kawaida.
Mafanikio siyo ajali, wala mafanikio siyo bahati, wala hakuna wachache ambao wamezaliwa ili kufanikiwa na wengi kuendelea kuhangaika na maisha ya kawaida tu. Mafanikio yapo wazi kwa kila mtu na mafanikio yanakwenda kwa wale ambao hawaishii kusema tu, bali wanayafanyia kazi.
Iko hivi, kama wanavyosema waswahili, unavuna ulichopanga, kwamba ukipanda maharage, kamwe usitarajie kuvuna mahindi. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio, yapo mambo ambayo ukiyafanya, yanakupeleka moja kwa moja kwenye mafanikio.
Mambo hayo yanaanza na nidhamu. Sijawahi kuona mtu aliyefanikiwa ambaye hana nidhamu. Nidhamu ni kiungo muhimu mno cha mafanikio, bila nidhamu hakuna mafanikio.
Leo nakwenda kukushirikisha nidhamu tatu muhimu unazohitaji kuwa nazo ili uweze kufanikiwa. Hivi ni nidhamu muhimu sana kwa kila mtu aliye makini na mafanikio kujiengea ili aweze kufanikiwa.
Angalia video ya kipindi cha leo, nimekushirikisha nidhamu hizi tatu na jinsi ya kuweza kujijengea hatua kwa hatua. Angalia, jifunze na chukua hatua.
Unaweza kuangalia video hiyo moja kwa moja hapo chini;
Na kama huoni video hiyo hapo, basi bonyeza maandishi haya kuiangalia video hii muhimu sana kwa mafanikio.
Nikuambie tu rafiki, kama unataka kuvuna mahindi, usijisumbue kupanda maharage. Hivyo kama unataka kufanikiwa, usiendelee kufanya yale ambayo watu wasiofanikiwa wanafanya, bali fanya yale watu waliofanikiwa wanafanya. Anza na nidhamu hizi tatu muhimu sana, zitakufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Usikose kuangalia video ya somo hili la nidhamu tatu muhimu, bonyeza maandishi haya kuangalia somo hili muhimu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.