Hongera sana rafiki yangu kwa mwaka huu mwingine wa 2017.
Ni nafasi ya kipekee sana ambayo tumeipata ya kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yetu na ya wale ambao wametuzunguka. Tusifurahie tu kwa mwaka kuwa mpya, bali tuifurahie siku hii nyingine nzuri ya leo na kila siku ambayo tunaipata kwenye maisha yetu.
Napenda kuchukua nafasi hii kukukumbusha hili muhimu sana rafiki yangu, maisha ya mafanikio hayaji kama ajali. Bali ni mkusanyiko wa siku nyingi za mafanikio madogo madogo. Hivyo kama unataka kuja kuhesabu mwaka 2017 kuwa mwaka wa mafanikio, basi hakikisha unaiishi kila siku, hakikisha kila siku unapiga hatua, na hakikisha unakuwa bora zaidi kila siku ukilinganisha na ilivyokuwa jana yake.
Nakupongeza sana kwa nafasi hii nzuri ambayo unaipata, ni nafasi ambayo unahitaji kuitumia vizuri, kwa sababu kadiri siku zinavyokwenda, muda wako wa kuwa hapa duniani unapungua.
Hatupendi kuwaza hili lakini wote tunajua hatima yetu ni kifo, na baada ya kifo hayatahesabiwa yale uliyomiliki, mali na fedha, bali kitakachohesabiwa ni namna gani umegusa maisha ya wengine.
Hivyo rafiki yangu, kila nafasi unayoipata, hakikisha unagusa maisha ya wengine.
Kama unafanya kazi, tumia kazi yako kugusa maisha ya wengine, kama unafanya biashara, tumia biashara yako kugusa maisha ya wengine. Chochote unachofanya, hakikisha kina mchango chanya kwenye maisha ya wengine, kinaongeza thamani kwenye maisha ya wengine, na utakuwa na mafanikio ya kweli kwenye maisha yako.
Sina mengi ya kukuandikia leo rafiki yangu zaidi ya salamu hizi za mwaka mpya 2017, nakusihi sana ukumbuke yale mambo matatu niliyokushauri uyafanye mwaka huu 2017, kumbuka ni matatu tu. Kama hukuyasoma yasome hapa.
Pia nikukumbushe usikubali kuingia kwenye mkumbo wa kauli za kujidanganya kama MWAKA MPYA MAMBO MAPYA, tofauti ya 2016 na 2017 ni 6 na 7, mengine yote yataendelea kubaki kama yalivyo, mpaka pale wewe mwenyewe utakapoamua kuchukua hatua ya kuyabadili.
Nitumie pia nafasi hii kukukumbusha kuhusu semina yetu ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO, mwisho wa kujiunga na semina ni kesho tarehe 02/01/2017. Tumia nafasi ya leo kulipa ada yako tsh 50,000/= kwa tigo pesa 0717 396 253 au mpesa 0755 953 887 ukishatuma fedha tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253. Kama hukupata maelezo kamili ya semina hii bonyeza hapa kupata ufafanuzi.
Ahadi yangu kwako kwa mwaka 2017 na kuendelea.
Tangu mwanzoni mwa mwaka 2013, AMKA MTANZANIA imekuwa na wewe, imekuwa inakupa makala yenye maarifa bora kabisa ambayo ukiyafanyia kazi maisha yako hayabaki kama yalivyokuwa. Makala za biashara, kazi, hamasa, mafanikio na nyingine nyingi umekuwa unazipata kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA bila ya kulipa gharama yoyote ile.
Ninachokuahidi kwa mwaka 2017 ni kuendelea kukushirikisha maarifa bora kabisa ambayo yatakuwezesha kufanya maamuzi bora kwenye maisha yako. Najua changamoto ni nyingi na kuna wakati hujui ufanye nini, nitakuwa bega kwa bega na wewe kupitia AMKA MTANZANIA.
Kazi yangu kubwa niliyochagua ni kuhakikisha nawashirikisha wengine maarifa bora kabisa yatakayowawezesha kubadili maisha yao na kupiga hatua. Nipo tayari kukuhudumia wewe kwa mwaka 2017. Kila siku utaendelea kupata makala nzuri ambapo utaondoka na kitu cha kujifunza na kufanyia kazi ili maisha yako yaweze kuwa bora kabisa.
Kama utaweza nakukaribisha pia ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA, ambapo tunakuwa karibu zaidi kwenye kundi la wasap na kila siku unapata makala nyingine nzuri, tofauti na unayoipata kwenye AMKA MTANZANIA. Pia kuna madarasa mbalimbali kupitia kundi la wasap.
Lakini kama hutaweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA sasa, bado utaendelea kufaidi sana kupitia AMKA MTANZANIA, kwenye KISIMA CHA MAARIFA unafaidi zaidi na tunakuwa karibu zaidi. Lakini kwenye AMKA MTANZANIA utaendelea kufaidi bila ya kulipa kiasi chochote cha fedha.
Siku moja nilikutana na mmoja wa wasomaji ofisini kwangu, alilipia huduma mbalimbali ninazotoa lakini hakuwa amelipia KISIMA CHA MAARIFA, ikabidi nimuulize kwa nini hulipii KISIMA CHA MAARIFA, maana siyo kwamba alikuwa amekosa fedha ya kulipia, alichonijibu kiliniacha mdomo wazi. Aliniambia kwa kweli haya ninayoyapata kwa bure tu, ninaona nina deni kubwa la kuyafanyia kazi, naona nikijiunga na KISIMA, nitaongeza deni hili liwe kubwa zaidi. Wacha nifanyie kazi haya kwanza, na tutajiunga pamoja. Nilimpa sababu nyingine nzuri za kujiunga.
Kama na wewe upo kwenye hali kama hiyo, unaona unayopata kwa bure ni mazuri mno, usiache kujiunga na KISIMA, kwa sababu mwaka 2017 yapo makubwa na mazuri kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Nakukaribisha sana rafiki tuendelee kuwa pamoja, kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Usisahau kulipia semina leo ili tuweze kuuanza na kusafiri pamoja kwa mwaka 2017.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.