Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

NYEUSI NA NYEUPE; Kwa Nini Watu Wengi Wanashindwa Kuacha Ajira Hata Kama Ni Ngumu Kwao Na Haziwalipi.

$
0
0

Habari za leo rafiki?
Karibu kwenye kipengele hiki kipya cha NYEUSI NA NYEUPE ambapo tunachambua jambo kwa namna lilivyo. Hapa tunaweka ushabiki wa aina yoyote pembeni na kuutafuta ukweli wenyewe wa jambo husika. Kwa kuwa siku zote ukweli huwa unauma, kuwa tayari kukutana na vitu ambavyo hutavipenda, lakini ndiyo ukweli wenyewe. Makala hizi zitakuwa zinakujia kila siku ya jumapili kupitia AMKA MTANZANIA.

Kwenye makala ya leo tunakwenda kuangalia kwa undani kuhusu ajira, hasa ugumu wa kuacha ajira ambayo ni ngumu na hailipi. Hili ni jambo ambalo nimekuwa naliona kwa wengi, watu wanang’ang’ana na ajira ambazo ni ngumu kwao na mbaya zaidi hata kulipwa hawalipwi. Lakini watu hao bado hawathubutu kuacha ajira hizo.

Miaka ya nyuma nimewahi kufanya kazi kwenye taasisi fulani, kulikuwa na wafanyakazi ambao wana miaka mingi wanadai taasisi hiyo lakini hawalipwi. Na wakati huo pia bado walikuwa hawapati mishahara yao kwa wakati, kwa kifupi maisha yao yalikuwa ni magumu, lakini bado hakuna ambaye alikuwa na wazo la kuondoka kwenye ajira hiyo. Mbinu walizokuwa wakipanga ni namna gani ya kupambana walipwe mishahara yao kwa wakati na kulipwa madeni yao. Na hapo ulikuwa ukiangalia, taasisi yenyewe ilikuwa haifanyi vizuri kibiashara kusema kwamba inatengeneza faida kubwa. 
 
KUPATA KITABU HIKI BONYENZA MAANDISHI HAYA.

Nimekuwa pia najifunza sana kwa wale ambao wananiomba ushauri na marafiki wengine. Wengi ambao tayari wapo kwenye ajira, wana ndoto ya siku moja kuondoka kwenye ajira hizo, lakini siku hiyo huwa haifiki, kila siku kuna sababu ya kwa nini waendelee kuwa kwenye ajira hizo.

Leo nataka tuangalie NYEUSI NA NYEUPE kwenye swala hili la kuacha ajira na kwenda kwenye ajira nyingine au kujiajiri. Hili ni jambo gumu kidogo, ambalo tunahitaji kuliangalia kwa kina ili tuweze kujua msingi wake na pale tunapotaka kuchukua hatua, tuwe na taarifa sahihi.

Tafiti nyingi ambazo zimekuwa zinafanywa, zinaonesha kwamba watu wengi hawaridhishwi na ajira walizonazo. Pia watu wengi ambao wamekuwa wanapatwa na msongo wa mawazo, ajira imekuwa chanzo kikuu cha kufikia hapo. Kwa sababu kazi inachukua karibu nusu ya muda wa mtu, kazi inapokuwa tatizo, hata maisha ya mtu yanakuwa tatizo kubwa. Tunaona haya kila siku, lakini kwa nini bado watu hawawezi kuondoka wenyewe kwa hiyari?

Kuna wengine ambao wanakuwa wanaona kabisa kazi zao hazina matarajio yoyote ya mbeleni. Kwa namna wanavyochukuliwa kwenye kazi hizo, wanaona kabisa hakuna anayejali kama wapo au hawapo. Lakini watu hao hawawezi kuchagua kuacha kazi hizo wao wenyewe, watasubiri mpaka wafukuzwe au kupunguzwa kazi.
Wapo wengi ambao wanafanya kazi miaka na miaka, lakini mishahara yao haijawahi kukutana. Yaani akipokea mshahara mmoja unaisha kabla mshahara mwingine haujatoka, anakuwa ni mtu wa kukopa na kulipa madeni kila mwanzo na mwisho wa mwezi. Mtu anaweza kwenda hivi kwa miaka kumi mpaka ishirini, lakini hawezi kufika mahali na kusema sasa imetosha, kazi hii siitaki tena.

Kuna watu wengi ambao wamekuwa wakiogopa kuacha kazi zao wenyewe, baadaye inatokea wamefukuzwa kazi hizo, ndiyo wanapata akili ya kufanya makubwa kwenye maisha yao. Baadaye wanakuwa na maisha bora sana na kushukuru sana kufukuzwa kwao kazi. Na hata wale ambao walikuwa nao kwenye kazi moja, ila wakabaki kwenye ajira, wakiwaangalia wanaona kweli maisha yao yamebadilika baada ya kufukuzwa kwenye ajira, na wakati wao wana ajira lakini maisha ni magumu. Lakini bado hawatathubutu kuacha ajira zao na kushika hatamu ya maisha yao.

Hapa kuna jambo kubwa na zito, ambalo huwezi kulichukulia juu juu, kwamba watu waamue kuteseka kama kuna njia nyingine ya wao kuwa na maisha bora. Ndiyo maana tunakwenda kuangalia NYEUSI NA NYEUPE kwenye hali hii ya kushindwa kuondoka kwenye ajira kwa hiyari yako mwenyewe.

Kwa nini ni vigumu sana mtu kuondoka kwenye ajira ambayo haimridhishi?

1.     Uongo wa zama na zama.
Sababu namba moja na kubwa kabisa ya watu kushindwa kuondoka kwenye ajira ni ule uongo ambao tumekuwa tunaimbiwa miaka na miaka. Uongo huu umenasa kabisa kwenye mawazo yetu na kuutoa ni kazi ngumu sana.
Fikiria tangu unazaliwa, unakua, unaenda shule ya msingi, sekondari, chuo na hatimaye kuingia kwenye ajira, wimbo ni mmoja, soma kwa bidii, faulu, utapata kazi nzuri na kuwa na maisha bora. Tumelishika hili maisha yetu yote, tumelifanyia kazi, na mwishowe tunapata kazi, lakini bado maisha yetu hayawi bora. Lakini mbona bado hatustuki na kuchuka hatua? Kwa sababu tunaendelea kudanganywa, tena na tena na tena.
Safari hii uongo unabadilika, kwamba umeshapata kazi, lakini maisha yako ni magumu kwa sababu upo ngazi ya chini, sasa kuwa na adabu, fanya kazi zako vizuri, tii sheria na utapanda cheo, siku moja utakuwa mkurugenzi wa kampuni au shirika hili na maisha yako yatakuwa bora sana. Sasa uongo huu ndiyo unamaliza wengi na ndoto zao. Hapa watu wanajiambia kwamba kama wakiweza kuvumilia, muda siyo mrefu watapanda vyeo na maisha kuwa bora.

Uongo huu una matatizo mawili;
Tatizo la kwanza, kadiri cheo kinavyoongezeka na kipato kuongezeka na matumizi nayo yanabadilika, ugumu wa maisha nao unaongezeka. Kwa kuwa mfanyakazi wa chini unaweza kwenda kazini kwa usafiri wa umma, lakini kadiri cheo kinapanda utaona huwezi tena kwenda na usafiri wa umma, unahitaji usairi wako, na siyo tu usafiri, bali usafiri wa maana, unaoendana na hadhi yako. Gharama zinaanza kwenda juu, kuanzia usafiri, mavazi, nyumba, na hata chakula unachokula ukiwa kazini.

Tatizo la pili; nafasi inayoangaliwa ni moja, wanaoiangalia ni wengi. Bosi ni moja tu kwenye kitengo cha kazi, mkurugenzi ni mmoja tu kwenye kampuni au taasisi, lakini kuna wafanyakazi zaidi ya 20 ambao wanaangalia nafasi hiyo moja. Kwa hesabu za kawaida tu ni kwamba haiwezekani kila mtu akapata nafasi hiyo, lakini bado tutajidanganywa, kwamba sisi ni bora zaidi ya wengine, hivyo tutaipata, na tunashangaa siku zinakwenda lakini hatuipati.

2.     Wazazi, familia, ndugu, jamaa na marafiki.
Hawa watu wanaotuzunguka, ni kikwazo kikubwa sana kwetu kufanya maamuzi ya kuondoka kwenye ajira. Kwa jamii zetu, ni vigumu sana kueleweka pale utakapowaambia watu wako wa karibu kwamba kazi uliyonayo huoni kama itakufikisha kule unataka, hivyo unaiacha. Hebu pata picha wewe ni kijana na unaenda kwa wazazi wako waliokusomesha na kuwaambia hii kazi ya ualimu niliyonayo kwa kweli hainifai, nimeamua kuacha na nifanye vitu vingine.... unaweza ukaachiwa hata laana. Hawawezi kukuelewa kabisa, kwa sababu wanajua wewe kuwa na ajira ya uhakika ndiyo maisha bora kwako na hata kwao pia.
Hivi ndivyo inavyokuwa kwa wenza, na hata marafiki zetu. Kila ukiwapa wazo lako la kuacha ajira, wanakuona labda utakuwa umechanganyikiwa. Inakuwa vigumu mno kuacha ajira wakati kila anayekuzunguka hakubaliani na wewe.

3.     Hofu ya kupoteza zile faida zinazotokana na ajira.
Kuna faida ambazo zinatokana na ajira, kiuhalisia huu pia ni uongo mwingine ambao umetumika kuwavutia watu kubaki kwenye ajira. Faida hizo ni kama bima ya afya, mafao ya uzeeni, fidia pale unapopata matatizo na kadhalika. Lakini hebu angalia kwa undani, bima ya afya si unakatwa mshahara wako? Mafao ya uzeeni je, si sehemu ya mshahara wako kukatwa? Lakini bado tunashawishika kwamba ajira ndiyo zinatupa vitu hivi.
Faida hizi zimekuwa zinatusaidia kwa sababu tumekosa nidhamu, ni vigumu sana mtu kujiwekea fedha ya dharura ambayo ataitumia pale yeye au mtu wake wa karibu atakapougua, hivyo kuwa na bima ya afya kunakuwa ni ahueni.
Pia ni vigumu sana mtu kujiwekea mwenyewe akiba ya uzeeni, hivyo mafao ya uzeeni kuonekana ni dili kubwa ndani ya ajira. Tusichimbe tu ndani zaidi kwenye mafao haya, maana nayo ni uongo mwingine ambao umekuwa unawafanya watu wabaki kwenye ajira. Niguse kidogo tu; angalia sakata linaloendelea kuhusu mafao, kwamba mtu hataweza kuchukua mafao yake mpaka afikishe miaka 60, hata kama ameacha kazi, ndiyo utajua mafao nayo siyo ya uhakika kama ulivyokuwa unafikiri.

4.     Hofu ya kutokuwa na uhakika na kule unakoenda.
Pamoja na ajira kuwa ngumu, lakini mtu anakuwa na kitu kimoja, kwamba ana uhakika wa kazi, na hata kama kipato ni kidogo, ana uhakika wa kukipata. Sasa mtu akifikiria kuacha hivi alivyonavyo sasa, na kwenda kufanya vile ambavyo hana uhakika navyo, hofu inamzuia kuchukua hatua. Na misemo yetu ya kiswahili, kwamba ni heri kidogo ulichonacho, kuliko kikubwa ambacho huna, basi tunashindwa kabisa kuchukua hatua.

5.     Kukosa mpango bora wa kutoka pale ulipo sasa.
Watu wengi ambao wamekwama kwenye ajira wamekuwa na fikra moja, kwamba ili waweze kutoka kwenye ajira na kujiajiri basi wanahitaji kuwa na mtaji mkubwa ili waanze biashara ambayo haitakufa. Hivyo wanajipa kazi ya kukusanya mtaji ili tuweze kuondoka kwenye ajira hizo. Lakini maisha nayo yanaendelea, changamoto hazikosekani. Hivyo ukikusanya na kufika kiasi fulani, mara kuna ndugu anaumwa inabidi utumie. Majukumu nayo yanaongezeka, gharama za maisha zinapanda, tunakuja kugundua kwamba zoezi hili la kukusanya mtaji ni gumu kuliko tulivyodhani.
Lakini uzuri ni kwamba matumaini hayakauki, kwamba kama tumeshindwa sasa, basi tusubiri mpaka tutakapostaafu, tutaweza kufanya yale tunayotaka kufanya. Na sababu tunajipa mbili; kwanza tutapata mafao, hivyo fedha haitakuwa tatizo, pili majukumu yatakuwa yamepungua, watoto wameshakua na kujitegemea hivyo ni sisi tu. Huu ni uongo mwingine ambao umepoteza maisha ya wengi.
Wapo ambao kweli wanafikia nafasi hiyo ya kustaafu na wanapewa mafao yao na kweli majukumu hawana lakini unajua nini kinatokea? Tafiti zinaonesha wengi hufariki ndani ya miaka mitano baada ya kustaafu kwao, tutalichambua hili kwa undani siku nyingine. Lakini ukweli ni kwamba mambo yamekuwa hayaendi kama watu wanavyokuwa wamepanga.

Ni hatua zipi ambazo mtu anapaswa kuchukua ili kuondoka kwenye mtego huu wa kushindwa kuondoka kwenye ajira?
Kwenye NYEUSI NA NYEUPE sikuachi hivi hivi, bali nakupa njia mbadala, hatua za kuchukua ili kutoka pale ulipokwama sasa. Na kama umezisoma sababu hizo za kuwa kwenye mkwamo, utakuwa umeanza kupata picha ni nini cha kufanya.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuanza kuchukua sasa ili kuondoka kwenye mkwamo wa kiajira.

1.     Badili kabisa mfumo wa mawazo na maisha yako.
Tukichukulia akili yako kama kompyuta, basi nitakuambia unatakiwa ku ‘format’ yaani kufuta kabisa zile fikra za kizamani na kuweka fikra mpya. Sahau kuhusu usalama wa ajira, sahau kuhusu faida za kwenye ajira. Anza kufikiria ni kipi unataka kwenye maisha yako na kama ajira uliyonayo sasa inakupatia au itakuwezesha kupata. Na ninaposema unachotaka siyo fedha pekee, bali hata kuridhishwa na kazi unayofanya, na kuipenda pia.
Unahitaji kuondoa fikra za zama zilizopita na kuweka fikra za zama hizi ambapo kuna taarifa nyingi ambazo unaweza kuzitumia kupata kile unachotaka kupata.
Waheshimu wale wanaokuzunguka, sikiliza maoni yako, lakini fanya maamuzi yako mwenyewe. Kumbuka kwamba ni wewe pekee utakayeyaishi maisha yako, hakuna mwingine anayeweza kukusaidia kuyaishi. Japokuwa wanakushauri na kukuonya mambo mengi, lakini bado wewe unahitaji kufanya maamuzi yako. Fanya maamuzi ambayo unajua unaweza kuishi nayo bila ya kujutia na siyo kufanya kwa sababu unataka kuwaridhisha wengine. Hivyo kama unachagua kuendelea na ajira yako, chagua ukijua ni jambo muhimu kwako, kama unachagua kuondoka, basi chagua ukijua utakuwa tayari kupambana na lolote utakalokutana nalo.
Ni kweli utawachukiza watu pale utakapochukua maamuzi ambayo hawakubaliani nayo, lakini baadaye watajifunza na kukuheshimu kwa maamuzi hayo.

2.     Anza kuchukua hatua ukiwa bado upo kwenye ajira yako.
Usiendelee kusubiri tena mpaka kila kitu kiwe sawa, uwe na mtaji wa kutosha ndiyo uondoke kwenye ajira na kwenda kufanya mambo mengine. Usisubiri tena mpaka ustaafu ndiyo uweze kuishi maisha ya ndoto yako. Badala yake anza sasa, anza wakati huu ukiwa bado upo kwenye ajira hiyo inayokusumbua. Na ninachoweza kukuambia ni kwamba unaweza kufanya chochote ukiwa bado upo kwenye ajira yako kwa sasa.
Kuhusu hili nimeandika kitabu kinaitwa BIASHARA NDANI YA AJIRA, ni kitabu ambacho kitakupa hatua kwa hatua namna unavyoweza kufanya biashara ukiwa bado umeajiriwa, pia kina mifano ya biashara ambazo unaweza kuanza kuzifanya ukiwa bado umeajiriwa. Nakushauri sana sana sana ukisome kitabu hiki, kitakupa mwanga mkubwa.
Kukipata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na utapata maelekezo ya kukipata kitabu hiki. Nasisitiza tena, kisome, kitakusaidia sana.

3.     Shika hatamu ya maisha yako.
Kitu kimoja ambacho kinawafanya watu wabaki pale walipo, ni kuamini kwamba kuna watu wa kuja kuwatoa hapo walipo. Wanaamini maisha yao ni magumu kwa sababu waajiri wao wanawalipa kidogo, au serikali imewatelekeza. Sasa wewe achana na kundi hili la watu, shika hatamu ya maisha ya maisha yako.
Acha kabisa kitu kinaitwa kulalamika, kama kuna kitu hukipendi kibadili, na kama huwezi kukibadili achana nacho.
Naamini kwa pamoja tumeweza kuona ukweli halisi wa ugumu wa kuondoka kwenye ajira na hatua tunazoweza kuchukua ili kuondoka kwenye mtego huu. Sasa kazi ni moja, kufanyia kazi haya ambayo tumejifunza, ili maisha yetu yaweze kuwa bora sana.
Nakutakia kila la kheri rafiki katika kufanyia kazi haya uliyojifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata Blog Yako Ya Kitaalamu Unayoweza Kutumia Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao, Soma Hapa.

$
0
0
Habari rafiki?
Wiki iliyopita niliendesha semina ya KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Zaidi ya marafiki 1000 walishiriki semina ile na wengi wamekiri kujifunza mambo mengi na makubwa. Kama ulikosa semina hii nzuri sana pole rafiki, lakini bado ipo njia ya wewe kunufaika na mafunzo yale niliyoyatoa. Na hapa nitakushirikisha njia unazoweza kutumia mpaka kumiliki blog yako mwenyewe ambayo utaitumia kutengeneza fedha kwenye mtandao. Katika mipango hii pia nitakupa nafasi ya kuendelea kuwa karibu na mimi ili tujifunze kwa pamoja. Soma hapa rafiki kisha uchukue hatua. Karibu sana.
Naomba nichukue nafasi hii kukupa mipango madhubuti ya kuweza kuanzisha na kukuza blog yako.


Mpango wa kwanza; Tangeneza blog yako mwenyewe ya bure.
Hapa ni wewe kutengeneza blog yako ya bure ambayo hutahitaji kuilipia tena. Na unahitaji maelekezo ya hatua kwa hatua ili kuweza kufanya hivyo. Nimeandika kitabu kinaitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kwenye kitabu hiki nimeonesha kwa njia ya picha hatua zote unazoweza kufuata na kuwa a blog yako mwenyewe ndani ya muda mfupi. kitabu hiki kinauzwa tsh elfu kumi na ni soft copy, kinatumwa kwa njia ya email.
Lakini kwa sababu wewe rafiki yangu umeshiriki semina hii ya blog, na napenda ukamilishe blog yako, nitakupa kitabu hiki kwa tsh elfu tano tu (5,000/=), kupata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu tano kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 kisha tuma email yako kwenye moja ya namba hizo pamoja na jina la kitabu na nitakutumia kitabu hicho mara moja. Ofa hii ya kupata kitabu cha blog kwa tsh elfu tano inaisha ijumaa tarehe 30/09/2016 hivyo chukua hatua sasa kama kweli unataka kuwa na blog nzuri.
Pia kitabu hiki kitakuwa kama rejea nzuri kwako, utakuwa na maarifa bora sana ya kufanyia kazi. Jipatie kitabu hiki leo.

Mpango wa pili; pata blog ya kitaalamu kwa ajili ya kuandika na kukuza hadhira yako.
Nimeandaa mpango maalumu kwa wale ambao hawataki kujihusisha kabisa na utengenezaji wa blog, tayari wao wana ujumbe wanataka kutoa au maarifa wanataka kuwashirikisha wengine lakini swala la kutengeneza na kurekebisha blog zao wenyewe hawaliwezi, na hawataki kujisumbua.
Nimetengeneza mtandao maalumu wa blog ambazo lengo lake ni kutoa maarifa na kufundisha, kuwafikia watu wengi na kuweza kutengeneza hadhira ya wasomaji. Blog hizi zitakuwa chini ya mtandao wa www.mtaalamu.net hii ina maana kwamba utakuwa na blog yako ambayo inaanza na mtaalamu.net, pia utakuwa na emaila yako inayoishia na mtaalamu.net kwa mfano blog yangu kwenye mtandao huu wa mtaalamu ni www.mtaalamu.net/makirita hapo nitaendelea kuwa nakushirikisha mambo mbalimbali kuhusu kutengeneza fedha kwa kutumia blog. Pia email yangu kwa mtandao huu ni makirita@mtaalamu.net

Kwa kujiunga na mtandao huu unapata blog yako ambayo inaanza na mtaalamu.net blog itakuwa na mwonekano rahisi (simple) na kusudi kubwa ni kuandika na kukuza hadhira. Pia utapata email yako ambayo utaweza kuitumia kwa mawasiliano na hata kuitumia kwenye email list yako. Utaunganishiwa blog yako na mitandao ya kijamii unayotumia, hivyo ukipost moja kwa moja inaenda kwenye mitandao hiyo. Na pia utatengenezewa na kuunganishiwa email list yako kwenye blog yako ili uweze kuikuza kupitia wasomaji wako.
Kupitia mtandao huu kazi yako itakuwa moja, kutoa maarifa na kukuza blog yako kuwafikia wengi, hizo kazi nyingine za kuhakikisha blog ipo hewani utaniachia mimi.

Unaweza kupata mfumo huu wa blog kwa kujiunga na kuwa unalipa ada ya tsh elfu 10 tu kila mwezi. Ni ada ambayo itakupa mengi na mazuri. Pia kwa kuwa na blog kwenye mtandao huu, utakuwa kwenye kundi maalumu la blog za wataalamu ambapo nitakuwa nawacoach bure kabisa. Nitakuwa nafuatilia blog ya kila mtu kwa ukaribu na kumhamasisha na kumshauri hatua bora za kuchukua.
Tuwasiliane sasa ili uweze kupata mpango huu wa blog, niandikie ujumbe kwa njia ya wasap kwenye namba 0717 396 253. Karibu sana.

Mpango wa tatu; karibu nikutengenezee blog yako mwenyewe kama unavyotaka iwe.
Kama unataka kuwa na blog yako nzuri na inayoendana na kile unachotaka, lakini huwezi kuitengeneza mwenyewe, naweza kukusaidia kufanya hivyo. Naweza kukutengenezea blog nzuri ambayo utaiendesha bure, ambayo itaishia blogspot.com au wordpress.com na pia naweza kukutengenezea blog nzuri ambayo unaimiliki mwenyewe, jina likaishia .com au .co.tz na ukawa na email zinazoendana na jina la blog yako. Blog ya kuendesha bure natengeneza kwa tsh elfu 50, ambapo unapata kila kituna blog ya kumiliki wewe mwenyewe natengeneza kwa tsh 300,000/= na kila mwaka utakuwa unalipia tsh 150,000/= kwa ajili ya jina la blog (domain name) pamoja na sehemu ya kuihifadhi kwenye mtandao (hosting space). Hapa utapata blog inayoendana na kile unachokitaka.

Pia kama utahitaji domain pekee au hosting ya blog yako tuwasiliane. Karibu sana kama utahitaji nikutengenezee blog yako pamoja na kuendelea kkushauri, nipigie simu kwenye namba 0717 396 253.

Mpango wa nne; karibu ujiunge kwenye kundi maalumu la wasap la PROFFESIONAL BLOGGERS.
Kama nilivyosema, kuwa mwenyewe ni rahisi sana kukata tamaa na kuishia njiani. Lakini ukiwa na kikundi cha watu ambao mnakwenda pamoja, inakuwa rahisi kupata hamasa na kuendelea hata pale unapokutana na changamoto au vikwazo. Pia itakuwa njia rahisi ya kuendelea kujifunza kila siku, kuuliza maswali pale ambapo unakutana na ugumu na kupata majibu ya kufanyia kazi.

Nimeanzisha kundi maalumu la bloggers nimeliita PROFFESIONAL BLOGGERS, kundi hili lipo kwenye wasap na linapokea watu wote ambao wameshaanzisha blog, au wana mpango wa kuanzisha blog. Katika kundi hili nitafundisha mengi ikiwa ni pamoja na uandishi wa makala zenye mvuto na kuhamasisha watu kuchukua hatua. Kujiunga na kundi hili unatakiwa kulipa ada ya kila mwezi ambayo ni tsh elfu 5 (5,000/=) pekee. Hiki ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na thamani kubwa utakayoipata ukiwa kwenye kundi hilo, na hapo unakuwa na nafasi ya kuweza kuniambia nitembelee blog yako na kukushauri zaidi.
Kwa wale ambao watakuwa wamejiunga na mtaalamu.net na kuwa na blog zao pale, hawatahitaji kulipa ada hii ya elfu tano, badala yake wataendelea kulipa ada ta tsh elfu kumi ili kuwa na blog zao za kitaalamu.

Kwenye kundi hili la wasap, nitakusaidia kuijengea nidhamu ya uandishi kama bado huna, maana hii ndiyo inawaangusha wengi.
Kujiunga na kundi hili, tuma ada ya mwezi tsh elfu tano kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 kisha tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253 wenye majina yako kamili na ujumbe kwamba unataka kuunganishwa kwenye kundi la PROFESSIONAL BLOGGERS. Karibu sana tuwe karibu.

Hii ndiyo mipango minne ya kuweza kukusaidia kusimama na blog yako. Chagua mpango wa blog utakaokufaa, kama ni kutengeneza blog yako mwenyewe, kuwa na blog kwenye mtandao wa mtaalamu (kitu ambacho nashauri sana) au nikutengenezee blog yako.
Kwa mpango wowote unaochagua, hakikisha unaingia kwneye kundi la wasap la PROFESSIONAL BLOGGERS, hapo ndipo elimu hii itakuwa inaendelea kila siku na maswali yako yatajibiwa kwa uhakika.

Karibu sana tufanye kazi pamoja, nikushirikishe kila ninachojua na kila ninachoendelea kujifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
www.kisimachamaarifa.co.tz

Faida Kubwa Ya Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano.

$
0
0
Watu wengi tumekuwa na mitazamo ambayo imekuwa haitusaidii hata chembe, kwani tumekuwa tunaamini katika kufanya kazi peke yetu pasipo kuwashirikisha wengine, lakini kufanya hivi ni sawa na kuzima moto kwa chafya, lakini ukweli ambao haufichiki ni kwamba ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wengine.

Hiyo ni falsafa nzuri sana husani katika suala zima la kuyasaka mafanikio. Pia katika suala zima la mafanikio tukumbuke ule usemi ambao husema ushirikiano ni nguvu na utengano ni dhaifu.

Ili kulielewa hili vizuri la kufanya kazi kwa shirikiano hebu angalia kisa hiki cha Yumba yumba. Tunaambiwa kwamba kupitia kisa hiki katika kisiwa fulani kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Michael.

Hata hivyo lakini watu wake walimfahamu zaidi kwa jina la Lipamila, kitu ambacho watu wengi walijifunza kutoka kwa mfalme huyo ni vile ambavyo alipenda sana kufanya kazi, hususani masuala ya kilimo, hasa katika kulima mbogamboga.


 Watu wengi sana katika kisiwa kile walifurahia sana kuwepo kwa mfalme yule mahala pale, kwani wengi wao walijifunza mambo mengi sana kutoka kwa mfalme.

Siku moja mfalme lipamila aliamua kuitisha mkutano mkubwa sana, alisisitiza kwa hali ya juu sana ya kwamba kila mtu siku ya mkutano huo,  alifanya hivo ili kuhakikisha ya kwamba kila mmoja ambaye alikuwepo katika kisiwa kile aweze kuhudhuria mkutano ule.

Hivyo taarifa zilisambaa katika kisiwa kile, ingawa kila mmoja alikuwa ana shauku ya kutaka kujua kunanini katika mkutano ule, kwani haijawahi kutokea kwa mfalme lipamila kuweza kusisitiza watu kuhudhuria mkutano ule kiasi kile.

Siku ya mkutano iliwadia na kila mmoja ambaye aliishi katika kisiwa kile alifika pasipo kukosa, ndipo mfalme akaanza kwa kusema "awali ya yote nipende kumshukuru Mungu kwa kuweza kutufikisha siku ya leo na hatimaye tumeweza kufika hapa"

Lakini jambo la pili nipende kuchukua fursa hii adhimu kwa kuwashukuru ninyi nyote kuweza kufika mahali hapa, pia nafahamu ya kwamba kila mmoja aliyo mahala hapa anawiwa kutaka kujua leo nitasema neno gani?

Lakini niwaambie ya kwamba huwezi kumuua chura kwa kumtupa ndani ya maji, maana yangu kuwaita hapa nataka nizungumze vitu ambavyo vitawasaidia katika maisha yenu ninyi nyote hivyo niwapongeze tena kwa kuweza kufika mahala hapa, 

Labda niende moja kwa moja katika lengo langu la kuwaita mahala hapa;

Jambo la kwanza ni kwamba nafahamu ya kwamba hapa tulipo kuna watu wa aina mbalimbali kutokana imani tofautitofauti na itikati za aina kadha wa kadha, lakini nataka niwaambie ya kwamba ili tuweze kufika mbali kimaendeleo na kimafanikio hatuna budi kuwa wamoja katika kufanya kazi kwa pamoja kama mchwa bila kujali tofauti zote ili tuweze kufika mbali kimafanikio, nasema hivi kwa sababu katika kisiwa hiki watu ni wamoja lakini hatuna ushirikiano katika mambo mengi sana.

Mfalme lipamila akashusha pumzi kidogo kisha akaendelea ..."Tunasema ya kwamba kisiwa chetu kinaogozwa na falsafa ya "HAPA KAZI TU" lakini kila mmoja amekuwa mbinafsi katika kufanya kazi lakini niwaambie ya kwamba ili kuona falsafa hiyo ni lazima kwa mmoja wetu tuweze kupeana mbinu mbalimbali ambazo zinatufanya tuweze kupata mafanikio kutokana na kuelimisha sisi kwa sisi, ifike mahali hata kilimo ambacho tunakifanya kiwe na tija, maana tukiwa na ushirikiano tunaweza kufika mbali. 

Tutaweka utaratibu ambao tulipama kilimo ambacho ni tofauti ni tulichozea, nimeweka utaratibu ambao tutahakikisha ya kwamba tutalima kilimo cha kisasa, yaani tutalima sehemu ndogo lakini mavuno yatakuwa mengine, nmefanya pia utafiti kuhusu masoko ya kuhusu mazao ambayo tutalima kwani tutauza sana sehemu nyinginezo endapo tutashirikiana pamoja.

Jambo jingine ambalo nilitaka kulizungumza nanyi siku ya leo ni kwamba nafahamu fika ya kwamba tatizo la ajira ni kubwa sana, 

"Je unataka kujua mfalme lipamila alizungumza nini katika suala la ajira?

Usikose mwendelezo wa makala haya juma lijalo siku kama hii ya leo, upate kitu kizuri cha kujifunza.

Makala hii imeandikwa na Afisa mipango Benson Chonya.

0757909042

Kitu Kimoja Kinachokuzuia Wewe Kuwa Na Blog Inayokuingizia Kipato.

$
0
0
Habari rafiki?
Wiki iliyopita tuliendesha mafunzo ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog. Tulijifunza mambo mengi na muhimu sana kupitia semina ile. Na mimi pia nilijifunza mengi kupitia maswali mbalimbali ambayo yalikuwa yanaulizwa na washiriki wa semina ile. Kupitia maswali yale, kuna kitu kimoja nimejifunza ambacho ni kikwazo kwa wengi kuanzisha na kukuza biashara zao. Katika makala hii tutaangalia kitu hicho kimoja na jinsi ya kuvuka kikwazo hiki ili kuwa na blog unayoweza kuitumia kutengeneza kipato.


Katika maswali mengi yaliyoulizwa na washiriki wa semina, swali moja lilikuwa linajirudia mara kwa mara. Swali hilo ni je nitaanzaje blog wakati bado sijafanya utafiti wa kutosha kwenye ile mada niliyochagua kuandikia? Kwa maana nyingine watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba inabidi usubiri na kujifunza sana mpaka ubobee ndiyo uweze kuwa na blog yako. Mwingine aliniambia kwamba kwa sasa anajifunza na kusoma vitabu vinavyohusiana na anachotaka kuandikia, hivyo akishakuwa tayari ndiyo ataanzisha blog.

Haya ni mawazo mazuri, lakini pia ni kikwazo kikubwa mno kwenye uanzishaji wa blog. Hii ni kwa sababu hakuna siku unayoweza kuamka na kusema leo nipo fiti kabisa, nimeshajua kila kitu na sasa naweza kuanzisha blog yangu. Nakuhakikishia siku hiyo haipo kabisa. Kila siku utajiona kuna kitu ambacho bado hujakijua vizuri, yaani kila siku kuna kitu cha kujifunza. Hivyo ukisema usubiri mpaka uwe tayari, utasubiri muda mrefu sana.

Changamoto nyingine kubwa ni kwamba vile unavyojifunza hubaki navyo kama vilivyo. Hii ina maana kwamba vingi unavyojifunza kila siku utavisahau, na hata kama utaandika mahali, bado kadiri siku zinakwenda utasahau. Utasahau vile vitu jinsi vilivyo lakini yale maarifa ya msingi utabaki nayo kwenye akili yako. Hivyo usifikiri kukisoma kitabu leo basi ndiyo umeshamaliza, siku siyo nyingi utasahau, hivyo utahitaji kukisoma tena, au kusoma vitabu vingine. Tangu nimeanza kusoma na kusikiliza vitabu, nimeshasoma na kusikiliza karibu vitabu 500, lakini siyo kwamba nakumbuka vitabu vyote karibu 500, ila yale maarifa ya msingi yaliyopo kwenye kitabu husika nakuwa nimeyabeba.

Hivyo basi rafiki yangu, ninachotaka kukuambia ni hiki, kama lengo lako ni kuwa na blog, basi wakati wa kuanzisha blog yako ni sasa, ni leo. Kama umeshajua ni vitu gani unataka kuandikia basi anzisha blog yako, hata kama hujafanya maandalizi ya kutosha. 
Ukishakuwa na blog ndiyo itakusukuma ujifunze kwa sababu unahitaji kuikuza blog yako. Na kadiri unavyokuwa na wasomaji wengi, ndivyo unavyozidi kusukumwa kujifunza na kuwapatia maarifa na taarifa bora. Kwa njia hii itakubidi ujifunze, tofauti na usipofungua kabisa na kusubiri uwe tayari, kwa sababu hutakuwa na cha kukusukuma kuwa tayari.

Hivi ndivyo ilivyo rafiki yangu, njia bora ya kujifunza kitu kwenye maisha ni kufanya, unajifunza mengi ukiwa unafanya kuliko unaposema unajiandaa. Pia nimekuwa nawaambia watu unaweza kuanza ukiwa unafikiria utaandika vitu fulani, lakini kadiri unavyokwenda ukajikuta unabadilika kulingana na taarifa unazokuwa unapata kila siku na wasomaji ulionao.

Hivyo rafiki yangu, kama unataka kuwa na blog, kuwa nayo leo au hutokuja kuwa nayo kabisa. Kuwa nayo leo kwa kuchagua kuanzisha blog na kuendelea kujifunza kadiri siku zinavyokwenda, au jiambie kwa sasa unajiandaa na utajiandaa maisha yako yote. Nawajua watu wengi ambao wanajiandaa kila siku na hawakaribii kuanza. Anza sasa na hayo mengine utajifunza kadiri siku zinavyokwenda.

MUHIMU;
Ofa ya kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG inaisha ijumaa tarehe 30/09/2016. Kitabu hiki kinakufundisha hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kutengeneza blog yako mwenyewe na kuikuza hatimaye kutengeneza kipato. Utakipata kitabu hiki kwa sasa kwa tsh elfu 5 tu, baada ya muda wa ofa kuisha bei itaendelea kuwa ya kawaida tsh elfu 10. Kupata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu 5 kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu.

Kuna nafasi ya kujiunga na kundi la wasap la PROFFESIONAL BLOGGERS, huku utajifunza mengi katika kuanzisha na kukuza blog yako. Pia utapata nafasi ya kuniuliza swali lolote kuhusu blog. Kujiunga na kundi hili unatakiwa kulipa ada ya tsh elfu 5 kila mwezi. Kujiunga tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253.

Pia kuna nafasi ya kuwa na blog ya kitaalamu kwenye mtandao wa MTAALAMU. Hapa unapata blog unayoweza kuitumia kukuza hadhira yako na baadaye kuigeuza kuwa sehemu ya kutengeneza kipato. Kwa kujiunga na mtandao huu unapata blog rahisi na iliyokamilika, email list, email yako maalumu na coaching kwenye swala la blogging. Kujiunga na mtandao huu tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253.

Karibu sana rafiki, kama unapata msukumo wa kuwa na blog ndani yako, basi kitu kimoja naweza kukuambia ni anza blog yako leo, hakuna siku bora kuliko leo na hakuna wakati utakuwa tayari kwa kila kitu. Anza na utakuwa unajifunza kadiri siku zinavyokwenda.
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani,
www.mtaalamu.net

Vielelezo 10 Muhimu Vinavyomtambulisha Kijana Na Kutambua Thamani Yake Hapa Duniani.

$
0
0
Habari Mpendwa Rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini hujambo kabisa na karibu tena ndugu msomaji katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza. Kila mtu ana faida yake hapa duniani aidha kwa kujua au kwa kutokujua. Tupo tofauti ndio maana kila mtu ana kitu cha kipekee au ana hazina ya kipekee ambayo bado haijagunduliwa. Wewe ni zawadi kwa wewe mwenyewe lakini pia wewe ni zawadi kwa dunia. Huu ndio wakati sahihi kwako kutoa thamani iliyoko ndani yako. Kila mtu ana deni katika hii dunia, ambalo anapaswa kulipa kabla hajaondoka duniani. Kama una tabasamu ujue kuna mtu anahitaji tabasamu lako, kuna mtu anahitaji upendo wako ambao kama ukiutoa atafarijika katika maisha hivyo utakua umeongeza thamani katika maisha yake.

Hivyo ndugu msomaji, napenda kukukaribisha katika somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza vielelezo muhimu vinavyomtambulisha kijana na kutambua thamani yake hapa duniani. Karibu mpenzi msomaji tuanze kwa pamoja mpaka mwisho wa somo letu. Vifuatavyo ni vielelezo muhimu vinavyomtambulisha kijana na kutambua thamani yake katika hii dunia.

1. Usemi; wewe kama kijana unasema nini juu ya maisha yako na watu wengine? Unasema nini na kuchukua hatua gani pale mambo yako na jamii yako kwa ujumla yanapokwenda vibaya? Unapomwona mwenzako anaangamia na madawa ya kulevya unasema nini? Unapomwona mwenzako amekata tamaa ya maisha wewe kama kijana unasema nini? Unachukua hatua gani? Unampatia ushauri sahihi au na wewe unaendelea kumsukumiza shimoni ili aendelee kutokomea kabisa? Wewe kama kijana unatakiwa kusema na siyo kukaa kimya na kuacha watu wakiangamia kama kuna sehemu inahitajika kusema ukweli sema na siyo kukaa kimya.

2. Mwenendo; unatakiwa kuwa na mwenendo mzuri katika maisha yako na maisha ya watu wengine. Ebu jiulize mwenendo wa maisha yako uliyokuwa nayo sasa ni mwenendo sahihi katika maisha yako? Mwenendo wako ni mzuri au mbaya? Jina lako likitajwa katika jamii watu wanasikia nini kutoka kwako au wanajifunza mwenendo gani kutoka kwako? Mtu akigugo jina lako katika mtandao atajifunza mwenendo au tabia gani hasi au chanya? Kijana unatakiwa kuwa na mwenendo mzuri kwenye maisha yako na jamii kwa ujumla.

3. Upendo; unaishi katika falsafa ya upendo katika maisha yako? Je unajipenda wewe mwenyewe? Kama jibu ni ndio unawapenda na wengine je unapenda kile unachofanya? Wewe kama kijana unatumiaje falsafa ya ujana wako ambayo ni kipindi cha sasa ukoje katika kugusa maisha ya wengine? Hivyo upendo ni kielelezo kinachomtambulisha kijana na kugundua nini thamani yake hapa duniani.
 

4. Imani; maisha ni imani. Lazima uwe na imani na yale unayoyafanya. Lazima kama kijana uwe na imani na maisha yako. Uwe na imani thabiti ya maisha ya kiroho. Unatakiwa ukue katika Nyanja tatu katika maisha yako nazo ni kiroho, kimwili na kiakili. Vitu hivi vitatu vinategemeana kama mizani au mafiga kama vile tunavyojua mafiga yanafanya kazi vema na kwa ustadi kama yakiwa matatu hivyo ukiwa na figa moja huwezi kupika chakula kikaiva. Hivyo ni muhimu kuwa na imani katika maisha yako.

5. Usafi; kijana anapaswa kuwa kielelezo cha usafi na siyo uchafu. Kuna baadhi ya vijana ukikutana nao huwezi kukaa nao karibu kwa sababu wananuka jasho, nguo chafu, yaani wamechoka wamechakaa, wengine wananuka sigara, wengine wananuka pombe. Hivyo basi, tabia kama hizi huwa zinaathiri watu wengine. Kama wewe ni kijana unatakiwa kuwa msafi na nadhifu wa mwili wako. Unatakiwa kujitunza na kujithamini mwili wako ni ndio nyumba yako yaani mahali wewe unaishi usiruhusu kila mtu kuuchezea mwili wako jitunze na jithamini. Kula vizuri, fanya mazoezi, kiufupi kula mlo kamili na usiruhusu mwili wako kuwa kama siti ya daladala au taulo la nyumba ya wageni kila mtu anayekwenda analitumia. Kuwa msafi wa ndani na wa nje wa mwili wako. Mtu akikuangalia uonekane kweli kijana na siyo mzee. Kuwa nadhifu na maridadi kama kielelezo cha usafi.

6. Bidii; hakuna kitu kinachoweza kutokea katika maisha yako kama wewe mwenyewe huna bidii katika kitu hicho. Kama wewe ni mwanafunzi unasoma hakikisha unaweka bidii katika masomo yako. Kama wewe unafanya kazi weka bidii katika kazi yako unayofanya. Juhudi ni muhimu sana katika maisha yako, kwenye chochote unachofanya. Hakuna kitu kirahisi na ingekuwa rahisi kila mtu angefanya. Kuna usemi mmoja unasema hivi ‘’ heri uzee kuliko uzembe’’ kama huna bidii katika maisha yako wewe ni mzembe na wazembe hawahitajiki katika karne hii. 

Hivyo basi, bidii ni kielelezo tosha cha kijana mahali popote pale ambapo kijana yupo. Ukiwa eneo la kazi na wewe ni kijana jaribu kufanya kazi tofauti ongeza thamani na uoneshe tofauti kuwa kweli wewe ni kijana na siyo mzee. Uwe sehemu ya mabadiliko chanya mahali ulipo.

SOMA; Kama Wewe Ni Kijana Unayataka Mafanikio,..Huu Ndio Ukweli Unaotakiwa Kuujua Ili Kufanikiwa.

7. Kusoma; kijana unatakiwa usome katika maisha yako siyo kukaa tu na kujishughulisha na mambo ambayo hayaongezi thamani katika maisha yako. Mwanafalsafa Jim Rohn aliwahi kusema kosa chakula lakini usikose kusoma kitabu. Je wewe kama kijana mara yako ya mwisho kusoma kitabu ni lini? Huenda hata ulivyokua shuleni, au chuoni hukujisumbua kusoma vitabu badala yake ulikuwa unatumia tu’ notes’ za mwalimu mpaka unamaliza. Kama wewe unaitwa kijana kuanzia leo anza kujifunza, anza kutafuta maarifa katika maisha yako kwani hujui ya kuwa maarifa ni chakula cha ubongo wako? Mbona wewe unakula kila siku halafu huilishi akili yako? Hujui ya kwamba unatakiwa kukua katika sehemu tatu yaani kiakili, kiroho na kimwili? Anza kusoma acha kutafuta sababu zisizokua na maana.

8. Onya; moja kielelezo cha kijana ni kuonya. Kama unaona watu wanafanya mambo na kwenda kinyume na maadili katika jamii unaonya? Huwezi kumuonya mtu juu ya jambo Fulani wakati na wewe ni mshirika wa mambo hayo. Chochote unachotaka kuonya hakikisha kwanza wewe uko vizuri. Unapomuonesha mwenzako kidole kimoja angalia vidole vingapi vinakurudia wewe? Tumia ujana wako kama kielelezo cha kuonya. Kama uko katika familia yako unaona kuna mtu anaenda kinyume mpe onyo lake kwa kumwambia ukweli yaani wewe onya wala usifunge macho. Kuwa mwaminifu katika maisha yako kwani uaminifu utakulipa.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Kijana Wa Kitanzania(kama una miaka kati 20 mpaka 30 soma hapa)

9. Kufundisha; hapa naongelea kwa kijana yoyote mwenye kipaji au karama Fulani katika maisha yake. Je wewe una kipaji? Kama una kipaji ulichopewa bure je na wewe unakitumiaje ili uweze kuwasaidia wengine? Kama una kipaji chako hakikisha unawafundisha wengine hicho kipaji chako. Hujui ya kwamba wewe ni zawadi kwa wewe mwenyewe na wewe ni zawadi kwa dunia nzima? Fundisha wenzako kile unachojua katika akili yako ambacho kitakua msaada kwa wengine. Kama una maarifa uliyoyapata darasani ni wakati wako sasa wa kufundisha dunia kile unachojua. Usiwe mchoyo au mbinafsi katika maisha yako kama una kitu cha msaada wafundishe wenzako kabla hujaondoka na zawadi uliyonayo. Una kipaji na karama ambayo bado hujaigundua na kuitoa duniani ninachokuomba usife na hazina uliyonayo itoe ili na wengine wajifunze.

10. Uadilifu, nidhamu na uaminifu; katika zama hizi za taarifa uadilifu, uaminifu na nidhamu umekua adimu sana. Uaminifu ni kutekeleza kile unachoahidi au kuwaambiwa watu. Kama unawaambia watu kuwa utawafanyia kitu Fulani hakikisha unatekeleza ahadi yako. Watu wamekosa uaminifu siku hizi hivyo unatakiwa umchunguze mtu kabla ya kufanya naye kitu fulani. 

Ukiwa na uaminifu utakulipa sehemu yoyote ile hata kama hujuani na mtu mtaweza kufanya kazi na mambo yakaenda vizuri. Pia unatakiwa kuwa mwadilifu yaani usimamie misingi uliyojiwekea katika maisha yako. Kama umeamua kuishi katika kusimamia ukweli basi simamia ukweli mpaka pumzi yako ya mwisho hapa duniani. Vile vile unatakiwa kua na nidhamu kwani nidhamu ni daraja la mafanikio katika maisha yako hivyo kuwa na nidhamu thabiti katika maisha yako.

SOMA; Ushauri Muhimu Kwa VIJANA, Okoa Miaka Hii Kumi Ambayo Utaipoteza.

Kwa kutamanisha, unatakiwa kudumu katika yote uliyojifunza leo. Kudumu maana yake ni kusimamia katika yote uliyoamua kufanya. Kama umeamua kusimamia ukweli basi dumu katika falsafa hiyo ya kusimamia ukweli. Kama wewe ni kijana usisubiri upewe ruhusa katika maisha kwani maisha ni muda na ni mafupi lakini ni marefu kama tu ukitumia muda wako vizuri hapa duniani. Unaweza kufanya na kwenda mbali zaidi kuliko mtu yeyote katika familia yako una uwezo mkubwa sana jaribu kuutumia leo.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leo ndiyo siku ya mwisho ya ofa ya kitabu cha blog, usikose nafasi hii ya kipekee.

$
0
0

Habari rafiki?
Ni matumaini yangu kwamba uko vizuri na unaendelea kuweka juhudi ili kuboresha maisha yako zaidi. Hongera sana kwa hatua hiyo unayochukua.

Naomba kuchukua nafasi hii kukukumbusha rafiki yangu ya kwamba leo ndiyo siku ya mwisho ya kupata ofa ya kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Leo ndiyo siku ya mwisho kukipata kitabu hiki kwa tsh elfu tano pekee (5,000/=) badala ya tsh elfu kumi ambayo ndiyo bei ya kawaida ya kitabu hiki.


Kama ulihudhuria na kujifunza kupitia semina ya blog niliyoendesha wiki iliyopita, basi ni muhimu sana uwe na kitabu hiki. Kwa sababu kitakuwezesha kutumia vizuri masomo yale uliyopata kuhusu blog. Pia kitakuwa rejea yako nzuri katika fursa hii ya kutengeneza kipato kwenye mtandao kwa kutumia blog.
Jambo moja ambalo mpaka leo sijawahi kulielewa ni hili rafiki yangu, pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa mtu kuchukua hatua, kesho ataniandikia rafiki yangu kwamba naomba unipe kwa ofa kwa sababu nilisahau, au sikuwa na uhakika. Marafiki wengine wataniambia hawakuwa na mtandao hivyo hawakupata taarifa kwa wakati. 

Naomba nikushauri hili rafiki yangu, hata kama huna mpango wa kufungua blog sasa hivi, ila unafikiri huko mbeleni utakuja kuwa na blog, basi nunua kitabu hiki leo. Hata kama huna uhakika kama utakuja kuwa na blog, mawazo yanakujia lakini huna uhakika, nunua kitabu hiki leo, kwa sababu wakati utakapokuwa na uhakika utakuta ofa hii imeshapita. Na kwa kununua sasa, hakuna chochote unachopoteza, kwa sababu kitabu hakiharibiki, utakitunza na kukisoma wakati ukiwa tayari.

Kukipata kitabu tuma fedha tsh elfu 5 (5,000/=) kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253. Kisha tuma ujumbe wenye email yako kwa usahihi kwenda kwenye moja ya namba hizo na utatumiwa kitabu muda huo huo uliotuma fedha. Chukua hatua sasa rafiki yangu.

Naomba nikusisitize tena rafiki, una muda leo, na tena usisubiri leo utasahau, sasa hivi unaposoma hapa, chukua hatua. Nakusisitiza sana kwa sababu kila mara watu wamekuwa wanakuja baada ya muda kuisha na wanakosa nafasi hizi nzuri. Sitaki wewe uikose kama unaitaka kweli, hivyo nakusisitiza chukua hatua sasa.
Kitabu hiki kina maelekezo ya kila hatua ya kutengeneza na kuendesha blog yako. Kina maelezo kwa picha na kwa lugha rahisi ya kishwahili, huhitaji kuwa na elimu yoyote ya mambo ya kompyuta au mtandao ndiyo uweze kutumia kitabu hiki. Kila kitu kimeelezwa kwa urahisi mno, ni wewe tu kuchukua hatua.

Nikutakie wakati mwema rafiki yangu, lakini hakikisha umepata kitabu chako kabla ya siku ya leo kuisha.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kupata Milioni Ya Ziada Kila Mwezi Hata Kama Huna Mtaji Wa Kuanzia.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Unajua leo ni lini? Leo ni tarehe 01/10/2016 hii ni tarehe mpya kabisa ya mwezi mpya ambapo mwaka unaelekea ukingoni. Leo tumeianza ngwe ya mwisho kabisa ya mwaka huu 2016. Ni ile robo ya nne ya mwaka 2016 tumekwenda kuianza leo. Unapoona tumefika ngwe ya mwisho, ni dalili kwamba mwaka siyo wetu huu. Mwaka unakaribia kutuaga. Hivyo basi kwa chochote ambacho ulikuwa umepanga kutimiza mwaka huu, ni muhimu sasa ukabadili kila mbinu kama bado hujaanza hata kukifanya.
Kwa wale ambao tulishiriki pamoja semina ya kuweka malengo mwaka huu 2016, na kuweka malengo ambayo walinishirikisha, tafadhali niandikie email kunijulisha umefika wapi na kama una changamoto yoyote ambayo inakuwa tishio kwako kufanikisha malengo yako.


Pia kwa wale ambao walijiunga kwenye program ya SUPERCOACHING, tuwasiliane ili kuboresha mikakati ambayo tulijiwekea kama bado mambo hayajakaa sawa kama tulivyokuwa tumepanga yawe. Kitu kimoja ambacho nakiamini ni hiki, chochote tunachotaka kwenye maisha yetu, kipo ndani ya uwezo wetu, ila tunahitaji kufanya zaidi ya uwezo wetu ili kuweza kukipata.
Rafiki yangu sasa nikukaribishe kwenye makala yetu ya leo ambapo tutakwenda kujadili jinsi ya kupata milioni ya ziada kila mwezi hata kama huna mtaji wa kuanzia kwa sasa. Lakini kabla hatujaingia huko, naomba nikumbushe haya machache.

Jana ilikuwa siku ya mwisho ya kupata ofa ya kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, watu wote ambao walituma fedha na ujumbe wenye email zao walitumiwa kitabu kile kwenye email zao. Kama ulituma fedha na hujapata kitabu kwenye email yako basi tuma ujumbe wenye meseji ya udhibitisho wa kutuma fedha pamoja na email yako kisha utatumiwa kitabu mara moja. Unaweza kutuma ujumbe huo kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887. Kama hukutuma fedha jana ili kupata kitabu hiko, unaweza kutuma leo tsh elfu 10 kwenye moja ya namba hizo pamoja na email yako kisha ukatumiwa kitabu hiko. Ofa imeisha jana rafiki yangu, usitume tena elfu tano, tuma elfu kumi. Karibu sana.

Kuna jambo moja muhimu naomba niliongelee kabla sijaingia kwenye mada ya leo. Jana mmoja wa msomaji na rafiki yetu alinipigia simu. Alikuwa na malalamiko kwamba tangu amejiunga na mtandao huu hajapokea mafunzo badala yake ni taarifa za kutuma hela ya kitabu tu. Nilikubaliana naye kwamba kwa wiki hii nimekuwa nawakumbusha wale wote ambao hawajapata kitabu kufanya hivyo. Lakini wiki iliyopita, kila siku kwa siku saba niliendesha semina ya blog bure kabisa ambayo kila mtu alikuwa na nafasi ya kuweza kushiriki semina ile. Na tangu mwaka 2013 nimekuwa natuma email kwa ninyi marafiki zangu, siyo kweli kwamba natuma email za kuuza vitu peke yake.

Kwa hiyo nilimshauri kama anaona anachopata ni matangazo pekee, basi akifika chini kwenye email kuna sehemu imeandikwa UNSUBSCRIBE, ukibonyeza hapo basi hutapata tena email yoyote kutoka kwangu. Na hili pia nataka niliseme kwa marafiki zangu wengine wote, kitu ambacho nakithamini mno ni muda wako, kuliko hata fedha yako. Sipendi kupoteza muda wako, na ndiyo maana najitahidi kadiri ya uwezo wangu kukuandalia maarifa bora, na kuhakikisha unayapata. Kama kwa namna yoyote utaona unapata matangazo kuliko unavyopata maarifa, basi shuka chini kabisa kwenye email, utaona sehemu imeandikwa UNSUBSCRIBE, ukibonyeza hapo unakuwa umejiondoa kwenye mfumo huu wa email. Sipendi nikupotezee muda wako, napenda uwe hapa kama kuna thamani unaipata kwenye maisha yako, kama hakuna basi hakuna sababu ya wewe kupoteza muda.

Baada ya wiki hii ya kuhakikisha kila rafiki yangu mwenye nia amepata kitabu cha blog, kuanzia kesho tutarudi kwenye ratiba yetu ya kawaida kwenye mfumo wa email. Kila jumapili tunakuwa na makala ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, jumanne, ONGEA NA COACH, na alhamisi, kwa mwezi wote huu wa kumi nitakuwa nakukumbusha kuhusu semina ya MILIONI YA ZAIDA, ambayo nitakupa maelezo zaidi hapo chini. Hivi ndivyo tutakavyokwenda kwa mwezi huu wa kumi. Karibu sana rafiki yangu.

Pole rafiki, nimeandika mengi lakini muhimu. Karibu kwenye ujumbe wetu wa leo ambapo nakwenda kukueleza na kukukumbusha kuhusu semina ya MILIONI YA ZIADA.
Tumekuandalia semina inayoitwa MILIONI YA ZIADA, hii ni semina ambayo itafanyika kwa njia ya kuhudhuria kwenye ukumbi, tofauti na semina zangu ulizozoea. Kwenye semina hii walimu wanne, ambao wengine taarifa zao nitakuletea, tutakufundisha na kukupa mbinu za kuweza kuyatumia mazingira uliyopo sasa, kutengeneza milioni ya ziada kila mwezi.

Hii ni semina ambayo mtu yeyote ambaye yupo makini na maisha yake hapaswi kuikosa. Kwa sababu kama ambavyo wote tumekuwa mashahidi, kadiri siku zinavyokwenda, mambo yanazidi kuwa magumu. Hii ina maana kwamba, mbinu tulizokuwa tunatumia awali kwa sasa haziwezi kuleta matunda mazuri tena. Sasa tunahitaji kuja na mbinu mpya kama kweli tunataka kupata matokeo bora. Kupitia semina hii utajifunza mbinu hizo mpya ambazo utaweza kuzitumia kuboresha maisha yako, kwa kujihakikishia kipato cha ziada.

Semina hii itafanyika jumapili ya tarehe 30/10/2016 pale BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO PLAZA. Tafadhali sana rafiki yangu, iwekee alama hiyo tarehe na usipange tukio jingine lolote katika tarehe hiyo isipokuwa kuhudhuria semina hii ya kipekee sana kwako. Na kama upo mkoani, anza kuweka ratiba yako vizuri ili uweze kusafiri na siku hiyo ya jumapili ya tarehe 30/10/2016 uwe dar kwa ajili ya kushiriki semina hii.

Ada ya kushiriki semina hii ni tsh 35,000/= na hapa ndipo pazuri sana. Nasema ni pazuri kwa sababu watu wengi wamekuwa wanatumia ada kama kigezo cha kushindwa kushiriki semina. Hivyo ili wewe rafiki yangu usikose semina hii nzuri ya kipekee, ili usiniandikie kwamba natamani kushiriki semina hiyo ila fedha sina, nimekuandalia mpango mzuri kwako ili kuweza kupata fedha hiyo.
Mpango huu utakuchukua siku 30, kuanzia lei tarehe 01 mpaka siku ya semina tarehe 30/10/2016, unachohitaji ni kila siku kuweka akiba ya angalau tsh 1,500/= unaweza hata kuweka tsh 2,000/= lakini hakikisha haipungui 1,500/=. Kila siku fanya hivi, swali ni je unawezaje kufanya hivi?

Anza kwa kupunguza gharama zozote ambazo umekuwa unaingia ambazo siyo za msingi. Mfano badala ya kununua maji ya kunywa kila siku, unaweza kuwa na chupa yako nzuri ya kubebea maji. Badala ya kunywa bia au soda kila siku, weka fedha hiyo akiba. Badala ya kununua vocha kila siku ambazo huzitumii kwa uzalishaji tunza fedha hiyo. Jaribu kwa siku hizi 60, uone unavyoweza kuokoa 1,500/= kila siku, utaona jinsi ambavyo maisha yako yataanza kubadilika.

Fanya hivi kila siku, na hakika utapata ada ya kushiriki semina hii ya kipekee. Hata kama hutaweza kushiriki semina hii, au hutashiriki kwa namna yoyote ile, bado nakusihi sana ufanye zoezi hilo, litakusaidia kuanza kushika hatamu ya maisha yako.

Semina ni tarehe 30/10/2016 rafiki, itunze tarehe hiyo. Ada ya kushiriki semina hii ni tsh 35,000/= rafiki, anza kuiandaa leo tarehe 01. Nina imani kubwa tutakutana kwenye semina hii na kwa pamoja tuweke mikakati ambayo italeta mapinduzi makubwa kwetu kifedha.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

NYEUSI NA NYEUPE; Unafiki Kuhusu Michango Ya Sherehe, Kwa Nini Kila Mtu Anailalamikia Lakini Bado Anatoa.

$
0
0
Habari rafiki yangu?
Karibu kwenye safu yetu ya makala za NYEUSI NA NYEUPE zinazokujia kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Kupitia makala hizi tunalichambua jambo kwa kina ili kujua ukweli na uongo wake uko wapi. Kisha mwishoni tunashauriana namna bora ya kuliendea jambo hilo au maamuzi bora ya kufanya.

Leo tunakwenda kuangalia kwa kina kuhusu michango ya sherehe ambao ni utaratibu uliojenga mizizi kwenye jamii zetu. Ni jambo ambalo limekuwa na unafiki mwingi sana, kila utakayekutana naye analalamikia michango hii kuwa mingi, lakini bado watu wanaendelea kutoa michango hii. Je ni nini kimejificha hapa, ni ukweli upi na uongo upi ambao hatujaujua bado? Karibu tujifunze kwa pamoja leo


Kuhusu michango ya sherehe.
Ni utaratibu wa kawaida kwenye jamii zetu ambapo pale mtu anapofanya sherehe, anawaomba watu wamsaidie kuchangia gharama za sherehe hiyo. Na kwa kuwa ni jambo zuri, basi watu wamekuwa wakitoa michango yao na baadaye kuhudhuria sherehe hiyo.

Sina hakika sana kama michango hii imekuwa asili yetu tangu zamani au tumeiga. Kwa sababu kwa kabila na kijiji nilichotokea mimi, zamani sikuwahi kuona watu wakichangishwa fedha kwa ajili ya sherehe. Sherehe nyingi zilikuwa zinafanyika majumbani na mwaliko ulikuwa kwa wote. Kitu ambacho nilikuwa naona ni watu kusaidia kile wanachoweza. Kwa mfano kama mtu ana viti basi anaazimwa, mwenye sufuria kubwa za kupikia na sahani za kulia anaazimwa, mwenye ujuzi wa kupika basi alijitolea kupika kwenye sherehe hizi. Na hata mwenye ndizi na aina nyingine za vyakula alijitolea ili sherehe iweze kwenda vizuri.

Lakini tangu sherehe zimeanza kufanyika kwenye kumbi kubwa za kisherehe, na vyakula kuanza kupikwa na wapishi wa kitaalamu, na vinywaji kuwa vya kisasa na siyo vya kienyeji, gharama za sherehe zimekuwa zinapanda kila mwaka. Kila mwaka kiwango cha kuchangia kwenye shere kimekuwa kinaongezeka. Na hata aina ya uchangishaji nayo pia imebadilika. Zamani mtu alikuwa anaweza kutoa kiwango chochote, kadiri ya uwezo wake na akahudhuria sherehe hiyo. Kitu ambacho ni chema sana, unakwenda kuwashuhudia watu wako wa karibu kwenye sherehe yao muhimu, na kuwaunga mkono pia. Lakini miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utaratibu wa kupangiwa kiwango cha kutoa, kwamba ukitoa chini ya kiwango fulani hupewi kadi ya kuhudhuria sherehe hiyo, bali utapewa asante tu. Yaani unaombwa mchango, halafu unalazimishwa ni kiwango kipi lazima uchangie.

SOMA;Hizi Ndio Aina Tano Za Dharura Za Kifedha(Angalizo; Michango Ya Sherehe Sio Mojawapo)

Aina za sherehe ambazo zinachangiwa pia imekuwa inabadilika karibu siku zinakwenda. Zamani tulizoea harusi pekee ndiyo zinachangiwa, kwa sababu ilionekana ni tukio kubwa. Lakini sasa hivi mpaka kipaimara watu wanachangishwa, mahafali watu wanachangishwa, na imeenda mbali mpaka kusherekea tarehe ya kuzaliwa pia watu wanachangishwa.
Sipati picha siku zijazo michango hii itafika mpaka wapi.

Kwa nini michango ya sherehe.
Zamani lengo la michango hii ilikuwa kuwaunga mkono ndugu jamaa na marafiki zetu pale ambapo wanafanya sherehe ya jambo muhimu kwa maisha yao. Hivyo tunaungana nao kwa kuwapa kile ambacho kipo ndani ya uwezo wetu, ili kuwawezesha kutimiza lengo lao. Ilikuwa ni hali ambayo watu wanajitoa kweli kweli, na wala hawalalamiki kuhusu mzigo wa michango hiyo. Au kuhoji kama wamepata huduma sawa na michango yao.
Lakini sasa hivi hatujui tena hata michango hii ya sherehe lengo lake hasa ni nini. Kwa sababu michango inakuwa mikubwa na hata utoaji wake umekuwa wa kulazimishwa zaidi kuliko hiari ya mtu mwenyewe.

Wapo ambao wanataka kufanya sherehe kubwa ili waonekane nao wamefanya sherehe kubwa, waweze kupata vipindi kwenye tv na iwe gumzo. Wapo ambao wanataka wapete kianzio cha maisha kupitia michango hiyo ya sherehe, ambapo linatengwa fungu la zawadi, hasa kwenye sherehe za harusi. Yapo malengo mengine mengi.

Kuna lengo moja ambalo hutasikia likisemwa popote, lakini watu wamelibeba kwenye mioyo yao. Watu wanachangisha watu kwenye sherehe kwa sababu na wao waliwachangia. Hili ni zito na hakuna atakayesema wazi, lakini wengi wanasukumwa na hili, mtu anachangisha watu kwa sababu ameshachangia sana wengine. Rafiki yangu mmoja amewahi kuwaambia wazazi wake kwamba hatafanya sherehe kubwa hivyo hahitaji kukusanya michango ya wengine, wazazi wake hawakukubaliana na yeye, kwa sababu wao wameshawachangia sana wengine, ni zamu yao na wao wachangishe wengine. Linaweza kuwa wazo zuri, nilichanga kwa wengine na sasa ni wakati wangu kuchangiwa, lakini wanasahau kwamba wanamweka kijana wao kwenye mzigo wa maisha yake yote, kwa sababu ukishachangiwa, huna namna utachangia wengine maisha yako yote.

Sababu nyingine inayoweza kuwa ya ukweli au uongo ambayo watu wanatumia ni kwamba ni heshima kutoa mchango wa sherehe. Eti kwamba kama utaandaa sherehe yako kwa gharama zako mwenyewe, halafu ukawaalika watu, wataona kama ni dharau, watu wanapenda kuchangia, inawapa heshima. Sitasema mengi hapo, inaweza kuwa ukweli au inaweza kuwa uongo, kulingana na mazingira uliyopo. Lakini kwa ujumla ni uongo.

Kwa nini unafiki kwenye michango hii ya sherehe?
Kutokana na uzito huu ambao michango ya sherehe imekuwa inapewa kila siku, watu wamekuwa wanailalamikia mno. Unakuta mtu ana kadi zaidi ya kumi kwa mwaka, ambapo akipiga mahesabu kwenye kadi hizo ni fedha kubwa mno kwake. Analalamikia hilo lakini analazimika kuchangia kwa sababu hana namna ya kukwepa. Hapa ndipo unafiki mkubwa unapoanzia.

SOMA; KAMA UNASHANGAA ‘BIG RESULT NOW’ HUJAYAANGALIA MAISHA YAKO VIZURI.

Sasa tuangalie NYEUSI na NYEUPE za kwa nini watu wanalazimika kuchangia japo haitoki ndani ya mioyo yao.

1.     Kuwa sehemu ya jamii.
Watu wengi wamekuwa wanalazimika kuchangia michango hii ili na wao kuwa sehemu ya jamii. Wanaogopa wasipochangia basi wataonekana wa tofauti kwenye jamii hivyo wanakazana kuchanga ili nao wawe sehemu ya jamii. Jamii ni kifungo cha watu kwenye mambo mengi, watu wanalazimika kufanya vitu siyo kwa sababu wanapenda, ila kwa kuwa kila mtu anafanya.

2.     Mategemeo ya kuchangiwa mbeleni.
Hili pia limekuwa linawafanya watu wachangie, kwa sababu wanatarajia mbeleni na wao wataomba kuchangiwa. Niliwahi kuongea na mtu fulani ambaye alikuwa analalamika michango mingi, nikamwambia kwani ni lazima uchangie? Akaniambia nina watoto wengi ambao sasa wameshakuwa vijana, wakianza kuoa na kuolewa nani atanichangia? Hivyo watu wanajiingiza kwenye kifungo ili na wao wachangishe watu baadaye.

3.     Kwa sababu tayari wao wameshachangiwa.
Yaani ukiangalia haya yote yanakwenda pamoja, na yote yanamfunga mtu kwenye mzunguko huu wa michango. Kama tayari ulichangiwa kwenye sherehe yako, utamkataliaje mtu anayekuletea kadi yake ya mchango, na unajua kabisa alikupa mchango wakati wa sherehe yako? Hiki ni kifungo ambacho wengi wamenasa huko.
Hizi ni sababu kuu ambazo zinawafanya watu kuwa wanafiki kwenye michango ya sherehe, wanachangia lakini wanakuwa na malalamiko na manung’uniko makubwa kuhusu michango wanayotoa.

Kama ilivyo kwenye kipengele hiki cha NYEUSI NA NYEUPE, sikuachi bila ya hatua za kuchukua. Sasa tuangalie hatua za kuchukua ili kuondokana na unafiki huu wa michango ya harusi.

1.     Chagua ni watu gani ambao utawachangia, weka vigezo.
Achana na sababu ya kijamii ambayo inawaweka watu wengi kwenye kifungo, wewe chagua ni watu gani ambao utakuwa tayari kuwachangia kadiri ya uwezo wako bila a kuwa na manung’uniko kwenye nafsi yako. Weka vigezo vyako vya kuchagua aina hiyo ya watu utakaowachangia, labda familia na ndugu wa karibu, marafiki wa karibu na watu wengine ambao wanapokuambia kuhusu sherehe zao, moja kwa moja unasukumwa kuwachangia na siyo mpaka ulazimishwe. Ukishakuwa na aina hii ya watu, wengine hata usifikirie mara mbili, usichangie.
Yaani kwa kifupi ni hivi, kama unapata malalamiko kwenye nafsi yako pale mtu anapokupa kadi yake ya mchango, basi usichangie.

2.     Kama tayari ulishawachangisha wengine.
Hapa tayari umeshajiweka kwenye kifungo, kama uliwachangisha wengine, na wao wanategemea wewe uwachangie. Na bora ingekuwa wanategemea uwachangie kwenye sherehe zao tu, mbaya ni kwamba watategemea uchangie hata kwenye sherehe za watu wao wa karibu. Hivyo hapo kunakuwa hakuna mpaka.
Unachoweza kufanya hapa ni kuweka mpaka, unawajua walikuchangia, basi wachangie wao wanapokuwa na shughuli inayowahusu wao moja kwa moja, nje ya hapo usichangie. Ukiweka kigezo hiki taratibu utajiondoa kwenye kifungo ambacho tayari umeshaingia.

SOMA; USHAURI; Kuendelea Na Masomo, Kuoa Au Kujenga, Kipi Bora Kufanya Kwanza?

3.     Kamwe, kamwe, kamwe, usiwachangishe watu kwenye sherehe yako.
Kama bado hujawachangisha watu, usiwachangishe, haya ni maamuzi bora kabisa unaweza kufanya kwenye maisha yako. Usijali wazazi, ndugu, jamaa na hata marafiki wanasema nini, usichangishe kabisa. Badala yake andaa sherehe inayoendana na uwezo wako na igharamie wewe mwenyewe, au na familia yako. 
Lakini siyo kuanza kuhangaika na kila mtu akuchangie.
Na kingine muhimu sana, usije kwa namna yoyote ile kuchukua mkopo kwa ajili ya kufanya sherehe, yaani hata ushawishike kiasi gani, usije kufanya jambo hilo hata kidogo. Ni afadhali usifanye sherehe kabisa kuliko kuifanya kwa fedha za kukopa.

Hili ni shimo ambalo nimekuwa naona watu wanajipeleka wenyewe, wanapopanga sherehe, wanatengeneza bajeti kubwa na kutegemea watu watachangia. Sherehe inapokaribia, watu wanakuwa hawajatoa michango ya kutosha bajeti ile, hivyo wanachofanya ni kuchukua mkopo kuhakikisha sherehe inafanyika kama ilivyopangwa. Hapo mtu anakuwa amejiingiza kwenye mashimo mawili, shimo la kwanza michango, shimo la pili mkopo.

Unafiki huu wa michango ya sherehe umekuwa ni wa pande zote mbili, kwa wanaochanga na wanaochangisha. Umefika wakati sasa kujiondoa kwenye vifungo hivi na kuishi maisha ya uhuru. Kwa sababu wengi wanaendelea na hili siyo kwa sababu wanapenda, bali kwa sababu hawajui jinsi gani ya kutoka.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

USHAURI; Kama Wateja Hawaji Kwenye Biashara Yako, Wafuate Kule Walipo.

$
0
0
Habari rafiki?
Karibu kwenye makala yetu ya ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia malengo ya maisha yetu. Kupitia makala hizi za ushauri tunapeana maarifa na mbinu za kuweza kufikia malengo na mipango ya maisha yetu licha ya changamoto tunazokutana nazo kila siku. na kama tunavyojua, changamoto ni sehemu ya maisha yetu.

Leo tunakwenda kushauriana kuhusu wateja wa biashara. Watu wengi wanapofunga au kupanga kufungua biashara, huwekeza muda mwingi kufikiria wazo la biashara na mtaji wa kuanza biashara hiyo. Lakini yapo maeneo mengine mengi ya biashara ambayo watu wamekuwa hawayafikirii wakati wanaanza. Hili hudhihirika pale biashara inapoanza na changamoto kuanza kuonekana.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Watu wengi wamekuwa wanafikiria kwamba ukishakuwa na biashara basi wateja watajaa kwenye biashara yako kununua. Hivyo wanachotafuta ni kuwa eneo zuri ili waonekane na wateja wa biashara hiyo. Mbinu hii ilifanya kazi zamani, ambapo wafanyabiashara walikuwa wachache. Kwa sasa watu wanaofanya biashara kama yako ni wengi, hivyo kutumia mbinu ya wakipita wanione, hutafanikiwa kwa sababu kabla hawajafika kwako wameshawaona wengine wengi kama wewe. Hivyo kama kigezo chao cha kununua ni kuona pekee, atanunua kwingine na siyo kwako.
Ipo njia ya kuwafanya wateja waje kununua kwako hata kama kuna wafanyabiashara wengine ambao ni wa karibu zaidi kwa mteja wako. Njia hii ndiyo tutajifunza kwenye makala yetu ya leo. Kabla hatujaingia kwenye njia hiyo, hebu tupate maoni ya msomaji mwenzetu;

Ninatoa huduma ya Secretarial kama biashara, ninavitendea kazi vya kutosha lakini wateja nilio nao ambao ni wakudumu wanapenda sana kukopa na hawalipi kwa muda wengine kutolipa kabisa. Kuna nyakati wateja wanachanganyia wakati mwingine nafungua nafunga hakuna kabisa mteja au unapata 2,000/ 1,000/ 200 au hakuna kabisa na nina miaka 5 sasa kasoro tangu nianze kutoa huduma hii. Nifanyeje sasa ili kukuza huduma yangu hii? Rose P. M.

Kama ambavyo tumesoma maoni ya msomaji mwenzetu hapo juu, changamoto yake kubwa ni hiyo ya kukosa wateja wa biashara yake. Na kama umesoma vizuri utaona anachofanya yeye ni kukaa eneo lake la biashara na kusubiri wateja, mbinu ambayo kwa sasa imepitwa na wakati.
Leo tunakwenda kujifunza upande wa pili wa wateja wa biashara yako. Kama changamoto yako kwa sasa ni wateja hawaji kwenye biashara yako, basi unachokwenda kufanya ni wewe kwenda kule ambapo wateja wapo. Inaonekana ni mbinu rahisi lakini utekelezaji wake ndiyo changamoto. Tutajifunza hapa jinsi ya kuweza kuwafikia wateja wako kule walipo.

SOMA; Mambo 20 niliyojifunza kwenye kitabu 85 INSPIRING WAYS TO MARKET YOUR SMALL BUSINESS. (Njia 85 za kutangaza biashara yako)

Unajuaje wateja wako walipo?
Hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya kuwafikia wateja wako, ni lazima ujue kule walipo. Na ili kujua walipo, kwanza lazima ujue wateja wa biashara yako ni watu wa aina gani, ukishawatambua vizuri wateja wako, ndiyo unaweza kuwafikia kule walipo.

Kwa biashara ya ‘stationary’ wateja ni wale watu ambao wanahitaji huduma za uchapaji, huduma za madaftari pamoja na kutengenezewa vitu mbalimbali vya maandishi. Hivyo hapa wateja wanaanzia kwenye maeneo yanayohusika na elimu, kuanzia walimu mpaka wanafunzi. Pia kunahusika na ofisi mbalimbali na hata watu wenye shughuli ambazo zitahitaji huduma ya uandishi. Mfani mtu mwenye sherehe ambaye anataka kuandaa kadi za kuwaalika watu kwenye sherehe hiyo.

Unawafikiaje wateja wako kule walipo?
Hapa kuna njia tofauti za kuwafikia wateja wako,
Kwanza wateja wako wanatakiwa kuwa na taarifa zako kwamba wewe upo na huduma gani unazotoa. Kwa sababu wateja wako wanapopata picha, kitu cha kwanza wanachofikiria ni nani anayeweza kuwatatulia shida hiyo. Hivyo wanapokuwa na taarifa zako, wanaanza kukufikiria wewe na kisha kuja kwenye biashara yako.

Hapa unahitaji kuhakikisha kila mtu ambaye anaweza kuwa mteja wako, basi anajua kwamba upo. Hivyo unahitaji kuwa na njia nzuri ya kuwafikishia wateja wa biashara yako taarifa zako kuhusu biashara unayofanya.
Hapa unaweza kuandaa vipeperushi ambavyo utawapa watu vinavyoeleza kuhusu biashara yako. Unaweza kia kuandaa matangazo mbalimbali ambayo yatawafanya watu wajue ulipo.

SOMA; Ijue sababu hii kubwa iliyopo nyuma ya biashara yako itakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Kwa biashara ya stationary kama ya msomaji mwenzetu Rose, unaweza kuandaa vipeperushi vyako na kuvipeleka kula maeneo ambapo wateja wako wanapatikana. Unaweza usiwafikie wote, lakini wale utakaowapata, watakuwa na taarifa za biashara yako.
Njia ya pili ni kwenda moja kwa moja kwa wateja wako na kuongea nao ili kuwapatia bidhaa au huduma unazotoa. Hapa unakutana na wateja na kuwashawishi kwa nini wanunue kwako, au kwa nini wafanye biashara na wewe.

Kwenye biashara ya stationary, unaweza kutembelea mashule na kuongea na walimu ili kuwapelekea zile huduma ambazo wanazihitaji. Mfano labda wanahitaji kupelekewa chaki, au wanahitaji kuchapiwa vitu mbalimbali. unaweza pia kuwapa punguzo maalumu ili waweze kushawishika kufanya kazi na wewe. Kwa kila mtu ambaye unaona anaweza kunufaika na biashara yako, usiache kuongea naye. Kuliko ukae kwenye biashara yako na upate elfu moja kwa siku, ni vyema ukapanga kuongea na wateja hata 10 kila siku, hutakosa wawili mpaka watatu watakaonunua kitu kwako.

Jambo muhimu la kuzingatia unapowafuata wateja kule walipo.
Toa huduma bora sana, mteja anaweza kukubali unapomwambia, lakini lengo lake ni kutaka kujaribu kama kweli huduma zako ni bora. Sasa wewe hutaki kuikosa nafasi hii nzuri sana na ya kipekee. Hakikisha mteja anaposema anajaribu basi anapata kile ambacho hajawahi kupata kwa wengine. Kumbuka mteja wako kwa sasa kuna maeneo mengine ambapo anapata huduma zake. Sasa anapojaribu yako, ni lazima uwe na sababu ya kumtoa kule alipo sasa na kumfanya awe mteja wako wa kudumu.
Hivyo mpe huduma bora sana, mtimizie kile anachohitaji na usiishie hapo pekee, bali nenda hatua ya ziada. Mfanye mteja afurahie kufanya kazi na wewe na awe tayari kurudi tena na kuwaambia wengine pia.

Nimalize kwa kusema biashara siyo kuwa na eneo zuri, wazo zuri na mtaji wa kuanza. Biashara n kitu ambacho kina vitu vingi vinavyoathiri. Ni lazima uweke juhudi kwenye kila eneo la biashara yako. Kama unaona wateja hawaji kwenye biashara yako, basi wafuate kule walipo. Na ukishawapata, wape huduma bora sana ili waendelee kuwa wateja wako wa kudumu.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz 

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Faida Kubwa Ya Kufanya Kazi Kwa Ushirikiano - 2.

$
0
0
Kufanya kazi kwa ushirikiano kwa majasiriamali yeyote yule anayetaka mafanikio ni jambo la muhimu sana. Kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano tunaona mafanikio na fursa nyingi huweza kuonekana huko kutokana na ushirikiana ambao unaweza kuonyeshwa kati ya mtu mmoja na mwingine.

Katika kuthibitisha hilo la umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano, wiki iliyopita na makala ya iliyopita tuliona jinsi ambavyo Mfalme Lipamila alivyoitisha mkutano na kuwaonyesha wananchi wake umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na jinsi ya kuweza kutatua pia tatizo la ajira kwa wananchi wake.


Mfalme Lipamila kuhusu ajira aliendelea kusema tutaweka utaratibu ambao tutalima kilimo ambacho ni tofauti ni tulichozea, nimeweka utaratibu ambao tutahakikisha ya kwamba tutalima kilimo cha kisasa, yaani tutalima sehemu ndogo lakini mavuno yatakuwa mengine, nmefanya pia utafiti kuhusu masoko ya kuhusu mazao ambayo tutalima kwani tutauza sana sehemu nyinginezo endapo tutashirikiana pamoja.

Jambo jingine ambalo nilitaka kulizungumza nanyi siku ya leo ni kwamba nafahamu fika ya kwamba tatizo la ajira ni kubwa sana, 

"Je unataka kujua mfalme Lipamalima atasema nini?

Mfalme lipamila alishusha pumzi Mmmmmh........kisha akendelea kwa kusema. Mara nyingi nilikuwa nikitafuta ufumbuzi ya jinsi ya kuweza kupunguza tatizo la ajira katika kisiwa chetu. Lakini tatizo hili litaisha endapo vijana wasomi na wasio wasomi pia katika suala zima la kubadili mtazamo juu ya suala zima la ajira.


Watu wengi ambao hawana ajira mitazamo yenu inafanana, wote mnaamini katika kujiriwa na serikali. Lakini niwaambieni ukweli kama mtaendelea na mtazamo huo nawahakakishia ya kwamba mtazadi kulaumu mpaka mtakapo acha kutumia pumzi ya dunia hii.

Maana ukweli ambao haufichiki ni kwamba katika kisiwa chetu idadi ya wahitimu kwa mwaka ni 800,000 lakini katika idadi hiyo watu ambao wanapata ajira ni jumla ya watu 80,000.

Watu wengi baada ya kusikia maneno hayo wengi walishangaa, wengine wakaona kama ni uongo, lakini Mfalme Lipamila akakandamizia kwa kusema haina haja ya kushangaa na huo ndio ukweli.


Na katika idadi ya watu ambao hawana ajira 70% ya watu hao hawana kazi maalumu za kufanya, na hii inapelekea katika kisiwa chetu kuwapo idadi kubwa ya watu ambao wanacheza kamali, kucheza pool table, kushinda kwenye vigodoro, wizi na mambo mengine mengi yasiyofaa katika jamii.

Lakini kwa kupitia ushirikiano wetu sisi sote tutasaidia kuweza, kupeana mbinu ambazo zitaweza kutusaidia, jambo la msingi ni kwamba kila mmoja wetu nafahamu fika anafikiri mambo mbalimbali, lakini ni lazima tukumbuke endapo tukiyaainisha mawazo yetu pamoja tutaweza kufika mbali.

Kama kuna baadhi ya watu wanataka kujikita katika ufugaji na kilimo tutatenga eneo kwa ajili ya wale ambao wapo tayari  kufanya kilimo na  tutashirikiana kulima na mwisho wa siku tutakuwa tumejikwamua katika suala hili.

Hapo nimezungumzia hasa katika kilimo na ufugaji lakini ipo siri kubwa sana, ya watu wengine pia kuweza kushirikishana mawazo yenu, kwamba mnataka kufanya nini, baada ya kupata majibu. Hapo tutasaidia kwa pamoja wafadhiri ambao watasaidia katika miradi yetu.

Pia niweze kuwahimiza ya kwamba tutatengeneze mazingira ya kujiajiri. hili ni jambo jema sana kwa mafanikio yenu. Pia kila mmoja wetu aweze kujifunza suala zima la uwekaji wa akiba wa pesa.

Endapo kila mmoja wetu akifanya hivyo baada ya muda fulani ataweza kujiajiri yeye mwenyewe kwa kuanzisha biashara yake.  Nimesema hivi kwa sababu kubwa suala la uwekaji akiba ni suala gumu.

Pia nafahamu pia hapa pia wapo wanafunzi ambao wanasoma hivyo nataka kuwaambia watengeneza mazingira ya wao kuweka akiba, wapo wale ambao bado wanasoma na huwa wanapata mikopo. Hivyo nao nawasihi wajifunze kugawa ile pesa ambayo wanapata na kuweka akiba ili pindi mmalizapo masomo muweze kutengeneza mazingira ya kujiajiri.

Mpaka kufikia hapo nimefika tamati ninachotaji kutoka kwenu ni utekelezaji ili kila mmoja wetu aweze kula mkate wake wa kila siku. Mwenyezi mungu awabariki sana na awatie nguvu na awalinde muweze kufika mafanikio yenu.

Baada ya hapo kila mmoja aliweza kufanya yale ambayo aliweza kuyaweka yale ambayo aliyasikia kutoka kwa mfalme Lipamila na hatimaye matunda yake yalionekana.

Hivyo nikusihi ya kwamba kwa kile chochote ambacho unajifunza uweze kukiweka katika matendo.

Afisa mipango Bensonchonya

Hii Ndio Faida Ya Kutumia Falsafa Ya Imani Ya Kidini Kwenye Malezi Bora Ya Watoto

$
0
0
Habari mpendwa Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vizuri licha ya kukumbana na changamoto za hapa na pale kwenye shughuli zako za kila siku. Usikatishwe tamaa na changamoto ishi maisha ya furaha na hamasa kubwa ya kufanya kazi kila siku. Kwani mpendwa rafiki, hujui ya kuwa changamoto ni sehemu ya maisha? Na maisha ni furaha anza kuwa na furaha hapo hapo ulipo kwani kuwa na furaha haihitaji wewe uwe na mtaji na kitu cha ajabu na cha kushangaza duniani hakuna duka linalouza furaha hapa duniani. Hivyo basi, mkurugenzi mtendaji wa furaha katika maisha yako ni WEWE mwenyewe.

Mpendwa Rafiki, karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza kwa pamoja faida ya kutumia falsafa ya imani ya dini kwenye malezi ya watoto. Karibu mpendwa msomaji, tuanze pamoja na tumalize pamoja. Natumaini kila mmoja wetu ana imani yake ya dini ambayo anaiamini hivyo basi, hakuna imani ya dini inayofundisha maadili mabaya kwa watoto yaani kufundisha mambo hasi yanayomharibu mtoto na kumpotezea dira ya maisha. Kwanza kabisa watoto wote ili waweze kuwa na msingi mzuri wa kiimani ni lazima wafundishwe kumjua Mungu aliyeumba vitu vyote hapa duniani vinavyoonekana na visivyoonekana.

Wazazi kama walimu wa kwanza kwenye malezi ya watoto wao ndio wakurugenzi watendaji wa kuhakikisha watoto wanakua katika malezi mazuri ya kuishi na kujua misingi na falsafa ya dini yao. Wazazi wengi sasa hivi wanaona ni fahari kubwa kumlea mtoto kidunia kuliko kuwafundisha watoto kumjua Mungu na kuwalea katika maadili ya falsafa ya imani ya dini. Kumlea mtoto kidunia kuna hasara kubwa kwani msingi mzuri wa jamii yetu ya leo unaanzia katika familia. Ili 
tuweze kuwa na jamii bora hatuna budi kuwalea watoto katika maadili mazuri hususani ya falsafa ya imani ya dini.


Mpendwa rafiki, watoto wanapaswa kufundishwa jinsi ya kusamehe na siyo kulipa visasi. Wazazi ndio maadui namba moja wa kuwafundisha watoto kulipa visasi badala ya msamaha. Kwa mfano, mtoto anaweza kugombana na mwenzake katika kucheza sasa mmoja wao akalia na miongoni mwa watoto wa wazazi hao anaenda kumwambia mwanangu tema mate hapa puuh! Tukamrushie kwa nini akupige. Kwa hiyo, mzazi badala ya kuchunguza kiini cha kosa na kuwapatanisha upya kwa kuwaambia wasameheane bali mzazi anamfundisha mtoto kurudisha kisasi. Ukimfundisha mtoto kulipa kisasi utazaa mauti. Mfundishe mtoto kuomba msamaha angali yuko mdogo kwani msamaha unarudisha uhusiano uliovunjika na kuleta uhusiano ulio kuwepo hapo awali. Haya yanakuwa ndio malezi mazuri ambayo falsafa ya dini hairuhusu kulipa visasi.

Watoto wanatakiwa kufundishwa upendo, upendo ndio falsafa kubwa kuliko falsafa zote, kwani upendo unagusa kila sehemu ya maisha yetu. Kama ukimpenda mwenzako huwezi kumfanyia ubaya ambao wewe hupendi kufanyiwa. Upendo huvumilia yote, upendo unaleta maisha ya amani na furaha. Unaleta maendeleo lakini chuki huzaa mauti tu. Kwa hiyo, ukimfundisha mtoto upendo unaohubiriwa katika falsafa ya imani ya dini basi tutakua tunafanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Mfundishe mtoto kuwapenda wenzake na watu wote wanaomzunguka.

Ndugu msomaji, mfundishe mtoto asiwe mbinafsi au mchoyo, maisha ya ubinafsi na uchoyo yametawala katika familia zetu. Hili tunaliona sana katika familia zetu unakuta baba mbinafsi, mama mbinafsi mtoto naye anaambukizwa ubinafsi ambao unakuja kuathiri jamii kwa ujumla. Ukimpa mtoto kitu mfundishe ampatie ndugu au rafiki yake n.k. kwa mfano, watoto wengine unaweza kuwapatia zawadi au kitu unawaambia wagawie na wengine au wenzako anaanza kulia na kutikisa mabega na kujitupa chini. Ukimuona mtoto anaanza tabia hiyo ikomeshe mara moja kabisa usipomkomesha unakua unaandaa bomu ambalo litakuja kukulipukia mwenyewe kama mzazi. Hatuwezi kuwa na kizazi kizuri kama tutawalea watoto katika ubinafsi na uchoyo. Wazazi mnatakiwa kuacha kuishi maisha ya ubinafsi na uchoyo na muanze na kuonesha mfano kwanza nyie na mtumie falsafa ya dini katika kupata malezi bora.

Kama wazazi mnatakiwa kurudi katika falsafa ya dini na kuwalea watoto kwenye misingi hiyo. Acha kukumbatia mambo ya kidunia na kupiga teke misingi ya dini kwenye malezi ya mtoto. Acha ile dhana ya kwenda na wakati na dunia katika malezi ya watoto na watoto wengi wanakuwa hawana hofu ya Mungu ndio maana baadaye wanakua wakatili, wanakosa uadilifu, nidhamu, uaminifu. Ukimlea mtoto katika misingi ya kumjua Mungu Naye Mungu atakubariki pia. Mlee mtoto katika imani thabiti aelewe vizuri imani siyo kuichukulia juu juu, hata wewe mzazi soma maandiko mbalimbali kuhusiana na imani yako mfundishe mtoto imani, siyo kupandikiza chuki tu.

SOMA; Hii Ndiyo Faida Ya Kupanda Mbegu Bora Kwa Wasaidizi Wako Wa K

Mzazi unapaswa kuonesha mfano, kwa watoto wako kama ni kusali basi mfundishe kusali, salini pamoja na nendeni pamoja kwenye nyumba za ibada. Usiwe mzazi wa kutoa amri tu bali kuwa mzazi wa kuonyesha mfano siyo amri tu. Kila unachosema kiendane na matendo yako. Usimfundishe mtoto tabia mbaya kama wewe ni mlevi basi usinywe pombe mbele ya watoto. Kama wewe ni mvutaji sigara usimuoneshe mtoto mfano mbaya mbele yake. Kazi ya mtoto iko katika malezi ndio maana wa swahili wanasema, kuzaa siyo kazi, kazi kumlea mwana. Mtoto ni malezi ndugu yangu ukimpatia mtoto malezi bora utampa mwanga katika maisha yake.
Mpe mtoto malezi bora ambayo hataweza kuyapata sehemu nyingine yoyote. Kama katika familia yenu hakuna aliyewahi kupewa malezi bora basi kuwa wa kwanza kumpatia mtoto malezi bora. Yaani toa thamani yako yote ya malezi bora ambayo hakuna mtu aliyewahi kupatiwa katika familia yenu.

SOMA; Adhabu Saba (7) Zisizostahili Katika Malezi Ya Watoto.

Hivyo , dini inafundisha upendo, unyenyekevu, uadilifu, uaminifu, nidhamu nzuri, kufanya kazi n.k. Dini haifundishi wizi kwa watoto, uchoyo, uchochezi, matusi, ubakaji, ulevi wa kupindukia nk. Bali dini inafundisha mtu ukweli, kuna falsafa ya ukweli inasema hivi ukiujua ukweli nao ukweli utakuweka huru. Ni kweli kabisa kama ukijua ukweli utakuweka huru katika maisha yako. Tunalelewa katika malezi ya nidhamu ya woga haya kwa sasa hayana nafasi tena. Mwambie mtoto ukweli ili uweze kumweka huru.

Mwambie ule usemi wa soma kwa bidii, pata alama nzuri utapata kazi sasa umepitwa na wakati. Mwambie dunia imebadilika ajira zimekuwa siyo za uhakika kama ilivyokua zama za mapinduzi ya viwanda na mwambie kwa sasa tupo zama za taarifa ili ufanikiwe unahitaji taarifa sahihi kwa wakati sahihi. Dunia ya sasa unatakiwa kufikiria nje ya ajira, mfundishe ukweli wote unaoujua bila kumficha naye atakushukuru.

Kwa kuhitimisha, mfundishe mtoto akue kiimani, akue kiroho, usimlee mtoto kidunia kwani hasara zaidi ni kwako binafsi na kwa jamii kiujumla. Mfundishe mtoto kuvua samaki na siyo kumpa samaki yaani mjengee msingi imara wa kujitegemea angali akiwa mtoto, mfundishe kufanya kazi na yale mambo chanya yote yanayopatikana kupitia falsafa ya imani ya dini.

SOMA; Njia Muhimu Za Kumfanya Mtoto Wako Ajione Wa Pekee.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

UCHAMBUZI WA KITABU; It’s Not About The Money (Tatizo Siyo Fedha Tatizo Ni Wewe).

$
0
0
Linapokuja swala la fedha, watu huweka hisia mbele kuliko fikra. Fedha imekuwa inachukuliwa kama kitu ambacho ni kiovu, wale ambao hawana wanawaona walionazo kama ni watu wasio wema. Masikini ambao hawana fedha wamekuwa wakijiona wao ni watakatifu kuliko matajiri wenye fedha. Wamekuwa wanajifanya hawapendi fedha wakati maisha yao yote wanaishi wakiambana kupata fedha za kusukuma maisha.

Inapokuja changamoto ya kifedha, iwe ni ukosefu wa fedha au fedha kutokukaa pale zinapopatikana, watu wengi wamekuwa wanapeleka lawama zao kwenye fedha. Wanasahau sehemu moja muhimu mno inayochangia kwenye changamoto hiyo ya kifedha.
Kwa ulimwengu wa sasa, kuna mwandishi ambaye amejifunza kuhusu fedha, na akajifunza kuhusu uhusiano wa mawazo, akili na fedha kwa undani. Mwandishi huyu ametumia miaka zaidi ya 40 kutafiti na kujifunza kuhusu fedha na mawazo ya watu. Kwa nini baadhi ya watu wanaweka juhudi kubwa lakini wanaishia kuwa na maisha magumu kifedha, na kwa nini baadhi ya watu wanaonekana kutokuweka juhudi kubwa lakini wako vizuri kifedha. Mwandishi huyu aliandika kitabu YOU WERE BORN RICH na leo tutakwenda kuchambua kitabu chake kingine kinachoitwa IT’S NOT ABOUT THE MONEY. Huyu siyo mwingine bali Bob Proctor.


Karibu tujifunze jinsi mawazo yetu na hatimaye tabia zetu zinavyoathiri hali zetu za kifedha.

1.     Fedha ni wazo.
Watu wengi wamekuwa wakifikiri fedha ni yale makaratasi ambayo wanabadilishana nayo na wengine. Fedha siyo karatasi jekundu lililoandikwa shilingi elfu kumi. Bali fedha ni wazo ambalo lina thamani ya kilichoandikwa kwenye karatasi. Kwa mfano kama mimi nina bidhaa ninayouza ambayo gharama yake ni shilingi elfu kumi, maana yake kuna wazo ambalo nimeweza kuligeuza bidhaa na thamani ya wazo hilo ni elfu kumi.
Kwa kujua hivi utaweza kuchukua hatua sahihi, kwa mfano kama kwa sasa una changamoto ya kifedha, maana yake huna mawazo yenye thamani kubwa kifedha. Anza kuja na mawazo hayo na utatatua changamoto yako kifedha.

2.     Fedha siyo lengo.
Hakuna mtu aliyepata utajiri mkubwa kwa kuweka lengo kuu kuwa kupata utajiri. Hapa ndipo watu wengi wanapokosea na kukuta wanahangaika maisha yao yote wasipate utajiri wanaotaka. Utajiri siyo lengo, bali utajiri ni matokeo ya wewe kukamilisha malengo yako mengine kwenye maisha. Lengo lako kuu lisiwe kupata utajiri, bali kutoa thamani kwa wengine.

3.     Hali yako ya kifedha ni matokeo ya wewe mwenyewe.
Hali ya kifedha uliyonayo sasa ni matokeo ya maisha yako kwa ujumla. Upo hapo ulipo kifedha kutokana na mawazo, mtazamo na matendo uliyonayo kwenye maisha yako linapokuja swala la fedha. Maamuzi unayofanya kila siku kwenye maisha yako, yanaathiri eneo lako la kifedha. Mtazamo wako juu ya kazi, utajiri na maisha kwa ujumla, unachangia hali uliyonayo.

SOMA; Utajiri Wako Uko Sehemu Hii Moja Muhimu, Acha Kupoteza Muda Huko Uliko Sasa.

4.     Fedha haiwezi kununua furaha.
Hii ndiyo kauli ya kijinga kabisa ambayo masikini wamekuwa wanajifariji nayo, kwamba fedha haiwezi kununua furaha. Ni kweli fedha haiwezi kununua furaha, kwani nani alituahidi fedha inanunua furaha. Furaha ni matokeo ya mtu kuwa na maisha bora, ambapo fedha pia inachangia kwenye ubora wa maisha. Hivyo acha mara moja kujifariji kwamba ni vizuri huna fedha kwa sababu hainunui furaha, wewe ishi maisha yako vyema, fanya kazi zako kwa ubora na fedha na furaha vitakuwa matokeo ya maisha yako.

5.     Thamani ya fedha ipo kwenye mzunguko.
Fedha ni kama maji, matone machache unaweza kuyadharau, lakini matone haya yanapoendelea nayaweza kuzaa mfereji, mifereji inapeleka mto a mtu kwenye ziwa au bahari. Fedha inafuata mtiririko huo, mtu anaweza kuanza na kiasi kidogo mno, kwa kukizungusha sawasawa, kwenye biashara au uwekezaji baada ya muda kiasi kile kinakua sana. Wale wanaozungusha fedha ndiyo wanaopata thamani yake. Wale wanaopata na kutumia pekee, wanabaki kuwa masikini. Usikubali fedha yoyote inayopita kwenye mikono yako iondoke yote, ondoa hata tone moja na zungusha.

6.     Utajiri unaanzia kwenye akili, siyo mfukoni.
Watu wengi hufikiri kwamba wakishapata fedha basi watakuwa na akili ya fedha. Lakini hiko ni kinyume, unakuwa na akili ya fedha ndiyo unaweza kuzishika kwa nidhamu na kufikia utajiri. Matajiri wote wana mtizamo tofauti kabisa katika swala la fedha ukiwalinganisha na masikini. Matajiri wanaijua misingi ya fedha na hawaikiuki, ila masikini, hawataki hata kujua misingi hiyo, wanaendesha maisha kama yanavyowajia.
Kitu cha kwanza kinachowatofautisha masikini na matajiri ni mtazamo wa kifedha. Na mtazamo huu unaanzia kwenye imani. Imani ya fedha ndiyo imekuwa kichocheo cha watu kufanikiwa na kikwazo kwa wengine kufanikiwa.

7.     Ufahamu wa kifedha ni muhimu.
Kikwazo kingine kwa watu kupata fedha ni ufahamu walionao kifedha. Watu wengi wana ufahamu mdogo sana kuhusu fedha, na ufahamu huu ni kile kiwango ambacho wamezoea kupata. Kwa mfano mfanyakazi anayelipwa milioni moja kwa mwezi, ameweka ufahamu wake wa kifedha kwenye kiwango hicho, hivyo hajawahi kufikiria vipi kama angeweza kupata mara kumi ya kipato alichonacho sasa. Hivyo pia kwa wafanyabiashara, wengi wanapata kipato kile kile kwa sababu ndiyo ufahamu wa kifedha walionao.
Ili kukuza ufahamu wa wako wa kifedha, anza kufikiria kama kipato chako kingekuwa mara kumi ya unachopata sasa. Fikiria ni kwa namna gani unaweza kuongeza kipato chako kwa kiasi hicho, utaanza kuzioana fursa zaidi za kuongeza kipato chako.

8.     Sikiliza wengine lakini chukua maamuzi yako.
Linapokuja swala la fedha, kila mtu ana ushauri wa kutoa. Hata watu ambao hawajawahi kutengeneza fedha kwenye maisha yao, wanaweza kuwashauri wenzao namna ya kutengeneza fedha. Hivyo watu wengi watakushauri mengi kuhusu fedha, lakini fanya maamuzi ambayo unajua ni bora kwako na utaweza kuyasimamia.

9.     Utajiri ni mchakato, siyo ajali au kitu cha haraka.
Hakuna kitu kinawapoteza masikini kama kushindwa kuelewa hili. Watu wamekuwa wakifiria kwamba kuna njia ya haraka ya utajiri ambayo matajiri wanaijua ila wao hawaijui. Utawasikia wanaongea mambo ya kijinga kama freemason na bahati. Lakini wale waliopaya utajiri, wanajua ni kwa namna gani imewachukua muda kupata utajiri huo.
Katika kutafuta njia hizo za mkato, masikini wengi wamekuwa wakiishia kutapeliwa hata ile fedha kidogo waliyonayo. Jua kwamba unahitaji muda ili kufikia uhuru wa kifedha, na usitafute njia ya haraka au njia ya mkato.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Millionaire Fastlane (NJIA YA HARAKA YA KUFIKIA UTAJIRI)

10.  Fedha haimbadilishi mtu, bali inamwonesha jinsi alivyo.
Imekuwa ni kawaida kusikia watu wakisema mtu fulani tangu amekuwa na fedha amebadilika sana. Labda amekuwa na roho mbaya kuliko hapo awali. Hivyo kuna ambao wamekuwa wanatumia hii kama sababu ya wao kutokupata fedha, wakiogopa zitawaharibu na kuwagombanisha na wengine.
Ukweli ni huu, fedha haina tabia yoyote, tabia wanazo watu, fedha inachofanya ni kuzionesha zile tabia za watu, jinsi zilivyo bila ya kificho. Kadiri mtu anavyokuwa na fedha ndivyo anavyokuwa na majukumu mengi, na kuweza kuwaathiri wengi. Hivyo kama alikwa na tabia mbaya basi itawaathiri wengi.

11.  Njia pekee ya kupata fedha ni hii; TOA THAMANI.
Fanya ufanyavyo, lakini mwisho wa siku kanuni ya fedha ni hii, unalipwa kulingana na thamani unayotoa. Nukta. Hakuna namna yoyote unavyoweza kwenda kinyume na kanuni hiyo. Unalipwa unacholipwa sasa kwa sababu hiyo ndiyo thamani unayotoa. Kama unataka kuongeza kipato chako, ongeza thamani unayotoa kupitia kazi yako au biashara yako.
Hapa napo kuna matatizo yanayowatofautisha matajiri na masikini, masikini anasema nikianza kulipwa vizuri ndiyo nitatoa thamani kubwa, tajiri anasema nitaanza kutoa thamani kubwa na najua nitalipwa vizuri. Sasa niambie wewe mwenyewe, kama ungekuwa umeajiri watu hao wawili, ungemwongezea yupi kipato?

12.                       Fikra hasi zimetawala sana jamii zetu, hasa linapokuja swala la fedha.
Kuna baadhi ya maeneo ukianza kuongea kuhusu fedha unaonekana kama mtu mwenye tamaa. Pengine unakatishwa tamaa kwamba unachofikiria hakiwezekani. Unahitaji kuwa makini sana na jamii inayokuzunguka, kama ni watu ambao wana fikra hasi kuhusu fedha, watakurudisha nyuma. Linda sana fikra zako dhidi ya fikra hasi zinazosambaa kwenye jamii.

13.                       Fanya kile unachopenda kufanya, ndipo utajiri wako ulipo.
Tatizo kubwa kwenye jamii zetu ni kwamba tangu tunakua na kwenda shule, tumekuwa tunaambiwa ni kazi zipi zinazoweza kutupa kipato na zipi hazifai. Kuwa daktari, kuwa mwalimu, kuwa mhandisi au kuwa mhasibu, kisha utapata kazi ya uhakika na kuwa na maisha mazuri. Matokeo yake tumekuwa na watu ambao wanafanya kazi wasizozipenda, hivyo hawatoi thamani kubwa na kipato chao kinakuwa kidogo.
Utajiri wako uko kwenye kile kitu ambacho unapenda kukifanya, maana hiki ndiyo utakuwa tayari kutoa thamani kubwa sana. Kama unapenda kuandika andika, kama unapenda kucheza cheza, chochote unachopenda kufanya, kifanye kwa namna unavyoweza kuongeza thamani kwa wengine na utaweza kutengeneza kipato.

14.                       Kama umeshapotea, anzia hapo ulipo.
Tunao watu wengi ambao wamepotea kwenye kazi na biashara zao. Wamejikuta kwenye kazi au biashara wasizozipenda, hii ni kwa sababu hawakupata msingi wakati wanaanza. Na sasa wamepata msingi lakini wanaona hawawezi kutoka kwa sababu ya majukumu waliyonayo. Watu hawa wanaweza kuanza kufanya kile wanachopenda kufanya, huku wakiendelea na kazi au biashara zao kwa sasa. Kama upo kwenye kundi hili usiendelee kusubiri, anza sasa. Hakuna siku itafika ambapo utaona uko tayari kwa kila kitu.

SOMA; Njia Nne Za Uhakika Za Kufikia Utajiri, Angalizo; Ajira Sio Mojawapo.

15.                       Hakuna kustaafu.
Ukiangalia watu wote ambao wameweza kufanikiwa sana kifedha, utagundua wanafanya kazi mpaka wakiwa na miaka 70, 80 na hata 90. Hii ni kwa sababu wanajua fedha haina kustaafu, na kingine muhimu ni kwamba wanakuwa hawafanyi kazi, badala yake wanafanya kile wanachopenda kufanya, ambacho wanachukulia ni sehemu ya maisha yao.
Kama unafikiria kustaafu zaidi kuliko unavyofikiria kufanya kazi au biashara yako, upo kwenye njia ambayo siyo sahihi. Pia usiangalie kustaafu kama ndiyo mwanzo wa kuyaishi maisha ya ndoto yako, bali maisha yako yawe ndiyo ndoto yako, kila siku.

16.                       Huwezi kupata mafanikio ya kifedha kama unataka kufanya vitu vya kawaida.
Kwa kifupi ni kwamba kama hakuna mtu amewahi kukushangaa kwa kile unachofanya, au kustuka au kukuambia unakosea, maana yake hakuna kikubwa unachofanya, unafanya kile ambacho kila mtu anakijua na amekizoea. Ni vigumu sana kupata utajiri kwa kufanya vitu vilivyozoeleka.
Unahitaji kufanya vitu ambavyo siyo vya kawaida, vitu ambavyo havijazoeleka, weka juhudi ambazo hazijazoeleka na utapata matokeo ambayo hayajazoeleka.

17.                       Usijihukumu kwa matokeo yako ya sasa.
Huwa tuna tabia za kuwahukumu watu kwa matokeo yao ya sasa. Na pia tunajihukumu sisi wenyewe kwa matokeo tunayopata sasa, tunaona pale tulipo ndiyo sehemu yetu na hivyo kuridhika. Hujawahi kujiuliza kwa nini mtu anaweza kufanya kazi miaka 10 au 20 kwa kipato kile kile na madeni kila siku. wanakuwa wamejihukumu na kukubali hukumu zao.
Haijalishi kwa sasa uko wapi, kesho unaweza kuwa bora zaidi ya leo. Na ili kesho uwe bora, ni lazima uchukue hatua leo. Anza kuchukua hatua leo kutengeneza kesho bora. Usikubali sababu yoyote uliyonayo sasa ikuzuie.

18.                       Sumu kubwa itakayokumaliza kwenye safari ya utajiri.
Ni kuiga. Kwa sababu fulani kafanya kitu fulani akafanikiwa, siyo uhakika kwamba na wewe ukifanya utafanikiwa. Binadamu tunatofautiana, na hakuna mtu yeyote hapa duniani anayefanana na wewe moja kwa moja. Uko hivyo ulivyo wewe tu hapa duniani. Sasa unapojaribu kuiga wengine, unachofanya ni kuzika uwezo wako wa kipekee ulionao. Kamwe kamwe usiige, jua kipi bora kwako a kipi unapendelea kisha weka juhudi zako zote hapo, utafanikiwa.

SOMA; Mambo Kumi (10) Muhimu Ya Kuzingatia Kabla Hujafunga Ndoa Na Utajiri.

19.                       Hakuna mtu ambaye hajawahi kushindwa.
Hadithi utakazosikia kwa wengi ambao hawajafanikiwa ni kwamba nilijaribu nikashindwa. Kama ile wale waliofanikiwa wao walikuwa na njia rahisi, hawakuwahi kushindwa. Sikiliza kila mtu alishawahi kushindwa, tena wale waliofanikiwa ndiyo wameshindwa mara nyingi kuliko wale ambao hawajafanikiwa. Hivyo acha kutumia kushindwa kama kigezo cha wewe kukosa mafanikio. Ukishindwa usikate tamaa, amka na endelea na mapambano.

20.                       Utajiri au umasikini unaanza na wewe mwenyewe.
Tatizo siyo fedha, tatizo ni mimi mwenyewe, jiambie kauli hii kila mara ambapo unajikuta kwenye changamoto za kifedha, itakusaidia mno kuchukua hatua sahihi. Fikra zako, maamuzi yako na matendo yako yanaathiri sana hali yako ya kifedha. Marafiki unaokaa nao muda mrefu wana mchango kwa hapo ulipo kifedha, kama unabisha waangalie marafiki zako wa karibu, utaona wote mnalingana kwenye swala la fedha. Vipindi vya tv unavyoangalia, magazeti na vitabu unavyosoma vinaathiri hali yako ya kifedha.

Kwa kifupi ni kwamba, kuondoka kwenye changamoto za kifedha, kufikia utajiri na uhuru wa kifedha, akili yako inahusika mno. Anza kuleta mapinduzi kwenye akili yako na linda akili yako isichafuliwe na mitazamo hasi ya kifedha. Utaweza kufanya maamuzi bora na kuweza kufanikiwa.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita


Jiwashe Moto, Watu Watakuja Kukuangalia Ukiungua.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Hamasa kidogo siku ya leo itakusukuma kuweka juhudi kwenye miezi hii michache iliyobaki kumaliza mwaka huu 2016. Mwaka ulianza taratibu na sasa unamalizika. Na swali ambalo nitakuuliza ni hili, je mwaka huu umeongeza maana yoyote kwenye maisha yako au unaishia kuuhesabu tu kama mwaka mwingine unaopita?

Kwa maana namaanisha miaka kumi ijayo, kuna kitu utaangalia na kusema mwaka 2016 nilifanya maamuzi sahihi ambayo yamekuwa bora sana kwangu? Kama hujafanya kitu cha aina hiyo kwenye mwaka huu, basi unaelekea kuupoteza rafiki yangu. Na nitakusihi sana leo hii, yaani sasa hivi utakapomaliza kusoma hapa, angalia ni kipi kimoja unachoweza kubadili kwenye maisha yako. Nakusihi tena rafiki, usikubali mwaka huu upite bila ya kufanya kitu cha tofauti na namba ambavyo umekuwa unafanya miaka mingine. 
WAHI TIKETI YAKO SASA, BONYEZA PICHA KUPATA TIKETI.

Vipo vitu vingi sana unavyoweza kuanza kufanya leo na ukabadili kabisa mwelekeo wa maisha yako kabla mwaka huu 2016 haujaisha. Angalia ni kipi hasa unachotaka kwenye maisha yako, na anza kukifanyia kazi. Acha kusubiri mpaka kila kitu kiwe sawa, na badala yake anza sasa. Kama utahitaji msaada wangu kwenye hatua gani uchukue au uanzie wapi, tuwasiliane.

Karibu rafiki kwenye kile ambacho napenda kukushirikisha kupitia makala hii ya leo. Leo nakuambia jiwashe moto na watu watakuja kukuangalia ukiungua. Sijajua kama umeielewa vizuri hiyo sentensi, lakini nitakuelezea ili uweze kuelewa vizuri.

Sehemu yoyote ambapo kuna giza, mwanga unaleta tofauti. Mwanga unafanya watu watoke kwenye giza na kusogea kwenye mwanga. Wote tunajua kwamba hakuna mwanga kama hakuna nguvu inayotumika kutengeneza mwanga huo. Nguvu hiyo inaweza kutokana na viumbe, ikatokana na madini au ikatokana na umeme.
Kwenye kazi au biashara ambayo unafanya, kuna watu wengi mno ambao wapo kwenye giza. Kuna vitu vingi ambavyo watu hawajui kama vipo au vinatokea. Wapo ambao maisha yao ni magumu kwa sababu tu hawana taarifa na maarifa sahihi ya kile wanachotaka kwenye maisha yako. Ndani ya giza hili, hakuna aliye tayari kutoa mwanga kwa sababu kutoa mwanga kunahitaji nguvu, na nguvu inatoka ndani ya yule ambaye anataka kutoa mwanga.

Ndiyo maana nakuambia wewe rafiki yangu, jiwashe moto na watu watakuja kukuangalia ukiungua, na siyo kukuangalia pekee, bali watafaidika na mwanga wako, na wewe pia utafaidika kupitia wao. Unapojiwasha moto, unatoa fursa na nafasi nzuri kwa wengine kupata maarifa na taarifa sahihi zinazowawezesha kuchukua hatua kuboresha maisha yao.

Kujiwasha moto maana yake ni kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho unafanya. Ni kujitoa kwa hali na mali, kufanya siyo kwa sababu wengine wanafanya, ila kufanya kwa sababu umechagua kufanya, na kwa sababu unataka kutoa mchango kwenye maisha ya wengine. Kwa sababu unajua mafanikio yako ni matokeo ya mafanikio ya wale wanaokuzunguka na wanaonufaika na kile unachofanya.

Unapojiwasha moto, unaacha kujionea huruma, unaacha uvivu, unaacha kufanya kwa mazoea na unajitoa hasa, unaweka kila tone la jasho, machozi na damu yako kwenye kile ulichochagua kufanya. Unakubali kuteseka kwa ajili ya wengine, siyo kwa sababu unataka uonekane unateseka, bali kwa sababu unafurahia kutoa mchango mkubwa kwenye maisha ya wengine.

Utakapoamua kujiwasha moto, wapo wengi watakaokuja na maoni ya ushauri wao, kwamba unafanya sana, kwamba umepitiliza, na maneno mengine ya kukata tamaa. Lakini mimi nataka nikuambie jambo moja, endelea kuchochea moto, wale wakatishaji tamaa siyo watu wazuri kwako. Achana nao na songa mbele, wewe angalia kile ambacho unatoa kwa wengine.

Huu ndiyo ujumbe wa hamasa ambao nataka uondoke nao siku ya leo rafiki yangu. Unapochagua kufanya kitu, kifanye kweli mpaka akila mtu akiangalia aseme kweli hapa kuna mtu amejitoa kufanya. Amua kufanya kweli, usiguse juu juu, bali fanya, na fanya kweli kweli.

Nasisitiza sana rafiki yangu, fanya kwa sababu ndiyo kitu unapenda kufanya, fanya kwa sababu unataka kutoa mchango wako kwenye maisha ya wengine na fanya kwa sababu unataka kuacha alama hapa duniani. Usifanye kwa sababu kila mtu anafanya, au kwa sababu umezoea kufanya au kwa kuwa wengine watakuona ukifanya. Ukiwa na sababu hizo za mwisho hutaweza kujiwasha moto, utajionea huruma na utafanya yale ambayo ni ya kawaida. Na sote tunajua, wale wote ambao wanafanya kwa kawaida, huishia kupata matokeo ya kawaida.

Mwaka unaisha rafiki yangu, fanya kitu leo, fanya kitu sasa.

Nikukumbushe haya muhimu;
1.     Karibu kwenye kundi la TELEGRAM la AMKA MTANZANIA, bonyeza maandishi haya kujiunga moja kwa moja kwenye kundi hili.
2.     Jiunge na mfumo wetu wa email, ambapo kila jumanne, alhamisi na jumapili nakutumia email nzuri za mafunzo na hamasa. Bonyeza hapa kujiunga na mfumo wa email.
3.     Tarehe 30/10/2016 tutakuwa na semina ya milioni ya ziada, itafanyika ubungo plaza, dar. Hii siyo semina ya kukosa rafiki, pata tiketi ya kuhudhuria semina hii, bonyeza hapa kupata tiketi ya kushiriki semina hii ya kipekee.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Epuka Migogoro Ya Ardhi Isiyo Na Ulazima Ili Uyafikie Mafanikio Yako Kwa Uhakika

$
0
0
Nimekuwa nikipokea maswali na maoni mbalimbali kuhusiana na Makala mbalimbali zilizopo kwenye Amka mtanzania. Lakini nimepokea maswali mengi zaidi yanayohusu ardhi tofauti na ujenzi. Hali hii inatokana na majengo kuwa sehemu ya ardhi kwa mujibu wa taaluma, sera na sheria za ardhi. Kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha watanzania tunabadilika na kila mmoja wetu anafanikiwa kupitia fursa zilizopo hivyo basi Katika kutimiza azma yetu, tumekuwa tukiwapa ushauri ili muweze kuvuka vikwazo mbalimbali vinavyowakabili. Hali hii inaonyesha na kudhihirisha kuwa kuna tatizo kubwa kuhusiana na umiliki na matumizi ya ardhi ndani ya nchi yetu, hali hii inawaumiza watu kimyakimya, hivyo basi kwa umoja wetu na kwa nafasi ya kila mtanzania tuhakikishe tunakuwa sehemu ya ufumbuzi wa migogoro ya ardhi ili turuhusu maendeleo yaweze kufanyika kwa haraka na wakati muafaka, maana ardhi ni rasilimali na kichocheo kikuu cha mafanikio ya kila mmoja wetu. Kupitia Makala hii nitatoa ufafanuzi juu ya mambo machache ambayo yamekuwa na uelewa tofauti katika jamii wakati mwingine kuwa chanzo cha migogoro. 
 
 
1.USIMAMIZI WA ARDHI
Kwa mujibu wa sheria za ardhi Tanzania, Ardhi ni mali ya Watanzania wote bila kujali jinsia wala tabaka. Ardhi ya Watanzania inasimamiwa na Rais kwa niaba ya Watanzania wote kama msimamizi na mdhamini mkuu wa ardhi. Kwa maana hiyo, mamlaka ya juu ya usimamizi wa ardhi ya Tanzania ni Rais wa Tanzania.
Hata hivyo, ili kuhakikisha usimamizi thabiti wa ardhi, serikali kupitia mfumo na muundo wa kiutawala inao wataalamu wanaotoa ushauri kwa serikali na wananchi katika masuala yote yanayohusiana na utawala, usimamizi, umiliki na utumiaji wa ardhi katika masuala endelevu. Wataalam wa Ardhi wa ngazi zote hufanya kazi kwa niaba ya Rais wa nchi. Miongoni mwa majukumu ya wataalamu ambao ni maafisa ardhi ni pamoja na kutoa hati za umiliki wa ardhi katika ardhi ya maeneo yaliyopimwa.
Mamlaka ya Serikali za Mitaa kama vile halmashauri za wilaya au manispaa zina uwezo wa kutoa maelezo yoyote yanayohusu ardhi kupitia kamati zake au maafisa wake kuhusiana na utawala wa ardhi chini ya Sheria ya Ardhi, kwa ardhi iliyo ndani ya mipaka ya eneo lake.
Halmashauri ya Kijiji imepewa wajibu wa kusimamia ardhi yote ya kijiji. Katika kutekeleza wajibu wake, Halmashauri ya Kijiji itabidi kuzingatia ushauri, mamlaka, uwezo, madaraka, haki na wajibu wa taasisi na mamlaka nyingine zilizotambuliwa na sheria kuhusiana na ardhi. Hata hivyo katika kuendesha utawala katika ardhi ya kijiji, Halmashauri ya Kijiji inafanya kazi kama mdhamini kwa niaba ya wanufaika ambao ni wanakijiji. Kwa maana hiyo chombo chenye madaraka ya mwisho katika usimamizi wa ardhi ya kijiji ni Mkutano Mkuu wa kijiji na ugawaji wote wa ardhi ya kijiji lazima uthibitishwe na Mkutano Mkuu wa Kijiji. Kutokana na uzoefu, kumekuwa kukijitokeza migogoro mingi ya ardhi katika maeneo ya kijiji hasa pale ardhi ya kijiji inapogawiwa kwa wawekezaji. Wanakijiji wanapaswa kufahamu kuwa viongozi pekee hawana mamlaka ya kugawa ardhi ya kijiji bila ya kuwashirikisha wanakijiji wote kupitia mkutano mkuu.

SOMA;  Mambo Matatu Ya Kuzingatia Kabla Ya Kufanya Uwekezaji Wa Majengo Ili Uepuke “Bomoabomoa

2. UMILIKI WA ARDHI
Upatikanaji wa ardhi Tanzania huwezeshwa kwa kupitia njia kadhaa ambazo ni halali na zinazokubalika kisheria katika jamii. Kwa ujumla mtu au taasisi anaweza kumiliki ardhi kwa ama kugawiwa, kurithishwa, kupewa, kutwaa au kununua. Kutwaa hutumika pale ambapo mtu huingia katika eneo kama vile pori na kusafisha kisha kuliweka katika matumizi. Njia hii ni kongwe sana hapa nchini lakini ni ngumu kutumia njia hii nyakati hizi za sasa kwa kuwa karibu ardhi yote ipo chini ya umiliki, hivyo kutumia njia hii ni kuchochea migogoro ya ardhi. Urithi; Mtu yeyote anaweza kupata ardhi kwa njia ya urithi. Anaweza kurithi ardhi kutoka kwa ndugu, mke/mume au wazazi wake. Jinsia au tamaduni na mila haviwezi kuwa kigezo cha kumnyima mtu haki hiyo ya kurithi ardhi. Mgao wowote utakao mnyima haki hiyo kwa misingi ya jinsia au mila ni batili na unaweza kuwafikisha wahusika mahakamani.
Kugawiwa na Serikali; Mtu yeyote anaweza kupata ardhi kwa kugawiwa na Serikali. Anaweza kuomba ardhi na Kamishina akiridhika kwamba umetimiza masharti atakugawia ardhi hiyo. Katika ardhi ya kijiji, serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kugawa ardhi. Kununua; Hii pia ni njia mojawapo ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia kupata ardhi Wakati mmiliki anapotaka kuuza ardhi yake iwe ya kijiji, hifadhi au binafsi, sheria inatoa ruhusa ya kununua kama unaweza. Upangishaji ni njia mojawapo ya kupata ardhi. Tofauti na njia nyingine za upatikanaji wa ardhi, upangishaji unakupatia haki pungufu na yule anayekupangisha.
Haki Miliki; Kwa muijibu wa sera na sheria za ardhi umiliki wa Ardhi unatambuliwa uko wa aina mbili:- Hakimiliki ya kiserikali (granted right of occupancy), na Hakimiliki ya kimila (customary right of occupancy). Aina hizi mbili za hati ya kumiliki ardhi Zina hadhi sawa kisheria. Ingawa hakimiliki ya kimila ilichukuliwa kama haki ya matumizi tu ya ardhi na haikubeba uzito kama ilivyo kwa hakimiliki ya kiserikali. Kwa hiyo, ilipotokea mgogoro kati ya wamiliki wawili, mmoja akiwa na hatimiliki ya kiserikali na mwingine akiwa na hakimiliki ya kimila, basi hakimiliki ya kimila ilionekana kuwa haina nguvu na hivyo kutotambuliwa. Kwa hivi sasa haki miliki ya kimila ina hadhi sawa sawa na hakimiliki kiserikali.
Hati miliki kimila ina hadhi ambayo kwa hali yoyote ni sawa na hati miliki inayotolewa kisheria: Yaweza kutolewa na Halmashauri ya kijiji kwa raia, familia ya raia kikundi cha raia wawili au zaidi, au chombo chenye hadhi ya shirika ambacho wabia wake wengi ni raia wa Tanzania.

SOMA; Ili Upate Mafanikio Ya Kudumu, Wekeza Kwenye Ardhi Na Majengo.

3. MATUMIZI YA ARDHI
Ardhi ni rasilimali ambayo hupanda thamani kwa kadri siku zinavyoenda na kwa kadri mahitaji ya ardhi yanavyoongezeka. Hivyo ardhi inaweza kuendelezwa kutoka hali iliyokuwa nayo kwenda hali nyingine tofauti. Miongoni mwa matumizi endelevu ya ardhi ni pamoja na kujenga majengo ya kukaa au kupangisha, kuitumia kwa kilimo cha biashara na chakula au kuitumia ardhi kwa shughuli za ufugaji. Kama ardhi itaendelezwa kwa kujenga majengo basi majengo yale yanaweza kutumika kama makazi ya mwenye nayo au kutumika kama makazi au majengo kwa ajili ya kupangisha kibiashara.
Njia nyingine ya kuitumia ardhi kama sehemu ya kitega uchumi ni kuuzwa kwa wanunuzi mbalimbali. Ardhi inatumika kupata dhamana ya mkopo kwa kutumia ardhi kama kitu cha usalama (security) kwa mkopeshaji wa mkopo. Mmiliki wa ardhi huweza kuomba mkopo katika taasisi za fedha kama vile benki kwa kuweka hati ya miliki ya ardhi yake kama dhamana ya mkopo aliochukua. Tanzania ni nchi iliyo kwenye mikakati ya maendeleo endelevu. Maendeleo endelevu hutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo maliasili kama ardhi.Taasisi za fedha pia zinachangia katika maendeleo kwa njia ya kuwapatia wananchi mkopo wa fedha kwa riba. Kutokana na nia ya kuhakikisha uwepo wa maendeleo, Serikali ilionelea ni vyema kurekebisha baadhi ya vipengele katika Sheria za Ardhi, 1999 na Sheria ya Usajili wa Ardhi (Sura 334) kupitia kutungwa kwa Sheria ya Rehani. Sheria ya Rehani inatumika kuongoza taasisi za fedha katika kukopesha fedha kwa wananchi.
Ardhi ni rasilimali kubwa ambayo inaweza kupangishwa kulingana na mahitaji ya wakati huo na kumletea faida kubwa mmiliki wake. Mojawapo ya shughuli za upangishaji zilizozeleka ni upangishaji wa nyumba kwa ajili ya pango la makazi au biashara. Kwenye ardhi ya kijiji upangishaji uliozoeleka ni upangishaji kwa ajili ya kilimo na ufugaji. Upangishaji wa aina hizi huweza kudumu kwa muda mfupi na muda mrefu. Upangishaji mwingine ambao una faida kubwa kwa hivi sasa ni upangishaji kwa wawekezaji kutoka makampuni makubwa ya kigeni na makampuni ya ndani ya nchi. Upangishaji huu wa ardhi una tija kubwa kwa wananchi hasa wanaomiliki ardhi mijini na vijijini. Ila tu, katika hatua hii ya upangishaji ni muhimu kwa wananchi kupata ushauri wa kisheria kabla ya kuingia mikataba. PiaMmiliki wa ardhi anaweza kuwekeza ardhi yake kama mtaji mkubwa wa biashara kwa ama yeye mwenyewe au kuingia ubia na mwekezaji mkubwa na kujipatia faida kubwa kwa maendeleo yake binafsi au taifa.

SOMA; Faida Za Uwekezaji Wa Majengo Kwenye Maeneo Salama Na Yaliyopimwa Na Wataalam Wa Ardhi

4. ZINGATIA USHAURI
Miongoni mwa chanzo kikuu cha migogoro wakati wa ujenzi ni umiliki wa ardhi, ili kuepuka hili fuata taratibu zote wakati wa uhamishaji wa ardhi kutoka miliki moja kwenda miliki nyingine kutokana na sababu kadhaa zikiwamo kuuza, kurithi au kugawiwa. Pia Ardhi inaweza kutwaliwa na matumizi yake ya awali yakabadilishwa kwa ajili ya uendelezaji wa matumizi mengine kwa manufaa ya umma na mwenye ardhi anastahili kulipwa fidia pindi azimio la utwaaji wa ardhi litakapopitishwa.
Tuendelee kuwa pamoja kupitia AMKA MTANZANIAtufike kwenye kilele cha mafanikio, pia endelea kufuatilia makala zijazo ili ujifunze zaidi.
Mwandishi wa makala hii ni mwanataaluma na mshauri wa ujenzi.
Anapatikana kwa: Simu: +255 685 729 888
Baruapepe: kimbenickas@yahoo.com

USHAURI; Jinsi Ya Kupata Wateja Wa Kudumu Kwenye Biashara Yako, Na Kuweza Kuikuza Zaidi.

$
0
0
Mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa, hiki ni kitu muhimu sana ambacho nataka wewe rafiki yangu ukielewe na ukifanyie kazi kila siku. Asitokee mtu yeyote yule akakuambia kinyume na hayo, labda kuna watu fulani ambao ndiyo wana haki ya kufanikiwa ila siyo wewe. Hiyo siyo kweli kabisa, wewe, hapo ulipo una haki ya kufanikiwa, na kwa kwenda pamoja na mimi, utajifunza yote muhimu unayopaswa kujua ili kufanikiwa.

Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto mbalimbali ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Nirudie tena hili ambalo nimekuwa nalisema mara kwa mara, na ndiyo ukweli wa maisha, kama hakuna changamoto, hakuna maisha na hivyo hakuna mafanikio. Changamoto ni sehemu ya maisha yetu, hivyo tunahitaji kuzitatua ndiyo tufanikiwe.
KUPATA MAELEZO KUHUSU SEMINA HII BONYEZA PICHA AU MAANDISHI HAYA.

Kwenye makala yetu ya leo tunakwenda kuangalia jinsi unavyoweza kupata wateja wa kudumu kwenye biashara yako na kuweza kuikuza biashara hiyo zaidi. Hii ikiwa ni changamoto ambayo tumeandikiwa na rafiki na msomaji mwenzetu Monie. Karibu usome changamoto hii na ushauri muhimu wa kuzingatia;

Changamoto inayonikabili ni kwamba ninawezaje kupata wateja wa kudumu na jinsi gani ya kukuza ama kutanua biashara ninayotaka kuanzisha? Monie P. P.

Kupata wateja wa kudumu kwenye biashara ni changamoto kubwa sana, na hili ndiyo limekuwa linaua biashara nyingi. Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba kuanzisha biashara ndipo mahali pagumu sana, lakini huu siyo ukweli, kuanzisha biashara ni kugumu, lakini kuendesha biashara mpaka ipate mafanikio makubwa, ni pagumu zaidi.

Ukianzisha biashara ni rahisi wateja kuja, wanataka kuja kupima biashara hii mpya ikoje, wanapokuja mara ya kwanza, ndiyo wataamua kama wataendelea kuja tena au hawatakuja tena kwenye biashara yako. Hivyo ni lazima uwe makini sana na uendeshaji wako wa biashara ili uweze kuwa na wateja wa kudumu.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kujua Biashara Inayolipa Eneo Ulipo.

Kumshawishi mteja aje kwenye biashara yako mara ya kwanza inaweza isiwe kazi ngumu, unaweza hata kudanganya ili tu afike, lakini kumfanya mteja arudi tena na tena na tena, na pia awalete wenzake, ni kazi ambayo wewe kama mfanyabiashara unahitaji kuifanya, na siyo kazi ndogo.

Je ni hatua zipi ambazo zitakuwezesha kupata wateja wa kudumu kwenye biashara yako?

1.     Tekeleza kile unachoahidi. Uaminifu ni muhimu.
Kuna mambo mengi ambayo utamuahidi mteja ili aje kwenye biashara yako, labda kupitia matangazo utakayotoa. Kuna sifa ambazo utaipa biashara yako na changamoto za wateja ambazo utasema biashara yako inatatua. Wateja watakuja kwako wakiwa na mategemeo ya kupata kile ulichosema watapata. Kama watafika na kupata, watakuamini na kuja tena na tena. Lakini kama watafika kwenye biashara yako na kupata huduma au bidhaa tofauti na ile uliyowaambia watapata, hawatakuamini na hawawezi kurudi tena.

2.     Nenda hatua ya ziada. Toa zaidi ya ulivyoahidi.
Kutekeleza kile ulichoahidi kila mtu anaweza kufanya hivyo, hivyo inaweza isikutofautishe sana na wafanyabiashara wengine. Kipo kitu kimoja cha kukutofautisha kabisa na wafanyabiashara wengine, na hili ni kwenda hatua ya ziada. Mfanye mteja akija kwenye biashara yako ashangazwe, aone kama anakuibia hivi. Asiamini huduma au bidhaa anazopata kwa bei ambayo amelipia. Angalia namna unaweza kufanya hivi bila ya wewe kupata hasara, na hilo linawezekana vizuri sana kama utaijua biashara yako vizuri.

3.     Usiwe na wateja, kuwa na marafiki.
Najua hapo juu nimekupa mbinu za kuwapata wateja, na hapa nakwenda kinyume kabisa na niliyokuambia hapo juu. Usiwe na wateja, badala yake kuwa na marafiki. Neno mteja linaweza kuwa na tafsiri ya kimaslahi pekee, kwamba huyu ni mteja ninachoaka kwake ni faida. Lakini biashara siyo faida pekee, bali pia kutoa mchango kwenye maisha ya wengine. Wachukulie wateja wako kama marafiki zako, na kama unavyojua, marafiki wanajaliana, hivyo jali kuhusu wateja wako a wao watajali kuhusu wewe. Watakuwa na wewe kwenye biashara yako mara zote.

SOMA; Hii ndiyo changamoto kubwa inayoua biashara ndogo hapa Tanzania.

4.     Usifikirie faida pekee.
Najua unafanya biashara ili upate faida, lakini hili lisiwe lengo lako kuu, kama unataka kujenga wateja wa kudumu kwenye biashara yako. Unapoangalia faida pekee kuna fursa utazikosa za kuwasaidia wateja wako, ambapo watakuthamini mno. Msukumo wa kwanza wa biashara kwako uwe kutoa mchango na thamani kwenye maisha ya wengine, kwa kufanya hivi faida itakuja bila hata ya kutumia nguvu kubwa.  Unapoangalia kuongeza thamani na maana kwenye maisha ya wengine, wanaliona hilo na wanakuamini zaidi. Watakuwa wateja wako wa kudumu.

5.     Tatua changamoto za wateja marafiki zako.
Marafiki wa biashara yako, kuna wakati ambapo watakutana na changamoto kupitia biashara yako. Labda watalipia huduma halafu wasiipate vizuri, au watanunua bidhaa na washindwe kuitumia. Au hata wakati mwingine watafanya makosa fulani ambayo yanawafanya washindwe kutumia au kufurahia bidhaa au huduma waliyonunua kwako. Wasaidie wateja wako kuondokana na changamoto hizo na watakuwa wateja wa kudumu kwenye biashara yako.

Je unawezaje kuikuza biashara yako?
Kwa kuanza na kutoa huduma bora kabisa kwa wateja wako, utakuwa na wateja ambao wanakuamini na kuiamini biashara yako, hii ni hatua muhimu kabisa na ya kwanza ya kukuza biashara yako.

Baada ya kuwa na wateja wa kudumu kwenye biashara yako, kila siku boresha biashara yako, wafanyabiashara wengi wamekuwa wanashindwa kutokana na kufanya kwa mazoea, sasa wewe usiwe hivyo. Badala yake badili na boresha biashara yako kila siku.

Wafikie wateja wengine wa biashara yako kupitia wateja ulionao sasa. Hii ni mbinu muhimu ya kuikuza zaidi biashara yako. Tumia wateja ulionao sasa kuwafikia wateja wengi zaidi. Unaweza kuwaomba wateja hao kuwaambia watu wao wa karibu ili nao wawe wateja wako.

SOMA; Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

Mwisho kabisa endesha biashara yako kisasa, usiendeshe kwa mbinu za kizamani. Weka vizuri kumbukumbu zako za kibiashara, kuwa na wafanyakazi waaminifu na wanaojituma na pia kadiri biashara inavyokuwa, wekeza faida kwenye biashara ili iweze kukua zaidi.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza ili uweze kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio, na uweze kufikia ndoto za maisha yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz 

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.


Sababu 4 Kwanini Unakata Tamaa Mapema Kwenye Ndoto Zako.

$
0
0
Kuna wakati katika safari ya mafanikio, hujikuta tuna malengo mazuri sana ambayo huamini kabisa yatatufikisha kwenye mafanikio makubwa. Hata hivyo, pamoja na uzuri  wa malengo hayo, hujikuta tena tunaanza kukata tamaa katika kuelekea kutimiza malengo hayo.
Je, umeshawahi kujiuliza ni nini hasa huwa chanzo ama sababu ya wengi kukata tamaa kuelekea kwenye ndoto zao? Kama ni malengo wanayo mazuri, kama ni hamasa wameanza nayo vizuri, je, sababu ipi ya ziada ambayo hupekea wao kukata tamaa ?
Yapo mengi sana ya kujiuliza, lakini kwa kusoma makala haya utajifunza na kupata majibu kwa nini hata wewe unaweza kukata tamaa kuelekea kwenye ndoto zako ambazo ulikuwa unaziamini.
Zifuatazo Ndizo Sababu 4 Kwanini Unakata Tamaa Mapema Kwenye Ndoto Zako.
1. Huamini tena kama utafanikiwa.
Kwa kawaida unapoanza kufanya jambo fulani, unaweza ukawa na matumaini makubwa sana ya kulifanikisha jambo hilo. Hata hivyo jinsi siku zinavyokwenda, pengine kutokana na changamoto za hapa na pale ni rahisi kujikuta unaanza kukosa tumaini la kufanikisha ndoto zako.
Hii ni sababu kubwa sana inayopelekea wengi kushindwa tena kuendelea na ndoto zao. Unapokuwa unakosa imani au matumaini na kile unachokifanya na kuamini kwamba hakiwezi kufanikiwa tena, basi huo ndio unakuwa mwisho wako.

Acha kupoteza tumaini la mafanikio yako.
Suluhisho.
Ng’ang’ania ndoto zako mpaka ufanikiwe. Siri ya mafanikio ipo kwenye kung’ang’ania na kuweka imani kubwa kubwa kwamba kwa vyovyote ni lazima nifanikiwe
2. Kushindwa kuona matokeo ya haraka.
Watu wengi huwa ni wepesi sana wakuacha ndoto zao hasa pale wanaposhindwa kuona matokeo ya haraka. Utakuta mtu kaanzisha mradi fulani mwezi huu, lakini anataka kuona mradi huo ukimzalishia upesi na kumpa faida ya kutosha ndani ya kipindi cha muda mfupi sana.
Ili kufanikiwa, jenga tabia ya kufatilia kitu mpaka uone matokeo yake ya mwisho. Acha kuishia kati na kutaka mafanikio ya haraka. Hakuna mafanikio ya kweli ambayo unaweza ukayapata kwa haraka sana. Mafanikio yote yanajengwa hatua kwa hatua, tena wakati mwingine kwa muda mrefu sana.
Suluhisho.
Unaposhindwa kupata matokeo ya haraka hebu kuwa mvumilivu. Kwa bahati mbaya sana wengi ambao huwa wana haraka, kufanikiwa kwao huwa kugumu sana. Hebu vumilia ili ujenge mafanikio ya kudumu kwenye maisha yako.
3. Kukosa nidhamu.
Mafanikio yoyote yale yanahitaji nidhamu ili uweze kuyafikia. Wengi huwa ni watu wa kushindwa kufikia malengo yao kwa sababu ya kukosa nidhamu. Moja ya nidhamu inayokosekana na kupelekea kukata tamaa mapema ni nidhamu ya kutenda kwa bidii na kwa nguvu sana kwa kile unachokifanya.
Ipo haja kubwa sana ya kuendeleza nidhamu ya kufanya kile unachokifanya hata kama unaona hakikuletei matokeo chanya. Kama utakosa nidhamu ya kufanya kwa bidii, kwa juhudi kubwa na kujituma ni wazi kabisa huwezi kufanikiwa kwenye maisha.
Suluhisho.
“Ni muhimu kujitengenezea nidhamu kubwa ya mafanikio ili ikusaidie kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio”.
4. Kuchukua ushauri mbovu.
Kati ya kitu ambacho huwa kinaonekana ni chepesi kupatikana ni ushauri. Pamoja na wepesi huo wa ushauri kupatikana, lakini kwa bahati mbaya ushauri mwingi huwa ni mbovu. Wengi wanaotoa ushauri huo huwa si wataalamu wa kile wanachokifanya.
Sasa inapotokea ukapewa ushauri mbovu na ukaufanyia kazi ni rahisi sana kukupoteza na kukufanya ukate tamaa kabisa juu ya ndoto zako. Ukiangalia kuna wakati wengi wamekatisha ndoto zao kwa sababu ya aina fulani ya ushauri ambao walipewa na kwa sasa umewapoteza.
Suluhisho.
“Jifunze kuchukua ushauri bora. Acha kubeba tu ushauri kwa kila mtu, hiyo itakuwa sio njia salama sana na sahihi kwako kama kila ushauri utaamua kuuchukua. Kumbuka ukipewa ushauri wa kitaalamu utafanikiwa”
Kabla sijaweka kalamu yangu chini, naomba uzingatie kwamba, kama huamini tena utafanikiwa, unataka matokeo ya haraka, umekosa nidhamu na unachukua ushauri mbovu kwa watu usiokusaidia, elewa hayo ndiyo baadhi ya mambo yanaweza kukufanya ukakata tamaa kwenye ndoto zako.
Chukua hatua za kubadili maisha yako na kwa makala nyingine za mafanikio tembelea DIRAYA MAFANIKIO kuweza kujifunza zaidi.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
www.amkamtanzania.com  

Uchambuzi Wa Kitabu; The Most Successful Small Business In The World (Kanuni Kumi Za Kuwa Na Biashara Ndogo Yenye Mafanikio Makubwa.)

$
0
0
Uchumi wa nchi yoyote inayoendelea au iliyoendelea unabebwa sana na biashara ndogo. Biashara ndogo ndiyo zinatoa ajira kwa wengi waliokosa ajira na pia zinawaongezea kipato wale ambao kipato cha ajira hakiwatoshi.

Pamoja na umuhimu huu mkubwa wa biashara ndogo, bado ndiyo zinakumbwa na changamoto kubwa katika uendeshaji na ukuaji. Wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa watumwa wa biashara zao, zinawategemea moja kwa moja na bado hawawezi kuzikuza.
Mwandishi Michael Gerber anatufundisha kanuni kumi za kusimamia kwenye biashara ndogo ili iweze kuwa na mafanikio makubwa. Katika kitabu chake cha THE MOST SUCCESSFUL SMALL BUSINESS IN THE WORLD, THE TEN PRINCIPLES, Michael anatushirikisha dhana ya mara 10,000. Kwamba biashara yoyote ndogo inaweza kukua zaidi ya mara elfu kumi ya ilipo sasa.

Je ungependa biashara yako ndogo iwe na mafanikio makubwa sana? Ungependa biashara yako ndogo ikue zaidi ya mara elfu 10 ya ilivyo sasa? Kama majibu yako ni ndiyo karibu tujifunze kanuni kumi za kuzingatia kwenye kuendesha biashara ndogo ili ziwe kubwa na zenye mafanikio.

KANUNI YA KWANZA; Biashara ndogo, ikijengwa vizuri inaweza kukua mara 10,000 zaidi ya ilivyo sasa.

1. Mafanikio ya biashara yoyote yanaanzia kwenye msingi ambapo biashara hiyo imejengwa. Kama biashara itajengwa kwenye misingi sahihi basi itaweza kukua na kuleta mafanikio. Wewe kama mfanyabiashara unahitaji kuweka misingi sahihi ya biashara yako, usichukulie kama ni kitu unajaribu, bali chukulia kama kitu cha kukujengea uhuru wako.
 

2. Makosa makubwa ambayo yanazuia watu wanaoanzisha biashara kuzikuza ni pale wanapogeuza biashara zao kuwa kazi. Wanachofanya ni kuanzisha biashara na wao ndiyo wanaofanya kila kitu, wanakazana kufanya na kukosa muda wa kufikiria zaidi ya biashara waliyonayo sasa. Usiigeuze biashara yako kuwa kazi, bali igeuze kuwa mashine ya kuzalisha kazi.

3. Ili kuijenga biashara yako kwenye msingi sahihi, na ili uweze kuikuza, basi anza kufikiria mara 10,000. Fikiria biashara yako mara elfu kumi ya ilivyo sasa. Kama ni duka fikiria una maduka elfu kumi, kama ni nyumba fikiria una nyumba elfu kumi. Biashara yoyote, ifikirie kwa kiwango cha mara elfu kumi ya hapo ulipo sasa. Ukishafikiria hivi sasa jiulize unawezaje kufika hapo.

SOMA; Namna Unavyoweza Kukuza Biashara Yako Hadi Kufikia Utajiri.

KANUNI YA PILI; Biashara ndogo haiwezi kuwa bora zaidi ya wazo la biashara hiyo.

4. Kama wazo pekee la biashara yako ni kufanya kazi na kupata fedha, basi hapo ndipo biashara yako itakapoishia, kila siku utapata kazi ya kufanya na kupata kipato cha kukutosheleza pale ulipo. Biashara haiwezi kukua zaidi ya hapo. Ili biashara ikue zaidi, ni lazima mawazo yako yawe zaidi ya kupata kazi na kuingiza kipato.

5. Tengeneza biashara ya kipekee kwa kuja na wazo la biashara linaloendana na wewe, na linaloweza kukua zaidi ya kuwa tu biashara ndogo. Kwa biashara yoyote unayofikiria kufanya, fikiria unawezaje kuikuza zaidi, unawezaje kufia mbali zaidi ya kufanya kazi na kulipwa kila siku. Wazo lako la biashara ndiyo litaiwezesha biashara kukua au kubaki kuwa ndogo milele.

6. Unapofikiria kuingia kwenye biashara, unapoifikiria biashara yako, basi pata taswira ya biashara kubwa. Hata kama unaanza na duka moja, fikiria kuwa na maduka mengi ziadi, au kuwa na duka kubwa zaidi. Ona ukiwa na watu wa kukusaidia kwenye biashara yako na siyo wewe peke yako kwa miaka yote.

SOMA; Mambo 20 niliyojifunza kutoka kitabu cha The Innovator’s Dilemma

KANUNI YA TATU; Biashara ndogo ni mfumo ambao vipande vyote vinachangia kufanikiwa au kushindwa.

7. Hakuna biashara ambayo inafanikiwa au kushindwa kwa sababu ya kitu kimoja. Biashara yoyote ni mfumo kamili wenye vipande ambavyo vinategemeana. Vipande hivi ndiyo vinafanya biashara ifanikiwe au ishindwe.

8. Biashara yoyote ina vipande vya ndani na vipande vya nje.
Vipande vya ndani ni mikakati ya kibiashara, uongozi wa biashara na mpango wa ukuaji.
Vipande vya nje ni wateja, washindani, fedha na mawasiliano.
Vipande hivi vinapokuwa vizuri, kwa pamoja vinajenga biashara yenye mafanikio. Kama kuna ambacho kitapuuzwa basi biashara itakufa na kushindwa.

9. Biashara yenye mafanikio ila ulinganifu wa vipande vyote muhimu vya biashara, na ulinganifu unaleta usawa kwenye biashara na usawa unaleta msimamo wa biashara hiyo.

KANUNI YA NNE; Biashara ndogo ni lazima iwe endelevu katika nyakati zote za kiuchumi, kwenye soko lolote na itoe thamani kwa wateja wake.

10. Biashara yako ili iweze kukua nakufikia dhana ya mara 10,000 ni lazima iweze kudumu na kuwa endelevu katika nyakati zote za kiuchumi, uchumi ukiwa mbaya au ukiwa mzuri, lazima biashara yako iweze kuwa endelevu. Pia biashara hiyo iwe inawezekana kufanyika popote, iweze kumudu soko lolote na muhimu zaidi iwe inatoa thamani kwa wateja wake.

SOMA; Kanuni Sita (6) Muhimu Za Kuzingatia Ili Uweze Kuwa Mjasiriamali Bora Na Mwenye Mafanikio.

11. unapoijenga biashara yako, mara zote mfikirie mteja wako. Na hapa kuna maswali muhimu sana ya kujiuliza kuhusu mteja wa biashara yako. Yuko wapi, ana changamoto gani, atanunua kwako mara ngapi, na faida kiasi gani utatengeneza kupitia kila mteja.

KANUNI YA TANO; Biashara ndogo ni shule ambapo kila mfanyakazi ni mwanafunzi mwenye lengo la kukua.

12. Ukuaji wa biashara yako, unategemea ukuaji wako binafsi na ukuaji wa wafanyakazi wako. Wewe mwenyewe na wafanyakazi wako mtakua kama mtakuwa tayari kujifunza. Hivyo ni muhimu mno wewe ujifunze na pia uwafundishe wafanyakazi wao na wao wenyewe pia wajifunze. Kama hamjifunzi, biashara haiwezi kukua.

13. Wafanyabiashara wengi wanapoingia kwenye biashara zao, hutingwa na kukosa muda wa kujifunza. Wengine huona kujifunza siyo muhimu kwao kama kufanya kazi na kuingiza kipato, hii imekuwa inawakosesha fursa za kukua zaidi.

14. Moja ya somo unalotakiwa kulijua na kuwafundisha wafanyakazi wa biashara yako ni nadharia ya kazi sahihi. Ni lazima kila mfanyakazi wa biashara yako ajue ipi ni kazi sahihi kwenye biashara yako. Hii ni kwa sababu muda ni changamoto na mambo ya kufanya ni mengi. Lazima muweze kuweka vipaumbele na kufanya yale ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa biashara. Kwa sababu siyo kila kazi inaweza kukuza biashara yako.

KANUNI YA SITA; Biashara ndogo lazima iwe na kusudi na maono makubwa.

15. Ukuaji wa biashara yoyote utategemea kusudi la kuanzishwa kwa biashara hiyo. Hivyo biashara yenye kusudi kubwa na maono makubwa itakua kuliko ile ambayo haina maono makubwa. Kuwa na maono makubwa kuhusu biashara yako na yaishi kila siku.

16. Moja ya kusudi la biashara inapaswa kuwa kutatua changamoto za watu. Japokuwa faida ni sehemu muhimu, biashara haiwezi kukua kama hakuna changamoto na matatizo ya watu inatatua. Hivyo usifikirie faida pekee, bali fikiria ile maana ambayo biashara yako inatengeneza kwa wengine.

KANUNI YA SABA; Biashara ndogo ni tunda la kusudi kubwa la yule anayeianzisha.

17. Biashara yako ni zao la mawazo yako, mtazamo wako na maono ya maisha yako. Huwezi kuwa na maono madogo ukaweza kuwa na biashara kubwa. Kama unaona biashara yako haikui, hebu anza kujiangalia wewe mwenyewe, ni maono gani makubwa unayo kwenye maisha yako.

18. Kila mtu ana kitu cha kipekee ambacho kipo ndani yake. Mtu akijua na kuweza kutumia kitu hiki ataweza kutoa mchango mkubwa kwenye jamii inayomzunguka. Kama unataka kujenga biashara kubwa na yenye mafanikio, jua kwanza ule upekee ulipo ndani yako. Kisha utumie kuanzisha na kukuza biashara yako.

KANUNI YA NANE; Biashara ndogo ina maisha yake yenyewe.

19. Biashara ni kitu ambacho kinajitegemea chenyewe, wewe kama mwanzilishi unaipa fursa ya kukua na kutoa mchango kwa wengine. Ichukulie biashara kama kitu kilichokamilika na kinachohitaji kusaidiwa ili kukua zaidi. Kwa dhana hii utaweza kukuza biashara yako.

20. Kisheria, kampuni ambayo inatambulika kama kitu kinachojitegemea, ndiyo maana inapofilisika mmiliki hahusiki kufilisiwa. Hivi ndivyo unavyopaswa kuifikiria biashara yako, itenganishe na wewe, usiifanye kuwa wewe, bali ifanye kuwa biashara unayoweza kujiendesha yenyewe, na hapo ndipo unaweza kupata uhuru wa kweli.

KANUNI YA TISA; Biashara ndogo ni chombo cha kiuchumi, kinachoendesha uchumi na kuimarisha uchumi wa jamii husika.

21. Dhana moja unayopaswa kujua kuhusu biashara ni kwamba biashara inajenga uchumi, na siyo kwamba uchumi unajenga biashara. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa kuelewa na hivyo kuruhusu biashara zao kufa pale uchumi unapobadilika. Katika nyakati ngumu za uchumi ndiyo biashara yako inapaswa kukua kwa sababu inachochea uchumi kukua. Hapa ndipo unahitaji kutoa thamani kwa wengine ili waweze kutoka kwenye hali ngumu ya kiuchumi.

22. Fedha ndiyo sehemu rahisi ya biashara. Watu wengi wamekuwa wakifikiria inapokuja swala la fedha, basi ndipo ugumu wa biashara ulipo. Lakini ukweli ni kwamba fedha ni sehemu rahisi ya biashara kama utaielewa fedha vizuri. Jua msingi wa fedha na namna inavyohusika kwenye biashara yako, na hutahangaika tena na fedha.

KANUNI YA KUMI; Biashara ndogo inatengeneza viwango ambavyo biashara nyingine zinapimwa kama zimefanikiwa au la.

23. Ili biashara yako iwe kubwa na yenye mafanikio, lazima iwe biashara ya mfano, lazima iwe biashara ya tofauti na ya kipekee, ambayo watu wataitumia kama kipimo kwa biashara nyingine, kama zimefanikiwa au la. Lazima ifike mahali kama watu wanataka kupima biashara imefanikiwa au la, basi waangalie kama inafanya kama biashara yako.

24. Unahitaji kujijengea viwango vya hali ya juu sana kwenye biashara yako, viwango ambavyo ni WORLD CLASS, viwango ambavyo havipatikani kwenye biashara nyingine yoyote. Kila siku fanyia kazi viwango hivyo na hakuna kitakachokuzuia kuwa na biashara yenye mafanikio.
Naamini umejifunza mengi kuhusu kuanzisha na kukuza biashara yako ili ikuletee mafanikio makubwa.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Mbinu Tisa (09) Za Kukuwezesha Kuwa Msikilizaji Bora Sehemu Yoyote Ile

$
0
0
Habari mpendwa Rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? natumaini unaendelea vizuri rafiki yangu na karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza kwa pamoja tofauti kubwa kati ya kusikia na kusikiliza.

Dunia ya sasa imejaa kelele nyingi. Na changamoto kubwa ni kupata mtu wa kukusikiliza kwani watu wengi wako bize na mambo yao ya kila siku. Kusikiliza ni kazi ngumu ambayo inawashinda watu wengi sana. Kumekuwa na desturi ya mtu kuongea bila hata ya kukaa kimya na kumsikiliza mwenzake amalize kuongea. Kuongea ni rahisi kuliko kusikiliza na tunashauriwa kwamba tuwe wasikilizaji bora kwani tutajifunza mambo mengi sana kuliko ukiwa mzungumzaji. Kusikiliza ni sayansi ambayo inahitaji kuhusisha mwili na akili vyote kwa wakati mmoja. Na kama ulikuwa hujui ndugu rafiki kuna tofauti kubwa kati ya kusikiliza na kusikia.
 
Kusikia (hearing) ni nini? Ni uwezo wa asili wa kupokea mawimbi ya sauti au jumbe. Kwa mfano, labda wewe uko darasani unasoma na mwalimu yuko mbele ya ubao anafundisha halafu unasikia nje sauti za magari, ndege na sauti mbalimbali huko nje wakati wewe ukiwa darasani hiyo ndiyo tunaita kusikia (hearing). Kusikia ni kitu ambacho kina kuja tu kiasili wala huwezi hata kukizuia kwa mfano; je wewe unaweza kujizuia kupiga chafya au Kukohoa? Kwa hiyo huwezi kujizuia kusikia, unasikia lakini unakuta akili yako na mwili wako haviko pale. Kwa mfano rafiki yangu hapo ulipo sasa umekaa unasoma makala hii akili yako na mwili wako umevielekeza katika kusoma makala hii lakini husikii watu, au sauti za vitu mbalimbali huko nje au pembeni yako? Sasa hiyo ndio maana halisi ya neno kusikia rafiki yangu.
Rafiki, mpaka sasa umeshajua nini maana ya kusikia. Je kusikiliza (listening) ni nini? Ni mchakato wa kuchagua nini cha kusikia kwa ajili ya kuelewa jambo fulani kwa dhumuni la tukio au shughuli fulani.

Kusikiliza ni kukusudia (intentional) una uwezo wa kuamua kusikiliza au kutokusikiliza. Kusikiliza inahusisha ujuzi ambao mtu anaweza kujifunza au kufundishwa. Kwa mfano, mwanafunzi darasani anasikiliza ili aweze kupata maarifa. Katika mahakama hakimu anasikiliza maelezo ya pande zote mbili kutoka kwa shahidi, mtuhumiwa na mawakili ili aweze kufanya hukumu.
Kwa hiyo, kuna tofauti kati ya kusikia na kusikiliza. Kuna muda mwingine tunasikia hata kama hatuko tayari kusikia kwa mfano, fikiria kelele zinazopigwa pale unapotaka kulala. Lazima utapokea mawimbi ya sauti kwa sababu una uwezo wa kusikia. Tunafanikiwa kusikia kwa sababu sisi siyo viziwi. Na kusikiliza ni kitu ambacho una hiyari nacho kusikia au kutosikiliza yaani una maamuzi ya kufanya. Kusikiliza ni kazi kuliko kusikia. Anza kuwa msikilizaji bora kuanzia leo.

Zifuatazo ni mbinu tisa (09) zitakazokuwezesha kuwa msikilizaji bora sehemu yoyote ile;

1. Kuwa na shauku ya kusikiliza. Vitu vingi tunavyofanya na kufanikiwa mara nyingi vinakuwa ni matokeo ya shauku. Hapa unatakiwa kuiambia akili yako kuwa unatakiwa kuelewa nini mwongeaji anaongea. Pili unatakiwa ujikite katika kile ambacho mwongeaji anasema. Kabla tukio fulani halijaanza kwa mfano semina, basi kitu cha kwanza wewe kuwa na shauku ya kutaka kusikiliza.

2. Kuwa wazi na jenga nia ya kujifunza. Kuna muda mwingine akili huwa inakataa kuingiza taarifa mpya hii inatokana na mitazamo mbalimbali tuliyojijengea sisi wenyewe. Unatakiwa kusikiliza vitu hata kama huviamini. Kumbuka kuna vitu hata wewe huwa unaongea na watu hawavipendi lakini wanakusikiliza hivyo basi, kusikilizwa ni hitaji la kila mtu hata kama anaongea kitu ambacho hakina maana. Kila mtu anapaswa kusikilizwa. Weka nia ya kutaka kujifunza na usijiwekee vikwazo katika akili yako ili ushindwe kusikiliza vizuri.

SOMA; Mambo 6 Yatakayokufanya Uzidi Kuwa Bora Na Mwenye Mafanikio Makubwa.

3. Ahirisha kuhukumu. Unatakiwa kuahirisha hukumu au kumkosoa mwongeaji kulingana na mwonekano wake. Kwa mfano unatakiwa usijikite katika kuangalia nguo alizovaa mwongeaji, sifa zake, mtindo wa kuongea na kadhalika. Wewe lengo lako ni kujifunza achana na mambo sijui kavaaje, na mengine. Wewe unatakiwa ujikite zaidi kusikiliza na kuchota maarifa. Mfano kama uko kwenye semina hakikisha wewe lengo lako ni kusikiliza na kuelewa yale unayofundishwa na achana na mambo mengine yanayotokea kama kuanza kumhukumu mwongeaji.

4. Jiweke tayari kimwili na kiakili. ‘’ unatakiwa kujikita (concentrate) kimwili na kiakili hata mwongeaji anapokuangalia anajua unasikiliza. Mwili wako ukae kama vile uko kwenye semina na iambie akili yako kuwa leo unakwenda kusikiliza semina na siyo kusikia semina. Dhibiti kutawanya mawazo kwa mfano, unakuta mtu kimwili yuko hapa lakini kiakili yuko dunia nyingine. Akili yako inakuwa inaruka ruka huku na huko haitulii kama vile nyani au tumbili anavyoruka ruka katika mti.

5. Muangalie mwongeaji usoni. Unashauriwa hapa kumuangalia pale anapokuwa anaongea. Macho yako na yake yaangaliane yaani muoneshe kuwa kuna mawasiliano kati ya mwongeaji na msikilizaji. Ukimuangalia mwongeaji utajifunza kwa lugha ya mdomo na lugha ya vitendo. Hivyo ni muhimu sana kumuangalia mwongeaji kwani unaweza ukaachwa katika kuelewa jambo pale anapokuwa anatumia lugha ya vitendo.

SOMA; Kitu Kimoja Ambacho Wapenda Mafanikio Wote Wanacho Kwa Pamoja.

6. Lenga katika kuelewa mtazamo wa mwongeaji. Hapa kama msikilizaji unatakiwa kusikiliza kwa lengo la kuelewa ni kitu gani mwongeaji anakiamini. Pale mwongeaji anapokuwa anaongea jambo wewe sikiliza kwa makini kabisa nini mzungumzaji anakiamini katika kile anachokiongea. Muda mwingine mzungumzaji anaweza akakosea akiwa katika jukwaa lakini hupaswi kumkosoa bali unatakiwa kuvumilia. Jaribu kuvuta picha ingekuwa ni wewe je ingekuwaje?

7. Bashiri na uliza maswali. Unatakiwa kutabiri au kubashiri maswali na kujiuliza hii njia nzuri itakayokuwezesha wewe kuwa macho na nini kinachoendelea. Bashiri je ni nini mzungumzaji anaweza kusema mbele. Unapokuwa katika semina au darasani jiulize maswali mbalimbali juu ya kitu unachosikiliza, hii itakufanya kukumbuka na kuwa macho na kitu kinachoendelea.

SOMA; Mbinu Saba(7) Za Kuongeza Ushawishi Wako Kwa Wengine Na Kupata Chochote Unachotaka.

8. Tazama/angalia kama vile unasikiliza. Unatakiwa kumuonyesha mzungumzaji kuwa unasikiliza yaani uko pale umekaa vizuri kimwili na kiakili. Kwa hiyo, mzungumzaji ataona mwonekano wako kama unasikiliza au la. Kama uko katika semina mzungumzaji anaongea na wewe umelala hii itampa picha mzungumzaji kuwa hamko pamoja. Ukiangalia kama vile unasikiliza unakuwa unampa hamasa mzungumzaji kuwa mko pamoja mnashirikiana. Unashauriwa kukaa vizuri, hakikisha mnaangaliana na mnashirikiana katika mijadala inayotokea katika semina nk.

9. Epuka vitu vitakavyokuletea kero. Ukiwa unaenda katika kusikiliza jambo kama ni semina au kitu Fulani hakikisha unavaa kulingana na sehemu husika. Vaa nguo kulingana na hali ya hewa kama unakwenda kwenye semina eneo la baridi hakikisha una vaa nguo za baridi vivyo hivyo katika joto. Kuvaa nguo ya joto sehemu ya baridi itakuletea kero ambayo baadaye inakuwa kama kizuizi na ikakupelekea usishiriki semina vizuri. Usikae karibu na mtu anayependa kuongea kwani atakupunguzia uwezo wa kujikita zaidi katika kusikiliza na kupoteza umakini.
Hivyo basi, kusikia siyo kazi bali kazi ni kusikiliza. Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Wahi Nafasi Hii Ya Kipekee Ya Kupata Milioni Ya Ziada Kwa Kuanzia Hapo Ulipo.

$
0
0
Habari za leo rafiki?
Ni matumaini yangu kwamba upo vizuri na unaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho umechagua kufanya kwenye maisha yako. Napenda nikukumbushe ya kwamba mafanikio yako, yapo hapo ulipo sasa, kwenye hicho ambacho umechagua kufanya sasa.
Unaweza kuniuliza kama ndivyo kwa nini mpaka sasa sifanikiwi? Kama mafanikio yapo hapo ulipo, kwenye hicho unachofanya, mbona mpaka sasa maisha yako yapo vile vile? Na hapa ndipo nitakapokupa siri kubwa, ambayo imewarudisha wengi nyuma licha ya juhudi ambazo wamekuwa wanakazana kuweka.

Unahitaji maarifa sahihi na mbinu sahihi ili uweze kupatumia hapo ulipo sasa kufanikiwa. Unahitaji mtazamo mpya wa kuangalia hapo ulipo na mazingira yanayokuzunguka ndiyo uweze kupatumia vizuri kwa mafanikio yako. Kumbuka macho hayawezi kuona kile ambacho akili yako haijui. Ili uweze kuziona fursa, ni lazima kwanza akili yako iwe inajua kuhusu fursa hizo. Ndiyo maana kuna watu wanazaliwa eneo fulani lenye fursa, lakini hawawezi kuzitumia, wanatoka watu mbali na kuja kunufaika nazo.

Hivyo basi rafiki yangu, una kazi kubwa ya kufanya. Una kazi kubwa ya kubadili mtazamo wako kuhusu maisha, kuhusu kile unachofanya na kuhusu mazingira ambayo upo. Una kazi kubwa ya kufanya ili kuzijua fursa mbalimbali zinazokuzunguka hapo ulipo, na jinsi unavyoweza kuzitumia kwa mafanikio yako.

Ni kazi ambayo unaweza kuichagua kuwa fupi au kuwa ndefu.
Kuichagua kuwa ndefu.
Kazi hii ya kupata maarifa na taarifa zitakazokuwezesha kubadili mtazamo wako na kuziona fursa unaweza kuichagua kufanya mwenyewe kwa kujaribu na kukosea. Hapa itakuchukua muda mrefu wa kujaribu mengi na kukosea mengi ili upate machache ya kufanyia kazi.

Kuichagua kuwa fupi.
Lakini pia unaweza kuchagua kazi hii iwe ya muda mfupi, kwa kujifunza kupitia wengine na kupata maarifa bora. Kwa njia hii utaepuka yale makosa ya wengine na hivyo kupunguza muda ambao ungeupoteza kujaribu na kukosea.

Otto von Bismarck  alipata kusema Only a fool learns from his own mistakes. The wise man learns from the mistakes of others. Akimaanisha kwamba wajinga hujifunza kwa makosa yao wenyewe. Werevu hujifunza kwa makosa ya wengine.
Je wewe unataka kuwa upande upi? Kujifunza kwa makosa yako mwenyewe pakee, au kujifunza kupitia wengine? Kama ni mwerevu utapenda kujifunza kupitia wengine, na hapa nina habari njema sana kwako;

Karibu kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA.
Tumekuandalia semina ya MILIONI YA ZIADA ambapo kupitia semina hii tutakushirikisha maarifa na taarifa za kukuwezesha kuongeza kipato chako kwa milioni ya ziada kila mwezi hata kama huna mtaji wa kuanzia kwa sasa. Taarifa kamili kuhusu semina hii zipo hapo chini;
Jina la Semina - Inaitwa "MILIONI YA ZIADA"
Itafinyika lini? – Itafanyika Jumapili ya tarehe 30 Octoba, 2016.
Itafanyika kwa muda gani? – Semina itaanza saa 3.45 asubuhi hadi saa 10.27 Jioni
Itafanyika wapi? – Itafanyika Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, Dar Es Salaam.
Ada ni Tshs ngapi? – utalipia Tshs 35,000 tu na utapata yafuatayo:
1.     Chakula kwa mtu mmoja
2.     Notibuku ya kuandika
3.     Kalamu ya kuandikia
4.     Mafunzo ya biashara kwa njia ya email na sms
5.     Utaingia kwenye kundi maalumu la wafanyabiashara ndani ya FaceBook
6.     Utakuwa ukipatiwa taarifa mbalimbali zitakazo kusaidia kukuza au kuanzisha biashara.
7.     Fursa ya ku network na wafanyabiashara wenzako.
8.     Utapata mafunzo ya jinsi ya kuingiza angalau “Milioni Ya Ziada” kila mwezi
Unalipia wapi? – Utalipa kwa njia ya simu kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253. Majina ni Amani Makirita. Ukishafanya malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na email yako kisha utatumiwa au kuletewa tiketi yako.

Kuwa mwerevu na jifunze kupitia wengine. Karibu sana kwenye semina hii ili uweze kupata maarifa sahihi ya kuongeza kipato chako kwa kuanzia hapo ulipo sasa.
Pata tiketi yako sasa, nafasi ni chache sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Ufahamu Ujenzi Wa Gharama Nafuu Wa Nyumba Bora Za Kisasa

$
0
0
Moja ya malengo niliyojiwekea katika kipindi chote cha uhai wangu ni kuhakikisha natumia uwezo wangu wote kuifanya Tanzania iwe moja ya nchi nzuri na salama kwa watanzania wote, napenda kuwa chachu ya mabadiliko endelevu ya nchi yangu Tanzania, njia mojawapo ni hii ya uandishi wa hizi Makala zinazowafikia maelfu ya watanzania popote walipo. Pia asanteni sana wasomaji wangu kwa maoni yenu mazuri na yenye tija kwa jamii yote ya Tanzania, nami nawaahidi kuwa nitaendelea kuwapa ushirikiano pasipokujali tofauti za aina yeyote ile. Hii inaonyesha mwonekano na ujasiri mkubwa sana walionao watanzania juu ya uwekezaji wa majengo tofauti na miaka kadhaa iliyopita. Uwekezaji wa majengo ni sekta mpya na inayokuwa kwa kasi sana hapa Tanzania tofauti na wakati mwingine wowote, mara nyingi jambo jipya huwa na changamoto zake ambazo ni tofauti na tulizozizoea, usikubali kirahisi hali yeyote isababishe usifikie malengo yako, njia sahihi ni kutafuta njia bora ya kuondoa changamoto zinazokukabili na siyo kukata tamaa. Makazi bora na salama ni haki ya kila Mtanzania, tuhamasishane kuweza kufikia viwango bora vya makazi ya kibinadamu. Maswali mengi Zaidi niliyoulizwa yanahusu ujenzi wa gharama nafuu. Wakati mwingine nasema ujenzi wa gharama nafuu ni kilio kikuu kwa watanzania walio wengi pasipo kujali tofauti ya vipato vyao. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kutimiza ndoto yako ya kuwa na makazi bora kulingana na kipato chako.


1. UBUNIFU WA MAJENGO
Ubunifu wa majengo ni hali ya kuumba taswira iliyo kwenye kufikiri na kuiweka katika hali Fulani ya mwonekano wa umbo halisi. Ubunifu huwa ni jambo la awali kwenye ujenzi. Ubunifu huu huwasilishwa kwa njia ya michoro ya kisanifu na hatimaye kutumika kuumba umbo halisia. Mara nyingi katika hatua hii ni vema ukajitathmini kama hicho unachofikiria kukijenga una uwezo nacho au la. Je ni mpango wa muda mrefu au muda mfupi? Unahitaji muda gani kufikia gharama halisi ya nyumba ya ndoto yako? Jipange na uwe mwenye nidhamu katika safari hii ya kufikia malengo haya. Ubunifu na mwonekano halisi wa nyumba yako hutafsiri gharama halisi ya nyumba yako. Zipo njia mbalimbali zinazotumika kupunguza gharama kwenye ujenzi wakati huohuo unafikia lengo kuu la mwonekano wa nyumba uitakayo. Mfano; njia ya kupunguza idadi ya kuta za ndani hasa zile zisizo na ulazima, kuwepo au kutokuwepo wa kuta hizo hakuathiri mgawanyo au mpangilio wa nyumba. Zungumza na msanifu majengo kuhusu mahitaji na malengo ya ndoto yako ya kuwa na nyumba uitakayo. Naamini atakushauri vizuri na atatumia taaluma yake kukusaidia kufikia kile unachofikiria kwa miaka mingi. Ubunifu ni muhimu sana, jenga nyumba bora na ya kisasa zaidi, ni bora ukajenga nyumba ndogo yenye mwonekano mzuri, kuliko nyumba kubwa na ukashindwa kuimaliza, huko ni kukosa mipango bora na yenye uhakika.

SOMA;  Hatari Tatu Zinazoukabili Uwekezaji Wako Wa Majengo Na Namna Ya Kuepukana Nazo.

2. USIMAMIZI WA UJENZI
Hii ni hatua muhimu sana ambayo haipaswi kupuuzwa, ni hatua ambayo ubunifu uliowasilishwa kwenye michoro kutafsiriwa na kuwa katika umbo lenye mwonekano halisi. Ni vema ukaambatana na mjuzi wa ujenzi katika kusimamia ujenzi wako ili akushauri kwenye hatua mbalimbali, ujenzi wa kisasa ni tofauti sana na ujenzi tuliozoea nyakati zilizopita, nyumba za kisasa zina mifumo mingi ili kukidhi mazingira halisi ya leo na kesho. Sayansi na teknolojia ya sasa inatulazimisha tutumie ujuzi wa kitaaluma kwenye ujenzi hata ule ambao ni mdogo Zaidi, hii ni kutokana na nyumba za kisasa kuhitaji mifumo mingi inayohitaji taaluma tofauti tofauti ili kukidhi mahitaji ya lazima kwa matumizi ya jengo. Ni muhimu sana kupangilia aina za kazi kiutendaji, ni mhimu sana kuwafahamu mafundi wako kiutendaji, pia ni muhimu sana kufahamu tabia za watu wote wanaohusika kwenye ujenzi wako. Usiwapuuze wazembe na wote wenye mtazamo hasi juu ya kile unachofikiria katika usahihi wake na kamwe usimwamini yeyote kwa maneno pasipo kujiridhisha, weka msimamizi bora, mwaminifu na mjuzi wa mambo ya ujenzi ili akusaidie kutembea katika dira uliyoichagua, namaanisha gharama, ubora na muda utakaoutumia kujenga nyumba hiyo. Weka mifumo itakayoweka wazi ununuzi wa vifaa vya ujenzi, matumizi yake na ulinganifu wake, mifumo hiyo itakusaidia kufanya uhakiki wa kila kilichotumika na uhalisia wa gharama zake. Kutofanya hivyo ni kujiweka kwenye hatari ya kutofikia lengo lako kwa uhakika, ni kujiweka katika hatari usioijua.

SOMA; Faida Za Uwekezaji Wa Majengo Kwenye Maeneo Salama Na Yaliyopimwa Na Wataalam Wa Ardhi

3. SERA NA UTAWALA KISIASA
Mara nyingi nimelisema hili na leo nalisema tena, ni muhimu sana kuwashauri viongozi wetu wa kisiasa kuwa vifaa vya ujenzi vipewe kipaumbele hasa kuhusu gharama kubwa ambazo watanzania wengi bado hawawezi kukidhi na kuwa na makazi bora ingawa ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kuwa na makazi bora na salama. Uchumi wowote ule, uwe wa mtu binafsi au wa nchi kwa ujumla huathiriwa na sera za wakati huo na vipaumbele vya utawala kisiasa. Makazi ni moja ya mahitaji ya lazima ya binadamu yeyote, kutokuwa na makazi bora na salama ni kuhatarisha uhai, kwa umoja wetu tuhamasishane tudai sera endelevu na rafiki zitakazotusaidia kupunguza makali ya gharama za ujenzi. Saruji, nondo, rangi, kokoto, mchanga, mabati ni moja ya malighafi katika ujenzi ambazo huzalishwa hapa hapa Tanzania, hivyo ni rahisi tukaweka mikakati ya kuwa na bei rafiki kwa watanzania wa vipato vyote na hatimaye kila mmoja wetu apate ahueni ya maisha. Wachumi na watu wa mipango ya maendeleo ya jamii naomba mtusaidie hili jambo.

SOMA; Ili Upate Mafanikio Ya Kudumu, Wekeza Kwenye Ardhi Na Majengo.

4. ZINGATIA USHAURI
Unapaswa kutambua kuwa ujenzi ni uwekezaji ambao haupaswi kulinganishwa na uwekezaji wowote uliokwishatokea, hivyo hupaswi kupuuza hatua yeyote uliyokwishaifanya na ambayo unatarajia kuifanya. Kwenye ujenzi hakuna jambo dogo linalopaswa kupuuzwa, unapaswa kujipongeza kwa kila hatua uliyofikia, endelea na ifanye nyumba yako kuwa mahali bora na salama kwa kila atakayefika hapo. Mambo hayo matatu ni miongoni mwa sababu zinazoathiri jitihada zetu za kuwa na makazi bora kwa gharama nafuu. Kutokuwa na ubunifu na usimamizi bora kabla na wakati ya ujenzi kutakuongezea gharama mara dufu Zaidi. Utawekewa malighafi zisizofaa na utaambiwa vitu ambavyo havipo wala havipaswi kuwepo kwenye mfumo wa ujenzi wako, huko ni kutengeneza nyumba nyingine usiyoijua. Ni hatari na hasara katika uchumi wako. Ni vema ukafanya ujenzi wako kwa uhakika na furaha kwa kutembea na mtu atakayelinda dira yako hata kukamilika kwake.
Tuendelee kuwa pamoja kupitia AMKA MTANZANIAtufike kwenye kilele cha mafanikio, pia endelea kufuatilia makala zijazo ili ujifunze zaidi.
Mwandishi wa makala hii ni mwanataaluma na mshauri wa ujenzi.
Anapatikana kwa: Simu: +255 685 729 888
Baruapepe: kimbenickas@yahoo.com
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>