Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

USHAURI; Jinsi Ya Kutatua Changamoto Ya Soko Kwenye Kilimo Cha Kibiashara.

$
0
0
Habari za leo rafiki?
Karibu kwenye makala yetu ya leo ya USHAURI WA CHANGAMOTO ambapo tunaangalia zile changamoto zinazotuzuia kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kwenye maisha. Hakuna njia iliyonyooka, kila kitu kina changamoto zake, na wakati changamoto inakusumbua, siyo rahisi kuona njia mbadala za kupita ili kutoka kwenye changamoto hiyo. Hapa ndipo tunapofanyia kazi kupitia kipengele hiki, kuziangalia changamoto hizi na hatua bora kuchukua.

Katika makala ya leo tunakwenda kuangalia changamoto ya masoko kwenye kilimo cha kibiashara. Kabla hatujaingia na kuangalia changamoto hii, tuangalizie kwanza kilimo kwa siku za hivi karibuni. Kwa sasa kilimo kimekuwa tu siyo kilimo, bali kimekuwa ujasiriamali na hata biashara kwa wengi ambao wanataka kujikwamua kiuchumi. Kadiri hali ya uchumi inavyokuwa ngumu, kukosekana kwa ajira na hata kutoridhishwa na kipato kwa wale walioajiriwa, watu wengi wamelazimika kuingia kwenye kilimo.


Kilimo kinaonesha dalili nzuri za kuweza kumtoa mtu yeyote anayekifanya vizuri na kwa ubunifu. Hii ni kwa sababu bado uhitaji wa mazao ya kilimo ni mkubwa ndani na nje ya nchi. Lakini pamoja na uwezo huu wa kilimo kuwatoa watu kifedha, bado changamoto ni nyingi. Changamoto zinaanzia kwenye upatikanaji wa shamba bora, upatikanaji wa maji ya umwagiliaji kwa sababu mvua sio za uhakika. Upatikanaji wa mbegu bora pia ni changamoto kubwa, wasaidizi kwenye shughuli hizi za kilimo nao wamekuwa changamoto, siyo watu wote wapo tayari kujitoa.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Ukiweza kuvuka changamoto zote hizo, za kuanzia shamba mpaka kuvuna, kuna changamoto kubwa inayokuwa mbele yako mkulima, changamoto hii ni soko. Kumekuwa na watu wa katikati ya mkulima na mlaji, watu hawa wanajulikana kama madalali. Hawa wamekuwa wakipata faida mara dufu kuliko hata mkulima aliyeteseka shambani kwa muda mrefu. Je unawezaje kutatua changamoto hii ya soko kwenye kilimo cha kibiashara? 

Hapa tutakwenda kushirikishana mbinu za kufanya hivyo. Lakini kabla hatujaingia kwenye ushauri wenyewe, tusome maoni ya mwenzetu aliyetuandikia kuomba ushauri juu ya hili;

Nina malengo ya kulima kilimo cha biashara cha matikiti maji, lakini changamoto kubwa ninayoiona ni soko, wakulima tunalanguliwa sana hasa mashambani na ukizingatia mimi ni mkulima ninayetaka kuanza, naomba msaada katika hili. Naishi dar maeneo ya kigamboni, Ahsante. David Haule.

Kwa mwenzetu David pamoja na wengine wote ambao mnapitia changamoto ya masoko kwenye kilimo, hapa kuna mambo muhimu sana kuzingatia ili kuondokana na changamoto hii ya masoko.

KWANZA; Angalia aina ya kilimo unachofanya au kutaka kufanya.
Kumekuwa na wimbi la watu kukimbilia kilimo cha zao fulani, kwa sababu tu kuna watu wachache waliofanya kilimo hiko na wakafanikiwa. Mfano mzuri ni kilimo cha matikiti maji. Zao hili ndiyo limekuwa kimbilio kwa kila anayefikiria kuingia kwenye kilimo. Hii ni kutokana na ufupi wa msimu wake na usambazaji wake kuwa mkubwa.
Kuna sheria moja ya uchumi inasema kwamba kadiri kitu kinavyopatikana kwa wingi, bei yake inakuwa ndogo. Na hili ndilo limekuwa linatokea kwa wakulima wanaolima mazao yanayoliwa na wengi. Unapofika msimu wa mavuno, bei inakwenda chini kwa sababu kila mtu anauza. Na hapa ndipo madalali wanaponufaika sana kwa kununua kwa bei ya chini sana na kwenda kuuza kwa bei ambayo wao watapata faida. Hawajali kama bei wanayonunua kwako mkulima itarudisha gharama zao, wanachoangalia ni kama wao wanapata faida.
Hatua ya kuchukua hapa ni epuka kulima mazao ambayo kila mtu anakimbilia kulima, na ikiwa ndiyo chaguo lako basi una vitu viwili vya kufanya, cha kwanza ni kulima tofauti na msimu, yaani ujipange ili unapovuna upatikanaji usiwe mkubwa. Cha pili soma namba mbili hapo chini.

SOMA; Fursa katika Kilimo cha Bustani

PILI; Hakikisha unatoa mazao bora sana.
Watu wengi wanapokutana na changamoto hiyo hapo juu, pale madalali wanapotaka kununua mazao yao kwa bei ya chini, hukataa na kuamua kupeleka mazao yao sokoni wao wenyewe. Na hapa ndipo wanapokutana na ukweli mchungu, wakifika sokoni, watu wanachagua ubora. Kwa zao kama tikiti maji, watu wanaangalia mbegu na ukubwa wa tunda. Ukipeleka matunda madogo utajikuta unapata hasara kubwa kuliko hata ungemuuzia dalali shambani.
Hivyo hakikisha kwa kilimo chochote unachochagua kufanya, mazao unayotoa ni bora sana. Unapokuwa na mazao bora, hata dalali akifika shambani, hatakuwa na nguvu ya kukuburuza, na akitaka kufanya hivyo unaweza kuamua kuyapeleka sokoni wewe mwenyewe. Kwa zao la tikiti, unapokuwa na matunda makubwa, mnahesabiana na dalali na kuuziana kwa bei fulani kwa kila tunda, lakini ukiwa na matunda madogo ananunua kama mzigo hivyo anakadiria tu bei.
Kilimo chochote unachochagua kufanya, hakikisha unatoa mazao bora sana. Weka juhudi kubwa, fuatilia kwa karibu kuhakikisha unatoa mazao ambayo unaweza kuyauza popote pale.

SOMA; Teknolojia Katika Kilimo: Kilimo Cha Greenhouse Na Aina Zake.

TATU; Tafuta njia mbadala za kusambaza mazao yako.
Kama umechagua kufanya kilimo cha kibiashara, basi unahitaji kutafuta njia mbadala ya kusambaza mazao yako. Unaweza kuyasambaza kwa kupeleka sokoni na kuuza kwa jumla, au unaweza kuyasambaza kwa kuuza kwa rejareja. Unachohitaji ni kuangalia wapi ambapo mazao yako yanaweza kuhitajika kisha tengeneza mtandao wako wa masoko. Kwa mazao ya nafaka unaweza kuuza moja kwa moja kwa walaji kama mahoteli, shule na hata taasisi nyingine zinazotumia nafaka katika vyakula.
Ili kuweza kusambaza mazao yako mwenyewe, unahitaji kuwa na mazao bora, ambayo yatawafanya watu wayafurahie.

NNE; Ongeza thamani ya mazao yako.
Tatizo kubwa ambalo wakulima wengi wanapitia ni kukosa taarifa za kutosha, na hivyo wenye taarifa wanazitumia kufaidika zaidi. Kwa mfano mtu analima mpunga na kuuza ukiwa kama mpunga. Mtu mwingine anaununua na kukoboa, anapata mchele na kuupanga katika viwango tofauti. Anatafuta vifungashio na kufunga mchele huo na kuuza kwenye maeneo mbalimbali, ikiwepo kusambaza nje ya nchi. Kwa mkulima wa kawaida anaweza kuona hili ni jambo kubwa sana ambalo yeye hawezi kufanya. Lakini kwa kupata taarifa sahihi mkulima yeyote anaweza kuongeza thamani kwenye mazao yake.
Kwenye zao lolote unalolima, jiulize ni kwa namna gani unaweza kuongeza thamani ili usiuze likiwa ghafi. Bei ya kitu ghafi na kilichoongezwa thamani ni tofauti kubwa sana. Fikiria ni namba gani unaweza kuongeza thamani kwenye zao unalolima.

SOMA; Jinsi Ya Kutatua Changamoto Ya Usimamizi Kwenye Kilimo Na Jinsi Ya Kupata Mtaji.

TANO; Pata taarifa, jielimishe kuhusu kile unachozalisha na kilimo kwa ujumla.
Kuna taarifa nyingi sana kuhusu kilimo lakini wakulima wanazo chache mno. Wakulima wengi wamekuwa wavivu kujifunza vitu vipya kuhusu kilimo. Wengi wamekuwa wakilima kwa mazoea, wengine wamekuwa na imani zisizo sahihi kwenye kilimo kuhusu matumizi ya mbegu za kisasa na mbolea za viwandani. Jielimishe kuhusu kile kilimo unachofanya, jua wengine wanaolima na wakafanikiwa ni mbinu gani wanatumia. Jua mbegu bora zaidi ni zipi na zinahitaji mazingira gani.
Unapoamua kufanya kilimo sehemu yako ya kujiingizia kipato, chukulia ile ndiyo kazi yako, na mara zote angalia fursa ya kujifunza kupitia kilimo unachofanya. Unapolima na kupata mazao ambayo siyo viwango ulivyotarajia, jiulize ni wapi ulikosea na wakati mwingine usirudie kosa hili.

Kilimo siyo rahisi hata kidogo, unahitaji kuweka juhudi kubwa kwenye kulima, kujifunza na hata kusambaza mazao yako. unahitaji kuweka juhudi kubwa ili kuweza kufikia malengo yako ya kifedha kupitia kilimo. Jambo zuri ni kwamba inawezekana, kwa sababu wapo wengi walioweza.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Njia Muhimu Za Kulinda Furaha Yako Wakati Wote.

$
0
0
Ni ukweli uliowaza kila mwanadamu aliye chini ya jua anahitaji kuwa na furaha ya kweli nay a kudumu maishani mwake. Hakuna mtu ambaye haitaki furaha  ya kweli kila mtu huitafuta kwa udi na uvumba na kwa njia anazojua yeye ili mradi zimfikishe kwenye furaha hiyo ya kweli.
Hata pamoja na shughuli nyingi ambazo binadamu anazifanya kila siku za kiuchumi, lakini shughuli hizo ukiziangalia huwa zinalengo jambo moja muhimu sana la kuitafuta furaha ya kweli. Mpaka hapo unaona furaha ya kweli ni kitu cha muhimu na kinatakiwa kulindwa wakati wote pale unapoipata.
Lakini kwa bahati mbaya, wengi huwa wanapotea kwa kufikiri sana kwamba ili uwe na furaha ya kweli ni lazima uwe na pesa nyingi kwanza. Kama ulikuwa unawaza hivyo umepotea. Furaha ya kweli haiji eti mpaka uwe na pesa na mali nyingi. Hilo linatokea vipi? Fuatana na mimi katika makala haya, nikupe njia za uhakika za kulinda furaha yako wakati wote.
1. Ishi sasa.
Njia pekee na nzuri ya kulinda furaha yako wakati wote ni kuamua kuishi sasa na wala sio jana au kesho. Watu wengi wanakosa furaha katika maisha yao kwa sababu ya kujibebesha mizigo mingi kwa wakati mmoja na ambayo inawelemea.
Kwa mfano utamkuta mtu anawaza sana jambo ambalo lilimuumiza sana jana au jambo la kesho ambalo hana uwezo wa kulitawala. Kwa mazingira kama haya inakuwa siyo rahisi kupata furaha ya kudumu. Hiyo inaonyesha ili uwe na furaha lazima uishi sasa kwanza kama vile hakuna changamoto inayokusumbua.

2. Jipende zaidi.
Siri nyingine ambayo unaweza kuitumia na ikakupa furaha ya kudumu ni wewe kuamua kujipenda. Hili unaweza ukalifanya hivi, kwa kuamua kujali afya yako wewe mwenyewe binafsi, lakini hiyo haitoshi hata kwa kupenda pia yale mambo unayoyafanya.
Mara nyingi wengi tunajikosesha furaha halisi kwa sababu ya kutokjipenda wenyewe. Usishangae sana na kujiuliza kivipi mtu anakuwa hajipendi? Hili linaweza kutokea kutokana na jinsi unavyoilinda afya yako. kama unaona afya yako huilindi vizuri, basi ni dalili tosha hujipendi.
3. Kuwa mkweli wakati wote.
Ukweli siku zote unauwezo mkubwa wa kukulinda na kukupa furaha wakati wote. Unapojijengea hulka au tabia ya kuwa mkweli, mara nyingi huo ukweli ni lazima ukupe furaha na uongo unakuwa kinyume chake lazima ukupotezee furaha .
Pengne unajiuliza kwa nini? Subiri kidogo nikwambie. Mara nyingi unapokuwa mwongo kila wakati utajikuta ule uongo unakufunga. Utajikuta ni mtu unaingia migogoro na watu wengi kwa sababu ya uongo. Kwa hali kama hiyo huwezi kuwa na furaha, tofauti na kama ungekuwa mkweli ungejenga furaha ya kudumu sana.
4. Penda familia yako.
Hakuna ubishi katika hili pia furaha ya kweli  inapatikana kutokana na wewe kujali na kupenda familia yako. Huwezi kuwa na furaha ya kweli kama nyumbani kuna mgogoro mkubwa. Kila wakati utakapokuwa ukiwaza familia kama kuna mgogiro litakuumiza sana.
Kwa hiyo iri kubwa hapa ilikudumisha furaha yako, tenga muda wa kufurahia maisha na familia yako. Hakikisha unajenga kila siku upendo kwa mke na watoto wako na kudumisha pia mahusiano na ndugu wengine. Kwa hilo litakusaidia kukupa furaha ya kweli maishani mwako.
5. Tekeleza majukumu yako.
Siku zote jifunze kuwa mtu wa kutekeleza majukumu yako mapema. Kama kuna kuna kazi unaifanya itekeleze mapema. Kwa kifupi, unatakiwa kuwajibika kwa kile unachokifanya bila kuacha. Ukifanya hivyo litakusaidia kuepuka lawama nyingi ambazo utapewa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yako.
Na kwa sababu ya hilo utake usitake ni lazima litakunyima furaha yako ambayo ungetakiwa kuwa nayo. Kwa hiyo mpaka hapo unaona kumbe siri nyingine ya furaha ya kweli ni kutekeleza majukumu yako kila wakati. kinyume cha hapo ni kujitakia mgogoro wa nafsi na kujikuta kukosa furaha.
Kwa kuzingatia mambo hayo ni msingi mkubwa sana wa kukusaidia kukupa furaha ya kudumu kwenye maisha yako wakati wote.
Endelea kutembelea www.amkamtanzania.comkujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

UCHAMBUZI WA KITABU; BRAIN STORM (Jinsi Unavyoweza Kuitumia Akili Yako Kupata Mawazo Bora Na Ya Kibunifu).

$
0
0
Kila mmoja wetu ni mbunifu, tofauti ya wale wanaoonekana ni wabunifu na wale ambao wanaonekana siyo wabunifu ni jinsi wanavyotumia akili zao. Wale ambao wanazitumia akili zako kupata mawazo tofauti na yale yaliyozoeleka wanaonekana kuwa wabunifu. Hakuna ambaye anazaliwa akiwa mbunifu, bali tunatofautiana kwa jinsi tunavyotumia akili ambazo tunazo.

Kila mmoja wetu anahitaji ubunifu kwenye maisha yake. Kuanzia kwenye kazi, biashara na hata maisha ya kawaida, ubunifu ni hitaji muhimu la kuwa na maisha bora na yenye mafanikio. Moja ya njia ya uhakika ya kushindwa kwenye jambo lolote lile ni kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, na kwa mtindo ule ule. Unapokuwa mbunifu unaweza kuja na njia tofauti na bora za kufanya mambo yako, kitu ambacho kitaongeza ufanisi wako.


Mwandishi Jason Rich, mwandishi wa kitabu; BRAINSTORM TAP YOUR CREATIVITY TO GENERATE AWESOME IDEAS AND REMARKABLE RESULTS anatupa mbinu za kuweza kutumia akili zetu kupata mawazo bora na ya tofauti ambayo yatatuwezesha kufikia mafanikio tunayotaka.
Karibu tujifunze pamoja kupitia uchambuzi huu wa kitabu hiki;

1. Ubunifu siyo tabia ya kuzaliwa nayo, yaani hakuna mtu amezaliwa akiwa mbunifu, kama ilivyo hakuna mtu amezaliwa akiwa anajua kusoma. Lakini kila mtu amezaliwa na zana moja muhimu sana katika ubunifu. Zana hii ni akili ambayo kila mmoja wetu anayo. Sasa kama ambavyo ulijifunza kusoma na kuandika, unahitaji kuifundisha akili yako jinsi ya kuja na mawazo ya kibunifu. Hivyo usikate tamaa na kuona wewe siyo mbunifu, bali jua namna ya kujifunza ubunifu.

2. Haijalishi unafanya kitu gani kukuingizia kipato kwenye maisha yako, unaweza kufanikiwa zaidi ya hapo ulipofikia sasa kama utaweza kuitumia akili yako vizuri. Akili yako ni kama mgodi ambao bado hajachimbwa kabisa. Kuna hazina kubwa sana ipi ndani yako. Unachohitaji ni kuiwezesha akili yako kuja na mawazo ya kibunifu, na kinachobaki ni wewe kutumia mawazo hayo kufika kule unakotaka kufika.

3. Ubunifu ni kujiruhusu kufanya makosa. Wengi wetu siyo wabunifu kwa sababu tunaogopa sana kukosea, tunaona tukijaribu kitu tukakosea watu watatucheka. Ubunifu ni kujipa ruhusa ya kufanya makosa mengi, na kisha kujua makosa yapi unaweza kuyatumia vizuri zaidi. Kila kitu unachokiona ni bora, jua kuna mtu alikuja na wazo la kitu hiko, na huenda wazo hilo lilikuwa la hovyo, lakini kwa kuliboresha waliweza kuleta kitu bora.

4. Hakuna mtu ambaye umri wake umempita kwa kuwa mbunifu. Kila mtu anaweza kuwa mbunifu bila ya kujali ana miaka mingapi. Watu wengi wamekuwa wanafikiri ubunifu ni kwa ajili ya vijana. Na hawa ni wale ambao kwa ukubwa wao wanaogopa kukosea na hivyo kufanya mambo kwa mazoea. Watoto wadogo ni wabunifu kuliko watu wazima kwa sababu watoto hawaogopi kuchekwa, hawaogopi kukosea.

5. Mawazo unayohitaji ili kuboresha kazi yako, kukuza biashara yako, kuimarisha familia yako, yote yapo ndani ya akili yako. Mawazo haya kuna mahali umeyafungia na hujaweza kuifikia. Ubunifu ndio utakaokuwezesha kufikia mawazo hayo ambayo tayari unayo.

SOMA; KILA MTU NI MBUNIFU, JE UNAUTUMIA UBUNIFU WAKO KUFIKIA MALENGO YAKO?

6. Kama wewe ni mwajiriwa, hakuna sehemu ambayo mawazo ya kibunifu yanahitajika kama ndani ya makampuni na mashirika. Makampuni na mashirika mengi huwa yanapoteza ubunifu kutokana na ukubwa wake na watu kufanya vitu kwa mazoea. Wewe ukiwa mbunifu unaweza kuja na mawazo ambayo yataboresha zaidi na wewe kunufaika zaidi pia.

7. Kama upo kwenye biashara, hakuna kitu unaweza kufanya kuepuka ubunifu. Unahitaji ubunifu kuwavutia wateja wako, unahitaji ubunifu kuwafanya wateja wanunue zaidi, unahitaji ubunifu kuwafikia watu wengi zaidi. Unahitaji ubunifu kupunguza gharama, unahitaji ubunifu kuongeza ufanisi. Kila siku kwenye biashara yako, ni siku ambayo unahitaji kuwa mbunifu zaidi. Na mawazo haya ya kibunifu yapo ndani yako, siyo kuangalia wengine wanafanya nini uige, bali tumia akili yako na wale wanaokuzunguka kupata mawazo bora.

8. Hatua ya kwanza ya kuwa mbunifu ni kufikiria nje ya boksi. Umekuwa unasikia hili neno FIKIRIA NJE YA BOKSI, lakini maana yake ni nini hasa. Maana halisi ya kufikiria nje ya boksi, ni kufikiria kile ambacho hujawahi kufikiria, kufikiria kama ile hali uliyopo sasa hujaingia bado. Kwa mfano kwenye biashara, ukiwa unafikiria kuongeza wateja, unaanza kufikiria kwa zile njia ulizotumia karibuni. Hapa unafikiria ndani ya boksi. Kufikiria nje ya boksi ni kufikiria kama ungekuwa huna mteja hata mmoja ungetumia njia gani kupata wateja, au kama ungekuwa unafanya biashara nyingine tofauti ungepataje wateja. Hapa unafikiria nje ya boksi na ni rahisi kuja na mawazo ya kibunifu.

9. Ubongo wetu umegawanyika kwenye sehemu kuu mbili, ubongo wa kulia na ubongo wa kushoto. Ubongo wa kushoto unahusika na vitu vya kufikiri vitu kama lugha, mahesabu na mengine yanayohusisha kufikiri, yanafanyiwa kazi kwenye ubongo wa kushoto. Ubongo wa kulia unahusika zaidi na mambo ya burudani na ubunifu. Mambo kama muziki, uchoraji, yanahusika zaidi kwenye ubongo wa kulia. Ili uwe mbunifu, ni muhimu uweze kutumia sehemu hizi mbili za ubongo wako vizuri.

10. Njia ya kwanza ya kuwa mbunifu ni kukataa vitu kama vilivyo. Hakuna kitu kinaua ubunifu kama kukubali kila kitu kama kilivyo na kufanya kwa mazoea. Unahitaji kuwa mpinzani, unahitaji kujikatalia hata wewe mwenyewe mara kwa mara. Unapojikuta unafanya kitu leo kwa sababu jana ulifanya, ni wakati mzuri wa kujiuliza kwa nini unafanya hivyo, je hakuna njia nyingine za kufanya?

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha The Truth About Innovation (Ukweli Kuhusu Uvumbuzi)

11. Ili kuwa mbunifu, mazingira yanahusika sana. Ni vigumu kuwa mbunifu kama upo kwenye eneo ambalo linakuletea msongo wa mawazo. Hivyo pale unapotaka kufanya zoezi la kupata mawazo ya kibunifu, tafuta eneo ambalo lina utulivu na linakufanya ujisikie vizuri. Inawezekana unapendelea eneo tulivu kabisa, au unapendelea muziki wa sauti ya chini. Jua mazingira yanayoendana na wewe na yatengeneza ili uyatumie kuwa mbunifu.

12. Unahitaji kuujua mwili wako mwenyewe, watu tunatofautiana kwenye nguvu za miili yetu kulingana na muda wa siku. kuna watu ambao wanakuwa wabunifu sana wakati wa asubuhi, wengine jioni wengine usiku wa manene. Wale wa asubuhi watadamka mapema wakati wale wa usiku wa manane watakesha. Jua ni wakati gani bora kwako na upange shughuli zako katika muda ule. Pia uzuie usumbufu kwenye muda huo.

13. Unaweza kufanya zoezi la kuja na mawazo ya kibunifu ukiwa mwenyewe au ukiwa na kikundi cha watu. Kila njia ina faida na hasara zake. Unapofanya mwenyewe unakuwa na uhuru zaidi lakini pia unakosa mawazo ya tofauti, unaweza kuishia na mawazo ambayo siyo tofauti sana na yale uliyonayo sasa. Unapofanya zoezi hili na kikundi cha watu, unapata faida ya kupata mawazo tofauti tofauti lakini una hasara ya kutumia muda mwingi na wakati mwingine kukatishana tamaa baina ya wale wanaohusika na kuja na mawazo ya kibunifu.

14. Unapofanya zoezi la kuja na mawazo ya kibunifu, kwanza jua ni kitu gani unataka kutatua, anza na tatizo. Kisha jipe muda wa kuja na mawazo hayo, usijiwekee ukomo wa muda, bali jiwekee ukomo wa mawazo. Usiseme nataka baada ya saa moja niwe nimepata wazo bora, badala yake jiwekee kwamba unahitaji kuondoka na wazo bora. Wakati unatoa mawazo au wengine wanatoa mawazo, usianze kuhukumu mawazo. Hata kama wazo linaonekana ni la kijinga kabisa, wacha mawazo yabubujike, baadaye mtachambua wazo moja moja.

SOMA; HII NDIO SABABU KUU YA WEWE KUTOFURAHIA MAISHA YAKO.

15. Angalia vitu kwa jicho la tofauti, hii ni njia moja muhimu ya kutumia wakati unafanya zoezi la kupata mawazo ya kibunifu. Angalia vitu kwa upande tofauti, jiulize kama ungekuwa upande mwingine ungeteka nini. Kwa mfano kama unataka kuongeza wateja wa biashara yako, jiulize kama wewe ungekuwa mteja ungetaka kupata nini? Je kama ungekuwa mshindani wa biashara yako, ungefanya nini ili kupata wateja wengi zaidi. Fikiria kwa njia hizo na utakuja na mawazo mengi.

16. Tumia milango yako yote mitano ya fahamu kuja na mawazo tofauti, tumia kuonja, kunusa, kusikia, kuona na kuhisi kuna na mawazo tofauti kwenye kile ambacho unataka kuongeza ubunifu wako. Kadiri unavyotumia milango yako ya fahamu, ndivyo unavyoona njia tofauti za kufanya kitu. Jiulize unataka watu waone nini, wasikie nini, wahisi nini, wapate ladha gani.

17. Uliza maswali, hoji sana. Hii ni njia ambayo itakuwezesha kupata mawazo ya kibunifu kutoka kwako na kwa wengine. Unapokutana na watu waulize maswali mengi ambayo yatakuwezesha kujifunza kupitia wao. Jihoji wewe mwenyewe kwenye kila unachofanya na utaona mawazo ya tofauti yanakujia. Kama hujui wapi uanzie kuuliza maswali kwa wengine, anza na maswali haya sita ya msingi sana.
Swali la kwanza ni NANI (WHO), anza swali lolote na nani....
Swali la pili ni NINI (WHAT), unaweza kuanza swali na nini....
Swali la tatu ni KWA NINI (WHY), uliza kwa nini kitu kipo kama kilivyo.
Swali la nne ni WAPI (WHERE), anza kuuliza wapi....
Swali la tano ni VIPI (HOW), uliza ni jinsi gani kitu kinafanyika.
Swali la sita ni LINI (WHEN), anza kwa kuuliza lini...

18. Anza na VIPI KAMA (WHAT IF). Moja ya njia unazoweza kutumia kupata mawazo ya kibunifu ni kujiuliza swali VIPI KAMA kwenye kile ambacho unakiona au kukifanya. Kama umemwona mbwa jiulize vipi kama mbwa angekuwa na miguu mitano, vipi kama angekuwa anataga, vipi kama asingekuwa na manyoya, jiulize maswali kama haya na jipe majibu, utaona akili yako unaanza kupata mawazo ambayo hujawahi kupata awali. Uzuri wa njia hii ni kwamba unaweza kuitumia popote. Hebu anza kuitumia hapa unaposoma hivi, jiulize vipi kama mimi ndiyo ningekuwa nimeandika haya, ningewezaje kuyatumia kwenye kazi yangu au biashara yangu, na je ni njia gani nyingine naweza kutumia kupata matokeo unayotaka kupata. Iruhusu akili yako ije na mawazo mengi uwezavyo.

SOMA; Mbinu 5 Zitakazokufanya Uwe Mbunifu Zaidi.

19. Ukishapata mawazo mengi kwa njia hii ya kuruhusu akili yako ibubujike na mawazo, sasa unahitaji kuyachambua mawazo hayo ili uone ni wazo lipi unaweza kulitekeleza. Katika kuchambua mawazo uliyopata, tumia njia hii ya utatu kuchambua kila wazo. Andika wazo kwenye karatasi kisha gawa safu tatu, safu ya kwanza andika faida, safu ya pili andika hasara na safu ya tatu andika madhara. Kisha orodhesha kila kitu kwenye safu yake, andika faida zote za wazo hilo, andika hasara zake na kisha andika madhara ya wazo hilo. Mwisho oanisha safu hizi tatu na ona wazo hilo linafaa kutekelezwa au la.

20. Ukishapata wazo ambalo unaweza kulitekeleza, kinachobaki ni wewe kulifanyia kazi wazo hilo ili uweze kupata kile ambacho unataka kupata. Unahitaji kuweka juhudi kubwa ili kuweza kufanikisha wazo lolote.

21. KITU KIMOJA MUHIMU CHA KUONDOKA NACHO KWENYE KITABU HIKI; Kama utasahau kila kitu kwenye kitabu hiki basi ondoka na kitu hiki muhimu na kitumie kwenye maisha yako ya kila siku; wewe ni mbunifu, kiungo kikuu cha ubunifu ulichonacho ni akili yako, kama unataka kuwa mbunifu, usiogope kukosea. Mwisho kabisa, tumia maisha yako ya kila siku kupata mawazo mapya na ya kibunifu, kila unachopitia, jifunze.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Haya Ndiyo Madhara Ya Kutotumia Falsafa Ya Ufagio Kwenye Maisha Yako.

$
0
0

Habari mpendwa Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vema na kama hauko vema basi nakupa pole na Mungu akusaidie hatimaye uwe salama. Basi ndugu msomaji karibu katika makala yetu ya leo.
Tupo duniani kwa ajili ya mapenzi ya Mungu na siyo kwa mapenzi yetu sisi. Kila mtu ana siku yake ya kuiaga dunia pale mwili na roho vinapotenganishwa hivyo basi usikubali siku ipite bila kuacha alama katika hii dunia yaani ufanye jambo ambalo mtoto atakayezaliwa kesho aje ajifunze kupitia wewe hata kama hautokuwepo duniani. Hakuna aliyeomba kuzaliwa wala kuandika barua kwa nini sasa watu wanakuwa na majivuno na vipaji ambavyo wamepewa bure ili kusaidia watu wengine?

Watu wenye vipaji na taaluma mbalimbali wamekuwa ni watu wa majivuno sana na kujiona wao ndio kila kitu katika hii dunia. Umekwenda shule au chuo kusomea ujuzi fulani ili uende ukatumikie jamii na siyo kujivunia ile elimu uliyonayo kuwakandamiza watu wa chini au watu wengine. Kama wewe ni daktari wito wako ni kutoa huduma kwa wagonjwa kuwahudumia vizuri na kuhakikisha unamsaidia mteja wako tatizo lake siyo kuonyesha majivuno mbele ya mteja wako. Duniani kuna kitu kinaitwa specialization of work yaani ubobezi wa kitu Fulani, kazi Fulani, mtaalamu wa kitu Fulani. Hivyo basi, kila mtu amebobea kwenye kitu Fulani ndio maana tuna wataalamu wa fani mbalimbali ambapo kwa pamoja tunaweza kutegemeana na kujenga dunia.


SOMA; Hizi Ndizo Sehemu Nne (4) Muhimu Za Kuchota Baraka Katika Maisha Yako.

Hakuna anayeweza kujitegemea kwa kila kitu hivyo basi, mwandishi Shabani Robert aliwahi kuandika katika moja ya mashairi yake na kusema kwamba kujitegemea siyo kujitosheleza. Kwa hiyo, lazima uwategemee wengine hata kama wewe ni mbobezi wa kitu Fulani. Lazima utahitaji watu wengine ili uweze kufanikisha mambo yako mengine. Majivuno ni mabaya yanaweza kukunyang’anya hata kile ambacho unacho. Usitumie kile ambacho unacho kuwadhihaki watu wengine bali tumia ulichonacho kuwasaidia watu wengine.

Watu wengi wamekosa kutumia falsafa ya ufagio katika maisha yao. Falsafa ya ufagio ni unyenyekevu. Na mtu aliyekosa unyenyekevu basi ana majivuno na kile ambacho anacho. Kama wewe ni daktari toa huduma yako kwa unyenyekevu na siyo kwa majivuno. Mhudumie mgonjwa kwa kumuonyesha falsafa ya unyenyekevu mpaka mgonjwa anahisi kupona hata kabla ya kutibiwa. Wasaidie watu kulingana na taaluma uliyonayo kwa unyenyekevu na siyo kuonyesha majivuno ya taaluma uliyonayo. Umesoma ili utoe huduma kwa watu na siyo kuonyesha majivuno ya kile ambacho unacho au elimu yako uliyonayo. Watu hawataki majivuno wanataka kupatiwa huduma kwa unyenyekevu wa hali ya juu. Tumia elimu/taaluma yako kuwasaidia wengine, kuwafariji watu katika matatizo wanayokubana nayo, kuwa tia moyo na kuwaonesha upendo katika huduma unayotoa.

SOMA; Mambo 10 Ambayo Ni Muhimu Kuyafahamu Kwenye Maisha Yako.

Waonyeshe watu unyenyekevu wako katika kutoa huduma, wahurumie kwani huruma ni zaidi ya kutoa sadaka ya pesa. Kama wewe ni mwalimu basi wafundishe wanafunzi wako kwa moyo, kwa ukarimu na kwa falsafa ya unyenyekevu . Wasikilize wanafunzi wako wanasema nini ,wasikilize wateja wako katika kile unachofanya wanasema nini. Kama wewe ni kiongozi wasikilize unaowaongoza wanasema nini usitawale kwa majivuno na kujiona wewe ndiye una stahili zaidi kuliko wengine. Wewe ndio unajua sana kuongoza kwa hiyo, wengine hawana nafasi ya kutoa mawazo yao hapana usifanye hivyo hata watu unaowaongoza wana mawazo mazuri hivyo wasikilize ili muweze kujenga kampuni au taasisi imara hapo ulipo. Ukiwa unaongoza taasisi au kikundi Fulani ukajiona wewe ndio kila kitu mambo yatakuendea mrama hivyo basi, waruhusu, washirikishe watu kutoa mchango wao.
Mtu aliyesoma anatakiwa kuwa mnyenyekevu kama vile hajui kitu. Hajivuni kulingana na elimu yake ya juu aliyonayo wala taaluma aliyonayo. Bali anakua msikilizaji mzuri, anatoa huduma kwa unyenyekevu.

Madhara ya kukosa unyenyekevu ni kuwa na majivuno. Hivyo basi, ukishakuwa na majivuno utajiona wewe ndio unastahili zaidi kuliko wengine. Utajiona wewe ndio miungu watu hapa duniani, utawadharau wengine, utakosa uaminifu na wengine, utashindwa kujifunza kwa wengine, utashikwa na wivu, utarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kwa hiyo, haya ndio madhara ya kukosa kutumia falsafa ya ufagio katika maisha yako ambayo ni unyenyekevu. Kama umewahi kufagia pale unapotakiwa kuinama lazima uiname uwe mnyenyekevu kama vile ufagio unavyokutaka ufanye. Haijalishi elimu au cheo ulichonacho unatakiwa kuwa mnyenyekevu katika maisha yako.

SOMA; Umuhimu Wa Mawasiliano Katika Kujenga Mahusiano Bora Ya Kijamii.

Mwisho, tunatakiwa kuishi katika falsafa ya ufagio ambayo ni unyenyekevu. Usiwe na majivuno kwani majivuno yatakufanya uwe na kiburi na hatimaye kuwadharau watu wengine. Umepewa kipaji ulichonacho ili kusaidia watu na siyo kujivuna na kuwaumiza wengine na kuwakandamiza eti kwa sababu wewe ndio umesoma. Tupo duniani kwa ajili ya kusaidiana na kila mtu anamtegemea mwenzake kukamilisha malengo yake na hakuna jeshi la mtu mmoja bali kuna jeshi la watu wengi na kujitegemea siyo kujitosheleza. Hivyo basi, ishi katika misingi na kusimamia falsafa ya unyenyekevu katika kutoa huduma bora.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Mtazamo unaohitaji ili kufanikiwa kwenye biashara yako.

$
0
0
Kama kuna kitu ambacho kinapatikana kila mahali kwa sasa ni mafunzo na ushauri kuhusu ujasiriamali. Mambo haya ya ujasiriamali yamekuwa maarufu kwenye zama hizi kutokana na ugumu wa kupatikana kwa ajira na ugumu wa ajira zenyewe kwa wale wachache wanaozipata. Sasa hivi watu wengi wanapanga au tayari wameshaingia kwenye ujasiriamali.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kitu kimoja muhimu sana ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba ujasiriamali siyo rahisi kama ambavyo watu wanafikiri kabla ya kuingia, au wanavyofundishwa. Ujasiriamali una changamoto zake na wengi wanaoingia kwenye ujasiriamali wanashindwa. Tafiti zilizofanywa kwenye nchi zinazoendelea zinaonesha kwamba kati ya biashara kumi zinazoanzishwa kila mwaka, biashara nane zinakuwa zimeshakufa inapofikia mwaka mmoja na nusu tangu kuanza kwa biashara hizo.
Kama wewe umeshaingia kwenye ujasiriamali au biashara, au ndiyo unapanga kuingia kuna mtazamo ambao unahitaji kuwa nao ili kuweza kuendesha biashara yenye mafanikio. Kwa kuwa na mtazamo huu sahihi utaepuka kujidanganya na kudanganywa na wengine na kuweza kufanya maamuzi sahihi kwenye biashara yako.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Business @ The Speed Of Thought. (Mbinu Za Kufanya Biashara Kwenye Zama Hizi Za Taarifa).

Mtazamo muhimu unaopaswa kuwa nao ni kuviona vitu katika uhalisia wake. Mara nyingi hatuoni uhalisia wa vitu, bali tunaona kile ambacho tunataka kuona au tunatarajia kuona. Namna hii ya kuangalia vitu inatukosesha fursa kubwa iliyopo kwenye vitu hivyo. Badala yake unafanya vitu kwa mazoea na hivyo kujiweka katika hatari ya biashara yako kufa pale mabadiliko yanapotokea. Mabadiliko yanatokea kila siku, hivyo ni muhimu kuwa umejiandaa kila siku.

Yafuatayo ni mambo muhimu kuzingatia ili kujijengea mtazamo wa kuiona biashara katika uhalisia wake.

Hakuna biashara ambayo ni rahisi kufanya.
Watu wengi wamekuwa wakikazana kutafuta biashara ambayo ni rahisi kufanya na itakayowaletea mafanikio ya haraka. Ukweli ni kwamba hakuna biashara ambayo ni rahisi kufanya au itakayokufikisha kwenye mafanikio ya haraka. Kila biashara ina ugumu wake, na huwezi kuujua ugumu huo mpaka pale utakapoingia kwenye biashara hiyo na kuifanya. Hivyo kigezo cha kuchagua biashara ya kufanya hakipaswi kuwa urahisi wa biashara, bali mapenzi na ile aina ya biashara unayofanya. Unapokuwa unapenda kile unachofanya, ugumu hauwezi kukuzuia kufanikiwa.

Kila biashara ina changamoto zake.
Sehemu kubwa ua ugumu wa biashara inatokana changamoto ambazo kila biashara inapitia. Katika nyakati hizi za changamoto ndipo biashara zinazofanikiwa na zinazoshindwa zinapotofautiana. Kila biashara inapitia changamoto mbalimbali. Changamoto hizi zinaweza kuwa kubwa au ndogo lakini zinakuwa na madhara kwenye biashara. Wafanyabiashara ambao wanafanikiwa, wanatarajia kukutana na changamoto hizi na wanajua wakizitatua wanapata mbinu bora zaidi za kibiashara. Wafanyabiashara wanaoshindwa hawategemei kukutana na changamoto, wanaona mambo yote yataenda kama walivyopangwa. Wanapokutana na changamoto wanakuwa hawajajiandaa na hivyo kukata tamaa haraka.

SOMA; Tabia Nne(4) zinazowatofautisha wafanyabiashara wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

Mabadiliko yanatokea kila siku, unahitaji kwenda na mabadiliko.
Moja ya vitu vinavyopelekea biashara nyingi kufa ni kuendeshwa kwa mazoea. Inafika wakati mfanyabiashara anafanya mambo kama kawaida, kama ambavyo amezoea kufanya wakati wote. Pale mfanyabiashara anapofanya kitu fulani kikampa matokeo mazuri, basi kila wakati anaendelea kutumia njia ile iliyompa matokeo mazuri. Njia hii inaweza kufanya vizuri kwa kipindi fulani, ila inahitaji kuboreshwa kadiri siku zinavyokwenda. Kuna mambo mengi ambayo yanabadilika kwenye biashara kila siku, unahitaji kuwa karibu na biashara yako, na kuifuatilia kwa umakini ili kuyaona mabadiliko haya mapema na kuchukua hatua.

Biashara inahitaji muda ili kukua na kufanikiwa.
Kitu kingine ambacho kinazuia biashara nyingi kukua ni ile haraka ambayo watu wanakuwa nayo kwenye matokeo ya biashara hiyo. Watu wanataka kuanzisha biashara leo halafu baada ya miezi michache wawe matajiri wakubwa kupitia biashara zao. Mawazo kama haya yanawapa hamasa mwanzoni, ila pale wanapokutana na changamoto na mafanikio kuchelewa wanakata tamaa na kuona biashara waliyochagua haiwafai. Tatizo halipo kwenye biashara, kwa sababu biashara yoyote ile kuna watu ambao wanaifanya na wanafanikiwa. Tatizo lipo kwenye ule mtazamo ambao mfanyabiashara anakuwa nao kwenye biashara yake. Anapofikiria ni sehemu ya kufanikiwa haraka, anajiweka kwenye nafasi ya kukata tamaa haraka.

SOMA; Wazo Bora Na Mtaji Pekee Havitoshi Kuifanya Biashara Ifanikiwe, Unahitaji Kitu Hiki Kimoja Muhimu Sana Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako.

Kila kitu kwenye maisha yetu kinaanzia kwenye mtazamo wetu, hivyo ndivyo ilivyo pia kwenye biashara na ujasiriamali. Wale wenye mtizamo sahihi wanaweza kuanzisha na kukuza biashara zao bila ya kujali wanapitia kipindi gani. Ila wale wenye mtizamo ambao siyo sahihi, wamekuwa wanashindwa kwenye biashara hata kama kila kitu kinakwenda vizuri. Anza kujijengea mtazamo sahihi kwenye biashara yako na utavuna matunda sahihi.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Barua Ya Wazi Kwa Wahitimu Wa Elimu Ya Juu Mwaka 2016, Ukweli Ambao Umekuwa Unafichwa Kwa Miaka 20 Iliyopita.

$
0
0
Umefika ule wakati ambapo mwaka wa elimu kwenye elimu ya juu Tanzania unakwisha. Na katika mwisho wa mwaka wa elimu, kuna wanafunzi ambao wanakuwa wamemaliza masomo yao, wamehitimu tayari kwa kwenda kulitumikia taifa. Huu ni wakati wa furaha kubwa kwa wahitimu, ambao wamekuwa kwenye mfumo huu wa elimu kwa kipindi kisichopungua miaka 16, katika kipindi chote hiki, walikuwa wanaiangalia siku hii ya kuhitimu.

Kwanza kabisa nitoe pongezi kubwa kwa wahitimu wote, iwe umehitimu ngazi ya cheti, stashahada au shahada, kwa sasa wewe umeshapata elimu ambayo unaweza kuitumia kwenye maisha yako na maisha yako yakawa bora sana. Kuwepo kwenye mfumo wa elimu kwa miaka hiyo mingi, wengine 16 wengine mpaka miaka 20 siyo kazi ndogo. Najua kuna wakati ulikutana na magumu ambayo yalitaka kukukatisha tamaa, lakini uliendelea kupambana mpaka leo umefikia kuhitimu.


Baada ya pongezi hizi naomba niende kwenye barua ya leo ambayo nimeiandaa maalumu kabisa kwa marafiki zangu ambao wamehitimu masomo yao ya elimu ya juu. Nimekua nikiandika makala hizi kila mwaka kuwashauri wahitimu, kusoma ya mwaka 2013 bonyeza hapa, 2014 bonyeza hapa, na 2015 bonyeza hapa na kupata mfululizo wa makala kwa wahitimu bonyeza hapa.

Kwenye makala ambazo nimekuwa naandika kila mwaka kwa wahitimu, naona kama nimeshagusia kila kitu. Hivyo kwenye makala ya leo nataka kukuambia kile ambacho hujawahi kuambiwa na wala hujawahi kusikia lakini ni ukweli. Kama ambavyo unajua, ukweli mara nyingi huwa unakuwa mchungu na hivyo watu hawapendi kuusikia. Ninachokwenda kukueleza leo ni ukweli mchungu sana, hivyo kama roho yako ni nyepesi ni vyema usiendelee kusoma. Kama upo tayari kuujua ukweli ili uufanyie kazi, basi karibu uendelee kusoma.

SOMA; KABLA HUJAANZA KUZUNGUKA NA BAHASHA SOMA HAPA.

Ukweli unaopaswa kuujua ni kwamba una miaka kumi ya mateso mbele yako, huu ni ukweli ambao umekuwa unafichwa kwa miaka 20 iliyopita. Kwa miaka 20 iliyopita, tangu unakua umekuwa unaimbiwa wimbo mmoja, soma ili ufaulu na uwe na maisha bora. Walikupa tu robo ya hadithi, hadithi nzima siyo rahisi kama hivyo, na sasa ndipo unapokwenda kuujua ukweli wenyewe kwenye maisha halisi.

Miaka kumi ijayo ndiyo miaka ambayo itatoa mwanga kwenye maisha yako yote utakayoishi hapa duniani. Miaka hii kumi itakuwa miaka migumu sana kwako, kitakuwa ndiyo kipindi cha kuamua ni kitu gani unataka kwenye maisha yako na kujenga misingi ya maisha yako. ni kwenye miaka hii kumi unaweza kujenga maisha bora au ukaharibu kabisa maisha yako.

Tukianza kuuchambua ukweli huu hatua kwa hatua, hapo ulipo sasa huna chochote zaidi ya kipande cha karatasi (cheti) ambacho kinaonesha masomo uliyosoma na ufaulu uliopata. Kipande hicho cha karatasi kilikuwa na matumizi mazuri sana siku za nyuma, ila kwa sasa matumizi yake yanafikia kuwa sifuri, kwa changamoto za ajira zilipo, unaweza kukosa popote pa kutumia cheti chako. Una cheti pekee, huna uzoefu wowote, huna ushuhuda wowote wa watu ambao wanaweza kuwaambia wengine kuhusu wewe na hakuna anayekujua wewe ni nani.

Kwa miaka hiyo uliyokuwa shuleni ulikuwa unakula tu, hukuwahi kuzalisha. Umekuwa unalipiwa ada na kupewa fedha ya matumizi, ulikuwa unatumia kwa raha, ukinunua kila ulichokuwa unataka, yote hii ni kula na inaelekea ukingoni wakati huu ambao unahitimu masomo yako. sasa dunia inaanza kukutaka siyo ule tu, bali pia uzalishe, na nafasi za wewe kuzalisha ni chache, hapo ndipo changamoto inakuwa kubwa zaidi.

Miaka kumi ijayo ni miaka ambayo unahitaji kuchagua ni kitu gani unataka kufanya na maisha yako, na kuweka juhudi zako zote katika kufanya kitu hicho. Miaka hii kumi itakuwa migumu, utakutana na changamoto nyingi na kukatishwa tamaa, lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba usikubali kukatishwa tamaa. Ukishajua ni kipi ambacho unataka kwenye maisha yako, weka juhudi ili kukifikia.

SOMA; Ushauri Muhimu Kwa VIJANA; Okoa Miaka Hii Kumi Ambayo Utaipoteza.

Kama ambavyo tayari utakuwa umeona mwenyewe, ajira ni changamoto, hivyo usipoteze muda kusubiri mpaka upate ajira, kaa chini na yapange maisha yako, chagua ni kipi unataka kufanya kwenye maisha yako, chagua ni jina gani unataka kuacha hapa duniani, na chagua ni kwa namna gani unataka kugusa maisha ya wengine, kisha anza kufanyia kazi ndoto yako mpya kwenye maisha.

Ninachotaka kukuambia ni kwamba chochote unachochagua kufanya, miaka kumi ijayo hakuna atakayejua kama hata upo, utakuwa ni wewe unateseka na kila unachofanya, lakini miaka hiyo kumi ikishapita, kila mtu atajua kuhusu wewe. Kila mtu atakuwa anakutafuta kwa sababu utakuwa umefanya makubwa sana, kama hutaishia njiani.

Kama utakuwa tayari kuteseka kwa miaka hii kumi ya maisha yako ya ujana, miaka mingi ijayo utaishi maisha bora sana kwa sababu utakuwa umejijengea misingi imara ya maisha yako. lakini kama utakwepa kuteseka sasa, utateseka maisha yako yote ya baadaye. Kwa sababu utafika wakati umri wa ujana umekwisha na huna tena nguvu za kuhangaika kujenga misingi imara.

SOMA; Ni Muda Kiasi Gani Unahitaji Ili Kufiki Mafanikio Makubwa? Soma Hapa Kujua.

Huu ndiyo wakati wa kuanzisha biashara bila hata ya kuwa na mtaji, huu ndiyo wakati wa kufanya kilimo, huu ndiyo wakati wa kuwatumikia wengine, kufanya maisha yao kuwa bora zaidi. Huu ni wakati mzuri kwako kuionesha dunia kwamba una kitu kikubwa kipo ndani yako, kitu hiki hakisemwi, badala yake kinaoneshwa, na unakionesha kwa kufanya. Hivyo weka maneno pembeni na fanya.

Mambo kumi muhimu ya kuzingatia kwenye miaka hii kumi na maisha yako yote kwa ujumla.
Kwenye miaka hii kumi ambayo unakwenda kujenga misingi ya makisha yako, na hata kwenye maisha yako yote, zingatia mambo haya kumi muhimu sana.

1. Kuwa mwaminifu na mwadilifu. Uadilifu ni kuwa na misingi yako ya maisha na kuisimamia. Uaminifu ni kutimiza kile ambacho umewaahidi wengine. Naweza kusema huu ndiyo mtaji pekee ambao kwa sasa unao kwenye maisha yako, usiupoteze.

2. Weka juhudi kubwa sana kwenye kazi, usikubali kuwa mvivu, usikubali kuwa mtu wa maneno, badala yake fanya kazi kwa juhudi kubwa na toa matokeo bora kwa wale wanaopokea unachofanya.

3. Uwekezaji pekee ulionao kwa sasa ni muda. Kuna vitu viwili tunavyoweza kuwekeza kwenye amisha yetu, fedha na muda. Kwa wahitimu walio wengi, fedha huna, hivyo kitu pekee unachoweza kuwekeza sasa ni muda. Wekeza muda wako vizuri kwenye mambo ambayo ni muhimu kwako na yatakulipa vizuri.

4. Ishi chini ya kipato chako, jijengee nidhamu ya fedha, usinunue vitu kwa mashindano. Haya ni mambo unayotakiwa kuyazingatia sana kwenye maisha yako ya kifedha, kwa sababu usipojijengea misingi mizuri sasa, utakuwa mtumwa wa fedha kwenye maisha yako yote. Epuka sana kitu kinaitwa madeni, hasa ambayo hayazalishi, unapoingia kwenye madeni mapema, ndivyo unavyouza uhuru wako kwa wengine.

5. Fanya maamuzi ambayo unaweza kuishi nayo. Pia jifunze kuwajibika kwa maamuzi uliyofanya. Huu ni wakati wa kuacha zile tabia za shuleni za kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Njia rahisi ya kushindwa kwenye maisha, ni kuiga wengine, kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.

6. Usilalamike, usilaumu, ni kupoteza muda. Kama kuna kitu hukipendi kibadili, kama huwezi kukibadili basi achana nacho. Kumbuka muda wako ndiyo rasilimali pekee uliyonayo kwa sasa, ilinde sana.

7. Zungukwa Na watu wazuri, watu wanaojua ni wapi wanaenda, watu wenye tabia zinazoendana na zako. Tabia zinaambukizwa, ukizungukwa na watu wenye tabia mbovu watakuambukiza tabia hizo mbovu. Wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka, mara zote hakikisha unazungukwa na watu sahihi.

8. Usimsikilize yeyote anayekuambia HUWEZI au HAIWEZEKANI, watu wote waliofanya makubwa kwenye dunia hii waliambiwa hawawezi au haiwezekani. Kama kuna kitu una ndoto nacho, hata kama ni cha kijinga kiasi gani, usikiue, bali kifanyie utafiti, uzuri wa dunia ya sasa ni kwamba taarifa zipo za kutosha hivyo utapata pa kuanzia. Mtu akikuambia huwezi au haiwezekani mpuuze mara moja, haijalishi ni mtu gani. Hata kama utajaribu na ukashindwa, hutabaki kama ulivyokuwa mwanzo, kuna mengi ambayo utajifunza.

9. Furahia ujana wako na tunza afya yako. ujana ni wakati ambao unakuwa na nguvu kubwa ya kuweza kufanya makubwa. pia unakuwa na uhuru wa kufanya mengi na kwenda mbali kwa sababu huna utegemezi mkubwa kwako. Utumie muda huu vizuri, lakini muhimu zaidi tunza afya yako, una miaka mingi mbele yako, usiiharibu kwa kuchagua maisha ya hovyo kama ya ulevi.

10. Jifunze kwenye kila siku ya maisha yako, soma vitabu kila siku, Soma AMKA MTANZANIA kila siku kwenye maisha yako, Soma KISIMA CHA MAARIFA kila siku kwenye maisha yako na karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA ambapo tutakuwa pamoja, bega kwa bega kwenye safari yako ya miaka 10 ya kujenga msingi bora wa maisha yako. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye neno KISIMA CHA MAARIFA, kwenda namba 0717396253 na utapewa maelekezo.

Nimalize kwa kusema kwamba unaweza kuitumia miaka hii kumi kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako, au unaweza kuitumia kwa kufanya yale ambayo kila mtu anafanya. Wewe ni mtu mzima sasa, maisha ni yako na maamuzi ni yako. Usiendeshe maisha ya kuiga kama ya shuleni, sasa unahitaji kufanya kile ambacho ni muhimu kwako, hata kama hakuna anayeamini kile unachofanya.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Namna Unavyoweza Kukuza Biashara Yako Hadi Kufikia Utajiri.

$
0
0
Watu wengi wamekuwa na mazoea ya kufanya biashara siku hadi siku kwa ajili ya kuingiza kipato kupitia biashara zao, lakini si kwa ajili ya kukuza biashara hizo kwa kiwango kikubwa hadi kufikia hatua ya kupata utajiri na kujitegemea kifedha. Wapo wengine ambao wamekuwa wakijaribu kujitumbukiza katika kusaka utajiri huo bila kujua chochote ni namna gani huo utajiri unatafutwa .

Watu hawa hawana kosa, hawakupewa siri ya kutengeneza pesa kupitia biashara zao na kujenga utajiri zaidi ya kukaa tu na kusubiri pengine faida kidogo wanayoipata. Ili kuwa tajiri huna budi kuwa na zana zinazotakiwa katika kuusaka huo utajiri.

Katika makala haya utajifunza kanuni za msingi ambazo unaweza kuzitumia katika kukuza biashara yako na kujijengea uwezo binafsi wa kutengeneza pesa na hatimaye kuwa tajiri. Kanuni hizo ni zipi?

Zifuatazo ni kanuni za msingi zitakazo kuongoza katika kukuza biashara yako na hadi kuufikia utajiri:-

1. Unapopata kiasi chochote cha pesa weka kidogo kama akiba.
Huna budi kutunza asilimia kumi ya kile unachochuma. Jilipe wewe kwanza, kwa faida ndogo unayoipata kupitia biashara zako. Weka kwenye kisanduku hela hiyo hata kama ni kidogo kwani ndiyo malipo yako wewe mtafutaji. Hiyo itakuwa akiba yako ya baadae. Utajikuta hela hiyo baada ya miaka mitatu au mitano itakuwa nyingi kiasi cha kwamba itakusaidia kuweza kufungua miradi mingine unayotaka kuanzisha.


 2. Dhibiti matumizi yako.
Hata uwe unaingiza faida nyingi vipi kama unashindwa kudhibiti matumizi yako biashara hiyo haitaweza kukua zaidi ya kiwango cha sasa. Maana ukiwa na matumizi ya ovyo itapelelekea wewe kupoteza pesa nyingi ambazo zilikuwa hazina sababu ya kupotea na pengine zingekusaidia kuwekeza katika eneo lingine.

Kitu cha kufanya ili uweze kudhibiti matumizi yako ni lazima kuwa na vitabu muhimu ambavyo vitakusaidia kuweka rekodi na hasa bajeti katika biashara yako kama Kitabu cha mapato na matumizi, Kitabu cha kuonesha ukwasi, na Kitabu cha bajeti. Kudhibiti matumizi ni njia mojawapo bora ya kukusaidia kukuza biashara yako ikiwa utaizingatia vizuri.

3. Jiwekee vyanzo vingine vya fedha.
Kama biashara yako imekuwa kubwa kabisa, huna haja ya kuendelea kufanya biashara hiyo peke yake. Tengeneza vyanzo vingine vya fedha, yaani kuwa na miradi mingi ambayo haikutegemei mpaka uwepo katika utendaji itakusaidia wewe kukupa muda wa kutosha kwa ajili ya kufikiri mipango mipya na udhibiti. Hata pale miradi yako inapokuwa inaenda kombo au vibaya inakuwa ni rahisi sana kutambua.

Vitega uchumi ambavyo utakuwa navyo vitakusaidia sana kukuza biashara zako mara dufu na zaidi kuongeza pato lako. Hii itakusaidia sana kuufikia utajiri unaoutafuta labda pengine nia hiyo uwe huna. Kwa hiyo, kukuza biashara na kuzitengenezea matawi ni suala la muhimu sana ambalo unatakiwa kulitambua kwamba linasaidia kukuza biashara zako kwa kasi kubwa.

4. Tunza mtaji wako.
Utakuwa hufanyi chochote cha maana kama utakuwa unapunguza mtaji wako. Kama umepata hasara katika biashara zako na unaona hasara hiyo inaweza kukata mtaji wako, basi hakikisha unakata gharama zisizo za lazima ili faida ndogo inayopatikana iweze kufidia hasara inayotaka kukata mtaji wako.

Usiwekeze kwa pupa fanya kwanza uchunguzi ukishaona biashara inalipa ndo ufanye au nenda kawaulize wataalamu wanaoijua hiyo biashara, vinginevyo bila kuwa makini katika hili utajikuta badala ya kukuza biashara yako ili ikuletee faida unaiua.

5. Uwe makini unapokopesha.
Katika bishara yako ili iweze kukua na kukutengenezea pesa ya kutosha huwa yapo mambo mengi sana unayotakiwa kuwa nayo makini. Mojawapo ni namna unavyokopesha Angalia unapokopesha usikopeshe wasiokopesheka. Kukopesha isiwe fimbo ya kujipigia mwenyewe kwenye biashara yako. Siyo lazima ukopeshe hata kama kuna ahadi na dalili nzuri za kulipwa kwa riba kubwa. Ukiwa makini katika hili pia utamudu kukuza biashara yako.

6. Ongeza uwezo wa kuendelea kupata pesa kupitia biashara yako.
Ni watu wachache wanaosoma baada ya kumaliza shule. Kama utaacha kuunoa ubongo wako kabisa lazima ujue utakwama. Lazima kuunoa ubongo wako kila wakati kwa kujisomea,kushiriki kwenye semina za biashara, na mambo kama hayo. Usiposoma ubongo wako utaota kutu na kamwe hutasonga mbele kwani itafika wakati utashindwa kukabiliana na changamoto hata ndogo tu zinazojitokeza kwenye biashara yako.

Uwezo wa kufanikiwa na kufika pale zaidi ya ulipo unao, unaweza ukatumia kanuni hizo kama msingi wa kujijengea namna unavyoweza kukuza biashara yako hadi kufikia utajiri.   

Kwa mbinu au kanuni zingine za biashara na mafanikio utaendelea kujifunza hapa hapa kwenye gazeti mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, kwani kumbuka elimu haina mwisho, nakutakia mafanikio mema na tukutane wiki ijayo kwa makala nyingine nzuri.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,




UCHAMBUZI WA KITABU; COACH YOURSELF TO WIN (Hatua Saba Za Kufikia Ufanisi Mkubwa Kwenye Kazi Na Maisha Yako Kwa Kuwa Kocha Wako Mwenyewe)

$
0
0
Kuna siri moja ambayo wachezaji wa michezo mbalimbali wanaijua na kuitumia ambayo wengine hawaijui au wanaijua lakini hawaitumii. Siri hii ni kuwa na mtu wa kukufuatilia kwenye kile unachofanya, na mtu huyo siyo tu anakufuatilia juu juu bali anakufuatilia kwa karibu, kukuonesha hatua muhimu ya kuchukua na kukuonesha ni wapi unapokosea. Mtu huyu anaitwa KOCHA. Karibu kila mchezo mchezaji anakuwa na KOCHA, hata michezo ya mchezaji mmoja mmoja kama masumbwi, watu hawa wanahitaji kuwa na KOCHA.

KOCHA siyo tu mwalimu kwamba anamfundisha mchezaji mbinu za ushindi, bali anamsimamia mpaka aweze kufikia kile anachotaka.
Kila mtu kwenye maisha yake anahitaji kuwa na KOCHA, kwa sababu siyo rahisi kujisimamia mwenyewe. Unaweza kuweka malengo na mipango mizuri lakini ukashindwa kuifikia kutokana na kukosa mtu wa kukusimamia kwa karibu. Unahitaji kuwa na KOCHA kwenye kazi yako, biashara yako na hata maisha yako kwa ujumla. Kocha atakusukuma uchukue hatua hata pale unapokaribia kukata tamaa.


Lakini pia siyo watu wote wanaweza kumudu gharama za kuajiri mtu awe kocha kwenye maisha yao, au hata kama wanamudu huenda hawana muda wa kukutana na kocha. Kuna habari njema kwa watu hawa, kwamba wanaweza kuwa MAKOCHA WAO WENYEWE. Wao wenyewe wanaweza kujisimamia mpaka wakaweza kufikia malengo na mipango yao kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla.
Mwandishi Howard Guttman anatupa hatua saba za kuweza kuongeza ufanisi wetu kwenye kazi na maisha kwa ujumla. Karibu tujifunze mbinu hizi sana kwenye uchambuzi wa kitabu hiki COACH YOURSELF TO WIN.
Karibu tujifunze kwa pamoja.

MAMBO MATATU MUHIMU UNAYOHITAJI KABLA HUJAWA KOCHA WAKO MWENYEWE.

Kabla hatujaingia kwenye hatua saba za kuongeza ufanisi wako kwa kuwa kocha wako mwenyewe, kuna mambo matatu muhimu unahitaji kuwa nayo ili uweze kuwa kocha wako mwenyewe.
MOJA; Unahitaji kuwa na taarifa sahihi za pale ulipo sasa na kule unakotaka kufika. Bila ya kujua ulipo na unapokwenda hutaweza kutoka hapo na hata ukitoka hutajua ni njia hani uchukue.
PILI; Unahitaji kuwa MWONGOZO, hapa unahitaji mtu au watu ambao watakuwa wanakuangalia na kukufatilia.
TATU; Unahitaji kuwa tayari kwenda nje ya mazoea yako, unahitaji kuwa tayari kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya, uchukue hatua ambazo ni hatari na ambazo huna uhakika nazo.

SOMA; KITABU CHA MAY; Biashara Ndani Ya Ajira; Jinsi Ya Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa.

Zifuatazo ni hatua saba za kuongeza ufanisi wako kwa kuwa kocha wako mwenyewe;


HATUA YA KWANZA; JE UNAWEZA KUWA KOCHA WAKO MWENYEWE.
Kabla hujaamua kuwa kocha wako mwenyewe ni lazima ujiulize kama unaweza kuwa kocha wako mwenyewe. Ili kujua kama unaweza kuwa kocha wako mwenyewe.

1. Ili uweze kuwa kocha wako mwenyewe unahitaji vitu vitatu; unahitaji kuwa na uwezo wa kubadilika, uwe tayari kubadilika na uwe na nia ya kubadilika. Unahitaji kujua kwamba zoezi la kubadilika linahitaji muda, siyo kitu cha haraka hivyo unahitaji kujipanga ili kufikia mabadiliko ya kweli.

2. Ili kuwa kocha wako mwenyewe unahitaji kubadili tabia zako na kufanya mabadiliko ya kudumu. Watu wengi hubadili tabia zao lakini baada ya muda mfupi hujikuta wamerudi tena kwenye tabia hizo. Hii ni kwa sababu wanakuwa hawajafanya mabadiliko ya kudumu kwenye tabia zao, bali wanakuwa wamebadili mbinu zao.

SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

3. Ili uweze kuwa kocha wako mwenyewe, lazima uwe na maelezo sahihi kwa tabia zako. Kwa ile tabia uliyonayo, usijichukulie wewe kama ndiyo ile tabia, badala yake jichukulie wewe ni wewe na tabia ni tabia, kwa njia hii inakuwa rahisi kubadilika. Kwa mfano usijiite mlevi, bali jiite mtu ambaye anakunywa pombe mara nyingi au kupita kiasi. Ukijiita mlevi maana yake umejipa utambulisho ambao utaendelea kuwa nao. Ila ukijiita mtu anayekunywa pombe mara nyingi au kwa wingi, unaweza kuanza kupunguza kiasi unachokunywa na hatimaye kuondokana kabisa na tabia ya kutumia pombe.

4. Tatizo lolote unalokutana nalo kwenye maisha yako, kuna namna ambavyo umechangia tatizo hilo, hivyo katika kuwa kocha wako mwenyewe, jiulize mchango wako ni upi kwenye kila unachopitia, hii inakupa nafasi ya kujua kipi hasa cha kubadili. Kama utawalaumu wengine pekee, hutaweza kutoka hapo ulipo sasa.

HATUA YA PILI; PANGA NIA YAKO (KUSUDI LAKO).
Ili kuwa kocha wako mwenyewe kwenye kubadili tabia zako, ni lazima uwe na NIA au KUSUDI kwa nini unataka kufanya mabadiliko kwenye maisha yako. nia ndiyo itakayokusukuma kuchukua hatua na kukufanya uendelee kuweka juhudi hata pale mambo yanapokuwa magumu.

5. Weka nia yako kwa nini unahitaji kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, nia hii iwe inakuvutia kuchukua hatua. Kwa nini unataka kupunguza uzito? Kwa nini unataka kuacha kuvuta sigara? Kwa nini unataka kuongeza ufanisi wako kwenye kazi? Fikiria jinsi utakavyonufaika na mabadiliko utakayoleta kwenye maisha yako.

6. Ni hadithi gani ulizonazo sasa kuhusu maisha yako na kile unachofanya. Kila mmoja wetu ana hadithi ya maisha yake, kwa vile anavyofikiri yapo na vile wengine wanavyomchukulia. Huwa tunaishi kadiri ya hadithi za maisha yetu. Jua ni hadithi gani unayoishi sasa na jinsi inavyokuzuia kubadilika.

7. Tengeneza hadithi mpya ya maisha yako. Hapa tengeneza hadithi itakayoendana na mabadiliko unayoleta kwenye maisha yako. Tengeneza hadithi ambayo itaendana na mabadiliko unayotaka kwenye maisha yako, itumie hadithi hiyo katika kukupa hamasa ya kuweka juhudi zaidi kwenye maisha yako.

HATUA YA TATU; CHAGUA WATU WA KUKUONGOZA NA KUKUSAIDIA.
Unapokuwa kocha wako mwenyewe, hatari kubwa ni kurudi nyuma. Pale unapojiwekea malengo na mipango yako mwenyewe, unapoanza kuifanyia kazi na ukakutana na changamoto ni rahisi kukata tamaa. Lakini unapokuwa umewaambia wengine kuhusu mipango yako, watakuwa wanakuuliza umefikia wapi. Hivyo hitaji kubwa la kuwa kocha wako mwenyewe, ni kuwaambia watu unaowaamini yale malengo na mipango yako.

8. Chagua ni watu gani ambao watakuwa kwenye timu yako ya kukufuatilia kwenye utekelezaji wa malengo na mipango yako. Ni lazima uwe na vigezo vya watu unaowaambia kuhusu nia yako. Siyo kila mtu anafaa kuambiwa, wengine wanaweza kukukatisha tamaa. Baadhi ya vigezo vya kuzingatia kwenye kuchagua watu wa kukusimamia ni hivi;
Wawe ni watu unaowaamini na wanakuamini wewe pia.
Wawe ni watu ambao wanajali kuhusu mafanikio ya maisha yako.
Wawe ni watu ambao wana muda wa kukufuatilia.
Wawe ni watu ambao wapo tayari kukuambia ukweli bila ya kuona aibu.

9. Jadili NIA yako ya kubadilika au kufikia malengo yako na wale watu ambao unataka wakufuatilia. Wajulishe ni wapi ambapo unataka kufika, wape mtiririko mzima na wape maeneo ambayo itakuwa rahisi kwao kukufuatilia wewe.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.

10. Wakati mwingine unaweza kujiunga na kikundi cha watu ambao wanafanyia kazi mabadiliko kama ambayo unayafanyia kazi wewe. Kwa mfano kuna vikundi vya watu wanaotaka kuacha kutumia pombe, au wanaotaka kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Angalia ni tabia gani unataka kubadili, au malengo gani unataka kufikia kisha angalia kama kuna kikundi cha watu wanaofanya kama unavyotaka kufanya wewe. Faida ya kuwa kwenye vikundi vya aina hii ni kwamba unajifunza moja kwa moja kutoka kwa wengine waliofanikiwa kufanya unachotaka kufanya.

HATUA YA NNE; POKEA MREJESHO.
Ukishakuwa na kikundi cha watu ambao wanakufuatilia kwenye malengo na mipango yako, unahitaji kuwa tayari kupokea mrejesho kutoka kwao. Mrejesho huu ndiyo utakaokupa mwelekeo kama upo kwenye njia sahihi au la.

11. Jifunze kupokea mrejesho hata kama siyo mzuri. Moja ya tabia zetu binadamu ni kupenda kujitetea, hasa pale watu wanapotuambia madhaifu yetu, huwa tunakazana kutoa sababu za kuonesha kwamba siyo madhaifu yetu. Unahitaji kuwa tayari kupokea mrejesho hata kama ni hasi na kuweza kuutumia kuboresha zaidi kile unachofanya.

12. Kuwa msikilizaji zaidi kuliko mwongeaji, unahitaji kusikiliza siyo tu kwa masikio, bali kwa mwili wako wote. Watu wanapoongea wanatoa ishara nyingi unazoweza kujifunza zaidi kutoka kwao. Sikiliza kwa makini.

13. Wafanye watu wakueleze zaidi kuhusiana na wewe na mwisho washukuru kwa kukupa mrejesho huo. Wahoji zaidi ili waweze kujieleza kwa jinsi wanavyokuona wao. Mwishoni washukuru ili waendelee kukupa mrejesho zaidi. Usikasirike wala kuwachukia, badala yake pokea kile wanachokuambua.

HATUA YA TANO; CHAKATA NA JIBU MREJESHO.
Ukishapewa mrejesho na wengine, kuhusu hatua unazochukua na malengo ambayo unayo, unahitaji kuchakata mrejesho huo na kisha kujibu yale ambayo ni muhimu.

14. Jiulize kuhusu mrejesho uliopewa na wengine, je unaendana na vile unavyojiona ndani yako? jiulize je ni kwa namna gani umekuwa unafanya mpaka watu wanakuona wanavyokuona. Pia jiulize ni mambo gani unahitaji kubadili ili uweze kuwa kwenye uelekeo sahihi.

15. Waahidi watu ni kipi utakachobadili ili uweze kufika kule unakotaka kufika. Kwa njia hii inakuwa rahisi watu kuona kama kweli una dhamira ya dhati ya kubadilika au kufikia malengo yako.

HATUA YA SITA; TENGENEZA MPANGO KAZI.
Umeshakuwa na nia ya kubadilika au kufikia malengo yako, umeshachagua watu wa kukufuatilia na umeshapata maoni yao, sasa kinachofuata ni kuwa na mpango kazi. Hapa unahitaji mpango ambao utaufanyia kazi ili uweze kufikia malengo yako au kubadili tabia zako.

16. Tengeneza mpango wa maendeleo binafsi (PERSONAL DEVELOPMENT PLAN). Mpango huu unakuwa na hatua utakazochukua ili uweze kufikia NIA yako ya mabadiliko, unakuwa na muda unaohitaji na kipi utafanya kwenye muda wako. Pia unakuwa na changamoto unazoweza kukutana nazo na zikakurudisha nyuma na njia ya kuzitatua.

17. Kutengeneza mpango siyo kujaribu kuitabiri kesho yako au kuitengeneza bali ni kujaribu kuiumba kesho yako. Hakuna awezaye kutabiri nini kitatokea kesho, lakini wote tunajua kuna mambo mengi sana yanayoweza kutokea kesho. Je katika hayo mengi yanayoweza kutokea yapi ambayo ni muhimu kwako kufanyia kazi? Hii ndiyo kazi ya kuweka mipango, kuchagua kipi kitakuwa kipaumbele kwako.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha YOU CAN WIN (UNAWEZA KUSHINDA)

18. Kupanga siyo rahisi, inahitaji ufikiri kwa kina na uwe na ubunifu mkubwa. Na pia mara nyingi mipango yako haitakwenda kama ulivyopanga. Ni muhimu kujua hili ili uwe tayari kuchukua hatua. Kwa vyovyote vile unahitaji kuwa na mpango, kwa sababu KUHINDWA KUPANGA NI KUPANGA KUSHINDWA.

HATUA YA SABA; FANYIA KAZI NA JITATHMINI.
Ukishakuwa na mipango kilichobaki ni utekelezaji wa mipango hiyo. Na siyo tu kutekeleza bali kuendelea kujitathimini ili kuona kama unaendelea kuwa kwenye njia sahihi.

19. Chagua hatua utakazochukua kila siku ili kuweza kubadili maisha yako au kufikia malengo yako. na njia nzuri ya kufanya hivi ni kugawa mambo yako kwenye hatua ndogo ndogo unazoweza kupiga kila siku. Hata kama mabadiliko unayotaka kufanya ni makubwa, usiangalie ukubwa na ukakutisha, badala yake angalia ni hatua hani unayoweza kuchukua kwenye siku yako ili kufikia mabadiliko unayotaka. Kama lengo lako ni kufanya mazoezi basi unaweza kuanza kwa kukimbia hatua chache kila siku, au kupiga pushup kumi kila siku. lengo ni kuanza na kuendele akufanya.

20. Hatari kubwa inayowapata wengi ni kurudi kule walikotoka baada ya kufanikiwa. Watu wengi wanaopanga kupunguza uzito huwa wanafanikiwa kuupunguza lakini baadaye uzito huo unarudi tena maradufu. Au watu wanafanikiwa kukuza baishara zao lakini baadaye zinaporomoka. Hii inatokana na kujisahau na kuanza kurudia zile tabia za zamani ambazo walishaziacha. Unahitaji kujitathmini kila siku kama hatua unazochukua zinaendana na mabadiliko unayotaka au malengo unayoyaendea.
Sasa umeshapata hatua zote saba za kuwa kocha wako mwenyewe, zifanyie kazi hatua hizi na maisha yako yatakuwa bora sana.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Mambo Mawili (2) Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Msamaha Wa Kweli.

$
0
0
Habari Mpendwa Rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vizuri na karibu tuanze pamoja na tumalize pamoja ambapo leo tutajifunza mambo mawili muhimu na ya msingi ya kuzingatia katika msamaha wa kweli.

Msamaha ni kuondoa uchungu ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe na kwa makusudi yako mwenyewe. Kusamehe ni kumfutia mtu deni. Kwa hiyo kama hujasamehe unadaiwa deni hivyo yakupasa usamehe kwa faida yako mwenyewe. Kusamehe ni amri na ni agizo la Mungu. Unaposamehe unakua unarudisha uhusiano uliopotea kati ya mkosa na mkosewa. Unaposamehe unakua unatoa uchungu ulioumbika moyoni mwa mtu na kuwa huru kimwili, kiakili na kiroho. Kutosamehe ni kubeba mzigo wa hiari ndani ya moyo wako. Samehe ili uweze kusamehewa.


Sio mara yako ya kwanza kusikia dhana ya kusamehe saba mara sabini mpaka leo hii. Huenda ulikuwa hujui nini maana ya kusamehe saba mara sabini. Kusamehe saba mara sabini maana yake kila siku hapa duniani unatakiwa kusamehe. Kwani ukizidisha saba mara sabini utapata mia nne na tisini hivyo basi, ndani ya mwaka kuna siku 365 inakupasa kusamehe hata zaidi ya mara moja ndio maana ya saba mara sabini ambayo unapata siku 490. Kwa hiyo msamaha hauna mwisho kila siku wewe ni kusamehe tu. Samehe kwa faida yako mwenyewe. Samehe hata kwa kulia machozi lia kabisa uondoe uchungu ulioumbika ndani ya moyo badala ya kubeba mzigo wa kutosamehe.

SOMA; Mambo Matatu Ya Kuzingatia Katika Msamaha.

Leo tutajifunza kitu kipya kabisa katika somo la msamaha. Karibu ndugu msomaji, na yafuatayo ni mambo mawili (2) ya msingi ya kuzingatia katika msamaha wa kweli.

1. Kitu Cha Kwanza Ni Kuchunguza Kiini Cha Kosa/Tatizo. Kabla hujafanya msamaha wowote chunguza kwanza kiini cha kosa au tatizo ni nini? Usifanye msamaha kabla hujajua kiini cha kosa au tatizo. Katika maisha yako, huenda umepitia mapito mengi na kujeruhiwa sana lakini huna budi kusamehe. Usiposamehe maana yake unaendelea kubaki na uchungu ndani ya moyo wako. Unachunguza kiini cha kosa ni nini? Pengine mtu anakuchukia tu bila sababu yoyote, anakuwa na wivu tu, ukifanya kitu kizuri hapongezi, mwingine tamaa inamuongoza nk.

Mfano halisi, kuna watu wanapatwa na uchungu kwa wengine kufanikiwa, mwenzako akipandishwa cheo kazini unakasirika unanuna kabisa sasa ukichunguza kiini cha kosa na kugundua mtu anakuchukia kwa sababu ya wewe kupandishwa cheo, kuonywa, kuambiwa ukweli na nk. ‘’ignore’’ puuzia na samehe kwa faida yako ukiona huna kosa na msalimie hata kama haitiki. Na ukichunguza ukiona huna kosa basi wewe msamehe na ukiona wewe ndio unakosa jishushe na rudi katika msamaha wa kweli.

Inapotokea makazini upo na wenzako halafu wanakuambia kuna dili la pesa hivyo unatakiwa ushiriki katika rushwa na wewe hutaki sasa na wewe ukakataa kushiriki je wale wafanyakazi wenzako watakua na mahusiano mazuri tena na wewe? Hapana hawawezi kuwa na mahusiano mazuri na wewe tena watakuita majina ya bandia kama vile mwacheni huyo mlokole na maneno mengi yanayohusiana na hayo. Sasa katika mfano huu ukichunguza kiini cha kosa au tatizo utagundua nani ni mkosa au mkosewa kama ukiona huna kosa baada ya kuchunguza kiini cha kosa katika jambo hilo puuza na endelea na maisha yako na kama wewe ndio mkosa omba msamaha. Hivyo basi, mpaka sasa ndugu msomaji, umeshapata picha nzima ya kuchunguza kiini cha kosa. Kwa hiyo, kabla hujafanya msamaha chunguza kwanza kiini cha kosa ili kujua nani ni mkosa/msababishi wa kosa na nani ni mkosewa.

MUHIMU KUSOMA; Sababu Kumi Na Moja(11) Kwa Nini Usiombe Ruhusa Na Uombe Msamaha.

2. Kitu cha pili ni kutambua kosa. Ili uweze kumsamehe mwenzako na kufanya msamaha wa kweli ni lazima atambue kosa. Hivyo basi, usifanye msamaha kama mkosaji hajatambua kosa lake. Mfano ‘mtu anakwambia ni samehe basi, kama nimekukosea’ sasa kama hujamkosea unaomba msamaha wa nini? Ndio maana tunasema ni lazima mkosa atambue kosa lake kabla hajafanya msamaha wa kweli. Mfano mwingine mtoto anaangalia tv akaambiwa zima tv huu ni muda wa kusoma basi mtoto anaanza kulia, kujitupatupa chini, kujigaragaza na kubamiza milango na kuonekana kama vile amekosewa. Sasa mzazi mwingine badala ya kumuacha mtoto atambue kosa lake mzazi anamtetea na hatimaye mtoto anaona kama hana kosa. Kama mzazi usitishike mtoto akilia mwache alie na baadaye atatulia na kutambua kosa lake.

USIKOSE HII; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2

Hivyo kuna watu wengi wanafanya msamaha pasipo kuchunguza kiini cha kosa, kutotambua kosa. Katika kufanya msamaha pitia hizo hatua hapo juu. Unatakiwa kushinda ubaya kwa wema. Usilipe kisasi wewe samehe kutoka moyoni usipambane na mtu, samehe uwe na amani, furaha na afya njema. Kumbuka uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Wasamehe watesi wako hata kwa machozi na achilia fundo lililo moyoni. Hata ukikumbuka ulipotoka na ulipo na unaona machozi yanatoka lia tu na uchungu utoke moyoni. Msamaha wa uongo unaongozwa na hisia na msamaha wa kweli unatoka moyoni na hauna masharti.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Usimamizi bora wa biashara kwa wale ambao bado wameajiriwa.

$
0
0
Kutokana na kipato cha mshahara wa kwenye ajira kutokutosheleza mahitaji, waajiriwa wengi wamekuwa wakianzisha biashara zao za pembeni. Hii pia imekuwa ni njia ya kujiandaa kutoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri wao wenyewe ili kuwa na uhuru mkubwa wa maisha yao. Ni kitu kizuri sana kwa waajiriwa kuweza kuendesha biashara huku bado wameajiriwa.

Watu wengi ambao wanaendesha biashara wakiwa bado wameajiriwa huwa wanakutana na changamoto kubwa sana kwenye usimamizi wa biashara zao. Hii hupelekea biashara hizo kushindwa kukua na kupelekea kufa kabisa kwa biashara hizo. Hili limekuwa linawaumiza watu wengi na kuwakatisha tamaa, wengine wasithubutu tena kuingia kwenye biashara.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Leo kupitia makala hii ya KONA YA MJASIRIAMALI, tutakwenda kujifunza namna bora ya kusimamia biashara yako kama bado umeajiriwa, ili uweze kukuza biashara hiyo na baadaye kuweza kuondoka kwenye ajira na kusimamia biashara yako moja kwa moja ili kuwa na uhuru kwenye maisha yako.

Wafanyabiashara wengi ambao bado ni waajiriwa wana changamoto moja kubwa sana ambayo ni muda. Wengi wamekuwa wakibanwa muda kwenye ajira zao na hivyo kukosa muda wa kuzifuatilia biashara zao kwa karibu. Pia watu hawa wamekuwa na changamoto ya nguvu, wengi wanatoka kwenye kazi zao wakiwa wamechoka sana na hivyo kushindwa kufanya mambo makubwa kwenye biashara zao. Hizi ni changamoto ambazo kila mfanyabiashara ambaye bado yupo kwenye ajira anahitaji kuzifanyia kazi ili aweze kuisimamia biashara yake vizuri.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kujua Biashara Inayolipa Eneo Ulipo.

Wafanyabiashara wengi ambao bado ni waajiriwa, wamekuwa wakiwaajiri watu wa kuwasaidia kuendesha biashara zao, lakini kutokana na kukosa muda wa kufuatilia biashara hizo kwa karibu, wanawaachia watu hao kila kitu kwenye biashara. Watu hawa wanafanya kila maamuzi ya biashara kama wanavyotaka wao wenyewe. Katika maamuzi haya yapo ambayo ni mazuri na mengi ambayo siyo mazuri kwenye biashara yako. Wakati mwingine uhuru wa aina hii umekuwa unawashawishi wasaidizi wengi kwenye biashara kufanya matumizi mabaya ya rasilimali za biashara na hata kuiba na kuondoka kwenye biashara hiyo. Hali kama hizi zimekuwa zinapelekea biashara nyingi kushindwa kukua na hata kufa kabisa.

Kitu kimoja muhimu sana ambacho kila mtu aliyepo kwenye biashara anapaswa kukijua ni kwamba kama unamiliki biashara, basi utajitajika kufanya mambo mengi wewe mwenyewe, kama unataka biashara hiyo ifanikiwe. Kuna vitu vingi ambavyo hakuna yeyote anayeweza kukufanyia kwenye biashara yako, bali wewe mwenyewe. Kuendesha biashara siyo kuwapangia watu majukumu na wewe kupumzika au kuwasimamia, badala yake ni wewe kufanya na wale wanaokusaidia huku ukiwaonesha ni namna gani ya kufanya, mara zote.

SOMA; Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

Wafanyabiashara ambao bado wameajiriwa wamekuwa wakilikwepa hili, wanatafuta watu wa kuwaajiri na kisha wanawaachia biashara zao. Kutokana na kukosa muda wanakuwa mbali na biashara zao wanakuja kustuka pale wanapoona biashara inakufa badala ya kukua.

Lakini changamoto ni nguvu na muda, je tunawezaje kupambana na changamoto hizi ili tuweze kusimamia biashara zetu kwa ukaribu?

Kwanza kabisa pangilia muda wako vizuri. Muda ulionao unatosha sana kama utaupangilia vizuri, unaweza usiwe na muda mwingi lakini huwezi kukosa walau masaa mawili au hata moja la kupita kwenye biashara yako kila siku ili kuweza kujua inaendeleaje na kujionea kwa macho yako mwenyewe. Ni muhimu uwe kwenye eneo la biashara kabisa, ili ujionee kila kinachoendelea, usikubali taarifa unazopewa kwa njia ya simu, nyingi siyo taarifa sahihi. Siku ambazo huendi kazini, kama mwisho wa wiki au siku za sikukuu, kaa kwenye biashara yako muda wote. Hata kama biashara ni ndogo, kuwepo pale na ona jinsi ambavyo wasaidizi wako wanaendesha biashara hiyo, ona jinsi wateja wanavyohudumiwa, ona jinsi maamuzi yanavyofanywa na kama huridhishwi na baadhi ya mambo toa maelekezo kipi cha kufanywa.

Pia unaweza kutumia njia za kisasa za kusimamia biashara yako ambapo unaweza kufuatilia kwa karibu popote ulipo. Zipo programu za kuweka kwenye biashara yako na wasaidizi wako wakawa wanaweka taarifa za biashara na wewe kuweza kuziona popote pale ulipo. Japokuwa programu za aina hii haziondoi umuhimu wa wewe kuwepo kwenye biashara, bado unahitaji kupata muda wa kuwa kwenye biashara yako.

SOMA; Sababu Tano Kwa Nini Biashara Nyingi Zinazoendeshwa Na Waajiriwa Huwa Zinakufa.

Iweke biashara yako karibu na kazini kwako au nyumbani kwako. Kama biashara ipo mbali na kazini na nyumbani, utashindwa kuifuatilia kwa ukaribu, kwa sababu unapokuwa umechoka ni vigumu kwenda mbali kuangalia biashara. Lakini biashara inapokuwa karibu na kazini kwako ni rahisi kupitia pale unapotoka kazini. Na kama ipo karibu na nyumbani ni rahisi kupitia pale unapoelekea nyumbani.

Muhimu zaidi ni kujitoa hasa siku za mwanzo za biashara yako, ni lazima uweze kwenda hatua ya ziada, ni muhimu ujitume hata kama umechoka. Jua ya kwamba unatengeneza uhuru wa maisha yako na weka juhudi kubwa ili kupata uhuru huo. Nakutakia kila la kheri katika ukuaji wa biashara yako.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

USHAURI; Hatua Tano(5) Za Kuanzisha Na Kukuza Biashara Kwa Wale Ambao Hawana Pa Kuanzia Kabisa.

$
0
0

Habari rafiki?
Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, hivyo ujanja siyo kuzikimbia changamoto, bali kukabiliana nazo na kuzishinda ili kuweza kusonga mbele zaidi. Hii ndiyo sababu kupitia AMKA MTANZANIA tuna kipengele cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia malengo makubwa tunayojiwekea kwenye maisha yetu.

Karibu kwenye makala yetu ya leo ambapo tunakwenda kupeana ushauri juu ya changamoto zinazowazuia watu kuanza biashara. Kwa zama hizi tunazoishi sasa, biashara ni kitu muhimu mno, iwe umeajiriwa au hujaajiriwa, unahitaji kuanzisha na kukuza biashara yako ili kuweza kujitengenezea uhuru wa kifedha. Na siyo lazima uache kazi yako ndiyo uanzishe biashara, kama ambavyo nimeeleza kwenye kitabu hiki; BIASHARA NDANI YA AJIRA (bonyeza kukipata) unaweza kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Imekuwa ndoto ya wengi kuanza biashara, lakini maswali ya awali kabisa ni nifanye biashara gani? Nianzie wapi? Nipate wapi mtaji? Nipate wapi soko la uhakika? Sasa leo kwenye makala hii ya ushauri wa changamoto, tunakwenda kuangalia pa kuanzia, namna ya kupata soko, mtaji na hata jinsi ya kuikuza biashara yako. kabla hatujaingia kwenye ushauri wenyewe, hebu tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusu hili;

Mimi ni mpambaji, nadarizi ila nasumbuliwa na mtaji na soko na ni mfugaji mzuri wa kuku wa mayai ila kwa sasa nipo nipo tu sijui hata pakuanzia naomba ushauri wenu na msaada wenu. Amina S. A

Hiyo ndiyo changamoto kubwa inayomsumbua msomaji mwenzetu, na nina hakika wapo wengi ambao wana changamoto kama hiyo. Swali ni je unatokaje hapo ulipo? Moja kwa moja tunakwenda kuangalia hatua unazoweza kuchukua, tukitumia mfano wa msomaji mwenzetu na mingine kwenye hali kama hizo.

HATUA YA KWANZA; Anzia hapo ulipo, hiyo ndiyo biashara uliyonayo tayari.

Kitu kimoja ambacho nataka kukuambia mwanzo kabisa ni kwamba hapo ulipo tayari una biashara, ni wewe kuijua na kuanza kuifanyia kazi. Je kuna kitu ambacho unapenda kufanya? Au kuna kitu ambacho una ujuzi nacho? Je kuna uzoefu wowote umepitia kwenye maisha yako ambao wengine hawajaupitia? Je kuna elimu uliyopata ambayo wengine hawana au wanaihitaji? Au je umeajiriwa au kuna watu walishakulipa kutokana na kitu ulichokifanya? Kama umejibu ndiyo kwenye swali lolote kati ya hayo hapo juu, basi tayari biashara unayo.

Kwa mfano wa msomaji mwenzetu hapo juu, ana ujuzi wa kupamba na wa kudarizi. Tayari ana biashara, tena nzuri sana ya kupamba na kudarizi. Kwa mwingine inawezekana ni ujuzi wa afya, au kilimo. Mwingine anaweza kuwa anapenda kuandika, mwingine kuimba. Mwingine anapenda kufuatilia michezo, au kutumia mitandao ya kijamii. Vyote hivi unaweza kuvigeuza na kuwa biashara.

SOMA; USHAURI; Kuanza Biashara Kwa Mtaji Kidogo, Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuikuza.

HATUA YA PILI; Angalia ni nani mwenye uhitaji wa kile unachofanya au unachotaka kufanya.

Ukishajua kile ambacho unacho, ambacho ndiyo unakigeuza kuwa biashara yako, angalia ni watu gani watahitaji huduma au bidhaa yako. Angalia ni watu gani ambao wana shida au mahitaji ambayo wewe unaweza kuyatimiza kupitia kile ambacho unakifanya.

Kwa msomaji wetu aliyetuandikia, wateja wake ni watu wanaofanya sherehe mbalimbali kama harusi au mahafali. Wateja wake pia ni watu wanaopenda mavazi yaliyodariziwa.
Kama vitu unavyofanya wewe ni vingine, angalia watu gani wanaweza kunufaika navyo. 

Kama unapenda kufuatilia michezo, angalia ni watu gani wanaweza kunufaika kupitia yale unayofuatilia leo. kama unapenda kutumia mitandao ya kijamii, angalia ni watu gani wanaweza kunufaika kupitia wewe kuwa kwenye mitandao ya kijamii. Kama unapenda kuandika, angalia ni watu gani wanaweza kunufaika na kile unachoandika. Kila unachofanya, wapo watu ambao wanakitafuta kwa hamu, ni jukumu lako kuwajua na kuwafikishia kile unachofanya.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuishinda Hofu Ya Kupata Hasara Kwenye Biashara.

HATUA YA TATU; Wape watu kile unachotoa bila ya malipo.

Hapa ninachukulia kwamba unaanzia chini kabisa, ambayo ni sehemu nzuri sana kuanzia kwa sababu sasa hivi huna namna ambavyo unatengeneza kipato. Hivyo unaweza kutoa huduma zako kwa wengine bila hata ya kulipwa. Kama unachotoa ni bidhaa basi anza kutoa kwa bei ya chini sana, ambapo hupati faida yoyote. Lengo ni watu wakujue wewe ni nani kwanza, hapo ulipo sasa hakuna anayekujua na hata ukiwaambia kuna kikubwa unaweza kufanya hakuna anayeweza kukuamini, hivyo unahitaji kujijengea uaminifu.

Kwa msomaji mwenzetu aliyetuandikia hapa, anaweza kuanza kutoa huduma zake za upambaji bure kabisa. Angalia sherehe mbalimbali zinazofanyika pale unapoishi na omba kujitolea kupamba bure kabisa, wao wanunue tu mapambo. Au kama hizi hakuna, tafuta watu wanaofanya upambaji, ambao tayari wameshajijengea majina, waombe kujitolea kuwasaidia kazi bure kabisa, wasikulipe chochote. Lengo hapa ni wewe ujifunze, pamoja na kuwaonesha wengine kile ambacho unacho. Pia kwenye kudarizi hivyo hivyo, anza kudarizi vitu vya nyumbani kwako/kwenu na wasaidie watu kudarizi. Kadiri watu wanavyoona kazi zako ndivyo wanavyotaka kufanya kazi na wewe.

Kwa shughuli nyingine kama uandishi, tafuta njia ya kuwafikishia watu maandishi yako kwa bure kabisa. Anza kwa kuwa na blog, na andika mara kwa mara, kwa kuanza fanya kila siku, andika hata kwa siku mara mbili au mara tatu, andika sana, andika vitu ambavyo mtu akivifanyia kazi maisha yake yatakuwa bora.
Kama unachofanya ni kufuatilia michezo, anza kuwapatia watu uchambuzi wa ile michezo ambayo unafuatilia, toa historia za ile michezo ambayo unaifuatilia, hakikisha watu wanapotaka taarifa kuhusu michezo hiyo, wanakuja kwako kwanza.

Hatua hii ya tatu ni hatua muhimu kwani hapa ndipo watu wanapokujua na kuanza kuwatengenezea utegemezi. Wafanye watu wakutegemee wewe kupitia kile ambacho unawapatia. Kumbuka kwenye hatua hii hakuna faida yoyote unayotengeneza, unatengeneza jina kwanza.

SOMA; USHAURI; Biashara Unazoweza Kuanza Kwa Mtaji Wa Tsh Laki Mbili Na Kuweza Kufanikiwa.

HATUA YA NNE; Anza kutoza gharama kwa wale wanaotaka zaidi ya unachotoa.

Ukishatengeneza jina lako, na watu wakaanza kukutegemea kutokana na matokeo bora unayotoa, sasa unaweza kuanza kuwatoza watu kwa kile cha ziada wanachotaka uwafanyie. Ni wakati gani w akufanya hivi utaona tu inakuja yenyewe, watu wataanza kukuuliza wenyewe kama unaweza kuwasaidia kwenye mambo yao yanayohusika na unachofanya, na wao wenyewe watakuuliza wakulipe kiasi gani. Hii ndiyo hatua muhimu kwako kujenga msingi sahihi na imara wa kibiashara.

Kwa mfano ambao msomaji mwenzetu ametuandikia, hapa ndipo unapoanza kutoa huduma yako ya upambaji kwa gharama. Hapa umeshatengeneza jina lako, umeshashiriki kwenye sherehe nyingi na watu wameanza kuambiana kuhusu wewe. Hapa umeshawaangalia wengine wanaofanya wana mapungufu gani na wewe unakuja na suluhisho bora kabisa.

Kama ni uandishi watu wanaanza kukuuliza kama unaweza kuwapa ushauri wa moja kwa moja, au kama kuna vitabu umeandika ambapo watu wanaweza kujifunza zaidi. Kama ni matumizi ya mitandao, watu wanaanza kukuuliza kama unaweza kuwatangazia biashara zao kupitia mitandao ya kijamii. Kama ni ufuatiliaji wa michezo, watu wanaanza kukuuliza kama unaweza kuwaelimisha zaidi kuhusu michezo hiyo, au kuwasaidia kutabiri michezo hiyo. Yapo mengi ambayo watu watahitaji kutoka kwako.
Unapofikia kwenye hatua hii ya nne, unahitaji kuwa umepitia biashara za wengine na kuona ni vitu gani unahitaji kufanya tofauti ili uwe bora zaidi ya wengine.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.

HATUA YA TANO; Kuza biashara yako.

Unapofika hatua hii ya tano sasa una biashara ambayo ina wateja, ambao wapo tayari kukulipa ili kupata bidhaa au huduma unayotoa. Hapa sasa ndiyo unaweza kusema una biashara, na unachohitaji kufanya hapa ni kuikuza biashara yako. unaweza kuona ndiyo sehemu rahisi, lakini ukweli ni kwamba hii ni sehemu ngumu, kwa sababu kila siku unahitaji kuja na mbinu mpya na bora za kukuza biashara yako.

Katika hatua hii ndiyo unaweza kuchukua mkopo wa kibiashara, kwenye hizo hatua nyingine za nyuma kamwe usichukue mkopo, utajipoteza. Chukua mkopo ukishakuwa na biashara ambayo tayari ina wateja wanaokulipa kwa kile unachofanya.
Hizi ndizo hatua tano muhimu ambazo mtu yeyote anaweza kuzitumia kutoka chini kabisa mpaka kufikia kumiliki biashara kubwa na yenye mafanikio.

Maswali ya haraka haraka na majibu yake;

Swali; je hatua hizi tano ni rahisi?

Jibu; hapana siyo rahisi hata kidogo, unahitaji kuweka juhudi kubwa sana, unahitaji kujifunza kila siku, unahitaji kuacha uvivu na unahitaji kubadili maisha yako moja kwa moja.

Swali; itanichukua muda kiasi gani kuanzia hatua ya kwanza mpaka hatua ya tano?

Jibu; ukiweka juhudi vizuri, ukajifunza vyema na kufanyia kazi yale unayojifunza, itakuchukua mwaka mmoja mpaka miwili. Ukiwa mzembe itakuchukua muda mrefu zaidi na hivyo utakata tamaa haraka. Ukitaka kufanya haraka zaidi ya hapo utashindwa kabisa.

Fanyia kazi hatua hizi tano kwenye biashara unayotaka kuanzisha kwenye maisha yako, na utajijengea biashara kubwa na yenye mafanikio. Muhimu ni uwe mvumilivu na ujitoe sana kwenye kile unachofanya. Usikate tamaa na jifunze kwa wengine ambao wamefanikiwa kwenye kile unachoanza kufanya wewe.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Mbinu Tatu (3) Muhimu Za Kukutoa Kwenye Umaskini Hadi Utajiri.

$
0
0
Kuna baadhi ya watu mbalimbali waliweza kueleza maana ya umaskini kutokana na wao wanavyoelewa. Wapo baadhi ya watu walisema kuwa umaskini hutokana mtu kuishi chini ya dola moja kwa siku. Wapo pia waliosema kuwa  neno umaskini halina maana sahihi kutokana na kila msomi alivyokuwa na tafsiri yake.

Tuachane na hayo na kuacha kila mmoja aweze kubaki na maana ambayo kila mmoja aweze kuelewa  mwenyewe kutoka  na anavyoona jinsi maisha yake na jamii kwa ujumla. Fuatana nami katika muda huu ili uweze kujua mbinu za kukutoa kwenye umaskini hadi utajiri.

Zifuatazo ndizo mbinu za kukutoa kwenye umaskini hadi utajiri.

1. Kuondokana na dhana  potofu.
Moja ya changamoto ambayo inatukumbuka wengi ni kuishi katika kuamini ya kwamba ni lazima ujihusishe na masuala ya kishirikina ili ufanikiwe zaidi. Misingi hiyo endapo utaishi nayo na kukua nayo itakufanya uamini ya kuwa maisha ya mafanikio hayapatikani kwa njia njia nyingne isipokuwa ushirikina. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya kweli yanapatikana kwa wewe kufanya kazi kwa bidii.

Kila jambo linahitaji juhudi za kiutendaji na si vinginevyo. Mafanikio yanayopatikana kwa njia ya ushirikina ni njia ya mkato yenye madhara makubwa ndani ya muda mfupi kama unabisha jaribu kufanya hivyo uone. Ukitaka kufanikiwa zaidi jambo la msingi ni  kufikiri mara mbili na kwa umakini wa hali ya juu huku ukibadili mtazamo .

Ondokana na dhana potofu zinazokuzuia kupata pesa.

2. Kujiamini kwa jambo lolote.
Kwa kuwa wewe ndiye msaka tonge kwa kutumia mbinu halali  za kimafanikio huku ukiongeza juhudi na ubunifu katika utendaji wako wa kazi huku ukiamini ya kwamba wewe ni zaidi ya watu mabilionea. Unajua kwa nini nimesema hivyo? ni kwa sababu wengi wetu hatuamini katika kazi ambazo tunazifanya.

Ukichunguza kwa umakini tofauti kubwa kati ya maskini na tajiri utagundua katika kauli zao.  Maskini akiwa anaenda kufanya kazi zake utashangaa wakati anaaga utamsikia naenda kuhangaika. Au ukimpigia simu ukimuuliza upo wapi kwa sasa utamsikia nipo kwenye mihangaiko tu ndugu yangu. Wakati kwa upande wa tajiri huwa ni kinyume chake ukimuuliza upo wapi atakwambia nipo kazini. Na asubuhi utamsikia naenda ofisi. 

Ukichunguza kwa umakini katika kauli hizo utagundua ya kwamba maskini ni mtu wa kutojiamini hata kidogo wakati wewe una uwezo wa kutengeneza kipato zaidi ya huyo anayesema naenda kazini. Ewe Msomaji wa makala haya endapo utaendelea na kauli zako hizo ya kwamba naenda kwenye mihangaiko ni kweli utahangaika mpaka pumzi itapokata hivyo ni wakati wako sahihi wa kubadili kauli zako kwa kusema huku unajiamini, na wewe unaenda kazini na ofisini.

3. Kubali kukosolewa.

Huwa nafurahi sana hasa pale tunapokutana na marafiki zangu tukiwa tunazungumzia mchezo wa mpira wa miguu. Huwa tunakuwa na hoja mbalimbali na kusema fulani kabebwa, huku wengine wakisema yaani leo kocha angemchezesha fulani ingewezekana tungeshinda. Unajua ni kwa nini nimekupa kisa hicho ukweli ni kwamba watu wanakuzunguka ni wazuri sana katika kugundua jambo ambalo unalolifanya   kwa kuona mapungufu na mazuri iliyonayo. Hivyo ni muda wako sahihi wa kuchukua maoni yao na kuweza kuyafanyia kazi ili kuweza kuboresha ofisi au jambo lako.

Ewe msaka Mafanikio kumbuka ya kwamba tumia kidogo ulicho nacho ili kupata mafanikio zaidi.

Imeandikwa na; Afisa mipango Benson Chonya.
Simu; 0757-909942
E-mail;
 bensonchonya23@gmail.com


UCHAMBUZI WA KITABU; THINK LIKE A CHAMPION (Fikiri Kama Mshindi, Elimu Isiyo Rasmi Kuhusu Biashara Na Maisha.)

$
0
0
Donald Trump mwaka huu 2016 anagombea uraisi wa nchi ya marekani. Mengi sana yamesemwa na kuandikwa kuhusu yeye kutokana na namna anavyochukulia mambo na namna anavyoyasema.

Donald Trump ni mtu ambaye amekuwa anasema kile anachojua ni sahihi bila ya kujali wengine wanachukuliaje. Anakataa kitu kinaitwa unafiki hasa kwenye siasa ambapo watu wanatafuta maneno mazuri ya kuongea ili wasiwakasirishe wengine. Kutokana na utayari wake wa kusema mambo kama yalivyo, amekuwa akichukiwa na wengi na pia kupendwa na wengi.

Licha ya kuwa mfanyabiashara na bilionea, Donald Trump pia amekuwa akinadika vitabu. Baadhi ya vitabu vyake ni ART OF THE DEAL, WHY WE WANT YOU TO BE RICH, NEVER GIVE UP na vingine vingi. Leo tutakwenda kuchambua moja ya vitabu vyake kinachoitwa THINK LIKE A CHAMPION. Kuna mengi sana ya kujifunza kupitia kitabu hiki ambacho ni mkusanyiko wa maandiko ya Donald Trump.

Karibu tujifunze kwa pamoja kupitia uchambuzi huu.

1. Huhitaji kuwa mvumbuzi mkubwa au mbunifu sana ili uweze kupata wazo bora la biashara. Badala yake unahitaji kuwa makini na maisha yanayokuzunguka, kuangalia kila ambacho kinaendelea kwenye maisha yako na hii itakupelekea wewe kupata mawazo ya tofauti kuhusu biashara.

2. Kuwa tayari kujifunza na mara zote kuwa tayari kupokea mawazo mapya. Pale unapofikiria na kujiona kwamba unajua kila kitu, ndiyo unakuwa mwisho wako wa kukua na kufanikiwa. Ili kufanikiwa kwenye maisha, ili kuendelea kuwa mbunifu ni muhimu uwe tayari kujifunza kila siku.

3. Usiridhike na mafanikio yoyote unayoyapata, kila hatua unayopiga jua ya kwamba kuna hatua nyingine nyingi zipo mbele yako. unapoanza kuridhika na mafanikio madogo unayopata ndiyo unakuwa mwisho wa mafanikio yako. mara zote weka mipango mikubwa zaidi pale unapofikia ile uliyoiweka mwanzo.

4. Hakuna mafanikio yanayokuja bila ya gharama. Chochote kikubwa unachotaka kwenye maisha yako, jua kuna gharama unayotakiwa kulipa. Jua gharama hiyo na kuwa tayari kuilipa ili uweze kupata kile ambacho unakitaka. Kadiri unavyojua gharama hiyo na kulipa mapema ndivyo unavyoweza kupata mafanikio hayo haraka.

5. Mara zote upo uwezekano wa kushindwa, kwa jambo lolote unalopanga kufanya, hata kama umejiandaa kwa kiasi gani, jua ya kwamba huwezi kuondoa kabisa uwezekano wa kushindwa. Jua upo uwezekano wa kushindwa na hivyo jiandae. Usitake kukutana na kitu chochote kwa mshangao, kuwa na maandalizi.

6. Uaminifu Ni kitu kikubwa na muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio. Watu wanakuwa tayari kufanya kazi na mtu ambaye wanaweza kumwamini. Watu wapo tayari kufanya biashara na mtu ambaye wanamwamini. Kama huna uaminifu, huwezi kufanikiwa kwenye jambo lolote kwenye maisha yako. Unaweza kupata matokeo unayotaka kwa muda mfupi, lakini hayatadumu kama hujajenga misingi ya uaminifu.

SOMA; Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Ikiwa Una Kipato Kidogo.

7. Unahitaji Hekima katika safari yako ya mafanikio. Na hekima inatokana na ujuzi/elimu, uzoefu na ufahamu. Hekima unajijengea mwenyewe kadiri unavyojifunza na kupambana na changamoto za maisha yako. hakuna mtu anayeweza kukupa hekima, hekima unaitengeneza wewe mwenyewe. Hekima itakuwezesha kufanya maamuzi bora katika nyakati za changamoto.

8. Washindi wanazaliwa na washindi wanatengenezwa. Usije ukajiambia kwamba wewe huwezi kuwa mshindi kwa sababu ya maisha uliyopitia, unaweza kujitengeneza na kuwa mshindi kwenye eneo unalotaka. Ili kuwa mshindi ni lazima ujue maana ya mshindi. Mshindi ni mtu ambaye ameonesha uwezo wa juu kwenye kile ambacho anakifanya. Pia mshindi ni mtu ambaye ananyanyuka tena hata kama hawezi kunyanyuka. Ushindi unaanza na wewe mwenyewe, kwa kuamua kuwa mshindi.

9. Ili uwe mshindi ni lazima ujifunze kutoka kwa washindi wengine. Hivyo kuwa na washindi ambao unawafuatilia kwenye kile wanachofanya. Iwe ni kwenye michezo, biashara kazi na hata maisha. Angalia jinsi washindi wanavyochukulia mambo yao, angalia jinsi wanavyotatua changamoto zao na angalia jinsi wanavyopeleka maisha yao. Kuna mengi sana unayoweza kujifunza kupitia washindi, jifunze na yaweke kwenye maisha yako.

10. Washindi wote wana tabia moja ya kipekee, wanakwenda hatua ya ziada. Washindi siyo watu anaofanya kile wanachoambiwa wafanye na kuishia pale, bali ni watu ambao wanajua kipi kinatakiwa kufanyika wanakifanya halafu wanakwenda mbali zaidi kuhakikisha wanakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Washindi wanatumia muda mwingi kujiandaa kuliko wengine ambao siyo washindi. Hivi ndivyo watu wanavyoshinda mashindano ya michezo, wanavyopandishwa cheo na wanavyokuza biashara zao, kwa kuwa tayari kwenda hatua ya ziada mara zote.

SOMA; KITABU; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

11. Shindana na wewe mwenyewe ili kuwa bora zaidi. Ni rahisi sana kutaka kuwashinda wengine, kwa sababu unaweza kujilinganisha nao kwa nje lakini kumbuka hakuna anayefanana na wewe kwa kila kitu. Hivyo unaweza kuwashinda wengine, lakini ukawa bado hujashinda, kwa sababu unaweza kuwa hujafikia uwezo mkubwa uliopo ndani yako. mara zote shindana na wewe mwenyewe. Hatua yoyote unayopiga kwenye maisha yako jiulize je hiki ndiyo bora kabisa ninachoweza kufanya? Jibu linatakiwa kuwa hapana halafu uongeze ubora zaidi. Ukijilinganisha na wewe unaweza kujiona umeshakuwa bora kumbe unajilinganisha na watu wenye uwezo mdogo sana ukilinganisha na ulionao wewe.

12. Hakuna njia yoyote ambayo imenyooka moja kwa moja, hakuna mpango wowote ambao unakwenda kama ulivyopangwa kwa asilimia 100. Hivyo kuwa na mipango mizuri lakini pia kuwa tayari kubadilika pale mambo yanapokwenda tofauti na ulivyotegemea. Hivi ndivyo washindi wanavyoweza kuzivuka changamoto wanazokutana nazo na kushinda. Usiwe mgumu kubadilika, kuwa tayari kubadilika kadiri mazingira yanavyobadilika.

13. Biashara ni kitu kimoja, KUTATUA MATATIZO YA WATU. Kama unataka kuwa kwenye biashara na ufanikiwe, basi tafuta matatizo yanayowasumbua watu na yatatue. Angalia ni kipi ambacho watu wanasumbuka nacho a waletee suluhisho. Ukifikiria kutatua matatizo ya watu, mara zote utaziona fursa za kuanzisha na kukuza biashara yako.

14. Hakuna mtu yeyote ambaye amepata kitu chochote kiurahisi. Hivi ndivyo tunavyopenda kuwaona washindi, kama watu fulani ambao wamebahatika kufika kwenye ushindi. Tunawaona pale ambapo wameshashinda, lakini hatuwaoni wakati wanajiandaa kushinda. Wanajiandaa kwa mateso makubwa, wanaweka juhudi kubwa kuliko ambavyo wengine wapo tayari kuweka, na hili linawafanya washinde. Kama unataka kuwa mshindi, ni lazima ujitoe, uache kujionea huruma na uweke juhudi kubwa mno.

SOMA; KITABU; KWA NINI MPAKA SASA WEWE NI SIO TAJIRI.

15. Njia bora kabisa ya kutatua matatizo au changamoto, ni kujiandaa kabla tatizo lenyewe halijatokea. Hakuna kitu kinachoumiza kama kukutana na tatizo ambalo hukuwa umejiandaa, washindi hawafanyi hivyo. Mara zote wanajiandaa. Na wanajiandaa kwa kujiuliza swali hili muhimu sana; JE NI TATIZO GANI LINAWEZA KUJITOKEZA? Jiulize swali hili kwenye kila unachofanya na fanyia kazi yale majibu unayoyapata. Hakikisha unakuwa na uelewa wa kila namna inayoweza kwenda tofauti na ulivyopanga na ni hatua zipi utakazochukua.

16. Weka umakini na mawazo yako yote kwenye kile kitu unachokifanya, kwa wakati husika. Washindi wote wanaweka mawazo yao kwenye kile wanachofanya na hivyo kulazimisha akili zao kuja na mawazo bora ya ushindi. Lakini wanaoshindwa wanatawanya mawazo yao kwenye mambo mengi na hivyo kushindwa kutumia akili zao vizuri. Chochote unachochagua kufanya, weka umakini na mawazo yako yote pale, utashangaa jinsi akili yako inavyoweza kukuletea matokeo bora.

17. Jitengenezee mwendo kasi wa mafanikio, kufanikiwa kwenye jambo moja haimaanishi utaweza kufanikiwa kwenye kila kitu. Unachohitaji ni kuwa na mwendokasi wa mafanikio ambao utakuwezesha kuendea kila changamoto kwa hamasa kubwa. Unaweza kujitengenezea mwendokasi wako kwa kujua jinsi mwili wako unavyofanya kazi. Jua ni wakati gani unakuwa na ubunifu mkubwa na nguvu kubwa za kufanya kazi. Wengine wako vizuri wakati wa asubuhi, wengine wakati wa jioni. Jua muda mzuri kwako na utumie vizuri.

18. Matatizo, vikwazo, makosa na hasara ni sehemu ya maisha. Ni vitu ambavyo tunatakiwa kuvikubali ili maisha yaweze kwenda. Hatupaswi kurudishwa nyuma na mambo haya badala yake yanahitaji kutusukuma kuelekea kwenye ushindi zaidi. Jifunze kwa kila unalopitia, ili usirudie kufanya kosa moja mara mbili.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Wahitimu Wa Elimu Ya Juu Mwaka 2016, Ukweli Ambao Umekuwa Unafichwa Kwa Miaka 20 Iliyopita.

19. Mara nyingi watu watakuwa wanafurahia kukudharau na kudharau mafanikio yako, usikubali watu hawa wakurudishe nyuma, badala yake jikubali wewe mwenyewe, jua kile ambacho unataka na kifanyie kazi. Jua ya kwamba ndani yako una uwezo mkubwa na usisite kusema mbele ya watu kuhusu wewe na kile unachofanya. Hii ndiyo njia ambayo watu watakujua na kujua kile unachofanya, na pia kuwashinda wale wanaokudharau.

20. Wakati mambo yanakwenda hovyo, wakati kila mtu anapitia changamoto ndiyo wakati ambao wengi wanafanya mabadiliko makubwa. uhitaji unawalazimisha watu kuwa wabunifu. Mara zote tumia wakati mgumu unaopitia kuhakikisha unafanya mabadiliko makubwa pale unapopitia wakati mgumu. Kwa sababu huu ndiyo wakati ambao utalazimika kubadilika hivyo badilika na kuwa bora zaidi. Mara zote kuwa na mpango mbadala, usiwe na mpango mmoja pekee, unapokuwa kwenye changamoto ni wakati wa kuangalia mpango mwingine unaoweza kukufikisha kwenye ndoto zako.

Kuna mambo mengi sana kuhusu biashara na maisha tunayoweza kujifunza kupitia Donald Trump, katika kujiandaa kwa maisha ya ushindi na mafanikio.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Hii Ndiyo Njia Ya Uhakika Ya Kupata Chochote Unachotaka Kwenye Maisha Yako Na Kufanikiwa.

$
0
0

Habari ya wakati huu Mpendwa Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Karibu tena katika siku hii nyingine mpya ambayo ni fursa kubwa kwetu na ya kipekee kabisa ya kwenda kuboresha maisha yetu bila kusahau kukua katika mafiga matatu ambayo ni muhimu kwa kila mwanadamu. Kama tunavyojua huwezi kuweka sufuria au chungu jikoni ambapo kuna mafiga mawili au moja. Mafiga matatu yana ushirikiano wa hali ya juu sana kama figa moja halipo basi mafiga mengine hayawezi kufanya kazi. Huenda ukawa unajiuliza mafiga matatu hayo ni yapi? Basi, ndugu msomaji, ninaposema unatakiwa kukua katika mafiga matatu namaanisha kwamba kukua katika sehemu kuu tatu nazo ni; kukua kiroho, kimwili na kiakili.


Ndugu msomaji, katika harakati zako zote hakikisha unakua katika sehemu hizo kuu tatu. Unatakiwa uwe sawa usikue tu kimwili, bali kua kiroho na kimwili. Na uwe na ushirikiano katika maisha yako kama mafiga matatu. Karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza kwa pamoja falsafa ya asili kabisa ambayo inagusa maisha ya watu wengine katika safari ya mafanikio. Huwezi kuikwepa falsafa hii katika maisha yako kama wewe uko hapa duniani. Je unajiua falsafa hii muhimu sana katika safari yako ya mafanikio ambayo unaitumia kila siku? Karibu twende sanjari mpaka mwisho wa safari hii.

SOMA; Mbinu Saba(7) Za Kuongeza Ushawishi Wako Kwa Wengine Na Kupata Chochote Unachotaka.

Kuna bahari inaitwa Bahari Mfu (Dead Sea) hii bahari iko pale mashariki na kati katika nchi ya Israel. Sifa kuu ya bahari hii ina mazoea ya kupokea maji tu pale mashariki na kati. Hii bahari yenyewe ni kupokea tu na haitoi hata tone ili kumegea wengine bali imeshikilia tu maji yote. Matokeo yake maji yananuka na hayafai kwa matumizi ya mwanadamu.

Kwa mfano huo, wa bahari mfu tunaweza kuuona katika maisha yetu ya kawaida. Watu wamekuwa kama bahari mfu wenyewe ni kupokea tu bila kutoa hata tone kwa wengine. 
Falsafa ninayoizungumzia hapa ni falsafa ya KUTOA NA KUPOKEA. Leo siyo mara yako ya kwanza kusikia hii dhana katika maisha yako kwamba unapopokea unatakiwa kutoa na unapotoa tarajia kupokea. Katika dunia ya leo kama unataka kufanikiwa unatakiwa usiwe kama bahari mfu. Ni wangapi wanapenda kupokea tu katika maisha yao bila kutoa? Umejaliwa kila kitu na Mungu je unatoa kuwasaidia wengine? Au umekuwa bahari mfu? Unapenda kupokea bure tu siku ukiambiwa kulipia gharama unakimbia hujui hata vya bure vina gharama?

Katika maisha ya mafanikio usitegemee kupokea kama hujatoa. Unapotoa ndio unapokea, je unayatumiaje maarifa uliyonayo kuwasaidia wengine nao waboreshe maisha yao? Kama una kitu katika akili yako na unaona kama kitakuwa ni msaada kwa wengine wasaidie na wengine ili nao wanufaike pia. Hujui jinsi unavyowasaidia wengine ndivyo na wewe unavyopokea kwa sababu unakuwa siyo bahari mfu tena bali una faida kwa wengine.

SOMA;  UCHAMBUZI WA KITABU; START WITH WHY, Jinsi Viongozi Wakubwa Wanavyohamasisha Watu Kuchukua Hatua.

Lazima utoe huduma ndio uweze kupokea malipo. Huwezi kupokea malipo bila kutoa huduma. Hivi karibuni bilionea Mohamed Dewji ambaye ndio bilionea kijana Afrika aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa instagramu hivi ‘’Mungu anapokubariki kwa utajiri usiboreshe kiwango cha maisha yako, boresha kiwango chako cha KUTOA’’ hakuna tajiri au mtu aliyefanikiwa aliwahi kufilisika kwa ajili ya kusaidia wengine. Hivyo basi, unapopata toa, na unapotoa ndio utapokea.

Unapopata mafanikio na wengine wanufaike pia na siyo kuwa kama bahari mfu unapokea tu hata hutoi kwa wengine. Tena katika utoaji unatakiwa kutoa kwa moyo na ukarimu. Kama una kipaji fulani katika maisha yako au taaluma fulani saidia kuwapa huduma watu kwa kile ambacho unacho. Ubinafsi na umimi hautakusaidia kitu. Huwezi kurefusha wasifu wako hapa duniani kwa kuangalia tu familia yako. Pale wasifu wako unaposomwa wakati upo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa usiwe hivi, marehemu aliacha mke na watoto watano, kumi, magari ya kifahari kumi na nyumba ya kifahari tayari wasifu umeisha. Sasa huu ni wasifu wa umimi au ubinafsi ambao unaonesha kujitoa kwa familia yako zaidi kuliko kwa watu wengine. Bora hata yule aliyekuwa na kibanda cha chipsi na kuajiri hata watu wawili atakua amegusa maisha ya watu wengine na atakumbukwa na watu kulingana na huduma yake ya chipsi aliyokuwa anatoa na kuajiri watu.

Usikalie maarifa ambayo unayo, ulienda shule kuyapata bali yatoe duniani ili yatengeneze dunia. Usiwe astashahada, stashahada, shahada, uzamili na uzamivu jina tu bali kuwa na vitendo kulingana na elimu yako uliyoipata. Wasaidie wengine waonje matunda yako uliyoyapata shule siyo kuwa msomi cheti wa maneno bila vitendo.

Kabla hujalalamika na kusema serikali haijanifanyia kitu fulani jiulize je na wewe umeifanyia nini serikali yako?, mwajiri wako hajakufanyia kitu fulani je na wewe umeongeza thamani gani kwa mwajiri wako?, wateja wako wamepungua katika biashara yako na n.k jiule je na wewe umewafanyia nini wateja wako? Kwenye kila kitu usitegemee kupokea kama na wewe hujatoa chochote. Hata ng’ombe hawezi kukupa maziwa kama na wewe hujamhudumia chakula chake ili akuzalishie maziwa. Ukiyahudumia mazingira vizuri nayo yatakuhudumia vizuri.

SOMA; Kama Una Wasiwasi Sana Katika Maisha Yako, Hakikisha Unasoma Hapa.

Kwa hiyo, ndugu msomaji, tunatakiwa kuishi katika falsafa hii unapopokea unatakiwa kutoa. Ukipokea bila kutoa unakuwa una deni hivyo unatakiwa kulilipa kabla hujaondoka hapa duniani. Tafadhali usiwe kama bahari mfu katika maisha yako kwani utakuwa unanuka mbele za watu maisha yako yamekuwa hayana msaada kwa wengine kama vile bahari mfu. Kama umepokea toa kwa moyo na ukarimu. Mali isikufanye udhulumu, udharau, utumikishe na kudhalilisha utu wa watu wengine. Na usiendelee kuishi kwa mazoea kwani mazoea yataendelea kuacha watu wakose Baraka za Mungu kwa miaka mingi. Hivyo amka na badilika.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Chuma ulete wa biashara yako ni huyu hapa na jinsi unavyoweza kumwepuka.

$
0
0
Moja ya changamoto ambazo zinasumbua biashara ndogo ni imani ambazo wafanyabiashara wanazo. Kuna dhana moja ipo kwenye mitaa yetu kwamba kuna watu ambao ni chuma ulete. Watu hawa wanapokuja kwenye biashara yako na kununua kitu, ukiwarudishia chenchi basi baadaye wanahamisha fedha zote kwenye biashara yako kwa nguvu za kishirikina. Watu wamekuwa wakihofia sana hili na hivyo kukataa kabisa kuwauzia baadhi ya watu ambao wanajulikana kama chuma ulete au wakiwauzia basi fedha zao wanaziweka pembeni, wanazitenga kabisa na fedha nyingine.

Mwanzoni nilipokuwa nasikia haya kutoka kwa wafanyabiashara nilikuwa nafikiri ni kitu cha utani tu, kwamba wanatania, lakini kila siku ninapokutana na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya ushauri au mafunzo, hili la chuma ulete huwa halikosekani. Kuna wakati mpaka nimesikia likijadiliwa kwenye vipindi vya redio na televisheni, watu wakilalamika kwamba mitaa fulani huwezi kufanya biashara kwa sababu wapo watu hao wanaofahamika kama chuma ulete.
KUPATA KITABU HIKI BIASHARA NDANI YA AJIRA, BONYEZA MAANDISHI AU PICHA HII.

Leo kupitia makala hii ya KONA YA MJASIRIAMALI tunakwenda kumwangalia chuma ulete huyu ambaye anatesa biashara yako ndogo na jinsi ya kupambana naye ili asiendelee kuharibu biashara yako.

Je chuma ulete wapo?

Swali muhimu la kuanza nalo kwenye makala hii ya leo ni je chuma ulete yupo? Je kuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete?

Mwanzoni nilipokuwa naulizwa swali hili kuhusu chuma ulete nilikuwa nawakatalia watu kabisa ya kwamba hakuna kitu kama hicho kinachoitwa chuma ulete. Nilikuwa nawaambia watu kwamba ni imani zao tu ndiyo zinawasumbua, hakuna chuma ulete yeyote ambaye anawachukulia fedha zao kwenye biashara. Lakini baadaye nikaanza kujiuliza kama chuma ulete hakuna, iweje watu wanapata hasara kwenye biashara zao? Iweje mtu mwisho wa siku yake wakati anapiga mahesabu anakuta amepata hasara kubwa? Hapa ndipo niliposhawishika kwamba lazima kutakuwa na chuma ulete.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuishinda Hofu Ya Kupata Hasara Kwenye Biashara.

Je chuma ulete wa biashara yako ni nani?

Baada ya kushawishika kwamba chuma ulete yupo, hatua iliyofuata ilikuwa kumjua chuma ulete kwenye biashara ndogo ni nani. Na hapa nilikuja na jibu ambalo lilinishangaza, kwa sababu lilikuwa na jibu la kweli ambalo likifanyiwa kazi chuma ulete huyo anakimbia kabisa. Jibu nililopata ni kwamba chuma ulete wa biashara zote ndogo ni mfanyabiashara mwenyewe. Ndiyo, yaani kama wewe ulishapatwa na chuma ulete kwenye biashara yako, basi chuma ulete huyo ni wewe mwenyewe. Hakuna mtu mwingine anayeweza kutoka nje ya biashara yako na kuweza kuchukua fedha kwenye biashara yako kwa njia za kishirikina. Fedha kwenye biashara yako zinaweza kutoka kwa njia mbili pekee, njia ya kwanza ni wewe uzitoe mwenyewe, na njia ya pili ni uzipoteze kizembe. Chuma ulete ni pale ambapo unapoteza fedha kizembe kwenye biashara yako.

Kabla hujakataa kwamba wewe siyo chuma ulete wa biashara yako, na kuendelea kusisitiza kwamba kuna watu wanakuja kwenye biashara yako na kuchukua fedha kwa njia za ajabu, naomba ujiulize swali hili; ulishawahi kusikia benki inalalamika kwamba wameibiwa fedha kwa chuma ulete? Umeshawahi kusikia biashara kubwa, kama makampuni wakilalamika kwamba kuna chuma ulete wanawaibia fedha? Kwa nini unafikiri ni biashara ndogo pekee zinazoandamwa na chuma ulete? Kama chuma ulete wangekuwa na nguvu hiyo ya kuchukua fedha kwa nguvu za ajabu, je unafikiri wangechukua fedha wapi, kwenye biashara yako ndogo au kwenye mabenki ambayo yana fedha nyingi?

Chuma ulete hawapo kwenye mabenki wala biashara kubwa kwa sababu kule kila kitu kinaendeshwa kwa taratibu. Hakuna fedha inayotolewa bila ya maandishi, hivyo mwisho wa siku kila kitu kinaonekana kimekwendaje, na mzunguko wote wa fedha unaonekana. Lakini wewe kwenye biashara yako fedha inazunguka bila ya mahesabu yoyote, ukitaka kununua kitu unatoa kwenye droo na kununua, nyumbani wakitaka fedha ya matumizi unatoa na kuwapa, akija mtu kukopa unachukua na kumpa. Unakuwa unajiambia baadaye utakumbuka, lakini kwa uchovu wa siku nzima, inapofika jioni huwezi tena kukumbuka kila kitu ulichofanya kwenye biashara yako kwa siku nzima. unafanya mahesabu na kugundua kuna hasara imejitokeza, na moja kwa moja unafikiria chuma ulete tayari wamekuibia. Nafikiri unaanza kupata picha ni kwa namna gani wewe mwenyewe ni chuma ulete wa biashara yako.

SOMA; Wakati Sahihi Na Wakati Mbaya Wa Kuchukua Mkopo Wa Biashara Benki.

Je unawezaje kuondokana kabisa na chuma ulete kwenye biashara yako?

Wahenga walisema, mali bila ya daftari, hupotea bila ya habari. Hii ndiyo dawa pekee ya chuma ulete kwenye biashara yako. Usikiamini kichwa chako na kufikiri utakumbuka kila kitu kwenye biashara yako, badala yake kuwa na daftari, na kila kitu kinachofanyika kwenye biashara yako kiandikwe. Andika kila fedha inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, andika kila mali inayoingia na kutoka kwenye biashara yako, na mwisho wa siku fanya mahesabu kuona kama mambo yanakwenda sawa, kwamba kilichotoka na kuingia kimekwenda sawa na mahesabu yaliyopo kwenye biashara.
Kitu kidogo kama daftari kinaweza kuikoa sana biashara yako, kama utakitumia vizuri na kuzingatia, utaweza kuwa na udhibiti mkubwa wa mzunguko wa fedha kwenye biashara yako. kumbuka fedha ndiyo damu ya biashara yako, hivyo ilinde kwa uwezo wako wote ili biashara yako iweze kustawi na kukuletea mafanikio.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hali Ya Kukosa Uthubutu Na Kuingia Kwenye Biashara Itakayokufikisha Kwenye Ubilionea.

Wewe ndiye chuma ulete wa biashara yako kwa kukubali kuendesha biashara yako kizembe bila ya kuwa na kumbukumbu sahihi za kibiashara. Ili kuondoa hali hii ya chuma ulete kwenye biashara, hakikisha unakuwa na kumbukumbu sahihi za biashara yako. usichukulie mambo kirahisi, huko ndiyo kunakuletea hasara kila siku. Kila la kheri.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Hii Ndiyo Faida Ya Kupanda Mbegu Bora Kwa Wasaidizi Wako Wa Kazi Katika Familia Yako.

$
0
0
Habari mpendwa Rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vema kuboresha maisha yako na kugusa maisha ya watu wengine. Ndugu msomaji napenda kukukaribisha tena katika makala yetu ya leo. Tafadhali tuende pamoja ili uweze kujua nimekuandalia nini siku hii ya leo.

Kumekuwa na matukio mbalimbali yanatokea yakihusu wafanyakazi au wasaidizi wa kazi za ndani. Matatizo mengi yanatokea katika familia nyingi hayaji tu kama radi lazima kuna sababu zinazopelekea kutokea kwa matatizo hayo. Huwezi kupanda mahindi shambani halafu ukategemea kuvuna mbaazi. Hivyo siku zote utavuna kile ulichopanda. Kama ukipanda mbegu bora ya upendo katika familia yako tegemea kuvuna mbegu bora ya upendo. Vivyo hivyo, kama ukipanda chuki katika familia yako tegemea kuvuna mauti. Hii ni sheria ya asili unapokea kile unachotoa.


Kwa tafiti zisizo rasmi, ukitembelea nyumba kumi kati ya nyumba hizo kumi moja tu ndio wanaishi vema na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Nyumba nyingi ni matatizo sana je matatizo haya yote yanasababishwa na nani? Lazima tuchunguze nini kiini cha kosa au tatizo kwanza. Huwezi kutatua tatizo bila kuchunguza kiini cha kosa. Visa vimekuwa vikitawala ndani ya nyumba nyingi kwa wale wanaoishi na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Wasaidizi wa kazi za ndani wanafanyiwa ukatili na waliowaajiri ndio maana nao wanalipa visasi kwa watoto wao. Wasaidizi wa kazi za ndani wanarusha visasi wanavyofanyiwa na waajiri wao kwa watoto. Watoto wanakua wahanga wa matatizo mengi wanaumizwa na kuteswa na kuona dunia ni chungu na siyo sehemu salama ya kuishi kutokana tu na kuishi maisha yaliyokosa upendo ndani yake. Waajiri wa kazi za ndani wanapandikiza chuki kwa wafanyakazi wao wa ndani na wasaidizi wao wanaona sehemu sahihi ya kulipiza kisasi ni kwa watoto. Hivyo wasaidizi wa kazi za ndani nao wanatoa kile walichopokea na siku zote chuki huzaa mauti. Ndio maana kuna faida kubwa sana kwa waajiri kupanda mbegu ya upendo ambayo itakwenda kuota kwa kila mwanafamilia na hatimaye watakuja kuvuna upendo.

SOMA; Umuhimu Wa Kuwa Na Familia Bora Ili Kujenga Jamii Bora.

Mpendwa msomaji, jaribu kuvuta picha ni matukio mangapi umeyasikia au kuyaona kwa macho yako yanayosababishwa na wafanyakazi wa ndani. Na je wahanga wakubwa wa matatizo hayo katika familia ni kina nani? Kama sio watoto? Wafanyakazi wa ndani ndio wanaonekana wana makosa au wakosa kama hujachunguza kiini cha tatizo au kosa kwanza. Wanawake wengi walio na waume zao wanawaachia wadada wa ndani kila kitu wafanye hata zile kazi ambazo hawapaswi kufanya, kazi ambazo angetakiwa kufanya na mama au mwanamke aliyeolewa ambaye yeye ndio mlinzi wa familia. Wanawake wengi wanawatengenezea mazingira mabaya wao wenyewe na unakuta nafasi ya mke sasa anachukua dada wa kazi. Kwa kisingizio kua yuko bize na kazi mpaka anasahau wajibu wake kama mke au mama wa familia. Lazima muwe na mipaka ya kazi na wasaidizi wenu wa kazi siyo kumuachia akufanyie kila kitu katika nyumba yako unayoishi. Wasaidizi wa kazi za ndani unakuta wanajua vitu vingi kuliko mama wa familia ndani ya nyumba sasa hii ni hatari sana.

Kutokana na mwanamke katika familia yake kushindwa kuwa mlinzi wa familia yake matokeo yake hata wale wanaume wasiokua waaminifu katika ndoa zao wanatembea na wasaidizi wao wa kazi kwa sababu mazingira hayo wanayasababisha wao wenyewe. Unampatia msaidizi wako wa kazi kufua nguo za muwe wako hata za ndani na kumwandalia kila kitu mume wako unafikiri unategemea nini? Hujaolewa kwenda kuwa mtalii wa nyumba bali mwanamke aliyeolewa anakwenda kuwa mlinzi wa nyumba yake na baba kuwa kichwa cha familia yake. Na kazi hizo wamepewa na Mungu. Ndio jukumu la mke na mume wakishindwa kutimiza wajibu wao kila mmoja kinachofuata ni machozi tu. Ukiwa ni mama wa kutoa agizo dada naomba nenda kamtandikie baba anataka kulala, au kamuandalie maji ya kuoga, chakula, mwangalie mtoto kama amekula, kama anaumwa, waangalie watoto kama wameenda shule nk na wewe umekaa sebuleni unaangalia tv na kubadilisha chaneli utakuja kupata hasara tu. Kama wewe ni mwanamke ndani ya nyumba usikwepe majukumu yako na kumwachia dada wa kazi na wewe kama ni baba wa familia simama kama kiongozi kweli na mwanamke linda nyumba yako.

SOMA; Huyu Ndiye Adui Namba Moja Kwenye Malezi Ya Watoto.

Mpendwa msomaji, unajua ni kwa nini matatizo yanatokea kwa wasaidizi wa kazi za ndani?

Sasa karibu ujionee viini vya matatizo hayo.

1. Kukosa upendo; wasaidizi wa ndani wanakosa upendo badala yake wanapewa chuki ambayo ndio inakuja kuzaa matatizo mengi katika nyumba nyingi. Hakuna kitu kama upendo wewe lisikie tu neno hili upendo lina maana kubwa sana kwa binadamu. Kama vile wewe unahitaji kupewa upendo na watu wengine mpatie na msaidizi wako wa kazi naye anakurudishia upendo. Mpende kama unavyojipenda wewe, kama unavyoipenda familia yako na mfanye awe sehemu ya familia yako. Vaa viatu vyake halafu utaona kama utavuna ubaya kutoka kwake.

2. Kukosa kuthaminiwa; mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, hitaji la kwanza la binadamu ni kuthaminiwa. Anza leo kumthamini mfanyakazi wako uone naye atakavyokuwa anakuthamini. Unatoa kile unachopokea katika maisha yako. Binadamu akihisi anakosa kuthaminiwa anakua amekufa kisaikolojia kabisa. Ni nani ambaye hahitaji kuthaminiwa? Kila mtu anataka kuthaminiwa katika hii dunia. Hakuna mtu aliyezaliwa kuja kupata mateso duniani mwache kila mtu afurahie na kuonja thamani yake hapa duniani.

3. Kukosa uhuru; kukosa uhuru ni utumwa katika maisha. Ndio maana watu wanapelekwa gerezani kufungwa ili wakose ule uhuru wao. Kila mtu anahitaji uhuru. Sasa hawa wasaidizi wa ndani hawapewi fursa ya uhuru. Ukimbana sana mtu na kukosa uhuru na ni mtu mzima lazima atatafuta uhuru. Naye ni binadamu anahitaji uhuru kama wewe, uhuru wa kufanya mambo yake na usimtawale kama vile mtoto mdogo.

4. Kudharauliwa, kutengwa na kuchukuliwa kama siyo sehemu ya familia; wasaidizi wa ndani wanachukuliwa kama watu wenye shida sana, siyo wa umuhimu na hafai kuwa sehemu ya familia. Wanalala sehemu isiyostahili kulala, wanavaa mavazi yasiyo nadhifu yaani ukienda nyumba nyingine unatamani hata kutokwa na machozi watoto wa familia wamevaa nguo nadhifu ukimuona yeye kachoka kabisa anachukuliwa siyo mtu muhimu. Mtu anayekupikia, kukuangalizia watoto na nyumba yako halafu unamdharau ndio maana hata wengine wanawekewa sumu kwa sababu ya mateso wanayofanyiwa na wanafamilia. Wakati wa kula chakula dada wa kazi anakula jikoni peke yake wanafamilia wamekaa mezani wanakula hivi wewe ungekuwa unafanyiwa hivi ungejisikiaje? Wakati mwingine hata chakula wanapewa masalia wanafamilia kwanza. Ishi na msaidizi wako kwa upendo.

5. Kutukanwa, kupigwa na kudharauliwa; baadhi ya wasaidizi wengine wanateswa na wanatukanwa matusi ya kila aina yaani wamegeuzwa kama jalala la matusi. Mwisho wa siku dada wa kazi anakua anapata majeraha ya moyo. Wengine wanapigwa na kuteswa na kunyimwa hata chakula. Halafu ukifanyiwa jambo baya utasikia wafanyakazi wa ndani sio watu siku hizi. Kabla ya kulalamika chunguza kiini cha kosa ni nani msababishi wa yote haya? Wanafamilia wanatendea vibaya wadada wa kazi ndio maana nao wanawatendea mabaya. Ndio maana dawa ya chuki huzaa mauti, unamfanyia mwenzako mabaya halafu unategemea mazuri? Sahau kuhusu hilo.

SOMA; Hizi Ndizo Sehemu Nne (4) Muhimu Za Kuchota Baraka Katika Maisha Yako.

6. Kusemwa maneno makali; wanasemwa maneno makali yenye chuki ambayo yanakwenda kutengeneza majeraha katika moyo. Maneno ni mabaya kwani yanakwenda kutengeneza chuki ndani ya moyo. Acha kuwasema sana maneno mabaya bali mtie moyo na hamasa ya kufanya kazi na kushirikiana naye hata kama unamlipa. Kuwa kiongozi mzuri katika familia yako.

7. Kutopewa nafasi ya kujieleza na kushindwa kumpata mtu wa kumuelezea matatizo yake; nguvu ya pesa wakati mwingine huwa inatumika kwa kuwakandamiza wadada wa ndani. Ananyimwa mahitaji ya msingi anaingiwa na tamaa ya kuiba halafu akiiba nguvu ya pesa inatumika anakamatwa na kupelekwa polisi bila hata kupewa nafasi ya kujieleza. Na kukichunguza kiini cha kosa utagundua mwajiri wake ndiye msababishi. Unakuta wakati ana shida anakosa mtu wa kumwambia watu wote ndani ya familia wamegeuka kuwa miiba hivyo anaendelea kubaki na uchungu ulioumbika na matokeo yake wanafanya matukio ya ajabu.

8. Kupewa ujira mdogo na kucheleweshewa ujira wao; dhahiri kwamba wafanyakazi wengi wa ndani wanalipa ujira mdogo na wanafanya kazi nyingi zaidi ya masaa 12 bila mapumziko. Kama anakufanyia kazi zako mpe stahiki yake hata kama ni kidogo. Kama humpatii mahitaji yake binafsi lazima umpatie hela ili aweze kujitegemea. Kuna wengine hawapewi kabisa wanaambulia maneno kama haya unakula bure tu, kulala hapa na kujaza choo hapa. Mambo kama haya unakuwa unamuumiza msaidizi wako.

Mwisho, ndugu msomaji, panda mbegu bora ya upendo kwa manufaa yako na kwa jamii nzima. Mpe malazi mazuri na chakula bora. Mtendee mwenzako kama vile unavyotaka wewe kutendewa na vaa viatu vya mwenzako. Kuwa mfano sahihi kama unamwambia msaidizi wa kazi kuamka saa 11 au 12 na wewe onesha mfano. Siyo wewe unatoa agizo halafu unaamka saa 2 jihukumu kwanza wewe mwenyewe kabla ya kumhukumu mwenzako.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Mambo muhimu ya kuzingatia unapochukua mkopo wa biashara.

$
0
0
Moja ya njia ambazo wafanyabiashara wanaweza kutumia kukuza biashara zao ni kuongeza mtaji. Ili kuongeza mtaji kuna mambo ambayo mfanyabiashara anaweza kufanya kama kuwekeza zaidi kwenye biashara yake, kupata ruzuku au kuomba mkopo. Mikopo ya kibiashara imekuwa rahisi kupatikana kwa sasa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Hii inatokana na wingi wa taasisi zinazotoa mikopo hii, kuanzia benki mpaka watu binafsi sasa wanatoa mikopo ya kibiashara.


Wapo wafanyabiashara wengi ambao wanalalamika mikopo imeharibu biashara zao. Wengi walikuwa na biashara zinazokwenda vizuri na hivyo kushawishika kwamba wakichukua mkopo mambo yatakuwa mazuri zaidi. Kinyume na matarajio yao, wanachukua mkopo na biashara inayumba mno na hata kuelekea kufa. Haya yote yanatokana na wafanyabiashara kuchukua mkopo bila ya kuzingatia mambo muhimu kuhusu mikopo ya kibiashara. Leo tutakwenda kujadili hili kwa kina ili unapokwenda kuchukua mkopo, uwe na uelewa na uweze kuutumia vizuri ili biashara yako iweze kukua zaidi.

SOMA; Chuma ulete wa biashara yako ni huyu hapa na jinsi unavyoweza kumwepuka.

Jambo la kwanza na muhimu kuzingatia ni matumizi ya mkopo wenyewe. Ukishaomba na kupata mkopo, huwezi kuutumia kama unavyojisikia wewe, au kwa sababu kuna changamoto fulani imetokea kwenye biashara yako basi unatumia fedha za mkopo kwa sababu unazo. Unahitaji kuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya mkopo wako. Tumia mkopo uliopata kwa shughuli ile uliyodhamiria kuchukulia mkopo. Ni muhimu uzingatie hili kwa sababu kuna mambo mengi yanaweza kujitokeza na yakakushawishi utumie mkopo tofauti na ulivyopanga. Unaweza kutumia lakini mwishowe ukasumbuka kwenye kulipa mkopo huo.

Chukua mkopo na uweke kwenye kitu ambacho tayari kinazalisha. Usichukue mkopo na kwenda kujaribu kitu kipya kabisa, hasa kama ni mfanyabiashara mdogo. Hiki ni kitu kingine muhimu unachotakiwa kuzingatia unapochukua mkopo. Unapochukua mkopo, unategemewa uanze kurejesha mkopo huo mapema iwezekanavyo, na njia pekee ya kurudisha mkopo huo na biashara yako ibaki salama, ni kuuweka kwenye eneo la biashara ambalo tayari linazalisha. Kwa njia hii utaongeza faida na hivyo kuweza kulipa mkopo wako. Lakini kama utachukua mkopo na kwenda kuanza kitu kipya, utajikuta unatakiwa kuanza kulipa mkopo kabla hata hujaanza kupata faida, na hivyo kutoa fedha nyingine kwa ajili ya kulipa mkopo.

SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

Usikuze mapato yako wala kupunguza matumizi yako. Wakati watu wanaomba mkopo, huwa wanapangilia mkopo huo kwa namna watakavyoutumia na mapato watakayotengeneza. Kwa hesabu hizi watu huona faida kubwa wanayoweza kupata kupitia mkopo wanaochukua. Ila hapo kuna tatizo moja, mara nyingi watu wanakuza mapato yao na kupunguza matumizi yao. Hii inawafanya waone faida ni kubwa, lakini wanapokuja kwenye uhalisia, mambo yanabadilika. Ili uweze kwenda vizuri, fanya mahesabu ya uhalisia, kwa kuangalia sasa mambo yanakwendaje. Kuchukua mkopo hakubadilishi sana mambo yanavyokwenda sasa, hivyo ni vyema kuwa na mipango inayoendana na uhalisia ili usivunjike moyo.

Hakikisha unakuwa na fedha ya ziada baada ya kutumia mkopo uliochukua. Kitu ambacho wafanyabiashara wengi wamekuwa hawazingatii ni kuchukua mkopo wote na kuweka kwenye biashara, wanabaki hawana fedha ya ziada na hivyo kutegemea kuanza kuvuna faida. Kama ambavyo kila mfanyabiashara anajua, changamoto hazikosekani kwenye biashara, matatizo ni sehemu ya biashara. Kwa mtu kuweka fedha zote kwenye biashara, inapotokea changamoto au tatizo, wanashindwa kulitatua kwa sababu fedha wanakuwa wameshatumia zote. Kuepuka hili tumia theluthi mbili au robo tatu ya mkopo kwenye biashara yako, na ile inayobaki ikae kama fedha ya dharura, ambayo utaweza kuitumia pale changamoto itakapoibuka. Kwa njia hii, ni vyema ukachukua mkopo ambao unazidi kidogo yale matumizi uliyojipangia, ili uweze kubaki na kiasi cha dharura.

SOMA; KITABU CHA MAY; Biashara Ndani Ya Ajira; Jinsi Ya Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa.

Kitu cha mwisho tunachokwenda kukumbushana hapa leo ni pale unaposhindwa kulipa mkopo kwa wakati, usikimbie wala kujificha. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiharibu sifa zao za ukopeshwaji kwa kukimbia pale wanaposhindwa kurejesha mikopo yao. Lakini kukimbia huko huwa hakuwasaidii na wakati mwingine kunawaletea hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kufilisiwa. Unaposhindwa kulipa mkopo kwa wakati, rudi kwa waliokukopesha na ongea nao, eleza hali yako ilivyo na mnaweza kupanga upya namna ya kulipa mkopo huo. Unapoonesha nia hii na wao wanapata moyo kwamba unajali kuhusu mkopo uliochukua. Ila pale unapoanza kukimbia, ukitafutwa hupatikani, unajenga picha hasi na hivyo kuwafanya wachukue hatua za kisheria ili kupata fedha zao. Hakuna asiyekutana na changamoto, na dawa ya deni ni kulipa, hivyo omba upatiwe muda zaidi uweze kulipa mkopo uliochukua. Unapoingia kwenye hali hii ya kushindwa kulipa, kazana ulipe na jifunze kupitia hali uliyopitia.

Mkopo unapaswa kuwa kichocheo cha biashara yako kukua, zingatia haya tuliyojifunza ili uweze kutumia vizuri mkopo wa kibiashara unaochukua. Kila la kheri.

TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Changamoto Ya Kukaribisha Matatizo Pale Unapokuwa Na Fedha.

$
0
0
Hivi umewahi kugundua ya kwamba kila unapokuwa na fedha ndipo matatizo yanayokuhitaji utumie fedha hizo yanakuwa mengi? Kwamba unapokuwa huna fedha hupati matatizo makubwa, ila ukishakuwa tu na fedha, mara mtoto ataumwa, au mazazi atapata shida, au wewe mwenyewe utajikuta kwenye changamoto ambayo inahitaji fedha? Unatumia fedha uliyoipata kutatua tatizo ulilokutana nalo na kushindwa kutekeleza mipango yako mingine! Basi hili ndiyo tunakwenda kujadili leo kupitia makala hii ya ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufanikiwa.

Habari rafiki yangu, karibu tena kwenye kipengele chetu hiki cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Tunajua ya kwamba changamoto ni sehemu ya maisha, hatuwezi kuzikwepa wala kuzikimbia, njia pekee ya kukabiliana na changamoto ni kuzitatua, na hapa ndipo tunapopeana mbinu muhimu za kukabiliana na changamoto tunazokutana nazo kwenye safari yetu ya mafanikio.

Leo kama nilivyokudokezea hapo mwanzo, tunaangalia changamoto ya kukaribisha matatizo pale unapokuwa na fedha. Hiki ni kitu ambacho kimekuwa kinatokea kwa watu wengi, wakati huna fedha huoni kabisa matatizo, lakini unapozishika fedha ndiyo matatizo yanajipanga kwa foleni, unajikuta fedha yote uliyopata imeishia kwenye matatizo, ambayo hata hukuwa nayo awali. Nimewahi kumsikia mtu akisema, watoto wake huwa wanaumwa kila mwisho wa mwezi, pale anapopokea mshahara wake. Ni tatizo kubwa ambalo limewazuia wengi kuweza kufanyia kazi malengo ya maisha yao.
http://www.amkamtanzania.com/p/kuwa-tajiri.html
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA PICHA AU MAANDISHI HAYA.

Sasa leo tunakwenda kumalizana na tatizo hili ili tuweze kupunguza vikwazo kwenye safari yetu ya mafanikio. Kabla hatujaanza kujadili ni hatua zipi za kuchukua ili kuondokana na tatizo hili, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusu hili;
Sema kweli mimi nikipata pesa ili nianzishe biashara yangu ndipo matatizo yanajitokeza na kujikuta natumia fedha yote kwenye matatizo hao, nifanyeje! Chacha N. W.
Changamoto anayopitia msomaji mwenzetu ni changamoto ambayo imewasumbua wengi na kuwazuia kufikia mafanikio kwenye maisha yao. Je tunawezaje kutatua changamoto hii ili tuweze kuishi maisha ya ndoto zetu?

SOMA; Kanuni Sita(6) Muhimu Za Kushinda Tatizo Lolote Unalokutana Nalo.

Hapa nakushirikisha mambo matatu muhimu kufanya ili kuondokana na changamoto ya kuwa na matatizo pale unapopata fedha.

Jambo la kwanza; acha kuyakaribisha matatizo.

Unaweza kushangaa, lakini ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya matatizo unayoyapata wakati unapokuwa na fedha unakuwa umeyakaribisha mwenyewe. Kwa sababu hakuna namna nyingine kwa ni i ukiwa huna fedha huoni matatizo, ila ukizishika tu matatizo lukuki yanajitokeza.

Na hii yote inaanzia kwenye akili yako, unapokuwa huna fedha, unapokutana na matatizo yanayohitaji fedha huhangaiki nayo kwa sababu huna fedha. Mengi unayapotezea na mengine kuyavumilia, kwa sababu huna njia ya kuyatatua. Ila pale unapokuwa na fedha, matatizo yale yale ambayo uliyapotezea na kuyavumilia ulipokuwa huna fedha yanapotokea tena, huyavumilii, badala yake unayatekeleza mara moja. Kwa njia hii unakuwa umeiweka akili yako kwenye hali ya kuangalia matatizo ya kutatua pale unapokuwa na fedha.

Sasa si unakumbuka kwamba tunapata kile ambacho tunakitafuta? Hivyo akili yako inakutii na kukuletea kile ambacho unatafuta, unapokuwa na fedha. Ukiwa huna fedha mtu akikueleza matatizo yake unayachuja sana ikiwa anahitaji msaada wako kweli au la. Mara nyingi unakuta hana uhitaji mkubwa sana. Ila unapokuwa na fedha mtu akikueleza tu tatizo lake unakimbilia kulitatua, hata bila ya kufikiri kwa kina ili kuona kama tatizo hilo linahitaji msaada wako kwa haraka kiasi hicho.

Hatua ya kuchukua ili kuondokana na hali ya kukaribisha matatizo ni kuepuka kuwa na viwango tofauti kwa tatizo moja pale unapokuwa una fedha na usipokuwa na fedha. Chunguza kila tatizo kama kweli linahitaji kutatuliwa kwa uharaka au linaweza kusubiri.

SOMA; Mambo 6 Yakukusaidia Kujua Shughuli Iliyokuleta Duniani.

Jambo la pili; fedha zisikubadilishe tabia.

Kuna watu ambao wakiwa hawana fedha na wakiwa nazo utawajua. Wakiwa hawana fedha utawakuta wamenyong’onyea, wanawahi kurudi nyumbani, hawaonekani kwenye maeneo yao ya kawaida. Kwa kifupi wanakuwa kama wana msiba. Lakini subiri pale wanapozikamata fedha, kila mtu atajua kabisa kwamba sasa wana fedha, atakuwa mchangamfu, ataonekana sehemu za matumizi na wengine kusema hadharani kwamba fedha wanazo.

Hali kama hii huwakaribisha watu ambao huenda hawana matatizo makubwa sana, lakini kwa kuwa wanaona una fedha, basi wanaleta matatizo yao. Kwa njia hii unajikuta unatoa fedha ili kuwasaidia. Muda wote hawakukuletea matatizo yao kwa sababu walijua huna fedha, hivyo hawatapata msaada. Sasa unaona, waliweza kuyavumilia matatizo hayo, ila kwa kuwa wamekuona unajionesha kuwa na fedha, basi na wao wanakuja na matatizo na amhitaji yao.
Hii inatokea kwa wale watu ambao ni wa karibu sana kwako, hivyo huwezi kuwakatalia.

Namna ya kuondokana na hili ni kuacha kuendeshwa na kubadilishwa tabia na fedha. Unahitaji kuwa mtu yule yule nyakati zote, iwe una fedha au huna. Kwanza kabisa usiruhusu mtu aweze kujua kama una fedha au huna kwa kuangalia tabia zako. Jijengee nidhamu ya fedha kwa kudhibiti matumizi yako na wale wanaokuzunguka watakuletea zile shida ambazo ni kubwa kweli, na siyo shida ndogo ndogo ambazo hata wao wenyewe wangeweza kuzitatua.

SOMA; TATIZO SIO FEDHA, TATIZO NI WEWE…..

Jambo la tatu; kuwa na fedha za dharura.

Kwa hayo mawili tuliyojadili hapo juu, hayaondoi yale matatizo ambayo ni makubwa na yanatuhitaji kuyachukulia hatua. Pale ambapo mtu kweli anaumwa na anahitaji kutibiwa, au kuna dharura imetokea na inatakiwa kutatuliwa. Hapa ndipo unahitaji kuwa na fedha za dharura. Fedha hizi utazitumia kwenye nyakati za dharura kweli, pale ambapo umepata tatizo au changamoto kubwa na inahitaji kutatuliwa haraka.

Hakikisha unakuwa na utaratibu wa kutenga fedha ya dharura kwenye kila kipato unachopokea, usitumie fedha mpaka iishe yote, tenga fungu la dharura. Unaweza kutenga angalau asilimia kumi ya kipato chako kila mwezi au kila unapopata kama sehemu ya dharura. Kwa njia hii matatizo yanayotokea hayataingilia ratiba zako.
Hayo ndiyo mambo matatu muhimu kuzingatia ili kuepuka matatizo kukunyemelea pale unapopata fedha. Yafanyie kazi ili kuzuia matatizo kuwa kikwazo cha wewe kutimiza ndoto zao kwenye maisha.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Njia Muhimu Za Kumfanya Mtoto Wako Ajione Wa Pekee.

$
0
0
Kwa wale ambao ni wazazi bila shaka wanajua malezi bora ni kitu cha msingi sana katika makuzi ya mtoto. Na malezi haya bora huwa hayaji tu kwa bahati mbaya, bali hujengwa hatua kwa hatua kwa kadri jinsi mtoto anavyokua.
Kwa kujua umuhimu wa hilo, hebu leo kupitia makala haya tuangalie hatua nyingine muhimu ya malezi kwa kujifunza njia nyingine za kumfanya mtoto wako ajione ni wa pekee. Je, njia hizi ni zipi? Fuatana nami kujifunza kupitia makala haya.
1. Tenga muda wa kua nae pamoja.
Unaweza ukamfanya mtoto wako akajiona wa pekee kwa kutenga muda wa kuwa nae. Muda huu unaweza kuutenga kwa kuwa na mtoto wako jioni unapokuwa  nyumbani au wakati mwingine kutembelea maeneo kama ‘beach’, mbuga za wanyama au makumbuso.

Kwa hiki kipindi kinakuwa ni muhimu sana kwako na mtoto wako kwa sababu, hapa mtoto anakuwa anajifunza mambo mhumu kutoka kwako. Kwa kifupi, hiki ni kipindi muhimu kwa mtoto kwa sababu anakuwa anajihisi ni wa pekee sana kwa kuona anajaliwa zaidi na wazazi, hasa kwa kuwa karibu nao.
2. Msikilize kile anachokisema.
Kuna wakati watoto wetu huwa wanapenda sana kutoa maoni yao. Inapotokea mtoto wako anakupa maoni ya kitu fulani, msikilize kile anachokisema, kisha msifie hata kama hayupo sahihi, lakini baada ya hapo kama ni kweli hayupo sahihi, chukua jukumu la kumrekebisha.
Kwa kufanya hivi kutamfanya mtoto wako atakuwa anakushirikisha mambo mengine mengi na kujiona wa pekee. Hiyo itamuongezra nguvu kubwa ya kujiamini kadri siku zinavokwenda. Na kwa mwendo huo unakuwa umemtengenezea ujasiri mkubwa utakao dumu kwa baadae.
3. Jali kile anachokijali mtoto wako.
Ikiwa moto wako anaonyesha anajali mchezo wa aina fulani, muunge mkono kama mchezo huo ni wa maana. Haimaanisha kujali huku, ujali kila kitu hapana. Kama pengine mchezo huo hauna maana mweleze na umtafutie kitu kingine.
Ili kuonyesha unajali zaidi, endelea kumdadisi ni kitu gani kingine anapenda au ni mchezo gani mwingine anaoupenda. Hapa utakuwa unamfanya mtoto wako azidi kujiona ni wa pekee kwako mzazi kwa kuwa unajali hisia zake na unazielewa.
 4. Mtengenezee utamaduni bora.
Pia njia nyingine ya kumfanya mtoto wako ajione wa pekee ni kule kumjengea utamaduni wako unaoupenda. Pengine unajiuliza ni utamamduni wa naman gani sikiliza, unaweza kujengea utamaduni wa kujiamini na kufikiri chanya.
Utafanikisha hili ikiwa utakuwa una mpa moyo na nguvu kwa yale anayoyafanya. Hiyo haitoshi kama anauwezo wa kusoma vizuri, unaweza ukampa vitabu vizuri vya kusoma vinavyozungumzia mambo chanya.
5. Muulize mambo muhimu.
Pia mjengee mtoto wako utaratibu wa kumuuliza mambo muhimu. Kwa mfano, ‘unapenda nini mwanangu, ukiwa mkubwa unataka kufanya nini,’ na mengineyo mengi maswali ya kidadisi. Hii itakuwa ni njia nzuri pia ya kumfanya toto wako afikiri vizuri na upya.
Kwa kuhitimisha, hizo ni baadhi ya njia ambazo unaweza ukazitumia na kumfanya mtoto wako ajione wa pekee na kufurahia maisha kwa ujumla.
Endelea kutembelea www.amkamtanzania.com kujifunza kila siku.

Ni wako rafiki,

Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,


UCHAMBUZI WA KITABU; NOTES FROM A FRIEND, Mwongozo Wa Kushika Hatamu Ya Maisha Yako.

$
0
0
Anthony Robbins ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ameyatoa maisha yake katika kuwasaidia wengine kufikia maisha ya ndoto zao. Yeye mwenyewe ameanzia kwenye mazingira magumu ambayo yalimpa hamasa ya kuweka juhudi ili kuwa na maisha bora. Aliweza kutoka kwenye mazingira magumu na kujitoa kuwafundisha na kuwahamasisha wengine ili nao waweze kuwa na maisha bora. Tony amenadika vitabu kadhaa kwenye eneo la maendeleo binafsi ya mtu, na pia amekuwa akiendesha semina ambazo zimeleta mabadiliko kwa wengi.
Katika kitabu chake tunachokwenda kuchambua leo, NOTES FROM A FRIEND, Tony anatushirikisha yale muhimu ambayo amekuwa akiyaandika na kuyahubiri kwenye semina zake. Ni mambo mazuri ambayo mtu yeyote akiyazingatia anaweza kubadili maisha yake.


Tony Robbins amekuwa akisimamia falsafa moja kwenye maisha yake, falsafa hiyo anaiita CANI, kifupi cha CONSTANT AND NEVER ENDING IMPROVEMENT, ikiwa na maana kwamba maboresho yasiyokuwa na kikomo. Hii ina maana kwamba kama unataka kuwa na maisha mazuri na ya ndoto yako, basi unahitaji kuwa bora kila siku ya maisha yako. Hii ndiyo kazi kubwa ambayo tumekuwa tunaifanya kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, kuhakikisha kila siku kwetu inakuwa bora sana.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Wahitimu Wa Elimu Ya Juu Mwaka 2016, Ukweli Ambao Umekuwa Unafichwa Kwa Miaka 20 Iliyopita.

Karibu kwenye uchambuzi wetu wa kitabu hiki ili tuweze kujifunza yale ambayo yatakwenda kubadili maisha yetu.

1. Njia pekee ya kujihakikishia furaha kwenye maisha yako ni kuwasaidia wengine kuwa na furaha kwenye maisha yao. Elewa vizuri hapo, siyo kuwafurahisha, bali kuwawezesha kuwa na furaha. Hakuna anayeweza kumpa mtu mwingine furaha, furaha zinaanza na sisi wenyewe. Hivyo chochote unachofanya kwenye maisha yako, hakikisha kinayafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi, watakuwa na furaha na wewe utakuwa na furaha.

2. Ili kuwa na maisha bora, ili kujihakikishia kipato kwenye jambo lolote unalofanya, kila siku jiulize swali hili; ni kwa njia hani naweza kuongeza thamani kwenye maisha ya wengine? Iwe ni kwenye biashara au kazi, ukijiuliza na kujibu swali hilo, na kisha kufanyia kazi majibu yako, utafanya kilicho bora na utafurahia maisha yako, na kipato chako kitakuwa kizuri mara zote. Mafanikio yetu yapo kwenye mafanikio ya wengine, ukiona hufanikiwi jua kwamba hujawawezesha wengine kufanikiwa au kuwa na maisha bora, anza na swali hilo kila siku.

3. Kufikiri chanya ni hatua moja muhimu kwenye kuwa na maisha ya mafanikio, lakini kufikiri chanya pekee hakutoshi kukufanya wewe uwe na maisha bora, unahitaji kuchukua hatua, na siyo hatua ndogo, bali hatua kubwa. Unahitaji kufikiri chanya, na wakati huo ukiwa na mipango na mikakati ya kufikia malengo yako kwenye maisha. Maisha yako hayatabadilika kwa kufikiri pekee, bali kwa kuchukua hatua za kuyabadili. Ni hatua gani unachukua kwa sasa ili kuboresha maisha yako?

4. Mabadiliko makubwa unayotaka kufanya kwenye maisha yako, yamegawanyika kwenye maeneo haya mawili muhimu;
Moja; unataka kubadili hisia zako juu ya vitu au maisha yako. kuna namna ambavyo unahisi au kufikiri maisha yako ambayo huipendelei, hivyo unataka kubadili hisia hizo.
Mbili; unataka kubadili matendo yako, unataka kufanya kitu cha tofauti na unachofanya sasa, unataka kubadili tabia ambayo unayo sasa.
Changamoto kubwa ni kwamba japokuwa kila mtu anataka kufanya mabadiliko kwenye maisha yake, ni wachache sana wanaoyafanya kweli, na katika hao wachache, ni wachache zaidi wanaodumu na mabadiliko hayo.

5. Jana yako siyo sawa na kesho yako. Watu wengi wamekuwa wakijikatisha tamaa ya kuchukua hatua kubwa ya kubadili maisha yao kwa sababu ya historia zao za nyuma. Kwa sababu huko nyuma walijaribu kufanya vitu wakashindwa, au kwa sababu wametokea mazingira mabovu, huwa wanaona hawawezi. Unachotakiwa kukumbuka ni kwamba haijalishi jana yako ilikuwaje, kesho ni siku nyingine tofauti, ambayo una uhuru wa kufanya chochote utakacho.

6. Ung’ang’anizi unalipa, na hii ndiyo sifa pekee inayowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Utawasikia walioshindwa wakikuambia nimejaribu sana lakini sijaweza, lakini ukihesabu mara walizoshindwa huenda ni mara tano au kama ni sana basi mara kumi. Kuna watu walijaribu zaidi ya mara elfu moja ndiyo wakapata walichotaka, na hawa ni wengi mno katika wale waliofanikiwa. Hivyo kama hujajaribu zaidi ya mara elfu moja, usituambie kwamba umejaribu mara nyingi ukashindwa, endelea kung’ang’ana na utapata unachotaka.

SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

7. Pamoja na kwamba unahitaji kuwa king’ang’anizi ili kufanikiwa, haimaanishi kwamba uendelee kufanya kitu kile kile ambacho umekuwa unafanya kila siku. Badala yake unahitaji kuboresha kadiri unavyokwenda, kila unapofanya na kushindwa, jifunze ni kipi unakosea na fanya marekebisho. Wanasema ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa njia ile ile na kutegemea matokeo tofauti, usiwe mjinga, kuwa king’ang’anizi kwa kujifunza na kuboresha zaidi.

8. Tony anatupa ujumbe mmoja muhimu sana, ambao anashauri sana tutoke nao kwenye kitabu hiki na tuufanyie kazi, ujumbe huu ni kuchukua hatua KUBWA na kwa mwendelezo. Iko hivi, watu wengi wamekuwa hawachukui hatua, na wale ambao wanachukua hatua wanachukua hatua ndogo sana kiasi kwamba hata wakipata matokeo hayawi bora kwao. Ila pia wale ambao wanachukua hatua hawana mwendelezo, wanaanza baadaye wanashindwa kuendelea au wanakata tamaa. Sasa sikia rafiki, unapoamua kuchukua hatua, CHUKUA HATUA KUBWA NA KWA MWENDELEZO, usiwe mtu wa kugusa na kuacha, kuwa mtu wa kuendeleza kile ulichoanza.

9. Ili uweze kuchukua hatua za kubadili maisha yako na kuwa bora zaidi, unahitaji kufanya MAAMUZI, sasa hili neno maamuzi limekuwa linatumia kirahisi sana mpaka watu wanaona kuchukua maamuzi ni kitu ambacho hakina uzito. Na wengine hawajawahi kuchukua maamuzi kwa muda mrefu mpaka wamesahau maana halisi ya kuchukua maamuzi. Tony anatuambia kwamba unapofanya maamuzi, maana yake unaamua hiyo ndiyo njia unayochukua, na hakuna cha kukurudisha nyuma, haijalishi unakutana na nini. Unapofanya maamuzi maana yake unaweka kila sababu pembeni na kuweka kila ulichonacho kwenye kile ulichoamua.

10. Maamuzi yanayofanyiwa kazi ni yale ambayo yanaaminiwa. Hivyo unahitaji kuwa na imani kwenye kile ambacho unakifanya, kama huna imani, hakuna chochote utakachofanya kikakusaidia. Kwa sababu unapokosa imani unaifunga akili yako, hata kitu ambacho kipo wazi kabisa, wewe hutakiona. Hivyo kuwa na imani kwamba unaweza na pia kile unachotaka kinawezekana, kwa njia hii utafungua akili yako na utaziona fursa nyingi.

11. Kwenye safari ya mafanikio hakuna kitu kinaitwa KUSHINDWA, Badala yake kuna kitu kinaitwa KUJIFUNZA. Kama umefanya kitu na ukapata matokeo tofauti na uliyotegemea, hujashindwa, badala yake umejifunza njia ambayo haifai, hivyo unaporudia tena, usitumie njia uliyotumia awali. Ukiwa na mtazamo huu, kamwe huwezi kukata tamaa. Lakini pale unapofikiria kukosa unachotaka ni kushindwa, utakosa nguvu ya kuendelea na mapambano.

12. Mafanikio ni matokeo ya kufanya maamuzi bora, kufanya maamuzi bora ni matokeo ya uzoefu tulionao, na uzoefu tulionao unatokana na maamuzi mabovu tuliyofanya. Hivyo usijilaumu kama unafanya maamuzi mabovu kwa sasa, unayahitaji ili uwe na uzoefu wa kuweza kufanya maamuzi mazuri. Jifunze kwenye kila kitu unachofanya, jifunze kwenye kila hali unayopitia na tumia uzoefu huo kufanya maamuzi bora zaidi.

SOMA; KITABU CHA MAY; Biashara Ndani Ya Ajira; Jinsi Ya Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa.

13. Ili kubadili maisha yako yaweze kuwa bora kabisa kuanzia leo, unahitaji kufanya maamuzi haya mawili, leo hii na siyo kesho. Yaani fanya maamuzi haya sasa hivi;
Moja; fanya maamuzi madogo ambayo ni rahisi kwako kufuata kila siku. isiwe kitu kigumu au kikubwa ambacho kinakuhitaji ufanye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. maamuzi haya madogo, yatabadili maisha yako kadiri unavyofanya kila siku.
Mbili; fanya maamuzi makubwa, ambayo yanakuhamasisha kuchukua hatua kubwa. Maamuzi haya yanakuwa ya kile kitu kikubwa unachotaka kwenye maisha yako.
Ni muhimu kuwa na maamuzi haya mawili, kwa sababu yale madogo yatakupa ushindi wa kila siku, na yale makubwa yatakupa matumaini ya siku zijazo. Kila siku chukua hatua kufikia maamuzi uliyojiwekea.

14. Kule unakopeleka mawazo yako ndiyo chanzo cha furaha au huzuni kwenye maisha yako. watu wenye huzuni na wanaokata tamaa ni wale ambao wanafikiria mambo mabaya wakati wote. Wao kwenye maisha yao wanaona mambo mabaya pekee, wanatumia muda mwingi kufikiria mambo hayo mabaya na hii inawakatisha tamaa. Wale ambao wanakuwa na furaha na hamasa ya kufanya zaidi wanaona mazuri kwenye maisha yao, wanatumia muda mwingi kufikiria hayo mazuri. Hivyo unapojikuta kwenye hali ya huzuni na kukata tamaa, jiulize ni maeneo gani ya maisha yako umekuwa unayafikiria kwa muda mrefu, kama unafikiria mabaya, lazima utakuwa na huzuni na kukata tamaa.

15. Kubadili hisia zako na mawazo yako, anza kwa kubadili mwili wako. Kama umekaa kizembe, utakuwa na hisia mbaya na kuwa na mawazo ya huzuni na kukata tamaa, lakini kama umekaa kikakamavu, unakuwa na hisia nzuri na kuwa na hamasa. Tony anatuambia, kulingana na tafiti zilizofanywa, tunaweza kubadili hisia zetu na mawazo yetu kwa kubadili miili yetu. Hivyo kama umekaa mahali na unaanza kuona unakuwa na mawazo na hisia hasi, nyenyuka na anza kufanya mambo yanayoashiria ushujaa. Unaweza kutembea au kuruka au kufanya chochote kinachochangamsha mwili wako. Kuna namna ya kutembea, kuongea na hata muonekano wa nje ambao unaendana na maisha ya mafanikio. Jua namna hizo na zijenge kwenye maisha yako.

16. Maneno tunayojiambia na kuwaambia wengine kila siku yana nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu, hivyo ni muhimu uyachague maneno yako kwa uangalifu. Unahitaji kutumia maneno ambayo yanaashiria mafanikio na maneno hayo yatakufanya ufikiri kwa mafanikio muda wote. Kwa mfano mtu akikuuliza unajisikiaje, usimwambie tu unajisikia vizuri au unajisikia kawaida, mwambie unajisikia vizuri sana, au hujawahi kujisikia bora kama wakati huo. Kwa njia hii hata kama hujisikii bora, utalazimika kujisikia bora. Mara zote tumia maneno yanayoashiria mafanikio, na utalazimisha akili yako kuona mafanikio.

17. Jinsi unavyoiona dunia, jinsi unavyoyaona maisha , ndivyo unavyotengeneza maisha yako. Kuna ambao wanaona maisha ni vita, hivyo kila mtu anapambana na mwingine, mtu huyu atalazimika kupambana na wengine ili kupona. Kuna ambao wanaona masiha ni mchezo, hivyo wanacheza sehemu yao ili kupata wanachotaka. Dunia moja lakini tuna mitazamo tofauti, hakikisha wewe una mtizamo utakaoendana na maisha unayotaka.

18. Hatua ya kwanza kabisa ya kufanikiwa kwenye maisha yako, ni kuweka malengo. Tumekuwa tunawaona watu ambao wamefanya makubwa, ambayo wengi hawajaweza kufanya, na mara nyingi tumekuwa tunashawishika kwamba watu hawa wana bahati, au walikuwa sehemu sahihi kwa wakati sahihi. Lakini ukweli ni kwamba watu hawa walikaa chini na kuweka malengo jua ni i wanataka kwenye maisha yao, na wakafanyia malengo hayo kazi na hatimaye kuyafikia. Je wewe una malengo gani? Je umeyaandika malengo hayo? Unayafanyia kazi kila siku?

SOMA; Mambo Kumi (10) Kuhusu Maisha Na Mafanikio Niliyojifunza Kutoka Kwa Edward Ngoyai Lowassa.

19. Usijiwekee kikomo kwenye uwezo wako na kile unachofanya. Mara nyingi sisi wenyewe tumekuwa tunajizuia kufanikiwa, kwa kujiambia kwamba hatuwezi kufanya makubwa, au kwamba tutashindwa. Leo jiulize swali hili; kama ungehakikishiwa kwamba huwezi kushindwa kwenye kile ambacho umechagua kufanya, je ungefanya nini? Hofu ya kushindwa imekuwa inatuzuia kuziendea ndoto zetu. Hebu weka hofu hii pembeni, hebu weka vikwazo hivyo pembeni na ona maisha yako kwa picha tofauti kisha chukua hatua.

20. Zoezi la siku kumi; kwa siku kumi, kuanzia kesho, dhibiti mawazo yako na hisia zako. Usikubali kabisa kufikiria jambo lolote hasi, wala usitoe maneno yoyote hasi, usilalamike wala kulaumu mtu yeyote. Zifanye siku kumi zijazo kuwa siku za wewe kuwa chanya na kuchukua hatua, na siyo kujishusha na kujikatisha tamaa. Ikiwa siku yoyote katika siku hizo kumi utajikuta umefikiri au kusema kitu hasi, basi kesho yake anza upya, fanya hivi mpaka utakapoweza kwenda siku kumi bila ya kuwa hasi. Fanya zoezi hili na utaona jinsi ambavyo amisha yako yanaweza kubadilika kwa nafasi kubwa.
Haya ndiyo mambo muhimu tunayapata kwenye kitabu cha rafiki yetu Anthony Robbins, yafanyie kazi ili kuboresha maisha yako zaidi.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>