Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

KITABU CHA JULY; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

$
0
0
Habari rafiki?
Karibu kwenye utaratibu wetu wa kujisomea vitabu ambapo kila mwezi kunakuwa na kitabu kimoja cha kujisomea. Kupitia vitabu hivi tunapata maarifa na hamasa ambayo inatuwezesha kuweka juhudi zaidi kwenye kile tunachofanya ili tuweze kupata matokeo bora na kufikia mafanikio makubwa.

Mwezi huu wa saba tunakwenda kusoma kitabu MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu. Kitabu mimi ni mshindi kinakuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi, maisha ambayo yanakutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanashindwa kufikia mafanikio makubwa.

Ukiangalia maisha ya washindi na maisha ya wale ambao wanashindwa yapo tofauti kabisa. Kuna namna ambavyo washindi wanachukulia mambo yao, wanavyotumia muda wao, wanavyotengeneza mahusiano yao na pia wanavyoshirikiana na wengine. Washindi wana njia tofauti za kuweka malengo ambayo wanayafikia na hivyo kuendelea kuwa washindi.
Kwa bahati mbaya sana maisha haya ya ushindi huwa hayafundishwi kwenye jamii zetu wala kwenye mfumo wetu wa elimu. Na hata wale wachache ambao wameweza kufikia ushindi, siyo wote ambao wana hamasa ya kuweza kuwashirikisha wengine mbinu zao. 

Kwa kukosa maarifa haya muhimu watu wengi wamekuwa wanafanya makosa ya wazi ambayo yanawazuia kufikia ushindi. Vitu kama uaminifu, matumizi mazuri ya muda, kuwa na shukrani ni vitu ambavyo kwa kawaida huwa hatuvipi uzito, lakini ndiyo vitu vyenye umuhimu mkubwa sana.
Kupitia kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI utajifunza mbinu zote za mafanikio na kazi yako inabaki kuzitumia kwenye maisha yako ili uweze kuwa na maisha ya ushindi.

Mambo gani mapya yaliyopo kwenye kitabu hiki?
Kama umekuwa ukisoma vitabu na makala ninazoandika, utakuwa unajua namna vitabu ninavyoandika vilivyo, sasa kitabu hiki kina haya ya ziada ambayo yatakupa maarifa zaidi na hamasa pia;

1. Kuna shuhuda za watu ambao wameshiriki mafunzo ya semina niliyotoa ya MIMI NI MSHINDI, wakielezea jinsi ambavyo mafunzo waliyopata yamebadili mtazamo wao kuhusu maisha yao na hatua wanazokwenda kuchukua. Kwa kusoma shuhuda hizi utaona ni jinsi gani inawezekana na kwako pia.

2. Kuna mifano halisi ya jinsi ambavyo mimi binafsi nimekuwa natumia mbinu hizi za ushindi unazokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki na zikaniletea matokeo bora. Siishii tu kukuambia mbinu hii ni nzuri, bali nitakuonesha nimewezaje kuitumia mimi binafsi na kuweza kupata matokeo mazuri.

3. Kwenye kila sura kuna zoezi la wewe kufanya, hivyo unapomaliza kusoma sura moja ya kitabu hiki kuna zoezi utapewa la kufanya, zoezi hili linakuwezesha wewe kutumia kile ulichojifunza kwenye maisha yako. hutaishia kuwa na maarifa ya juu juu, badala yake utakuwa na namna ya kuyatumia maarifa hayo ili kupata matokeo bora.

4. Kitabu hiki kimeandikwa kwa nafsi ya kwanza, yaani kitabu kizima ni kama unajiambia wewe mwenyewe. Bada ya jina la kitabu kuwa WEWE NI MSHINDI, kwamba mimi nikuambie wewe, unajiambia wewe mwenyewe kwamba MIMI NI MSHINDI, na kitabu chote kipo hivyo, karibu kila kitu utakuwa unajiambia mwenyewe. Hii ina matokeo bora sana kisaikolojia kwa sababu inasisitiza umiliki wa kile unachojiambia.

5. Mwisho wa kitabu hiki kuna TAMKO KUU LA USHINDI, hapa unajipa tamko la ushindi ambalo lina misingi 20 utakayoisimamia. Kwa kujiambia tamko hili na kulirudia kila siku unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanyia kazi yale uliyojifunza.
Kitabu hiki ni kizuri sana kwako kukisoma, kwani kitakufanya wewe ujishauri mwenyewe njia bora kwako kuchukua ili kufikia ushindi.

Kitabu hiki kinawafaa watu gani?
Kila kitabu kina watu wake, na hakuna kitabu kimoja ambacho kinamfaa kila mtu. Hivyo na kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI ni kwa wale ambao wanataka kuishi maisha ya ushindi, wale ambao wanataka kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Na mafanikio siyo kifedha pekee, bali kwenye kila eneo la maisha.

Wale ambao wamesharidhika na pale walipo, au wameshajiona wanajua kila wanachotaka kujua, kitabu hiki hakiwafai.

Pia wale ambao hawataki kuwa na maisha ya ushindi, wameshakubali kwamba wao ni wa chini na hakuna kinachoweza kuwatoa pale walipo kitabu hiki hakiwafai.
Lakini wale ambao wamekutana na changamoto kwenye maisha yao na wanaelekea kukata tamaa na kuona mambo hayawezekani, hiki ni kitabu kimoja wanachohitaji kukisoma haraka na kisha kurudi kwenye mapambano yao. Kwa sababu kupitia kitabu hiki utajifunza ni nini kimekufikisha hapo ulipo na namna gani ya kutoka hapo.

Mfumo wa kitabu na namna ya kukipata.
Kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI kipo kwenye mfumo wa softcopy (nakala tete) ambayo unaweza kusomea kwenye simu yako ambayo umekuwa unatumia kusomea makala za AMKA MTANZANIA. Pia unaweza kusomea kwenye tablet kama unayo na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta kama unapendelea hivyo. Hii ni njia rahisi ya kujisomea vitabu na kuweza kutembea navyo popote unapokwenda.
Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email na hivyo unaweza kukipata popote ulipo duniani bila hata ya kutoka hapo ulipo.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=). Kupata kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI, tuma fedha tsh elfu 10 kwa MPESA 0755953887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717396253 Majina kwenye namba hizo ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo yenye jina la kitabu MIMI NI MSHINDI pamoja na email yako na utatumiwa kitabu.

Karibu sana tuongeze maarifa kwa pamoja ili tuweze kuishi maisha ya ushindi yatakayotuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye kila tunachofanya.
Kumbuka chochote unachotaka kwenye maisha yako kinaanza na wewe mwenyewe. Na ili uweze kuanzisha kile unachotaka unahitaji maarifa sahihi ya kufanya hivyo na sehemu mojawapo ya kupata maarifa haya ni kujisomea vitabu.

Nakutakia kila la kheri katika kutumia maarifa utakayoyapata kwenye kitabu hiki.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Umuhimu Wa Kujenga Tabia Ya Kusamehe Mapema.

$
0
0
Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio.

Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao. Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo.

Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya leo, kesho mpaka kesho kutwa usiweze kuyasahau. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress).


Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Usipo msamehe mtu kunakupelekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama katika dimbwi kubwa la mawazo.


Hata hivyo mawazo hayohayo yanakupekea kujikita katika tabia zisizo za kimaadili kwa mfano ulevi, wizi na mengineyo mengi. Na pindi mtu atendapo  mambo hayo ambayo chanzo chake huwa ni mawazo madhara yake huwa ni makubwa kama nilivyoweza kuanisha hapo juu.

Basi bila kupata kigugumizi cha kusoma makala hii hebu jaribu kusoma kwa umakini na uingie  katika kilindi cha nafsi yako harafu jiulize umebeba vitu gani juu ya watu wengine? Kisha jaribu kutafakari kwa umakini tena mambo hayo yamekuathiri kwa kiwango gani?

Baada ya kupata majibu sahihi juu ya jambo hilo, zama tenda katika mishipa ya ubongo wako kisha tafakari bila ya kujionea huruma ya kwamba unachukua hatua gani juu ya swala hilo. Majibu sahihi ambayo utakuwa umeyatafakari ndiyo ambayo yatakufanya uweze kuona mwangaza kwenye giza ni wapi ambapo unatakiwa kuelekea.

Pasipo kupoteza maana ya somo hili nieleze sasa ni kwa nini ni muhimu kusamehe;

1. Huongeza furaha ya moyo (piece of mind).

Kusamehe mtu mwingine humfanya mtu huyo kuwa huru kwa kila jambo ambalo analifanya. Kwani kama nilivyosema hapo awali ya kwamba watu wengi tumebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zetu, hata hivyo kutoka na mizigo hiyo mizito tunashindwa kupiga hatua za kimafanikio.

Hivyo ili kuweza kupiga hatua za kimafanikio hatuna budi kuweza kujifunza kuweza kuwasemehe watu wengine waliowahi kutokosea . Hata vitabu vya dini vinatukumbusha ya kwamba Mungu tabia yake kusamehe, hivyo nasi hatuna budi kusamehe wengine. Vitabu hivyo hivyo vya dini vinasema ya kwamba samehe  saba mara sabini. Na endapo utasamehe unafungua milango ya mafanikio yako.

Jifunze kusamehe.
2. Kusamehe ni njia ya mafanikio.

Endapo leo utaamua kusamehe ni ishara ya kwamba utaonekana katika sakata la kuwa katika wimbi la mawazo , hata hivyo kupelekea wewe kuwa na mawazo chanya, mara kadhaa watu ambao hawana ule moyo wa msamaha kwa namna moja ama nyingine huwa hawapo sawa kwani huwa hawana amani hata kidogo.


Hata hivyo kama kweli uyataka maisha yawe sawa ni muda wako sahihi wa kuvutua vile vyote vilivyomo katika nafsi yako kinyume cha hapo utakuwa unapotea hajalishi ulikwazika kwa kiasi gani. Pia ukumbuke wabaya watu, pia watu hao hao ndio wazuri na wana mchango mkubwa katika safari yako ya mafanikio.


3. Kusamehe huimarisha afya.

Afya njema ni njia ya kupata Mafanikio, moja ya kanuni ya kutaka kupata mafanikio ni kwamba unahitaji kuwa na afya njema ili uweze kuimarika na kupata Mafanikio hayo. Hebu tutafakari kidogo hivi leo ukipata ugonjwa wowote na kukufanya usiweze kuendelea na kazi yako hivi huwa unaathirika kwa kiasi gani katika jambo lako? Kama umepata majibu nafikiri utakuwa umeona umuhimu wa  kuwa na afya njema.

Watu wengi hawana hamasa za kiutendaji wa mambo mbalimbali kwani dhahiri ya kwamba miili yao tayari imeathiriwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na mawazo ambayo yamesabishwa na watu wanaokuzunguka.


Kuna magonjwa ambayo Mara nyingi husababishwa na mawazo kama vile pressure. Hivyo endapo utamua kuwasamehe watu wengine ambao waliwahi kukosea unaweza kuwa katika misingi ya kuimarika kiafya kiujumla, na kufanya hivyo kutakufanya uweze kuongeza uwezo wako wa kufikiri hata kukupelekea kuweza kupiga hatua za kimafanikio.

Hivyo tambua na elewa inahitajika nguvu ya msamaha ambayo leo itakufanya uweze kupata Mafanikio ya kweli.

Makala hii imeandikwa na Afisa mipango; Benson Chonya

UCHAMBUZI WA KITABU; Sign-Posts On The Road To Success (Alama Muhimu Kwenye Safari Ya Mafanikio).

$
0
0
Hakuna mtu ambaye hapendi kufanikiwa, hakuna mtu ambaye anataka maisha yake yawe magumu siku zote, kila siku awe mtu wa kuteseka na kuhangaika. Lakini bado watu wengi wamekuwa hawayapati mafanikio licha ya kuyatamani sana. Sababu kubwa ya wengi kushindwa kufikia mafanikio licha ya kuyatamani ni kutokujua hasa ni kipi wanataka na pia kutokujua dalili kama wanaelekea kwenye mafanikio au la.
Hili ndilo lililomsukuma E. W. Kenyon kuandika kitabu sign-posts on the road to success. Kupitia kitabu hiki tunajifunza mambo yote muhimu kuhusu mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Karibu tujifunze kwa pamoja kupitia uchambuzi wa kitabu hiki;

1. Endelea kufanya. Kinachowatofautisha wale wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni uvumilivu kwenye kile wanachofanya. Kwa kila jambo ambalo mtu anafanya, changamoto na vikwazo huwa havikosekani. Wale wanaoshindwa huwa hawawezi kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo kukata tamaa. Wanaofanikiwa wanaendelea kung’ang’ana na hivyo kupata mafanikio.
Chochote ambacho umechagua kufanya, endelea kufanya hata kama mambo yanaonekana magumu kiasi gani. Hata usiku uwe na giza kiasi gani, kutakucha na jua litawaka tena, hivi ndivyo mafanikio yalivyo.

2. Kuwa bora zaidi ya wakati uliopita. Kila unapopata nafasi ya kufanya kile ambacho umechagua kufanya, hebu kifanye kwa ubora kuliko ulivyofanya wakati uliopita. Ongeza ubora zaidi na kamwe usifanye kwa mazoea. Unaweza kuongeza ubora kidogo sana lakini baadaye ukapata matokeo bora sana.
Mafanikio makubwa hayatokei kama ajali, bali yanatokana na vitu vidogo vidogo vilivyofanywa kwa muda mrefu.

3. Jitegemee wewe mwenyewe. Hakuna kinachowazuia wengi kufikia mafanikio kama kuwategemea wengine. Ili uweze kufanikiwa lazima uwe tayari kusimama mwenyewe, unawategemea wengine moja kwa moja kwa kila kitu ni kupoteza nguvu zako. Hutakuwa na uwezo wala uhuru wa kufanya kile ambacho unajua ni bora kwako.
Kuwa tayari kusimama mwenyewe, kuwa na nidhamu na jitume sana, hakuna kitakachokuzuia.

4. Kila kitu unachohitaji ili kufikia mafanikio makubwa tayari kipo ndani yako. unachohitaji ni wewe kuweza kujua kile ambacho unacho na kuweza kukitumia. Ndani yako kuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo ambayo wengine hawawezi kufanya, jijue vizuri na fanyia kazi kile ambacho kipo ndani yako.

5. Ufanye mwili wako kuwa mtumwa wako. Safari ya kufikia mafanikio siyo rahisi kama ambavyo wengi wanaota. Safari hii ni ngumu na mwili wako haupendi vitu vigumu, hivyo utajaribu kukufanya wewe uwe mtumwa wa mwili wako. Wewe utataka kuamka mapema ili kufanya yale ya muhimu lakini mwili wako utakudanganya ulale kidogo kwa sababu bado umechoka.
Kufanikiwa unatakiwa kuufanya mwili wako kuwa mtumwa wako, siyo wewe usikilize mwili bali mwili ukusikilize wewe na kufanya vile unavyotaka kufanya.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.

6. Ni wewe mwenyewe unayeweza kujiletea mafanikio makubwa.
Ni wewe mwenyewe unayeweza kujua ni kipi hasa unachoweza kukifanya.
Ni wewe mwenyewe utakayeweza kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hilo kwa ajili yako. wengine wanaweza kuanzisha tu moto, ila ni wewe unayetakiwa kuuchochea ili uendelee kuwaka.

7. Ipe akili yako mlo kamili. Mlo kamili wa akili yako ni maarifa sahihi yanayoendana na kile ambacho unafanya na unataka kufanikiwa. Jifunze mbinu bora za kufanya kile unachotaka kufanya, ifanye akili yako iweze kuzioana fursa na kuzitumia vizuri.
Watu wengi wamekuwa wanalisha akili zao uchafu ambao unazidumaza zaidi. Uchafu huu ni habari za udaku, kufuatilia maisha ya wengine, habari zenye hofu na mengine ambayo hayana manufaa.

8. Nidhamu binafsi ni kitu kimoja muhimu sana ambacho kitaamua kama mtu anafanikiwa au la. Bila ya nidhamu binafsi huwezi kupata mafanikio, na kama ukiyapata basi yatakuwa hatari sana kwako kuliko ambavyo ulikuwa kabla ya kufanikiwa. Ni muhimu ujijengee nidhamu binafsi ili uweze kujidhibiti na kufanya yale ambayo ni muhimu kwako.

9. Kuna wewe wawili, kuna wewe wa nje ambaye ndiye unaonekana kwa wengine na kuna wewe wa ndani ambaye hakuna anayekuona. Wewe wa nje anapenda sana kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, hata kama hakina manufaa kwake. Wewe wa ndani anajua kabisa ni nini anataka na kipi muhimu kwako kufanya. Tatizo huyu wewe wa ndani anazidiwa nguvu na wewe wa nje. Anza sasa kumsikiliza wewe wa ndani na kumpa nguvu kuliko wewe wa nje.

10. Weka maisha yako yote kwenye kile ambacho umechagua kufanya. Usijaribu kitu chochote kwenye maisha, ni kupoteza muda wako ambao ni muhimu na huna wa kutosha. Kama umeamua kufanya kitu, weka maisha yako yote kwenye kitu hiko, ona kwamba hiko ndiyo kitu pekee ambacho unataka kisimame kwa niaba yako, weka akili, moyo na maarifa yako yote kwenye kile unachofanya. Kwa njia hii hakuna kitakachokuzia kufikia mafanikio.

11. Mashirika makubwa yanawatafuta watu ambao wanaweza kuyaingizia faida. Watu wengi wanatafuta mtu anayeweza kuwatatulia changamoto za maisha yao. Je wewe unaweza kuwa mtu huyu ambaye anatafutwa na wengi? Siyo vigumu kuwa mtu huyu, unachohitaji ni kutoa matokeo ambayo ni bora sana, ambayo watu wengine hawawezi kuyatoa.

12. Usikubali kutumika maisha yako yote. Katika kipindi fulani kwenye maisha yako, utatumika na wengine, lakini usikubali kubaki hapo maisha yako yote. Usikubali wengine wakutumie wewe kutimiza ndoto zao huku wewe ukibaki kuwa kawaida. Jiwekee muda ambao utatumika na baada ya hapo anza kujitumia wewe mwenyewe.
Kama upo kwenye ajira unatumika na wengine, usikubali kutumika maisha yako yote.

SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

13. Kuwa makini na wale wanaokuzunguka, zungukwa na watu ambao ni washindi, watu ambao wamefanikiwa na hawa watakupa hamasa ya kufanikiwa zaidi. Kama utazungukwa na watu walioshindwa, huwezi kupiga hatua. Hii ni kwa sababu watakurudisha nyuma kwa maneno na vitendo.

14. Maneno yana nguvu kubwa ya kujenga au kuharibu. Kuwa makini na maneno yako, kwa kuongea na hata kuandika. Hakikisha unaongea na kuandika kile ambacho una uhakika nacho na unaweza kukisimamia. Usiwe sehemu ya wanaosambaza maneno ambayo hayana msaada kwa wengine.

15. Uaminifu na uadilifu ni nguzo ambazo huwezi kuzikwepa kama kweli unataka kufanikiwa. Kuna watu ambao wanafanikiwa kwa njia ambazo siyo za uaminifu, lakini mafanikio yao huwa hayadumu. Hata uwe na uwezo mkubwa kiasi gani, hata uwe na biashara bora kiasi gani, kama siyo mwaminifu huwezi kufika mbali.

16. Dunia inakudai. Watu wote walioleta mabadiliko makubwa duniani, walifanya hivyo kwa sababu waliona maisha ya watu yangeweza kuwa bora zaidi. Zikagundulika simu, kompyuta, mtandao wa intaneti na kila kitu ambacho tunatumia na kufurahia. Swali ni je wewe unawezaje kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi?
Dunia inakudai wewe utoe mchango kwa wengine kama ambavyo umetumia michango iliyotolewa na wengine. Unawezaje kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi kwa wengine kuishi?

17. Kisiasa na kijamii tumefundishwa kuwachukia watu ambao wametuzidi kifedha au kimafanikio. Tunaona wamefika pale walipo kwa sababu walipata bahati au kuna njia ambazo siyo halali wamezitumia. Huku ni kujidanganya ili tusijione sisi ni wadhaifu.
Ukweli ni kwamba watu wote ambao wamefanikiwa na wakadumu na mafanikio hayo kwa muda mrefu wamepigana sana kufika pale walipo. Wanapambana usiku na mchana kuongeza ubora kwenye kile wanachofanya.
Unapokutana na watu wanasema fulani kafanikiwa kwa sababu ni fisadi au kwa sababu ametokea familia bora, kimbia haraka sana, maana unapoteza muda wa kufikia mafanikio na wakati huo pia unapumbazwa uone mafanikio hayawezekani kwako.

18. Wafanye watu wakutegemee wewe. Hii ndiyo njia ya uhakika kabisa ya kufanikiwa. Kama watu wanakutegemea wewe kwa mambo ambayo ni muhimu kwenye maisha yako, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa. Wafanye wateja wako wakutegemee wewe kwa bidhaa na huduma bora, na wawe na uhakika kwamba wakifika kwako lazima watapata suluhisho la matatizo yao. Mfanye mwajiri wako akutegemee wewe kiasi kwamba mambo yake hayawezi kwenda bila ya wewe kuwepo, hapa utajijengea thamani kubwa na kuweza kupata matokeo makubwa.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Hali Ya Kukosa Uthubutu Na Kuingia Kwenye Biashara Itakayokufikisha Kwenye Ubilionea.

19. Kuna vitu vitatu ambavyo vinawazuia wengi kwenye safari ya mafanikio;
Kitu cha kwanza ni kuchelewa kufanya maamuzi. Watu wengi wamekuwa wanachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, au wanafanya maamuzi lakini utekelezaji unawachukua muda. Wanapokuja kustuka wanakuta fursa imeshakwisha.
Kitu cha pili ni uvivu wa akili, hapa watu wengi hawapendi kufanya vitu ambavyo vitaumiza akili zao. Badala yake wanaangalia ni kitu gani wengine wanafanya na wao wanaiga. Au wanafanya vitu kwa mazoea.
Kitu cha tatu ni kuongea hovyo na kuwa hasi. Kuwa na mtazamo hasi wa kujikatisha tamaa kwenye kila jambo ni adui mkubwa wa mafanikio. Kuongea hovyo pia ni hatari sana, wengi wamekosa fursa nzuri kutokana na kuongea kwao.

20. Je kila mtu anaweza kufanikiwa? Hili ni swali ambalo wengi wamekuwa wanauliza na wengi wamekuwa wanajitetea nalo, kwamba kila mtu hawezi kufanikiwa, au kila mtu akiwa tajiri nani atamfanyia kazi mwenzake.
Jibu la swali hili ni NDIYO kila mtu anaweza kufanikiwa. Na kipimo cha mafanikio siyo kimoja kwa kila mtu, kila mtu ana kitu ambacho ni muhimu ziadi kwake.
Kuna mfanya usafi wa ofisini ambaye ana mafanikio kuliko rubani wa ndege. Mafanikio hasa yanaanzia kwa mtu mwenyewe, kwa kufanya kile ambacho anasukumwa kufanya kutoka ndani yake, na kuwa na mchango mkubwa kwenye maisha ya wengine.
Mafanikio ni yako, hakikisha kila siku unaishi maisha ya mafanikio.

Nakutakia kila la kheri katika kutekeleza haya uliyojifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

MUHIMU; Kupata vitabu vya kiswahili vya kujisomea tembelea MOBILE UNIVERSITY kwa kubonyeza hayo maandishi. karibu sana tujifunze kwa pamoja.

Sehemu Kumi (10) Unazoweza Kupata Muda Wa Kujiongezea Maarifa Kupitia Kusoma Vitabu.

$
0
0
Habari mpendwa rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vema na kama hauko vizuri pole kwani changamoto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Karibu tuweze kujifunza ndugu mpendwa msomaji.

Katika swala la kujifunza katika jamii yetu bado limekuwa ni gumu sana. Ukikutana na watu kumi ukiwauliza unapenda kusoma vitabu utasikia wakisema napenda kusoma vitabu ila sina muda. Muda umekuwa kisingizio kwa watu wengi kutupia lawama zao zote katika muda. Watu wanasingizia muda umekuwa tatizo lakini mimi nakataa nasema muda sio tatizo. Habari njema ni kwamba Mungu ametuzawadia zawadi au rasilimali muhimu kuliko zote ambayo ni muda. Kila binadamu aliye hai ana muda wa masaa 24 kwa siku hivyo kwa wiki moja kila mtu ana jumla ya masaa 168 sasa katika masaa 168 kwa wiki nzima unakosa muda kweli wakusoma vitabu na kuongeza maarifa?

Akili yako inahitaji maarifa kila siku ili iweze kukua, akili yako inahitaji chakula kila siku kama unavyolisha tumbo lako nalo linahitaji maarifa. Hazina ya akili yako ni maarifa na maarifa yanapatikana katika kusoma vitabu, makala chanya, na siyo kusoma magazeti ya udaku, kusikiliza habari nyepesi nyepesi zisizokuwa na upembuzi yakinifu. Jinsi unavyokaa bila kusoma ndivyo akili yako inakaa inazidi kulala ukisoma nayo inazidi kuamka. Jitahidi kusoma na kufikiri kila siku ndio zoezi la akili yako. Kuwa na shahada, astashahada, stashahada, uzamili na uzamivu siyo mwisho wa kusoma au kujifunza bali huo ndio mwanzo wa kujifunza. Usiridhike na maarifa uliyonayo bali kuwa na njaa kali ya maarifa elimu uliyopata darasani ni msingi tu wa kusoma. Mtu anayesoma anakuwa tofauti sana na mtu asiyesoma vitabu tafadhali nakuomba anza kujifunza kuna faida nyingi zisizoelezeka.
Sasa leo ni siku ya kuondoa visingizio vya kukosa muda wa kusoma vitabu kwani leo utaweza kujifunza sehemu za kupata muda wa kusoma vitabu na kuongeza maarifa. 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA

Zifuatazo ni sehemu ambazo unaweza kupunguza au kuacha kabisa na kupata muda wa kusoma vitabu;

1. Kuangalia Luninga au Tv;
Kuangalia televisheni ni moja ya adui wako mkubwa anayekumalizia muda na kuharibu afya yako ya mwili wako. Kuna watu wanaangalia tv zaidi ya masaa mawili kwa siku. Kama umeamua kusoma vitabu punguza muda wa kuangalia tv na soma kitabu. Kabla hujafikiria kuangalia tv fikiria kwanza kusoma kitabu kwani utakua umejikomboa. Hivyo basi, kama wewe unakosa muda wa kusoma vitabu tafadhali punguza kuangalia tv, kufuatilia filamu au tamthilia mbalimbali na utapata muda wa kusoma kitabu. Kuangalia tv, filamu na tamthilia vitakuongezea msongo wa mawazo na kukujaza mtazamo hasi na kuishi maisha ya kuigiza kama vile mwigizaji filamu.

2. Kutembelea Mitandao Ya Kijamii;
Mitandao ya kijamii kwa karni ya sasa umekuwa ni ugonjwa unaopotezea watu muda. Watu wanapoteza umakini katika kazi zao na kupata matokeo mabovu. Kama ulikuwa unatembelea mitandao ya kijamii kila saa moja na unahisi usipoangalia unapitwa kubali kupitwa na habari za mitandaoni lakini usikubali kupitwa na kusoma kitabu. Punguza muda wako mwingi unaotumikia katika mitandao ya kijamii na pata muda wakusoma kitabu. Kama unaweza kutumikia mitandao ya kijamii kwa muda wa saa moja hadi mawili toa hapo na muda wa kusoma kitabu utakua umejikomboa kutoka katika hatari.

3. Kukaa Vijiweni Na Kupiga Stori;
Huwa napenda sana kuwahamasisha watu kusoma vitabu nikiona watu wamekaa vijiweni na kupiga stori na kubishana mambo ya siasa, mipira nakadhalika huwa naumia sana jinsi wanavyopoteza na kusahau kuwa maisha ni muda bila kutumia muda wako vizuri utakua unajipunguzia muda wa kuishi duniani kama tunakubali kuishi katika falsafa ya maisha ni muda. Badala ya kusingizia huna muda wa kujifunza acha kwenda vijiweni au punguza na tumia muda huo kusoma kitabu utakua mbali sana kifikra kwani umasikini wa mtu unaanzia akilini siyo mfukoni.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Sign-Posts On The Road To Success (Alama Muhimu Kwenye Safari Ya Mafanikio).

4. Kuchati na Kuongea na Simu;
Kuna watu ni wataalamu wa kuchati na kuongea na simu tena wanajisifu mimi kwa kuchati meseji mia moja zinaisha mara moja na hakuna kitu cha msingi katika kuchati huko bali ni kukosa kazi ya kufanya. Kama una kazi ya kufanya huwezi kuchati utaweka umakini wako katika kazi. Kwa hiyo, kama kisingizio ni muda basi punguza muda wa kuchati hovyo na kuongea na simu na utapata muda wa kusoma kitabu na kuongeza maarifa.

5. Kutokuwa na Ratiba;
Kama unaishi maisha yasiyokuwa na ratiba basi maisha yako ni sawa na mtu ambaye anasafiri na hajui anapokwenda. Usipokuwa na mwelekeo basi mwelekeo wowote utakuchukua kwa kingereza wanasema if you don’t have a direction, any direction will take you. Kuwa na ratiba ndugu, utapata muda wa kusoma kitabu na ratiba yako ndio itakua mwongozo wa siku yako hivyo huwezi kurukia na kufuatilia mambo ambayo hayako katika ratiba yako kwani ikifika jioni utajithamini siku yako ilikuwaje na kama utakua hujafuta ratiba yako utakua hujatimiza malengo yako.

6. Kuamka Mapema Alfajiri;
Kama unataka kupata muda wa kusoma na kuendelea na shughuli za kila siku amka mapema soma kwanza kabla kelele za dunia hazijaanza hapo utakua umeanza siku yako vema. Acha tabia ya kulala zaidi ya masaa elekezi ya watu wa afya inavyoelekeza, kama una tabia ya kulala hovyo kupita kiasi ni hatari pia kwa afya yako. Kama una tabia ya kusifika wewe ni bingwa wa kulala sana tafadhali acha na tumia hiyo fursa kujiongezea maarifa kwa kusoma vitabu.

7. Kuacha Uvivu; kama mtu ni mvivu hata wa kuhudumia mazingira anayoishi, mwili wake mwenyewe ni shida hata kuhudumia akili yake pia itakua ni shida. Uvivu ni mbaya sana unaharibu mambo mengi ya watu. Dawa ya uvivu ni kufanya sasa na siyo baadae hakikisha sababu zote za uvivu unakwenda kuzizika na uwe huru. Hivyo, kupitia kuacha uvivu utapata muda wa kusoma vitabu utakua unafanya shughuli zako kwa wakati
SOMA; KITABU CHA JULY; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

8. Acha Kauli Za Kujifariji;
Kuna mabingwa wa kujifariji kupita maelezo nitasoma baadae, nitaanza kusoma nikiwa nimepata kitu fulani, nitaanza kusoma nikimaliza masomo yangu na kauli nyingi za kujifariji na kujiona wewe ndio mshindi kumbe ni mshindwa. Kujifariji ni kuongozwa na hisia. Maamuzi ya hisia yanaongozwa na ubongo wa kati ambao ndio unatawala hisia zote, hasira, furaha nk ukikubali kuongozwa na ubongo wa juu ambao ni ubongo unafanya maamuzi sahihi kwa njia ya mantiki. Acha kauli kama hizi na jipatie muda wa kusoma kitabu.

9. Kuwa Na Shauku Na Maamuzi Ya Utayari;
Kuwa na shauku ni nguvu yenye hamasa ndani yake. Ukiamua kufanya maamuzi ya utayari wa kusoma vitabu na hamasa iliyoko ndani yako huwezi kukosa muda wa kusoma kitabu. Kama vile unavyotafuta muda wa kula chakula na hata kwenye kusoma nako utakua na njaa ya kusoma na hatimaye utapata muda wa kujifunza.

10. Umbea, Majungu, Kusengenya Na Kuhukumu;
Kabla hujaanza kupiga umbea, kuhukumu, kusengenya , majungu na wivu jiulize sababu kumi kwanza unapata faida gani chanya? Kama hakuna acha chukua kitabu na anza kusoma kwani utapata maarifa ya kutosha. Maarifa ndio silaha ya mtu makini utapimwa kama wewe ni mtu makini kulingana na madini adimu yanayotoka ndani ya kinywa chako na siyo umefanya umbea kiasi gani. Kwa hiyo ukiacha vitu hivi umbea, majungu, kusengenya, kuhukumu, watu bila kujua ukweli na kuwa na wivu na wenzako bila sababu na muda huo ukautumia kwenye kusoma utakua mbali sana kama ukianza sasa zoezi hili.

Hatua ya kuchukua;
Kama umeamua kubadilika na kuzizika sababu zote hizo hapo juu hongera sana. Kama unataka kuanza kuwa mtu wa kusoma vitabu na hujui wapi pa kuanzia fuata maelekezo haya; kuna kundi la kusoma vitabu liitwalo Tanzania Voracious Readers (TVR) katika kundi hili tunasoma vitabu viwili kwa wiki na kujadili mambo tuliyojifunza kupitia vitabu hivyo siku ya jumamosi kupitia mtandao wa Telegram.
Pia kuna vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ambavyo utaweza kuvipata na kukufikia hapo ulipo na kuanza kuongeza maarifa.

Kupata vitabu vya kiswahili vya kujisomea tembelea MOBILE UNIVERSITY 

Hivyo kama utahitaji kujiunga na kundi la Tanzania Voracious Readers wasiliana na mimi ( Deogratius Kessy ) kwa simu namba 0717101505 au Makirita Amani kwa simu namba 0717396253.

Mwisho, kila binadamu ana muda sawa, punguza mambo hasi uliyojifunza leo na jifunze mambo chanya. Punguza hata kukaa baa na kunywa pombe utapata muda kusoma kitabu, kuhudhuria vikao visivyokuwa na tija, kulalamika na kulaumu utapata muda mzuri wa kujifunza. Kumbuka maarifa ndio hazina ya akili yako na adui wa akili yako ni wewe mwenyewe.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Wazo Bora Na Mtaji Pekee Havitoshi Kuifanya Biashara Ifanikiwe, Unahitaji Kitu Hiki Kimoja Muhimu Sana Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako.

$
0
0
Mafanikio ya biashara hayatokani na kuwa na wazo bora na mtaji pekee. Wengi wamekuwa wakifikiria vitu hivi viwili kabla ya kuanza biashara na hata wanapoanza biashara. Ambacho wengi hawaangalii ni kwamba kuna watu ambao wamekuwa na mawazo mazuri sana ya kibiashara, na wakawa na mtaji mkubwa pamoja na watu waliopo tayari kuwekeza kwenye biashara zao. Lakini watu hao wameshindwa vibaya sana kwenye biashara walizojaribu kufanya.

Watu hawa wamekuwa na kila kitu tunachoamini kinahitajika ili biashara kukua, wazo bora, mtaji mkubwa pamoja na mtandao mzuri. Vitu vyote hivyo vinafanya kazi vizuri lakini matokeo yanakuwa tofauti na wengi walivyotarajia. Je hapa tatizo linatokea wapi? Ni bahati mbaya? Au watu wanachezewa michezo ambayo siyo mizuri?
Matatizo mengi kwenye biashara huwa yanaanzia kwenye msingi na falsafa ya biashara yenyewe. Misingi hii inawekwa na mwanzilishi wa biashara na inatakiwa kusimamiwa na kila mtu anayekuwepo kwenye biashara ile. Tatizo la biashara nyingi ni kwamba hakuna misingi iliyo wazi na hivyo kila mtu kwenye biashara ile anafanya maamuzi yake mwenyewe. Na hata pale ambapo misingi ipo, siyo wote wanaifahamu na kuitumia kwenye maamuzi ya kila siku.
 
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA PICHA AU MAANDISHI HAYA.

Biashara yoyote kama yalivyo maisha, ili iweze kufanikiwa, inahitaji kuwa na misingi ambayo inafuatwa. Inahitaji kuwa na falsafa ambayo watu wote kwenye biashara wanaiamini na hata wateja wanaiamini. Biashara isiyokuwa na misingi na falsafa, haiwezi kudumu muda mrefu, kwa sababu itafika wakati wa changamoto, watu watafanya maamuzi mabovu na yataigharamu biashara. Pia wateja wanashindwa kujua biashara inasimamia nini, kwa sababu kila wakati wanapata huduma tofauti. Wateja wanapokosa msimamo kwenye biashara hawajisikii amani kuendelea kupata mahitaji yao kwenye biashara ile.

Wewe kama mfanyabiashara unahitaji kujijengea misingi na falsafa ya biashara yako, ukishakuwa na misingi hii hakikisha kila anayehusika kwenye biashara anaijua na kuisimamia wakati wote. Pia hakikisha wateja wananufaika kupitia msingi na falsafa hiyo na kuhamasika kuendelea kufanya biashara na wewe.

Misingi ya biashara ni nini?

Misingi ya biashara ni vile vitu ambavyo biashara inasimamia, vile vitu ambavyo ni lazima biashara yako ifanye kwa mteja. Pia kuna vitu ambavyo ni mwiko kwa biashara yako kufanya. Misingi hii ndiyo itakayoweza kutoa utatuzi pale ambapo kuna changamoto kwenye biashara yako. Misingi ndiyo inawawezesha watu waliopo kwenye biashara yako kuweza kufanya maamuzi sahihi hata pale ambapo wanakuwa hawana taarifa za kutosha.
Baadhi ya misingi muhimu unayohitaji kujijengea kwenye biashara ni uaminifu, uadilifu, kuweka maslahi ya mteja mbele na kwenda hatua ya ziada katika kumhudumia mteja. Misingi ya biashara inatofautiana kulingana na aina ya biashara na malengo ya mfanyabiashara mwenyewe.

Falsafa ya biashara ni nini?
Watu wengi wakisikia falsafa wanaogopa na kuona ni kitu kigumu, wanaona ni kitu cha kwenda kusomea ili kuwa na imani fulani. Lakini huo siyo ukweli, falsafa ni kile kitu ambacho mtu anasimamia. Ile sababu ambayo inawafanya watu kufanya kile ambacho wanafanya licha ya kuwepo na vitu vingine vya kufanya. Falsafa yako kibiashara ndiyo inayowafanya wateja waje kununua kwako licha ya kuwepo kwa wafanyabiashara wengine kama wewe. Falsafa ndiyo inayokuwezesha kumudu ushindani mkali ulipo kwenye biashara unayofanya.

Ili kuweza kujenga falsafa ya biashara yako, unahitaji kujua KWA NINI biashara yako ipo. Ni changamoto gani, au mahitaji gani ya wateja ambayo biashara yako inatimiza. Kama biashara yako itaondoka leo ni kitu gani kikubwa ambacho watu watakikosa. Jua hili na mambo yako yote kwenye biashara yawe yanasaidia hilo. Jenga falsafa ya biashara yako ambayo itamwezesha mteja kuwa na uhakika kila anapofanya biashara na wewe. Falsafa ya biashara haijengwi kwa kushusha bei au kwa kutoa ofa, wala falsafa haijengwi kwa kuwapa wateja hofu. Bali falsafa ya biashara inajengwa kwa kuwafanya watu waamini kile unachofanya, kwa sababu kina manufaa kwako. Angalia biashara yako inawasaidiaje watu na fanya hilo kuwa dhumuni kuu la biashara yako.
Usifanye biashara kwa mazoea, kwamba umeona fursa, fedha unazo na wazo umelipata, bali tengeneza biashara itakayodumu kwa muda mrefu kwa sababu ina misingi na falsafa. Pia usiwe tu na falsafa na misingi kwenye makaratasi, bali vifanye vitu hivi kuwa maisha ya biashara yako kila siku, kwa kuvifanyia kazi kila siku kwenye biashara yako.

Nakutakia kila la kheri katika kujenga falsafa na misingi ya biashara yako.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
MUHIMU; Kwa ushauri wa biashara pamoja na mimi kuwa kocha wako tafadhali bonyeza maandishi haya kupata utaratibu. Karibu tufanye kazi kwa pamoja.

USHAURI; Jinsi Ya Kuepuka Dharura Zako Na Za Wengine Kuwa Kikwazo Cha Kufikia Malengo Yako.

$
0
0
Habari rafiki yangu?
Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia malengo yetu. Kupitia makala hizi za ushauri wa changamoto tunapeana mawazo mbadala ya kuweza kutatua zile changamoto ambazo ni kikwazo kwetu kufikia malengo na mipango yetu.

Waswahili huwa wanasema mipango siyo matumizi, wakiwa na maana kwamba japo unaweza kuweka mipango mizuri na mikubwa, bado utekelezaji utakuwa tofauti na ulivyokuwa umepanga. Haiwezekani kila kitu kikaenda kama unavyotaka wewe, na kama itatokea hivyo basi unachofanya siyo kikubwa au kama ni kikubwa basi haiwezi kutokea mara nyingi.

Kitu chochote kikubwa utakachopanga kufanya, utakapoanza kutekeleza utakutana na changamoto mbalimbali. Kama hukujipanga vizuri ni rahisi sana kwako kukata tamaa na kuishia pale baada ya kujiaminisha kwamba haiwezekani. Leo kwenye makala hii ya ushauri wa changamoto tutakwenda kuangalia jinsi ya kuzuia dharura zako binafsi na za watu wa karibu yako kuwa kikwazo kwako kufikia malengo yako.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA

Kabla hatujaingia kwenye ushauri juu ya hili, haya hapa ni maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na changamoto hii;

Changamoto yangu unakuta umeishaweka malengo yako mfano. Ya mwezi 1 au miezi 6 inatokea tatizo la ndugu na marafiki wameuguliwa au wakiwa na shida mbalimbali wanaomba msaada wako na unakuta una familia watoto wanasoma na kitega uchumi unacho kimoja tu. Ukikataa kwamba Huna pesa wanakulaumu nifanyeje? Naomba ushauri wako. Nakutakia ujenzi mwema wa Taifa. P. W. Marwa.

Pamoja na wewe kupanga mambo yako vizuri, bado huwezi kuzuia dharura kutokea kwako na kwa wale ambao ni wa karibu kwako. Hivyo unahitaji kuwa na mpango wa ziada juu ya dharura hizi kama kweli unataka kufikia malengo yako. Kwa kukoa mpango wa ziada, unajiweka kwenye nafasi ya kushindwa kabla hata hujaanza kufanya kile ulichopanga kufanya. Nina mambo matatu muhimu sana nataka kuyaongea kuhusiana na hili la dharura na malengo yako;

Jambo la kwanza jua dharura zipo na zitaendelea kuwepo.
Hata siku moja usijitetee ya kwamba kilichokuzuia wewe kufikia malengo yako ni dharura ambazo umekutana nazo kwenye maisha yako. kwa kusema hivi utakuwa unawaonesha watu kwamba bado hujakomaa na hukuwa umejitoa kweli katika kuyafikia malengo yako.

Dharura zipo na zitaendelea kuwepo, huwezi kuzuia watu kuumwa au kupata changamoto ambazo zinahitaji msaada wa haraka. Hivyo kama wewe kweli umejipanga kufikia malengo yako, ni lazima uwe na fungu la ziada kwa ajili ya dharura hizi. Unahitaji kuwa na kiasi cha fedha ambacho umekitenga kwa ajili ya dharura ambazo zinajitokeza kwenye maisha yako na ya wale ambao ni wa karibu kwako.
Kwa kuwa na fungu hili utaweza kuituliza akili yako na kuweza kufanyia kazi malengo yako. Wewe mwenyewe unajua ni kiasi gani cha dharura unaweza kuhitaji kwa kipindi cha mwezi au kipindi kingine, kuwa na kiwango cha aina hiyo.

Kitu cha pili; kuwa na vigezo vya wewe kutoa msaada kwenye dharura za wengine.
Kwenye haya maisha, watu huwa wanatafuta njia rahisi ya kuondokana na matatizo na changamoto zao. Na watu wakishapata njia hiyo rahisi huwa hawajiumizi tena kufikiria. Hivyo kama umekuwa ni mtu wa kuwasaidia wengine wanapokuwa kwenye dharura, watu watakuwa na utegemezi mkubwa kwako. Kila wanapopata tatizo kidogo wanakuja kwako kwa sababu wanajua utawasaidia.
Sasa wewe usiwe mtu wa kusaidia kila kitu, hata vitu vidogo ambavyo mtu angeweza kutatua mwenyewe. Badala yake weka viwango au vigezo ambavyo utatumia kutoa msaada kwa wengine. Na mtu anapokuja kwako kwa kutaka msaada kwa dharura yake, mpe njia nyingine anazoweza kuzitumia kutatua changamoto zake. Ukianza kuwapa njia hizi utaona wengi wanapunguza kuleta changamoto ndogo ndogo.

Sikufundishi uwe na roho mbaya, bali nakufundisha uweze kuwasaidia watu kutatua changamoto zao wenyewe, hasa zile ambazo ni ndogo. Hata kama huna njia ya kuwashauri njia nyingine za kufuata, unaweza kuwahoji ni juhudi kiasi gani wameshachukua mpaka kufika pale walipo sasa. Ninachotaka ufanye ni isiwe rahisi kwako kutoa misaada hasa midogo midogo. Yaani mtu anapopata changamoto asiache kutafuta njia nyingine kwa sababu upo, bali awe ameshatafuta kila njia na imeshindikana ndiyo akaja kwako.

Kwa kufanya hivi utasaidia mambo mawili muhimu sana;
1. Utawajengea watu uwezo wa kuanza kufanyia kazi changamoto zao na kuacha kuwa tegemezi wa moja kwa moja.
2. Utapunguza mzigo wa moja kwa moja kwako, hasa changamoto ndogo ndogo ambazo watu wanaweza kutatua wenyewe.

Kitu cha tatu ni kuongeza vyanzo vyako vya mapato.
Kuwa na chanzo kimoja cha kipato, hasa ajira ni hatari kubwa sana kwenye maisha ya sasa. Zamani ilikuwa ni kitu salama kabisa, lakini kwa sasa ni hatari kubwa. Ajira zimekuwa siyo za uhakika tena na maisha yanakwenda kasi kuliko ajira inavyokwenda. Kipato cha ajira kinaongezeka taratibu wakati gharama za maisha zinaongezeka kwa kasi kubwa.

Hivyo unahitaji kutengeneza vyanzo vya ziada vya mapato. Na unaweza kutengeneza vyanzo hivyo ukiwa bado upo kwenye ajira yako. hii itakupa uhuru hasa unapokutana na changamoto. Wafanyakazi wengi huwa wanapata shida sana wanapokutana na changamoto katikati ya mwezi, kwa sababu fedha wanakuwa hawana na hivyo kuishia kwenye mikopo ambayo wanatozwa riba kubwa. Mwisho wa siku mtu anakuwa anafanyia kazi riba za mikopo, kwa sababu anapopokea mshahara anaishia kulipa mikopo yenye riba kubwa, halafu anaanza tena kukopa.

Unaweza kuwa na vyanzo nane tofauti vya mapato. Kujua jinsi ya kujitengenezea vyanzo hivi tofauti vya mapato, nunua kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, Jinsi ya kuanza na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Bonyeza hayo maandishi kukipata.
Fanyia kazi haya ambayo umejifunza na utaweza kuondokana na changamoto hii ya dharura kuwa kikwazo cha kufikia malengo yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Mambo 6 Ya Kukusaidia Kuboresha Kipato Chako.

$
0
0
Miongoni mwa kitu kinachowatesa watu wengi katika safari ya mafanikio, ni kule kutaka kuona kipato chao kinakuwa siku hadi siku. Wengi huwa wanahamasa kubwa ya namna hii, ya kutaka kuona kipato chao kinakua hali ambayo husababisha hata watafute pesa usiku na mchana.
Pamoja na kiu hiyo kubwa, kitu cha kujiuliza mimi na wewe ni wangapi kati ya watu hawa ambao wanaelewa njia sahihi za kuboresha kipato chao? Inawezekana ni wachache wanaojua na wengi kubaki hawaelewi sana. Lakini kupitia makala hii naomba nikukumbushe njia za kukusaidia kuboresha kipato chako kila siku.
1. Epuka matumizi yasiyo ya lazima.
Kama unaishi maisha ya kuwa na matumizi mabovu ya pesa kila wakati, elewa kabisa itakuwa ngumu sana kwako kuweza kuboresha kipato chako. Hutaweza kujihakikishia kipato cha kudumu kama matumizi yako ni mabovu. Kila wakati kuwa makini sana na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima kwako.
Kumbuka unapokuwa unatumia pesa zako vizuri, hiyo itakusaidia sana katika suala zima la kuboresha kipato chako na kuwa cha kudumu. Kwa nini hiyo iko hivyo? Ni kwa sababu utaokoa pesa nyingi ambazo ungezipoteza. Hivyo kwa vyovyote vile ni lazima itakusaidia kuboresha kipato chako.

Tengeneza vyanzo vingine vya kukuingizia pesa.
2. Tengeneza bajeti ya kukuongoza.
Siri nyingine ya kukusaidia kujihakikishia kipato cha kudumu ni kutengeneza bajeti. Hakikisha unatengeneza bajeti yako ambayo itakuwa inakuongoza katika suala zima la matumizi ya pesa. Usiishi tu kiholela bila kuwa na bajeti yako maalum.
Watu wengi wanashidwa kutengeneza pato lao la kudumu kwa sababu hawana bajeti ya kudumu. Unapokuwa na bajeti inakusaidia sana usitumie pesa zako hovyo. Hiyo ikiwa na maana pesa zako zitatumika kwa utaratibu na zitadumu.
3. Tengeneza  vyanzo vingine vya pesa.
Huwezi kuboreshakipato chako na kikawa cha kudumu kama huna vyanzo vingine vya pesa. Ni lazima uwe na vyanzo vingine vya pesa mbali na hicho ulichonacho. Hiyo itakusaidia sana kuboresha pato lako kila kukicha.
Kwa mfano kama umeajiriwa, tafuta namna ambayo unaweza ukatafuta biashara nyingine ya kukuingizia pesa. Kama umejiajiri na una biashara moja, halikadhalika unatakiwa kutafuta kitu kingine cha kukusaidia kuingiza pesa. Hiyo itakuwa ni njia sahihi sana kwako pia ya kuboresha kipato chako.
4. Weka akiba.
Kujiwekea akiba ni mbinu nyingine ambayo unaweza kuitumia kuboresha kipato chako. Acha kuthubutu kutumia kila pesa uliyonayo mpaka ukabaki huna kitu. Ni lazima uwe na akiba itakayokusaidaia katika kuwekeza na pia katika dharura zingine za kimaisha.
Kwa kiasi chohote cha pesa unachopata tenga nyingine iwe akiba yako. Hata kama pesa hiyo ni ndogo sana usiidharau, baada ya muda itakuwa ni pesa nyingi ambayo itakusaidaia. Kwa kufanya hivyo utajiweka katika mazingira mazuri ya kuboresha kipato chako.
5. Tengeneza nidhamu ya pesa.
Hata kama unaingiza pesa nyingi kiasi gani lakini ikiwa wewe binafsi huna ile nidhamu ya pesa basi hiyo itakuwa ni sawa na kazi bure. Ni vizuri sana kujitengenezea nidhamu ya pesa itakayokuongoza katika kuboresha kipato chako kila kukicha.
Kwa kifupi hayo ndiyo mambo machache yanayoweza kukusaidia kuboresha kipato chako ikiwa uatayafanyia kazi.
Nakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA kila siku.
Kwa malaka nyingine nzuri za mafanikio tembelea pia DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

UCHAMBUZI WA KITABU; START WITH WHY, Jinsi Viongozi Wakubwa Wanavyohamasisha Watu Kuchukua Hatua.

$
0
0
Kuna aina tofauti za uongozi, kuna uongozi wa mabavu na kuna uongozi wa hamasa. Uongozi wa mabavu ni pale mtu anapolazimisha watu kufanya kitu fulani ambacho ni muhimu kufanyika. Uongozi wa hamasa ni pale ambapo mtu anawahamasisha watu kuchukua hatua na watu wanafanya hivyo kwa sababu wanaona ni muhimu kwao kufanya hivyo. Hawasubiri kulazimishwa badala yake wanajitoa na kufanya wenyewe.
Uongozi wa mabavu unaweza kuleta matokeo mtu anayotaka ndani ya muda mfupi, lakini ndani ya muda mrefu unaharibu mahusiano ya anayeongoza na anayeongozwa na hivyo kushindwa kupata matokeo ambayo mtu anataka. Uongozi wa hamasa ni uongozi ambao una manufaa makubwa sana kwa baadaye, unahitaji muda kujenga lakini baada ya hapo mambo yanakwenda vizuri.


Mwandishi Simon Sinek kwenye kitabu chake START WITH WHY anatupa mbinu moja muhimu ya kuweza kujijenga na kuwa viongozi wa hamasa. Njia hii ni kujua kwa nini unafanya kile ambacho unakifanya. Wewe ukishajua kwa nini unafanya, unaweza kuwahamasisha wengine na wao wakachukua hatua.
Simon ana falsafa yake moja anayoipa mkazo sana kwamba WATU HAWANUNUI KILE UNACHOUZA BALI WANANUNUA KWA NINI UNAUZA. Akiwa na maana kwamba watu wananunua ile sababu unayouza ambayo inaendana na wao. Na kwa tahadhari tu sababu unayouza siyo kupata fedha, bali ile thamani kubwa unayotoa.

Karibu kwenye makala hii ya uchambuzi wa kitabu hiki, ambapo tutajifunza mbinu za kuwa viongozi wa hamasa. Kila mtu ni kiongozi kwa nafasi fulani, unaweza kuwa kiongozi wa kisiasa, kiongozi wa dini, kiongozi wa kikazi, kiongozi wa kijamii na hata kiongozi wa kifamilia. Katika kila aina ya uongozi misingi ni ile ile, karibu tujifunze leo ili tuweze kuchukua hatua na kuwa viongozi bora.

1. Kwenye kitu chochote kinachofanyika, kuna misingi mikuu mitatu. Misingi hii inafananishwa na miduara mitatu, ambayo inaanzia nje kwenda ndani. Misingi hii ni kama ifuatavyo;

NINI UNAFANYA (WHAT), Hapa mtu anakuwa anajua kile ambacho anakifanya. Kila mtu anajua anachofanya, na hivyo ni rahisi mtu kusema anafanya nini. Kwa bahati mbaya msingi huu hauhamasishi watu wengi.

JINSI UNAVYOFANYA (HOW), Hapa mtu anakuwa anajua jinsi ya kufanya kile anachofanya. Siyo wote wanaojua jinsi ya kufanya, lakini hata wale wachache wanaojua bado hawawezi kuwashawishi wengi.

KWA NINI UNAFANYA (WHY), Hapa mtu anakuwa na sababu inayomsukuma kufanya kile ambacho anafanya. Ni wachache sana wanaojua kwa nini wanafanya kile wanachofanya, na hawa ndio wanaofanikiwa sana. Wale wanaojua kwa nini wanafanya, wanaweza kuwahamasisha wengi zaidi na kuwa viongozi bora.
 

2. Njia mbovu ya kuwahamasisha watu ni kuanza na nini, jinsi na kumalizia na kwa nini. Watu wengi wanapojaribu kuwahamasisha wengine ili waweze kuchukua hatua fulani, iwe ni kununua au kuweka juhudi, huanza na kile wanachofanya. Hapa huwaambia watu kile wanachofanya na kuwataka wachukue hatua, kama tulivyoona kujua unachofanya hakuhamasishi, na hivyo wanashindwa kushawishi wengine.

3. Njia sahihi ya kuwahamasisha wengine ni kuanza na KWA NINI, unapoanza na kwa nini unafanya unachofanya, unaingia ndani ya mioyo ya watu, wanaelewa kile unachofanya na wanachagua kuwa upande mmoja na wewe. Kwa nini inawahamasisha watu na kuweza kuchukua hatua.

4. Hakuna bidhaa au huduma yoyote iliyopo sokoni sasa ambayo haina upinzani. Biashara yoyote unayofanya au utakayopanga kufanya, watakuja watu wengine wataifanya vizuri kuliko wewe au wanatoa kwa bei ya chini kuliko unavyotoa wewe. Hivyo bila ya kuwa na kitu kinachowahamasisha na kuwavutia watu kufanya biashara na wewe, huwezi kuendelea kuwa nao, wataenda kwa wengine wanaofanya vizuri kuliko wewe.

5. Biashara yoyote unayoifanya, jua ni kwa nini unafanya kile unachofanya. Nisisitize tena, kupata fedha au faida siyo sababu inayoweza kuwahamasisha wengine. Fikiria kama fedha isingekuwa changamoto kwako, ni thamani ipi kubwa unayoitoa kwenye maisha ya wengine. Hii ndiyo sababu kuu na itumie kujenga uhusiano mzuri na wateja wako.

SOMA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

6. Kuna njia mbili pekee mtu anaweza kuzitumia kuathiri tabia ya binadamu. Yaani kama unataka kumfanya mtu yeyote afanye kile unachotaka afanye, awe ni mteja, mtoto, mwenza, mfanyakazi, unaweza kutumia njia hizi mbili;
Njia ya kwanza ni kudanganya na kutishia. Hapa unaweza kutumia hofu kumfanya mtu achukue hatua unayotaka achukue. Unaweza kumdanganya kwamba kwa kuchukua hatua hiyo atanufaika zaidi. Au unaweza kumtishia kwamba kama asipochukua hatua basi mambo yatakuwa mabaya sana kwake. Njia hii inaleta majibu ya muda mfupi, ila baadaye inaharibu sana.
Njia ya pili ni kuhamasisha. Hapa unampa mtu sababu kwa nini ni muhimu kwake kufanya kile ambacho unamtaka afanye. Na yeye mwenyewe anaamua kuchukua hatua kwa sababu ni muhimu kwake. Aina hii inajenga mahusiano mazuri baina ya wale wanaohusika.

7. Dunia ya sasa inaendeshwa kwa udanganyifu, hofu na vitisho. Hii ni kuanzia kwenye biashara, jamii, familia mpaka kwenye siasa. Watu wanatafuta njia ya mkato ya kuwahamasisha wengine kuchukua hatua na hivyo kutumia udanganyifu, hofu na vitisho. Viongozi wa kisiasa wamekuwa wakitumia udanganyifu kupata kuungwa mkono. Wafanyabiashara wamekuwa wakitumia hofu kuwasukuma watu wanunue. Na viongozi wa kikazi, kijamii, kidini na kifamilia wamekuwa wanatumia vitisho kuwafanya watu wachukue hatua fulani wanayotaka wachukue.

8. Hakuna mchezo mbaya kufanya kwenye biashara kama kutumia bei kama kigezo cha kupata wateja. Wafanyabiashara wengi hufikiri kushusha bei au kupunguza bei kutavutia wateja wengi. Kweli kunawavutia kwa muda mfupi, lakini mshindani wako anapojua hilo na yeye akashusha bei basi wateja watahamia kwake. Unahitaji kuwa na sababu ambayo wateja wako wanaiamini na wanaendelea kufanya biashara na wewe hata kama kuna mwingine ana bei ndogo kuliko wewe.

9. Biashara inayofanikiwa ni ile ambayo ina wateja waaminifu, wateja ambao wanaichukulia biashara hiyo kama sehemu ya maisha yao. Wateja hawa ndio wanaoendelea kuwa kwenye biashara na kuwaleta wengine wengi kwenye biashara hiyo. Ili biashara iweze kuwa na wateja waaminifu, lazima kuwe na kitu ambacho kinawahamasisha wateja kuendelea kuwepo kwenye biashara hiyo. Na hamasa hiyo inahitaji kutokana na manufaa makubwa wanayoyapata.

10. Watu hawanunui kile unachouza (WHAT) bali wananunua ile sababu unayouza (WHY). Kile unachouza kila mtu anaweza kuuza, lakini ile sababu unayouza wengine hawawezi kuiiga. Unachohitaji ni kuijua sababu hii, na kuitumia kama njia ya kutengeneza wateja waaminifu kwa biashara yako. unapotoa sababu ya kwa nini unauza unachouza, unakutana na watu ambao wanaamini kile ambacho unaamini wewe na mtakwenda pamoja. Ukishawapata watu hawa huhitaji tena kutumia nguvu nyingi kuwafanya wanunue, badala yake wataona kununua ni wajibu wao, kwa sababu wote mpo pamoja. Ijenge biashara yako kwenye msingi huu na utakuwa na biashara bora sana kwako.

11. Ni hitaji letu sisi binadamu kuona kwamba tupo sehemu ya jamii fulani ambayo inaendana na sisi. Ndiyo maana watu wapo tayari kufanya mambo ambayo siyo muhimu kwao ili tu wawe pamoja na wale wanaofanya mambo hayo. Pia binadamu tunapenda kuwa sehemu ya kitu kikubwa, ambacho tunakiamini na kuona kinahusiana na sisi. Unaweza kutumia hitaji hili la binadamu kuwahamasisha wale unaowasimamia au wateja wako. Kwa kujua ni kitu gani wanachoamini na ukajiweka kwenye kile unachotaka wafanye.

12.Watu wanapokuwa na sababu ya kufanya kitu ambayo inaendana na kile wanachoamini, wapo tayari kufanya maamuzi hata kama hawajapata taarifa za kutosha. Hii ndiyo sababu kuna ambao huwa wanaonekana wanafanya maamuzi hatari lakini wanapata matokeo bora. Watu hawa wanakuwa wanaamini sana kile wanachofanya na kuwa wanakielewa vizuri. Kwa njia hii kuna baadhi ya hisia huwa zinawajia na kuona maamuzi wanayofanya ni sahihi. Amini kwenye kile unachofanya na utaweza kuwaaminisha wengine wengi zaidi.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Sign-Posts On The Road To Success (Alama Muhimu Kwenye Safari Ya Mafanikio).

13. Wakati mwingine watu wanafanya kitu ili kuonekana kuwa nao wao wanafanya. Lakini kutaka huku kuonekana kunaanza na kuamini kile ambacho wanakwenda kufanya. Kuna watu wananunua bidhaa au huduma fulani ili wengine wawaone na wao ni watu wa aina fulani. Pia kuna watu ambao wanakubali kufanya kazi fulani kwa sababu wanataka waonekane ni sehemu ya mchango kwenye kazi hiyo. Jua mahitaji ya watu ni yapi na watimizie, utawahamasisha kuchukua hatua.

14. Ukishajua kwa nini unafanya unachofanya, unahitaji kujua unakifanyaje. Hapa kwenye kujua jinsi ya kufanya ndipo penye misingi muhimu ambayo mtu anaisimamia katika kutekeleza kile anachofanya. Bila ya misingi ile sababu ya kufanya haitaweza kufikiwa. Na watu wanapohamasika kwa ile sababu ya kufanya, wanapenda kuona misingi iliyopo kwenye ufanyaji. Kwenye jinsi ya kufanya ndipo penye nidhamu na utamaduni unaotumika, iwe ni kwenye kazi, biashara au jamii.

15. Kila unachosema na kila unachofanya kinatakiwa kuendana na kile unachoamini. Ile sababu ya kwa nini unafanya unachofanya ndicho unachoamini, jinsi unavyofanya ndivyo unavyotekeleza ile imani yako. Na nini unachofanya ni matokeo ya mwisho. Unapokuwa na sababu ya kufanya, lakini huna misingi unayosimamia kwenye ufanyaji, huwezi kupata matokeo unayotarajia kupata. Maneno yako na matendo yako ni lazima yaendane kama kweli unataka kupata unachotaka kupata.

16. Ili uweze kuwahamasisha wengine, ili uweze kufikia kile unachotaka kufikia, unahitaji kuwa halisi. Kuwa na sababu ambayo inatokana na wewe kweli na kisha ifanyie kazi . Unapokuwa halisi unafanya kile ambacho unakiamini kweli, na unaweza kupambana hata kama unakutana na changamoto. Kuwa halisi ni hitaji muhimu la kupata mafanikio yakudumu. Unaweza kuiga au kuigiza na ukapata mafanikio, lakini kwa kukosa uhalisia mafanikio hayo hayawezi kudumu.

17. Binadamu tuna uwezo mkubwa wa kujua ni mtu gani yuko halisi na yupi ambaye anaigiza au ambaye ana ajenda nyingine binafsi. Mtu anaweza kuongea kwa hamasa sana, lakini kama hayupo halisi, watu wataona hilo na hawatakuwa tayari kufanya kile ambacho anawataka wafanye. Kuwa halisi kwenye kila unachofanya, utawavutia wale halisi na watakuwa tayari kufanya kile ambacho unawataka wafanye.

18. Kwenye biashara, watu wanaposhawishika kwamba maamuzi wanayofanya ni sahihi kwao, wapo tayari kulipa gharama yoyote ambayo wanaweza kulipa. Hivyo jukumu la mfanyabiashara siyo kumshawishi mtu kuhusu bei ya kitu, bali kumwonesha ni kwa namna gani kitu kile ni muhimu kwake. Mtu anachukua maamuzi ambayo anajua ni muhimu kwake na hivyo kuwa tayari kulipa gharama ili kupata kile wanachotaka.

SOMA; Sehemu Kumi (10) Unazoweza Kupata Muda Wa Kujiongezea Maarifa Kupitia Kusoma Vitabu.

19. Lengo la biashara siyo kumuuzia kila mtu ambaye anataka kununua, bali kumuuzia yule ambaye anaamini kile unachouza, ambaye atanunua na kufaidika na kuja kununua tena na tena na kuwaleta wengine pia. Unapochagua kufanya biashara na watu hawa wanaoamini kile unachoamini, watu hao wanajenga uaminifu mkubwa na wewe na wanakuwa tayari kufanya kile unachowataka wafanye, kwa sababu wanakuamini huwezi kufanya kitu ambacho hakina manufaa kwao.

20. Kuongoza na kuwa kiongozi ni vitu viwili tofauti kabisa, wengi hawajui na hivyo kuchanganya.

Kuwa kiongozi (BEING A LEADER) maana yake unashika madaraka ya juu na unakuwa ndiyo mwamuzi wa mwisho. Una mamlaka ya kuwafanya watu wachukue hatua iwe wanapenda au hawapendi kufanya hivyo.

Kuongoza (LEADING) maana yake watu wanakuwa tayari kukufuata, siyo kwa sababu wanalazimika kufanya hivyo na wala siyo kwa sababu wakikufuata ndiyo wanalipwa, ila kwa sababu wameamua kukufuata. Wanaamua kukufuata kwa sababu wanakuamini kwa kuwa unaamini kile wanachoamini, wanakufuata kwa sababu umewapa sababu ambayo inaendana na kile wanachoamini.
Maisha ya furaha na mafanikio yanatokana na kuongoza na siyo kuwa kiongozi, nenda kaongoze na siyo tu kutaka kuwa kiongozi.

Kila mtu ni kiongozi kwenye nafasi fulani ya maisha yake, kila mtu anahitaji kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani, tumia haya uliyojifunza hapa ili kuimarisha ushawishi wako, kujenga mahusiano bora na kuweza kufikia maisha ya ndoto yako, yenye furaha na mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri,
Rafiki Na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Hawa Ndiyo Watu Muhimu Sana Wanaoleta Mabadiliko Katika Jamii Yetu.

$
0
0
Habari ndugu Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini hujambo na karibu katika makala yetu ya leo. Kila siku ni siku mpya kwako hivyo basi, usikubali kupitwa na maarifa yaani usikubali siku kupita bila kujifunza kitu kipya kwako. Na siku nzuri ya kuanza kujifunza ni leo yaani sasa hivi na siyo baadae au kesho kwani kesho na baadae hauna uhakika nazo muda ambao una uhakika nao ni sasa hivi.

Katika jamii zetu tumekuwa tukiaminishwa / kufundishwa kuwachukia watu ambao wametuzidi kimafanikio au kifedha na kujazwa mitazamo hasi isiyohesabika. Wale watu wanaofanya vitu chanya katika jamii ndio watu wanaochukiwa na watu au jamii yenye mtazamo hasi. Watu chanya ni wachache sana katika jamii yetu ndio maana watu wakiwaona watu ambao wapo tofauti nao lazima wawajengee chuki bila sababu. Watu wenye mitazamo hasi ni wengi sana katika jamii yetu hivyo basi, hawapendi kuona mtu akibadilika hata kidogo wanapenda kuona kila siku ufanane na wao.

KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Ndugu msomaji, leo tutajifunza kwa mifano halisi kabisa katika jamii yetu makundi au aina ya watu wanaochukiwa bila sababu ya msingi na makundi ya watu hao ni kama ifuatavyo;

Watu wanaosema ukweli; Kuna msemo huwa unasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu lakini huyu msema ukweli ambaye ni mpenzi wa Mungu ni mtu ambaye anachukiwa sana katika kila idara ya maisha yetu. Mtu anayesema ukweli na kusimamia ukweli katika jamii anaonekana ni adui mkubwa zaidi ya maadui wakubwa watatu aliyowahi kuwasema Mwalimu Nyerere ambao ni ujinga, maradhi na umasikini. Kwa mfano, unaweza kuwa na rafiki yako na ukamweleza ukweli juu ya mwenendo wake wa maisha labda kuna sehemu amekwenda mrama na wewe lengo lako ni kumrekebisha tu basi ukimwambia ukweli chuki, uadui na wivu ndio unaanzia hapo. Ataona kama wewe siyo mtu mwema kwake kwa kumwambia ukweli. Hamtaweza kuwa marafiki tena kama zamani bali mtakua maadui kama vile paka na panya. Kama mlikuwa mnasalimiana hataweza tena kukusalimia bali atakukua anakusemea maneno hasi katika jamii na kuendelea kukuua kwa ulimi tu.
Watu wanaosimamia ukweli katika maeneo ya kazi wanaonekana ni maadui wakubwa. Wale wanaosema ukweli lazima watatengwa na wenzao hata ufanisi wa kazi utapungua na ushirikiano katika kazi utapungua. Habari itakayokuwa ni kupiga umbea na majungu. Katika kila sehemu ya maisha yetu wale viongozi wa sehemu mbalimbali wanaosema ukweli huwa wanachukiwa tu watu wenye mtazamo hasi.

SOMA; TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Uaminifu.

Hatua ya kuchukua; hatuwezi kupata maendeleo bila kusimamia ukweli. Ukiujua ukweli nao ukweli utakuweka huru. Kwanini sasa tuendelee kutokuwa na uhuru kwa kuogopa kusema ukweli? Kama wewe ni mtu chanya na unapenda kuona mabadiliko katika jamii endelea kusema ukweli na kusimamia ukweli bila kuogopa. Kama ni kanisani, msikitini sema ukweli, kama ni kwenye familia sema ukweli na kusimamia ukweli, sehemu yoyote ile endelea kusema ukweli wala usiogope. Kuficha ukweli ni sawa na mtu anayeingia kwenye tanuri la moto utaendelea kuungua na moto katika nafsi yako na kupata majeraha ya moyo na kukosa uhuru katika maisha yako.

Watu Wanaofanya Kazi Kwa Bidii; wale watu wanaofanya kazi kwa bidii huwa wanakua na matokeo mazuri sana katika kile wanachofanya. Ile juhudi yao ya kufanya kazi kwa kujituma ndio inawatofautisha na wale watu wanaofanya kazi zao kwa mazoea yaani kwa kawaida hatimaye utofauti huo ndio unazaa chuki kati yao. Kama mwenzako amejituma na kupata matokeo mazuri kwa nini na wewe usijitume na kupata matokeo mazuri? Badala ya kuanza kumchukia na kuanza kuoneana wivu bila sababu ya msingi. Kama uko kazini angalia yule mtu anayefanya kazi zake kwa kujituma na kwa muda kama atapendwa na wenzake lazima atachukiwa kwa sababu amejitoa katika kundi hilo hamfanani tena. Kama ulikuwa katika timu ‘bata’ ukaachana nao lazima watakuchukia kwa sababu umewaacha katika sehemu ya hatari na umekwenda katika sehemu ya salama. Ulikuwa katika timu umbea, majungu, kumesengenya na kuhukumu ukabadilika wale wenzako uliowaacha kule lazima watakusemea vibaya na kukuchukia.

Hatua ya kuchukua; Kama ulikuwa ni mtu wa kujituma katika kazi zako endelea kuwasha moto wa kujituma mwisho wa siku watakuja kukuelewa na kuwa mwalimu wao. Usiogope kuchukiwa kwa sababu unajituma katika eneo fulani la maisha yako. Tunahitaji watu wanaojituma ili kuleta maendeleo katika jamii na si vinginevyo.

SOMA; Tabia Hizi Nne(4) Ulizonazo Zinakuzuia Wewe Kufikia Mafanikio Makubwa.

Watu Waaminifu Na Waadilifu; uaminifu unalipa sana kwenye kila eneo la maisha yetu. Sasa siku hizi uaminifu na uadilifu umekuwa adimu sana katika zama hizi za taarifa. Watu waaminifu wanaonekana ni watu wa ajabu katika jamii yenye mtazamo hasi. Kila mtu anapenda kuwa na mpenzi mwaminifu, mfanyakazi mwaminifu na mwadilifu na n.k. Waajiri wanahangaika kuwatafuta watu waaminifu na waadilifu watakaoweza kufanya nao kazi. Serikali nayo inahangaika kila siku kuwatafuta watu waadilifu na waaminifu katika kazi na kuendelea kusisitiza uaminifu na uadilifu katika kazi. Bila uaminifu na uadilifu mambo lazima yaende mrama. Sasa wale watu ambao ni waaminifu na waadilifu ndio watu wanaochukiwa na kutoungwa mkono katika kusimamia falsafa ya uaminifu na uadilifu. Kwa mfano, wale watu ambao ni waaminifu katika maisha yao ya ndoa wanaonekana ni maadui kwa wale watu ambao wamezoea ‘michepuko’ na kuona ‘michepuko’ ndio dili kuliko uaminifu watakutengenezea mazingira ya kukuandaa na mitego mbalimbali ili uweze kunasa na kuingia katika kundi lao hivyo usikubali kunasa na kuwa katika kundi la watu ambao hawana uaminifu na uadilifu.

Hatua ya kuchukua; bado dunia inahitaji watu waaminifu na waadilifu hivyo ni fursa nzuri ya kuwekeza katika uaminifu na uadilifu. Kama wewe ni mzazi, mlezi, mwalimu anza leo kuwafundisha watoto falsafa ya uaminifu na uadilifu tokea wakiwa wadogo. Uaminifu na uadilifu utakupa faida kubwa katika maisha yako hivyo endelea kuwasha moto wa uaminifu na uadilifu.

Kwa kuhitimisha, tunahitaji watu chanya ili kuendeleza dunia. Watu hasi wapo kwa ajili ya kubomoa jamii na siyo kujenga. Tunatakiwa kuwapenda wale watu wanaoleta mabadiliko chanya katika jamii yetu na kujifunza kupitia kwao na siyo kuwachukia. Mabadiliko yanaletwa na watu chanya hivyo basi, wanahitajika watu chanya wengi ili kujenga jamii. Tusitawaliwe na wivu na tamaa zitakazotupeleka mahali pabaya na ishi katika maisha yanayompendeza Mungu na jamii kwa ujumla na tuendelee kuweka juhudi na maarifa katika kazi tunazofanya.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Tabia Nne(4) zinazowatofautisha wafanyabiashara wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

$
0
0
Biashara siyo kuuza na kununua pekee, wengi wanaoingia kwenye biashara kwa mtazamo huu wa kuuza na kununua huwa hawafiki mbali. Na wala biashara siyo kuwa na wazo na mtaji pekee, wengi wamekuwa na mawazo mazuri na mtaji wa kutosha, lakini walipoingia kwenye biashara hawakuweza kufika mbali.

Biashara na ujasiriamali ni kitu ambacho kinategemea mambo mengi kutoka kwa mwendeshaji. Na moja ya vitu vinavyostawisha au kuua biashara ni tabia ambazo mtu anayeendesha biashara anakuwa nazo. Biashara inabeba zile tabia ambazo mwanzilishi wa biashara ile anakuwa nazo. Na hata mfanyabiashara anapoajiri, hata wafanyakazi wake wanaishia kufanya kazi kama anavyofanya yeye.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Hivyo kabla hujalalamika kwa nini biashara yako haiendi vizuri, ni vyema ukajichunguza kama tabia zako zinachangia kuikuza au kuiua biashara yako. Kupitia makala hii ya leo tunakwenda kuangalia tabia za wafanyabiashara ambazo zinaiwezesha biashara kufanikiwa.

Kuwa tayari kuweka juhudi kupita kawaida ni moja ya tabia ambazo zinawezesha biashara kukua. Biashara siyo rahisi hata kama mtu una wazo bora na una wasaidizi wengi. Wewe kama mwendeshaji na mmiliki wa biashara unahitajika kuweka juhudi kubwa kwenye biashara yako. unahitaji kujua kila kitu kinachoendelea kwenye biashara yako na kuona kama maamuzi yote yanayofanywa ni sahihi. Unapoona biashara yoyote inakufa, jua kuna uzembe ulikuwa unajitokeza kwa muda mrefu mpaka imefikia hatua ya kuleta hasara. Iwapo mmiliki wa biashara anakuwa karibu na biashara yake, na kuweka juhudi kubwa, atakuwa ameshaona mapema tatizo lolote linalojitokeza.

Kama wewe ni mfanyabiashara au unapanga kuingia kwenye biashara, basi jua unahitaji kuweka juhudi kubwa sana kwenye biashara yako. Unahitaji kuijua biashara yako nje ndani, jua kila kinachoendelea kwenye biashara hiyo ili uweze kuchukua hatua mapema pale changamoto zinapotokea.

SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

Kuwa tayari kujifunza kila siku ni tabia nyingine ambayo inasaidia biashara nyingi kukua. Kwa dunia ya sasa mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa sana, biashara unayofanya leo hii kuna uwezekano miaka kumi ijayo isiwepo kabisa. Tumeona jinsi ambavyo maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyoweza kuua biashara nyingi. Kwa mfano kwa sasa kila mtu anaweza kutumia intaneti kwenye simu yake ya mkononi, kwa namna hii biashara ya mikahawa ya intaneti imekufa. Ili kuweza kuona mabadiliko ya aina hii kabla hayajaleta madhara kwenye biashara, ni lazima mfanyabiashara awe tayari kujifunza kila siku kuhusu biashara yake na biashara kwa ujumla. Ni muhimu ajue mwenendo wa kibiashara upoje na hatua zipi muhimu za kuchukua. Kwa dunia ya sasa ni hatari sana kufanya biashara kwa mazoea.

Kwa wafanyabiashara wote ni muhimu kujifunza kuhusu biashara yako na biashara kwa ujumla kila siku. Jifunze mbinu bora za kuikuza biashara yako, kuongeza mkopo, kuajiri na pia kusimamia biashara yako ili uweze kuikuza.

Uaminifu ni tabia muhimu mno kwenye ukuaji wa biashara yoyote ile, bila ya uaminifu hakuna biashara. Kwa dunia ya sasa, hata kama mteja anahitaji kununua kwako mara moja tu, kama hujawa mwaminifu kwake kwa kumpa kile kweli anachohitaji, ana nafasi kubwa ya kukunyima wateja wengi zaidi. Watu sasa wana nguvu kubwa ya kuweza kuwasiliana na watu wengi ndani ya muda mfupi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Jambo lolote ambalo limewakera watu watashirikishana kupitia mitandao hii. Hivyo kama mteja hakuridhika, ni rahisi kuwaambia wengine na hivyo kukunyima wateja wengi zaidi. Uaminifu ni nguzo muhimu sana kwenye biashara, kwa sababu hakuna biashara kama hakuna wateja na hakuna wateja kama hakuna uaminifu.

Unapoamua kuingia kwenye biashara, kuwa mwaminifu, ahidi kile unachoweza kutekeleza na tekeleza kile unachoahidi. Usiongeze chumvi ili kuuza, unaweza kuuza mara moja na ikawa ndiyo mwisho wako kumuuzia mteja huyo na wengine wanaofahamiana naye. Kama kuna kitu ambacho bidhaa au huduma yako haiwezi kufanya kuwa mkweli na mweleze mteja wako hivyo, atakuamini na mtafanya biashara pamoja kwa muda mrefu.

SOMA; Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

Uvumilivu ni tabia nyingine ambayo imewezesha biashara nyingi kukua. Hakuna biashara ambayo haikutani na changamoto, hakuna biashara ambayo kila wakati tangu inaanza imekuwa inatengeneza faida tu. Kila biashara inapitia magumu, hasa mwanzoni. Kuna wakati biashara inakuwa inajiendesha kwa hasara, wakati mwingine wateja wanakuwa wasumbufu, bado pia wafanyakazi nao wanakuwa changamoto. Biashara yoyote inayoonekana kufanikiwa leo, imepitia changamoto nyingi huko nyuma. Ni uvumilivu wa waendeshaji wa biashara hizo ndiyo umewawezesha kufika pale walipo sasa.

Unapochagua kuingia kwenye biashara, jua unahitaji kuwa mvumilivu sana. Kama unaingia kwa lengo la kupata faida ya haraka, utakata tamaa mapema sana. Jiandae kuweka juhudi kubwa huku ukiwa mvumilivu na utapata matokeo bora kupitia biashara hiyo.
Mafanikio ya biashara yako yanaanza na wewe mwenyewe, biashara itakua au kufa kutokana na hatua unazochukua wewe mwenyewe. Chukua hatua bora ili biashara yako iweze kukua.

Nakutakia kila la kheri katika kufanyia kazi haya uliyojifunza.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
MUHIMU; Kama unataka ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu, bonyeza maandishi haya na utapata maelekezo. karibu sana tufanye kazi kwa pamoja.

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Matumizi Mabaya Ya Mtandao Wa Intaneti Na Kutumia Vizuri Muda Wako Kujiongezea Kipato.

$
0
0
Kama kuna mapinduzi ambayo kizazi hiki kinayashuhudia kwa macho basi ni mapinduzi ya kiteknolojia hasa kwenye kompyuta na mtandao wa intaneti. Mapinduzi mengi yaliyotokea huko nyuma hatukuwepo, tumekuwa tunayasikia tu kama mapinduzi ya viwanda.
Uzuri wa kuwa hai wakati wa mapinduzi ni kwamba unakuwa na nafasi kubwa ya kunufaika na mapinduzi hayo kuliko wale wanaokuja baadaye au waliochelewa kuyatumia mapinduzi hayo. Kwa mfano watu wengi ambao wanashikilia rekodi ya kuwa matajiri sana duniani walitokana na mapinduzi ya viwanda yaliyotokea karne ya 19 ulaya na marekani. Watu kama John Rockefeller walitumia vizuri mapinduzi ya viwanda kujijengea utajiri mkubwa.
Tukija kwenye zama zetu hizi za mapinduzi ya kiteknolojia, tunaona jinsi ambavyo mtandao wa intaneti umezalisha mabilionea wakubwa duniani. Watu kama Mark Zuckerberg, mmiliki wa mtandao wa Facebook ni bilionea aliyezalishwa na mapinduzi haya ya kiteknolojia. Wapo wengi ambao wananufaika sana na mapinduzi haya, swali ni je wewe unanufaikaje na mapinduzi haya? Hili ni swali muhimu tunalopaswa kujiuliza kila siku.


Mtandao wa intaneti umekuja na faida nyingi sana kwetu, kuanzia kuboresha kazi zetu, biashara zetu na hata maisha yetu kwa ujumla. Sasa hivi ni rahisi kutangaza biashara na hata kuwafikia wateja popote walipo duniani. Ni rahisi kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.
Lakini kila chenye faida hakikosi hasara, na mtandao wa intaneti umekuwa na hasara nyingi ambazo zimewazuia watu kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Mtandao wa intaneti umekuwa na ulevi mkubwa hasa kwa watumiaji ambao unawafanya washindwe kuweka muda kwenye yale mambo ya muhimu kwao. Leo kupitia makala hii ya ushauri wa changamoto tutaona jinsi ya kuondokana na ulevi huu ili kuweza kutumia muda wetu vizuri na kufikia malengo yetu.
Kabla hatujaangalia kwa undani hatua za kuchukua, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na changamoto hii.

Mimi nina changamoto mbili zinazonisumbua;
1. Kuondokana na matumizi mabaya ya internet kuna wakati internet inanisaidia sana lakini muda mwingine naitumia vibaya sana.
2. Pia siwezi kutumia muda vizuri.
Alex Thomas.

Alex pole sana kwa changamoto unayopitia, hii ni changamoto ambayo imekuwa inawasumbua wengi. Mimi binafsi nikiri ya kwamba kati ya mwaka 2010 mpaka 2011 nilikuwa mlevi mkubwa wa mitandao ya kijamii, lakini kuanzia 2012 niliweza kujua njia sahihi ya kunufaika na mtandao huu badala ya kupoteza tu muda. Lakini pia nikiri mara kwa mara bado napata changamoto ya kujikuta napoteza muda kwenye mitandao, lakini kwa kuwa nimeshajua najistukia haraka na kuacha kupoteza muda.
Hivyo basi Alex, mimi mwenyewe na wasomaji wote wa AMKA MTANZANIA, tutakwenda kushirikiana njia bora za kuondokana na ulevi wa mitandao hasa ya kijamii. Karibuni sana.
Kuna mengi sana ambayo tunaweza kushauriana kuhusu mitandao ya kijamii, lakini leo nitapenda tujadili kwa kina mambo matatu muhimu ya kila mmoja wetu kuzingatia ili kuweza kudhibiti matumizi yake ya mitandao ili asipoteze muda.

Jambo la kwanza; kuwa na utaratibu maalumu wa kutembelea mitandao hii.
Moja ya kitu kinachofanya matumizi ya mitandao kuwa changamoto ni ukaribu wake na urahisi wa kuitumia. Kwa kuwa mitandao hii ipo kwenye mikono yetu, nikimaanisha simu zetu za mkononi, ni rahisi sana kuingia hasa pale unapopata hata dakika moja. Urahisi huu unafanya tukiwa na upweke kidogo tu tufungue mitandao. Baadaye tunaingiwa na hofu kamba tusipofungua muda mrefu basi tunapitwa, na hivyo tunajikuta kila baada ya dakika chache tunachungulia tena tuone kipi kipya.

Utafiti uliowahi kufanywa, kuhusiana na simu hizi za kiganjani, unaonesha watu wanazishika simu zao mara nyingi mno, na mara zote ni kwenye mitandao ya kijamii.
Ili kuondokana na ulevi huu, jiwekee utaratibu wa kuingia kwenye mitandao hii ya kijamii kwa muda fulani wa siku. usikubali kila dakika uwe ‘online’, jitengee muda maalumu kila siku au kila baada ya masaa fulani ndiyo uingie kwenye mitandao hii. Muda mwingine uweke kwa ajili ya kazi na zima kabisa data kwenye simu yako.
Unapokuwa kwenye kazi ambayo inahitaji umakini, usikatishe ili kuingia kwenye mitandao, kwani unaporudi kwenye kazi yako unapoteza muda mwingi zaidi.

SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

Jambo la pili; ondoa taarifa za mitandao ya kijamii unazopata kupitia simu yako.
Kwenye simu zetu kuna kitu kinaitwa ‘notification’ hii ni ile taarifa ambayo simu yako inakupa kwamba kuna mtu kakutumia ujumbe, au kapenda picha yako kwenye mtandao. Taarifa hizi zina nguvu ya kukusukuma uchukue hatua haraka kuona ni ujumbe gani umetumiwa au nani kasema nini kuhusu ulichoweka kwenye mitandao.
Ili kuondokana na hili, futa kabisa kupotea taarifa hizi za kila kinachoendelea kwenye mitandao. Kwa njia hii hutasukumwa kufungua badala yake utafungua pale muda wako uliojipangia unapokuwa umefika.

Na kama unaona huwezi kuondoa notification, ondoa kabisa zile application ambazo ni za mitandao ya kijamii, na badala yake uwe unaingia moja kwa moja kupitia mtandao. Siyo lazima uwe na app zote za kufungua kila aina ya mtandao, kwa sababu kwa kuwa nazo utajikuta umetengeneza utaratibu wa kuzunguka kwenye mitandao hii. Kwa mfano unaanza na facebook, unaangalia kisha unaenda instagram, ukimaliza unaenda snapchat, unatoka hapo unaingia wasap, kisha telegram, ukifika huko ni muda unarudi kuangalia tena kama kuna jipya facebook, kisha instagram, na unajikuta unarudia mzunguko mzima hata mara tatu. Ukiondoa zile app ambazo siyo muhimu sana utapunguza kutembelea ile mitandao ambayo siyo muhimu kwako.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Pesa Zako Na Kuwa Tajiri.

Jambo la tatu; nufaika na mitandao hii.
Kama umeshafanya njia hizo mbili lakini bado huwezi kujizuia kutembelea mitandao hii kila mara, basi angalia ni kwa namna gani unaweza kunufaika na itandao hii. Yaani angalia unawezaje kuitumia kujiingizia kipato. Na habari njema sana kwako ni kwamba kila mtu, narudia tena KILA MTU anaweza kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.
Kwa kuanza, angalia ni vitu gani unapenda sana kutembelea kwenye mitandao hii, ni vitu gani unapenda kufuatilia zaidi. Ukishajua vitu hivyo angalia ni kwa namna gani unaweza kuwasaidia wengine wanaohitaji taarifa zinazohusiana na vile unavyopenda kufuatilia. Na hapo unaweza kuanzisha ukurasa maalumu kwa ajili ya mambo hayo na hata kuwa na blog au tovuti.
Pia unaweza kutumia mitandao hii kuboresha kazi unayofanya au biashara yako. unaweza kutumia mitandao hii kupata wateja wa kile unachofanya au kutoa taarifa kwa wale wanaohusika na unachofanya. Pia unaweza kutumia mitandao hii kufanya tafiti zinazohusu kazi au biashara yako. zipo njia nyingi za kunufaika ni wewe kuchagua kipi kinakufaa.

Ili kujua namna unavyoweza kujitengenezea kipato kupitia mtandao wa intaneti, nimeandika kitabu kinaitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kitabu hiki kina maelekezo yote na kwa njia ya picha ya jinsi unavyoweza kutengeneza blog yako mwenyewe na kuitumia kibiashara. Kitabu ni softcopy hivyo unaweza kusomea kwenye simu yako au kompyuta yako na kinatumwa kwa email. Gharama ya kitabu ni tsh elfu 10, kukipata tuma elfu kumi (10,000/=) kwa namba 0717396253 au 0755953887 kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu.
Hakikisha unanufaika na matumizi yako ya mitandao, usiwe tu mlaji, bali pia kuwa mzalishaji na uongeze kipato chako.
Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Ukifuata Maamuzi Haya, Utabadilisha Maisha Yako Kabisa.

$
0
0
Maisha uliyonayo sasa ni matokeo ya maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye maisha yako. Maamuzi yoyote unayoyafanya kila siku, yana uwezo wa kufanya maisha yako ya kesho kuwa mazuri au mabaya.
Kwa mfano, upo hapo na maisha yako hivyo kwa sababu ya maamuzi kadhaa ambayo ulishawahi kuyafanya kipindi cha nyuma. Maamuzi yako uliyokuwa ukiyafanya iwe kwa kujua au kutokujua ndiyo yaliyokufikisha hapo.
Kwa hiyo unaona ili kufanikiwa, maaumuzi mazuri ni kitu cha msingi sana. bila kuwa na maamuzi ya msingi itakuwa ni ndoto kubwa kufikia mafanikio. Ndio maana kila wakati unatakiwa ujiulize maamuzi ninayo yafanya sasa yanajenga maisha yangu au yanabomoa.
Ukishajua aina ya maamuzi sahihi unayotakiwa kuyafanya itakusaidia sana kubadilisha maisha yako. kwa kawaida wengi huwa ni watu wa kuharibu maisha yao kwa kufanya maamuzi yasiyo na miguu wala kichwa. Kwa kifupi wanafanya maamuzi yanayo wagharimu sana.
Ili kufanikiwa tunaona, ni lazima kujijengea maamuzi sahihi yanayokuongoza kwenye mafanikio. Kupitia makala hii leo, tutajifunza aina ya maamuzii ambayo ukiyafuata kila wakati yatabadilisha misha yako kabisa. Je, ni maamuzi yapi sahihi unayotakiwa kuyafata ili yakupe mabadiliko ya kweli?
1. Uamuzi wa kuchagua kufikiri.
Tatizo walilonalo watu wengi ni watu wa kuwaza tu na sio kufikiri. Naona unashangaa unawaza naongea kitu gani? Sikiliza, ipo tofauti kubwa kati  ya kufikiri na kuwaza.
Kufikiri ni mchakato unakufanya ukupe majibu juu ya suluhisho la matatizo yako. Unapokuwa unafikiri unakuwa unaweza ni nini ufanye ili uwaze kufanikiwa au kutoka kwenye hali ngumu uliyonayo.

Lakini unapowaza, unakuwa hutafuti sana suluhisho la mambo yako, zaidi unakuwa unaongozwa na matukio ya kawaida. Sasa ili uweze kufanikiwa ni lazima sana kwako wewe kufikiri na kupata majibu ya kie unachokitaka.
Ni muhimu kuchagua kufikiri kwa sababu hiyo itakupa mafanikio makubwa. Jiulize binafsi unafikiri au unawaza tu. Kama unawaza tu, elewa kufikia mafanikio yako itakuwa ni ngumu sana.
2. Uamuzi wa kuchagua kile tunachokizingatia.
Kile unachokizingatia sana kwenye akili yako ndicho unachokipata. Hauwezi kupata kitu ambacho hujakiweka kwenye akili yako. Kila wakati angalia ni kipi unachokizingatia sana na kukiwaza kila wakati kwenye akili yako? Kwani hicho bila shaka ndicho utakachokipata bila wasiwasi.
Unaweza ukawa shahidi katika hilo, hebu angalia yale mambo yote uliyoyatimiza kwenye maisha yako. Ukifatilia utagundua kwamba mambo hayo uliyazingatia sana kwenye akili yako kwa namna moja au nyingine ndiyo uliyoyapata. Hivyo, ni muhimu kuwa na uamuzi wa kuzingatia kile unachokitaka, utakipata hicho.
3. Uamuzi wa kuchagua kupanga mipango bora.
Kuchagua kufikiri vizuri na kuchagua kile tunachikizingatia hiyo peke yake haitoshi. Ili kuweza kubadilisha maisha yako kabisa pia unatakiwa pia kujiwekea mipango bora. Ni lazima kuweza kukaa chini na kupanga  kitu gani ni unachokitaka katika maisha yako.
Ukiishi tu kiholela bila kujiwekea mipango mizuri hiyo itakusumbua sana hata kufikia mafanikio yako makubwa. Watu wenye mafanikio makubwa ni watu wa kuishi kwa mipango mizuri ambayo badaae huamua kuisimamia mpaka itimie.
4. Uamuzi wa kuchukua hatua.
Kupanga mipango mizuri pekee hakutasaidia kama hatua sahihi hazitachukuliwa. Hivyo, hatua ni kitu cha muhimu sana ambacho kila wakati unatakiwa kukizingatia ii kuweza kufanikiwa. Bila kuzingatia kuchukua hatua kwa hakika hiyo inakuwa ni sawa na kazi bure.
Kumbuka kwa kuzingatia kila wakati uamuzi wa kuchagua kufikiri, uamuzi wa kuchagua kile tunachokizingatia, uamuzi wa kuchagua mipango bora na uamuzi wa kuchukua hatua dhidi ya maisha yako, hiyo itakusaidia sana kwako wewe kuweza kufanikiwa na kubadilisha maisha yako.
Nikutakie siku njema na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri, tembelea DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

UCHAMBUZI WA KITABU; Business @ The Speed Of Thought. (Mbinu Za Kufanya Biashara Kwenye Zama Hizi Za Taarifa).

$
0
0
Sasa tunaishi kwenye zama za taarifa ambapo wale ambao wana taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kuchukua maamuzi sahihi ndiyo wanaofanikiwa kwenye jambo lolote wanalofanya. Ni zama za kipekee sana ambazo tunaishi sasa ambapo mtu mmoja anaweza kushindana na kampuni kubwa.
Mtu mmoja mwenye kompyuta iliyounganishwa na mtandao wa intaneti anaweza kuwafikia watu wengi kuliko gazeti lenye wafanyakazi 50. Hii ndiyo nguvu ya zama hizi za taarifa, ambapo kompyuta na mtandao wa intaneti umeleta mabadiliko kwenye kila eneo la maisha yetu.

Kila mtu analijua jina la BILL GATES, huyu ni mtu tajiri namba moja duniani na pia mwanzilishi wa kampuni kubwa ya kompyuta inayoitwa MICROSOFT. Linapokuja swala la kompyuta na mtandao wa intaneti, basi wote tunaweza kukubaliana kwamba Bill Gates anajua hayo kuliko wengi wetu. Hivyo tuna wajibu wa kumsikiliza na kujifunza kutoka kwake.

Mwaka 1998, wakati mtandao wa intaneti ulikuwa bado haujapamba moto kama sasa, wakati huo wachache na hasa wenye uwezo mkubwa ndiyo walikuwa wanamiliki kompyuta, Bill Gates aliona mbali sana, aliona dunia ambayo karibu kila mtu atakuwa anatumia kompyuta yake mwenyewe. Aliona jinsi ambavyo kompyuta na mtandao wa intaneti utakavyoathiri kila eneo la maisha yetu, kuanzia kazi, biashara na hata afya zetu.
Lakini wakati huo wengi hawakuona hilo, wengi waliendelea kufanya biashara kwa mazoea. Bill Gates aliandika kitabu BUSINESS @ THE SPEED OF THOUGHT kuwaamsha wale ambao hawakuona mapinduzi haya makubwa. japokuwa kitabu hiki amekiandika muda mrefu, nimeona mengi ambayo bado huku kwenye nchi zetu zinazoendelea hatujaweza kuyafanyia kazi.


Biashara nyingi bado zinaendeshwa nje ya mtandao wa intaneti, yaani wafanyabiashara wengi bado hawapatikani kwenye mtandao wa intaneti na hawajaweza kutumia maendeleo haya ya kiteknolojia katika kurahisisha biashara zao.
Karibu kwenye uchambuzi wa kitabu hiki cha Bill Gates ambapo tunakwenda kujifunza namna tunavyoweza kutumia kompyuta na mtandao wa intaneti kufanya kazi zetu, biashara zetu na hata maisha yetu kwa ujumla kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.

Karibu tujifunze kwa pamoja.

1. Hakuna wakati ambapo biashara zimekuwa na ushindani mkali kama sasa, na ushindani huu unatokana na urahisi wa kuingia kwenye biashara. Hivyo njia ya uhakika ya mfanyabiashara kujiweka mbele ya wengine ni kuwa bora sana kwenye kile anachofanya, na kuwa bora kunatokana na taarifa anazopata na namna anavyozifanyia kazi. Wafanyabiashara wenye taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kuchukua hatua mapema ndiyo wanaunufaika na fursa zinazojitokeza kila wakati. Pata taarifa sahihi ili uweze kufanikiwa kwenye biashara unayofanya.

2. Taarifa zinazopatikana kwa sasa ni nyingi kuliko muda ambao mtu anaweza kupata wa kuzichambua na kuzifanyia kazi. Hivyo tatizo siyo tu kutokuwa na taarifa, bali kuweza kuchambua taarifa muhimu kutoka kwenye taarifa nyingi. Hapa Bill Gates anasema ni lazima uwe na mfumo mkuu wa taarifa kwenye biashara yako (DIGITAL NERVOUS SYSTEM). Kama ulivyo ubongo wako, unakusanya taarifa kutoka kila eneo la mwili wako na kuchukua hatua ili uweze kuwa hai. Hivyo ndivyo unavyopaswa kuitengeneza biashara yako, uwe na mfumo ambao utakusanya taarifa, kuzichakata na kuzitumia katika kufanya maamuzi sahihi.

3. Mzunguko wa taarifa kwenye biashara ndiyo uhai wa biashara. Haitoshi tu kuwa na taarifa, bali kama taarifa hizi atakuwa nazo kiongozi na wale wa chini yake hawana, haiwezi kuwa na msaada. Kila mtu anayehusika anapaswa kuwa na taarifa sahihi ili aweze kufanya maamuzi sahihi. Kuna ule ufanyaji biashara wa kizamani ambapo mmiliki wa biashara alikuwa anaficha baadhi ya taarifa wafanyakazi wake wasizijue, hii ina madhara makubwa kuliko faida. Pale kila anayehusika kwenye biashara anapojua kila kinachoendelea, anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi yatakayoiwezesha biashara kukua.

SOMA;  KITABU CHA JULY; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

4. Kama unafikiri una taarifa za kutosha kuhusu biashara yako, jaribu kujibu maswali haya kuhusu biashara yako;
a/. Wateja wako wanafikiriaje kuhusu bidhaa au huduma unayotoa kwenye biashara yako?
b/. Ni matatizo gani ambayo wateja wako wanataka yatatuliwe?
c/. Ni vitu gani vipya wanataka uongeze kwenye biashara yako?
d/. Ni changamoto gani ambazo mshirika wako wa kibiashara(kama yupo) anazipata kupitia biashara mnayofanya kwa pamoja?
e/. Ni maeneo gani ambayo washindani wako wa kibiashara wanapata faida kubwa ambayo wewe bado hujayajua?
f/. Je mabadiliko kwenye mahitaji ya wateja wako yanaweza kukusukuma wewe kubadili biashara unayofanya>
g/. Ni masoko gani mapya yanajitokeza ambayo bado hujaingia?
Kama huna majibu ya kutosha kuhusu maswali hayo basi huna taarifa za kutosha kuhusu biashara yako.

5. Hakuna kampuni inayoweza kujitamba kwamba iko salama kwenye soko lake, kwa ulimwengu wa sasa wenye ushindani mkali, kitu chochote kinaweza kuigwa. Biashara makini lazima mara zote iwe inaangalia mwenendo wa soko lake. Unaweza kufanya hivi kama utakuwa na taarifa za kutosha.

6. Kila kampuni/biashara ni lazima iweze kutumia mtandao wa intaneti katika kukusanya, kusambaza na kutoa taarifa zake. Hivyo kila biashara inahitaji kuwa na tovuti, hapa ndipo nyumbani kwa biashara, ambapo wateja wanaweza kujua kuhusu biashara hiyo. Pili kila biashara lazima iwe na mfumo wa barua pepe (email) ambapo watu wote wanaohusika kwenye biashara hiyo wanaunganishwa pamoja kwenye mfumo huo. Tatu kila biashara inahitaji kuwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo sehemu kubwa ya wateja wapo huko.

7. Pamoja na matumizi makubwa ya mtandao wa intaneti, haitakiwi kuondoa umuhimu wa ana kwa ana. Bado kampuni inapaswa kufanya vikao vya ana kwa ana, lakini vinakuwa vimerahisishwa na mtandao wa intaneti. Kwa mfano kabla ya watu kuhudhuria kikao wanakuwa wameshatumiwa ripoti kupitia email zao na wanakuja wakiwa tayari wameipitia na maoni yao kuhusu hali inavyokwenda.

8. Kila biashara ni sawa na mwili wa binadamu, ambapo kuna vitu muhimu vinavyofanya uhai wa mwili uendelee kuwepo. Mfano moyo unasukuma damu inayosambaza virutubisho mwilini, na mapafu yanayoleta hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu kwa maisha. Kwenye biashara moyo ndiyo uzalishaji ambao unatoa bidhaa au huduma ya biashara husika. Na mapafu ndiyo usimamizi wa biashara ambao unafanya biashara iendelee kuwa hai. Ili biashara iweze kufanikiwa, lazima mifumo hii iweze kufanya kazi kwa pamoja. Unapokuwa na taarifa sahihi kuhusu biashara yako, unaweza kuwa na usimamizi mzuri.

9. Mtandao wa intaneti unamwondoa mtu wa kati kwenye biashara nyingi. Kabla ya ujio wa intaneti, kati ya mzalishaji na mlaji kulikuwa na mtu wa kati, au watu wa kati ambao walikuwa wakitoa bidhaa na huduma kutoka kwa mzalishaji kwenda kwa mlaji. Lakini mtandao wa intaneti unamwezesha mlaji kununua moja kwa moja kutoka kwa mzalishaji.
Kwa mfano zamani kampuni za mawakala wa usafiri wa ndege, zilikuwa zikipata faida kubwa kwa kuwasaidia watu kukata tiketi za ndege, lakini sasa hivi karibu kila shirika la ndege linamwezesha mteja kukata tiketi yake mwenyewe akiwa nyumbani kwake kupitia mtandao wa intaneti kwenye tovuti ya kampuni.

10. Njia pekee ambayo mtu wa kati anaweza kuendelea kunufaika ni kuongeza thamani kwenye biashara husika. Huwezi kuendelea kuwa mtu wa kati kwa kufanya kile ambacho mteja anaweza kufanya mwenyewe kupitia mtandao wa intaneti. Badala yake mtu wa kati anahitaji kuongeza thamani ambayo itafanya mteja kupata huduma bora zaidi.
Kwa mfano wa kampuni ya uwakala wa safari za ndege, badala ya kumsaidia mtu kukata tiketi pekee, wanahitaji kumshauri mtu kuhusu usafiri bora, kumweleza kuhusu kule wanakotaka kwenda na mengine mengi muhimu. Kama hutaweza kuongeza thamani unaondolewa sokoni.

11. Mtandao wa intaneti umetoa uhuru mkubwa sana kwa wateja kuweza kupata kile ambacho wanakitaka, kile hasa kinachoendana nao. Zamani wafanyabiashara ndiyo walikuwa na nguvu ya kuamua ni nini wazalishe na mtu alilazimika kununua hata kama hakiendani naye kama anavyotaka. Uwepo wa wazalishaji wengi, na urahisi wa kupata taarifa unawapa wateja uhuru wa kutafuta kile hasa wanachotaka. Hivyo unahitaji kuwa na taarifa za kutosha kuhusu wateja wako ili uweze kuwa nao kwa muda mrefu, kwa kuwapa kile wanachotaka.

12. Kwa biashara zinazotoa huduma, mtandao wa inateni unatoa nafasi mbili, ni ama uwe mtoaji wa ujazo mkubwa kwa gharama ndogo, au utoe kile ambacho kinaendana na mteja moja kwa moja kwa gharama kubwa. Hapa unachagua kati ya kutoa kitu cha kawaida, ambacho kitawafaa wengi kama utauza kwa bei rahisi au utoe kitu cha kipekee ambacho kinaendana na wateja wachache ambao wapo tayari kulipa gharama kubwa. Unahitaji kuwa na taarifa ndiyo uweze kuamua unakwenda upande upi. Kila upande una faida na hasara zake.

13. Mtandao wa intaneti hauwezi kuondoa nafasi ya watu, bali inafanya watu kuwa bora zaidi kwenye kazi zao. Haina maana kwamba ujio na ubora wa intaneti kadiri siku zinavyokwenda utaondoa kabisa uhitaji wa watu, badala yake utawawezesha watu kufanya maamuzi bora zaidi. Biashara bado zinahitaji watu kuendesha na hivyo hakuna haja ya kuhofia nafasi za watu kuchukuliwa na teknolojia. Ila wale ambao hawataichukua teknolojia hii na kuitumia, nafasi zao zitapotezwa.

14. Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo tunavyozidi kugundua matumizi bora zaidi ya mtandao wa intaneti. Hii ina maana kwamba hapa tulipo bado hatujajua matumizi yote ya mtandao huu, kadiri siku zinavyokwenda ndiyo tunajua zaidi. Kwa mfano wakati mtandao huu unaanza, watu walikuwa wakitumia email na tovuti pekee, ni zaidi ya miaka kumi baadaye ndipo watu waligundua mitandao ya kijamii kupitia mtandao huu. Hatujui miaka kumi ijayo itakuwaje, lakini itakuwa bora kuliko ilivyo sasa, hivyo usikubali kuachwa nyuma. Wale walioona mitandao ya kijamii ni mambo ya vijana, wanajuta sasa, kuwa tayari kujifunza na kubadilika.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Sign-Posts On The Road To Success (Alama Muhimu Kwenye Safari Ya Mafanikio).

15. Mtandao wa inateni unatuwezesha kutengeneza jamii mpya za watu ambao tunaendana. Sasa hivi hulazimiki kuungana na ile jamii inayokuzunguka, badala yake unaweza kutafuta jamii inayoendana na kile unachoamini na mkawa pamoja kupitia mtandao wa intaneti. Makundi ya kwenye mitandao ya kijamii kama facebook na wasap yanawaleta pamoja watu wanaoamini kitu kimoja. Tumia nafasi hii kujenga jamii ya watu wanaoendana na biashara yako au kupata taarifa za kutosha kuhusiana na biashara yako.

16. Mtandao wa intaneti umerahisisha sana ufanyaji wa kazi kwenye biashara na makampuni. Zamani ilikuwa ukitaka kufanya kitu kwenye biashara yako ni mpaka uajiri mtaalamu wa kukifanya na hivyo kumlipa mshahara pamoja na kuingia gharama nyingine kama za posho za makazi, matibabu na kadhalika. Lakini mtandao wa intaneti umerahisisha sana hili, huhitaji tena kuajiri kwa kila jukumu la biashara yako. kuna majukumu unaweza kutafuta mtu kupitia mtandao wa intaneti, akafanya na likikamilika mkataba wenu unaishi hapo.
Kwa mfano kama unataka kutengeneza tovuti ya biashara yako huhitaji kuajiri msanifu wa kukutengenezea tovuti hiyo, badala yake unaweza kutoa jukumu hili kwa mtu anayetoa husuma hizo, akakutengenezea na mkishamaliza kila mtu anafanya mambo yake. Taarifa kama hizi unazipata kupitia mtandao wa intaneti.

17. Mtandao wa intaneti unatoa uhuru mkubwa wa mtu kuamua kujiajiri mwenyewe bila ya kuungana na wengine na kuwa washirika. Kwa mfano zamani mwanasheria alihitaji kujiunga na wenzake ili kuanzisha kampuni ya kisheria, au daktari kuungana na wenzake ili kutoa huduma za kitabibu. Walifanya hivi ili kusaidiana kutafuta wateja. Lakini sasa hivi kwa kuwa na kompyuta na mtandao wa intaneti na taarifa za kutosha, mwanasheria mmoja anaweza kuwa na kampuni yake ya kisheria, au daktari mmoja anaweza kutoa huduma za kitabibu kwa wateja wengi atakaopata kupitia mtandao huu.
Karibu kila utaalamu unaweza kunufaika na matumizi ya mtandao wa intaneti, kuanzia ualimu, uhasibu, ubunifu, usanifu, uinjinia, udalali na kazi nyingine.

18. Mtandao wa intaneti umefupisha muda ambao bidhaa inatumia tangu kuzalishwa mpaka kufika sokoni. Zamani bidhaa ilizalishwa, kisha inachukuliwa na mtu wa kati, na ndipo inapelekwa kwa mteja. Lakini sasa hivi mteja anaweza kununua moja kwa moja kutoka kwa mzalishaji. Hii inafupisha mzunguko wa wauzaji wa jumla na rejareja. Kwa kuwa na taarifa sahihi, biashara inaweza kuchukua hatua mapema na kunufaika na fursa. Dunia ya sasa watu wanataka bidhaa bora, kwa bei nafuu na wanataka bidhaa hizo sasa. Ni wewe mfanyabiashara kujua na kuchukua hatua.

19. Kila kampuni huwa inafanya makosa, kila biashara inapitia nyakati ambazo ni ngumu na changamoto ni kubwa. Biashara yoyote lazima itegemee nyakati kama hizi na hivyo kukusanya taarifa za kutosha ili kuweza kujua ni wakati gani sahihi wa kuchukua hatua. Ni lazima biashara iwe n adata za kutosha kuhusu uzalishaji wake, wateja wake, mauzo yake, faida zake. Na taarifa hizi zinapaswa kuwa kwenye mfumo ambao mabadiliko yoyote yanayotokea yanaonekana haraka. Kwa mfano kuwa na chati zinazoonesha mwenendo wa biashara, mambo yanapobadilika ni rahisi kuonekana.

20. Habari njema kwako, kwa kuwa na kompyuta, na mtandao wa intaneti una uwezo mkubwa wa kufanya chochote unachotaka, unayo dunia kwenye mikono yako. unaweza kumfikia mteja yeyote pale alipo, ni wewe kuwa na taarifa sahihi na kuchukua hatua sahihi. Hakuna ambacho huwezi kukifanya kupitia mtandao huu wa intaneti, hasa kwenye kukuza biashara yako;
Unaweza kuuza vitabu, nyimbo, video, nguo, viatu, mazao, huduma na vingine vingi. Uwepo wa mitandao ya kijamii umefanya kuwafikia wengi zaidi kupitia mtandao huu. Usikubali kuwa mtumiaji tu wa mitandao hii, badala yake anza kuifanya kuwa sehemu ya biashara yako. Kama hujui unawezaje kutumia mitandao hii kuboresha biashara yako karibu nikushauri namna bora ya kutumia mtandao kuboresha biashara yako. Nitafute kwa wasap kwenye namba 0717396253, karibu sana.

Hakuna uhuru mkubwa tunaoufaidi sasa kama mtandao wa intaneti, hakuna mapinduzi makubwa tunayoyashuhudia kama mapinduzi ya taarifa, usibaki mtazamaji, ingia ucheze.
Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Huyu Ndiye ‘STAA’ Muhimu Unayepaswa Kumfuatilia Kila Siku Kwenye Maisha Yako Ili Ufanikiwe.

$
0
0
Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini unaendelea vema katika kutimiza majukumu yako ya kila siku na hatimaye kujenga taifa imara. Maendeleo yako yanaletwa na wewe mwenyewe na taifa letu linajengwa na mimi na wewe katika yale mambo ambayo tunayafanya kila siku kwenye kazi zetu. Kiongozi pekee katika maisha yako anaweza kukuletea mabadiliko ni wewe mwenyewe. Wala usitegemee serikali ndio itakuletea mabadiliko au kiongozi fulani. 
 
Hakuna mtu anayefikiria maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe. Ukiendelea kusubiria kiongozi au serikali ikufanyie mabadiliko utakua unachelewa kwenye kila kitu katika maisha yako. Aliyekuwa gavana, mwigizaji na raisi wa awamu ya 40 wa Marekani Ronald Reagan aliwahi kunukuliwa akisema ‘’ Government is not solution to our problem; Government is the problem’’ akiwa na maana ya kwamba ‘’serikali siyo suluhisho la matatizo yetu; Serikali ni matatizo’’ kama ulikuwa hujui ukweli kuhusu hili ukweli ndio huu sasa. Kama ulikuwa hujui jua leo na amka na badilika.


Ndugu msomaji, hutakiwi kumlalamikia mtu yeyote wala kumlaumu mtu yeyote kwa maisha uliyo nayo sasa hivi. Jambo muhimu unalotakiwa kufanya ni kuchukua hatua na kuboresha pale ambapo panahitajika kuboreshwa.
Habari njema ni kwamba ndugu msomaji, leo tutakwenda kumjua ‘staa’ au mtu muhimu sana wa kumfuatilia kila siku katika maisha yako ili kuishi maisha sahihi. Na kama unajiuliza maswali mengi katika akili yako je ni ‘staa’ gani au mtu muhimu unayepaswa kumfuatilia katika maisha yako jibu la swali lako utalipata hapa endelea kusoma mpaka mwisho.

SOMA; Hawa Ndiyo Watu Muhimu Sana Wanaoleta Mabadiliko Katika Jamii Yetu.

Siku hizi watu wamekuwa wakifuatilia mambo ambayo hayana mchango kwao na kuamua kufuatilia watu ambao siyo sahihi katika maisha yao. Mtu muhimu au staa muhimu unayepaswa kumfuatilia katika maisha yako ni wewe mwenyewe. Ni bora kutumia nguvu na juhudi ulizonazo katika kufuatilia maisha ya watu wengine na kuelekeza juhudi na nguvu zako katika kuboresha maisha yako.

Ni utumwa kila siku ukiamka na kuanza kufuatilia leo msanii fulani amevaa nguo gani? Ameweka picha gani?, ameposti kitu gani, anatoka na nani au uhusiano wao umekuwaje ni kupoteza muda na nguvu zako bure. Badala ya kufuatilia mahusiano ya mastaa fulani katika maisha yako na anza kujifuatilia wewe mwenyewe katika maisha yako kwani wewe ndio staa wa maisha yako. Tumia muda na nguvu zako katika kufuatilia maisha yako na hapo ndio utaona mabadiliko katika maisha yako. Una mambo mengi ya kujifuatilia katika maisha yako, kujichunguza na kujitathmini kila siku. Watu wanatafuta muda wa kufuatilia maisha yao na siyo kutafuta muda wa kufuatilia maisha ya watu wengine. Wewe ndiyo staa pekee unapaswa kujifuatilia kila siku katika maisha yako.

Maeneo matatu muhimu unayopaswa kujifuatilia kila siku kabla ya kufutilia ya watu wengine ni kama ifuatavyo; unatakiwa kujifuatilia kila siku na kujitathimini kimwili, kiroho na kiakili. Jiulize kila siku maisha yako ya kiroho yako katika hali gani? Kila siku ni siku bora na mpya katika maisha yako ya kukua kiroho. Kaa katika hali ya ukimya yaani mahali palipo tulia anza kutafakari maisha yako, tafakari maisha yako wapi umetoka na wapi unakwenda? Kabla ya kuhukumu watu wengine jihukumu kwanza wewe mwenyewe. Usiwe mtu wa kuyahukumu maisha ya watu wengine anza kujihukumu kwanza wewe je wewe uko katika njia sahihi? Hakuna mtu ambaye amekamilika kuliko mtu mwingine ukisema umekamilika basi unajidanganya mwenyewe. Endelea kukua katika sekta hii na kumfuatilia staa muhimu katika maisha yako ambaye ni wewe mwenyewe.

Fanya tafakuri na siyo tafakari katika kujichunguza maisha yako ya kimwili yanaendaje. Kuna tofauti kati ya kutafakari na kutafakuri. Kutafakari ni kutafakari kwa kina na kutafakuri ni kutafakari kwa undani zaidi yaani unachimba kiundani kwa kingereza unaweza kusema ‘indeep’’ je unapata muda wa kufanya mazoezi? Unakula vyakula bora vinavyojenga mwili wako na kukupa kinga dhidi ya magonjwa? Unapata muda wa kutosha wa kupumzika yaani muda wa kupumzisha mwili wako ili kuamka na nguvu mpya? Mwili wako nao unahitaji mapumziko siyo kufanya tu kazi bila kujali afya. Jali afya kwanza kwani kazi unayofanya haiwezi kufanyika kama afya yako ikiwa mbovu. Kuna mambo mengi ya kujifuatilia katika maisha yako kabla ya kumfuatilia mtu mwingine. Unafuatilia malengo yako uliyojiwekea? Unafanya kazi zako kwa ubora na ufanisi? Unaongeza thamani katika eneo lako la kazi ulilopo? Kwa hiyo, chunguza na kutafakari kwa undani zaidi juu ya maisha yako.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; START WITH WHY, Jinsi Viongozi Wakubwa Wanavyohamasisha Watu Kuchukua Hatua.

Hazina ya akili yako ni maarifa. Je una maarifa ya kutosha katika akili yako? Unatakiwa kutumia muda wako katika kukua kiakili. Hakikisha unapata muda kila siku wa kulisha akili yako maarifa ya kutosha. Usipende kufuatilia habari hasi kwani habari hasi moja ina zaa hasi nyingine. Pendelea kuingiza habari chanya katika ubongo wako kwani ndio hazina ya akili yako. Badala ya kufuatilia habari za udaku fulani kafanya nini anza kujifuatilia umesoma vitabu vingapi na vinakusaidiaje kuboresha maisha yako. Maisha ni muda na ni marefu kama ukitumia muda wako vizuri. Tafuta maarifa chanya kwa faida ya maisha yako na ishi maisha yako kwa faida yako.

Mwisho, mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema maisha ambayo hayachunguzwi ni maisha ambayo hayana thamani kuishi. Hivyo basi, ni vema kuchunguza maisha yako kila siku na kujihukumu mwenyewe kabla ya kuhukumu mwingine. Mwandishi Makirita Amani aliwahi kuandika hivi katika ukurasa wa 481; jifukuze kwanza wewe mwenyewe. Usisubiri mpaka ufukuzwe bali jifukuze wewe mwenyewe ili uweze kuwa bora zaidi.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Njia Mbili(2) Rahisi Unazoweza Kuzitumia Kutengeneza Kipato Kupitia Mtandao Wa Intaneti.

$
0
0
Mtandao wa intaneti umeleta mapinduzi makubwa sana kwenye kila eneo la maisha yetu. Mtandao huu umefanya maisha kuwa rahisi kwa kutoa huduma ambazo hapo mwanzo hazikuwa zikipatikana. Kwa mfano mawasiliano, kupitia mtandao wa intaneti unaweza kuwasiliana na mtu popote pale alipo duniani kwa gharama ndogo.

Mtandao huu wa intaneti una nguvu kubwa katika kuanzisha na kukuza biashara. Pamoja na nguvu hii kubwa bado watu wengi hawajaweza kuutumia vizuri mtandao huu kwenye biashara zao. Inakadiriwa ya kwamba ziadi ya watanzania milioni 12 wanatumia mtandao wa intaneti. Na idadi hii inaongezeka kila siku kutokana na ujio wa simu za gharama ndogo ambazo zinaweza kutumia mtandao wa intaneti.


Je unawezaje kuutumia mtandao huu wa intaneti kibiashara?
Kuna njia mbili ambazo unaweza kuzitumia kwenye mtandao huu wa intaneti kibiashara. Njia ya kwanza ni kufanya mtandao wa intaneti kuwa ndiyo njia kuu ya kufanya biashara yako. Pili ni kutumia mtandao wa intaneti kukuza biashara yako ambayo haifanyiki kwa njia ya intaneti.

Kufanya mtandao wa intaneti kuwa njia kuu ya kufanya biashara.
Hapa unautumia mtandao wa intaneti moja kwa moja kujiingizia kipato. Hii ni njia rahisi ya kuanzisha biashara ambayo haina vikwazo vingi kama njia za kawaida. Kupitia njia hii, mtandao wa intaneti unakuwa ndiyo sehemu kuu ya biashara yako.
Hapa unaanzisha biashara yako kwenye mtandao huu wa intaneti, unapata wateja kupitia mtandao huu na pia unatoa huduma au bidhaa zako kupitia mtandao wa intaneti.

Hii ni nia rahisi ya kufanya biashara kwa sababu huhitaji kuwa na sehemu maalumu ya kufanyia biashara yako, hivyo unapunguza gharama za kibiashara, unaweza kuendesha biashara ukiwa hata nyumbani kwako. Pia huhitaji kuwa na bidhaa unayozalisha wewe, unaweza kumuunganisha muuzaji na mnunuaji na wewe ukapata faida yako.
Pia unahitaji gharama ndogo kuanzisha biashara ya aina hii, ukishakuwa na kompyuta na uwezo wa kuunganishwa kwenye mtandao wa intaneti tayari una nafasi kubwa ya kuanzisha biashara kupitia mtandao huu.

Baadhi ya biashara unazoweza kufanya kwenye mtandao wa intaneti.
1. Unaweza kufanya biashara ya kutoa taarifa kuhusu jambo fulani. Inawezekana taarifa za matukio, au taarifa za kibiashara, au mafunzo mbalimbali ambayo watu wanayahitaji. Kwa njia hii unaweza kujitengenezea kipato kupitia matangazo ambayo watu wanaweza kuweka kwenye mtandao wako. Pia unaweza kuwatoza watu ada ya kupata taarifa unazotoa.

2. Unaweza kutengeneza duka lako kwenye mtandao wa intaneti, watu wakafika pale, wakajichagulia bidhaa, wakaziagiza na kisha wewe kuwatumia. Hapa unakuwa na bidhaa zako au za wengine ambapo unatumia mtandao kama duka lako. Hapo utaweka maelezo ya bidhaa hizo pamoja na bei zake. Pia utaweza utaratibu wa malipo na watu wanajua jinsi ya kuzipata.

3. Unaweza kutoa huduma zako mwenyewe kupitia mtandao huu. Kama wewe ni mshauri, unaweza kutumia mtandao wa intaneti kuwafikia watu ambao wanahitaji huduma yako ya ushauri. Pia unaweza kutumia njia hii ya mtandao katika kutoa huduma zako moja kwa moja na watu wakakulipa.

Kutumia mtandao wa intaneti kukuza biashara yako.
Hata kama biashara yako haifanyiki moja kwa moja kwa njia ya intaneti, bado unaweza kutumia mtandao huu kuikuza ziadi. Hapa namaanisha biashara yako inafanyika kwa njia za kawaida, ili mteja apate bidhaa au huduma ni lazima aje kwenye eneo unalofanyia biashara. Kwa njia hii biashara yako i akuwa haitegemei mtandao wa intaneti moja kwa moja. Unaweza kukuza biashara yako kwa njia zifuatazo;

1. Unaweza kutumia mtandao kutangaza biashara yako na kufikia wateja wengi zaidi. Hapa utaweka matangazo na maelezo ya biashara yako kwenye mtandao na watu wanapokuwa na uhitaji, wanatafuta na kukutana na taarifa zako. Hii ni njia rahisi ya kutangaza biashara ukilinganisha na njia nyingine za kutangaza.

2. Unaweza kutumia mtandao kutoa taarifa muhimu kwa wateja wako kuhusu biashara yako. hapa unawafahamisha wateja wako kuhusu kinachoendelea kwenye biashara yako. Hii inawafanya wateja kuwa na taarifa sahihi kuhusu biashara yako ili kuweza kufanya maamuzi sahihi.

3. Unaweza kutumia mtandao wa intaneti kujenga jamii ya wateja wa biashara yako. hapa unaweza kutengeneza makundi kwenye mitandao ya intaneti ambayo yanawaleta pamoja wateja wa biashara yako. Kwa umoja wao unaweza kuwapa taarifa muhimu na pia kuweza kutatua changamoto ambazo wateja wanakutana nazo kwenye biashara yako.

Kama bado biashara yako haijaanza kutumia mtandao wa intaneti, unapoteza nafasi nzuri ya kukuza biashara yako. Ujue na kuutumia mtandao wa intaneti katika kuanzisha na kukuza biashara yako.
Kama bado hujajua unawezaje kutumia mtandao wa intaneti katika biashara yako soma kitabu JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG bonyeza hayo maandishi kupata kitabu hiko.

Nakutakia kila la kheri katika kuanzisha na kukuza biashara yako kupitia mtandao wa intaneti.
Rafiki Na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Ushauri Muhimu Kwa Wahitimu Wa Kidato Cha Sita 2016, Kozi Bora Kusoma Na Maisha Baada Ya Kufeli.

$
0
0
Huu ndiyo ule wakati wa mwaka ambapo wahitimu wa elimu ya sekondari kidato cha sita wamepata matokeo ya mitihani ambayo wameifanya. Na katika wakati kama huu kuna makundi makubwa mawili ya watu. Kundi la kwanza ni wale ambao wamefaulu vizuri mitihani yao na hivyo kuwa na sifa za kuendelea na elimu ya juu. Kundi la pili ni wale ambao wamefeli mitihani yao na hivyo kukosa sifa za moja kwa moja kuendelea na elimu ya juu. Nawakaribisha wote kwenye makala hii ya leo kwani kuna mengi muhimu ya kujifunza.


Kwa kuanza nipende kuwapongeza wahitimu wote kwa hatua hiyo kubwa mliyofikia kwenye maisha yetu. Haijalishi kama umefaulu mtihani au umefeli, kuweza kuhitimu kidato cha sita ni hatua kubwa umepiga kwenye maisha yako. kwa hesabu za miaka saba ya elimu ya msingi na miaka sita ya elimu ya sekondari, siyo chini ya miaka 13 umekuwa kwenye mfumo wa elimu. Ni safari ndefu, hongera kwa kuwa mvumilivu mpaka kufikia hatua hii.

Ushauri kwa wale waliofaulu mitihani yao juu ya kozi bora kusoma.
Maswali yanayoulizwa na wahitimu wengi ambao wamefaulu vizuri ni wasome kozi gani ambayo ni nzuri, ambayo itawawezesha kuwa na maisha mazuri. Swali hili kwa sasa lina majibu tofauti na ilivyokuwa miaka mitano iliyopita. Miaka ya zamani kozi za sayansi kama uinjinia na udaktari zilionekana kuwa kozi bora kusoma kutokana na upatikanaji wa uhakika wa ajira na kipato kizuri. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, hakuna tena kozi ambayo mtu akimaliza ajira ni uhakika na hata kipato siyo cha uhakika kama ilivyokuwa ikionekana hapo zamani.

Kujibu swali la kozi ipi bora mtu asome, ni kugumu kwa sababu kadiri siku zinavyokwenda mambo yanazidi kubadilika.

Mimi Makirita nina ushauri huu muhimu kuhusu kozi bora ambayo wewe mhitimu wa elimu ya sekondari unaweza kusoma. Kozi hiyo ni ile inayoendana na kile unachopenda kwenye maisha yako. chagua kozi ambayo inaendana na vipaji vyako. Hii ndiyo itakuwa kozi bora kwako, kwa sababu utaziona fursa nyingi na nzuri pale utakapohitimu.
Changamoto kubwa inaweza kuwa kwamba mpaka sasa hujajua kipaji chako ni nini. Na hii inatokana na jamii zetu kutokuweka mkazo mkubwa wa mtu kujua na kutumia kipaji chake. Umekuwa unakazana kusoma ili ufaulu, hivyo mengine yote umeweka pembeni.

Kama mpaka sasa hujajua vipaji vyako ni nini basi soma makala hizi na zitakupa mwanga wa vipaji vyako;
SOMA; Jinsi Ya Kugundua Vipaji Vilivyopo Ndani Yako.
SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

Ushauri kwa wale ambao wamefeli mitihani yao na hivyo kukosa sifa za kuendelea na elimu ya juu.
Pole sana kwako kama umefeli mtihani wa kidato cha sita. Napenda nikuambie kitu kimoja, kufeli shule siyo kufeli maisha, sawa najua umeshaambiwa hili mara nyingi lakini huamini kwa sababu wewe ndiyo unajua ni kwa namna gani kufeli kumekuumiza, hasa kama ulikuwa umejiandaa vizuri. Huu ndiyo wakati ambao unahitaji kufanya maamuzi muhimu sana kuhusu maisha yako. huu ndiyo wakati unaohitaji kuamua ni kitu gani hasa unachotaka kwenye maisha yako, sahau zile hadithi za jamii na jiangalie wewe, unataka kufika wapi kwenye maisha yako.

Kama unataka kuendelea na elimu basi chagua ni njia ipi utatumia mpaka kufikia kile kiwango cha elimu unachotaka. Kama unataka kuanza kujitengenezea kipato basi chagua ni njia ipi utakayotumia, ni elimu ipi ya ziada unayohitaji na ni thamani gani ambayo upo tayari kutoa kwa wengine.
Fanya haya sasa, usiendelee kupoteza muda wako kufikiria kwa nini umefeli mtihani, badala yake shika hatamu ya maisha yako na anza kuweka juhudi kwenye lile eneo ambalo umechagua kuchukua hatua.

Ushauri muhimu kwa wote, bila ya kujali umefaulu au umefeli.
Kwa kumaliza kidato cha sita, wewe sasa ni kijana ambaye unaelekea kwenye utu uzima. Kuna mambo muhimu hapa nitakushauri uanze kuyazingatia.

1. Anza kujitegemea wewe mwenyewe kifikra na kimaamuzi. Kama umeshafikisha miaka 21 na kuendelea, jifunze kufanya maamuzi muhimu ya maisha yako wewe mwenyewe. Acha kuangalia wengine wanafanya nini ndiyo na wewe ufanye, badala yake fanya kitu chenye maana kwako.

2. Usifanye kitu chochote kama huna malengo na mipango uliyojiwekea. Usifanye vitu kwa mazoea, au kwa sababu kila mtu anafanya. Fanya kitu unachojua kinakupeleka wapi na jua ni hatua zipi unazotumia kufikia kile unachotaka.

3. Anza kujitengenezea kipato chako mwenyewe. Hata kama unapata kutoka kwa wazazi au kwa njia nyingine kama mkopo wa elimu, jifunze kutoa thamani kwa wengine na uweze kujitengenezea kipato. Kama hujui njia zipi unazoweza kujitengenezea kipato chako soma makala hizi;

SOMA; Biashara Ambazo Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Anaweza Kufanya Bila Kuathiri Masomo Yake.
SOMA; JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

4. Chagua sana watu unaohusiana nao, unautumia nao muda wako mwingi. Wanasema ndege wanaofanana huruka pamoja. Na tabia zako ni wastani wa tabia za watu watano wanaokuzunguka. Ni wakati sasa uanze kuangalia ni watu gani unaohusiana nao, marafiki na watu wako wa karibu. Usikae na watu ambao hawajui ni wapi wanakoelekea, usikae na watu wasiojielewa. Chagua sana wale unaotumia nao muda wako. Ni bora uwe na marafiki wachache lakini wenye msaada kwako kuliko kuwa na marafiki wengi ambao wanakupoteza.

5. Jifunze kila siku, KILA SIKU. Iwe utaendelea na masomo au la, kujifunza ndiyo kwanza kumeanza. Unahitaji kujifunza kila siku, kwa kusoma vitabu vizuri, kusoma makala nzuri na kuhudhuria semina na mafunzo mbalimbali. Kusoma habari za udaku na magazeti siyo kujifunza, tenga muda wa kujifunza kila siku. isipite siku bila ya kujifunza kitu kizuri kwenye maisha yako.

6. Chagua falsafa ya maisha yako na ijenge na kuisimamia. Huenda huko ulikotoka ulikuwa unasimamiwa kila kitu na wazazi wako au walimu wako. Sasa hivi umeachiliwa uingie duniani, ambapo kuna kila aina ya changamoto. Huenda hukupata msingi mzuri wa huko duniani unakokwenda. Ili uweze kupona kwenye dunia hii yenye kila aina ya changamoto, unahitaji kuwa na falsafa unayoisimamia kwenye maisha yako. Ni lazima ujiwekee miiko wewe mwenyewe, wa mambo gani utafanya na yapi hutofanya hata iweje. Falsafa yako ndiyo itajenga tabia yako na kuweza kukuvusha kwenye changamoto.

7. Weka juhudi kubwa kwenye chochote unachochagua kufanya. Fanya kama ndiyo kitu pekee unachoweza kufanya. Kwa sasa huna sifa yoyote kwenye dunia hii, sasa ndiyo wakati wa kujijengea sifa. Sifa zinajengwa kwa vitendo, hivyo popote unapopata nafasi ya kufanya kitu, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Watu watakukumbuka kila wakati, na fursa nyingi zitakuja upande wako.

8. Kuhusu kula bata, kuwa makini. Wewe kama kijana unahitaji kupata muda wa kupumzika na kujistarehesha pia. Lakini kuwa makini sana, kuwa makini mno kula kwako bata kusiwe ndiyo kuharibu maisha yako. usipendelee kutumia vileo kama pombe, havina faida kubwa kwenye mwili wako. Usijaribu kabisa kuvuta kitu chochote kile, ni hatari sana kwa afya yako. usithubutu kabisa kutumia madawa ya kulevya, hata udanganywe kwa kiasi gani kwamba unaonja tu, kuna vitu vinaonjwa ila siyo madawa ya kulevya, ni hatari mno.

9. Kuwa mwaminifu, kuwa mwadilifu. Timiza kile ambacho unaahidi, sema ambacho unaweza kusimamia. Mara zote maneno yako na matendo yako viendane.

10. Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA, ambapo tutakuwa karibu zaidi tukijifunza kila siku kupitia kundi la wasap na makala kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye neno KISIMA CHA MAARIFA.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Sababu Zako Zinatosha, Sasa Ni Wakati Wa Kufanikiwa.

$
0
0
Kama una changamoto nyingi zinazokuzunguka acha kutumia changamoto hizo kama sababu ya kushindwa kwako kufanikiwa.
Kwa sababu umejaribu tena na tena na umefanya kazi kwa bidii, acha pia kutumia hiyo kama sababu ya kushindwa kwako kufanikiwa.
Eti kwa sababu huna mtaji wa kutosha, halikadhalika usiitumie ikawa sababu ya wewe kushindwa kufika kule unakotaka kimafanikio.
Acha kushindwa kufanikiwa eti pia kwa sababu uchumi wa dunia umekaa vibaya.
Sababu yoyote ile unayoiona ina maana usikufanye ukashindwa kwa lile ulilopanga. Ukitoa sababu hizo na ukaamua kupigana bila kujali unakabiliana na kitu gani ni hakika lazima ufanikiwa.
Kushindwa kwa namna yoyote ile ni kubaya sana. Acha kuhalalisha kushindwa kwako kwa sababu fulani fulani hivi.  Unapoamua kwamba sasa ushindwa na huwezi tena, elewa kabisa karibu kila kitu kinakufa kwenye maisha yako.

Ukishindwa utajikurta ni mtu wa kuua ndoto zako na hata maisha yako ya kimafanikio kwa baadae. Ikiwa utashindwa kufanikiwa, kumbuka hakuna mtu atapenda sana kukusogelea. Utakuwa kama mzoga uliokufa. Hakuna mtu ambaye anapenda kuwa karibu na maskini. Huna msaada.
Ni wakati wako sasa wa kuamua kutokushindwa sasa, bila kujali ni sababu gani ambayo inakuzunguka wewe.
Inawezekana ukawa huna mtaji, umekosa hamasa, umekatishwa tamaa, umejaribu sana na umeshindwa. Hayo yote yasiwe sababu kubwa sana ya wewe kushidwa. Sababu zako zimetosha sasa, ni wakati wa kufanikiwa, na kuamua kwamba na kwenda kufanikiwa bila kujali kitu.
Kama utaamua kuendeleza sababu kama ndiyo chanzo cha kutofanikiwa kwako ni kweli hutaweza kufanikiwa. Utakuwa ni sawa na mtu anayejipa matumani yasiyo na maana yoyote.
Kataa ushindwa kokote kusitokee katika maisha yako eti kwa sababu fulani fulani. Badala ya kuona kushindwa kwako kunatokana na sababu fulani, zifanye sababu hizo ndizo ziwe chanzo cha mafanikio yako makubwa.
Kwa mfano unaweza ukawa unaona hujafanikiwa kwa sababu hukusoma. Sasa kutokusoma huko kufanye iwe ndio sababu ya kutengeneza mafanikio makubwa mpaka wengine washindwe kujiamini.
Kaa chini, tafakari na utaona una uwezo mkubwa sana ndani yako ambao unaweza ukautumia na ukakupa mafanikio. Hivyo, jiambie mwenyewe pamoja na kwamba sijasoma lazima niwe tajiri mwenye mafanikio makubwa sana.
Ukisema kwa kumaanisha na ukachukua hatua basi baada ya muda hayo maneno yako yataumbika na kutengeneza uhalisi wa kile kitu unachokitamka kwenye maisha yako.
Fanya uamuzi mkubwa wa kukataa kuzuia mafanikio yako eti kwa sabubu hii au ile. Ishi maisha yako kwa kutengeneza  sababu kwa nini unatakiwa kufanikwa. Ila usiende kinyume cha hapo ukawa na sababu za kushindwa kwako.
Tatizo walilonalo watu wengi wanazo sababu nyingi zinazohalalisha kushindwa kwao. Kama bado unakusanya habari nyingi, sababu nyingi zinazokufanya wewe ushindwe, kumbuka huo muda umekwisha.
Sasa wakati ulionao ni wakati wa mafanikio yako. Tengeneza sababu nyingi za kufanikiwa kwako jinsi unavyoweza. Unaweza ukaziandika hata kwenye kijitabu chako zikafika hata mia. Lakini lilokubwa kuwa na saabu za kufanikiwa kwako ambazo zitakusaidia kutoka hpoa.
Kla wakati utakapoakaa na kutafakari juu ya maisha yako, jikumbushie hizo sababu zako za kwanini ni lazima ufanikiwe. Ukizijua sababu za kufanikiwa kwako hilo litakupa hamasa kubwa sana ya kutafuta mafanikio yako kwa udi na uvumba.
Daima uamuzi ni wako kufanikiwa au kutofanikiwa. Uamuzi ni wako kutafuta sababu za mafanikio au kutafuta sababu za kushindwa. Lakini jambo la msingi kwako leo jifunze sana kutafuta sababu za mafanikio yako, ukiweza hilo utafika mbali na hakika utakuwa tajiri.
Endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.comkila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,



UCHAMBUZI WA KITABU; TAO TE CHING (Falsafa Ya Uchina Ya Kukuwezesha Kuwa Na Maisha Bora Na Yenye Mafanikio).

$
0
0
TAO TE CHING kwa matamshi ni DAO DE JING ni kitabu ambacho kinaeleza kwa undani falsafa ya Uchina inayojulikana kama TAOISM kwa matamshi DAOISM. Taoism ni falsafa ya zamani sana ya china ambayo imekuwa ikichukuliwa kama dini. Falsafa hii ilitoa mwongozo kwa watu jinsi ya kusihi maisha yanayoendana na sheria za asili za dunia.

Falsafa hii imekuwepo kwa muda mrefu kabla haya ya falafa na dini nyingine kama ukristo na uislamu. Kupitia falsafa hii, msisitizo unawekwa kwamba kama kila mtu ataishi kama sheria za asili zinavyotaka maisha yaende, basi tutakuwa na dunia bora. Neno Tao limekuwa likichukuliwa kama njia iliyo sahihi, au msingi wa kufanya jambo fulani.


Kuna mambo mengi kuhusu maisha tunayoweza kujifunza kupitia falsafa hii. Leo kupitia uchambuzi wa kitabu hiki TAO TE CHING nitakwenda kukushirikisha yale muhimu. Angalia jinsi unavyoweza kuyatumia kwenye maisha yako ili kuwa bora sana. Kumbuka huna haja ya kuipokea falsafa hii kama ilivyo, au kuamini kila kitu kilichopo kwenye falsafa hii, badala yake unachagua yale yanayoendana na maisha yako.

Kitabu hiki kimeandikwa zaidi ya miaka 500 kabla ya kuja kwa Kristo, lakini mafundisho yake yanatufaa sana kwa dunia ya sasa. Hapa kuna madini yenye karibu miaka elfu 3 lakini bado yanatufaa kwenye maisha yetu ya sasa.
Karibu sana tujifunze kwa pamoja.

1. Ili kuwa na maisha bora, unahitaji kufanya yale yanayoendana na asili ya dunia. Ukizingatia sheria za asili utafanikiwa, ukienda kinyume na sheria za asili utakutana na ugumu. Kama ilivyo unahitaji kupanda ndiyo uvune, ukivuna kabla hujapanda, utajikuta kwenye wakati mgumu.

2. Uzuri na ubaya vyote vina asili moja. Panapokaa uzuri ndipo panapokaa ubaya. Hivyo mtu hawezi kuwa mzuri na mbaya kwa wakati mmoja, ni lazima achague kuwa mzuri au kuwa mbaya.

3. Kitu chochote ambacho ni kigumu sasa, kuna wakati kilikuwa rahisi. Na kwa mantiki hiyo, kitu unachoona ni rahisi sasa, baada ya muda kitakuwa kigumu. Hivyo kuwa makini na vitu rahisi unavyovichukulia poa sasa, vitakuja kuwa vigumu na vikushinde.

4. Kadiri unavyokazana kupata kitu au kuonekana na wengine, ndivyo unavyozidi kukosa kitu hiko. Yaani kama unakazana kuwafanya watu wakuone wewe ni mwema, hawatakuona mwema. Huhitaji kulazimisha vitu, unahitaji kufanya kilicho sahihi na utapata matokeo sahihi. Kama unataka watu wakuone mwema, huhitaji kujionesha, unahitaji kufanya mema, kila wakati bila ya kujali watu wanakuona au la.

5. Ni bora kuwa kama maji, maji ndiyo kitu chenye nguvu kubwa sana duniani. Na sababu hiyo ni kuwa tayari kubadilika. Maji huwezi kuyapasua kwa jiwe, kwa sababu ukiyapiga na jiwe yanabadili muundo wake. Lakini ukipiga jiwe kwa jiwe, yanapasuana. Maji yanaweza kupenya kwenye uchochoro wowote. Kuwa tayari kubadilika kama maji, endana na mazingira yoyote unayojikuta upo, na hakuna kitakachoweza kukuzuia kufanikiwa.

SOMA; Njia Mbili(2) Rahisi Unazoweza Kuzitumia Kutengeneza Kipato Kupitia Mtandao Wa Intaneti.

6. Sema kila unachoweza kukisimamia, na simamia unachosema. Simamia au ongoza wengine kwa usawa, fanya unachofanya kwa ubora, fanya mambo yako kwa wakati. Usilalamike wala kulaumu wengine. Hii ndiyo njia ya asili, ifuate.

7. Watu wanapoacha njia ya asili (Tao) ndipo mabaya yanapowakuta, watu wanadhulumiana na taifa kuangamia. Kama kila mtu ataifuata njia ya asili, tutaishi kwa amani na kushirikiana.

8. Kujisifu hakutakufanya ufanikiwe, kuonesha vile ulivyonavyo hakukufanyi uwe na maisha bora. Kujiona wewe ndiyo bora siyo njia nzuri ya kuongoza. Kufanya hayo yote ni kuenda kinyume na njia ya asili.

9. Hakuna kitu chochote unachoweza kukidhibiti kwenye dunia hii. Hivyo kujaribu kudhibiti vitu ni kujiweka kwenye nafasi ya kuumia. Fanya kwa kadiri ya uwezo wako, lakini jua kuna vitu vingi huwezi kudhibiti, hivyo kuwa tayari kupokea matokeo utakayopata.

10. Usitake kufanikiwa kwa kuwaangusha wengine, usifurahie kuanguka kwa wengine kunakokuweka wewe juu. Fanikiwa kwa juhudi unazoweka kwenye kile unachofanya, na siyo kwa kuwarudisha wengine nyuma.

11. Kuwaelewa wengine kunakufanya uwe na busara, kujijua wewe mwenyewe unakuwa umefikia kwenye kiwango cha juu kabisa cha uelewa. Kuwashinda wengine unahitaji nguvu, kujishinda wewe mwenyewe unahitaji mamlaka/utawala. Wajue wengine, lakini muhimu zaidi jijue wewe mwenyewe vizuri.

12. Kuna watu wanaonufaika kwenye kupoteza na kuna watu wanaopoteza kwenye kunufaika. Yaani hali yoyote ile inayotokea iwe nzuri au mbaya, kuna watu wanapata matokeo yasiyotegemewa. Yaani wakati ambao mambo ni magumu kuna watu wananeemeka, na katika wakati ambapo mambo ni mazuri kuna ambao wanataabika. Ukitaka kuneemeka hata pale mambo yakiwa magumu, fuata njia ya asili.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Matumizi Mabaya Ya Mtandao Wa Intaneti Na Kutumia Vizuri Muda Wako Kujiongezea Kipato.

13. Kila kitu kinapaswa kuwa na kiasi, ili kuwa na maisha bora, na uweze kuishi kwa muda mrefu, jua kipi ni kiasi kwako, jua ni wakati gani wa kuacha, usitake kupata kila kitu, usitake kushinda kila kitu, wakati mwingine acha na utanufaika zaidi.

14. Using’ang’ane na vitu ili watu wakujue kwa vile ulivyonavyo. Bali ng’ang’ana na kufanya ili watu wakujue kwa sifa zako. Utakapoondoka hapa duniani, hakuna atakayehadithia ulimiliki nini bali watu watahadithia ulibadilije maisha ya wengine. Chochote unachofanya, hakikisha unaongeza thamani kwa wengine.

15. Kadiri sheria zinavyokuwa nyingi, ndivyo wahalifu wanavyokuwa wengi. Kadiri vizuizi vinavyokuwa vingi ndivyo watu wanavyokuwa na maisha ya hovyo. Kadiri taifa linavyokuwa na silaha kubwa, ndivyo taifa hilo linavyokuwa ovu.

16. Jipange kwa ugumu wakati mambo ni rahisi, dhibiti makubwa wakati yakiwa bado ni madogo. Mambo yote magumu yanaanza kwa urahisi, na yale makubwa yanaanzia kwenye udogo. Unapoona mambo ni rahisi sana, jua kuna wakati utakutana na ugumu, jiandae mapema.

17. Safari ya maili mia moja inaanza na hatua moja. Ghorofa kubwa imejengwa kwa matofali. Hivyo chochote kikubwa unachotaka, unahitaji kuanza kwa hatua ndogo mpaka kuja kukipata. Usikate tamaa.

18. Kuna hazina tatu muhimu unazoweza kuzitumia kwenye maisha yako ili yawe bora;
Hazina ya kwanza ni huruma, kuwa na huruma kwa wengine.
Hazina ya pili ni kutokutumia zaidi ya unachopata, wengine wanaita ubahili.
Hazina ya tatu ni kutokwenda kinyume na sheria za asili.

19. Watu wanapoona hawashurutishwi kufuata kitu, wanachagua kukifuata wao wenyewe. Asili ya watu ni kupinga, hivyo unapolazimisha watu wafanye kitu, watakataa kufanya kwa sababu hawataki kulazimishwa. Lakini unapowafanya wachague kufanya wenyewe, wanafanya bila ya shida. Wape watu sababu, usiwalazimishe.

20. Maneno ya kweli siyo ya kufurahisha. Maneno yanayofurahisha siyo ya kweli. Vitu vizuri haviwavutii watu, na vitu vinavyowavutia watu siyo vizuri. Watu wenye busara siyo waliosoma, na waliosoma siyo wenye busara. Vitu vinavyoonekana kwa nje ni tofauti kabisa na vilivyo kwa ndani. Usidanganyike kwa kuona kwa nje, mara nyingi unachoona nje ni tofauti na kilichopo ndani.

Ni imani yangu mpaka sasa una falsafa ya maisha yako, kwa sababu maisha bila ya falsafa hayana mwelekeo wowote. Haya uliyojifunza leo, ongeza yanayofaa kwenye falsafa yako. Na kama mpaka sasa huna falsafa ya maisha yako, tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz na ujiandikishe ili uwe unapokea makala za FALSAFA MPYA YA MAISHA kila siku ya jumapili.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.
Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Hizi Ndizo Sehemu Nne (4) Muhimu Za Kuchota Baraka Katika Maisha Yako.

$
0
0
Habari mpendwa Rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Natumaini hujambo na karibu katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza pamoja na hatimaye kuongeza maarifa.
Tukiishi katika maisha ya visasi hatutafika bali tutazaa mauti. Ni vema kusamehe kwa faida yako na kisasi mwachie Mungu apambane na watesi wako. Mtesi wako mwekee kaa la moto kichwani, atembee nalo mwishowe litamchoma. Katika maisha kuna watu ambao wamekuwa miiba katika miili ya watu. Wamekuwa vikwazo kwako, wamekusababishia majeraha ya moyo, wamejeruhi nafsi yako kwa namna moja au nyingine. Hivyo basi, kila mtu atakua amepitia mateso fulani katika maisha yake na kuumizwa sana nafsi yake.

Ili upate furaha ya moyo yakupasa kuondoa uchungu ulioumbika ndani ya moyo wako. Unaondoa uchungu ulioumbika katika moyo wako kwa kusamehe na kuanza maisha mapya. Samehe ili uweze kusamehewa na wala usilipe kisasi kwa mtu aliyekufanyia ubaya bali njia pekee ni kumwachia Mungu apambane na watesi wako. Samehe kwa faida yako wewe mwenyewe.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA

Ndugu mpenzi msomaji, karibu katika makala yetu ya leo tujifunze sehemu za kuchota Baraka katika maisha yako. Kuna mambo mengine huwa unayafanya katika maisha bila kujua kama unajitengenezea mazingira ya Laana au Baraka. Maisha ya laana au baraka unayatengeneza wewe mwenyewe kwa kujua au kutokujua. Zifuatazo ni sehemu nne (4) muhimu za kuchota Baraka katika maisha yako.

1. Mungu; kila mtu ana imani yake ya dini lakini dini ni kiunganishi cha wewe kukutana au kuwasiliana na Mungu.’’ Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu, dunia na watu wote wakaao ndani yake ‘’hakuna mtu aliyejitoa kwa Mungu wake na akakosa kumpa Baraka katika maisha yake. Ukijitoa kwa Mungu kuna faida kubwa maisha yako yatakuwa na Baraka tele na wala sio laana. Kwahiyo, ukitaka kujichotea Baraka jitoe kwa Mungu wako , fanya kwa moyo kazi zake wala hutapungukiwa bali utazidi kuongezewa. Watu wanajisahau kwa kuhangaikia mambo ya kidunia na kumsahau Mungu. Mrudishie Mungu shukurani kwa yale aliyokujalia nawe utabarikiwa.

2. Wazazi; wazazi ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hakuna aliyeandika barua azaliwe na mzazi Fulani katika maisha yake. Ukweli ni kwamba wote tumejikuta tumezaliwa na wazazi ambao leo tunao. Unatakiwa kuwaheshimu wazazi wako. Wapokee na wapende kama walivyo hata kama wana udhaifu wapokee kwani ni wazazi wako waliokuzaa. Kuna baadhi ya wazazi ambao kweli walikuwa ni mwiba katika maisha yako lakini huna budi kuwasamehe. Mzazi amepewa mamlaka ya kukubariki au kukulaani hivyo ni vema kuwapenda wazazi wako. Mfano, kuna watu ambao wamewatelekeza wazazi wao bila hata ya kuwasaidia wakiwaacha wakiteseka katika shida wakati wana uwezo wa kuwasaidia.

Watunze wazazi wako, jitoe kwa wazazi na tumia muda na nguvu zako kuwatunza na kuwasaidia wazazi wako ili ujichotee Baraka. Kama usipojitoa kwa wazazi wako na mtoto wako naye hatakuja kujitoa kwako ukiwa mzee kwani atajifunza kupitia wewe kipindi ulikuwa huwathamini wazazi wako. Watunze na wapende wazazi wako wote bila kuwa bagua bila mama usingeweza kupatikana na bila baba usingeweza kupatikana. Kama wazazi wako wamekukosea waombee na mwachie Mungu apambane nao. Tekeleza wajibu wako wote kama mtoto kama ni kufanya kazi basi fanya kwa moyo na kufurahia kazi unazopewa. Kwa hiyo, kwa kujitoa kwa wazazi wako ni njia ya kujichotea Baraka katika maisha yako. Maisha yako yanaweza yasiende kama unakosa kuwatii na kuwaheshimu wazazi wako.

3. Watu Wengine; mwanafalsafa mmoja Zig Ziglar aliwahi kusema hivi ‘’ ukitaka kufanikiwa katika maisha yako saidia watu wengine kupata kile wanachokitaka na wewe utapata kile unachokitaka katika maisha yako’’ hii ni falsafa ya kweli kabisa katika maisha. Kama ulikuwa hujui basi anza leo kuifanyia kazi. Watu wengine ndio wanakusaidia wewe kufikia malengo yako. Huwezi kufanikiwa bila ya watu hivyo basi ni muhimu sana wewe kujenga mahusiano mazuri na watu ili uweze kufanikiwa.
Kumsaidia mtu siyo pesa tu kuna njia nyingi za kusaidia watu. Unatakiwa kuishi maisha ambayo yana msaada kwa watu wengine. Wasaidie watu kupata kile wanachokitaka na wewe unajichotea Baraka tele katika maisha yako. Toa maisha yako kwa ajili ya watu wengine hakika hutapata hasara wala laana bali utajichotea Baraka nyingi katika maisha yako.

4. Familia Yako; kama una familia basi jitoe kwa moyo katika familia yako ili uweze kujichotea Baraka na kufanikiwa katika kazi zako. Hudumia familia yako kwa moyo na kwa upendo. Jitoe kwa familia yako bila kujibakiza kuwa na upendo wa kujitoa kwa ajili ya familia yako. Wasaidie watoto wako, mke au mume wako katika kutatua matatizo yao. Usigeuke kuwa mwiba katika familia yako. Kuna wazazi wengine wanatelekeza familia zao kwa kukwepa majukumu. Ni rahisi kukwepa majukumu yako lakini ni ngumu kukwepa matokeo ya majukumu yako. Kama katika familia yako mnaishi maisha ya paka na panya hakuna amani wala upendo siyo maisha hayo kabisa.
Waswahili wanasema tembo wakipigana nyasi hulia au huumia hivyo basi, wazazi wakigombana na kuwa na magomvi kila siku wahanga wakubwa wa matatizo katika familia ni watoto. Wazazi wakiwa na ugomvi katika familia wahanga wakubwa ni watoto. 

Wazazi wanageuka kuwa kero na vikwazo kwa watoto kwa kujeruhi mioyo ya watoto. Fanya watoto wako wafurahie kuwepo duniani na siyo kujihisi siyo sehemu salama ya kuishi. Unatakiwa kujitoa kwa upendo na kuwa tayari kufa kwa ajili ya familia yako.
Kwa kutamatisha, kama unaweza kujitoa kwa mambo ya kidunia basi, usisahau kujitoa kwa Mungu wako, wazazi wako, familia yako na watu wengine pia ili uweze kujichotea Baraka katika maisha yako. Kama umekosana na mwenzako sameheaneni kwani kusamehe ni kurudisha uhusiano wa awali kati ya mkosewa na mkosa.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Mambo Matano(5) Muhimu Ya Kuzingatia Unapoomba Na Kupokea Ushauri Wa Biashara.

$
0
0
Moja ya vitu ambavyo vinapatikana kwa urahisi sana kwenye jamii zetu ni ushauri. Karibu kila mtu anaweza kumshauri kila mtu kuhusu kila kitu. Hakuna kitu ambacho watu wapo tayari kutoa kama ushauri. Sema tu tatizo lako na kwa haraka sana watu wanakupa ushauri ambao kwa wao wanaona ni bora kwako kufuata. Lakini ushauri huu unaotolewa na kila mtu siyo ushauri bora kufuata kwenye kila unachofanya. Wapo watu wengi ambao wamepokea ushauri na kuutumia ukawapa matokeo mabaya kuliko yale ambayo walikuwa nayo.

Ushauri wa biashara umekuwa unatolewa kirahisi sana. Nenda popote na waulize watu ni biashara gani nzuri nifanye, kila mtu atakupa maoni yake, na watakupa mifano jinsi wengine walivyonufaika na biashara hiyo wanayokushauri. Usipofanya tathmini ya kutosha, unaweza kuingia kichwa kichwa na mwisho ukajikuta unaumia badala ya kunufaika.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA
 
Leo tunakwenda kushirikishana mambo ya kuzingatia katika ushauri ili uweze kupata ushauri bora utakaoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

1. Pata ushauri wa kitaalamu.
Kuwa makini na ushauri unaopokea, jiulize unatoka wapi ushauri huo. Pokea ushauri kutoka kwa watu ambao wana uzoefu na uelewa juu ya kile wanachokushauri. Hapa utapata ushauri unaoendana na uhalisia. Unapopata ushauri kutoka kwa wanaofanya, unapata kile hasa unachokwenda kukutana nacho, hapa unapewa ukweli unaoendana na kile unachotaka kujua.

Wale wasiokuwa na uzoefu au utaalamu watakuambia vitu ambavyo wao pia wamesikia. Huenda walisikia watu wanasema biashara fulani inalipa, wakaona watu watatu wanaofanya biashara hiyo na inawalipa, halafu wanakushauri na wewe. Kwa njia hii hutapata picha halisi ya kile unachokwenda kufanya. Kuwepo kwa watu wachache waliofanikiwa kwenye biashara fulani hakuifanyi biashara hiyo kuwa bora.
SOMA; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya.

2. Siyo kila kitu kwenye ushauri kitakufaa wewe.
Jambo jingine muhimu sana kuzingatia kwenye ushauri ni kujua kwamba siyo kila kitu kwenye ushauri kitakufaa wewe katika biashara yako. Badala yake unahitaji kuangalia ni vipi kwenye ushauri unaopata vinakufaa kwenye biashara yako. Pia angalia namna ambavyo unaweza kuboresha ushauri unaoupata uendane na biashara yako wewe. Anayekupa ushauri atakupa kulingana na uzoefu wake yeye, lakini wewe ndiye unayeijua biashara yako vizuri zaidi, hivyo jua kipi unaweza kukitumia wapi.
Ushauri siyo msaafu kwamba utumike kama ulivyo, bali unahitaji kuuchambua na kuona ni vitu gani vinaweza kwenda na hali uliyonayo wewe. Pokea ushauri na uchambue ukiangalia biashara yako na malengo yako ya kibiashara.

3. Mambo yanabadilika, kilichowezekana jana siyo lazima kiwezekane leo.
Hili ni muhimu kulizingatia kwenye ushauri unaopokea, wengine watakupa ushauri ambao ulileta matokeo mazuri siku za nyuma. Lakini kutokana na mabadiliko ambayo yametokea, ushauri huo unaweza usitoe matokeo bora kwa sasa. Unapopokea ushauri, angalia nyakati ambapo ushauri huo ulikuwa bora, kisha angalia nyakati hizi baada ya mabadiliko. Kisha angalia ni jinsi gani unaweza kuboresha ushauri huo uendane na hali ya sasa. Hata kwenye biashara yako mwenyewe, mbinu zilizokufikisha hapo ulipo sasa, siyo zitakazokupeleka mbali zaidi, ni lazima ujue mabadiliko yanayotokea yanakuhitaji wewe ubadili nini.

4. Unaweza kujishauri mwenyewe pia.
Kila kitu unachofanya kwenye biashara yako, kitumie kama sehemu ya kujifunza. Hivyo unapokutana na changamoto yoyote kwenye biashara yako, jikumbushe changamoto kama hizo ulizopitia siku za nyuma, ulichukua hatua gani na ukapata majibu gani. Hapa unaweza kurudia hatua hizo ulizochukua au kuchukua hatua tofauti na ulizochukua awali. Pia unaweza kuwaangalia wengine jinsi ambavyo wamekuwa wanafanya mambo yao, na ukajiuliza kwenye hali kama hii, mtu fulani angefanya nini? Hapa unaweza kujishauri wewe mwenyewe na kupata matokeo mazuri. Mtu huyu unayemtumia kama mfano anakuwa ni mtu anayekuhamasisha kutokana na mafanikio aliyopata kwenye kile anachofanya.
SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kutajirika kwa kuanza na shilingi elfu moja

5. Ushauri wa bure una gharama kubwa.
Kila ushauri unaopokea unaulipia, unaweza kuchagua kulipa mwanzo na kupata ushauri bora ambao utakuepusha na hasara, au unaweza kuamua kuchukua ushauri wa bure na ukalipa wakati utakapotumia ushauri huo na kupata hasara. Ushauri wa bure una gharama kubwa kwa sababu utapata ushauri ambao siyo bora na hivyo utakapoutekeleza lazima utakutana na changamoto na kupata hasara. Hivyo usikimbilie ushauri wa bure, ni vyema ukachukua muda kuchuja kila ushauri unaoupata kabla hujaufanyia kazi.
Hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kujua kila kitu mwenyewe, hii ndiyo maana tunahitaji ushauri mara kwa mara ili tuweze kufanya maamuzi bora kwenye biashara zetu. Hakikisha ushauri unaoupata unaufanya uendane na biashara yako kabla hujaanza kuutumia.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako,
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kwa ushauri bonyeza maandishi haya kupata utaratibu wa ushauri. karibu sana.
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>