Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Maswali Na Majibu Kuhusu Semina Ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO.

$
0
0


Rafiki yangu,

Tarehe 04/01/2017 tutaanza semina yetu ya siku kumi itakayoendeshwa kwa siku kumi kwa njia ya mtandao wa wasap. Hii ni semina mahususi ya kuuanza mwaka 2017, ambapo mwaka huu tunakwenda kuuanza kiutofauti kabisa ili tuweze kufanya makubwa pia. Kwa kifupi, tunakwenda kufanya makubwa mwaka 2017 bila ya kuwa na malengo. Hili limekuwa linawachanganya watu na wasielewe hili linawezekanaje, ndiyo maana leo nimeandaa makala hii ya kukupa wewe ufahamu zaidi kuhusu semina hii ili uweze kuchukua hatua stahiki.
 

Kabla hatujaingia kwenye maswali na majibu, nikueleze kidogo kuhusu semina hii.

Rafiki, maelezo kamili kuhusu semina pamoja na masomo yatakayofundishwa yapo hapo chini;

SEMINA; 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO.

Semina ya siku 10; 04/01/2017 – 13/01/2017

Semina itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Mafunzo yatatolewa kwa njia ya maandishi na sauti.

Masomo ya semina;

Siku ya kwanza; karibu 2017, mwaka wangu wa mafanikio makubwa zaidi.

Siku ya pili; kauli tatu za kutuongoza mwaka huu 2017 na jinsi ya kuzitumia kufanikiwa.

Siku ya tatu; kwa nini malengo ni kikwazo kwa kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.

Siku ya nne; mbadala wa malengo, umuhimu wa mfumo na jinsi ya kutengeneza mfumo wa maisha.

Siku ya tano; mfumo wa mafanikio ya kifedha, ondoka kwenye madeni na anza kuwekeza.

Siku ya sita; mfumo wa mafanikio ya kikazi, fanya makubwa kwenye kazi na/au biashara yako 2017.

Siku ya saba; mfumo wa mafanikio ya kiafya, mwongozo muhimu wa kuwa na afya imara kwa ajili ya mafanikio.

Siku ya nane; mfumo wa mafanikio ya kifamilia na kijamii, wape nafasi wale muhimu kwenye maisha yako.

Siku ya tisa; mfumo wa kuweza kupambana na changamoto yoyote utakayokutana nayo mwaka 2017 ili isikuzuie kufanikiwa.

Siku ya kumi; mambo 10 muhimu ya kuepuka kwa mwaka huu 2017 ili kuweza kuwa na maisha ya mafanikio.

Hivi ndivyo tunavyokwenda kuuanza mwaka 2017 pamoja rafiki, nitahakikisha kwa pamoja tunafanya makubwa sana mwaka 2017.
Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina hii ambayo pia itakuwa ni ada ya wewe kuendelea kupata mafunzo kutoka kwangu na wanamafanikio wengine kwa mwaka mzima. Kwa kulipa ada unajiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA wasap na kupata nafasi ya kusoma makala nzuri za kila siku kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA.

Ada ya kushiriki semina ni kulipia ada ya uanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni tsh elfu 50 kwa mwaka (50,000/=).

Ada inalipwa kwa tigo pesa 0717 396 253 au mpesa 0755 953 887 majina kwenye namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishafanya malipo tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253 kisha nitakuweka kwenye kundi la semina.

Mwisho wa kulipa ada na kujiandikisha ni tarehe 02/01/2017. Zimebaki siku mbili pekee rafiki, chukua hatua sasa.

Karibu kwenye sehemu ya pili ya makala ya leo ya maswali na majibu kuhusu semina hii.

Kabla ya kuangalia maswali a majibu nikushirikishe ujumbe wa msomaji mwenzetu ambaye aliniandikia kuhusiana na semina hii;

Habari za siku Kocha wangu Makirita, kuna jambo nataka kuliomba kwako ukiwa kama Kocha wangu kwa mwaka sasa. Umekuwa ukifundisha jinsi ya kuweka malengo ya muda mfupi na muda mrefu nashukuru kwa ushauri wako umenisaidia kwa kiwango kikubwa malengo yangu ya muda mfupi nimeyatimiza. Na mwaka huu 2017 nilipanga kutimiza yale ya muda mrefu. Lakini siku za hivi karibuni umekuwa ukinishauri mwaka 2017 niishi bila malengo. Ni sawa kabisa ushauri wako nakubaliana nao na nahisi kuna kitu cha ziada nitajifunza au nitapata nikishiriki semina iliyoandaliwa lakini naomba hiyo semina unishirikishe mwaka 2018 panapo majaaliwa. Huu mwaka 2017 kuna malengo niliweka na naomba kwanza niyatimize. Nahisi nikishiriki hiyo semina kama nitavuruga mipango yote niliyojiwekea mwaka 2017.

Kama ambavyo msomaji mwenzetu ameniandikia hapo, ana hofu kubwa kwamba mwaka bila ya malengo utavuruga mipango yake ya maisha. Naomba nimjibu na kukujibu wewe ya kwamba siyo kwamba mwaka 2017 tunaenda kukaa tu kizembe na kuacha mwaka uende. Bali ipo njia bora sana ya kuweza kupata kile tunachotaka, na njia hiyo haihusishi kuweka malengo. Upo mfumo mzuri wa kukuwezesha wewe kufanya makubwa, ambao ni wa uhakika na unaweza kuutegemea tofauti na malengo ambayo yatakutesa, kukunyima furaha na kukufanya uahirishe maisha kwa kuwa hujafikia malengo hayo.

Ndiyo maana nakusihi sana wewe kama rafiki yangu, na kama umekuwa unanufaika na maarifa ninayokushirikisha, basi karibu tujaribu njia hii ya tofauti ya kufanya makubwa kwenye maisha yetu. Shiriki semina hii, utaona namna unaweza kushika usukani wa maisha yako, na kuwa na furaha kila siku, hata kama bado hujapata kile unachotaka. Maana kuwa na furaha tu ni dalili tosha kwamba utafanikiwa, na siyo kutegemea mafanikio yakuletee furaha, haiendi hivyo.

Nakusihi rafiki, njoo ushiriki semina.

Maswali na majibu.

Swali; semina inafanyika wapi, tunahudhuriaje?

Jibu; semina inafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap, huhitaji kuhudhuria popote, unafuatilia semina ukiwa hapo ulipo sasa, popote pale Tanzania.

Swali; je kama sina simu ya wasap nitawezaje kushiriki?

Jibu; kama huna simu ya wasap huwezi kushiriki, hili ni hitaji namba moja. Hivyo pata simu yenye wasap mapema ili uweze kushiriki.

Swali; simu yangu ina uwezo mdogo, ni simu ndogo, je nitaweza kufuatilia mafunzo haya vizuri?

Jibu; ndiyo, unafuatilia vizuri, ukishakuwa na wasap tu inatosha. Huhitaji kuwa na simu kubwa sana au yenye memory kubwa, mafunzo yatakuwa kwa maelezo na sauti ambazo hazitachukua nafasi kubwa.

Swali; je nikishalipa ada naendeleaje kunufaika?

Jibu; utakuwa kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambapo kila siku, kwa mwaka mzima utajifunza kupitia makala, tafakari na mafanikio ya wengine.

Swali; je kama mimi tayari ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA nahitaji kulipa ada ya semina?

Jibu; kama ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA bado haijamaliza muda wake, huhitaji kulipa ada ya semina. Kama ada imemaliza muda wake basi unahitaji kulipa ada yako kwa wakati ili uweze kushiriki semina.

Swali; je kama nipo bize na nabanwa na kazi, nitaweza kweli kushiriki semina?

Jibu; ndiyo unaweza vizuri sana, tena inakuhusu mno. Masomo ya semina yanatolewa asubuhi, maswali majibu na mijadala inafanyika jioni, mchana kila mtu lazima afanye kazi zake kama kawaida, samahani siyo kama kawaida, ila kwa juhudi na maarifa makubwa.

Rafiki, nina hakika umepata ufafanuzi zaidi kuhusu semina hii kupitia maswali na majibu hayo. 

Kama una swali jingine ambalo sijajibu hapo, niandikie moja kwa moja kwa njia ya wasap kwenye namba 0717 396 253, na nitakujibu. Usitume kwenye email, naweza kuchelewa kuona swali lako halafu ukawa umeikosa nafasi hii ya kipekee.

Nakukaribisha sana rafiki, mwaka 2017 nataka twende bega kwa bega mwaka mzima.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>