Habari za leo rafiki yangu?
Hongera sana kwa kuendelea kuwa msomaji wa makala hizi ninazoandika, ninaamini kipo kitu ambacho unapata ndiyo maana mpaka sasa tupo pamoja. Ingekuwa hakuna unachopata, nina imani kabisa usingeendelea kupoteza muda wako kusoma makala hizi. Nasema asante na karibu sana tuendelee kuwa pamoja.
Leo nina ujumbe mfupi sana kwako, na nataka nikuambie wazi ya kwamba kazi yangu kubwa niliyochagua ni wewe. Ndiyo namaanisha wewe hapo ndiyo kazi yangu. Nimechagua kukushirikisha kila ninachojua, ninachojifunza na nilichopaya uzoefu nacho kupitia maisha ya kila siku. Nikiamini kuna thamani kubwa ambayo utaweza kuipata kupitia haya ninayokushirikisha.
Nimechagua kuandika na kukushirikisha maarifa kila siku ya maisha yangu. Kama tu ninaendelea kupumua basi nitahakikisha kuna kitu kizuri unapata kutoka kwangu. Hivyo nazidi kukusisitiza, tuendelee kuwa pamoja kwa sababu safari yetu hii ni ya maisha.
Nimewahi kukuambia ya kwamba safari ya kujifunza haina mwisho. Hii elimu tunayoipata haina kuhitimu, ni lazima ujifunze kila siku mpaka unapoondoka hapa duniani. Wapo baadhi ya watu tuliokuwa nao pamoja siku za nyuma, tukijifunza pamoja. Baadaye nafikiri waliona wameshahitimu, wameshajua kila kitu na kuanza kufanya mambo yao wenyewe bila ya kujifunza. Kilichotokea ni kufanya maamuzi ambayo yaliwarudisha nyuma sana. Hivyo nakusisitiza sana rafiki, hata kama hutajifunza kupitia kazi zangu, basi tafuta njia nyingine yoyote ya kujifunza.
Ujumbe wa leo nataka kukushirikisha njia nyingine ambazo unaweza kujifunza kupitia kazi zangu. Na njia hizi ni sauti na video.
Zipo makala za sauti ambazo nimekuwa naandaa na zinapatikana kwenye mtandao wa SPREAKER, kuzipata makala hizi za sauti na kuweza kuzisikiliza bonyeza maandishi haya. Pia hakikisha unanifollow ili uendelee kupokea mafunzo zaidi kutoka kwangu.
Pia unaweza kusikiliza makala mojawapo kama hivi; Listen to "JINSI YA KUEPUKA KUTAPELIWA NA FURSA MPYA." on Spreaker.
Njia nyingine ya kupata mafunzo ninayotoa ni kwa njia ya video.
Zipo video ambazo nimekuwa naandaa zenye mafunzo mbalimbali.
Unaweza kuangalia video hizi kupitia chanel yangu ya youtube kwa kubonyeza maandishi haya. Pia hakikisha unasubscribe ili uendelee kupokea video zaidi kutoka kwangu.
Unaweza kuangalia moja ya video zangu hapa;
Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Mwisho kabisa nakukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kama unataka tuwe karibu zaidi, kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi na kama unataka kupata ushauri wangu wa moja kwa moja kwenye yale unayofanya, basi karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kuna ada unatakiwa kulipa, ambayo ni tsh elfu 50 kwa mwaka. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na yale utakayokwenda kujifunza.
Kama kwa sasa huwezi kulipia ada hiyo, endelea kujifunza kwa njia hizi nilizokushirikisha hapa, ambazo ni za bure kabisa.
Karibu sana tuendelee kujifunza pamoja. Kumbuka hii ni safari ya maisha, hakuna kuhitimu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uh