Habari za leo rafiki?
Ni imani yangu unaendelea vyema na harakati zako za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Kumbuka hili ni jukumu lako wewe mwenyewe, hakuna mwingine anayekosa usingizi ili maisha yako wewe yawe bora. Shika jukumu hili kila siku na usilaze damu, kama ni mapambano basi haya ni ya maisha yako yote. Muhimu zaidi unahitaji kuyafurahia mapambano haya kwa hatua yoyote uliyopo, kwa sababu ukisema usubiri mpaka ushinde ndiyo uyafurahie, utachelewa sana.
Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto ambapo tunashirikishana yale muhimu kwa mafanikio yetu. Kwenye makala ya leo tunakwenda kushauriana kuhusu kuongeza elimu kama njia ya kuongeza kipato. Je ni njia sahihi ya kutumia? Na kama siyo ipi njia sahihi?
Kabla hatujaangalia kama ni njia sahihi au la, na kuona hatua bora za kuchukua, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyeomba ushauri kwenye hili;
Habari? Naomba ushauri wako kuhusu kusomea masters of education, ina mchango katika kuongeza kipato au nijikite zaidi na shughuli binafsi baada ya kazi? Nisaidie ushauri. Goodluck M.
Habari Goodluck,
Kuongeza elimu ya darasani, siyo njia sahihi ya kutumia kama lengo ni kuongeza kipato. Kwa sababu elimu ya darasani unayokwenda kuipata inakuongezea sifa ya kuajiriwa au kupandishwa daraja kama upo kwenye ajira. Hivyo pamoja na elimu kubwa unayoweza kupata, bado utarudi kwa mtu kuomba ajira, na yule anayekuajiri ndiyo atapanga kiasi gani ulipwe mshahara.
Na hata kama ajira tayari unayo, kwenda kusoma na kurudi, bado hakutaongeza kipato chako maradufu, badala yake kutaongeza kwa kiasi tu. Kwa mfano kama kipato chako kwa ngazi uliyoajiriwa ni milioni moja kwa mwezi, ukienda kusoma na kurudi hakitaruka mara moja na kufika milioni tano, badala yake kitafika labda milioni mbili. Japokuwa kipato kinaongezeka kidogo, hakiendani na uwekezaji ambao utakuwa umeweka kwenye elimu yako. Kuanzia kwenye muda na hata fedha.
Ukiangalia kwa undani, kama lengo kuu ni kuongeza kipato basi kuongeza elimu ya darasani siyo njia sahihi. Changamoto nyingine kubwa kwenye hili ni wingi wa wenye elimu kubwa kama unayokwenda kutafuta au zaidi. Na wote hao wapo kwenye kazi ambazo huenda bado hazijawaongezea kipato au kipato kilichoongezwa hakiwatoshelezi.
SOMA; Hatua Tatu Za Kufikia Utajiri Kwa Kuanza Na Kipato Kidogo Kabisa.
Kufikiria kupata shahada ya uzamili au uzamivu kama njia ya kuongeza kipato ni moja ya hadithi za zamani ambazo kwa sasa hazifanyi kazi. Ni sawa na ile ya nenda shule, soma vizuri, faulu na utapata kazi nzuri itakayokufanya uwe na maisha bora. Nafikiri kwa sasa hata watoto wa shule ya msingi hawadanganyiki tena na hilo, kwa sababu uhalisia upo wazi kabisa. Hadithi ya shahada zaidi ilikuwa nzuri wakati bado wengi hawakuwa na elimu kubwa, hivyo mtu kuongeza shahada kulimpa fursa za kupata nafasi za uongozi, kwa mfano kwa taaluma ya ualimu basi ilimpelekea kuwa afisa elimu wa wilaya, au kwa taaluma ua udaktari basi ilimfanya kuwa mganga mkuu wa wilaya au mkoa. Pia ilitoa nafasi ya mtu kupata ukuu wa kitengo fulani, lakini sasa hadithi hiyo ukweli wake umeisha.
Lakini bado kusoma ni muhimu;
Usininukuu vibaya kwamba nimesema watu wasiongeze shahada zaidi na kubobea kwenye taaluma zao. Nilichosema ni usijidanganye ukiongeza shahada basi kipato chako kitaongezeka maradufu, utaumia sana kama hilo litakuwa ndiyo lengo, kwa sababu hutalifikia.
Lakini nakusisitiza sana kama kweli unataka kubobea kwenye taaluma yako, kama unataka kujua zaidi ili kuweza kutoa huduma bora zaidi, basi nenda kaongeze elimu zaidi. Pata shahada ya uzamili, uzamivu na hata ikiwezekana kuwa profesa kabisa. Lakini fanya hivyo kwa malengo sahihi, ambayo ni kujua zaidi kile ulichochagua kufanya na hivyo kuweza kuwasaidia wengi zaidi na kutoa huduma bora zaidi.
Kama una shahada ya kwanza ya ualimu soma shahada zaidi ili uweze kufundisha wanafunzi wa juu zaidi, badala ya kufundisha wanafunzi tu, uweze kufundisha walimu watakaokwenda kufundisha wanafunzi zaidi, na utakuwa umetoa mchango mkubwa. Hivyo pia kwa shahada ya udaktari, kwa kusoma zaidi na kuwa daktari bingwa, utaweza kuwasaidia wengi wenye matatizo makubwa zaidi. Na kwa kuweza kutoa huduma bora na kwa wengi zaidi, itapelekea kipato chako kuongezeka.
Naomba twende sambamba hapa, elewa vizuri kwamba kwa kuongeza elimu ya darasani, kunakupa wewe fursa ya kutoa huduma bora zaidi na hii itapelekea kipato chako kuongezeka. Lakini kama utaenda kuongeza elimu kwa lengo la kipato kukua, itakukatisha tamaa. Kwa sababu ongezeko la kipato litakuwa dogo kuliko matarajio yako na hiyo itakuumiza.
Je ni njia gani utumie kuongeza kipato chako zaidi?
Zipo njia nyingi, lakini kubwa ni kuwa na biashara au uwekezaji ambao unakuzalishia hata kama haupo pale moja kwa moja. Kama upo kwenye ajira, hakikisha unakuwa na biashara ya pembeni ambayo utaweza kuisimamia vizuri na kuikuza kiasi cha kukuwezesha kuondoka kwenye ajira hiyo kama haikutoshelezi. Na kama huwezi kuanza biashara basi anza kuwekeza, na kadiri unavyokwenda utatengeneza kipato cha uhakika.
SOMA; Hii Ndiyo Mifereji Nane (08) Ya Kipato Ambayo Kila Mtu Anayetaka Utajiri Anapaswa Kuwa Nayo.
Kama lengo lako kubwa ni kuongeza kipato, badala ya kwenda kuongeza shahada ambayo itakuchukua muda wa zaidi ya mwaka na gharama kubwa, tumia nusu ya gharama hizo na muda huo kuanzisha kitu kipya ambacho utajifunza na kukisimamia kwa nidhamu ya hali ya juu sana.
Jipe kama miaka miwili ya kuanza kitu ambacho utakiita shahada ya uzamili kwako, unakichukulia kwa nidhamu kama ambavyo ungechukulia masomo yako na kuhakikisha miaka miwili inapokwisha, ambao ni wastani w akupata shahada ya uzamili, unakuwa umepiga hatua kubwa.
Nikuambie ya kwamba ukiweza kufanya hivi, miaka miwili utakuwa umefanya kitu kikubwa sana.
Rudi shuleni kwa sababu sahihi, ili baadaye usije kujilaumu na kusema ningejua. Usiendelee kuishi hadithi zilizopitwa na wakati, zama zinabadilika, unahitaji kubadilika pia.
Kama unataka kuanzisha biashara ukiwa bado umeajiriwa, unahitaji sana kusoma kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA. Kama mpaka sasa bado hujakisoma, kipate sasa na uweze kukisoma. Kupata kitabu hiki tuma ujumbe kwenye namba 0717396253 na utapewa utaratibu wa kupata kitabu hichi.
Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.