Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

Hizi Ndizo Hazina Saba (07) Muhimu Katika Maisha Ya Ndoa.

$
0
0
Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa AMKA MTANZANIA? Natumaini ni buheri wa afya kabisa. Mpendwa msomaji, napenda kukualika katika makala hii ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja.
Mtu pekee unayeweza kumbadilisha na kumuongoza kama vile unavyotaka wewe ni wewe mwenyewe na wala siyo mwenza wako au watu wengine. Kama unataka kumpata mtu sahihi wa kuishi naye katika maisha ya ndoa anza kuwa wewe mwenyewe, kuwa mtu sahihi halafu utampata mtu sahihi anayeendana na wewe. Usipoteze muda kumtafuta mtu sahihi wakati wewe mwenyewe siyo sahihi. Usimbadilishe mwenzako wakati wewe mwenyewe hujabadilika hivyo basi, anza kubadilika kwanza wewe na wengine watabadilika.


Watu wengi kabla ya kuingia maisha ya ndoa wanakua na tabia tofauti, kila mtu anakua na tabia yake ambayo anaificha ili mwenzake asiione. Kwa lugha rahisi watu wanapoanza uhusiano wanakua wanavaa maski usoni yaani wanavaa nyuso za bandia. Hapa kila mhusika anakua anaficha makucha yake badala ya kuwa muwazi kwa wenzake. Badala ya kua wazi kwa mwenzako na kuonyesha udhaifu wako kama mwenzako atakupenda kulingana na udhaifu wako wewe unaficha makucha yako na matokeo mnakua mnatengeneza bomu nyie wenyewe na linakuja kuwalipua wakati mnapokua katika maisha ya ndoa.

SOMA; Hizi Ndiyo Njaa Mbili Zinazowasumbua Wanandoa Katika Maisha Yao Ya Ndoa.

Kama wewe unalalamika kuwa maisha ya ndoa ni magumu kuna wenzako wanafurahia na kuona maisha ya ndoa ni ya furaha. Kuishi maisha ya furaha katika ndoa ni uamuzi wako wewe mwenyewe wala huhitaji wahisani kutoka nje. Maisha ya furaha katika ndoa unayachagua wewe mwenyewe na maisha ya kutokua na furaha katika maisha ya ndoa unayasababisha wewe mwenyewe.

Mpenzi msomaji, maisha ni furaha na hujazaliwa kuja duniani kuteseka. Una nguvu kubwa sana ya kuchagua kuishi vyovyote unayotaka kuishi katika maisha yako ya ndoa. Mtu pekee anayeweza kuleta furaha katika ndoa yako ni wewe mwenyewe. Usisubiri kupewa ruhusa ndio uanze kuishi maisha ya ndoa yenye furaha, usisubiri ukamilifu katika ndoa yenu ndio muanze kuishi maisha ya furaha bali wakati sahihi wa kuishi maisha ya furaha ni sasa hivi na siyo kesho. Mna kila kitu cha kuwafanya muwe na furaha msiendeshwe na sababu za nje jitoe kulingana na nafasi yako. Kama maisha yenu ya ndoa yanaendeshwa na sababu za nje (external factor) basi, mpo katika hatari ya kuingia shimoni.

Kuna vitu vingi vinavyosababishwa na wanandoa wenyewe kufanya maisha yao kuwa machungu badala ya furaha. Mfano, kulalamika na kulaumiana. Utamaduni wa kulalamika na kulaumiana katika maisha ya ndoa unazaa mtazamo hasi mkubwa sana. Unakuta baba ni mlalamikaji na mama ni mlalamikaji sasa hapo unategemea ndoa kuwa na furaha? Badala ya kulalamika na kulaumiana mnatakiwa kukaa chini na kuchunguza kiini cha tatizo ni nini? Kulalamika na kulaumiana ndio kunafanya ndoa kukosa furaha, amani, upendo n.k. msitupiane mpira katika hili bali kueni watatuzi. Kulalamika na kulaumiana na kila mmoja kuona mwenzake ndio mkosaji na yeye hastahili ndio adui wa furaha yenu. Msilalamike kwani mnapoteza nguvu na muda wenu bure.

SOMA; Hawa Ndio Maadui Wakubwa Wawili Wa Uchumba Au Ndoa Yako.

Ndugu msomaji, karibu sasa katika kiini cha somo letu la leo ambapo leo tutajifunza hazina saba muhimu katika maisha ya ndoa. Na hazina hizo ni kama ifuatavyo;

1. Kusaidiana; maisha ya ndoa yana hitaji hali ya kusaidiana sana katika shida na raha. Usimpende mwenzako wakati tu akiwa mzima. Mwenzako anapokua na tatizo mtu wa kwanza wa kumsaidia ni mwenza wake. Kama wenzako amepatwa na tatizo vaa viatu vya mwenzako msaidie kutafuta suluhisho la tatizo na siyo kumuacha peke yake. Tabia ya kusaidiana inaleta furaha, faraja katika maisha ya ndoa. Badala ya kugeuka kuwa mwiba kuwa msaada. Onesha hali ya kujali na kumsaidia mwenzako pale anapokua anaumwa, mhudumie kwa ukarimu wa hali ya juu mpaka ahisi anapona. Maisha ya ndoa yako kama biashara na mteja wako mkubwa ni mwenza wako hivyo hakikisha unamhudumia vizuri katika kiwango cha hali ya juu mpaka mteja wako asiwe na wazo la kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine. Kama mteja wako unampatia huduma bora na ya uhakika na hakuna kitu anachokosa hawezi kuondoka. Hakikisha unampatia mwenza wako huduma bora. Kwa hiyo, maisha ya ndoa ni kusaidiana unatakiwa kuweka vyeo na nyadhifa mbalimbali ulizonazo kazini kwako na kujishusha na kuwa mnyenyekevu kwa mwenzako.

2. Kutiana moyo; mtu wa kwanza wa kukutia moyo katika jambo Fulani unalofanya ni mwenza wako wa ndoa. Mpe moyo mwenza wako. Kuwa kichocheo cha hamasa katika kile anachofanya. Mwenzako akiwa katika wakati mgumu mtie moyo na kumpa matumaini, muoneshe uko naye bega kwa bega. Kwa namna hii mtafanya ndoa yenu kua na furaha na wala siyo huzuni. Usigeuke kuwa kikwazo kwa mwenzako, bali kuwa mwanga wa kumuonesha njia ya kule anapotaka kwenda. Mpeane maneno ya faraja yenye kutia nguvu, hata kama mko katika wakati mgumu msikate tama, mtie moyo mwenzako. Na habari njema ni kwamba hakuna matatizo ya kudumu katika dunia hii changamoto haikai kwa muda mrefu, inakuja na kuondoka hakuna tatizo la kudumu. Mwenzako anapofanya vizuri unatakiwa kumpongeza katika kila jambo. Usiwe mchoyo wa pongezi kwani kutoa pongezi haina gharama. Hii ndio hazina ya kuifanya ndoa yenu kuwa na furaha.

3. Kusikilizana; Katika hali ya kawaida kusikiliza ni kazi kuliko kuongea. Kila mtu ana haki ya kusikilizwa. Mwache mwenza wako aongee mpaka amalize na wewe kaa kimya wala usimwingilie anapokua anaongea. Hata kama mwenzako hana cha maana cha kuongea wewe muheshimu tu na msikilize kwa unyenyekevu. Msikilize naye ajione anathaminiwa katika hii dunia. Katika maisha ya ndoa kuwa msikilizaji mzuri utafanya ndoa yako kuwa ya furaha. Kuna wengine wanahitaji kusikilizwa lakini hawapati nafasi ya kusikilizwa. Unatakiwa kuonesha ukaribu hata wa kuuliza swali kuonesha kuwa uko karibu naye. Kusikilizana huleta ukaribu wa pamoja.

SOMA; Vikwazo Vitano(5) Vinavyoharibu Mahusiano Yetu Na Ndoa Zetu Na Jinsi Ya Kuviepuka.
 
4. Kukubaliana; katika maisha ya ndoa mnatakiwa kukubaliana kulingana na mapungufu yenu au madhaifu yenu. Kwanza hakuna aliye mkamilifu kwenye kila kitu katika hii dunia. Unatakiwa kumpokea mwenzako jinsi alivyo. Mfundishe pale anapoenda vibaya. Usimhukumu mwenzako kwa sababu ya madhaifu yake. Hakuna aliyekua sahihi kuliko mtu mwingine. Mnatakiwa kuondoa hali za kujiona kuwa wewe unastahili zaidi kuliko mwenzako. Mnatakiwa kuchukuliana madhaifu yenu na kila mmoja aheshimu madhaifu ya mwenzake na siyo vinginevyo.

5. Kuaminiana; uaminifu ni hazina katika maisha ya ndoa. Uaminifu siku hizi umekua adimu sana kwenye kila kitu siyo tu maisha ya ndoa. Kile unachomfanyia mwenzako na wewe utafanyiwa. Unatakiwa kuwa mwaminifu kwa mwenzako na kumuamini mwenzako katika maisha yenu ya ndoa. Kama kuna kitu unakiona kinakosekana katika ndoa yenu kiwekeni wazi badala ya kuacha tatizo kuendelea kuwa tatizo. Kama mwenzako ni mwaminifu unatakiwa kulipa uaminifu. Imekua ni mazoea na kama vile ni fasheni siku hizi watu kuwa na michepuko ndio dili na kusahau kuwa ndoa yako ndio dili hivyo unatakiwa kurudi katika mstari. Uaminifu ni tunda adimu sana linalotafutwa katika maisha ya ndoa. Kila mtu anahitaji uhuru wa kufanya mambo yake hivyo kuwa na uaminifu katika maisha yenu ya ndoa na kila mmoja ampe mwenzake uhuru kwani kama uaminifu upo basi ndio silaha kuu katika ndoa yenu.

6. Kuheshimiana; kila mtu anahitaji kuheshimiwa. Usimdhalilishe mwenzako mbele ya watu kwani ni fedheha kubwa. Unatakiwa kuheshimu kile anachopenda mwenzako na wala usimlazimishe kufanya kile unachopenda wewe kufanya. Kila mtu ana machaguo yake na kuchagua ni maamuzi pia. Kama ukiwa na heshima siku zote utatenda kwa heshima. Unatakiwa kuheshimu mawazo ya mwenzako. Unatakiwa kuheshimu hisia za mwenzako. Usigeuke kuwa mtawala na kumuongoza mwenzako kwenye kila kitu bali unatakiwa kumpa mtu uhuru wa kufanya kile ambacho anapenda ili mradi tu asitoke nje ya utaratibu na kutovunja sheria nyingine za ndoa. Matatizo huanzia pale unapomlazimisha mwenzako kufanya vile unavyotaka wewe.

SOMA; Mambo Kumi (10) Muhimu Ya Kuzingatia Kabla Hujafunga Ndoa Na Utajiri.

7. Kuvumiliana na kusameheana; siri ya maisha ya ndoa ni kuvumiliana na kusameheana. Tatizo linapotokea siyo kukimbiliana katika kutalakiana bali mnatakiwa kutatua na kuvumiliana. Kama umekosa uvumilivu katika maisha ya ndoa basi hata safari ya kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako itakushinda. Kila kitu kinahitaji uvumilivu. Mwenzako akikukosea mnatakiwa kusameheana na kufutiana hatia iliyo kati yenu na siyo kulipiana visasi. Msamaha unaondoa uchungu ulioumbika katika mioyo yenu na unarudisha mahusiano mapya ya awali.
Kwa hiyo, tunatakiwa kuishi maisha ya furaha kwa kutumia hazina hizi saba tulizojifunza leo. Wanandoa wengi wanakabiliwa na changamoto ya kutoridhishana katika tendo la ndoa. Kuridhishana katika tendo la ndoa ni kushirikishana zawadi ya tunda la ndoa. Kila mlengwa anapaswa kumhudumia mteja wake vizuri ili kuepuka matatizo ya mara kwa mara.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Hii ndiyo changamoto kubwa inayoua biashara ndogo hapa Tanzania.

$
0
0
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa watu kuingia kwenye biashara. Hii imetokana na hali ya uchumi kuwa ngumu na kipato kimoja, hasa cha mshahara kutokutosheleza mahitaji ya msingi ya maisha. Pia kumekuwa na fursa nyingi za mahitaji ya watu na hivyo watu kuchukua nafasi kutimiza mahitaji hayo na wao kujipatia faida.

Kumekuwa na watu wengi ambao wanafungua biashara ndogo za uchuuzi, na wengine uzalishaji wa bidhaa za vyakula na mavazi. Wapo pia ambao wameingia kwenye kilimo cha kibiashara, na kulima mazao ya matunda na bustani, ambayo yanachukua muda mfupi kulimwa na pia yana uhitaji mkubwa. Fursa zote hizi zimetoa nafasi kwa watu kujiongezea kipato kupitia biashara.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA HAPA.

Licha ya kuwepo kwa fursa hizi nzuri za uhitaji wa watu, na licha ya wengi kuingia kwenye biashara hizi, kumekuwa na changamoto moja kubwa sana ambayo imekuwa inaua biashara nyingi ndogo zinazoanzishwa. Tumekuwa tunaona watu wengi wanaanzisha biashara zao wakiwa na hamasa kubwa ya kufanya vizuri, lakini haipiti miezi sita biashara hiyo inakuwa imefungwa. Tunaona watu wanakwenda shambani wakiwa na hamasa kubwa ya kupata faida kwenye kilimo wanachokwenda kufanya, lakini inapofikia wakati wa kuvuna, uzalishaji unakuwa mdogo tofauti na mategemeo, au bei ya soko inakuwa ndogo kuliko gharama mtu alizoingia.

SOMA; Kuanza Biashara Kwa Mtaji Kidogo, Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuikuza.

Biashara nyingi zimekuwa zikipata hasara na kupelekea kufungwa kutokana na changamoto hii ambayo inawakumba wafanyabiashara wengi. Leo kupitia makala hii tutakwenda kuichambua changamoto hii kwa kina, ili uweze kuondoka na kitu cha kufanyia kazi, na unapoanzisha au kukuza biashara uliyonayo sasa, usiingie kwenye makosa ambayo umekuwa unafanya miaka yote.

Changamoto ambayo imekuwa inaua biashara nyingi ndogo hapa Tanzania, ni namna ya kufikiri ambayo wafanyabiashara wanayo. Watu wengi wanaingia kwenye biashara wakiwa hawana taarifa kamili. Wanaingia kwenye biashara wakiwa na taarifa za upande mmoja pekee wa biashara, na hivyo kupata shida pale wanapokutana na changamoto za upande mwingine wa biashara. Kwa kifupi, watu wengi wanaingia kwenye biashara wakiwa na wazo moja tu, nikizalisha watu watanunua, au nikiuza, watu watakuja kununua. Hii ni mbinu ambayo ilikuwa na mafanikio zamani, wakati wachache ndiyo walikuwa wanafanya biashara, ila kwa sasa karibu kila mtu anafanya biashara, unahitaji mbinu za ziada ili kuweza kuikuza biashara yako.

Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye biashara baada ya kuona wengine wanafanya, na kwa kuwa wanaona watu hao wanafanya na wana wateja, basi moja kwa moja wanahitimisha kwamba biashara hii ina wateja wengi na inalipa, wacha na mimi niingie kwenye biashara hii. Wengine wamekuwa wanaingia kwenye biashara baada ya kusikia watu wanasema biashara hiyo inalipa, wanahamasika kupitia maneno wanayosikia, na kujikuta wameshaingia kwenye biashara ambayo hawakuijua vizuri. Kwa kuangalia kwa nje, kila biashara inalipa, kwenye hesabu za makaratasi, kila biashara inalipa. Nimekuwa nawaambia watu, sijawahi kuona mchanganuo wa biashara ambao una hasara, lakini karibu kila biashara ina hasara. Kwa kuangalia upande huu mmoja wa biashara, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiingia kwenye biashara na kujikuta kwenye wakati mgumu.

SOMA; Changamoto Ya Matumizi Mazuri Ya Fedha Za Biashara.

Hapa nakushirikisha mambo matatu muhimu ya kuzingatia kabla hujaamua kuingia kwenye biashara yoyote ile, iwe ni kuuza bidhaa, huduma au kufanya kilimo cha kibiashara.

Moja; fanya utafiti wa biashara kabla hujaingia kwenye biashara hiyo. Usiingie kwenye biashara kwa sababu unaona watu wanafanya na wana wateja, au kwa sababu umesikia kila mtu anaimba kilimo fulani kinalipa. Jipe muda na fanya utafiti, na utafiti huu ninaokuambia ufanye siyo wa kwenda kutafuta na kusoma kwenye mtandao au vitabu, badala yake watembelee wale wanaofanya biashara hiyo. Fanya nao urafiki na jifunze mengi kutoka kwao, namna wanavyo endesha biashara zao, changamoto wanazokutana nazo, na hata wanavyozitatua. Pia fanya utafiti kwa wateja wa biashara hiyo, wanapatikana wapi, mahitaji yao ni yapi na uwezo wao wa kumudu gharama za biashara husika.

Mbili; ifikirie biashara kwa ujumla, ifikirie kama mfumo na siyo kama kitu kimoja. Biashara yoyote, kwa kiwango cha chini kabisa inahitaji kuwa na angalau mifumo mitatu, usimamizi, uzalishaji na masoko/uuzaji. Wengi wanaoingia kwenye biashara huwa wanafikiria uzalishaji pekee, usimamizi na masoko/uuzaji huwa wanafikiri ni vitu vinavyokuja vyenyewe pale biashara inapokuwa imeshaanza. Matokeo yake ni watu wengi kuingia kwenye biashara na baadaye kukosa soko. Unapoingia kwenye biashara, jua kwa kina kuhusu usimamizi wa biashara hiyo, unachozalisha na soko lako na namna unavyolifikia soko hilo.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuingia Kwenye Biashara Baada Ya Kumaliza Masomo Ya Chuo.

Tatu; jitofautishe na wafanyabiashara wengine. Japo kwa sehemu kubwa wazo lako la biashara utakuwa umelipata kutoka kwenye mawazo ya wengine, usifungue biashara inayofanana na wengine kwa kila kitu. Tafuta njia ya kujitofautisha, hata kama biashara mnayofanya inafanana. Lazima uwe na kitu ambacho wateja wanakipata kwako tu na siyo kwa wengine. Kama biashara zinafanana, basi toa huduma bora zaidi ya wanazotoa wengine. Mteja anapokuwa kwenye biashara yako, ajisikie tofauti kabisa na akienda kwenye biashara nyingine. Njoo na mbinu tofauti za ufanyaji wa biashara yako, kama wengine wanasubiri wateja waje kwenye biashara zao, wewe unaweza kuwafuata wateja kule walipo.

Ni hatari sana kuingia kwenye biashara ambayo hujaijua vizuri, hakikisha umefanya utafiti, kujua biashara nzima na kujitofautisha na wengine. Kwa kufanya hivi utaondokana na changamoto inayoua biashara nyingi. Kila la kheri.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

USHAURI; Jinsi Ya Kutengeneza Biashara Isiyokutegemea Wewe Moja Kwa Moja Na Kupata Uhuru Wa Kibiashara.

$
0
0
Habari za wakati huu rafiki yangu?
Hongera kwa juhudi kubwa unazoendelea kuweka kwenye maisha yako na hivyo kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha yako. Najua mpaka sasa haupo kama ulivyokuwa hapo awali, kwa kujifunza na kufanyia kazi yale unayojifunza, maisha yako yameweza kuwa bora zaidi.

Karibu kwenye makala yetu ya leo ya kipengele cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia maisha ya ndoto zetu. Kama ambavyo nimekuwa nasema mara kwa mara, changamoto ni sehemu ya maisha yetu, hatuwezi kuzikimbia badala yake tunatakiwa kuzitatua na kusonga mbele. Kama unakutana na changamoto ni dalili nzuri kwamba kuna mambo makubwa unafanya kwenye maisha yako, lakini kama huna changamoto, kuna uwezekano mkubwa hakuna mambo makubwa unayofanya.
Katika makala yetu ya leo ya ushauri, tutakwenda kuangalia namna unavyoweza kutengeneza biashara ambayo haikutegemei wewe moja kwa moja.

Changamoto moja kubwa kwenye biashara ndogo na za kati ni biashara kumtegemea mfanyabiashara moja kwa moja. Hii ina maana kwamba kutokuwepo kwa mfanyabiashara kwenye eneo la biashara, basi biashara inakuwa imefungwa. Na pale mmiliki wa biashara anapoumwa au kupata matatizo, moja kwa moja na biashara yake pia inapata matatizo.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Moja ya malengo na faida za kuanzisha biashara, ni kupata uhuru wa kazi na kipato. Unaanzisha biashara ili uweze kuchagua namna unavyofanya kazi zako na mtu asikuwekee kikomo kwenye kipato chako. Lakini kama biashara yako inakutegemea wewe moja kwa moja, unakuwa hujapata uhuru uliokuwa unafikiria, badala ya kumiliki biashara, biashara inakuwa imekumiliki wewe.

SOMA; Wazo Bora Na Mtaji Pekee Havitoshi Kuifanya Biashara Ifanikiwe, Unahitaji Kitu Hiki Kimoja Muhimu Sana Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako.

Je unawezaje kuondoka kwenye kumilikiwa na biashara mpaka kuweza kuimiliki biashara? Hiki ndiyo tutakachojadili na kujifunza kwenye makala yetu ya leo. lakini kabla hatujaingia na kujadili kwa kina, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na hili;
Habari coach? Naomba unisaidie ni namna gani mtu unaweza kutengeneza mfumo bora wa biashara na biashara unaweza kujiendesha bila kukutegemea mmiliki moja kwa moja (kuweza kumiliki biashara sio biashara kukumiliki wewe) kwa biashara ndogo na za kati. Ahsante. Seleman E. M.

Kama ambavyo ametuandikia msomaji mwenzetu hapa, kuna watu wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati ambao wamemilikiwa na biashara zao na siyo kuzimiliki biashara zao. Tunafanyaje ili kuondokana na hili, tunajadili kwa kina hapo chini. Karibuni sana tujifunze ili kuboresha biashara zetu na maisha yetu kwa ujumla.

1. Usianze biashara bila ya kuwa na ndoto kubwa.

Sababu moja kubwa inayowafanya wafanyabiashara kubaki kwenye utumwa wa biashara kwa miaka mingi ni ndoto zao za kibiashara. Wengi wamekuwa wakianza biashara kama sehemu ya kutengeneza kipato cha ziada. Kwa hiyo wanapotengeneza kipato hicho cha ziada hakuna kingine kikubwa kinachowasukuma, hivyo wanaishia hapo.
Unahitaji kuwa na ndoto kubwa za kibiashara, unahitaji kuiona biashara yako ikikua na kuwasaidia watu wengi zaidi kuwa n amaisha bora. Ndoto hii kubwa ndiyo itakusukuma na kutengeneza biashara inayojitegemea.

Unaruhusiwa kuanza biashara kidogo, lakini usianze biashara bila ya kuwa na ndoto kubwa. Uzuri wa ndoto ni bure, hakuna anayekutaka ulipie ndoto kubwa ulizonazo, hivyo jiwekee ndoto kubwa za biashara yako, jinsi itakavyokuwa kubwa na kugusa maisha ya wengine.

SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

2. Tengeneza mifumo ya biashara mapema kabla hata hujaihitaji.
Tatizo jingine kubwa kwenye biashara ndogo na za kati ni kukosekana kwa mfumo wa biashara. Wengi wamekuwa wakifikiria kwamba biashara ni kuuza na kununua, au kutengeneza na kuuza. Hivyo wanapeleka nguvu zao maeneo hayo, wanajikuta wametingwa kila siku, lakini hawaoni hatua kubwa wanazopiga.
Unapoiendesha biashara nzima kama kitu kimoja, biashara haiwezi kujitegemea, kwani ni wewe pekee unayeweza kuielewa biashara hiyo vizuri. Ukiajiri mtu mwingine hawezi kuielewa vizuri kama wewe na hivyo kukutana na changamoto.

Tengeneza mifumo inayoeleweka ya biashara yako, ambapo majukumu kwenye mifumo hiyo yanaweza kupewa watu wengine. Kwa kuanzia na kwa biashara ndogo na za kati, angalau weka mifumo mitatu. Uzalishaji, usimamizi na masoko na mauzo. Kwenye uzalishaji hapa ndipo bidhaa au huduma inaposimamiwa katika manunuzi au matengenezo. Masoko na mauzo hapa ndipo biashara inamfikia mteja wako, usimamizi hapa ndipo shughuli zote za biashara zinaposimamiwa.

3. Ajiri watu bora na waamini.
Kitu kingine kinachowafanya wafanyabiashara wadogo na wakati kuwa watumwa wa biashara zao, ni pale wanapofikiri kwamba hakuna mtu anayeweza kuendesha biashara zao vizuri kama wao wenyewe. Hali hii inawazuia kuweza kuajiri watu ambao wangeweza kuwasaidia kuendesha biashara zao, hivyo kukazana kufanya kila kitu wao wenyewe.

Unahitaji kuajiri wafanyakazi bora, kisha kuwaamini kwamba watatekeleza majukumu yao na kuwakabidhi majukumu hayo. Ukishaajiri haimaanishi ndiyo umemaliza, badala yake unaendelea kufuatilia kwa karibu ili kujua maendeleo ya biashara yako yanakwendaje, hasa kwa maeneo hayo ambapo umeajiri.
Muhimu hapa ni kupata wafanyakazi bora, na siyo bora wafanyakazi. Kwa sababu wafanyabiashara wengi, wamekuwa wakiajiri watu ambao wanataka mshahara kidogo, mara nyingi watu hawa wanakuwa siyo bora kwa ukuaji wa biashara yako.

SOMA; Kitu Kimoja Ambacho Watu Wengi Wamekuwa Wanadanganywa Kuhusu Biashara.

4. Usiajiri mtu, ajiri nafasi.
Hapo juu tumeshaona kwamba unahitaji kuajiri watu watakaoweza kukusaidia kuendesha biashara yako. Hapa tutaangalia jambo moja muhimu sana katika kuajiri, kwa sababu hapa ndipo makosa makubwa sana yamekuwa yanafanywa na kuwaathiri wafanyabiashara wengi.

Wafanyabiashara wadogo na wa kati, wamekuwa wanaajiri mtu. Yaani wanamwajiri mtu, halafu akifika kwenye biashara ndiyo wanamfikiria anaweza kufanya shughuli zipi. Hii ni hatari kubwa kwa sababu siku akiondoka, ni vigumu kumpata mwingine kama yeye na hivyo biashara yako inatetereka.

Katika kuajiri, usimwajiri mtu halafu akifika ndiyo uangalie anaweza kufanya nini, badala yake ajiri nafasi za kazi. Yaani mwajiri mtu ukiwa tayari una majukumu ambayo anapaswa kuyatimiza, kulingana na mfumo wa biashara yako. unaweza kuajiri mtu kwa ajili ya uzalishaji, au masoko na mauzo na kadhalika. Muhimu ni kuhakikisha mfanyakazi anayajua majukumu yake kwenye biashara yako, na hata watakapotaka kuondoka, unaweza kupata wengine wa kuziba pengo lao.

5. Gawa majukumu yako kwa wengine.
Changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ni kung’ang’ania kufanya kila kitu wao wenyewe. Wakati mwingine wanafanya hivi wakiamini wanaweka ubora zaidi, wakati mwingine wanafanya hivi kuepuka gharama za kuwalipa wengine.

Lakini kuna vitu viwili ambavyo una uhaba navyo na ni muhimu sana kwako, muda na nguvu. Haijalishi una hamasa kubwa kiasi gani ya kufanya shughuli zako, kuna masaa 24 pekee kwenye siku yako, huwezi kuongeza hata dakika moja. Pia kadiri unavyofanya mambo mengi, mwili wako unachoka na nguvu zinatumia.

Kuondokana na hali hii, orodhesha majukumu yako yote kisha angalia ni majukumu yapi ambayo yanakuhitaji wewe kweli. Yale mengine ambayo kuna watu wanaweza kuyafanya vizuri, watafute watu hao na wayafanye. Siyo lazima uwe umeajiri watu hao, unaweza kuwapa wakufanyie kama vibarua au kwa mikataba maalumu.

Lengo kuu la kuanzisha biashara ni kupata uhuru wa kipato na muda, sasa kama biashara inakuwa inakutegemea wewe moja kwa moja, bado hujaweza kutengeneza uhuru wako kwenye muda na kipato. Fanyia kazi haya tuliyojifunza hapa na utaanza kuona mabadiliko kwenye biashara yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Kama Utafanya Mambo Haya, Hakuna Tena Wa Kukuzuia Kufanikiwa.

$
0
0
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa yapo mambo ya lazima ambayo unatakiwa kuyafanya karibu kila siku ili ufanikiwe. Naamini hilo lipo wazi kabisa, hiyo ikiwa na maana kwamba huwezi kufanikiwa bila kufanya mambo hayo.
Wengi hufikiri kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na akili ya ajabu  na ufanye mambo makubwa sana. kama hayo ndiyo mawazo yako, hapana hiyo haiku hivyo, mafanikio yanahitaji ufanye mambo kadhaa kwa muendelezo bila kuacha hata kama ni madogo.
Bila shaka unaweza ukawa hunielewi vizuri. Kupitia makala haya naomba nikushirikishe mambo machache ambayo ukiyafanya mara kwa mara katika maisha yako, uwe na uhakika hakuna mtu atakaye kuzuia kufanikiwa tena. Mafanikio yatakuwa ni haki yako.  
1. Kuwa mtu wa vitendo.
Siri ya ushindi wa mafanikio yako haipo kwenye kujua vitu peke yake au kuongea. Kuwa mtu wa vitendo. Kama kuna jambo umelikusudia lifanye.  Acha matendo yako yaongee zaidi na hapo ni lazima ufanikiwe.

2. Kutokuridhika mapema.
Sumu kubwa ya mafanikio ni kule kuridhika mapema. Ikiwa unataka kufikia kilele cha mafanikio makubwa, achana na kuridhika na mafanikio madogo yasiyokufikisha popote. Tafuta mafanikio makubwa zaidi ya hayo.
3. kutokuhamasishwa na pesa.
Chagua kufanya kazi bidii zote bila kusukumwa na msukumo wa nje kama vile pesa. pesa iwe ni matokeo na siyo kichocheo cha wewe kufanya kazi. Kama utafanya hivyo bila kusukumwa na pesa uwe na uhakika utafanikiwa.
4. Kujitawala.
Wakati wote jifunze kujitawala kwa mambo yako. jifunze kutawala muda, nidhamu na pesa zako. Ikiwa utaweza kumudu kujitawala wewe mwenyewe ni wazi uatajitengenezea mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
5. Kutokuogopa kushindwa.
Kama kuna kitu umepanga kukifanya, hebu kifanye bila woga. Acha kuwaza ikiwa ikatokea nimeshindwa itakuaje? Jitoe mhanga kufanikisha ndoto zako mpaka zieleweke. Kwa kufanya hivyo utakuwa mshindi.
6. Kuwa wewe kama wewe.
Mafanikio hayaji kwa kuiga vitu sana kwa wengine. Mafanikio yanakuja kwa kujijengea misimamo yako mwenyewe na kusimamia kile unachokiaminikwamba ni lazima kikufanikishe.
7. Kujifunza kila siku.
Ikiwa utakuwa unawekeza kwenye maarifa kila siku tambua ni lazima ufanikiwe. Hakuna maarifa ambayo yanaweza yakakuacha eti ukawa mtupu, ikiwa utafanyia kazi. Amua kujifunza siku zote za maisha yako.
8. Kujiamini.
Huwezi kupata mafanikio bila kujiamini. Msingi mkubwa wa mafanikio unatapatikana kwa kufanya mambo yako kwa kujiamini tena kwa sehemu kubwa. Ukijiamini utafanikisha mambo mengi na makubwa sana.
9. Kujiwekea malengo.
Kujiwekea malengo pia ni silaha mojawapo kubwa ya kukusaidia kufanikiwa. Kama huweki malengo, ni ngumu sana kwako wewe kuweza kufanikiwa kwa kile unachokifanya. Weka malengo na kisha yafuate kila siku mpaka ndoto zako zitimie.
10. Kutokuwa na kinyongo.
Ni lazima ifike mahali ukubali kwamba ili ufanikiwe hutakiwi kuwa na kinyongo na watu waliofanikiwa. Inabidi ujifunze vile vilivyowafanikisha hadi wakafikia hapo. Ukifanya hivyo, hapo utakuwa mshindi na pia utajikuta unatengeneza mafanikio kwa upande wako.
11. Kutunza muda vizuri.
Muda ni pesa. Ni vyema ukajua namna ya kutunza muda wako vizuri ili ukusaidie kufikia mafanikio makubwa. Wengi waliofanikiwa hawapotezi muda wao hovyo hata kidogo.
12. Kutokujiwekea sababu.
Chochote unachopanga kufanya, hakikisha umekifanya. Acha kujiwekea sababu zako zisizo na maana kwamba hujafanya hiki kwa sababu hii au ile. Ukiishi kwa kutojiwekea sbababu ni lazima utafanikiwa kwa viwango vya juu sana.
Kwa ufupi hayo ndiyo mambo ambayo ukiyafanya ni lazima ufanikiwe. Chukua hatua kuelekea kwenye ndoto zako.
Pia kwa makala nyingine za mafanikio na maisha, tembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

UCHAMBUZI WA KITABU; BE YOUR OWN BRAND (Pata Kile Unachotaka Kwa Kuwa Vile Ulivyo Wewe)

$
0
0
Moja ya changamoto kubwa kwa zama hizi, ni watu kuiga kile ambacho wengine wanafanya. Yaani akitokea mtu mmoja akawa ameanzisha mtindo fulani mpya, na ukawa na mafanikio, basi kila mtu anaiga mtindo huo. Iwe ni vipindi vya tv au redio, uandishi na hata aina za biashara.
Wengi wa wanaoiga vitu kwa wengine, huwa hawafanikiwi kama wale walioanzisha, na sababu kuu ni moja, hakuna kitu kimoja kinachoweza kumfaa kila mtu, ila kila mtu ana kitu cha kipekee kwake, ambacho akikijua na kukifanya, atafanikiwa sana.
Ni sababu hii ilipelekea waandishi David McNally na Karl Speak kuandika kitabu BE YOUR OWN BRAND, yaani mtu uweze kujijenga wewe kama wewe, kutokana na utofauti ulionao na wengine.


Niseme tu kwa uwazi, hakuna wakati ambao tunahitaji kujitofautisha na wengine kama zama hizi. Hii ni kwa sababu chochote unachofanya sasa, iwe ni kazi au biashara wapo watu wengi wanaofanya kitu hicho. Sasa kama utakuwa unafanya kwa ukawaida, kama wengine, unajichimbia kaburi, kwani hakuna atakayekukumbuka. Ukiweza kujitofautisha, utaweza kujenga mafanikio makubwa kwa chochote ulichochagua kufanya, hata kama ni kuuza maji, au kufagia barabara.
Karibu tujifunze kwa pamoja namna tunavyoweza kutengeneza majina yetu na kuwa wa kitofauti na wa kipekee na hatimaye kufikia mafanikio makubwa sana.

1. Kila mtu ana BRAND (chapa/jina) na kila mtu anaweza kutengeneza jina lake hilo likawa la kipekee sana kwake. Ili kujijengea jina au chapa yako, huhitaji kubadili haiba yako, badala yake unahitaji kujua kile ambacho tayari kipo ndani yako na uweze kukitumia vizuri. Huhitaji kuwa kama mtu fulani uliyemwona amefanikiwa ili ufanikiwe, ila unahitaji kuwa wewe ili ufanikiwe. Tofauti ya wale wenye brand kubwa na wanaoshindwa kuwa brand kubwa ni kujitambua na kutumia uwezo mkubwa ambao mtu anao.

2. Kutengeneza jina lako kunaanza na kile unachokifanya kwa wengine. Hukuzi jina lako kwa kujitangaza, unakuza jina lako kwa jinsi unavyogusa maisha ya wengine, kwa namna unavyowafanya kuwa bora zaidi. Hivyo unapofikiria utakuzaje jina lako, anza kujiuliza ni watu gani ambao unaweza kuwasaidia kubadili na kuboresha maisha yao. Unahitaji kujenga mahusiano bora na watu ili waweze kulikuza jina lako. Mahusiano haya yanaanza na namna unavyowafanya wajisikie kupitia wewe. Kuna usemi kwamba watu watasahau kile ulichowaambia, watasahau kile ulichofanya lakini kamwe hawatasahau jinsi ulivyowafanya wakajisikia/walivyohisi. Ndiyo maana tunawakumbuka sana waliotukasirisha au kutufurahisha kuliko waliokuwa wanaongea tu.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha The Four Purposes of Life (Makusudi manne ya Maisha)

3. Hapo ulipo wewe tayari ni brand, tofauti ni kama brand yako ni kubwa au ndogo. Wewe ni brand kwa sababu kuna picha au taswira ambayo watu wanaipata wakisikia jina lako au wakikutana na wewe. Kwa mfano ni taswira gani inakujia kwenye akili yako unaposikia jina Makirita Amani? Basi hivyo pia kuna namna watu wanapata taswira wanaposikia jina lako, iwe ni kwenye familia, kazi na hata biashara. Hii ina maana kwamba nguvu ya brand zetu, inaanzia kwa wale wanaotuzunguka.

4. Inapokuja kuhusu brand yako, unachofikiri wewe hakina uzito kama kile wanachofikiri wengine kuhusu wewe. Habari mbaya au nzuri kuhusu wewe ndizo ambazo zinawapa watu taswira kuhusu wewe. Hivyo unahitaji kuwa makini kwenye kila unachofanya, ili kisije kuwa kinapingana na unavyotaka watu wakuchukulie.

5. Kutengeneza brand yako, haitoshi tu kwa wewe kuwa tofauti na wengine, bali unahitaji kuleta tofauti kwenye maisha ya wengine. Wewe unaweza kuamua kuwa tofauti, ila kama hakuna tofauti unayoweza kusababisha kwenye maisha ya wengine, hakuna anayeweza kukukumbuka. Mara zote fikiria ni tofauti gani unaweza kuleta kwenye maisha ya wengine.

6. Kwenye zama hizi tunazoishi za mitandao ya kijamii, ni muhimu sana uwe makini na brand yako. Tangu zama za kale kumekuwepo na umbeya duniani, lakini kwa zama za sasa, mitandao ya kijamii inamwaga petroli kwenye moto wa umbeya. Hii ina maana kwamba umbeya unasambaa kwa kasi sana zama hizi kuliko zamani. Hivyo unahitaji kuwa makini sana na kile unachofanya.

7. Brand yako inaweza kuathiriwa na wale watu unaohusishwa nao, watu wanakuhukumu kutokana na tabia za marafiki zako au wale unaokaa nao muda mrefu. Hivyo kama unaonekana na matapeli, moja kwa moja watu wanachukulia na wewe ni tapeli. Ni muhimu ujue ni brand gani unataka kujenga kisha jihusishe na wale watakaopelekea watu kuona brand yako sawasawa.

8. Kuna funguo kuu tatu za kuifanya brand yako kuwa kubwa na imara.
Moja ni UTOFAUTI, ni kitu gani cha tofauti unachofanya au unachosimamia. Huwezi kuwa brand kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Mbili ni UHUSIANO, kile unachofanya, kinahusiana vipi na wale watu unaowalenga. Brand yako inatokana na namna wengine wanavyojisikia kwa kuwa na wewe au kufanya kazi na wewe.
Tatu ni MSIMAMO, ni kwa namba gani maneno na matendo yako yanaendana wakati wote. Kama unabadilika kila mara, huwezi kujenga brand ambayo watu wanaiamini.

SOMA; Huyu Ndiye Mwalimu Wa Kwanza Na Muhimu Sana Kwenye Malezi Ya Mtoto.

9. Brand yako inaanza kuwa imara pale unapochagua kitu unachoamini na kukisimamia. Ni lazima uchague kitu ambacho unakiamini kutoka ndani ya moyo wako, na upo tayari kukisimamia hata kama dunia nzima inakupinga. Unapochagua kitu unachoamini, ndiyo unajitenga na kundi na kutengeneza kitu cha tofauti ambacho watu wataweza kukihusisha na wewe. Namna unavyoweza kutetea na kufanyia kazi kile unachoamini, ndivyo watu wengi wanavyovutiwa na wewe, na wao wanakuamini na kuwa pamoja na wewe.

10. Watu watavutiwa kuwa na wewe kutokana na kile unachosimamia kwa kuamini na maadili uliyojiwekea. Brand ni mahusiano yako na wengine, kadiri watu wanavyokuamini, ndivyo brand yako inavyozidi kukua. Hivyo linda sana imani yako kwa wengine, usifanye kile kitakachowafanya watu waanze kuhoji uaminufu wako.

11. Ili kujenga mahusiano mazuri kati ya unachofanya na wale ambao unataka wakipate, usijifikirie wewe kwanza, bali anza kuwafikiria hao wengine. Kuna usemi wa Zig Zigler kwamba unaweza kupata chochote unachotaka kupata, kama utawawezesha wengine kupata kile wanachotaka. Hivyo kama unataka kuwa tajiri, wawezeshe wengine kuwa matajiri kupitia kile ambacho wanakitaka wao, na wewe unaweza kuwapatia.

12. Katika kujenga imani yako na wale wanaokuzunguka, hakikisha kila unachofanya, kinaendana na ile picha unayotaka kujenga. Kama unataka kujenga picha kwa wengine kwamba wewe ni makini, basi mara zote kuwa makini, kwenye mambo makubwa na madogo. Kama unataka kujenga picha kwamba wewe ni mwaminifu, basi kuwa mwaminifu kwenye mambo yako yote. Maneno yako yanapoanza kupishana na matendo yako, unapoteza kabisa imani ya watu kwako, na unaharibu brand yako.

13. Watu wanaikubali brand na kushirikiana nayo kupitia maeneo haya matatu muhimu, yajue na yatumie kujenga brand yako.
Moja; UMAHIRI, je ni kipi ambacho watu wanakipata kutoka kwenye brand husika. Hapa unachagua maeneo ambayo unayafanyia kazi. Hapa unajikabidhi majukumu ambayo watu wakija kwako wewe utayatatua.
Mbili; VIWANGO, je unafanya kile ulichochagua kwa viwango gani? Hapa unapima ubora wa jinsi unavyofanya mambo yako, na viwango ndiyo vinakutofautisha wewe na wengine?
Tatu; MTINDO, je unafanya kile unachofanya kwa namna gani ya tofauti? Hapa ni namna unavyowasiliana na kushirikiana na wengine.

14. Kabla hujaanza kutengeneza brand yako, ni lazima uhakikishe kwamba unaweza kumwonesha mtu unayetaka kujenga naye mahusiano kwamba unaweza kumtatulia matatizo yake au kutimiza shida zake. Huu ndiyo msingi mkuu, kwa sababu kama huwezi kutatua tatizo au kutimiza kile unachofanyia kazi, hata ungekuwa tofauti na ukawa na mbinu nyingi kiasi gani, hazitasaidia. Kwa kifupi chagua eneo ambalo unataka kujulikana kupitia hilo, inaweza kuwa michezo, uandishi, kazi au biashara.

15. Jijengee miiko na maadili ili uweze kufanya kile unachotakiwa kufanya bila ya kuharibu brand yako, hata kama unapitia hali gani. Ni rahisi sana kujisahau hasa pale mtu anapoanza kupata sifa kwa kufanya kitu kizuri, wengi huanza kuharibu na baadaye sifa zao kuharibika. Ili lisikukute hili, jiwekee maadili na miiko. Maadili ni namna unavyofanya mambo yako. Miiko ni yale mambo ambayo ni lazima uyafanye au kamwe hutoyafanya hata kitokee nini. Ili kujenga brand unahitaji kuwafanya watu wajue wakija kwako lazima wapate kitu fulani, na pia wajue kwa namna yoyote ile wewe huwezi kufanya vitu fulani, ambavyo haviendani na wewe.

SOMA; Siri Kubwa Ya Kukutoa Kwenye Umaskini.

16. Msingi mkuu wa brand yako ni kujua uhalisia wako. Watu wengi wamekuwa wakikazana kuwa kama wengine na kujikuta wanaharibu zaidi. Unahitaji kujua uhalisia wako, jua ni maeneo gani uko vizuri na maeneo gani ambayo una madhaifu. Usihangaike na madhaifu, badala yake tumia yale ambayo uko imara. Uhalisia ndiyo mgongo wa brand. Unapoiga wengine unafika wakati unachoka, lakini unapofanya kile kinachoendana na uhalisia wako, huwezi kuchoka, maana hayo ndiyo maisha yako.

17. Linapokuja swala la mafanikio, unahitaji kutumia maadili na miiko yako kufanikiwa. Watu wengi wamekuwa wakipindisha maadili na miiko yao ili tu kufanikiwa, na jamii zimekuwa zikiaminishwa hivyo. Kuna watu wamekuwa wakisema kabisa kwamba huwezi kuwa tajiri kama siyo mwizi au fisadi. Lakini ukweli ni kwamba brand inayodumu ni ile inayosimamia maadili na miiko yake. Hivyo unaweza kuchagua kupindisha maadili na miiko yako ili ufanikiwe haraka lakini mafanikio hayo yasidumu, au usimamie maadili na miiko yako, uchelewe kufanikiwa lakini ufanikiwe milele.

18. Ili kujua uhalisia wako ambao utakuwezesha kujenga brand yako hatua hizi tatu muhimu unapaswa kuzipiga;
Moja; jua kusudi la wewe kuwa hapa duniani(PURPOSE). Upo hapa duniani kufanya nini? Ulikuja duniani kutoa mchango gani? Kila mtu anapaswa kujua hili, na unalijua wewe mwenyewe, hakuna wa kukufundisha.
Mbili; tengeneza maono yako(VISION). Je ni ndoto zipi ambazo unazo kwenye maisha yako? ni kitu gani cha tofauti unataka kufanya hapa duniani? Maono yako ndiyo yatawavutia watu kuandamana na wewe.
Tatu; Maadili yako (VALUES), ni kipi ambacho unasimamia kama ukweli? Ni mambo gani muhimu zaidi kwako? Ni vitu gani upo radhi kufanya au kutokufanya katika safari yako ya mafanikio? Maadili yako ndiyo yanawafanya watu wakuamini.

19. Bila ya kujali unapitia nini, bila ya kujali uko wapi, simamia kile unachoamini. Kuna wakati ambapo brand yako itajaribiwa, kila mtu anapitia majaribu fulani kwenye maisha yako. unafika wakati ambapo mambo yanakuwa magumu kiasi kwamba uko tayari kusaliti kile ulichokuwa unasimamia mwanzo, ukisaliti unaharibu kabisa brand yako, lakini unapoendelea kusimamia kile unachoamini hata kama unapitia magumu, unajenga brand imara. Nafikiri umekuwa unaona jinsi wanasiasa wanavyopoteza kuaminiwa na kuitwa wasaliti pale wanapotoka chama kimoja na kwenda kingine. Simamia kile unachoamini, wakati wote.

20. Kujenga BRAND (JINA/CHAPA) YAKO ni kazi kama zilivyo kazi nyingine. Ni kazi ambayo unahitaji kuifanya kila siku na kila wakati. Kwenye kila kitu unachosema au kufanya, dunia inakuangalia. Na dunia hii ya mitandao ya kijamii, pamoja na simu zenye uwezo wa kurekodi picha na sauti, linda sana BRAND yako, maana hapo ndipo mafanikio yako yalipo. Kila siku na kila nafasi unayoipata kukutana na mteja au mtu yeyote, ni nafasi nzuri kuitangaza na kuikuza brand yako. hakikisha mtu yeyote anayekutana na wewe, haondoki kama alivyokuja, tafuta namna ya kuongeza thamani kwenye maisha yake, hata kama ni kumfanya atabasamu.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako. tumia haya uliyojifunza kujenga brand yako, na kuweza kuishi maisha ya mafanikio. Katika ulimwengu huu wa sasa, ambapo mtandao una nguvu kubwa, moja ya njia za kutumia kujenga brand yako ni mtandao wa intanet na mitandao ya kijamii. Unahitaji kuitumia vizuri kutangaza jina lako. Kama hujaanza kutumia mitandao hii, na ungependa kuweza kuitumia vizuri kukuza jina lako, biashara yako na hata kutengeneza kipato, wasiliana nami kwa namba 0717396253. Karibu sana.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

SEMINA; Tengeneza Fedha Kwa Kutumia Blog.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu,
Mwaka 2014 niliendesha semina kwa njia ya mtandao iliyokuwa na jina JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kwenye semina ile niliwashirikisha mambo yote muhimu kuhusu blog, jinsi ya kuitengeneza na hata kuikuza. Wengi walihudhuria semina ile na kujifunza, baadaye nilitoa kitabu kwa mfumo wa kielektroniki (pdf) kilichokuwa kinaelezea kwa undani zaidi jinsi mtu anavyoweza kutengeneza kipato kwa kutumia blog.

Waliohudhuria semina na kusoma kitabu kile wameweza kufungua blog zao, wapo ambao wameweza kukuza blog hizo mpaka kufikia hatua ya kuuza vitu kupitia blog zao, wengine wamepata fursa za kuandika makala kwenye magazeti kutokana na blog zao. Lakini pia wapo ambao wameanzisha blog na kuishia njiani, wameshindwa kuzikuza na hatimaye kuona kama kutengeneza fedha kwenye mtandao ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kabla hatujaendelea nataka nikuhakikishie kitu hiki kimoja, kutengeneza fedha kwenye mtandao ni kitu ambacho kinawezekana, na mtu yeyote ambaye amejitoa na yupo tayari kuweka juhudi, ni lazima atengeneze kipato kwenye mtandao kwa kutumia blog yake.

Rafiki, nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye semina nyingine ya KUTENGENEZA KIPATO KWA KUTUMIA BLOG. Katika semina hii tunakwenda kujifunza mambo yote muhimu ya kuanzisha na kukuza blog, pamoja na kuangalia changamoto ambazo zimekuwa zinawarudisha watu wengi nyuma. Tutakwenda kuangalia kwa undani mambo yote muhimu mtu anapaswa kuzingatia ili kuweza kujenga biashara yake kupitia blog.
Jambo moja muhimu sana kuhusu semina hii ni itakujia bure kabisa, hutahitaji kuchangia hata senti moja, badala yake utajifunza na kama utatumia yale utakayojifunza, utaweza kujitengenezea uhuru wa kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Semina hii itakuwa ya siku saba, na itaanza tarehe 19/09/2016 na kuisha tarehe 25/09/2016. Hizi ni siku saba za uhuru wa maisha yako, hakikisha hukosi mafunzo haya.

Utajifunza nini kwenye siku hizi saba?

Siku ya kwanza; karibu kwenye ulimwengu wa taarifa, maana ya blog na kwa nini ni muhimu KILA MTU awe na blo yake.

Siku ya pili; jinsi ya kuchagua mada itakayokufaa wewe na kuchagua hadhira yako ambayo baadaye itaweza kukunufaisha.

Siku ya tatu; vitu muhimu unavyohitaji ili kuweza kuendesha blog yako vizuri na kuikuza.

Siku ya nne; umuhimu wa EMAIL LIST katika kutengeneza kipato, matumizi ya mitandao ya kijamii na mitandao mitatu muhimu ya kuitawala.

Siku ya tano; jinsi ya kuchagua bidhaa au huduma unazoweza kuuza kwa kutumia blog yako.

Siku ya sita; kuandaa bidhaa/huduma ya kuuza pamoja na mchakato wote wa kuuza kwa kutumia blog.

Siku ya saba; hatua za kuchukua kukuza blog yako na kutatua changamoto zinazowafanya wengi kushindwa.

Hizi ni siku saba za kupata mambo yote muhimu unayopaswa kujua kuhusu kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog.

Uzuri ni kwamba unakwenda kujifunza kutoka kwangu ambaye nimeweza kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog, hivyo nakwenda kukupa siri zote ninazozijua mimi, na kazi inabaki kuwa kwako kama kweli unataka kukuza kipato chako.

Semina hii inawafaa hasa watu gani?
1. Wamiliki wote wa blog kwa sasa, iwe unatengeneza kipato au la.
2. Waajiriwa wote ambao wamekuwa wanafikiria kuwa na kitu cha pembeni kinachowaingizia kipato, yaani waajiriwa ni muhimu mno kujifunza kupitia semina hii.
3. Wahitimu wa elimu ya juu ambao bado wanatafuta kazi, hakuna sehemu nzuri ya kuanzia kama kwenye blog.
4. Wanafunzi wa elimu ya juu, hawa watapata maandalizi bora kabisa huku wakiwa bado wapo masomoni.
5. Mmiliki yeyote wa biashara za kawaida, yaani zisizo za mtandaoni. Kama unamiliki biashara halafu huna blog au tovuti, umeamua kujipoteza mwenyewe, njoo ujifunze.
6. Mtu yeyote ambaye anatumia mitandao ya kijamii na anapenda kuwashirikisha watu wengine vitu vizuri.

Kama umeweza kusoma hapa, maana yake tayari una vitu vinavyohitajika ili kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog, karibu sana ushiriki semina hii.

Uendeshwaji wa semina.
Semina hii itaendeshwa kwa njia mbili;

Njia ya kwanza ni kupitia email, kwa siku saba za semina, kila siku utatumiwa somo la semina kwenye email yako. Kwa nini napenda sana kutumia email? Kwa sababu unaweza kutunza masomo haya na kuwa unayarudia maisha yako yote, tofauti na njia nyingine kama wasap ambapo ni rahisi kupoteza masomo hayo.

Njia ya pili ni kupitia mtandao wa TELEGRAM ambao unafanana na wasap, huko pia masomo yatawekwa, lakini utakuwa mahususi zaidi kwa maswali na majibu. Kila jioni ya siku husika kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu kuhusu somo husika, hivyo kila mshiriki atapata nafasi ya kuuliza swali na nitajibu moja kwa moja huku kila mtu akijifunza, hata kama hajauliza swali. Kwa nini TELEGRAM na siyo wasap? Kwa sababu telegram inaweza kuchukua watu wengi sana ukilinganisha na wasap, pia ina uhuru mkubwa wa mtu kujiunga mwenyewe, ninachofanya ni kukupa link na ukibonyeza tayari umeingia, haina haja unipe namba nikuunganishe.

Najiungaje na semina hii?
Kama upo tayari kunufaika na mtandao wa intaneti, na upo tayari kutengeneza fedha kwa kutumia blog, karibu sana kwenye semina hii. Kujiunga na semina hii fuata hatua hizi mbili;

Hatua ya kwanza jaza fomu ya kujiunga, kwa kuweka taarifa zako, jaza fomu hapo chini au bonyeza maandishi haya kujaza fomu.
 
Hatua ya pili jiunge na kundi la TELEGRAM, kwanza hakikisha una telegram kwenye simu yako, kama huna nenda kwenye PLAY STORE na search TELEGRAM MESSENGER, ukishaipata iweke kwenye simu yako na unganisha namba yako kama unavyounganisha kwenye wasap. Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno SEMINA kwa njia ya telegram kwenye namba 0717396253 au bonyeza maandishi haya na moja kwa moja utaingia kwenye kundi la semina.

Chukua hatua sasa.
Mwisho wa kujiungana semina hii ni tarehe 16/09/2016, lakini nakusihi sana ujiunge leo kwa sababu nafasi zinaweza kujaa, mfumo wetu wa email una kikomo cha kupokea watu, hivyo kuhakikisha hukosi semina hii jiunge leo hii.

Karibu sana tujifunze kwa pamoja jinsi ya kutengeneza fedha kwakutumia blog, kama mimi nimeweza, hata wewe unaweza.
Karibu sana.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Changamoto Kuu Mbili (02) Za Ajira Na Jinsi Unavyoweza Kununua Uhuru Wako Kwenye Ajira.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu tena kwenye mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ambapo tunashirikishana maarifa muhimu ya kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi kila siku. Kila siku ni siku nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi ili kuhakikisha maisha yetu yanakuwa bora. Swali la msingi sana ambalo tunapaswa kujiuliza ni je, juhudi hizi tunaziweka wapi? Kwa sababu kama unaweka juhudi kwenye yale yale ambayo umekuwa unayafanya, utazidi kupata matokeo yale yale. Yaani kama ulikuwa unachimba shimo, unapozidi kuweka juhudi ndiyo unazidi kuingia kwenye shimo refu.

Leo napenda kuongea na waajiriwa wote, na waajiriwa watarajiwa, juu ya changamoto za ajira na jinsi mtu anavyoweza kununua uhuru wake kutoka kwenye ajira. Waajiriwa namaanisha wale wote ambao wanauza muda wao na utaalamu wao kwa watu wengine, yaani unampa mtu muda wako na utaalamu wako na yeye ndiye anayeamua akulipe kiasi gani. Waajiriwa watarajiwa namaanisha wahitimu wa ngazi mbalimbali ambao kwa sasa wanatafuta kazi. Na huu ndiyo msimu wa kuhitimu hivyo maombi ya kazi na ushauri kuhusu kazi yamekuwa mengi.

Tuanze kwa kuusema ukweli kama ulivyo, japo ukweli huwa unaumiza, lakini hata kuukwepa bado hakuubadilishi kuwa ukweli.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA

Kosa kubwa kabisa ambalo mtu anaweza kufanya kwenye maisha yake dunia nzima, ni kuchagua kuwa mwajiriwa pekee kwa miaka yake yote. Na kosa kubwa kabisa mtu anaweza kulifanya hapa Tanzania ni kuchagua kuwa mwajiriwa wa umma pekee maisha yake yote. Ninaposema pekee namaanisha mtu anategemea ajira tu kuendesha maisha yake, hana chanzo kingine cha kipato zaidi ya ajira aliyonayo.

SOMA; Je Ungependakutengeneza kipato kwenye mtandao kwa kuanzia hapo ulipo sasa? Bonyeza hapa kujua zaidi.

Kwa nini ni kosa kubwa sana kutegemea ajira pekee kwa ajili ya kipato?

Kwa sababu kunakutengenezea utegemezi wa kipato. Kipato kimoja hakiwezi kutosheleza mahitaji yote ya maisha, na hivyo mtu kuwa tegemezi, badala ya kuwa na uhuru wa kifedha. Kwa kutegemea chanzo kimoja pekee, mtu anaishi kwa hofu kwa sababu iwapo chanzo hiko kimoja kitapotea, basi maisha yake yapo kwenye hatari kubwa.

Na jambo jingine muhimu sana ni kwamba, chanzo kimoja cha kipato, hakiwezi kukufanya kuwa tajiri, na ni nani ambaye hapendi kuwa tajiri? Kuna watu watajisikia vibaya kwa sababu nimetaja neno tajiri hapo, kama vile ni mwiko. Sawa tuachane na hilo la utajiri, muhimu ni kwamba unahitaji kuwa na uhuru wa kifedha, unahitaji kuamka asubuhi ukiwa na hamasa ya kwenda kuweka juhudi kubwa na kutoa huduma bora, na siyo kuamka ukiwaza leo nikamkope nani, au leo nitoe kisingizio gani kwa wanaonidai. Hiki ni kitu ambacho huwezi kukipata kwenye ajira.

Kwa ni kosa kubwa kwenye maisha ya Mtanzania ambaye amechagua kuwa mtumishi wa umma kwa maisha yake yote?

Kwa sababu ambazo zipo wazi, kwanza kabisa, siku za nyuma ilikuwa ni uhakika wa ajira, watu walikimbilia kupata ajira serikalini ambapo walikuwa na uhakika wa kuwa na ajira hizo mpaka pale watakapostaafu. Hata kama kipato ni kidogo, lakini wengi walikimbilia ajira hizi kwa sababu walikuwa wanaona wanakuwa na muda wa kufanya mambo yao. Lakini ulikuwa ukiwachunguza hawa watu wanaokuambia wana muda wa kufanya mambo yao, hakuna makubwa waliyokuwa wanayafanya.

Pili siku za hivi karibuni, ajira za umma umekuwa mwiba mkali, imekuwa ni sehemu ya kufanya kazi kwa nidhamu ya woga, utaalamu umekuwa hautumiki tena badala yake watu wamekuwa wakiangalia lipi ambalo litawafurahisha viongozi na kulifanya hilo. Hii imewafanya waajiriwa wengi kufanya kazi wakiwa na hofu kubwa. Unajaribu kumhoji tu mtu kwa nini anakuhudumia vile anavyokuhudumia anakujibu nalinda kibarua changu, na hapo anakuwa anafanya kitu ambacho hukutegemea afanye hivyo. Hapo hatujaangalia wale ambao ‘wanatumbuliwa’ bila ya kupewa nafasi ya kusikilizwa au kuonywa.
Sasa tumeyajadili haya siyo kukupa wewe nafasi ya kujifariji, au kulalamikia haya yanayoendelea, ila tuangalie namna unavyoweza kuchukua hatua. Unanijua mimi vizuri, sitaki upoteze muda wako kulalamika na kulaumu kama wengi wanavyofanya, ninachotaka ufanye ni kuchukua hatua, kwa sababu maisha yako ni jukumu lako wewe mwenyewe, kama kuna kitu hukipendi ni wajibu wako kukibadili, na kama huwezi kukibadili basi achana nacho.

Ni hatua gani unaweza kuchukua kuondokana na changamoto hizi za utegemezi wa ajira?
Watu wengi wamekuwa wanahubiri kwamba acha kazi nenda kawe mjasiriamali. Kama vile ujasiriamali ni kitu cha kwenda kuanza na kufanikiwa hapo hapo, UJASIRIAMALI NI MTINDO WA MAISHA, nitakuja kuandika kwa kina juu ya hilo. Lakini nataka nikuambie kwamba hutumii ujasiriamali kama mbinu ya kutoka kimaisha, bali unachukua ujasiriamali kama mtindo wa maisha umechagua kuishi. Hivyo unaweza kuanza kuuishi popote ulipo, iwe umeajiriwa au huna ajira.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.

Nina mapendekezo mawili;

Pendekezo la kwanza, kama wewe ni kijana, ambaye umehitimu masomo yako na unatafuta ajira kwa zaidi ya miaka miwili ila hujapata, achana kabisa na hilo swala la kutafuta ajira. Kama miaka miwili umekuwa unazunguka na bahasha hujapata ajira, ni wakati sasa wa kuangalia upande wa pili. Weka bahasha na vyeti kabatini na anza mapambano yako mwenyewe, jipe miaka mingine miwili ya kwako tu, kufanya kila unachoweza kufanya mpaka kuhakikisha umesimama. Nina uhakika, kwa miaka miwili, kama umechagua kufanya kitu, utafika mbali sana, kuliko kuendelea kusubiri ajira ambazo zinazidi kuwa changamoto kila siku.

Pendekezo la pili, kama wewe ni mwajiriwa, ambaye umekuwa kwenye ajira kwa muda mrefu na maisha yako yote yanategemea ajira, sikuambii uache kazi na kwenda kupambana, ila nakuambia anza mapambano ukiwa hapo hapo kwenye ajira. Ila ninataka nikuambie ukweli zaidi, ambao hutaki kuusikia, chagua kuteseka zaidi ya unavyoteseka sasa, hakuna uhuru unaoletwa kirahisi, uhuru unapiganiwa. Hii ina maana kwa mfano, uanzishe biashara wakati bado upo kwenye ajira yako ya sasa, kwa hiyo uende kazini, ukitoka, badala ya kwenda kupumzika, uingie kwenye biashara yako. Na mwisho wa wiki, ambapo huendi kazini, badala ya kupumzika, uende kwenye biashara yako.
Hii inaweza kupelekea kufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku, kupunguza muda wa kupumzika na wa kulala, na kuachana na marafiki ambao umezoeana nao, hiyo ndiyo gharama ya uhuru wa kifedha, lazima uwe tayari kuilipa kama kweli unataka kupata uhuru.

SOMA; KITABU CHA MAY; Biashara Ndani Ya Ajira; Jinsi Ya Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa.

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema, tengeneza vyanzo tofauti vya kipato, usitegemee kipato kimoja pekee, iwe ni kwenye kazi au biashara. Kadiri unavyokuwa na vyanzo vingi, ndivyo unavyokuwa huru kifedha, kwa sababu chanzo kimoja kikiwa na changamoto, vyanzo vingine vinaendelea kutiririsha kipato.

Nakutakia kila la kheri katika kununua uhuru wa maisha yako kupitia uhuru wa kipato.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

USHAURI; Hatua Tano Za Kuchukua Kwa Mwalimu Anayetafuta Ajira Lakini Hajapata.

$
0
0
Habari rafiki?
Karibu kwenye kipengele chetu cha leo cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Je wewe ni mwalimu? Je umekuwa unatafuta kazi bila ya mafanikio yoyote? Leo nataka nikushirikishe mambo matano unayoweza kuanza kuyafanya mara moja na ukaondoka kwenye hali ya kutokuwa na ajira uliyopo sasa.


Nimekushirikisha ushauri huu ambao niliutoa kwenye kundi letu la telegram la AMKA MTANZANIA, ambapo mwenzetu aliomba ushauri wa ajira. Nimeona ushauri huu unaweza kuwasaidia wengi zaidi hivyo usome na fanyia kazi yale unayojifunza. Kama utapenda kujiunga kwenye kundi hili hakikisha una TELEGRAM kwenye simu yako (inapatikana playstore kama wasap) kisha bonyeza maandishi haya na moja kwa moja utaingia kwenye kundi la AMKAMTANZANIA TELEGRAM.
Karibu tujifunze kupitia ushauri wa leo;

Natafuta kazi, Habari wapendwa,
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 30, naishi Dar es salaam, Nina elimu ya postgraduates diploma in education, nafundisha history na kiswahili, nina uzoefu wa kufundisha kwa mwaka 1, degree yangu ya kwanza nilisomea mambo ya human resources, nina uzoefu wa kazi ya human resources kwa miezi 6. Nilifanikiwa kuanzisha biashara lakini haikuenda vizuri kutokana na kutokuwa na usimamizi wa kutosha, hivyo naomba yoyote anisaidie kupata kazi yoyote au inayoendana na nilivyosomea ili niweze kusimama tena, na kutafuta mtaji.

NDUGU,

Kwanza nikupe pole sana kwa changamoto unayopitia. Naelewa jinsi ambavyo huenda umetafuta kazi kwa muda bila ya matumaini. Pia muda uliowekeza kwenye elimu ni mwingi na hivyo unahitaji kutumia elimu hiyo vizuri.

Sasa mimi sitaki nikuchoshe na mengi hapa, nataka uniambie kama kweli una njaa na hasira ya kutoka hapo ulipo sasa, kwa kufanya lolote ambalo utahitajika kufanya.
Na kama ni ndiyo basi hapa nakushauri mambo matano (5) ya kuanza kufanya kesho....

1. Andika barua ya kuomba nafasi ya kufundisha kwa kujitolea bila ya kulipwa chochote, na chagua shule kumi zilizopo kwenye eneo linalokuzunguka, shule za sekondari au za primary kwa english medium. Katika shule kumi, hutakosa hata mbili ambazo watakuita kuongea na wewe, waombe wakupe nafasi ya kujitolea kufundisha, wakikupa nafasi hiyo, fanya kazi iliyo bora mno, wafundishe watoto vizuri mno, kiasi kwamba thamani yako iongezeke, fursa zaidi zitakuja.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Wahitimu Wa Elimu Ya Juu Mwaka 2016, Ukweli Ambao Umekuwa Unafichwa Kwa Miaka 20 Iliyopita.

2. Kwenye eneo unalokaa, ongea na wazazi wote ambao watoto wao wanasoma sekondari au hata primary, kisha waombe uwafundishe kwa muda wa ziada, jioni au mwisho wa wiki. Tafuta eneo unaloweza kufanyia zoezi hilo, waombe uanze kufundisha hata bure kwanza, halafu wakiona mabadiliko kwa watoto wao, ndiyo uanze kuwachaji kidogo.

3. Kwenye eneo unalokaa, kama kuja watu wenye uwezo kiasi ambao wana watoto wanaosoma, unaweza kuongea nao na ukawa unawafundisha watoto wao majumbani kwao. Popote unapopata nafasi fanya kazi bora sana.

4. Anzisha blog, ambayo inawafundisha wageni kiswahili fasaha, wewe ni mwalimu wa kiswahili, hivyo tengeneza mfumo ambao unaweza kumsaidia mtu asiyejua kiswahili akajifunza vizuri, mwanzo hutakuwa na wasomaji wengi, ila wewe target wale ambao ni wageni, na wapo wengi mno, kuna wachina wana njaa ya kukijua kiswahili.
Nyongeza, hapo kwenye blog toa huduma ya translation, labda kingereza kuja kiswahili, au kama unaweza kiswahili kwenda kiingereza. Kuna wengi wanahitaji huduma hiyo.

SOMA; Shiriki Semina Ya Bure Ya Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Kwa Kutumia Blog.

5. Kaa chini na wazo lolote la biashara ambalo unalo kwa sasa, ambalo upo tayari kutoa kila tone la jasho lako kufanyia kazi, yaani iwe passion yako kweli. Liandike wazo hilo vizuri, angalia ni sehemu ipi ya chini kabisa unayoweza kuanzia, kiasi kidogo kabisa unachoweza kuanza nacho. Kisha waangalie watu wote wanaokuzunguka, ambao una mahusiano nao ya kindugu au kirafiki. Wachague wale ambao unajua watakuelewa, kisha zungumza nao kwa namna wanavyoweza kukusaidia kwa wazo hilo ulilonalo.

Anza na hayo, unaweza kuchagua mawili au matatu au yote na uone lipi litawezekana kwako, ila blog anza nayo hata kesho, miaka mingi ijayo utajishukuru sana.
Kama kwa namna yoyote ile wakati unasoma huo mtiririko napo ulikuwa unajiambia mimi siwezi hili au siwezi hili, niseme tu hutaweza kutoka hapo ulipo.
Nimalize kwa kukuambia kwamba kama umechagua kitu cha kufanya hapo, na ukishajipanga kufanya, nitafute, nitakucoach bure kabisa, ukishakuwa na mpango tayari.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Dunia Inabadilika, Biashara Zinabadilika, Kazi Zinabadilika Na Wewe Badilika Hivi.

$
0
0
Habari za leo rafiki?
Nina habari njema sana kwako ambazo nahitaji kukuambia kabla hatujajadili mada ya leo. habari hizo ni kwamba semina yetu ya PATA MILIONI YA ZIADA, hata kama huna mtaji, iliyokuwa ifanyike tarehe 22/10/2016 tumeisogeza mbele na sasa itafanyika jumapili ya tarehe 30/10/2016. Hii ni nafasi nzuri kwako kufanya maandalizi ya kushiriki semina hii nzuri ya kukuwezesha kuongeza kipato chako. Kupata nafasi ya kushiriki semina hii bonyeza maandishi haya.


Semina yetu ya bure ya TENGENEZA KIPATO KWA KUTUMIA BLOG inayokwenda kuanza tarehe 19/09/2016 iko pale pale hivyo kama bado hujajiandikisha wahi mapema, zimebaki siku tatu tu za kujiandikisha. Fomu ya kujiandikisha ipo ndani ya makala hii.

Mabadiliko ya dunia.
Karibu rafiki yangu kwenye makala yetu ya leo ambapo tutakwenda kujadili kwa kina kuhusu mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani. Ni ukweli ulio wazi kwamba dunia inabadilika, na inabadilika kwa kasi kubwa mno.

Tukiangalia miaka kumi iliyopita, vitu vyote ambavyo tunatumia kwa sasa, havikuwepo au kama vilikuwepo basi havikuwa maarufu kama sasa. Miaka kumi iliyopita, mitandao ya kijamii tunayotumia na kufurahia sasa haikuwepo au kama ilikuwepo basi ilikuwa michanga sana.

Miaka kumi iliyopita gharama za kupata simu zilikuwa juu kuliko ilivyo sasa, na hakukuwa na kitu kinaitwa ‘smartphone’.
Miaka kumi iliyopita, ungeweza kuwahesabu watu wanaomiliki kompyuta au simu, lakini leo hii watu wengi zaidi wanamiliki vifaa hivi. Hakika dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana.

SOMA; Mabadiliko; Yalikuwepo, Yapo Na Yataendelea Kuwepo.

Mabadiliko ya biashara.
Biashara nazo zinabadilika kwa kasi kubwa, tukiangalia miaka kumi iliyopita na sasa kibiashara, kuna mabadiliko makubwa mno. Miaka kumi iliyopita, ungetaka kuanzisha biashara ilikubidi uwe na mtaji mkubwa, ukodi eneo la biashara na uwepo kwenye biashara yako muda wote. Ilikuwa ukitaka kutangaza biashara yako ni lazima ujiandae kwa fedha nyingi ili uweze kupata nafasi kwenye tv, redio au gazeti. Na hata kupata mtaji wa kukuza biashara ilikuwa changamoto kubwa, taasisi zilizokuwa zinatoa huduma hiyo zilikuwa chache.

Lakini tunapoangalia leo, miaka kumi baadaye, kuingia kwenye biashara imekuwa rahisi mno. Kumekuwa na biashara mpya ambazo huhitaji hata kufungua eneo la biashara, unaweza kuendesha biashara kubwa ukiwa nyumbani kwako, ofisi ikawa hata kitanda chako, au sehemu nyingine unayoweza kuchagua ya kufanyia kazi yako.
Kwa sasa unaweza kutangaza biashara yako kwa maelfu ya watu bure kabisa, bila kulipa gharama yoyote. Pia unaweza kutengeneza mahusiano bora na wateja wako kupitia biashara yako.

Kitu muhimu zaidi, kwa sasa ukitaka kupata mtaji wa kibiashara, ni rahisi kuliko miaka kumi iliyopita. Sasa hivi kama unazo sifa za kupata mkopo, utafuatwa na taasisi za mikopo wakikuomba wakukopeshe, watakuambia unakopesheka na kukupa sababu nyingi kwa nini uchukue mkopo wao. Mambo yamebadilika mno katika miaka hii kumi.

Mabadiliko ya kazi.
Sehemu ambayo imepata mabadiliko makubwa mno ni kazi au ajira. Miaka kumi iliyopita na kurudi nyuma, wimbo maarufu ulikuwa ni huu; nenda shule, soma kwa bidii, faulu vizuri mitihani yako, nenda chuo kikuu(au vyuo vingine), somea utaalamu fulani, ukihitimu utapata ajira nzuri na kuwa na maisha mazuri. Ilikuwa ni njia ya uhakika ambayo watu waliifuata na kuwa na maisha yanayotabirika, kwamba kama utasoma na kufaulu, una uhakika wa kuwa na kazi. Lakini tunapoangalia leo, njia hii haipo tena, wengi wamesoma na kufaulu vizuri lakini kazi hakuna.

Hata wale ambao wapo kwenye ajira tayari, mabadiliko ni makubwa mno, miaka kumi iliyopita mtu alikazana sana apate kazi serikalini kwani ilikuwa ni uhakika wa kazi mpaka unastaafu. Lakini sasa hivi hakuna mwenye uhakika wa kazi, hata serikalini, tumeshuhudia watu wengi wakipoteza kazi zao.

Njia za kuajiri nazo zimebadilika sana, zamani vilitumika vyeti kuajiri, aliyesoma na kufaulu vizuri alikuwa na uhakika wa kuajiriwa kutokana na vyeti vyake. Lakini sasa hivi kila mtu ana vyeti hivyo, sasa waajiri wanatafuta sifa za ziada ndiyo waweze kumwajiri mtu.

Ni kitu gani kimebadili yote haya?
Swali muhimu kujiuliza ni je mabadiliko haya makubwa yanayoendelea duniani, chanzo chake ni nini? Ni nguvu gani ipo nyuma ya mabadiliko haya makubwa?
Jibu ni moja, ukuaji wa teknolojia na uwepo wa mtandao wa intaneti. Mtandao wa intaneti pekee umeleta mabadiliko makubwa mno kwenye maisha, kazi na hata biashara.

Mabadiliko haya yataendelea kuwepo kwa sababu teknolojia bado inakuwa, na mtandao wa intaneti ndiyo kwanza unaongezeka kasi na gharama zake zinapungua. Kila siku watu wengi zaidi wanaweza kutumia mtandao huu wa intaneti.

Mabadiliko yako wewe.
Baada ya kuona mabadiliko yote haya, swali ni je wewe unabadilikaje? Je unabadilika au umeendelea kung’ang’ania yale ambayo yameshapitwa na wakati? Je unasubiri mpaka uwe na mtaji mkubwa ndiyo uanze biashara? Au unasubiri mpaka watu wakuone umesoma ndiyo wakuajiri?

Vipi kuhusu kipato chako, je kinakutosha? Kama hakikutoshi ni hatua zipi umechukua ili kukiongeza?
Kuna maswali mengi mno ninayoweza kukuuliza rafiki, lakini kitu cha muhimu nataka kukuambia hapa ni kwamba unatakiwa kubadilika. Unahitaji kuchukua hatua ili uweze kunufaika na mabadiliko haya yanayoendelea duniani. Usiishie kuwa mtazamaji na usikubali kuburuzwa na mabadiliko haya, badala yake wewe unahitaji kuwa kinara wa mabadiliko, uweze kwenda nayo sambamba.

Unawezaje kuwa kinara wa mabadiliko na kunufaika na mabadiliko haya?
Kuna njia moja ambayo namshauri kila mtu aitumie ili kuweza kuwa kinara wa mabadiliko. Njia hiyo ni matumizi sahihi ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Kama tulivyoona, nguvu kubwa ya mabadiliko inatokana na ukuaji wa teknolojia na mtandao wa intaneti, sasa unawezaje kuingia kwenye mabadiliko haya?

Njia ni rahisi, unaanza kwa kuwa na blog yako ambayo utaitumia kulitengeneza jina lako na/au biashara yako. kwa kuwa watu wengi wanatumia mtandao wa intaneti kama sehemu yao ya kupata taarifa, wanapokuwa na shida au hitaji lolote, basi wanaanza kutafuta kwenye mtandao wa intaneti. Hivyo unapokuwa kwenye mtandao huu, unatengeneza njia rahisi ya watu kukufikia kwa kile unachofanya.

Kama unafanya biashara, unaweza kuielezea na kuitangaza biashara yako kupitia blog yako.

Kama umeajiriwa unaweza kujitengeneza na kujitangaza kama mtaalamu wa ule ujuzi ambao umeajiriwa nao, na ukatumia nafasi hiyo kutoa huduma kama za ushauri kwa wenye uhitaji.

Kama ni msanii unaweza kutumia blog kuwasiliana na hadhira yako, pia kuwapa huduma zako.

Kama ni mwanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu unaweza kuitumia blog kama sehemu ya kujifunza, yaani kile unachojifunza, unaweza kuwashirikisha wengine kupitia blog yako.

Kama huna ajira wala biashara, unaweza kuifanya blog yako kuwa biashara yako kuu, na hapo ukaitumia kutengeneza wateja na baadaye kipato.
Kila mtu ambaye ameweza kusoma hapa nilipoandika, anaweza kumiliki blog yake na akaitumia kutengeneza kipato.

Je wewe ungependa KUTENGENEZA KIPATO KW AKUTUMIA BLOG?
Kama jibu ni ndiyo basi ipo nafasi nzuri na ya kipekee kwako kutimiza ndoto yako hiyo. Nimeandaa semina ya bure ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao kwa wiki moja, kuanzia tarehe 19/09/2016. Kwenye semina hii utajifunza yote muhimu kuhusu kutengeneza fedha kwa njia ya blog.

Najiungaje na semina hii?
Kama upo tayari kunufaika na mtandao wa intaneti, na upo tayari kutengeneza fedha kwa kutumia blog, karibu sana kwenye semina hii. Kujiunga na semina hii fuata hatua hizi mbili;
Hatua ya kwanza jaza fomu ya kujiunga, kwa kuweka taarifa zako, jaza fomu hapo chini au bonyeza maandishi haya kujaza fomu.


Hatua ya pili jiunge na kundi la TELEGRAM, kwanza hakikisha una telegram kwenye simu yako, kama huna nenda kwenye PLAY STORE na search TELEGRAM MESSENGER, ukishaipata iweke kwenye simu yako na unganisha namba yako kama unavyounganisha kwenye wasap. Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno SEMINA kwa njia ya telegram kwenye namba 0717396253 au bonyeza maandishi haya na moja kwa moja utaingia kwenye kundi la semina.

Chukua hatua sasa.

Mwisho wa kujiungana semina hii ni tarehe 16/09/2016, lakini nakusihi sana ujiunge leo kwa sababu nafasi zinaweza kujaa, mfumo wetu wa email una kikomo cha kupokea watu, hivyo kuhakikisha hukosi semina hii jiunge leo hii.
Karibu sana tujifunze kwa pamoja jinsi ya kutengeneza fedha kwakutumia blog, kama mimi nimeweza, hata wewe unaweza.

Karibu sana.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

UCHAMBUZI WA KITABU; Secrets Of The Richest Man Who Ever Lived (Siri 31 Za Mafanikio Za Mfalme Selemani)

$
0
0
Katika mazingira yanayofanana na kwa nyakati zinazofanana, kuna watu wanafanikiwa sana huku wengine wakishindwa kabisa. Ni kitu gani kinawatofautisha hawa wanaofanikiwa na wale wanaoshindwa? Hili ni swali la dola bilioni moja, yaani ni swali lenye thamani kubwa, ambalo limekuwa linajibiwa na vitabu vingi ambavyo vimeandikwa kuhusu mafanikio.

Kitu kimoja ambacho kimejidhihirisha katika tafiti nyingi zilizofanywa, kuhusu wanaofanikiwa na wanaoshindwa, ni kwamba wale wanaofanikiwa, kuna vitu wanavifanya tofauti kabisa, ambavyo wanaoshindwa hawavijui, au wanavijua ila hawapo tayari kuvifanya, kwa sababu siyo vitu ambavyo wanapenda kufanya.

Mafanikio ni swala na kupandisha maji kwenye mlima, unahitaji kutumia nguvu ya ziada, tofauti na kuyateremsha kwenye mlima, unahitaji kufanya mambo ambayo hutaki kufanya, unahitaji kuonekana wa tofauti, au hata wakati mwingine uonekane umechanganyikiwa.

Leo tunakwenda kuchambua na kujifunza kutoka kwenye kitabu cha mwandishi Mudock, ambaye ameyapitia maisha ya mfalme Selemani, na kuja na siri 31 ambazo zilimfanya afanikiwe sana. Najua kwamba unaposikia jina mfalme Selemani, moja kwa moja picha inayokujia ni ya HEKIMA, kwa sababu huyu ni mmoja wa watu wenye hekima kubwa kuwahi kuwepo kwenye historia ya dunia hii. 
 

Karibu tujifunze kwa pamoja, siri 31 za mafanikio ya mfalme Selemani, tuzitumie ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

1. Selemani aliamua kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa kabla yake. Aliamua kuwa wa tofauti na wengine. Pale ambapo watu walikuwa wanahofia yeye ndiyo alipata ujasiri, wakati watu wanatembea yeye alikimbia. Selemani alipitia magumu kwenye maisha yake, lakini hakukubali kushindwa, alipambana na kufanikiwa.

SOMO; Usikubali kuwa wa kawaida, fanya kile ambacho wengine hawapo tayari kufanya. NENO; BE UNCOMMON.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Katika Kwenye Kitabu Cha The Art Of Living.

2. Selemani alikuwa na ndoto kubwa ambayo alikuwa na mapenzi nayo. Selemani alijua ni kitu gani hasa anataka kwenye maisha yake, na siku zote alifanyia kazi ili kupata kile anachotaka. Ni watu wachache sana wanaojua ni nini hasa wanataka kwenye maisha yao.

SOMO; Jua ni nini hasa unataka kwenye maisha yako, kuwa na ndoto kubwa unayoipigania.

3. Selemani alifanya HEKIMA kuwa nguzo yake kuu. Imeandikwa kwamba Mungu alipomuuliza Selemani achague chochote anachotaka, alichagua HEKIMA, na kwa kuwa na hekima alipata kila alichokitaka. Selemani alikuwa na hekima kiasi kwamba wafalme wa maeneo mengine walikuwa wakienda kwake kuomba ushauri, na walienda na dhahabu ambazo zilimfanya azidi kuwa tajiri.

SOMO; Kuwa na hekima, jifunze na fanyia kazi yale unayojifunza kila siku.

4. Selemani alikuwa akijiamini, na hili liliwafanya wale wanaomzunguka kumwamini zaidi. Wale wanaojiamini wanakuwa tayari kufanya makubwa, hata kama hakuna mwingine anayefanya, na kule kujiamini kwao kunawafanya wengine wavutiwe kuwa karibu nao.

SOMO; Kabla wengine hawajakuamini, jiamini wewe mwenyewe kwanza. Hakuna mafanikio kama hujiamini.

5. Selemani alitambua mapungufu na madhaifu yake. Hakuna mtu anayejua kila kitu, lakini wengi huwa wanajifanya wanajua kila kitu, hili linawazuia kujifunza na hivyo kushindwa kufanikiwa. Selemani alijua kuna vitu vingi hajui, na hivyo alikuwa tayari kujifunza kwa wale wanaojua. Hili lilimfanya apate hekima na maarifa mengi yaliyomletea mafanikio zaidi.

SOMO; Hujui kila kitu, kuwa tayari kujifunza kila mara na kila wakati, usidharau chochote au yeyote unayekutana naye, kuna mengi ya kujifunza.

6. Selemani alitangaza ndoto yake kubwa kwa kila mtu. Selemani alijua kwamba kuwa na ndoto kubwa na kisha kuifanya siri ni kujidanganya wewe mwenyewe, maana ukikutana na changamoto utakata tamaa, kwa sababu hakuna anayejua. Selemani alitangaza ndoto zake kubwa kwa watu, hii ilimfanya kuendelea kuweka juhudi hata pale anapokaribia kukata tamaa, kwa sababu kila mtu anaijua ndoto yake.

SOMO; Kama una ndoto kubwa kwenye maisha yako, waambie watu waijue wazi, wapo wengi watakupinga na wapo watakaokupa moyo, hao wote watakupa nguvu ya kuendelea kuifanyia kazi, ili kuwaonesha wale wanaokupinga wanakosea, na kutokuwaangusha wale wanaokuunga mkono. Ndoto zangu kubwa mbili ambazo nimekuwa nazisema wazi wazi ni kuwa bilionea (USD) na kuwa raisi wa nchi yangu Tanzania. Zako wewe ni zipi?

SOMA; Kama Unafikiri Huwezi Kuwa Bilionea Soma Hapa Na Uanze Kuelekea Kwenye Ubilionea.

7. Selemani aliomba ushauri wa watu wengine. Hakuomba na kuchukua ushauri kwa kila mtu, bali kwa watu ambao wamefanya kile ambacho anataka kufanya yeye. Au waliofanya makubwa.

SOMO; chochote unachofanya, kuna wengine ambao wameshakifanya, utaokoa muda na nguvu kwa kuomba ushauri kwa njia ya kukutana na hao waliofanya au kusoma vitabu vyao. Usianze mradi au jambo lolote kubwa kwenye maisha yako kabla hujapata ushauri wa ana kwa ana au wa kusoma kutoka kwa yule ambaye ameshafanya.

8. Selemani aliwapenda sana wale wanaomzunguka na aliwashirikisha kwenye ndoto yake kubwa. Selemani alijua ni vigumu kuweza kufikia ndoto zake kubwa bila ya ushirikiano wa watu wengine, na njia bora ya kupata ushirikiano wa wengine ni kuwapenda.

SOMO; Wapende watu, waamini na wao watakuamini kisha washirikishe ndoto yako kubwa, watafurahi kuwa sehemu ya ndoto hiyo, na mtafanikiwa kwa pamoja.

9. Selemani alieleza wazi matarajio yake kutoka kwa wengine. Mara zote alikaa chini na mtu na kuwekeana makubaliano kabla hawajaanza kushirikiana. Hili lilipunguza makosa na hali ya kutokuelewana baada ya kuanza ushirikiano.

SOMO; kitu chochote ambacho unafanya na mtu mwingine, hakikisha mmeelewana vizuri, kuweni na utaratibu ambao upo wazi na kila mtu ajue majukumu yake na matarajio ya mwenzake. Usifanye kitu kwa makubaliano ya juu juu, mtasumbuana baadaye.

10. Selemani alitengeneza mpango wa kufikia ndoto yake kubwa. Hakuishia tu kuwa na ndoto kubwa, badala yake aliweka mpango wa namna gani atafikia ndoto hiyo, kisha akachukua hatua kufikia ndoto zake kubwa.

SOMO; Usiishie tu kuwa na ndoto, bali kaa chini na andika mpango wa utekelezaji wa ndoto yako. usiishie tu kupanga na kuandika mpango, badala yake fanyia kazi kila siku.

11. Selemani alikuwa na ratiba ya matumizi ya muda wake. Alijua ya kwamba zawadi pekee yenye thamani kubwa ni muda, muda ndiyo sarafu ya maisha yetu. Tunapimwa siyo kwa kile tulichopata kwenye maisha, bali kwa jinsi tulivyotumia muda wetu. Kwa maisha yako yote utakuwa unauza muda wako, swali ni je unamuuzia nani na kwa gharama gani?

SOMO; Linda sana muda wako, usiache ukuponyoke, pangilia siku yako kabla hujaianza, usipoteze muda kwa mambo ambayo siyo muhimu kwako. Kupoteza muda ni kupoteza maisha.

12. Selemani alijadiliana kwenye kila kitu alichotaka kwenye maisha yake, hakukubaliana na hali ilivyo, badala yake alijadiliana ili kupata kile ambacho anataka yeye, na siyo kile anachopewa. Katika kuhakikisha anapata kile anachotaka, alihakikisha anajua wengine wanataka nini na kuwapatia. Alitaka kila mtu ashinde, hivyo kupata ushindi mkubwa.

SOMO; Ili upate kile unachotaka, unahitaji kujadiliana na wale ambao wanapaswa kukupa unachotaka. Na katika majadiliano yako, angalia ni namna gani kila mtu anaweza kushinda (WIN - WIN)

SOMA; Falsafa Tatu(3) Za Maisha Yako Na Jinsi Zinavyoweza Kukuletea Mafanikio Makubwa.

13. Selemani mara zote alisikiliza pande zote mbili kabla hajafanya maamuzi. Hili lipo wazi kwenye mfano wa wanawake wawili waliokuwa wanagombea mtoto mchanga. Wanawake hawa wote walikuwa na watoto wachanga, mtoto mmoja akafa, mama wa yule mtoto aliyekufa akamchukua mtoto wa mwenzake na kusema ndiyo mtoto wake. Kesi ilifikishwa kwa mfalme Selemani ambaye aliwasikiliza wote, kisha akasema kwa kuwa kila mtu anamng’ang’ania mtoto huyu, basi nitamkata na kisu katikati kila mtu achukue kipande, mwanamke mmoja alisema sawa, bora kila mtu akose, lakini mwingine akasema usimuue mtoto, bali mpe huyo mwenzangu, mtoto aishi. Hapo Selemani alimpa mtoto yule mwanamke aliyekataa mtoto asiuawe.

SOMO; Kabla hujafanya maamuzi, kabla hujahukumu, hebu jaribu kusikiliza pande zote mbili, utajifunza mengi ya kukusaidia kufanya maamuzi sahihi.

14. Selemani mara zote alisisitiza mikataba kabla ya kufanya kitu. Mara zote alihakikisha amejua kitu vizuri kabla ya kuingia, hii ilimwepusha kufanya maamuzi ambayo siyo bora kwake.

SOMO; usiamini vitu juu juu, badala yake jua kwa undani. Kabla hujaingia makubaliano ya kikazi au kibiashara na mtu, ni vyema mkawa na makubaliano yaliyoandikwa, vinginevyo mtakuja kuumbuana.

15. Selemani mara zote aliajiri watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi aliyotaka ifanywe. Hakuchukua tu mtu ni mtu, bali alihakikisha anachukua aliye bora, ambaye atatoa matokeo bora.

SOMO; Unapoajiri, usiangalie mtu anayetaka tu kazi, au ambaye yupo tayari kulipwa fedha kidogo, bali ajiri mtu aliye bora, anayeweza kuleta matokeo bora.

16. Selemani alikataa kuharakisha mambo. Mara zote Selemani alijipa muda wa kutafakari na kujifunza kabla hajafanya mazoezi. Alijua kabisa kuharakisha lazima ukosee. Kudhibitisha hili muulize mtu yeyote ambaye amewahi kuibiwa, kutapeliwa au kufanya makosa, mara nyingi aliharakisha au aliharakishwa. Ukishaona watu wanakusisitiza uharakishe kwa sababu ukichelewa utaikosa fursa, nusa harufu ya kuibiwa au kutapeliwa.

SOMO; Usiharakishe kufanya maamuzi, jipe muda w akutafakari na kujifunza kabla hujaamua ni hatua zipi unazochukua.

17. Selemani alitumia muda wake vizuri kwenye maeneo ambayo yanamletea matokeo bora. Hakuishia tu kupangilia muda wake, bali alihakikisha ameweka vipaumbele kwenye yale maeneo na mambo ambayo ni muhimu kwake.

SOMO; Kuwa na vipaumbele vya maisha yako, na ugawe muda wako kulingana na vipaumbele vyako. Popote unapowekeza muda wako mwingi, ndiyo matokeo utakayopata kwenye maisha yako.

18. Selemani alikuwa tayari kukabiliana na wapinzani wake. Selemani alijua migogoro haikosekani, na njia sahihi ya kutatua migogoro ni kukabiliana na wale ambao una mgogoro nao. Selemani hakuacha mgogoro ukue bila ya kutatuliwa, badala yake alihakikisha kila mtu ambaye ana mgogoro naye, unamalizwa kwa kutatuliwa au kwa mtu huyo kuondolewa kabisa.

SOMO; Usiache mgogoro wowote ukue, kitu ambacho kilikuwa kidogo kinaweza kukua na kuleta madhara makubwa baadaye. Kabiliana na wale ambao una matatizo nao kwa sasa, na tatueni matatizo hayo.

SOMA; Una Nini Cha Tofauti Mpaka Watu Wakufuate Na Kukusikiliza? Jua Hapa.

19. Selemani alikuwa na hamasa kubwa ya kufikia ndoto yake kila siku. ni kawaida kwa watu kuwa na hamsa pale wanapoanza ndoto zao, lakini baadaye hamasa hii hupotea kabisa na mwishowe kukata tamaa. Selemani alijua moto wowote ambao hauchochewi huwa unazima, hivyo alichochea ndoto yake kubwa kila siku, kwa kukutana na watu wanaohusika na ndoto yake.

SOMO; usikubaki ule moto wa mafanikio unaowaka ndani yako uzime, na kama hutaki uzime unahitaji kuuchoche kila siku. jihamasishe kila siku kwa kujifunza na kufanyia kazi ndoto yako hata kama ni kwa hatua ndogo. Pia zungukwa na wale watakaokuhamasisha kuliko kuzungukwa na wanaokukatisha tamaa.

20. Selemani alikataa kabisa kuvumilia ukosefu wa uaminifu. Kukosa uaminifu ni kasa mbaya ambayo inaweza kubomoa maisha ya mtu yeyote. Selemani alipoona mtu aliyemwamini amekosa uaminifu, hakumvumilia hata kidogo, alimchukulia hatua mara moja. Unapofanikiwa unakaribisha watu wengi, ukiwaruhusu watu ambao siyo waaminifu kuwa karibu na wewe, watakuangusha.

SOMO; kuwa mwaminifu, halafu usijihusishe kabisa na mtu ambaye siyo mwaminifu. Ataharibu mafanikio yako.

21. Selemani alikuwa mtu wa shukrani. Selemani alishukuru kwa kila kitu kilichokuwa kinatokea kwenye maisha yake, kwa njia hii alizidi kupata zaidi na zaidi. Je wewe ni vingapi unavyo mpaka sasa lakini umekuwa hushukuru, badala yake ni kunung’unika kwa yale uliyokosa?

SOMA; Shukuru kwa kila jambo kwenye maisha yako, unapokuwa mtu wa kushukuru, unapata mazuri zaidi kwenye maisha yako.

22. Selemani alikuwa na washauri (MENTORS) na aliwaamini washauri wake. Washauri, MENTORS ni daraja kati yako na mafanikio yako, hakuna mtu ambaye ameweza kufanikiwa yeye mwenyewe, unahitaji kuwa na washauri, iwe ni wa moja kwa moja au wasio wa moja kwa moja. Lazima kuwe na watu ambao unawaangalia na wanakusukuma zaidi kuelekea kwenye mafanikio yako.

SOMO; Kama upo makini na mafanikio unayoyataka, unahitaji kuwa na MENTORS katika safari yako ya mafanikio, tofauti na hapo unapoteza muda wako, maana utakuwa unafanya makosa na kurudia makosa yale yale kila mara.

23. Selemani alijifunza kutokana na majanga yake. Hakuna wakati mzuri wa kujifunza kwenye maisha kama wakati wa majanga. Selemani alijua majanga yanamfika kila mtu na njia bora ni kujifunza kupitia majanga hayo ili kuwa bora zaidi. Tofauti ya matajiri na masikini ni matajiri wanayapokea majanga na kujifunza, wanafanikiwa kutokana na majanga waliyopitia. Lakini masikini wanayakimbia majanga, na kuyatumia kama sababu ya kutokufanikiwa.

SOMO; Jifunze kupitia majanga na magumu unayopitia, usiyatumie kama sababu ya kushindwa, bali yatumie kama sababu ya kufanikiwa.

24. Selemani alichunga sana maneno ya kinywa chake. Alijua sumu ya maneno ya hovyo na namna yanaweza kuvuruga amani na mahusiano mazuri. Selemani alichagua maneno yake vizuri ili kuhakikisha haleti maana mbaya kwa wale anaozungumza nao. Ni mara ngapi umewahi kusema neno kwa nia njema lakini watu wakachukulia ulikuwa na nia mbaya? Hapo jua hukuchagua maneno yako vizuri.

SOMO; linda sana ulimi wako, chagua kwa makini maneno unayotumia katika mawasiliano yako na wengine. Neno dogo linaweza kuleta matatizo makubwa.

25. Selemani hakuwahi kupoteza muda wake kubishana na mpumbavu. Selemani alikuwa mkali sana juu ya wapumbavu, na alisema wazi kwamba kwa namna yoyote ile usijihusishe na mpumbavu, usimsahihishe, wala usimkosoe kwa sababu atakuona wewe ndiye unayekosea na kukupotezea nguvu zako. Hakuna kipindi ambacho ushauri huu ni mzuri kama sasa, maana wapumbavu wanazidi kuwa wengi kadiri siku zinavyokwenda, kaa nao mbali, watakuhamisha kwenye safari yako ya mafanikio.

SOMO; Wajue wapumbavu, na waepuke haraka sana, usijaribu kubishana au kumwelewesha mpumbavu, hata kuelewa na atakupotezea muda wako. Mpumbavu ni mtu asiyejua, na hajui kama hajui, hivyo mara zote hujiona yupo sahihi kuliko wengine.

26. Selemani aliwazawadia wale ambao walimsaidia kufikia ndoto yake. Alijua ili kuwahamasisha watu kuweka juhudi zaidi, unahitaji kutambua mchango wao na kuwapa zawadi kulingana na juhudi wanazoweka. Kile ambacho watu wanazawadiwa, ndicho wanachoendelea kufanya.

Somo; wape watu zawadi kutokana na juhudi wanazoweka kukusaidia kukamilisha ndoto yako. iwe ni wafanyakazi au washirika, kile unachowazawadia watu kwa kufanya, wataendelea kukifanya.

27. Selemani alijijengea sifa ya HEKIMA na UADILIFU. Kinachokufikisha kwenye mafanikio, ni ile sifa yako, jinsi ambavyo watu wanakuchukulia. Na hii inatokana na namna unavyofanya mambo yako, wala siyo kwa jinsi unavyosema unafanya, bali jinsi unavyofanya. Selemani alihakikisha maneno yake na matendo yanaendana.

SOMO; Kwa mwadilifu, timiza lile unaloahidi, fanya kile unachosema utafanya, na mara zote hutakosa cha kufanya, utaaminika na wengi.

28. Selemani alielewa nguvu ya muziki katika kutuliza akili na kupumzika. Selemani alikuwa na nyimbo nyingi ambazo zilimburudisha. Na yeye mwenyewe aliweza kuandika nyimbo zake, zaidi ya elfu moja.

SOMO; Chagua miziki ambayo inaendana na wewe, ambayo ukiisikiliza moyo wako unasuuzika, na mwisho wa siku unapokuwa umechoka, sikiliza miziki hiyo, utapata nguvu na hamasa ya kuendelea na mapambano. Unajua ni kwa nini majeshi yana bendi za muziki?

29. Selemani alihakikisha wale wanaomjua ni watu ambao ni wa muhimu kwake. Hakuruhusu kila mtu ajue maisha yake binafsi, kwa sababu alijua kwa kufanya hivyo anawapa watu nafasi ya kutumia taarifa hizi kumwangamiza. Pamoja na mengi kuandikwa kuhusu Selemani, ni machache sana yanayojulikana kuhusu maisha yake binafsi.

SOMO; Usiyaanike maisha yako hadharani, usitake kila mtu ajue kila kitu kuhusu maisha yako, taarifa nyingine zinapaswa kuwa kwako na kwa wale unaowajua tu. Huwezi kujua ni mtu gani atachukua taarifa zako na kuzitumia vibaya kujifaidisha. Na hili ni gumu sana hasa enzi hizi za mitandao ya kijamii, ambapo watu wanasukumwa kutangaza kila kitu cha maisha yao.

30. Selemani aliajiri watu ambao wana furaha, hakuajiri mtu asiye na furaha. Hii ni kwa sababu watu wenye furaha wana ufanisi mkubwa, wana hamasa na siyo watu wa kulalamika kila wakati. Ni watu ambao wanawahamasisha wale wanaowazunguka.

SOMO; ajiri na fanya kazi na watu wenye furaha. Kama utafanya kazi na watu ambao hawana furaha, watu ambao kila wakati wanalalamika na kunung’unika, kila siku yako itakuwa hovyo na utaona kukata tamaa. Zungukwa na watu wenye furaha.

31. Selemani alikuwa mwaminifu kuhusu ukomo wa utajiri wake. Licha ya kuwa mtu tajiri kuliko wote, lakini alijua kuna mambo ambao utajiri hauwezi kutatua. Licha ya kuwa na dhahabu, ardhi na kila aina ya mali, kuna nyakati ambazo Selemani alikuwa mpweke na alikiri kwamba wote tumetoka mavumbini na mavumbini tutarudi, bila ya kujali una utajiri kiasi gani.

SOMO; Hata uwe tajiri mkubwa kiasi gani, kuwa mnyenyekevu, jua kuna vitu ambavyo fedha haiwezi kutatua. Kuwa na maisha ya kawaida, ambayo yanakuridhisha wewe na yana mchango kwa wale wanaokuzunguka.

Kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa mfalme Selemani, aliandika vitabu vingi vya misemo na nyimbo, aliweza kuwaongoza watu wake kwa haki na kupata utajiri mkubwa. Tunaweza kujifunza haya na sisi pia tukawa na maisha bora kama aliyokuwa nayo yeye.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Mbinu Nane (8) Za Kuanza Siku Yako Kwa, Furaha, Hamasa Ya Hali Ya Juu Ili Kuwa Na Mafanikio Makubwa.

$
0
0
Habari mpendwa rafiki na msomaji wa AMKA MTANZANIA? Natumaini unaendelea vema kabisa na pole kwa majukumu lakini pia na changamoto unazokutana nazo hupaswi kukata tamaa bali zipokee na kabiliana nazo kwani ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Karibu mpenzi msomaji tujifunze kwa pamoja.
 
Hali ya watu kukosa tumaini la maisha na kukata tamaa katika maisha limekuwa ni wimbi kubwa katika jamii zetu. Kukata tamaa katika jambo lolote linaanzia na jinsi ulivyoianza siku yako, jinsi unavyoyachukulia mambo kwa mitazamo tofauti aidha chanya au hasi. Kama ni mtu wa kuamini katika uwezekano uko sehemu salama na kama uko katika hali ya kutoamini katika uwezekano wa mambo na kuona mambo hayawezekani uko sehemu ya hatari.

Leseni ya kuweza kufika pale unapotaka kwenda unayo wewe mwenyewe. Leseni ya kuamka utoke kwenye giza na kwenda kwenye mwanga iko mikononi mwako. Upo duniani kufurahia zawadi ya uhai, hujaja duniani kuishi kwa mateso na leseni ya kuingia katika maisha ya furaha na kutoka katika maisha ya mateso iko mikononi mwako.


Mabadiliko yoyote katika maisha yako yanahitaji leseni moja tu nayo ni maamuzi. Kama uko katika chumba kilichofungwa madirisha na milango halafu unajisaidia haja zote humo humo basi, hali ya hewa ya chumba hicho kitakua ni mbaya. Hivyo basi, badala ya kulalamika hali ya hewa imekua mbaya na dunia imekua mbaya basi fanya maamuzi ya kukifanya chumba chako kuwa sehemu salama ya kuishi. Kuna matatizo mengine yako ndani ya uwezo badala ya kulalamika fanya maamuzi ya kutatua usisubiri mhisani aje akutatulie matatizo yako.

SOMA; Kwa Nini Ni Muhimu Sana Wewe Kuwa Na Furaha.

Kwa hiyo, ndugu msomaji, matatizo ya mtu yanatatuliwa na mtu mwenyewe kwani hakuna mtu anayejua matatizo ya mtu zaidi ya yeye mwenyewe. Na hakuna mtu anayeweza kutatua matatizo ya mtu ndio maana kuna msemo unasema ya ngoswe muachie ngoswe.

Ndugu msomaji, karibu katika somo letu la leo ambapo tutajifunza mbinu za kuanza siku yako kwa hamasa ya hali ya juu na mafanikio makubwa. Na zifuatazo ni mbinu za kuanza siku yako 
kwa furaha na hamasa ya hali ya juu na mafanikio makubwa;

1. Kuamka Mapema Alfajiri; Kwanza kuamka mapema inaleta afya ya akili, mwili na kadhalika. ukitaka kuanza siku yako kwa furaha, hamasa na mafanikio makubwa siku yako amka mapema. Lala mapema na amka mapema ili mwili wako uweze kupata mapumziko mazuri kwa ajili ya uzalishaji wa siku inayofuata. Mtu anayeamka mapema alfajiri anakua na uwanja mpana wa kuianza siku yake kwa furaha na hamasa ya hali ya juu. Ukichelewa kuamka utaanza kukimbizana na muda na hutofanya mambo yako kwa ustadi wa hali ya juu na kuipangilia siku yako. Unapoamka asubuhi unaweza kuchagua kua na furaha au kutokua na furaha. Kama umeharibu asubuhi umeharibu siku yako nzima.

2. Fanya Juhudi, Sala, Tafakari (Meditation); kama unaweza kusali na kufanya tafakari katika hali ya ukimya fanya. Hakikisha akili yako haihami katika jambo lako husika na kwenda nje ya mada. Hii itakusaidia kua huru kiakili hata kimwili hatimaye ujihisi mwenye furaha na amani. Akili yako inahitaji kupata muda wa ukimya ambao ni tafakari. Tafakari inakusaidia kupata kuisikia sauti yako ya ndani inasema nini. Hivyo, hii itakusaidia kuanza siku yako kwa furaha na hamasa kubwa.

3. Soma Kitabu/Sikiliza Vitabu Vilivyosomwa; Utamaduni wa watu wengi kusoma kwao ni wakati wakiwa shule tu baada ya kumaliza anakua amefunga kila kitu. Jijengee utamaduni wa kusoma kila siku asubuhi kabla kelele za dunia hazijaanza. Lisha akili yako chakula cha kutosha ambacho ni maarifa. Unatakiwa kukua kiroho, kimwili na kiakili. Sasa huwezi kukua kiakili kama husomi vitabu. Jinoe tafadhali, usiridhike na maarifa uliyonayo. Kama hujawahi kusafiri na kuijua dunia basi anza kusoma vitabu utasafiri na kuzijua nchi nyingi na vitu vingi. Unatakiwa kubadilika kila siku kama vile kalenda inavyobadilika.

SOMA; Viungo Vikuu Vitatu(3) Vya Furaha Ya Kudumu Kwenye Maisha.

4. Usisikilize Habari; Kama unataka kuanza siku yako hovyo basi anza kusikiliza habari, uchambuzi wa magazeti nk. Habari hazitakusaidia bali zitakuhubiria vitu ambavyo vitakwenda kuharibu siku yako na hatimaye kukusababishia kukosa furaha na hamasa ya kwenda kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi wa hali ya juu. Ni vema usikilize hata sauti za hamasa au nyimbo za hamasa zinazokupa furaha na hamasa kuliko kuanza siku na kusikiliza nyimbo za huzuni. Huwezi kuondoa huzuni kwa kusikiliza nyimbo za huzuni. Kwa kifupi, epuka kusikiliza mambo hasi yote yatakayoharibu siku yako.

5. Jinenee Maneno Chanya (Affirmation); Kile ambacho unajiambia kila siku na kujithibitishia ndiyo kinachotokea katika maisha yako mara nyingi. Kama unapenda kujiambia wewe una bahati kila siku utakua na bahati, kama unajiambia wewe ni mtu wa nuksi tu na mikosi tu basi utakua hivyo. Hivyo jihadhari sana na ulimi wako kwani kinaumba kile unachosema. Pendelea kujiambia mambo chanya na siyo hasi. Kwa mfano, katika kikundi cha kisima cha maarifa kupitia mtandao wao whatsapp huwa wanaanza siku yao kwa kujinenea maneno chanya kama vile leo ni siku bora sana kwangu, namshukuru Mungu kwa zawadi hii nakwenda kufanya kilicho bora na nategemea kupata kilicho bora, kwa kusimamia misingi ya uaminifu, kujituma na nidhamu. Kwa hiyo ukijiambia kila siku maneno hayo asubuhi utakua wapi baada ya mwezi mmoja? Lazima utabadilika utakua unajipa leseni ya kuwa mwana mafanikio bora na kuachana na kulalamika hovyo. Mwandishi Makirita aliwahi kuandika hivi katika moja ya tafakari zake ambazo anatoa kila siku asubuhi ‘’kila siku fikiria na jiambie maneno chanya kama;
Ø Ninaweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu.
Ø Leo ni siku bora sana kwangu, nakwenda kufanya makubwa na nategemea kupata matokeo bora.
Ø Nina bahati nzuri kila wakati, mambo yangu yanakwenda vizuri kila mara.
Ø Mimi ni mwana mafanikio, kila siku kwangu ni siku ya kufanikiwa.
Ø Duniani ni sehemu bora sana ya kuishi, na mimi nakwenda kuifanya izidi kuwa bora zaidi.’’ Unaweza kuziona na kudharau kauli kama hizo lakini anza leo kujiambia halafu utaona mabadiliko chanya yatakavyokuja kwenye maisha yako.

SOMA; Kauli Kumi(10) Zitakazobadili Mtazamo Wako Kuhusu Furaha Na Kukuwezesha Uwe Na Furaha Ya Kudumu.

6. Usianze Siku Yako Kwa Kutembelea Mitandao ya Kijamii; Mitandao ya kijamii siku hizi imekua ikihubiri habari hasi sana na kukatisha tamaa watu wengi sana. Mtu anapoanza siku yake kwa kufungulia mtandao wa kijamii na kukuta habari ya kuumiza moyo na kuona wenzake wakifanya vitu Fulani na kuweka matukio ya picha ambayo mara nyingi siyo maisha yao halisi. Watu wanavyoona mtu anaweka picha katika mitandao ya kijamii na kuweka mazuri akija kujilinganisha na yeye mwenyewe anajikuta anaingia katika shimo la maisha ya maigizo na mwishowe kukata tamaa, wivu nakadhalika.

SOMA; Njia Muhimu Za Kulinda Furaha Yako Wakati Wote.

 7. Andaa Ratiba Ya Siku Nzima; Kuanza siku bila ratiba ni sawa na kujenga nyumba bila kuwa na msingi. Msingi wa siku yako unaanza na kuweka ratiba. Orodhesha mambo utakayofanya na mpango kazi wako wa siku nzima. Kwa kufanya hivi utakua umewasha moto mzuri wa hamasa na kuifanya siku yako kuwa bora sana.

8.  Maliza Siku Yako Kwa Kuifanyia Tathimini; hapa sasa ndio unafanya tafakari je siku yako ilikuwaje? Ilikwendaje? Unajiuliza maswali na kujipima ili kupata mrejesho wa siku yako nzima kulingana na ratiba yako uliyojiwekea.

SOMA; Mambo Sita(6) Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Maisha Yenye Furaha Na Mafanikio Makubwa.

Mwisho, jiamini wewe ni mshindi na hakuna mtu kama wewe duniani kote, una kitu ulichonacho ndani yako ambacho ni msaada kwa dunia hivyo itoe hiyo hazina uliyonayo. Usisubiri ruhusa anza hapo hapo ulipo. Huwezi kuwa mchoraji mzuri kama hujaionesha dunia kuwa unachora. Una thamani kubwa ndani yako ambayo mtu mwingine hana itoe na acha kulalamika kwani kulalamika ni utamaduni unaozalisha wavivu wengi.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

MUHIMU; Leo Ndiyo Siku Ya Mwisho Ya Kujiunga Na Semina Ya Bure Ya Kutengeneza Fedha Kwa Blog.

$
0
0
Habari rafiki yangu?
Nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwakaribisha wale wote ambao wamechukua nafasi ya kujiunga na mafunzo ya semina nitakayoendesha wiki ijayo kuhusu kutengeneza fedha kwa kutumia blog.
Kwenye taarifa hii ya leo nataka kuwakumbusha wale ambao bado hawajajiunga na semina hii kuchukua hatua SASA HIVI kwa sababu mwisho wa kujiunga na semina hii ni LEO IJUMAA ya tarehe 16/09/2016.



Yamebaki masaa machache ya wewe kupata nafasi hii ya kipekee hivyo ni vyema kuchukua hatua sasa kama kweli unapenda kushiriki semina hii. Baada ya siku ya leo kuisha, yaani saa sita kamili usiku wa leo, mfumo wetu wa kujiandikisha na semina hii utafungwa na hivyo hutaweza tena kupata nafasi hii. Kama unataka kujifunza jinsi unavyoweza kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu ulionao sasa kutengeneza kipato, basi nafasi ndiyo hii, hutapata nyingine. Chukua hatua sasa hivi, usisubiri tena.
Kama ndiyo unapata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu semina hii, basi maelekezo mafupi yapo hapo chini, yasome na jiunge mara moja.

KUHUSU SEMINA HII;
Hii ni semina ya kujifunza KUTENGENEZA FEDHA KWNEYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.
Itafanyikaje; semina itafanyika kwa njia ya mtandao, kwa email na telegram. Mafunzo yanatumwa kwenye email na maswali na majibu yatakuwa kwa njia ya telegram. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani.
Inafanyika lini; ni kwa siku saba, kuanzia jumatatu tarehe 19/09/2016 mpaka jumapili tarehe 25/09/2016.
Gharama za semina; ni bure kwako wewe rafiki yangu, lakini thamani unayoipata ni kubwa mno.

UNAJIUNGAJE NA SEMINA HII?
Kama upo tayari kunufaika na mtandao wa intaneti, na upo tayari kutengeneza fedha kwa kutumia blog, karibu sana kwenye semina hii. Kujiunga na semina hii fuata hatua hizi mbili;
Hatua ya kwanza jaza fomu ya kujiunga, kwa kuweka taarifa zako, jaza fomu kwa kubonyeza maandishi haya kujaza fomu.

Hatua ya pili jiunge na kundi la TELEGRAM, kwanza hakikisha una telegram kwenye simu yako, kama huna nenda kwenye PLAY STORE na search TELEGRAM MESSENGER, ukishaipata iweke kwenye simu yako na unganisha namba yako kama unavyounganisha kwenye wasap. Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye neno SEMINA kwa njia ya telegram kwenye namba 0717396253 au bonyeza maandishi haya na moja kwa moja utaingia kwenye kundi la semina.

MUHIMU;
1. Kama Umeshajiunga lakini una wasiwasi taarifa zako hazijafika, kesho jumamosi utatumiwa email kwa mfumo wa semina. Hivyo kama mpaka kesho hutapokea email ya semina, nitakupa maelekezo ya kufuata.
2. Kama unapata shida ya kujiunga na TELEGRAM, labda simu yako haina uwezo huo, au ukiwekwa kwenye kundi la semina hulioni, fanya mabadiliko kwenye mpangilio(setting) wa Telegram yako. kama hutaweza kabisa kupata telegram basi utapokea mafunzo ya semina kwa njia ya email.
3. Muda wa kujiunga ukiisha, mfumo wetu wa kuandikisha utafungwa, hutaweza kupata nafasi hii tena.
4. Kama una ndugu, jamaa au rafiki yako ambaye unaona anaweza kunufaika na mafunzo haya, usisite kumshirikisha, mtumie email hii kwa maelezo yaliyo hapo chini na pia mwelekeze namna ulivyojiunga wewe ili na yeye ajiunge.
Chukua hatua sasa.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

MUHIMU; Angalia Email Yako Kuona Kama Umedhibitishwa Kupokea Mafunzo Ya Semina.

$
0
0
Habari rafiki yangu?
Jana ilikuwa siku ya mwisho ya kujiunga na semina ya KUTENGENEZA FEDHA KWEYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kama ndiyo unapata taarifa hizi kwa mara ya kwanza umeshachelewa kwani hakuna nafasi nyingine ya kujiunga.
 
Dhumuni la ujumbe huu wa leo ni kutaka kuhakikisha kila aliyejiunga kwa kuweka taarifa zake amepokea ujumbe unaohusiana na semina hii ambao umetumwa leo.
Leo umetumwa ujumbe wa semina kwa wale wote ambao wamejiunga na semina ya KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. 
 
Hatua za kuchukua kama ulijiunga na semina kwa kujaza fomu ya semina.
 
1. Ingia kwenye email yako ambayo ulijiandikisha nayo kwenye semina, utakuta email ya semina imetumwa, Kichwa cha email ni; Karibu Kwenye Semina Ya Kutengeneza Fedha Kwa Kutumia Blog ifungue na kuisoma. Baada ya hapo bonyeza email iliyokutumia ujumbe ule ambayo ni maarifa@kisimachamaarifa.co.tz kisha iweke kwenye mawasiliano (ADD TO CONTACTS) yako ili ujihakikishie kupokea email zote za mafunzo.
 
2. Kama umeangalia email yako na hujaona email ya semina iliyotumwa angalia kwenye maeneo mengine ambapo email huwa zinaenda zikija kwako. Kwa mfano kama unatumia GMAIL, angalia kwenye PROMOTIONS au UPDATES, utaikuta email huko. Kama haipo huko angalia kwenye SPAM emails, utaikuta emal huko.
 
3. Kama bado huioni email pamoja na kutafuta kila eneo, nenda sehemu ya kusearch kwenye email yako, kisha andika au kopi kicha cha email iliyotumwa kisha tafuta. Kichwa ni; Karibu Kwenye Semina Ya Kutengeneza Fedha Kwa Kutumia Blog, tafuta hiyo kwenye email yako.
 
4. Kama pamoja na juhudi zote huoni email, na una uhakika ulijiunga na mafunzo haya basi tuma ujumbe kwa njia ya TELEGRAM wenye majina yako kamili, email yako kwa usahihi na namba yako ya simu, kisha utaunganishwa kwenye semina. Ujumbe utume kwenye namba 0755 953 887. 
 
Naomba kusisitiza, ujumbe utumwe kwa njia ya telegram, siyo wasap wala mesej ya kawaida, na ujumbe uandike majina yako kamili, email yako kwa usahihi na namba yako ya simu na muhimu zaidi tuma kwenye namba 0755 953 887 na siyo ile namba nyingine ya tigo iliyozoeleka.
Zoezi hili ni kwa siku ya leo jumamosi tarehe 17/09/2016. Baada ya hapo zoezi hili litafungwa kabisa, hivyo chukua hatua sasa.
 
Karibu sana tujifunze kwa pamoja.
Rafiki yako,
Makirita Amani.
www.kisimachamaarifa.co.tz

USHAURI; Ushauri Unaoweza Kuwapa Vijana Ambao Hawana Ajira Ila Wanataka Kutoka Kimaisha.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto  zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara kwa mara, na utanisamehe kama umeanza kuchoka, lakini lazima nirudie tena na tena kwamba changamoto hazikwepeki. Kwenye safari hii ya mafanikio, changamoto ni lazima, na hivyo hatuwezi kuzikimbia ila kuzitatua. Na muhimu zaidi ni kujua kwamba kama ingekuwa rahisi basi kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa. Ni ngumu na changamoto zipo kila hatua ndiyo maana ni wachache pekee wanafikia mafanikio hayo makubwa. Najua wewe rafiki yangu ni mmoja wa wachache hawa, hongera sana.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA HAPA.

Kwenye makala ya leo nitakwenda kukushirikisha ushauri unaoweza kuwapa vijana ambao kwa sasa hawana ajira ila wanataka kutoka kimaisha. Leo nataka utoke na kitu cha kumwambia kijana, kama ni wewe sawa, au kama kuna kijana alishakuomba ushauri wa aina hii basi unaweza kumwambia haya utakayojifunza leo, au kwa kumsaidia zaidi mtumie kabisa makala hii ili asome mwenyewe.
Kabla hatujaona ushauri unaoweza kuwapa vijana hawa wanaotaka kutoka kimaisha ila changamoto kwao ni ukosefu wa ajira, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na changamoto hii;

Nina vijana kama 60 napenda kuwafundisha kupitia mitandao na wakati mwingine tunakutana ana kwa ana. Changamoto kubwa kuna waliosoma kozi mbalimbali na hawana kazi, nifanyeje hata waweze kujianzishia cha kufanya. Nimekuwa nakusoma sana na wakati mwingine natumia masomo yako kuwatumia wasome ila sijajua jinsi ya kuwasaidia watoke kimafanikio. Hata ukitembelea facebook utakutana na group linaitwa Youth Family angalia hata posts zetu tunazowafundisha. Kazi kubwa wanaona pesa ndio jawabu wafanyaje sasa.
Teddy C. A.

Habari Teddy,
Hongera sana kwa moyo wako mzuri wa kupenda kuwafundisha wengine mambo mazuri ya kuwawezesha kuwa na maisha bora. Ni roho ya kipekee kwa sababu kufundisha ni kujali, wapo wengi wenye maarifa lakini hawapo tayari kuyatoa kwa wengine.
Pia asante sana kwa kuwa msomaji na kuwashirikisha vijana masomo ninayotoa, ninaamini kwa njia moja au nyingine nimewezesha kufanya maamuzi bora ya maisha yao.
Sasa kuhusiana na changamoto uliyotuandikia, ni kweli kuna vijana wengi ambao hawana ajira na hii inakuwa changamoto kwao kuweza kufikia ndoto zao. Ukiongeza na kwamba wengi wamesoma na hivyo matarajio yao yalikuwa kutumia elimu waliyoipata kutoa huduma kwa wengine.

Umefanya hatua nzuri kuwa unawafundisha vijana hao maarifa mbalimbali, ila kuna hatua moja ambayo hujawawezesha kupiga, hatua hiyo ni kuchukua hatua. Unajua ni vizuri sana kujifunza, lakini hata ujifunze kiasi gani, hata usome vitabu vizuri kiasi gani, na hata uyaelewe mambo kiasi gani, kama hutachukua hatua, hakuna kitakachobadilika, utabaki pale pale ambapo upo wakati wote.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Sasa umefika wakati wa wewe kuwawezesha vijana hao kuchukua hatua, watumie yale ambayo wamekuwa wanajifunza katika kuboresha maisha yako. Lakini hili ni gumu kutokana na mtazamo ambao vijana hao wanaweza kuwa nao. Huenda wengi wanafikiria ajira kama hatua yao ya kuanzia, hivyo wanasubiri mpaka wapate ajira hizo. Lakini kwa kuwa ajira zimekuwa siyo za uhakika, kuna umuhimu wa kuangalia upande wa pili kwenye hili.

Kwa utaratibu ambao mmejiwekea na vijana hawa katika mafundisho yenu, waambie wale ambao wapo tayari kuchukua hatua, wapo tayari kuweka sababu zao pembeni na kuchukua hatua, waanze kwa kufanya kitu. Wachague kitu ambacho wanaweza kufanya kwa pale ambapo wapo, sijajua mazingira yao yapoje, lakini kila mmoja akiangalia pale ambapo yupo, ataweza kuona hatua anazoweza kuchukua.

Kaa chini na kila ambaye yupo tayari kuchukua hatua na siyo sababu, mwambie aangalie mazingira yanayomzunguka, aangalie vitu ambavyo amekuwa anapendelea kufanya au kufuatilia, kisha aangalie elimu ambayo ameipata sasa. Akae chini na kufikiri kwa kina, kwa msaada wako kama inawezekana, aangalie ni namna gani anaweza kutumia kila kinachomzunguka kujiajiri au hata kuajiriwa.

Baadhi ya hatua ambazo mtu anaweza kuchukua, kulingana na mazingira aliyopo zinaweza kuwa;
Kuomba kazi ya kujitolea kulingana na ujuzi alionao kwenye maeneo ambayo yanaendana na taaluma yake. Aweze kuona maeneo yanayoendana na taaluma aliyosomea, na aombe kazi ya kujitolea, asitake malipo badala yake kupata uzoefu na pia kujua mambo mengi zaidi kuhusiana na kazi hizo.

SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

Kijana pia anaweza kujikusanya na wenzake, wakachangishana fedha ndogo ndogo na kuwaomba watu wao wa karibu wawaongezee mchango kidogo na wakaanza mradi wowote wanaoweza kuweka juhudi zao. Wanaweza kufanya kilimo kama wapo kwenye eneo lililopo karibu na mashamba, hapa wanaweza kuanza na hatua ndogo na kisha kukua. Wanaweza kufikiria miradi mingine inayoendana na maeneo waliyopo na kiasi cha fedha wanachoweza kuanzia. Mfano wanaweza kuanzisha mradi wa kuosha magari kama wapo maeneo ya mjini, mradi huu wanaweza kuanza na kiasi kidogo cha fedha, na wakaweka juhudi kubwa kuukuza. 

Miradi ipo mingi, ni uwezo wa vijana kufikiri na utayari wa kuweka juhudi.
Kitu kingine ambacho vijana wanaweza kufanya ni kuingia kwenye ujasiriamali wa biashara taarifa. Hapa kijana anatoa taarifa za kitaalamu kulingana na uzoefu alionao, elimu aliyopata na taaluma aliyosomea. Kijana anaweza kufungua blog yake, ambayo ni bure kabisa au kwa gharama ndogo, na kuitumia kutoa taarifa sahihi kwa watu. Hapa anaweza kuweka juhudi kubwa na akawa mtu wa kutegemewa katika utoaji wake wa taarifa, baadaye akageuza blog yake kuwa sehemu ya kipato chake. Na hapa kwenye ujasiriamali wa taarifa itabidi uwashauri wanunue kitabu changu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG ukibonyeza hayo maandishi utapata utaratibu wa kupata kitabu hiko.
Yote haya ambayo nimependekeza na mengine yanayofanana na hayo, ni mambo yanayoweza kufanywa na yeyote ambaye amejitoa kweli na anataka kubadilika. Lakini tatizo ni moja, inatakiwa mtu aweke juhudi kubwa, mtu aache uvivu, aache sababu, aache maisha aliyozoea kuishi ili kuweza kufanya hayo. Vinginevyo atakuwa na kila sababu kwa nini kila mradi niliopendekeza hauwezi kufanikiwa kwake.

Baada ya kuwashauri hayo vijana, chagua kubaki na wale ambao wanachukua hatua pekee, kama kuna ambao hawataki kuchukua hatua, ni vyema ukawaacha wakafanya kile ambacho wanaona ni sahihi kwao kufanya. Kwa sababu kukaa nao watawarudisha nyuma hata wale ambao wanafanya. Nina uhakika kwa asilimia mia moja kijana atakayechukua hatua yoyote, hawezi kubaki pale ambapo yupo sasa. Tatizo siyo fedha wala fursa, bali tatizo ni utayari wa mtu kuchukua hatua, kuweka sababu pembeni na kufanya jambo la tofauti kwenye maisha yako.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.

Teddy nikutakie kila la kheri katika kazi hii kubwa uliyochagua kuifanya, usichoke kuifanya, ila ifanye na wale ambao wapo tayari kuchukua hatua. Usifurahie tu kuwa na watu ambao wanapenda mafunzo, badala yake wawe tayari kufanyia kazi mafunzo hayo.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Jinsi Ya Kutengeneza Mtandao Wa Ajira, Ili Uweze Kutimiza Mafanikio Yako.

$
0
0
Mtandao wa ajira ni mfumo unakupa fursa wewe kuweza kujuana na watu mbalimbali  wanaofanya kazi tofauti tofauti kutoka sehemu mbalimbali. Kama tunavyofahamu ya kwamba kutafuta ajira katika ulimwengu huu wa uchumi unaokua ni suala gumu sana, hivyo ili kuweza kupunguza ugumu huo inatupasa tuweze kujua mbinu mbalimbali zitakozotufanya kuweza kutengeneza ajira tunazozihitaji kwa urahisi zaidi. Mtandao wako ni lazima ni ujue ni wapi unakotaka kwenda kufanya kazi.

Mtandao huu wa ajira unaweza ukatengeneza kwa kuangalia ndugu zako ,marafiki zako, wasomi mbalimbali, wachungaji na mashehe, wafanyakazi mbalimbali na watu wengineo ambao unahisi watakusaidia kuweza kupata ajira uipendayo kiurahisi zaidi. Ili kuweza  kutengeneza mtandao wa ajira  unachotakiwa kufanya ni kuwa na mahusiano mazuri na watu wote wanaokuzunguka bila kuzingatia nafasi zao za kazi,dini, kabila wala rangi.

Njia hii  mara nyingi itakuwezesha kupata kazi ambazo  mara nyingi ajira hizo huwa hazitangazwi, hivyo mara tu ya kutengeneza mtandao wako ajira  unatakuwa kwanza kupata taarifa mbalimbali za kazi. Mtandao wa ajira naweza nikafananisha  na sawa na kusema mvuvi mwenye nyavu kubwa na nzima ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kuvua samaki wengi ikiwa atujua namna ya kuutumia wavu huu.

Moja sababu ya watu wengi kushindwa  kutengeneza mtandao wa ajira  ni kutokana aibu na kutokujiamini. Aibu ndio sababu kubwa ambayo mtu huwa anawaza ya kwamba ataonekanaje? .Kuna usemi mmoja husema kuwa maisha huanza pale woga unapoisha Hivyo basi ili kuweza kufanikiwa kimaisha na kupata kazi uipendayo unatakiwa kukata mzizi wa aibu ulionao ili uweze kufanikiwa na kutimiza ndoto zako.

Namna ya kutengeneza mtandao wa ajira na kupata kazi kiurahisi.

1.Tengeneza orodha ya majina ambao watakusaidia kutengeneza mtandao wa ajira.
Chukua karatasi na peni jaribu kufikiri kwa makini zaidi na kuanza kuorodhesha majina  ya watu tofauti tofauti na kazi zao wanazofanya na kuona ni nani atakusaidia wewe kupata ajira kiurahisi, pia  unaweza kufanya uchunguzi wa kutosha kabla hujaanza kutengeneza orodha ya majina hayo ili kuona nani atakusaidia wapi. Watu hao tunaweza kuwaangalia katika sekta binafsi, vyuo, shule ,kanisani, kwenye vyombo vya habari, waajiriwa wa serikali na watu wengine kama vile wanaofanya kazi na ndugu zako na rafiki zako.

JITOLEE KUFANYA KAZI.

 2. Kujitolea
Ni kitendo cha kufanya kazi bila kutegemea malipo. Kufanya kazi kwa kutegemea pesa hupunguza ufanisi wa utendaji wa kazi mzuri . Kujitolea humpa  mtu ambaye anajitolea uwezo wa kiufanisi na  utendaji wa kazi. Lakini vile vile kujitolea humpa mtu uwezo wa kupata kazi kwa urahisi.

Kwa mfano mtu amejitolea katika kampuni au taasisi fulani halafu mwisho wa siku kampuni au taasisi hiyo inahitaji mfanyakazi anayoweza kutenda kazi ya mtu yule aliyejitolea mwisho wa siku kampuni au taasisi haitalazimika hata kutangaza nafasi ya ajira , bali italazimika kumuajili mtu yule ambaye alijitolea. Hivyo kujitolea inaweza kukufanya wewe uweze kupata kazi kwa urahisi kama tuliyvo ona katika mfano huo.

3. Tengeneza hisia za kujiamini.
Ndugu mpendwa ili kuweza kutengeneza  mtandao wa ajira na kupata kazi kwa urahisi amini ya kwamba unaweza kufanya kitu ambacho kitakufanya kupata kazi kwa urahisi. Kujiamini ni siri kubwa ya mafanikio katika maisha na ndoto ya maisha kufanikiwa pale mtu anapoweza kujiamini na kuachana na habari ya woga. Hivyo unachotakiwa hapa ni kuwa na hisia za kujiamini ili uweze kufanikiwa.

4. Fanya kitu tofauti na wengine.
Kabla ya kuanza kutengeneza mtandao wa ajira na kujua mbinu zitakazo kufanya upate ajira kiurahisi unatakiwa kuwa ni mtu mwenye kujituma katika mambo yako binafsi pia uwe ni mtu wa kufuatilia fursa mbalimbali zenye kuleta mabadiliko katika maisha yako na watu wengine.Kufanya kitu tofauti na wengine lazima ufikiri kwa umakini wa hali ya juu ni kitu gani ukikifanya kitakutafutisha wewe na wengine.

Kwa mfano wewe unapenda kuwa mtangaziji wa  Radio fulani na unataka kufanya kazi katika radio. Kitu cha kwanza kabisa tuma maombi ya kujitolea baada ya hapo fuatilia vipindi vya radio na kuwa mbunifu je ni kitu gani utakifanya katika radio hiyo endapo utapata nafasi ya kufanya kazi ili kuonekana tofauti na wafanyakazi wengine ambao utawakuta kazini hapo. Wajiri walio wengi wanatamani kuona mfanyakazi ambaye ni mbunifu ili kuweza kuongeza idadi kubwa ya wateja.

5. Kuwa maono yenye kutimiza malengo yako.
Huu ndio muda sahihi kufanya maamuzi wa kupanga vitu ambavyo utaviifanya mbeleni ili kuweza kutimiza ndoto na malengo yako.Kuna usemi mmoja unasema,’’ ndoto sio ile ambayo unaota usiku,  bali ndoto ya kweli ni ile inayokufanya wewe usilale. Ili kutimiza malengo yako’’.ukishindwa kupanga mambo yako kwa sasa basi mipango yako nayo itafeli pia kufeli kupo kwa aina mbili  ambazo ni kutenda bila kufikiri na kufikiri bila kutenda.

Pia kuwa na maono tofauti licha ya kufikiri kuajiliwa peke yake. Maono  hayo yawe ni yakuweza  kutengeneza kitu cha kukutengenezea pesa.Pia kama wewe ni mwanafunzi lazima ufikiri maisha yako baada ya shule yatakuwaje hii itakufanya wewe  uwe mbunifu na kutengeneza kitu tofati na wengine. Maono lazima ufikilie kitu ambacho haunacho leo hii ila ikipewa fursa hiyo uweze kutenda kwa ukamilifu.

Makala hii imeandikwa na afisa mipango na maendeleo Benson chonya
Simu; 0757-909942




Hatua Muhimu Za Kuchukua Kama Umekosa Nafasi Ya Kushiriki Semina Ya Blog.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Napenda kuchukua nafasi kutoa pole kwa wale marafiki wote ambao wamekosa nafasi ya kushiriki semina ya blog ambayo imeanza tarehe 19/09/2016. Nilitoa taarifa za semina hii kwa wiki mbili na niliweka mwisho wa kujiunga kuwa tarehe 16/09/2016. Nilisisitiza mno watu wajiunge kwa sababu ninatoa semina hii bure kwa marafiki zangu ili waweze kupata maarifa haya muhimu ya zama hizi. 


Pamoja na taarifa hizi nilizotoa kwa kusisitiza bado kuna marafiki zetu wengi ambao wamekosa nafasi hii ya kushiriki semina ya KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG. Marafiki wengi wameniandikia baada ya muda wa kujiandikisha na semina kuisha, wengi tuliwaandikisha kwa siku ya jumamosi na jumapili. Lakini marafiki wengine wengi zaidi wameniandikia hata baada ya semina kuanza, wakiomba kujiunga kwa sababu walikosa taarifa mapema. 

Kwa kweli hapo pamekuwa pagumu sana kwangu, natamani marafiki zetu hawa nao wajifunze, lakini pia mfumo tunaotumia kutoa mafunzo haya upo tofauti. Iko hivi rafiki yangu, washiriki wa semina hii ni wengi, kama elfu moja hivi, sasa huwezi kutuma somo kwa kila mtu mmoja mmoja mpaka wafike elfu moja, au kukopi email zao na kuwatumia somo. Badala yake tunatumia mfumo wa email unaoitwa AUTORESPONDER, kwa mfumo huu, somo likishatengenezwa linakwenda moja kwa moja kwa watu wote wanaolipokea, mara moja bila ya kukopi kwa kila mtu.
Hivyo ni haiwezekani kumwongeza mtu baada ya masomo kuanza, na ndiyo sababu nilikuwa nasisitiza sana watu wajiunge ndani ya muda tuliotoa na pia kudhibitisha mapema.

Lakini bado naumia ninapopokea email na meseji za marafiki ambao wanatamani sana kushiriki mafunzo haya. Nimefikiri kwa muda na kuona siyo vyema marafiki hawa wakabaki hivi hivi wakati wana kiu ya kujifunza kuhusu blog. Hivyo nimekuja na suluhisho ambalo litakuwa msaada kwa yule ambaye anataka kuchukua hatua kweli.
Nimenadika kitabu kinaitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, kitabu hiki kina mbinu zote muhimu za kutengeneza blog, kuikuza na kuweza kuitumia kutengeneza kipato. Ni kitabu ambacho kipo kwenye mfumo wa softcopy (PDF) na kinatumwa kwa email, hivyo unaweza kukinunua na kutumiwa popote ulipo. Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=).

Lakini kwa wewe rafiki yangu, ambaye umekosa nafasi ya kushiriki semina ya blog, utakipata kwa tsh elfu tano (5,000/=) tu. Hii ni nafasi ya kipekee kwako rafiki yangu kupata maarifa haya muhimu. Pamoja na kupata kitabu hiki, nitakupa nafasi ya kuniuliza swali lolote kuhusu blog ambalo hujaelewa kwenye kitabu hiki, ndani ya wiki hii. Hivyo pata kitabu hiki leo, kisome, anza kuchukua hatua na niulize swali lolote nitakusaidia.
Ofa hii nimeitoa kwa marafiki zangu waliokosa semina pekee, na itaenda mpaka mwisho wa wiki hii. Ili kupata kitabu hiki, tuma fedha tsh elfu tano (5,000/=) kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/airtel money 0717 396 253 kisha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye email yako kwa usahihi na neno NIMEKOSA SEMINA.
Fanya hivyo rafiki yangu ili kiu yako ya kuwa na blog iweze kutimia. Kumbuka kutuma fedha na baadaye ujumbe wenye email na neno NIMEKOSA SEMINA, hilo ndiyo litakuwa neno la kupata ofa hii.

Nakusihi tena rafiki yangu, kama kweli lengo lako ni kuwa na blog, chukua hatua sasa, hutakuja kupata tena nafasi nzuri kama hii unayoipata sasa. Na mwisho wa ofa hii ni jumapili tarehe 25/09/2016. Chukua hatua sasa.
Nautakia kila la kheri kwenye hatua unazochukua kila siku ili kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

UCHAMBUZI WA KITABU; PROSPERITY ON PURPOSE (Mwongozo wa kuishi maisha ya mafanikio makubwa).

$
0
0
Linapokuja swala la mafanikio, mengi yamesemwa na kuandikwa. Kwa kifupi kila mtu ana la kusema kuhusu mafanikio, kuanzia waliofanikiwa wenyewe mpaka wale ambao wameshindwa.
Pamoja na mengi ambayo tayari yamesemwa na kuandikwa bado kuna mengi tunahitaji kujifunza na kujikumbusha kila siku kuhusu mafanikio. Na hapa ndipo mwandishi Justin Herald anapotupa mwongozo wa kuishi maisha ya mafanikio.


Kwa kuanza mwandishi anatofautisha utajiri na maisha ya mafanikio. Kuna watu ambao lengo lao kwenye maisha ni kuwa matajiri, hivyo chochote wanachofanya, wanaangalia fedha kwanza. Ila pia wapo watu ambao wanataka kuishi maisha ya mafanikio, wanaangalia namna wanavyoweza kuboresha maisha ya wengine na yao pia. Wale wanaowaza utajiri pekee wanaweza kuupata ila maisha yao yanakuwa siyo bora na hawayafurahii. Ila wale wanaotaka maisha ya mafanikio, wanakuwa na maisha bora na utajiri pia.


Mwandishi anatukumbusha kwamba utajiri siyo lengo kuu la maisha, ila utajiri ni matokeo ya kuwa na maisha ya mafanikio. Hivyo kama tunataka kuwa na maisha bora na ya utajiri, tusiangalie utajiri pekee, bali tuangalie mafanikio kwa ujumla, yetu na ya wale wanaotuzunguka. Utajiri utakuwa matokeo ya yale maisha ya mafanikio tunayoishi.
 
SOMA; Kama Unataka Mafanikio Makubwa Katika Maisha Yako, Acha Kuogopa Kufanya Mambo Haya.

Karibu tujifunze yale muhimu kutoka kwenye uchambuzi wa kitabu hiki.
1. Tofauti kuu ya utajiri na mafanikio.
Mwandishi anatukumbusha ya kwamba utajiri ni pale ambapo tunajifikiria sisi wenyewe, tunafikiria kupata kile ambacho tunakitaka. Tunaweza kukazana na kupata, lakini maisha yetu yanaendelea kuwa yalivyo. Lakini maisha ya mafanikio ni pale unapojifikiria wewe na wengine. Pale unapoangalia ni jinsi unavyoweza kufanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.

2. Kanuni kuu nne za maisha ya mafanikio.
Zipo kanuni nyingi za maisha ya mafanikio, ila ukizileta kanuni hizi pamoja, unapata kanuni kuu nne ambazo ni kama ifuatavyo;
Moja; ni lazima uwe na dhamira na kiu ya kweli ya kutoka pale ulipo sasa, lazima uwe tayari kuleta mabadiliko kwenye maisha yako, ujitoe na usikubali kurudishwa nyuma na chochote.

SOMA; Kama Unafanya Mambo Haya 10 Katika Maisha Yako, Ni Lazima Ufanikiwe.

Mbili ni lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kufika pale unapotaka kufika. Hii ni kwa sababu katikati ya safari utakutana na vikwazo, changamoto na vishawishi vingi. Kama huna nidhamu, huwezi kufika.

Tatu; ni lazima uwe mnyenyekevu. Bila ya unyenyekevu huwezi kuwa na mafanikio makubwa, na ukiyapata hayatadumu. Hii ni kwa sababu mafanikio yako yanatokana na ushirikiano bora na wengine, na usipokuwa mnyenyekevu ukifanikiwa utaharibu mahusiano yako na wengine.

Nne; ni lazima uwe tayari kupokea mrejesho wa wengine. Siyo mara zote utapata kile unachotaka, au kukubaliwa kile unachoomba. Unahitaji kuweza kupokea mrejesho hasi na chanya kutoka kwa wengine na kufanyia kazi.

 3. Usiweke lengo la kuwa tajiri.
Kuna tofauti kubwa ya kuwa tajiri na kuwa na mafanikio ya kifedha (uhuru wa kifedha). Unapoweka lengo la kuwa tajiri, kila unachokiangalia unaangalia fedha pekee, siyo mbaya lakini utajinyima fursa nyingi. Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye mambo ambayo siyo mazuri kutokana na uchu wako wa utajiri. Lakini lengo lako linapokuwa mafanikio ya kifedha, au uhuru wa kifedha, unakuwa na mtazamo wa tofauti unajua kwamba unawahitaji wengine katika safari yako hiyo. Unawajenga wengine ili wewe kuweza kufikia lengo lako.

SOMA; Dalili Sita(6) Kwamba Una Fikra Hasi Zinazokuzuia Kufikia Mafanikio Na Jinsi Ya Kuondokana Nazo.

4. Kitu kimoja kinachoweza kukuzuia usifanikiwe.
Uchoyo ni tabia moja ambayo imewazuia watu kuishi maisha ya mafanikio. Na mara zote wale watu ambao wanaangalia fedha pekee ndiyo wamekuwa wachoyo sana. Hii ni kwa sababu wanaogopa kupoteza fedha na hivyo kuzishikilia, kwa njia hii wanazidi kujinyima fursa za kuwaongezea kipato. Epuka uchoyo kama lengo lako ni kuwa na maisha ya mafanikio.

5. Ubinafsi ni sumu kubwa ya mafanikio.
Kitu kingine ambacho kimekuwa kinawazuia watu kuishi maisha ya mafanikio ni ubinafsi. Ubinafsi ni tofauti kidogo uchoyo, kwenye uchoyo unashikilia kile ulichonacho na hutaki wengine wakipate, kwenye ubinafsi unajifikiria wewe zaidi hata kama wengine wataumia kwa kufanya hivyo. Unapokuwa mbinafsi huku ukiwa na lengo la kuwa tajiri, utaumiza watu wengi mno. Hii itakuzuia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa/

6. Mafanikio siyo lele mama.
Kitu kimoja kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni mtazamo walionao kuhusu mafanikio. Waliofanikiwa wanajua kabisa kwamba mafanikio siyo lele mama, wanahitaji kuweka juhudi na bidii kubwa ili kupata kile wanachotaka. Na hata wakishakipata, wanahitaji kuweka juhudi zaidi ili kulinda na kuongeza zaidi. Lakini wale wanaoshindwa, wana mtizamo tofauti, wanaamini wale waliofanikiwa walipata bahati ambayo wao bado hawajaipata. Na pale wanapojitahidi kuongeza bidii kidogo na kupata mafanikio madogo, wanajisahau kabisa na kuacha kuweka juhudi, mwishowe wanaanguka.

SOMA; Hii Ndiyo Siri Kubwa Ya Kuishi Maisha Marefu Na Yenye Mafanikio Makubwa.

7. Upo hapo ulipo sasa kwa sababu.
Hujafika hapo ulipo sasa kwa ajali au bahati mbaya, bali umejitengenezea mazingira yote yanayokuzunguka sasa. Siyo serikali, siyo wazazi na wala siyo marafiki, bali wewe mwenyewe, kwa kufanya au kutokufanya vitu fulani, umejifikisha hapo ulipo sasa.
Sasa hii ni habari njema sana kwa sababu;
Kwanza; unaweza kuwa na kesho bora kuliko leo, kwa sababu ulichofanya jana unaweza kukibadili leo.
Mbili; unaweza kuchukua hatua leo na kesho ukawa na maisha ya tofauti na uliyo nayo leo.

8. Tofauti ya umasikini na fikra za kimasikini.
Kuna watu ambao ni masikini, ambao hawa siku moja wanaweza kutoka kwenye umasikini na kuwa na maisha ya mafanikio. Ila kuna watu ambao wana fikra za kimasikini, ambao hawa hawawezi kutoka kwenye umasikini wao kwamwe, mpaka pale watakapobadili fikra zao za kimasikini. Mpe chochote mtu mwenye fikra za kimasikini na atakupa sababu ya kuendelea kuwa masikini.

SOMA; Kama Unataka Kuwa Tajiri Katika Maisha Yako, Hakikisha Unaishi Maisha      Haya.

9. Kichocheo cha fikra za kimasikini.
Kitu kimoja ambacho kinachochea sana fikra za kimasikini ni kufikiria vile vitu ambavyo huna badala ya kufikiria vile ambavyo unavyo kwa sasa. Watu wenye fikra za kimasikini muda wote wanalalamikia vile vitu ambavyo wamekosa, wana kila sababu kwa nini hawapigi hatua kwenye maisha yao. Lakini hawawezi kuangalia kile walichonacho sasa na jinsi wanavyoweza kukitumia kufika mbali zaidi.

Ondokana kabisa na fikra za aina hii, usitumie muda mwingi kufikiria unachokosa, badala yake angalia vile ulivyonavyo na unavyoweza kuvitumia kuondoka hapo ulipo sasa.

10. Mfano wa nusu glasi kwenye fikra za kimasikini.
Katika kupima mtazamo wa watu, mfano wa nusu glasi umekuwa ukitumika. Mfano huu ni inachukuliwa glasi ya maji na kuwekwa maji nusu, kisha mtu anaulizwa anaona nini. Kuna ambao wataona glasi imejaa nusu, hawa wana mtazamo chanya kwamba angalau kuna kitu. Ila kuna ambao wataona glasi ipo tupu nusu, hawa wana mtazamo hasi wa kuona walichokosa.
Wenye fikra za kimasikini wao muda wote wanaona glasi ipo nusu tupu na kutafuta nani wa kuijaza au nani kaifanya iwe tupu. Hili linawazuia kutumia fursa ya nusu iliyopo kuboresha maisha yao zaidi.

11. Tabia ambazo tumekuzwa nazo ni kikwazo cha mafanikio.
Kila binadamu anazaliwa akiwa mpya kama kitabu kipya. Anavyokua anajifunza kutokana na mazingira yanayomzunguka. Jamii zetu nyingi hakuna miongozo ya maisha ya mafanikio, hivyo watu wamekuwa wakiishi maisha ya kusogeza siku, watoto nao wanaiga maisha hayo. Ndiyo maana utakuta maisha kwenye jamii yanafanana kwa kiasi kikubwa.
Uzuri ni kwamba unaweza kuvunja tabia hizi ulizofundishwa kwenye jamii na kujijengea tabia za mafanikio.

12. Unahitaji kufanya kitu cha tofauti na unavyofanya sasa.
Kama maisha yako yapo vile vile miaka nenda miaka rudi, hakuna mchawi hapo, bali maelezo ni rahisi, umekuwa unafanya kitu kile kile miaka yote hiyo. Kwa mfano, kama wewe ni mwajiriwa ambaye unategemea mshahara wako pekee kuendesha maisha, hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako.
 Kama unataka maisha yako yabadilike, ni lazima uanze kubadilika wewe kwanza, uanze kubadili vile unavyofanya, uanze kufanya kwa tofauti na hapo utaona matokeo ya tofauti.

13. Akili pekee haitoshi, wazo bora au ajira bora pekee haitoshi.
Unahitaji kuwa na mapenzi makubwa sana kwenye kile unachofanya kama kweli unataka kuwa na maisha ya mafanikio. Na hapa ndipo maisha ya mafanikio yanapotofautiana na utajiri. Kwa mfano mtu anaweza kufanya kazi ambayo inamwingizia kipato kikubwa, akawa tajiri lakini bado akawa na tatizo kubwa, ile kazi haipendi na hivyo kuona maisha yake kama utumwa. Hivyo ili kuwa na maisha ya mafanikio ni lazima upende sana kile unachofanya. Unapokuwa na mapenzi makubwa kwenye kile unachofanya, hata kama kipato siyo kikubwa, utakuwa na maisha bora.

SOMA; Kama Una Maisha Haya Hufiki Popote, Kimafanikio.

14. Vikwazo na changamoto hazikwepeki.
Panga malengo makubwa utakavyo, weka mipango bora uwezavyo. Lakini usisahau kitu hiki kimoja, vikwazo na changamoto havikwepeki, hata ungejiandaa kiasi gani. Na hapa ndipo tofauti nyingine kati ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa inapoonekana. Wanaofanikiwa wanategemea kukutana na vikwazo na wanavitatua, wanaoshindwa hawategemei vikwazo, hivyo wakikutana navyo wanaacha kabisa kufanya kile wanachofanya.
Kumbuka hili kila siku unapoamka kitandani, hakuna njia ya mteremko ya kukufikisha kwenye mafanikio. HAKUNA.

15. Chochote unachojaribu kufanya siyo kipya.
Wewe siyo mtu wa kwanza kufanya kile ambacho unajaribu kufanya, wapo wengine walishafanya kabla yako, wengine wakafanikiwa huku wengine wakishindwa. Hivyo chochote unachofanya, jifunze kwa wengine waliofanya pia. Wengi hawana muda wa kujifunza, wanaishia kufanya kwa mazoea, na hivyo kuendelea kuwa kawaida. Na mbaya zaidi, wanarudia makosa yale yale ambayo waliowatangulia waliyo yafanya na wakashindwa. Jifunze sana juu ya kile unachofanya kwenye maisha yako.

16. Viungo vinne vya maisha ya mafanikio.
Tumegusia sana tofauti ya utajiri na maisha ya mafanikio. Utajiri unapima eneo moja la maisha ambalo ni fedha. Maisha ya mafanikio yana maeneo mengine muhimu ambayo ni lazima tuyazingatie kama tunataka kuwa na maisha ya mafanikio.
Moja; afya, kama huna afya ya mwili huwezi kupambana ili kufanikiwa.
Mbili; hisia, kama huwezi kudhibiti na kusimamia vizuri hisia zako, mafanikio kidogo yatakupoteza kabisa.
Tatu; mahusiano, yafaa nini kuwa na utajiri mkubwa ikiwa huna maelewano na ndugu zako au familia yako?
Nne; fedha, hapa ndipo wengi wanapoishia kuhesabu, wanazishika lakini wanashangaa maisha bado ni magumu kwao.

17. Mafanikio ni kutoa na kupokea.
Wanaoshindwa wanajua kitu kimoja, mafanikio ni kupokea, kupata tu wakati wote na hakuna kutoa. Wanaofanikiwa wanajua mlinganyo sahihi, mafanikio ni kupokea na kutoa. Huwezi kupokea kama hutoi, na hivyo wamekuwa wanatoa kwa wengine. Ni asili ya dunia kwama kila pengo lazima lizibwe, na pengo dogo linaweza kuzibwa na kifusi kikubwa. Hivyo wanaofanikiwa wanatumia vizuri kanuni hii ya asili, wanatoa na baadaye wanapokea mara dufu.

SOMA; Je, Unataka Kuishi Maisha Ya Mafanikio Siku Zote? Hakikisha Unaishi Maisha Haya Kila Siku. 

18. Unapotoa kuwa na mtazamo sahihi.
Kama tulivyoona ili ufanikiwe lazima pia uwe mtoaji na siyo mpokeaji peke. Ila kuwa makini unavyotoa, hutoi ili upokee, kama vile kurudishiwa, badala yake unatoa kwa sababu unataka kutoa. Na siyo kwamba ukitoa leo basi kesho unapokea, inaweza kuchukua hata miaka, lakini lazima utapokea. Na muhimu zaidi usitumie kutoa kwako kama nafasi ya kuwanyanyasa wengine. Usianze kuwaambia watu mimi nilikupa hiki hivyo na wewe nipe hiki, kanuni ya asili haiendi hivyo. Toa kwa moyo mmoja, usitegemee kupata chochote kutokana na kutoa kwako. Huenda hata unayempa hatakushukuru, usijali wewe umetaka kutoa.

19. Utumie uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Ni tafiti za kisayansi zinaonesha kabisa kwamba uwezo ulio ndani yetu ni mkubwa mno kuliko ambavyo tunautumia. Yaani uwezo tunaoutumia kwenye maisha yetu ya kawaida, ni mdogo sana ukilinganisha na uweo mkubwa tulionao. Ukitaka kupima hili angalia pale unapojikuta kwenye hali ya hatari au changamoto, utajikuta unafikiri kuliko ilivyo kawaida yako. Kuishi maisha ya mafanikio ni lazima utumie uwezo huu mkubwa uliopo ndani yako. Japo huwezi kuutumia wote, hakikisha kila siku unapiga hatua kubwa zaidi ya ulizopiga nyuma.

20. Tabia ni kiungo muhimu mno katika kuishi maisha ya mafanikio.
Kuna watu hata wapewe nini, bado maisha yao yanakuwa magumu, hii inatokana na tabia ambazo wamejijengea. Tabia zinaweza kukupeleka kwenye mafanikio au zinaweza kukuzuia kufikia mafanikio yako.
Mwandisi ametushirikisha tabia nne muhimu tunazohitaji kuwa nazo ili kufanikiwa;
Moja; maadili, lazima uwe na miiko ya vitu gani lazima ufanye na vipi huwezi kufanya kamwe.
Mbili; kujitoa kwa ajili ya kufanikiwa. Kuna wale ambao wanasema watafanya, na kuna wale ambao wanafanya, hawarudishwi nyuma na chochote.
Tatu; ujasiri, kama huwezi kupambana hutafika mbali.
Nne; unyenyekevu, tumeshajifunza huko juu.
Kama umechagua kuishi maisha ya mafanikio, basi lazima ujue mwongozo sahihi na kuufuata. Mafanikio siyo bahati waliyotengewa wachache. Bali ni matokeo wanayopata wale wanaoyafanyia kazi.
Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Karibu twende pamoja kwenye safari hii ya mafanikio, tujifunze kwa pamoja kila siku. Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA tuwe karibu zaidi. Kujiunga tuma ujumbe wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya whatAssp kwenda namba 0755 953 887. Karibu sana, mafanikio ni haki yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Tabia Nane (8) Zinazo Dhoofisha Mahusiano Yako Ya Ndoa, Uchumba Na Mengine Na Hatua Za Kuchukua.

$
0
0
Habari mpendwa rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vema kiroho, kimwili na kiakili pamoja na kuifanya dunia kuwa sehemu salama kabisa kila mmoja wetu kuishi. Mimi na wewe tunatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko ambayo tunataka kuyaona katika dunia hii. Kama unataka maisha yako yabadilike kuwa sehemu ya mabadiliko na siyo kulalamika. Kama unataka watu wabadilike anza kubadilika kwanza wewe mwenyewe. Kama unataka kupata mtu/watu sahihi katika maisha yako kuwa mtu sahihi kwanza wewe mwenyewe utawapata watu/mtu sahihi katika maisha yako.
Hii ni sheria ya asili kabisa kwamba usitegemee kupata kile ambacho hukitoi. Utapata kile ambacho unatoa na kama unatoa haba utapokea haba wala usitegemee miujiza ya kupata vinginevyo.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza kwenye kitabu cha The DNA of Relationships(Vinasaba Vya Mahusiano).

Karibu ndugu msomaji, katika somo letu la leo ili tuweze kuongeza maarifa katika ubongo wetu kwani maarifa ni hazina ya kuishi maisha sahihi hapa duniani. Na zifuatazo ni tabia nane zinazodhoofisha mahusiano yako ya ndoa, uchumba kutokua na furaha na mengine;

1. Kukosoa; Tabia ya kukosoa ni mbaya sana katika mahusiano yoyote yale. Kwa mfano, unaweza kua katika mahusiano mazuri na rafiki yako halafu huyo rafiki yako yeye ni mtu wa kukosoa tu yaani hathamini kile ambacho unafanya ukifanya kitu kizuri hapongezi bali yeye anatafuta mabaya tu ili aweze kukukatisha tamaa usisonge mbele. Kila mtu anahitaji pongezi pale anapokua amefanya kitu kizuri kutoka kwa watu wake wa karibu na sasa kama wewe una tabia ya kukosoa acha mara moja.
Hatua ya kuchukua; Kabla hujaanza kumkosoa mwenzako kwa kitu alichofanya jiulize je wewe ulishawahi kufanya nini ukakosolewa? Kwa sababu kuna watu wengine wao hawajawahi kufanya chochote katika hii dunia na kuifanya kuwa sehemu salama ya kuishi tokea Mungu aiumbe dunia. Bali kuna watu wako kwa ajili ya kuharibu tu na kukosoa. Hivyo kama una watu kama hawa katika maisha yako wakimbie na usiwashirikishe mipango yako kwani watakuwekea ukungu wa kutokuona mbele.

SOMA; Vikwazo Vitano(5) Vinavyoharibu Mahusiano Yetu Na Ndoa Zetu Na Jinsi Ya Kuviepuka.

2. Kulalamika; Kulalamika imekua desturi sana katika maisha ya leo kila mahali wamejaa walalamikaji. Mfano, labda katika ofisi Fulani kiongozi mlalamikaji, wafanyakazi wake wote walalamikaji yaani ukianzia getini unaanza kupokewa na walalamikaji. Sasa tabia kama hii inadhoofisha mahusiano yetu kabisa. Utamaduni wa kulalamika hovyo bila kuchukua hatua huwa unazaa wavivu wengi sana. Kama wewe uko katika mahusiano ya ndoa, uchumba, urafiki na mengine acha tabia ya ulalamikaji kabisa.
Hatua ya kuchukua; Kama kuna kitu unaweza kukibadilisha ambacho kipo ndani ya uwezo wako basi ukibadilishe na kama kipo nje ya uwezo wako nyamaza usilalamike. Muda unaotumia kulalamika chukua hata kitabu soma ukurasa mmoja utapata tumaini la maisha.
 

3. Kulaumu; Maisha ya kulaumu ni maisha ambayo hayana furaha. Sasa kama wewe muda mwingi unautumia katika kulaumu utapata wapi furaha? Kuna watu wanajilaumu kila siku kulingana na mambo waliyofanya hapo awali, kuwalaumu wengine kwa nini kitu Fulani hakipo hivi au kimeenda vile. Usilaumu, maisha ya kulaumu ni maisha hasi hayo ambayo yanaziba fursa na baraka nyingi katika maisha yako.
Hatua ya kuchukua; usiwe mtu wa kulaumu katika maisha yako kama jambo limetokea limeshatokea huwezi kulibadili tena bali chukua hatua kwa wakati wa sasa na acha kulaumu vitu vya wakati uliopita. Mwingine analalamika hata jinsi alivyoumbwa na huwezi kujibadilisha jinsi ulivyoumbwa kama umejikuta umeumbwa jinsi ulivyo basi jipokee jinsi ulivyo ili uishi maisha ya furaha.

4. Kukosa uvumilivu; Maisha ya mafanikio yanahitaji uvumilivu. Kama uko kwenye uhusiano wa ndoa mnatakiwa kuvumiliana kama mlivyoweka agano lenu siku ya kwanza. Mkiwa mnaishi maisha ya kujifananisha na watu wengine hakika mtakata tamaa ya maisha na hatimaye kila mmoja wenu kuingia na hali ya kukosa uaminifu katika maisha ya ndoa. Uvumilivu wenu katika maisha ya ndoa utazaa matunda mazuri sana kama kila mmoja katika nafasi yake akiwajibika ipasavyo. Kama kila mmoja akikwepa majukumu katika nafasi yake basi hakika hawezi kukwepa matokeo atakayopata katika nafasi yake.

SOMA; Umuhimu Wa Mawasiliano Katika Kujenga Mahusiano Bora Ya Kijamii.

5. Kutosamehe; Kwanza muasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe. Sasa wewe binadamu uliyeumbwa na huyo Mwasisi Huyo kwa nini hutaki kusamehe? Hujui kusamehe ni kuponya majeraha ya nafsi? Maisha ya ndoa nyingine yamejaa kutosameheana kila mtu kashika hamsini zake maisha ya ndoa kati ya wawili hao hatimaye yanakua hayana furaha. Mtunga zaburi anasema, kama Bwana angehesabu makosa yetu nani angesimama? Hakuna hata mtu angeweza kusimama. Lakini Mungu mwenye huruma anatusamehe kwa nini wewe hutaki kumsamehe mwenzako? Kutokusamehe kunadhoofisha mahusiano yoyote yale katika maisha yetu ya kila siku. Na kama tukisameheana tunarudisha uhusiano wetu uliovunjika awali. Unarudisha upendo wa awali uliopotea.
Hatua ya kuchukua; kila siku ni zawadi kutoka kwa Mungu. Unatakiwa kusamehe kila siku ya Mungu katika maisha yako. Kusamehe ni kumfutia mtu deni, je una madeni mangapi mpaka sasa ya kutosamehe? Inuka nenda kasamehe leo usisubiri kesho kwani hujui kama kesho utakua hai au la hivyo usikubali kufa huku ukiwa na deni la kutosamehe. Ndugu, kama una madeni ya hela unadaiwa, je hata madeni ya kutokusamehe unashindwa kulipa?

6. Mabishano; mabishano yanaleta fedheha katika mahusiano yetu. Wanaobishana kila mmoja anataka akubalike kama yeye ndio bora kuliko mwenzake. Sasa hali hii inawafanya hata watu kuingia katika hali ya magomvi na hatimaye kusababisha mauti. Watu wakiwa katika mabishano husababisha ugomvi, hasira, huleta visasi na hatimaye chuki ambayo chuki huzaa mauti.
Hatua ya kuchukua; epuka mabishano katika mahusiano yoyote uliyonayo sasa hivi kama ni ndoa, urafiki, uchumba nakadhalika.

7. Kumdhibiti au kumtawala mwenza wako; kila binadamu ana tabia yake hapa duniani. Ni ngumu sana kumdhibiti mwenzako ambaye ulishamkuta na tabia ambazo tayari anazo. Kila mtu anapenda uhuru katika maisha yoyote yale. Usimtawale mwenzako kama mtoto mdogo vile yaani afanye vile unavyotaka wewe. Matatizo mengi huwa yanaanzia hapa ambapo kila mmoja anataka kumtawala mwenzake. Wanaume wengi hupenda kuwatawala wenza wao na kutowapa uhuru katika maisha yao ndio maana matatizo hayaishi. Muelewe mwenzako na anataka nini na siyo kumkataza kila kitu kama mtoto kwani kila mtu anatakiwa kuwa na uhuru lakini pia haijalishi uko kwenye ndoa au la kila mtu ana thamani yake ambayo anatakiwa kuitoa katika hii dunia kabla hajafa. Sasa kwa nini unataka mwenzako afe na hazina aliyokua nayo ambayo bado hajaitoa duniani?

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Law Of Attraction

8. Vitisho; maisha ya vitisho siyo maisha ya kuishi. Mke anatoa vitisho kwa mume wake vivyo hivyo kwa watoto. Mahusiano hayawezi kuimarika kwa kupeana vitisho kila siku. Maisha ya vitisho ni maisha ambayo yamejaa hofu. Kwanini tusiponye mahusiano yetu na tuondoe hofu iliyotawala katika mahusiano yetu? Mahusiano yamejaa hofu baba anawajaza watoto hofu, viongozi wanawajaza watu wanaowaongoza hofu hivyo maisha yamegeuka kuwa hofu badala ya furaha. Maisha ya vitisho yanafanya dunia kuwa si sehemu salama ya kuishi. Maisha ya vitisho yanaharibu thamani au hazina walizo nazo watu katika kuifanya dunia kuwa bora zaidi.
Mwisho, maisha ni furaha, upendo, amani, muda, uhuru. Kila mmoja wetu atumie nafasi yake kuifanya dunia kuwa bora na salama kwa kila mmoja wetu kuishi. Wawezeshe wenzako kupata kile wanachokitaka kwanza, na wewe utapata usiwe na ubinafsi kabisa kama ingekua watu wengine ni wabinafsi sidhani kama dunia ingekua hivi ilivyo leo. Mabadiliko ni mimi na wewe.

Njia Bora Ya Kuepuka Majungu Na Kukatishwa Tamaa Kwenye Eneo Lako La Kazi.

$
0
0
Habari za leo rafiki? 
Karibu tena kwenye mtandao wetu wa AMKA MTANZANIA ambapo tunajifunza mambo mbalimbali ambayo yanatuwezesha kuwa na maisha bora zaidi kila siku. Kama ambavyo tunajua, kila siku ni siku ya kujifunza, hakuna siku ambayo mtu utaamka na kusema tayari nimeshajua kila kitu. Kila siku kuna changamoto mpya na hivyo kujifunza kila siku ni muhimu.
Kwenye makala yetu ya leo, tunakwenda kuangalia njia bora ya kuepuka majungu na kukatishwa tamaa kwenye eneo lako la kazi. Hakuna sehemu ambazo zimekuwa na majungu kama sehemu za kazi, hakuna sehemu ambazo zimewakatisha watu tamaa, kuua ndoto zao na kuwafanya wawe kawaida kama sehemu ya kazi.

Ukikutana na mtu ambaye ndiyo anaanza kazi anakuwa na hamasa kubwa sana, anakuwa na mipango ya jinsi atakavyoitumia kazi hiyo kufanya makubwa kwenye kazi na kwenye maisha yake pia. Anakuwa amejipanga vizuri sana. Lakini baada ya kuanza kazi, ile hamasa yote inapotea, mipango yote mikubwa inayayuka na anaishia kuwa kawaida, kama walivyo wafanyakazi wengine.

Ukichunguza sababu kubwa zinazowafanya watu wachukie kazi zao, sababu inayopolekea wengi kuwa na msongo wa mawazo kwenye kazi zao, ni kutoka kwa wafanyakazi wenzao. Kwa kuwa mtu anatumia karibu nusu ya muda wa maisha yake kwenye kazi, wale wanaomzunguka kwenye kazi wana ushawishi mkubwa kwake.
 

Kumekuwa na majungu na ukatishwaji tamaa mkubwa sana kwenye maeneo ya kazi. Pale mtu anapojitahidi kufanya kazi yake vizuri, anaonekana ni kiherehere au anajipendekeza kwa bosi. Wengine wanamwambia usijisumbue, hayo makubwa unayofikiria hapa haiwezekani. Na wanaotoa maneno kama haya ni wale wazoefu kwenye kazi hiyo, ambayo wamekaa pale kwa muda mrefu. Ni vigumu sana kuwapinga watu hao kwa sababu ya ugeni wa mtu na uhalisia kwamba kama mtu amekaa kwenye kazi hii kwa miaka 20 anajua mengi kuliko mimi ambaye hata mwaka sina. Kwa kufikiri hivi, wengi wamekuwa wanaishia kukata tamaa.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuepuka Majungu Kwenye Eneo La Kazi

Leo nataka nikuambie ya kwamba, hupaswi kukata tamaa, hupaswi kuwasikiliza wale wanatoa majungu, hata kama ni aliyekuajiri, unachohitaji kufanya wewe ni kimoja pekee, fanya kazi iliyo bora, kulingana na ujuzi wako na uwezo mkubwa ambao upo ndani yako.
Kitu kimoja muhimu unachopaswa kujua ni hiki, huwezi kuwazuia watu kusema kile wanachotaka kusema. Ukikazana kufanya kazi bora watakusema kwamba una kiherehere na kujipendekeza. Ukifanya kazi a hovyo watakusema kwamba ni mzembe na huna ujuzi wa kazi. Kwa vyovyote vile wanaotaka kusema watasema, hivyo ni muhimu wewe ufanye kile ambacho ni sahihi kwako.
Hii ndiyo njia bora kabisa ya kuepuka majungu na kukatishwa tamaa kwenye eneo lako la kazi, fanya kile ambacho ni sahihi kufanya, kila wakati. Na siyo kwamba ukifanya hivi wataacha kutoa majungu na maneno ya kukatisha tamaa, hapana, wataendelea kutoa maneno hayo, lakini kwa kuwa wewe hutawasikiliza na kuacha, watafika wakati watachoka, kwa sababu watajifunza wewe husikilizi, wewe ni mtu wa viwango vyako na hakuna namna wanaweza kukurudisha nyuma. Baada ya muda watu watakuwa wanakuheshimu kupitia kazi yako, na watakuona wewe ni mtu wa tofauti na pekee.

SOMA; Mambo Nane(8) Yatakayokufanya Uwe Na Fikra Chanya Kila Wakati Ili Uweze Kufikia Mafanikio.

Rafiki wacha leo nikupe siri moja kuhusu saikolojia ya binadamu, mara zote watu hupinga kile kitu ambacho wao hawawezi kufanya au hawawezi kuwa nacho. Kwa sababu hawataki kuamini kwamba kuna watu wengine wanaoweza kufanya kile kinachowashinda wao kufanya. Hivyo wanatafuta njia ya kuhakikisha mtu hafanyi tofauti na wanavyofanya wao. Siri nyingine kubwa ya kisaikolojia ni kwamba watu huheshimu na wakati mwingine kusujudu kile ambacho kinaonekana ni kikubwa kuliko wao, kile ambacho kinaonekana ni kikubwa kuliko maisha ya kawaida. Sasa hapa ndipo ilipo nafasi ya wewe kutokea, onekana kuwa na uwezo na ufanisi mkubwa kuliko ilivyo kawaida, mwanzoni watafikiri wewe ni viwango vyao, hivyo watajaribu kukupinga na kukukatisha tamaa. Lakini wakigundua hurudi nyuma, moja kwa moja wanaanza kukuheshimu, kwa sababu unakuwa umevuka ile hali ya ukawaida ya binadamu.

Jiwekee viwango vyako mwenyewe na fanya kazi kwenye viwango hivyo, viwe viwango vya juu sana, ambavyo wengine wanaviangalia kwa mbali tu, hawathubutu hata kuvifikiria. Fanyia kazi viwango vyako hivyo na watu wataanza kukuelewa.

SOMA; Kama Utafanya Mambo Haya, Hakuna Tena Wa Kukuzuia Kufanikiwa.

Kitu kingine muhimu sana unapaswa kujua ni kwamba watu wanawaheshimu sana wale watu wanaoonekana kuwa na msimamo. Kama kuna kitu ambacho unakisimamia kwa kujiamini, hata kama siyo kitu sahihi, kuna watu wengi watakuamini na kukuheshimu. Lakini kama kila wakati unabadilika kutokana na watu wanavyokupinga, basi wanakuona wewe huna msimamo na hivyo kukudharau.
Rafiki, nimalize kwa kusema kwamba, majungu na kukatishwa tamaa kwenye maeneo ya kazi ni kitu ambacho hakitaisha kwa wewe kuwasikiliza wale wanaosema, bali kitaisha kwa wewe kuendelea kufanya kile ambacho ni sahihi mara zote. Hivyo basi jiwekee viwango vyako vya utendaji, na visimamie hivyo mara zote. Usiwasikilize watu wanaokushauri jambo lolote ambalo ni tofauti na viwango vyako na siyo sahihi.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Swali Moja La Kujiuliza Kila Siku Ili Kupata Hamasa Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.

$
0
0

Habari rafiki?
Kama ambavyo wote tunajua, safari ya mafanikio siyo safari rahisi, ina changamoto na vikwazo vingi. Watu wengi wanaanza safari hii lakini hawafiki mbali. Matumaini makubwa waliyokuwa nayo yanazima kabisa pale wanapokutana na magumu na changamoto. Hili ndiyo limekuwa linatokea kwa wengi na hivyo kushindwa kupiga hatua kwenye maisha yao.

Leo tunakwenda kuangalia swali moja muhimu la kujiuliza kila siku ili kupata hamasa ya kuendelea na safari yako ya mafanikio. Kupitia swali hili utaweza kuvuka kila changamoto unayokutana nayo, hata kama itakuwa changamoto kubwa kiasi gani.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Swali ambalo unapaswa kujiuliza kila siku kwenye safari yako ya mafanikio ni hili; JE NI KITU GANI KINANISUKUMA KUFANYA HIKI NINACHOFANYA? Kwa lugha nyingine ni kwa nini unafanya kile ambacho umechagua kufanya? Unapokuwa na sababu ambayo inakusukuma na sababu hii ikawa kubwa, hakuna kikwazo au changamoto inayoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa.

Sasa jibu la swali hili linaweza kuwa jibu rahisi au jibu halisi.

Jibu rahisi ni lile jibu la juu juu ambalo haliwezi kukuvisha wakati wa changamoto. Kwa mfano kama jibu ni unafanya ili upate fedha, kama utafanya lakini ukakosa fedha, moja kwa moja hutaweza kuendelea kufanya. Kwa sababu lile kusudi ulilonalo unaona halitimii. Au kama jibu lako ni unafanya kwa sababu kila mtu anafanya, au unataka uonekane na wewe unafanya, ni rahisi kuishia njiani, kwa sababu majibu haya hayana uzito wa kushindana na changamoto utakazokutana nazo.

Jibu halisi ni lile ambalo umelitambua baada ya kutafakari kwa kina, pale ambapo umeweka tamaa zako pembeni na kuangalia kwa uhalisia kile hasa unachofanya. Kwa mfano unapoangalia mchango unaotoa kwa wengine kupitia kile unachofanya, unapata hamasa kubwa ya kuendelea hata kama unakutana na changamoto. Kwa sababu unajua wapo watu ambao wananufaika kupitia kile ambacho unafanya. Au unapofanya kitu ili kutumia uwezo mkubwa ambao upo ndani yako, kwa sababu unajua unaweza, basi hutakatishwa tamaa na changamoto utakazokutana nazo.

Ili uweze kufikia jibu halisi la kwa nini unafanya kile unachofanya, ni lazima ujijue wewe mwenyewe, ni lazima ujitambue unataka nini kwenye maisha yako, na upo tayari kutoa nini ili upate kile ambacho unakitaka. Zifuatazo ni hatua muhimu za kuzingatia;

Moja; jitambue wewe ni nani.

Jitambue wewe ni nani na umekuja kufanya nini hapa duniani, jua ni maeneo gani ambayo uko vizuri na jua ni maeneo yapi ambayo una udhaifu. Kwa kujua haya, utaweza kuweka nguvu kubwa kwenye yale maeneo ambayo uko vizuri na kuachana na yale ambayo upo dhaifu. Pia jua ni mambo gani ambayo unapendelea kwenye maisha yako. Changamoto kubwa ambayo inafanya watu wanakuwa na maisha magumu, ni kufanya kazi au biashara ambazo hawazipendi, wanakuwa wanafanya kwa sababu tu wanataka fedha au kwa sababu kila mtu anawategemea wafanye. Unahitaji kuvuka hatua hii.

Mbili; jua ni kipi upo tayari kutoa ili kupata kile unachotaka.

Wote tunajua, na kama ulikuwa hujui jua leo, hakuna kitu cha bure, kila kitu unachotaka na kupata kwenye maisha yako kina gharama yake. Ni lazima uwe tayari kulipa gharama ili kupata kile unachotaka. Na kadiri unavyotaka vitu vikubwa, ndivyo gharama ya kulipa inakuwa kubwa. Jua gharama na kuwa tayari kuilipa, kuwa tayari kuweka juhudi kubwa, kuwa tayari kutoa mchango mkubwa kwenye maisha ya wengine, na ndipo utakapoweza kupata kile unachotaka kufanya.

Kauli moja ninayotaka ujikumbushe ni hii rafiki; huwezi kufanikiwa kama hujawawezesha wengine kufanikiwa. Je wewe ni watu gani umejitoa kuwawezesha kufanikiwa? Wajue na chukua jukumu hilo haraka.
Tatu; kuwa tayari kujifunza na kubadilika.

Hakuna njia moja ambayo ukipita lazima ufike kwenye mafanikio, kila mtu ana njia yake ya kipekee, hivyo hata kama watu watakushauri vitu vya kufanya, bado ni wewe mwenyewe utakayejua njia halisi kwako. Na hii ni changamoto kwa sababu hatuzaliwi na kitabu cha maelekezo ya kile ambacho tunatakiwa kufanya. Hiki ni kitu tunachopaswa kukijua wenyewe, na tunakijua baada ya kujaribu vitu vingi. Ili uweze kufikia kile hasa ambacho ni maalumu kwako, ni lazima ujaribu vitu vingi tofauti tofauti. Katika kujaribu vitu hivi, kuna ambavyo utavipenda sana na utakuwa tayari kuvifanya hata kama ni vigumu. Ili ufikie hatua hii ni lazima uwe tayari kujifunza na kubadilika.

Mtazamo sahihi na chanya juu ya kile unachotaka, ni hitaji muhimu mno kwenye safari ya mafanikio. Hii ni kwa sababu ya ugumu wa safari hii na hivyo kuhitaji kitu cha kukupa hamasa kwenye kila hatua unayopiga. Jua kwa nini hasa unataka kile ambacho unataka, na hakuna kitakachoweza kukurudisha nyuma.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>