Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Kitu Cha Kuepuka Kuongozwa Nacho Katika Ulimwengu Wa Mambo Leo.

$
0
0


Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na umeianza siku yako kwa imani chanya itakayokuwezesha kufika pale unapotaka. Rafiki, mambo mengi tunayofanya yanahitaji sana imani ili uweze kufanikiwa kama kazi unayofanya sasa huna imani nayo ni ngumu kufanikiwa na kufika pale unapotaka. Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo haionekani kwa macho lakini ukiikosa katika moyo wako ndiyo utaweza kuona umuhimu wake.

Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo lakini pia, kukualika tena kwenye somo letu la leo. Kwa hiyo, nakusihi sana tuweze kuambatana pamoja mpaka mwisho wa kipindi hiki.

Mpendwa rafiki, dunia ya leo imejaa kelele za kila aina na watu wamekuwa na mahangaiko mengi ya huku na huko. Wengine wanateseka kwa kutoujua ukweli na ni kweli mahangaiko mengi ya binadamu ni kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi na kutoujua ukweli. Kama ukiujua ukweli nani atakuyumbisha? Labda uamue wewe mwenyewe kuyumbishwa lakini ukiujua ukweli utabaki kwenye njia sahihi.

SOMA; Hizi Ndizo Nguvu Tatu Za Kukupa Maisha Unayoyatamani.

Mpendwa msomaji, malengo yetu mahususi ya leo ni kutaka kujua kitu cha kuepuka kuongozwa nacho katika ulimwengu wa mambo leo? Karibu rafiki ili tuweze kupata jawabu wote kwa pamoja. Kitu cha kuogopa kuongozwa nacho ni hofu. Tunaona katika jamii zetu, familia zetu, na hata sehemu zetu za kazi watu wanafanya kazi kwa kuongozwa na hofu badala ya utulivu wa akili. Tunashuhudia matokeo ya watu wanaokubali kufanya kazi kwa kuongozwa na hofu ya mkuu wake, au kiongozi wake.

Kama mzazi ni mkali basi mtoto atakuwa anafanya kazi kwa kuongozwa na hofu ya baba yake. 

Kwa hiyo, maisha yamekuwa yanaongozwa na hofu iliyotawala katika jamii zetu. Hofu zinawafanya watu mpaka kudiriki kupindisha ukweli. Hofu zinawafanya watu kuzalisha kazi kwa hofu na kupata matokeo ya hovyo, watu hawatumii uwezo wao wanaoujua kuzalisha kitu Fulani.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinachoitwa FLIGHT PLAN The Real Secret Of Success.

Mpendwa msomaji, inabidi ifike mahali tukubali kuongozwa na akili na siyo kukubali kuongozwa na hisia ambazo ni kama vile hofu, hasira, furaha na n.k, naomba unipe majibu tunakwenda wapi? 

Hofu zimetawala kila mahali inafikia wakati hata watu wanauabudu uongo kwa kukubali kufanya mambo kwa hofu. Mwalimu anafundisha darasani anawajengea wanafunzi wake hofu ambayo inawafanya hata kushindwa kuulizwa maswali mbalimbali, mwanafunzi anashindwa hata kuhoji pale mwalimu anapokuwa ameenda mrama.

Ndugu, mara nyingi watu wanaoongoza wenzao kwa kuwajengea hofu ni wale ambao hawana uwezo wa kuongoza, hana kitu kichwani, kwa mfano, mwalimu mmoja, alikuwa akifundisha somo Fulani kwa wanafunzi wake, sasa Yule mwalimu alikuwa amekosea yaani alienda mrama ni katika hali ya kawaida kwa binadamu kukosea. Sasa wanafunzi mmoja, akanyoosha mkono ili apate kuuliza na kupata ufafanuzi wa kweli juu ya somo hilo, sasa mwalimu alipandwa na hasira na kuanza kumshutumu mtoto ina maana wewe unajifanya unajua kuliko mimi? Sasa utaona nitakachokufanyia katika mitihani yako mwalimu alijibu.

SOMA; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 3

Unaona hapo mpendwa msomaji ni namna gani mwalimu alivyoanza kuanzisha hofu kwa mwanafunzi wake, yaani anataka alazimishe kile anachojua yeye kwa wanafunzi hata kama siyo sahihi na mwanafunzi akubali na wakati mwanafunzi yeye hataki uongo anataka ukweli.

Binadamu wote sisi hakuna anayejua zaidi ya mwingine hivyo kila mmoja wetu anaweza kujifunza kutoka kwa mtu mwingine. Mdogo anaweza kujifunza kwa mkubwa na mkubwa anaweza kujifunza kwa mdogo ndivyo ilivyo hivyo, hatuangalii elimu, umri katika kujifunza kila mmoja ni mwalimu kwa mwenzake. Hivyo, ruhusu kujifunza kwa wengine na usiangalie tu na kuamini kile unachojua wewe ndiyo sahihi na wengine hawana maana.

Mpendwa msomaji, kuna kitu kinaitwa information bias, yaani kile unachojua wewe ndiyo unaona ni sahihi na wengine siyo sahihi yaani unajiangalia wewe tu hutaki kujifunza hata kwa wengine, kwa mfano mtu anataka kuwalazimisha watu kuwa kile anachoamini yeye na wengine waamini hivyo hivyo kama mtu anaamini kuwa ajira ndiyo njia pekee ya mtu kuweza kufanikiwa basi anataka na wengine waamini vivyo hivyo.

Hatua ya kuchua leo, rafiki, usikubali kuongozwa na hofu mahali popote pale, wewe kama ni kiongozi acha tabia ya kuongoza wenzako kwa kupandikiza hisia za hofu ili watu washindwe kuhoji na kupata ukweli. Ukweli ni zawadi ya asili ambao utaendelea kuuficha lakini utaonekana tu. Kuwa tayari kujifunza kwa kila mtu na usimlazimishe mtu kuamini kile unachokiamini wewe.

Kwa kuhitimisha, tumealikwa kuepuka kuongozwa na hofu na badala yake tukubali kuongozwa na akili. Ili tuweze kujenga jamii bora tuanze na kujenga misingi imara katika familia zetu kwa kuwaongoza kwa akili na siyo kwa kuwaongoza kwa hisia yaani kuwajengea hofu kama inavyoonekana katika jamii.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti zake kwa kujifunza zaidi kila siku,www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>