Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

Taarifa muhimu kuhusu KISIMA CHA MAARIFA.

$
0
0
Habari rafiki?
Naomba nichukue nafasi hii kukupa taarifa muhimu kuhusu KISIMA CHA MAARIFA kwa wale ambao tayari ni wanachama na ambao siyo wanachama.
Kulikuwa na tatizo la kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambapo baadhi ya wanachama walishindwa kuingia na kusoma makala kama ilivyo kawaida. Tatizo hili lilitokana na mfumo wetu kuwa na shida fulani.
Kwa sasa tumebadili mfumo na kuwa bora zaidi. Kwa sasa kila mwanachama anaweza kujiandikisha na kubadili taarifa zake yeye mwenyewe, tofauti na ilivyokuwa awali.
Kutokana na mabadiliko haya ya mfumo, kuna baadhi ya taarifa za wanachama zimebadilika, ikiwepo password.
Hivyo nawaomba wanachama wote mchukue hatua zifuatazo;
  1. Nenda kwenye kisima cha maarifa, kisimachamaarifa.co.tz fungua makala yoyote kusoma, itakuletea taarifa kwamba ili usome makala lazima uwe mwanachama au ulog in.
  2. Log in kwenye nafasi iliyotolewa, weka username na password, kisha bonyeza logi n. Kama utafanikiwa utaendelea kusoma makala. Kama itashindikana itakuambia logi n failed, bonyeza click here to continue.
  3. Itakuletea upya fomu ya kujaza, bonyeza sehemu ya kulog in, bonyeza sehemu ya FORGOT PASSWORD, CLICK HERE TO RESET ukibonyeza hapo itakuletea fomu ya kuomba kubadili password.
  4. Weka username yako na email yako, utatumiwa email ya kubadili password, fuata maelekezo.
  5. Nenda kwenye email yako kuangalia email iliyotoka Makirita Amani Kisima cha maarifa, kama huioni nenda kwenye spam email, kama huioni nenda sehemu ya kusearch kisha search MAKIRITA AMANI KISIMA CHA MAARIFA.
  6. Ukishapata email kuna link utabonyeza itakuletea sehemu ya password mpya, kuna password itapendekezwa, usichukue hiyo, ifute na weka password mpya utakayoikumbuka.
  7. Badilisha password yako na utatumiwa email ikikuambia password imebadilishwa.
Kwa wale ambao siyo wanachama, ingia; www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha au BONYEZA MAANDISHI HAYA kujiandikisha. Ukishajiandikisha utatumiwa email yenye maelekezo ya kuwa mwanachama. Hutaweza kulog in mpaka pale uanachama wako utakapodhibitishwa. Ukijiunga halafu ukawa hujapokea email angalia kwenye spam email utakuta email.
Karibu sana, kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, jiunge leo kwa kutembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha au KUBONYEZA HAPA KUJIUNGA
Niombe radhi kwa usumbufu wowote ambao umeupata katika kipindi hiki.
Tuendelee kuwa pamoja, tukishirikishana maarifa bora ya kufanya maisha yetu kuwa bora zaidi na kufikia mafanikio makubwa.
Kama unaendelea kupata shida kusoma makala kwenye KISIMA CHA MAARIFA, nitumie ujumbe kwa njia ya wasap kwenye namba 0717 396 253
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

NYEUSI NA NYEUPE; Kwa Nini Habari Hasi Zinavuma Na Kupendwa Sana Na Wengi, Na Jinsi Ya Kujitoa Kwenye Mkumbo Huo.

$
0
0
Habari za jumapili ya leo rafiki yangu?
Karibu kwenye makala yetu nyingine ya NYEUSI NA NYEUPE, hapa tunauangalia ukweli wenyewe kama yulivyo, hatufuniki au kuficha chochote. Jembe tunaliita jembe na kijiko tunakiita kijiko, hata kama itakuumiza kwa namna yoyote ile. Kama ambavyo tunajua, kitu pekee kinachoweza kukuweka huru ni kuujua ukweli. Unaweza kuukataa ukweli, unaweza kuukwepa ukweli lakini hayo yote hayawezi kubadili ukweli.
Leo tunakwenda kuangalia eneo moja muhimu mno, eneo ambalo nimeona wengi wakilishangaa na wengine kujikuta kwenye mkumbo bila ya kujua wameingiaje, na mbaya zaidi hawajui watatokaje. Hili ni eneo muhimu kwa sababu kila siku tunakutana na mambo haya.


Nunua gazeti lolote kusoma na habari utakayokutana nayo ukurasa wa mbele ni habari hasi au inayokujaza hofu. Ukisoma vichwa vya mbele vya habari pekee, na ukaondoka bila ya kuangalia ndani, unaweza kusema dunia imefika mwisho kabisa, hakuna tena jambo zuri linaloweza kufanyika.
Fungulia habari yoyote kwenye televisheni au redio, na habari za kwanza unazokutana nazo ni habari ambazo ni hasi, habari ambazo zitakupa hofu kubwa. Utasikia mtu kajiua au kaua wenzake, utasikia mapigano ya watu au waasi na serkali. Utasikia kila aina ya habari ambayo itakufanya uone dunia inaisha kabisa.

Zamani mambo haya yalikuwa yanaishia kwenye magazeti, redio na tv, lakini sasa hivi kimekuja chombo kipya cha habari ambacho kinachochea moto wa habari hasi. Chombo hiki kimekuwa hatari sana kwa sababu kinawafikia watu wengi kwa haraka mno na kwa masaa yote 24 ya siku. chombo hiki ndiyo kimenifanya niandike leo kwa sababu naona namna watu wengi wakipotezwa na chombo hiki, bila ya kuja hatua za kuchukua.

Chombo ninachozungumzia hapa ni mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya kupashana habari kwa urahisi siku hizi. Huhitaji kusubiri mpaka muda wa taarifa ya habari, au usubiri mpaka magazeti yachapwe, mitandao ya kijamii itakupa habari pale pale inapotokea. Kwa mfano ikitokea ajali, mpaka uisikie kwenye habari ni usiku wakati wa taarifa za habari, au upewe kama habari mpasuko baada ya muda fulani kupita, chombo cha habari kijidhihirishie kwamba habari ni ya kweli, pia utasubiri mpaka kesho yake ndiyo usome kwenye magazeti. Lakini hali haipo hivyo kwenye mitandao ya kijamii, ajali imetokea sasa, kama kuna mwenye simu na mtandao upo basi dakika hiyo hiyo picha za ajali zipo kwenye mitandao.
Hivyo mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya kusambaza habari hasi na hofu kwa urahisi zaidi na kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja. Hii imeleta changamoto kwa wengine.

SOMA; MITANDAO YA KIJAMII; JE NI BARAKA AMA LAANA KWAKO?

Kabla sijaendelea nataka nikiri kwamba mitandao ya kijamii imekuwa na faida kubwa sana kwetu, imeweza kutuunganisha na hata kutuingizia kipato. Lakini kila chenye faida huja na kasoro zake. Na hapa tunaangalia kasoro moja ya mitandao hii, ambayo kila mtumiaji anapaswa kuijua ili kuweza kuiepuka.

Kwa nini habari hasi na zenye hofu zinapewa kipaumbele kikubwa?

Tuanze na mifano hai kabisa ya kila siku;
Kuna mambo mengi mazuri yanafanywa na watu, lakini hutaona watu wakiyapa kipaumbele, ila pale jambo moja baya linapofanywa, kila mtu atajua kuhusu jambo hilo.

Kuna tafiti nyingi sana ambazo zinafanywa kila siku na watafiti wa kijamii, kisayansi na kitabibu, lakini hutaona watu wakizijadili na kushadadia. Ila unapokuja utafiti kwamba katika kila watanzania wanne, mmoja wao ana matatizo ya akili, kila mtu ataijua na kujadili tafiti hiyo.

SOMA; Mambo 4 Yanayosababisha Uwe Na Fikra Hasi.

Kuna madaktari wengi wanafanya kazi zao kwa kujituma, wapo wanaokesha kwenye kazi zao kuhakikisha wagonjwa wao wanakuwa na afya njema, hutaona madaktari hawa wakiwa mjadala wa kitaifa. Ila anapotokea daktari mmoja akafanya makosa na mgonjwa akapata matatizo basi itakuwa habari ambayo kila mtu ataijua na kuijadili, watu watatoka kulaani vile wawezavyo.

Kuna walimu wengi wanafanya kazi zao kwa moyo wa kujitoa. Walimu hao wapo katika mazingira mabovu, lakini wanaendelea kuweka juhudi kuhakikisha wanatoa mchango bora kwa kujenga taifa letu, wanafanya mambo ambayo hata hawalipwi. Lakini hutasikia habari za walimu wa aina hii zikiwa gumzo la kitaifa, ili kuwapa moyo na kuwahamasisha wengine nao kuwa kama wao. Lakini inapotokea mwalimu mmoja amefanya kosa kwenye kazi yake, ambalo linapelekea hali ya elimu kutokuwa nzuri, kila mtu atajua, kila mtu atajadili, kila mtu atalaani. Hata asiye na habari za kutosha atakuwa na la kusema.
Kwa haya na mengine mengi yanayotokea kwenye maisha yetu ya kila siku, ni lazima tujiulize kwa nini habari hasi zinapewa kipaumbele kuliko habari chanya? Na hapa ndipo tunahitaji kuzama ndani, ili kuja na nyeusi na nyeupe kuhusu hali hii.

Sababu ya kwanza; tunaishi maisha ya miaka 3000 kabla ya kuja kwa Kristo (3000B.C)
Hii ina maana gani?
Hapo zamani sana, huenda mbali zaidi ya mwaka nilioandika hapo, maisha ya wanadamu yalikuwa hatarini. Binadamu walikuwa wakiishi kwenye mazingira ambayo siyo salama, walikuwa wakiishi maporini pamoja na wanyama. Hivyo wakati wowote mtu angeweza kuliwa na mnyama mkali, kudhuriwa na wadudu na hata kudhurika na mazingira hayo hatari.

Hivyo basi, wale wazee wetu wa enzi hizo wakajifunza namba ya kuhakikisha wanapona, na hivyo kujifunza namna ya kuiona hatari kabla hata haijatokea. Kwa hiyo kama yupo porini na kusikia kishindo inabidi aanze kukimbia hata kama hajui ni nini kimesababisha kishindo hiko. Huenda ni mnyama mkali anakuja, au huenda ni jiwe limeanguka. Kwa kukimbia kabla ya kuona kishindo kimesababishwa na nini, kulipelekea mtu kuokoa maisha yake. Kama kishindo ni cha mnyama, basi amepona kuliwa, na kama kishindo ni cha jiwe, basi hakuna ambacho amepoteza kwa kukimbia.

Kwa kifupi, risk ya kukimbia ilikuwa ndogo kiliko kukaa wakati hujui ni kipi kinakuja. Hivyo watu walijifunza kuangalia mambo hasi kwanza kwenye kila mazingira waliyopo. Hali hii waliirithishwa kwa vizazi vilivyofuata na mpaka sasa imefika kwetu. Akili zetu zinatoa kipaumbele kwa mambo hasi na ya hofu kuliko mambo chanya. Na miili yetu ina mfumo wa kuhakikisha tunapona kwenye mazingira hayo. Nafikiri umewahi kufukuzwa na mbwa na kujikuta unapanda ukuta ambao ukija kujaribu kuupanda tena huwezi, hivi ndivyo mwili ulivyojipanga kuhakikisha unakuwa salama.

SOMA; Dalili Sita(6) Kwamba Una Fikra Hasi Zinazokuzuia Kufikia Mafanikio Na Jinsi Ya Kuondokana Nazo.

Sababu ya pili; kuhakikisha siyo sisi au siyo watu tunaowajua.
Inapotokea hali fulani ambayo siyo nzuri, kwa mfano ajali, huwa tunapenda kujua wa kwanza ili kuhakikisha sisi hatuhusiki moja kwa moja, au wale ambao ni wa karibu kwetu hawahusiki. Hii pia ni zao la hofu ile ambayo tunaishi nayo kwamba mazingira siyo mazuri. Hivyo tunapendelea kujua habari hasi ili kujihakikishia kwamba sisi wenyewe na wale wa karibu yetu hawahusiki na wapo salama kabisa.

Sababu ya tatu; kuwa wa kwanza kutoa habari za ukombozi, za kishujaa.
Kwa sababu watu wengi wanapenda habari hasi, na wanazichukulia kwa uzito, hii inakuwa ni ufahari kwa yule ambaye atatoa habari hiyo kwa mara ya kwanza. Hivyo mtu anapopata habari hasi, kabla hata hajaielewa au kuijua vizuri, anakimbilia kuisambaza ili awe wa kwanza kutoa habari hiyo.
Kuna kiufahari fulani ambapo watu wanakipata pale wanapoona ni wa kwanza kutoa habari fulani ambayo watu wanajali sana. Hivyo hii inawasukuma watu kuhakikisha wanatoa habari hizo wa kwanza kabisa kabla wengine hawajazitoa. Ndiyo maana mara nyingi habari hasi zinazotolewa mwanzoni huwa ni za uongo.

Kwa mfano ajali imetokea, mtu aliyepo kwenye ajali, au aliyefika mapema, atatoa picha haraka na kusema ajali mbaya sana imetokea, watu wengi mno wamefariki. Hapa anasambaza habari yenye hofu kubwa kwa wengine. Maana unaposema watu wengi sana, ni watu wangapi. Kwa nini mtu kama huyu asingesubiri miili ikatolewa, ikahesabiwa wangapi wamefariki, wangapi majeruhi na kisha akawajulisha watu kwamba ajali imetokea na watu watano wamefariki. Wote tunajua sababu ni kwa nini, mpaka asubiri watu watolewe, atachelewa kutoa habari, atakuta wengine wameshaitoa. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa wale ambao wanapokea habari na kuzisambaza kwa wengine

Tufanye nini ili kuondoka kwenye mkumbo huu wa habari hasi na zenye hofu?
Kama ambavyo nimekuwa nakuahidi kupitia kipengele hiki cha nyeusi na nyeupe, sikuachi hivi hivi, bali nakupa hatua za kuchukua ili kuondokana na hali hii.

Moja; tambua kwamba maisha ni bora sana sasa kuliko siku zilizopita.
Haijalishi vyombo vya habari vinakuambia au kukuhubiria nini, maisha tunayoishi sasa ni bora kuliko ya siku zilizopita. Kwa kipimo chochote na kwa viwango vyovyote, maisha ni bora, ulinzi ni mzuri na mazingira ni rafiki kwa chochote unachotaka kufanya. Usipokee hofu na habari hasi kama zinavyotolewa.

Mbili; chunguza kila habari hasi au yenye hofu unayopokea.
Siwe tu mtu wa kupokea kila habari na kuichukua kama ilivyo na wewe kuisambaza. Badala yake ichunguze, hoji na dadisi. Jiulize habari hiyo imebeba ukweli kiasi gani. Je ina uhalisia kiasi gani. Na je ina msaada gani kwenye maisha ya wengine.

Tatu; usiwe mtu wa kusambaza habari hasi.
Unapopokea habari, usikimbilie kuisambaza. Ichunguze kwa makini na ona kama kuna manufaa yoyote, kama hakuna basi achana nayo, wala usiiseme kwa wengine. Usijijengee sifa ya kuwa mtu wa kutoa habari hasi na zenye hofu.

SOMA; Huyu Ndiye ‘STAA’ Muhimu Unayepaswa Kumfuatilia Kila Siku Kwenye Maisha Yako Ili Ufanikiwe.

Nne; jua biashara kuu ya habari ni kujenga hofu kwa watu.
Vyombo vya habari vinahitaji wasomaji na watazamaji ili kuingiza kipato, iwe ni kwa wao kulipa moja kwa moja au kupata matangazo. Hivyo kila chombo kinakazana kupata wasomaji wengi. Njia rahisi ya kufanya hivi ni kuwajaza watu hofu, ili wakae kwenye vyombo hivyo kupata habari lazima wawe na hofu kwamba kuna kitu wanakosa au kuna kitu lazima wakijue la sivyo maisha yao yatakuwa hovyo.

Tano; usisome habari za mbele za magazeti, usianze siku yako kwa kuangalia au kusikiliza habari na usiangalie habari kwenye tv.
Chagua aina ya habari unazotaka kupata, labda za biashara, afya, uchumi na nyingine kama hizo. Habari zisizoendana na hizo achana nazo. Hatujaikia mwisho wa dunia na hata tukifikia utasikia hata kwa wengine, siyo lazima uwe karibu na kila habari. Halafu hakuna kikubwa unachokosa kama hutafuatilia habari kila siku.

Hivyo ndivyo habari hasi na zenye hofu zinatumika na wengine kujitengenezea kipato huku zikiwafanya wanaozipokea kuona maisha siyo mazuri. Epuka kabisa habari hizi hasi na zenye hofu. Maisha ni bora sana sasa kuliko siku za nyuma.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

USHAURI; Ufanyeje Pale Familia Yako Inapopinga Ndoto Zako?

$
0
0
Changamoto ni sehemu ya kudumu ya maisha yetu, japo tunaweza kuona changamoto kama kikwazo chetu cha kuwa na maisha ya mafanikio, changamoto zitaendelea kuwepo kadiri tunavyoishi. Changamoto zako za kimaisha zitaisha pale maisha yako yatakapokwisha. Kama bado unaishi basi nikuhakikishie jambo hili moja, utakutana na changamoto.
Hivyo basi, kujifunza njia bora za kutatua changamoto tunazokutana nazo ni hitaji muhimu la kila binadamu.

Ni matumaini yangu kwamba wewe rafiki yangu ni mzima kabisa, uko vizuri ukiendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile ulichochagua kufanya kwenye maisha yako. Kwa juhudi kubwa unazoendelea kuweka, tegemea kupata matokeo bora sana.
 
KUPATA TIKETI YA KUSHIRIKI SEMINA HII PIGA SIMU NAMBA 0717396253 AU 0755953887

Karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto, ambapo tunashauria namna bora ya kutatua changamoto tunazopitia kwenye maisha yetu. Leo tunakwenda kuangalia changamoto ya ndugu wa karibu na familia kupinga ndoto yako. Yaani unakuwa na ndoto ya maisha yako, unakuwa na malengo na mipango mikubwa ya maisha yako, lakini watu wako wa karibu wanakuambia unachofikiria hakiwezekani au hakitakunufaisha. Badala yake wanakuja na ndoto nyingine ambazo haziendani na wewe.
Kabla hatujaangalia hili kwa undani na hatua za kuchukua, tupate maoni ya msomaji mwenzetu.

Mimi changamoto yangu ni familia yangu inanilazimisha nikaajiriwe niachane na biashara yangu ya library na ndoto zangu za kucheza soka nizifute. Bernard Z. P.

Hii ni changamoto kubwa kwenye safari ya mafanikio, kwa sababu mara nyingi familia zetu, hasa wazazi, wamekuwa wakitamani kuona maisha yetu yanakuwa bora sana. Hivyo wamekuwa wakikazana kutushauri namna bora ya kwenda na haya maisha ili tuwe na maisha bora. Sasa pale inapotokea ndoto yako inatofautiana na kile wazazi wanachofikiria, inakuwa changamoto kubwa.

SOMA; Kuwa Dereva wa Maisha Yako

Je ni hatua gani unazoweza kuchukua ili kutatua changamoto hii?

1.     Waelewe familia na wazazi wako.
Kabla ya kuchukua hatua yoyote, kwanza waelewe wazazi na familia yako. Elewa kwamba ndani ya mawazo yao wanataka wewe ufanikiwe, wanataka wewe uwe na maisha bora. Hivyo wanajitahidi kuangalia njia bora kwako kuweza kuwa na maisha mazuri.
Japokuwa wanataka uwe na maisha mazuri na ufanikiwe, haimaanishi wapo sahihi kwenye kile ambacho wanataka ufanye. Huenda kile wanachokushauri ufanye ndiyo kitu pekee wanachojua kinafaa. Hawajui kama kuna njia nyingine za kuwa na maisha bora na ya mafanikio.

Kwa mfano kwa wazazi na familia nyingi za Kitanzania, wanaamini sana kwenye ajira. Wanaamini mtu akishakuwa na ajira basi ana uhakika wa maisha. Licha ya changamoto zilizopo kwenye ajira, licha ya uhaba wa ajira uliopo, wao wanaamini ajira ndiyo kila kitu. Hata pale mtu anapokuwa na mpango wa kufanya biashara, au kujiajiri, hushauriwa kuanza na ajira kwanza.
Ni vyema ukaelewa hili kabla hujachukua hatua yoyote, maana litakusaidia katika maamuzi utakayofanya.

2.     Wasikilize na elewa hofu yao iko wapi.
Pale ambapo ndoto zako na za familia yako zinatofautiana, wasikilize na jua hofu yao iko wapi. Wazazi na familia yako wana hofu juu ya ndoto uliyochagua. Kuna kitu wanahisi utashindwa kufanya na hivyo maisha yako kuwa magumu.
Jua hofu yako iko wapi, ili utakapofanya maamuzi ya kwenda na ndoto yako, uweze kuitetea na kuisimamia kwa maisha yako yote.

SOMA; Mambo Yanapokuwa Magumu Unafanya nini?

3.     Kumbuka wewe ndiye utakayeishi maisha yako.
Wazazi na familia yako wanaweza kuwa na nia nzuri sana kwako, lakini ukweli ni kwamba, wewe pekee ndiye utakayeishi maisha yako. Hakuna mtu mwingine atakayekuja kuishi maisha yako kwa ajili yako. Hivyo unapofanya maamuzi, fanya ukijua utayaishi muda wote wa maisha yako.
Wazazi na familia wanaweza kukupa mipango mizuri sana ya namna ya kuishi maisha yako, lakini kumbuka wewe pekee ndiye utakayeyaishi. Kuyachukua mapendekezo yao ili kuwaridhisha, kutakufanya uishi maisha ambayo huyafurahii. Hivyo chagua kama unataka kuwa na maisha bora kwako au ya kuwaridhisha wengine.

4.     Kumbuka hakuna njia moja ya uhakika kwa wote.
Hakuna njia moja ya uhakika ya mafanikio kwa watu wote. Hakuna kitu kimoja ambacho kila mtu akikifanya basi atafanikiwa. Binadamu tunatofautiana, anachofanya mmoja akafanikiwa, mwingine anaweza kufanya akashindwa kabisa. Kuna ambao wanaweza kufanya ajira na wakawa na maisha bora, wengine wakifanya biashara ndiyo wanakuwa na maisha mazuri.
Hivyo licha ya ushauri utakaopewa, jua siyo kila kitu kitafanya kazi kwako, hivyo fanya maamuzi kutokana na vile vitu unavyopendelea kufanya na ambavyo upo tayari kujitoa kwa hali ya juu.

5.     Fanya maamuzi na yaishi maamuzi hayo, usijilaumu baadaye.
Ukishawaelewa wazazi na familia, kisha ukajiangalia wewe mwenyewe ni vitu gani unapendelea kufanya, sasa unaweza kufanya maamuzi ya maisha yako. Fanya maamuzi ambayo utaweza kuyaishi. Fanya maamuzi ambayo utayasimamia hata pale mambo yatakapokuwa magumu, na kwa uhakika yatakuwa magumu.

Kwa maamuzi utakayofanya, usijilaumu au kuyajutia pale unapopata matokeo ya tofauti na ulivyotegemea, badala yake jifunze kwa kila hatua na boresha zaidi.

Utakapofanya maamuzi ambayo ni tofauti na ushauri na mategemeo ya wazazi na familia, ukikutana na changamoto watasema tulikuambia sisi, sasa kama na wewe utakuwa mtu wa kujilaumu, utayaharibu maisha yako. Fanya maamuzi na kuwa tayari kupokea lolote ambalo litakuja kwenye maisha yako. Chagua kufanya kile ambacho upo tayari kukifanya kwa moyo wako wote, hata kama kipato siyo kikubwa mwanzoni.

SOMA; Kama Utafanya Uamuzi Huu Leo, Utabadilisha Hali Yako Ya Kipato Kabisa.

Fanyia kazi mambo hayo matano tuliyoshauriana ili kuweza kufanya maamuzi bora ya maisha yako. Chochote unachofanya, kumbuka wewe ndiye mhusika mkuu, wengine wanaweza kukushauri, lakini wewe pekee ndiye unayepaswa kufanya maamuzi ya maisha yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz 

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.
Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Mambo Yanayokufanya Uwe Adui Mkubwa Wa Maisha Yako.

$
0
0
Katika safari ya maisha, wakati mwingine binadamu huwa tuna watu tunaowaita maadui wa mafanikio na maisha kwa ujumla. Na mara nyingi watu hawa huweza kuwa ni marafiki, ndugu au jamaa zetu wa karibu sana.
Na inapotokea ukawatambua maadui hawa wa maisha yako, ambao wanasababisha usifanikiwe kwa kawaida huwa tuna hasira nao sana. Inakuwa iko hivyo kwa sababu hao ndio wanaozuia juhudi zetu za makusudi za kufanikiwa kwetu.
Hivyo kwa misingi hiyo, binadamu hujikuta yuko makini sana na maadui hawa ili wasije wakasababisha ashindwe kusonga mbele. Hujikuta hata kuweka ulinzi au watu wa kumpa taarifa juu ya adui zake wamafanikio.
Lakini pamoja na tahadhari zote hizo ambazo huchuliwa ili kuwajua maadui wako wa maisha, yupo adui mkubwa sana ambae huwa hachukuliwi umakini wowote na adui huyu ndiye husababisha maisha yako yawe magumu.
Hebu tuchukulie ukagundua kwamba adui mkubwa wa maisha yako ni wewe mwenyewe, hapo utafanyaje? Ni ukweli usiofichika kuna wakati hujikuta ni maadui wakubwa sana wa maisha yetu bila kujijua sisi wenyewe.
Inawezekana unajiuliza kivipi unaweza kuwa adui mkubwa wa maisha yako?
Yafuatayo Ni Mambo Yanayokufanya Uwe Adui Mkubwa Wa Maisha Yako.
1. Kutokubadilika.
Ili kufanikiwa, unahitaji mabadiliko endelevu na ya kila siku kwenye maisha yako. Kwa mfano, unatakiwa kubadilika kutoka kwenye hali ya mazoea mabaya uliyonayo na kwenda kwenye hali nyingine bora zaidi ya kimafanikio.
Mabadiliko kwenye maisha yako ni muhimu sana yanakufanya ili usidumae kimafanikio. Kwa msingi huo, kila siku unatakiwa kufanya kitu chanya, ambacho kinaweza kikabadili maisha yako leo na hata kesho.

Ikiwa utakuwa hubadiliki, moja kwa moja utakuwa unajitengezea uadui mkubwa wewe mwenyewe kwenye maisha yako. Kwa kifupi, maisha yako na ya familia yako hayataweza kuwa mazuri kama tu hutaweza kubadilika kwa kiasi kikubwa.
2. Kujishusha sana.
Kama kila wakati unafikiri huwezi kufanya kitu fulani au hata ukifanya kitu hicho kitakuwa chini ya ubora, basi wewe ni moja ya adui mkubwa sana wa mafanikio yako .Kujishusha kwa namna yoyote hakufai.
Kwa kuendelea kujishusha kwenye maisha yako hatafika popote. Hiyo ikiwa na maana kwamba hakuna jambo ambalo utajaribu zaidi ya kujiona huwezi. Kama unajishusha sana kwenye maisha yako elewa wewe ni adui wa maisha yako pia.
3. Kutegemea wengine.
Kuna watu ambao wao kila wakati wanategemea wengine kwa kila kitu. Hawa ni watu ambao hawako tayari kufikiri changamoto zao wakiwa wao kama wao. Ni watu wakuangalia kama wakikwama ni nani atawasaidia?
Inapotokea ukawa kama watu hawa, ambapo hata changamoto ndogo hutaki kutatatua unategemea mtu mwingine awe mzazi au serikali akutatulie chamgamoto hizo, elewa pia unafitini maisha yako na pia ni adui mkubwa wa maendeleo yako mwenyewe.
4. Kuamini wengine sana.
Wapo watu ambao kujiamini wao kama wao ni shida. Ni watu ambao hawaamini uwezo mkubwa walionao ndani mwao zaidi wanaamini wengine ndio wanaoweza kufanya jambo fulani.
Ikiwa kama unajiona unaamini watu wengine sana kuliko unavyoweza kujiamini wewe, elewa kabisa nawe pia unatengeneza uadui na maisha yako. Unatakiwa kujiamini wewe ili usiwe adui mkubwa wa maisha yako.
5. Kuogopa sana.
Kuna masemo ‘usemao woga wako nio umaskini wako’. Hii ni kweli kabiasa, kama wewe ni mwoga karibu kwa kila kitu huwezi kuambuliwa lolote katika haya maisha yenye changamoto nyingi.
Maisha yanakutaka uwe jasiri ili uweze kuyashinda , bila kuwa jasiri na ukamua kuendekeza woga, elewa maisha yatakushinda na wewe ndiye utakuwa adui wa kwanza kwa kuharibu maisha yako.
6. Kuwaza sana hasi.
Mtu yeyote ambaye kila wakati anawaza hasi, si rahisi sana kwa mtu huyu kuweza kufanya mambo ya kumsaidia kufanikiwa. Hiyo iko hivyo kwa sababu kila wakati atajiona ni mtu asiyeweza kufanya kitu chochote.
Sasa ili uepuke hali hiyo na usiwe adui mkubwa wa maisha yako ni lazima utambue namna ambayo itakusaidia kuwaza chanya kila wakati. Ukifanya hivyo, itakusaidia sana kuweza kufanikiwa.
7. Kusikiliza sana maoni ya wengine.
Njia ambayo naweza kusema ni mbaya ya kuishi maisha yako, ni kule kuishi kwa kutegemea mawazo ya wengine sana kuliko yako. Ili uweze kufanikiwa ni lazima uamini sana kwanza mawazo yako. Hayo ya wengine ni kama nyongeza.
Kama unaishi maisha ya kusikiliza sana mawazo ya watu wengine ni jambo la hatari sana kwako. Kwa kuishi maisha haya inakufanya moja kwa moja kutokufanikiwa kwenye mambo mengi kwa sababu ya kusikiliza wengine tu hata wale wanao kupoteza.
8 . Kutokutaka kukosea.
Hawa ni watu ambao mara nyingi hawataki kufanya maauzi magumu ya kubadili maisha yao kwa sababu tu ya kuogopa kukosea. Kila siku hujikuta ni watu wa maisha yaleyale kwa sababu hakuna hatua kubwa wanayoweza kuchukua ya kuweza kubadili maisha yao.
Inapofika mahili ukawa ni mtu wa kuogopa kukosea huwezi kufanikiwa. Hakuna kitu ambacho unaweza ukakifanya kwa asilimia mia moja bila kufanya kosa lolote. Makosa ni muhimu katika kukua kimafanikio. Kama utaendelea kushikilia kutokukosea basi pia nawe ni adui mkubwa wa maisha yako.
9. Kusubiri mambo yawe mazuri.
Wapo watu ambao wao kila siku wanajipa moyo kwamba siku moja maisha yatakuwa mazuri. Tatizo la watu hawa sio kujipa moyo hivyo, bali tatizo lipo hufanya hivyo huku wakiwa hawachukui hatua yoyote.
Ikiwa inatokea hivyo kwako na unaendelea kujipa moyo kwamba mambo yangu yatakuwa mazuri na huchukui hatua muhimu, wewe unakuwa ni sawa na adui wa maisha yako. Maisha yako hayataki ahadi, yanahitaji uchukue hatua.
Kwa kawaida yapo mambo mengi ambayo yanaweza kutufanya tuweze kuwa maadui wakubwa wa maisha yetu. Miongoni mwa mambo hayo ndiyo kama hayo tuliyokwisha yaangalia kwenye makala haya.
Nikutakie siku njema na ansante sana kwa kutembelea  AMKA MTANZANIA kwa ajili ya kujifunza.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio soma DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza na kuboresha maisha yako.  
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

Tabia Moja Ya Binadamu Ambayo Unaweza Kuitumia Kunufaika Kibiashara.

$
0
0
Moja ya vitu ambavyo kila mfanyabiashara anapaswa kujifunza , ni tabia za binadamu. Hii ni kwa sababu mahusiano ya kibiashara, kati ya mfanyabiashara na mteja wake, yanategemea sana uelewa ambao mfanyabiashara anao juu ya tabia za asili za binadamu. Na kama unavyojua, biashara za zama hizi ni biashara za mahusiano, mtu hanunui kwako kwa sababu unauza, ila ananunua kwako kwa sababu anakujua wewe na biashara yako.
 
KUPATA TIKETI YA SEMINA PIGA SIMU 0717396253/0755953887

Leo nataka nikushirikishe tabia moja ya asili ya binadamu ambayo unaweza kuitumia kunufaika kibiashara. Kwa kujua tabia hii na kuitumia vizuri, utaweza kuikuza biashara yako mara dufu na kupata wateja wengi watakaodumu kwenye biashara yako.  Kabla hatujaanza kuangalia tabia hii, niseme wazi kwamba tabia utakayoenda kujifunza hapa siyo ya kuwalaghai watu, bali kuwapa watu kile wanachotaka na wao wanakupa unachotaka.

Sheria moja ya dunia ni nipe nikupe, yaani watu ni rahisi sana kutoa pale ambapo unakuwa umeshawapa. Hii nayo ni tabia nyingine muhimu ambayo inaendana sana na ile tutakayojifunza leo. Lakini hii hatutaijadili kwa kina, tutafanya hivyo kwenye makala zijazo.

SOMA; Tabia Nne(4) zinazowatofautisha wafanyabiashara wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

Kuna tabia moja ya asili ya binadamu ambayo kila mfanyabiashara anatakiwa kuijua na kuweza kuitumia vizuri. Tabia hii ni UBINAFSI. Kila binadamu ni mbinafsi, ndiyo namaanisha hata wewe na mimi ni wabinafsi. Tunachotofautiana ni viwango vya kuonesha ubinafsi wetu. Lakini mara zote huwa tunajifikiria sisi. Na ubinafsi siyo jambo baya, kwa sababu ndiyo unatuwezesha kujijali na hatimaye kuweza kuishi. Tatizo ni pale ubinafsi wako unapoingilia maslahi ya wengine, ndipo matatizo huanza.

Sasa turudi kwenye matumizi ya ubinafsi wa watu kwenye biashara yako. Iko hivi, kila mtu anapenda kupata vitu bora kwa kutumia fedha kidogo. Ndiyo maana mara nyingi watu wanapopewa bei, huwa wanataka kupata punguzo. Ukipewa vitu viwili vyenye ubora sawa, kimoja kikawa ghali, na kingine kikawa rahisi, utachukua kile cha bei rahisi. Au kama unapewa mikate miwili kwa bei sawa, ila mmoja ni mkubwa na mwingine ni mdogo, utachukua ule mkubwa, labda kama mdogo una vitu vya ziada.
Unaona sasa rafiki, tunapenda kujipendelea, tunapenda kupata kilicho bora kwa gharama kidogo. Tunapenda kupata zaidi ya tunavyopata.

Je unawezaje kutumia tabia hii ya ubinafsi wa watu kunufaika kibiashara?

Kwanza tuangalie njia ambayo siyo sahihi kutumia njia hii.
Kuna wafanyabiashara wengi ambao wamekuwa wanatumia tabia hii, iwe kwa kujua au kwa kutokujua, ila wanaitumia kimakosa na inawagharimu baadaye. Wanachokifanya wafanyabiashara hawa ni kuweka bei kubwa ya vitu vyao kuliko uhalisia, ili mtu anapoomba kupunguziwa, basi wakipunguza ifike kwenye ile bei ambayo ni halisi.

Huku ni kudanganya na hakuna kitu ambacho watu hawapendi kama kudanganywa. Kadiri unavyofanya hivi watu watajenga tabia ya tofauti ambayo haitakuwa nzuri kwa biashara yako. Watajizoesha kwamba kila kitu kwako kinauzwa kwa bei ambayo siyo halisi, hivyo yule anayeweza kupambana akapunguziwa basi ndiyo anafaidi.

SOMA; Wazo Bora Na Mtaji Pekee Havitoshi Kuifanya Biashara Ifanikiwe, Unahitaji Kitu Hiki Kimoja Muhimu Sana Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako.

Wakati mwingine inajenga picha mbaya kabisa, kwa mfano mtu mmoja kanunua kitu kwako, na yeye hakujua kama unapunguza bei, hivyo ulipomwambia bei yeye akalipa na kupata alichotaka. Sasa atakaposikia mwingine kanunua kwa bei ya chini kuliko yeye, ataona umemwibia fedha. Mteja kama huyu anaweza sirudi tena kwenye biashara yako. Na kama atarudi basi hatakuwa na imani kwako.

Njia sahihi ya kutumia tabia hii.
Ipo njia sahihi ya kutumia tabia hii ya ubinafsi ambayo kila mmoja wetu anayo. Njia hii ni kutoa thamani kubwa sana kuliko fedha ambayo mtu analipa. Hapa mtu lazima atakuja kwako na ataendelea kuwa mteja mzuri kama kweli atapata thamani hiyo mara zote.

Unachofanya ni kutoa thamani kubwa sana kwa bei ambayo haiendani na thamani hiyo, kiasi kwamba mteja anaona kama anakuibia hivi. Unatoa thamani ambayo mteja hawezi kuipata sehemu nyingine yoyote, hii inamfanya akutegemee wewe na awe mteja wako wa kudumu. Kwa kutoa thamani kubwa, mteja atakuja yeye na pia atawaambia wengine. Tabia nyingine ya binadamu ni kwamba kizuri hawawezi kula wenyewe, hivyo watawaambia na wengine pia.

Kitu muhimu nataka ujue ni kwamba kutoa thamani kubwa haimaanishi uuze vitu kwa bei rahisi, unaweza kuuza bei ile ile ambayo imezoeleka lakini unaongeza thamani kubwa mno. Au wakati mwingine hata ukauza kwa bei ya juu lakini bado thamani ikawa kubwa sana kiasi kwamba watu wakawa tayari kulipia thamani hiyo.

SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

Njia hii ya kuongeza thamani inafaa sana kwa wale ambao wanatoa huduma au wanatengeneza bidhaa zao wenyewe. Lakini pia inawafaa mno wale wanaofanya biashara ya rejareja. Japokuwa kwenye biashara ya reja reja bidhaa ni ile ile na bei ni zile zile, bado unaweza kuongeza thamani kubwa kwa namna unavyowauzia wateja wako bidhaa zile. Kauli zako kwa wateja wako zinaweza kuwafanya wajisikie vizuri na wapende kuja kwenye biashara yako mara zote. Wewe mwenyewe unajua, kuna biashara ukienda unajisikia vizuri na nyingine unajisikia vibaya jinsi unavyopokelewa na kuhudumiwa. Sasa wewe wafanye wateja wako wajisikie vizuri kuwa kwenye biashara yako.

Ni asili ya binadamu kuwa wabinafsi, tunapenda kupata zaidi kwa kutoa kidogo. Angalia biashara yako, ona ni namna gani unaweza kuwapa wateja thamani zaidi na wao watakuwa tayari kununua kutoka kwako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Hii Ndiyo Nyumba Adimu Sana Kupatikana Katika Zama Hizi Za Taarifa.

$
0
0
Habari mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa AMKA MTANZANIA? Natumaini hujambo na unaendelea vyema katika shughuli zako za kila siku za kukupatia kipato na kugusa maisha ya watu wengine, yaani kuishi maisha ya maana hapa duniani.  Karibu mpendwa rafiki katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Natumaini rafiki yangu unajua kuwa kwa sasa tunaishi katika karni ya ishirini na moja (21) na tupo katika zama za taarifa ili ufanikiwe kwa sasa unahitaji taarifa sahihi na kwa wakati sahihi.  Na zama hizi za taarifa zinahitaji kila mtu awe na maarifa sahihi ili yaweze kumsaidia kuishi maisha ambayo ni sahihi na yenye maana kwa ujumla.

Mpendwa rafiki na msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu katika makala yetu ya leo ambapo tutajifunza falsafa moja kutoka kwa mwanafalsafa mkubwa aliyeishi na kuzaliwa kabla ya Yesu kuzaliwa na siyo mwingine bali ni mwanafalsafa Plato. Mwanafalsafa Plato aliwahi kusema, ‘’ a house that has a library in, it has a soul’’ akiwa na maana ya kwamba nyumba ambayo ina maktaba ndani ni nyumba ambayo ina roho. Kila mtu anaishi katika nyumba iwe ni nyumba yako uliojenga au uliopanga lakini unaishi katika nyumba. Je falsafa hii inagusa namna gani?

SOMA; Sehemu Kumi (10) Unazoweza Kupata Muda Wa Kujiongezea Maarifa Kupitia Kusoma Vitabu.

Ukweli ni kwamba nyumba nyingi wanazoishi watu hazina maktaba ndani. Nyumba nyingi ni mabingwa wa kuwa na makochi makubwa, flat screen tv nk. Jaribu kupita nyumba kumi katika jamii unayoishi halafu angalia ni nyumba gani wana maktaba au wana vitabu ndani. Wengi wanapenda kununua vitu kama cd za nyimbo, tamthilia mbalimbali na kukaa nazo kuliko kununua vitabu. Nyumba nyingi ni maskini wa vitabu na nyumba nyingi hazina roho na roho ya nyumba ni vitabu. Katika vitabu tunapata maarifa ambayo yanatusaidia kuishi maisha sahihi.

Maisha ya wanafalsafa wengi ni maisha mazuri sana yenye furaha, amani na mafanikio na kama ukifuatilia maisha ya mwanafalsafa hakika utaujua ukweli nayo kweli itakuweka huru. Yatupasa tuanze kuamka katika majumba yetu badala ya mgeni kuja kwako na kumfungulia tv aangalie mpe kitabu asome aonje roho ya nyumba yako. Akisoma hata ukurasa mmoja atakua ameongeza thamani katika maisha yake. Anza kununua vitabu na kuweka maktaba yako ndogo nyumbani. Katika nyumba yako hakikisha unaishi weka sehemu ya maktaba ambayo ndio roho ya nyumba yako.

Haitoshi kuwa na maktaba tu bali uhai wa maktaba ni wasomaji wa vitabu. Vitabu vinunuliwe na visomwe. Tukiwa tunajenga utamaduni wa kusoma vitabu kwa kila familia tutajenga jamii bora sana na tutafanya dunia kuwa sehemu salama ya kuuishi kwa kila mmoja wetu. Tuanze kwa kila familia kuwa na maktaba za vitabu kwetu. Tuache mambo ambayo hayana faida kubwa katika maisha yetu bali tujenge kizazi imara na jamii imara. Kila mtoto alelewe katika utamaduni wa kusoma vitabu kwani ndio njia sahihi ya kumfundisha mtoto kuvua samaki na siyo kumpa samaki.  Kama unaona ni fahari kumwachia mtoto aangalie sana tv bila kusoma vitabu ujue unamharibu mwenyewe mtoto wako.

SOMA; KITABU CHA APRIL; THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu).

Mpendwa rafiki, mwanafalsafa na mwandishi  Jim rohn aliyezaliwa karni ya ishirini (20) na kufariki dunia karni ya ishirini NA moja ( Septemba 17,1930- Desemba 5, 2009) naye aliwahi kusema, ‘’ successful people have  big libraries. The rest have big flat screen Tvs in their home’’ akiwa na maana ya kwamba watu waliofanikiwa wamekuwa na maktaba katika nyumba zao na wengine waliobakia wamekuwa na tv kubwa za kisasa.  Hivyo basi, unaona mwanafalsafa huyu anavyotuambia ukweli kama alivyotuambia mwanafalsafa Plato. Plato yeye aliishi na kuzaliwa kabla hata ya Yesu lakini leo maneno yake yanadhihirika na mwanafalsafa aliyefariki katika karni hii 21 naye anatuambia ukweli huo huo.

Siku hizi katika nyumba nyingi fasheni ni kuweka flat screen ili naye aende na wakati kama wenzake wanavyoenda. Lakini ukiangalia katika upande wa roho ya nyumba hakuna kitu. Ukiwa na  maktaba ndani ndio unaonesha uhai wa nyumba yako kuliko kuwa na tv kubwa nyumbani. Tunatakiwa kuishi maisha ya kifalsafa yaani falsafa ni msingi wa maisha ya binadamu ambayo unaelezea ukweli kupitia uhalisia wa dunia. Jinsi unavyofikiria na unavyoishi unatumia falsafa bila ya wewe mwenyewe kujua.
Kila nyumba inatakiwa ianze leo kuwa na maktaba na kuanza kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kila siku na kuachana na kutumia muda mwingi katika kuangalia luninga. Kuangalia luninga sana na kwa muda mrefu ni faida hasi kiafya lakini ukisoma vitabu sana ni faida chanya kiafya.  Kuwa balozi wa kuhamasisha jambo hili sehemu yoyote uliyopo. Tuna kazi kubwa kwa kila mmoja wetu kusaidiana ili kufuta ujinga. Taifa haliwezi kukua kama tukikaa na kushinda katika makochi na kuangalia tv taifa litakuwa kama watu wakifanya kazi kwa juhudi na maarifa.

SOMA; Hivi Ndivyo Tabia Ya Kupenda Kujisomea Ilivyoboresha Maisha Yangu. Inawezekana Hata Kwako Pia.

Sasa katika kufanya kazi kwa juhudi haitoshi bila kuwa na maarifa ya kutosha. Maarifa tunayapata katika vitabu vyetu vinavyopatikana katika maktaba zetu. Habari njema ni kwamba katika zama za taarifa unaweza kuwa na maktaba yako ndani ya simu yako imejaa vitabu, kompyuta, na nk. Unatakiwa kutembea na maktaba sehemu yoyote unayokwenda kuanzia leo.

Hatua ya kuchukua; anza leo kutembea na kitabu ukipata muda sehemu yoyote ile chukua kitabu soma. Katika simu yako kama umejaza vitabu ambavyo havina faida chanya futa weka vitabu, kama kwenye kompyuta yako umejaza nyimbo, movie za aina mbalimbali na sirizi (mpangilio wa matukio) mbalimbali futa na weka vitabu. Kama familia yako haina kitabu anza leo kutenga eneo la maktaba na muanze desturi ya kusoma kitabu. Karibu pia katika klabu yetu ya kusoma vitabu viwili kwa wiki. Katika kundi hili tunapokea watu makini ambao hawana sababu yaani excuses. Kujiunga na kikundi hiki tuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba +255717101505 ili uweze kujifunza kwa hamasa na kwa nidhamu bila kuahirisha.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com


Utaratibu Wa Kupata Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

$
0
0
Habari rafiki yangu katika mafanikio?
Nichukue nafasi hii kukupa habari njema ya kwamba kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa sasa kinapatikana katika mfumo wa kuchapishwa. Mwanzo kitabu hiki kiliatikana katika mfumo wa nakala tete (softcopy) ila sasa unaweza kukipata kama kitabu cha kawaida, na kuweza kukisoma popote ulipo.

Ni kitabu kizuri sana kwa wale wote ambao wanapenda kuanzisha na kukuza biashara zao. Kitabu kinaitwa biashara ndani ya ajira, lakini siyo kwa wale waliopo kwenye ajira pekee. Kitabu hiki kinamfaa mtu yeyote anayetaka kuanzisha na kukuza biashara yake, iwe ameajiriwa au la.

Ndani ya kitabu hiki kuna mambo muhimu sana utakayojifunza kama;
1.     Jinsi ya kupangilia muda wako vizuri na kuweza kuudhibiti na kuutumia vizuri.
2.     Biashara unazoweza kuanza kufanya kama bado hujaanza kufanya.
3.     Uwekezaji unaweza kuanza kufanya sasa, ili miaka ijayo uweze kuwa na uhuru wa kifedha.
4.     Mifereji nane ya kipato unayohitaji kutengeneza ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha.
5.     Jinsi ya kutengeneza mfumo bora wa kuendesha biashara yako ili kupata uhuru.
6.     Hatari za kuepuka ili biashara yako ifanikiwe.
7.     Na mengine mengi...

Kama unavyoona hapo, siyo kwa wale walioajiriwa pekee, bali kila mtu ana kitu cha kujifunza kupitia kitabu hiki.
Nakushauri sana rafiki yangu, pata na usome kitabu hiki, hutabaki kama ulivyo sasa.


Utaratibu wa kupata kitabu hiki.

Kwa sasa kitabu kinapatikana kwangu, hivyo kwa wale waliopo dar, unaweza kufika ofisini kwangu Tabata Kimanga na kupata nakala yako ya kitabu, au kulipia kitabu na kuletewa pale ulipo. Utaratibu wa kukiweka kitabu hiki kwenye maduka ya vitabu unaendelea, na taarifa nitawapatia.
Kwa wale waliopo mikoani, kitabu kinatumwa kwa njia ya basi, hivyo unalipia gharama ya kitabu na nauli kisha unatumiwa kitabu kule ulipo. Utaratibu wa kuwapata mawakala kwenye mikoa mbalimbali unaendelea na nitawapa taarifa kadiri tunavyokwenda.

Gharama ya kitabu na namna ya kukipata.

Gharama ya kitabu ni tsh elfu 10 (10,000/=).
Kama upo dar fika ofisini tabata kimanga, utapata nakala yako. Pia unaweza kufanya malipo ya tsh elfu 10 kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 na kisha kutuma taarifa zako na ukaletewa kitabu pale ulipo.

Kama upo mkoani, utahitajika kutuma gharama za nauli ya kusafirisha kitabu. Hivyo tuma gharama ya kitabu tsh elfu 10 pamoja na nauli tsh elfu 15 kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 kisha tuma taarifa zako, majina kamili, namba ya simu na sehemu ulipo, ksiha utatumiwa kitabu hiki.
Karibu sana upate maarifa haya muhimu kwa maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.


Kama wewe upo dar au mkoani na ungependa kuwa wakala wa kuuza na kusambaza kitabu hiki kizuri, tuwasiliane kwa simu namba 0717 396 253. Kuna kamisheni nzuri kwa kila kitabu utakachoweza kuuza. Karibu tufanye kazi pamoja.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Fursa Ya Kuwa Wakala Wa Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

$
0
0
Habari rafiki?
Nichukue tena nafasi hii kukukumbusha ya kwamba kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA kwa sasa kinapatikana kwenye mfumo wa kuchapishwa. Sasa unaweza kupata na kusoma kitabu hiki.
Katika makala iliyopita nilitoa maelezo kuhusu kitabu hiki. Hapa napenda kutoa ufafanuzi juu ya mambo mawili muhimu.


Moja; gharama ya nauli ya kitabu kwa wale waliopo mikoani.
Gharama ya kitabu ni tsh elfu kumi (10,000/=) na kama upo mkoani unaweza kutumiwa kwa njia ya basi, hapo utahitaji kuongeza nauli ya kutuma kitabu hiki ambayo itakuwa tsh elfu tano (5,000/=). Hivyo jumla ya gharama unazopaswa kutuma kama upo mkoani ni tsh elfu 15, elfu kumi ya kitabu na elfu tano ya nauli ya kitabu.

Mbili; utaratibu wa kuwa wakala wa kitabu hiki.
Jana nilitoa fursa kwa wale ambao wangependa kuwa mawakala wa kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA kwenye mikoa mbalimbali. Nimepata mwitikio mkubwa wa watu wengi ambao wangependa kuwa mawakala wa kitabu hiki.
AMKA MTANZANIA ni mtandao ambao unawafikia watanzania karibu nchi nzima. Katika kila mkoa yupo msomaji na mfuatiliaji mzuri wa AMKA MTANZANIA. Hivyo tunahitaji kuwa na mawakala kwa kila mkoa wa Tanzania.
Natoa fursa hii ya kuwa wakala wa kitabu hiki popote ulipo Tanzania.

Utaratibu wa kuwa wakala ni kama ifuatavyo;
1.     Utanunua kitabu kimoja kwa tsh 7,500/= na utakiuza kwa tsh 10,000/= kiwango cha chini cha kununua ni vitabu 10.
2.     Unahitaji kuwa sehemu ambayo watu wanaweza kukufikia, au wewe unaweza kuwafikia kwa urahisi.
3.     Unahitaji kuongea na watu kuhusu kitabu hiki, na mimi pia nitawaeleza watu wa eneo ulipo kukutafuta wewe kupata kitabu hiki.

Muhimu; hii ni fursa nzuri kwako kuweza kuwafikia wengi na hata kutengeneza kipato cha ziada. Utahitajika kuwekeza kiasi cha fedha kwa kulipia angalau vitabu kumi kwa bei hiyo ya tsh 7,500/= kwa kitabu kimoja.

Muhimu zaidi; hakuna hatari yoyote ya kupoteza fedha uliyonunulia vitabu hivi. Kama hutapata watu wa kuvinunua, (kitu ambacho ni vigumu kutokea) nitakurejeshea fedha uliyolipia na utanitumia vitabu. Muhimu ni vitabu viwe kwenye hali nzuri.

Gharama ya kitabu na namna ya kukipata.
Gharama ya kitabu ni tsh elfu 10 (10,000/=).
Kama upo dar fika ofisini tabata kimanga, utapata nakala yako. Pia unaweza kufanya malipo ya tsh elfu 10 kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 na kisha kutuma taarifa zako na ukaletewa kitabu pale ulipo.

Kama upo mkoani, utahitajika kutuma gharama za nauli ya kusafirisha kitabu. Hivyo tuma gharama ya kitabu tsh elfu 10 na nauli tsh elfu 5, jumla elfu 15, kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 kisha tuma taarifa zako, majina kamili, namba ya simu na sehemu ulipo, kisha utatumiwa kitabu hiki.

Karibu sana upate maarifa haya muhimu kwa maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK


Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuanza Biashara Kutoka Sifuri Mpaka Faida Ya Mamilioni.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu kwenye makala yetu ya leo katika mtandao wako wa mafunzo na hamasa AMKA MTANZANIA. Kama ambavyo umekuwa unategemea, kupitia mtandao huu unapata maarifa yanayokuwezesha wewe kufanya maamuzi sahihi ya maisha yako. Ninaweza kukuahidi ya kwamba utaendelea kupata maarifa haya kila siku.

Leo nataka tujadili na kugusia kidogo jinsi unavyoweza kuanzisha biashara, kutoka sifuri mpaka faida ya mamilioni.
Najua swali la kwanza utakalojiuliza, hasa kama bado hujaingia kwenye biashara ni je inawezekana? Na mimi nitakujibu, ndiyo inawezekana, tena sana.


Swali la msingi unalohitaji kuuliza ni je nawezaje kuanza biashara kutoka chini mpaka kufika faida ya mamilioni? Na hapo ndipo tunaweza kujadili kwa kina, na kukuonesha hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kufanya hivyo.
Kuna maswali ambayo inabidi uache kujiuliza, kwa sababu yanakupoteza kwenye safari yako ya kuanzisha na kukuza biashara yako. Baadhi ya maswali hayo ni kama;

Ninahitaji kwenda wapi ili niweze kuanzisha biashara hiyo itakayokuwa kubwa? Swali kama hili linakupoteza kwa sababu huhitaji kwenda sehemu fulani ya tofauti ndiyo uweze kuanzisha biashara yako, badala yake unaweza kuanzisha biashara hapo hapo ulipo sasa na kuweza kuikuza zaidi. Kujiuliza unapaswa kwenda wapi ni kupoteza muda wako, kwa sababu muhimu siyo pale ulipo, bali muhimu ni kile kilichopo ndani yako.

Kipi kilicho ndani yako ambacho ni muhimu katika kuanzisha na kukuza biashara yako?

Hapa ndipo muhimu, hapa ndipo unapata majibu ya maswali na changamoto zako. Kinachopaswa kuwa ndani yako, ambacho kitakuwezesha kuanzisha na kukuza biashara yako ni maarifa sahihi na mtazamo sahihi.

Ndiyo, vitu viwili muhimu sana, maarifa sahihi na mtazamo sahihi juu yako binafsi, biashara unayofanya na biashara kwa ujumla.
Kwa kifupi ni kwamba, ili uweze kubadili maisha yako, ili uweze kuanzisha na kukuza biashara yako, huhitaji kwenda sehemu ya tofauti, bali unahitaji kupata maarifa na mtazamo tofauti.

Na hapa ndipo nakupa fursa nzuri sana na ya kipee kwako kupata maarifa sahihi na mtazamo sahihi wa kuanzisha biashara na kuikuza. Hapa ndipo nakukaribisha kwenye mafunzo ya kipekee sana, ambayo yatakutoa hapo ulipo kimaarifa na kifikra, na kukupeleka hatua nyingine, ambayo itakuwa bora sana kwako.
Karibu kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA, kwenye semina hii nitakufundisha hatua kwa hatua na kwa mifano, jinsi unavyoweza kuanzia biashara chini kabisa, yaani sifuri na kuikuza mpaka kufikia faida ya mamilioni.

Mwalimu na rafiki yetu Felix Maganjila, atafundisha jinsi ya kuikuza biashara ambayo kwa sasa imedumaa au haipigi tena hatua. Hapa utapata maarifa na mtazamo sahihi wa kuirudisha biashara yako kwenye uelekeo sahihi.
Watakuwepo walimu wengine pia, watakaokupa maarifa sahihi ya kuanzisha na kukuza biashara zao.

Karibu sana kwenye semina hii, naweza kukuhakikishia kitu kimoja, hutatoka kama ulivyoingia, bali utatoka ukiwa mtu wa tofauti, ambaye ataweza kuyatumia mazingira yake kufanya makubwa.

Semina hii itafanyika jumapili ya wiki hii, tarehe 30/10/2016 pale Blue Pearl, ubungo plaza. Ni semina ya siku nzima ambapo utapata mafunzo yote muhimu, ukitoka unakuwa wa tofauti kabisa.
Kiingilio kwenye semina hii ni tsh 35,000/= kwa tiketi moja. Utapata kalamu na kitabu cha kujiandikia, chakula cha mchana na vitu vingine.

 Ili kuweza kuweka mipango vizuri, na kuhakikisha semina hii inakupa thamani unayotegemea kupata, mwisho wa kulipia na kupata tiketi za semina hii itakuwa siku ya ijumaa tarehe 28/10/2016. Hivyo zimebaki siku 4 pekee za kupata fursa hii ya kipekee ya kuanzisha na kukuza biashara yako.

Kama hupendi kukosa fursa hii, nakushauri sana ulipie tiketi yako mapema. Kupata tiketi tuma ada hiyo ya kushiriki kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili pamoja na mawasiliano yako. Chukua hatua leo rafiki, hustahili kukosa maarifa haya ya kipekee sana kwako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Kama Unaishi Sana Kwa Kufikiri Hivi…Huna Mafanikio.

$
0
0
Acha kufikiri kwa kudhani kwamba ni kazi rahisi kutekeleza jukumu fulani eti kwa sababu umemuona rafiki yako kalifanikisha jambo hilo kwa urahisi. Inaweza ikawa ni ngumu sana kuliko unavyowaza, kwa sababu hujui changamoto alizozipitia.
Acha kufikiri kwamba eti kuuliza jambo fulani ambalo hulijui, linaweza likakupotezea uaminifu wako kwa watu. Kama hizo ndizo fikra zako basi zitakuwa zinakuangusha.  Kama kuna kitu hukijua uliza na itakusaidia sana kufanikiwa.
Acha kufikiri eti kwa sababu umeshindwa kwa jambo unalolifanya basi eti maisha yako ndio hayawezekani tena kuwa ya mafanikio. Unaweza kufanikiwa kwa kuanza tena upya hata kama imetokea umeshindwa mara mia moja.
Acha kuchukulia kwa kudhani kwamba kwa sababu unaona mambo ni magumu, mipango haiendi na ndoto zako uniona kama hazitimii, ukaona maisha ndio basi hayawezekani. Maisha yako yanaweza kubadilika tena na kuwa bora zaidi ya hapo ulipo.

Acha kufikiri kwamba utakataliwa kwenye jambo ambalo hata bado hujaomba. Kama kuna kazi unaitaka peleka barua, acha kudhani kwamba hutapata hata kabla hujaomba.  Acha kufikiri hivyo mara moja. Fikra hizo ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako.
Acha kufikiri mawazo yako ni lazima yatakuwa hayana thamani hata kabla hujayaotoa. Kama una mawazo ya kutoa sehemu yatoe mawazo hayo bila kujishauri. Badili kampuni yako kwa kutoa wazo lako na wala usilifiche. Nani kakwambia kwamba wazo lako halina thamani?
Acha kudhani kila mtu ana hamasa kubwa ya kufanikiwa kama uliyonayo wewe. Ikiwa utajiaminisha hivyo basi utakuwa unajidanganya. Wengine ni wasindikizaji tu wala hata hawana mpango wa kufanikiwa sana kama ulivyo wewe.
Acha kudhani kwamba utatatua changamoto kubwa kwenye maisha yako kwa kuweka juhudi kidogo na za kawaida. Huwezi kutataua changamoto hizo kwa ‘staili’ hiyo. Inatakiwa kuweka juhudi nyingi na tena kwa nguvu nyingi ili kushinda changamoto za kimaisha.
Acha kufikiri maisha uliyonayo leo au kile kinachofanya vizuri leo kinaweza kufanya vizuri hivyo hata kesho ikiwa hutachukua hatua za kukiboresha. Ikiwa utakuwa unafikiri hivyo, andika maumivu, ni lazima utashindwa sana mpaka utashangaa.
Acha kufikiri kwa kudhani kwamba ipo njia ambayo unaweza kuitumia kukimbia changamoto zako mwenyewe. Hakuna njia ambayo unaweza kuitumia kukimbia changamoto zako. Kama unafikiri ipo, unajidanganya na jiandae kushindwa.
Acha kujifikiria huwezi kufanikisha mambo makubwa eti kwa sababu kila mtu ukimuangalia hakuna aliyefanikiwa kwa sehemu kubwa. Uwezo huo wa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa unao tena sana hata kama wengine hawajafanikiwa kwa kiwango hicho.
Acha kufikiria kwamba changamoto uliyonayo ni kubwa sana na huiwezi. Kama unajifikiria hivyo basi ni wazi huwezi kufanikisha jambo lolote. Kila changamotio unayoiona mbele yako, una uwezo wa kukabiliana nayo na kuishinda.
Kumbuka, kuna wakati tunashindwa sana katika maisha kwa sababu ya kuishi kwa kufikiri au kudhani. Ili ufanikiwe unatakiwa uishi kwa uhalisia na sio kuishi kwa kufikiri iko hivi kumbe uhalisia uko vile.
Wengi wamekua wakikwama kwa sababu ya kudhani. Je, jiulize ni mara ngapi umekuwa ukichukulia na kuamini kwamba jambo linatakiwa hivi, kumbe badala yake linakuwa vile.
Kuanzia sasa acha kuishi kwa kudhani tena…kama utaendelea kushi kwa kufikiri…kama utaendelea kuishi kwa kudhani…basi hakuna mafanikio makubwa utayoweza kuyaambulia.
Endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.com kila siku.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

Uchambuzi Wa Kitabu; From Poverty To Power (Utambuzi Wa Mafanikio Na Amani).

$
0
0
Kila mtu anapenda kuwa na maisha mazuri, kila mtu anapenda kuwa na mafanikio kwenye maisha yake. Lakini ni wachache kwenye jamii zetu ambao wanaishia kuwa na mafanikio kweli, ni wachache ambao wanaishi yale maisha ya ndoto zao, huku wengi wakisumbuka na maisha mpaka siku wanaondoka hapa duniani.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kipi kinawatofautisha wale wanaofanikiwa na wale wanaoishia kuwa kawaida. Wengi walifikiri ni asili, lakini kwa watu wa asili moja bado wapo waliofanikiwa na wapo walioshindwa. Wakafikiri huenda ni mazingira, lakini ndani ya mazingira sawa, kuna waliofanikiwa na wapo walioshindwa.
 

Ni baada ya uchunguzi na ufuatiliaji wa muda mrefu ndipo imekuja kugundulika tofauti ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa inaanzia kwenye akili zao, inatokana na mawazo yao. Ukichukua mawazo ya wanaofanikiwa, ni tofauti kabisa na ya wale wanaoshindwa.
Hapa ndipo mwandishi James Allen, anapotuonesha namna mawazo yetu yalivyo na nguvu ya kutengeneza maisha yetu. Karibu tujifunze kupitia kitabu chake cha FROM POVERTY TO POWER.

1. Hakuna mtu ambaye hajawahi kupitia magumu kwenye maisha yake, hakuna mtu ambaye hajawahi kukutana na majaribu. Hakuna moyo ambao haujawahi kuvunjwa, hakuna akili ambayo haijawahi kukutana na usumbufu wa mawazo. Hakuna nyumba ambayo haijawahi kukutwa na magonjwa na misiba. Kuwepo kwetu hapa duniani ni sababu namba moja ya kukutana na haya, na hivyo tunahitaji kujua njia sahihi ya kuondokana nayo.

2. Mabaya yote tunayokutana nayo kwenye maisha yetu, yanarekebishika. Mabaya haya siyo ya kudumu, labda kama sisi wenyewe tutayafanya yadumu. Hivyo unapopitia mabaya, usikate tamaa na kuona ndiyo mwisho wa safari, badala yake jua ni mapito tu na safari itaendelea.

3. Msingi wa mabaya na maovu yote ni ujinga. Kwa kukosa uelewa watu wamekuwa wakichukua hatua ambazo zinawafikisha kwenye mabaya, au kushindwa kuchukua hatua za kuwaondoa kwenye mabaya wanayopitia. Hivyo dawa ya uhakika ya kuondokana na mabaya na maovu ni kujielimisha na kuondokana na ujinga.

4. Kila mtu ana dunia yake, na dunia ya mtu imetengenezwa kwa mawazo yake, tamaa na msukumo alionao ndani yake. Kutokana na hivi vinavyotengeneza dunia ya mtu, mtu anaweza kuona dunia yake ni ya uzuri na furaha au akaona dunia yake ni ya mabaya, uovu na maumivu. Dunia unayoiona na kuiishi umeitengeneza wewe mwenyewe kwenye mawazo yako.

5. Hakuna kinachotokea nje ya mtu ambacho kinajenga au kuharibu maisha ya mtu. Maisha ya mtu yanajengwa au kubomolewa na kile ambacho kipo ndani yake. Na hapo tunaanzia kwenye mawazo yake. Kama yanayotokea nje ya mtu yangekuwa na nguvu, tungetegemea watu wote waliopo kwenye mazingira sawa basi maisha yao yawe sawa. Lakini hali haipo hivyo, hii ikimaanisha kwamba licha ya yale yanayotokea nje ya mtu, maamuzi hasa yapo ndani yake.

6. Watu huamini kwamba zile tabia walizonazo ndizo ambazo wengine wanazo. Hivyo mtu ambaye ni mwongo, huamini kila mtu ni mwongo, mwenye wivu anaona kila mtu anamwonea wivu. Hali kadhalika kwa tabia nyingine zote, ziwe nzuri au mbaya. Hii ina maana kwamba kama unataka wengine wawe na tabia tofauti, anza kujiangalia kwanza wewe una tabia gani.

SOMA; Mambo Sita(6) Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Maisha Yenye Furaha Na Mafanikio Makubwa.

7. Sheria kuu ya asili ni ile ya SABABU NA ATHARI. Sheria hii inasema kwamba kila ambacho kinatokea, kimesababishwa. Kila unachokiona ni athari za mambo yaliyosababishwa. Unavuna kile ulichopanda ni upande mwingine wa sheria hii. Hii ina maana kwamba upo hapo ulipo sasa kutokana na mambo uliyofanya huko nyuma. Na matokeo ya kesho yatategemea utakachofanya leo.

8. Hakuna nafasi ya walalamikaji kwenye dunia hii. Kwa sababu walalamikaji ni watu ambao hawapendi kuchukua hatua, bali wanatafuta wa kuwasingizia. Walalamikaji hawana nafasi kwa sababu wanakwenda kinyume na sheria ya asili. Wao wanakataa ya kwamba hawajasababisha ile hali waliyonayo sasa, wakati kwa asili wao wenyewe wamechangia kuwa pale walipo sasa.

9. Watu wengi wamekuwa wakiishi maisha ya kujidanganya (delusion), kwa kuamini vitu ambavyo haviendani na sheria ya asili. Watu hawa wamekuwa wakijikuta wanaumia kila mara kwa sababu wanakataa kukubaliana na sheria hii. Hawataki kukubali pale ambapo walikosea, au kuepuka kuchukua hatua ambazo zinawapelekea kwenye matatizo zaidi.

10. Hakuna kitu kibaya, cha kujiharibu kama kujidharau wewe mwenyewe. Kujidharau kunawafanya watu wengi kushindwa kuchukua hatua na kushika hatamu ya maisha yao. Watu wamekuwa wakijiona wao ni waathirika na hawawezi kuchukua hatua kwa lolote wanalopitia. Hii inawafanya kuendelea kuwa kwenye hali ngumu na kuishia kuwa na maisha mabovu.

SOMA; Huu Ndio Msingi Mkuu Wa Maisha Ya Furaha, Amani Na Mafanikio Makubwa.

11. Njia ya uhakika ya kuondoka kwenye umasikini au hali yoyote mbaya ni kuachana na mawazo hasi na ubinafsi ambao upo ndani ya mtu. Ubinafsi umewafanya wengi kuwa kwenye gereza la umaskini na matatizo yao wenyewe. Unapoachana na ubinafsi, na kuacha mawazo hasi, unaanza kuona mchango wako kwa wengine na kuziona fursa zaidi.

12. Utajiri na mafanikio ya kweli havipimwi kwa fedha pekee, bali kwa maisha ambayo mtu anaishi. Kama mtu ni mwema, atakuwa na maisha mazuri na wale wanaomzunguka, na atakuwa na mafanikio, hata kama hana fedha nyingi. Kama mtu amekosa wema, hata kama ana fedha nyingi kiasi gani, hana mafanikio ya kweli.

13. Ili kupata mafanikio ya kweli, ni lazima uweze kujidhibiti wewe mwenyewe. Ni lazima uweze kuyadhibiti mawazo yako, uondokane na mawazo hasi na ubinafsi na ukaribishe mawazo safi ya mafanikio. Kama huwezi kujidhibiti wewe mwenyewe, utatoa nafasi kwa vitu vingine kukudhibiti. Hakuna mafanikio kama huwezi kujidhibiti.

14. Imani na kusudi ndiyo nguvu kuu inayoendesha maisha ya mtu. Hakuna kitu ambacho imani thabiti na kusudi imara vinashindwa kukamilisha. Unahitaji kuwa na umani kwamba unaweza, kuwa na imani kwamba inawezekana, pia unahitaji kujua kusudi la maisha yako. Ukilifanyia kazi kusudi hili kwa imani, mafanikio ni yako.

SOMA; Mbinu Moja Rahisi Sana Ya Kufanikiwa Kwenye Kazi Yoyote Unayofanya.

15. Haijalishi kusudi la maisha yako ni nini, fanya kusudi hilo kwa akili zako zote, moyo wako wote na nguvu zako zote. Yaweke mawazo yako yote kwenye kufanya kusudi la maisha yako na utaweza kuvuka magumu yoyote unayokutana nayo. Kila siku unahitaji kuyatuliza mawazo yako na kuhakikisha yapo kwenye kusudi la maisha yako, usiyaruhusu yakutoroke na uanze kufikiria vitu vya kukuondoa kwenye kusudi hilo.

16. Mwili wako ni zao la akili yako, afya yako ni matokeo ya mawazo yako. Magonjwa na changamoto nyingine za kiafya unazopitia, zinatokana na mawazo ambayo umeruhusu yatawale akili yako. Ukiweza kudhibiti mawazo yako, na ukajenga nidhamu ya maisha yako, afya yako itakuwa imara.

17. Kama unalalamika kwamba kazi yako inakuchosha, basi jua unafanya kazi ambayo siyo kusudi la maisha yako, na sahau kuhusu mafanikio. Unapofanya kazi inayotokana na kusudi la maisha yako, hakuna kitu kinaitwa kuchoka, utashangaa muda unapita lakini bado una hamasa ya kufanya. Uchovu tunaoupata kwenye kazi unatokana na mioyo yetu kuwa kinyume na kile tunachofanya, na hivyo kushawishi miili yetu ikatae kufanya kitu hicho, hapo ndipo unapata uchovu.

18. Mbingu na kuzimu ni hali ambazo zipo ndani ya mtu. Mtu anapokuwa mbinafsi na kujifikiria yeye mwenyewe, anayaona maisha yake kama kuzimu. Lakini mtu anapoachana na mawazo hayo, na kuanza kuona maisha ya wengine ni muhimu, anayaona maisha yake kama mbingu. Hivyo hali yoyote unayopitia sasa, hebu kaa chini na yakague mawazo yako. Ukishajua basi dhibiti mawazo yako ili maisha yako yawe mbingu na siyo kuzimu.

19. Mafanikio ya kweli kwenye maisha yanaenda kwa wale ambao ni WAADILIFU, WAAMINIFU, WENYE SHUKRANI NA UPENDO. Ni vitu vinne ambavyo vinaanzia ndani yako, haijalishi kama umetokea familia masikini au tajiri, haijalishi una elimu kubwa au ndogo. Unachohitaji ili kufanikiwa kwenye haya maisha ni UADILIFU, UAMINIFU, SHUKRANI NA UPENDO. Ukiweza kufanya maisha yako kuwa tabia hizi nne, ni lazima utafanikiwa, lazima.

20. Dunia inatupa sisi kila kitu, lakini bado dunia imejaa utajiri wa kutosha, hatuwezi hata kuumaliza. Lakini baadhi yetu tumekuwa tunakazana kupata kila kitu, lakini tunaishia kuwa masikini wakubwa. Hivyo siri ya utajiri ni sheria ya asili, toa kile ambacho unacho. Unapotoa kile ulichonacho, unatengeneza deni, na dunia lazima ikulipe kwa kile ambacho umetoa. Ni sheria, inafanya kazi mara zote na kwa kila mtu.

Nimalize uchambuzi huu kwa kukupa wazo moja muhimu ambalo hupaswi kulisahau wakati wowote ile. Mawazo yako ndiyo yanajenga au kubomoa maisha yako, hakuna bahati wala hakuna mchawi. Unapoona mambo hayaendi vizuri, anza kuyakagua mawazo yako, anza kuangalia mambo ambayo umekuwa unafanya, na utaona sehemu unayopaswa kurekebisha.
Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Maswali Na Majibu Kuhusu Semina Ya Milioni Ya Ziada.

$
0
0

Habari za leo rafiki yangu,
Ni matumaini yangu uko vyema na unaendelea kuweka juhudi kubwa ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Najua unakumbuka ya kwamba mtu pekee wa kuyafanya maisha yako kuwa bora ni wewe mwenyewe, hakuna mwingine anayeliweza hilo. Hili ni jukumu lako ambalo unapaswa kulifanyia kazi kila siku, usilisahau rafiki.


Pia nina imani unajiandaa vyema na semina ya tarehe jumapili hii ya tarehe 30/10/2016 ambapo tutakwenda kujifunza kuhusu kuongeza kipato chako kwa zaidi ya milioni moja.
Kama bado hujalipia tiketi yako ya kushiriki semina hii fanya hivyo leo ili usikose nafasi hii ya kipekee kwako kuweza kupata maarifa na mtazamo sahihi wa kuongeza kipato chako.

Semina itafanyika jumapili hii tarehe 30/10/2016 pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.
Ni kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 11 jioni.
Gharama ya tiketi ni tsh 35,000/=
Utapata kitabu cha kuandikia, kalamu na chakula cha mchana.
Tutakuwa walimu na wanenaji wanne, ambao nitakuletea sifa zao kesho.

Kulipia tiketi yako tuma tsh 35,000/= kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na sehemu ulipo.
Fanya hivyo leo hii rafiki yangu, ili usikose nafasi hii ya kipekee kwako kupata maarifa ya kuongeza kipato chako.

Leo nataka kutoa majibu ya maswali ambayo nimekuwa naulizwa na wengi kuhusiana na semina hii ya MILIONI YA ZIADA. Nina imani kupitia maswali haya utapata ufafanuzi wa kutosha popote ambapo hujaelewa.

Swali; vipi kwa sisi ambao tupo mikoani na hatuwezi kuhudhuria, tutapataje mafunzo hayo?

Jibu; kipaumbele cha kwanza kabisa kiwe kuhudhuria semina, kwa sababu kuna nguvu kubwa sana unayoipata kwa kuwa ndani ya ukumbi wa semina kuliko kusoma au kufuatilia mafunzo ukiwa sehemu nyingine. Ndani ya ukumbi wa semina kuna nguvu kubwa ambayo inakuingia na unatoka ukiwa na hatua za kwenda kuchukua, tofauti na unapopata mafunzo kwa njia nyingine, unaweza kuona bado hujawa tayari. Pia unapata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa moja kwa moja. Bado pia utakutana na watu wapya na hivyo kukuza mtandao wako.
Kama inatokea umebanwa kabisa na hutaweza kuhudhuria moja kwa moja basi utaweza kushiriki semina ambayo tutatoa kwa njia ya mtandao (webinar). Hii ni semina ambayo inaendeshwa moja kwa moja na wewe kufuatilia kwa njia ya mtandao. Utaweza kushiriki semina hii popote ulipo kama ukiwa na mtandao wa intaneti. Kutakuwa na gharama za kushiriki semina hii.

Swali; kwa nini msiandae DVD za semina ili na sisi ambao hatutahudhuria tuweze kupata kile ambacho waliohudhuria wamefanya?

Jibu; kuandaa na kusambaza dvd za masomo haya ni kazi nyingine kubwa ambayo kwa sasa hatutaweza kuifanya. Kazi hii ya kuandaa semina pekee ni kubwa sana, kuandaa na kusambaza dvd itakuwa kubwa zaidi.
Njia bora tuliyoandaa kwa wale watakaokosa ni kushiriki semina hii tutakayoandaa kwa njia ya mtandao.

Swali; je ni kweli nikihudhuria semina hii nitaweza kuongeza kipato changu kwa milioni na zaidi?

Jibu; ndiyo, ukihudhuria semina hii utapata maarifa sahihi  ambayo kama utayafanyia kazi, ninaweza kukudhibitishia kwamba kipato chako kitakua. Tutakwenda kukushirikisha maarifa ya kile ambacho sisi wenyewe tunafanya na mbinu bora zaidi za kuongeza kipato chako kwa kuanzia pale ulipo sasa.

Swali; gharama ni kubwa sana, siwezi kupata punguzo?

Jibu; kwa semina ya siku nzima, zaidi ya masaa nane na unapata chakula pamoja na huduma nyingine, gharama ya tsh 35,000/= siyo gharama kubwa. Ukilinganisha na maarifa utakayopata, naweza kusema huu ni uwekezaji mdogo sana unaofanya, ambao utakuletea marejesho makubwa ukiyafanyia kazi.

Swali; napenda kushiriki semina hii lakini sina fedha ya kulipa ada ya ushiriki.

Jibu; fanya vyovyote uwezavyo (ila usiibe) upate fedha ya kushiriki semina hii. Kwa sababu kama mpaka sasa hujaweza kupata fedha hii ya kushiriki, basi unahitaji sana haya maarifa tunayokwenda kutoa. Kinachokufanya mpaka sasa unakosa fedha ya kuongeza maarifa ya kukuwezesha kuongeza kipato chako, ni kukosa maarifa sahihi na mtazamo sahihi wa kuendesha biashara itakayokuingizia kipato.

Omba, itisha michango na fanya njia nyingine yoyote kupata ada ya kushiriki, fikiria kama umepata dharura ya ugonjwa na lazima upate elfu 35 ungetumia njia gani kupata fedha hiyo? Itumie mbinu hiyo kupata fedha ya kushiriki semina hii.

Nitumie nafasi hii kukukaribisha sana kwenye semina hii kubwa na ya kipekee. Ni semina pekee nitakayotoa mafunzo ya moja kwa moja mwaka huu 2016. Karibu sana tujifunze kwa pamoja.
Pata tiketi yako sasa, tuma fedha tsh 35,000/= kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na mahali ulipo. Kumbuka zimebaki siku mbili pekee kupata tiketi ya kushiriki semina. Chukua hatua sasa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Vichocheo Saba Vinavyowasha Moto Wa Mafanikio Kwenye Jambo Lolote Lile.

$
0
0
Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu uko salama rafiki na unaendelea na shughuli zako za kila siku. Napenda kukualika katika makala yetu ya leo nakusihi ungana nami mwazo hadi tamati ya makala hii.

Katika makala yetu ya leo tutajifunza vichocheo saba vinavyowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile. Katika kufanya kazi mbalimbali watu hufanya kazi kulingana na hamasa wanayopata kwenye maisha yao. Kuna aina mbili za hamasa yaani hamasa ya ndani (intrinsic motivation) na hamasa ya nje (extrinsic motivation). Kama unataka kufanikiwa na kupata hamasa ya kudumu kwenye jambo lolote lile tumia hamasa ya ndani lakini ukitegemea hamasa za nje huwa hazidumu sana utafanya leo kesho hamasa imetoweka. Licha ya kuwa na hamasa zote mbili lakini mtu ambaye anapenda kazi huwa ni mtu ambaye ana hamasa ya ndani atafanya bila kujali kitu chochote kile. Mpenzi msomaji, karibu sasa tujifunze vichocheo vinavyowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile katika maisha yako.
 

1. Juhudi ; siku zote ukiwa unajituma na kufanya kazi kwa juhudi hakika utafika mbali. Juhudi ni moja ya kichocheo kinachowasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile. Kama huna juhudi au bidii ni sawa na kuchora sifuri kwenye maji rafiki yangu kwani juhudi ni kama lifti inayokuvusha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kama unataka ushindi tumia kichocheo cha juhudi na utafanikiwa kwenye jambo lolote lile.

2. Maarifa; silaha ya kuchochea mafanikio ni maarifa. Huwezi kufanya mambo kienyeji na ukategemea kufanikiwa. Dunia imebadilika na mabadiliko yanaendelea kutokea kila siku kwenye maisha yetu. Hata ufanye kazi kwa kujituma namna gani lakini kama huna maarifa sahihi kwenye akili yako ni kazi bure. Lazima ujifunze kulingana na hitaji la soko linavyokwenda sasa na fanya mambo kulingana na mabadiliko yanayotokea kwa jamii na dunia nzima.

SOMA; Mambo Kumi(10) Muhimu Usiyojua Kuhusu Mafanikio, Na Jinsi Yanavyokurudisha Nyuma.

3. Nidhamu; nidhamu ni daraja la mafanikio mpendwa rafiki yangu. Nidhamu siyo jambo la mchezo rafiki yangu unajisimamia mwenyewe bila shuruti na mtu yeyote. Kwa mfano, unajiwekea nidhamu ya kuamka saa kumi au kumi na moja kila siku alfajiri bila sababu au unajiwekea nidhamu ya kuandika makala kila siku katika maisha yako. Kuna mambo mengi ambayo ukiwa unafanya kama huna nidhamu lazima ushindwe. Nidhamu ni utii na kuheshimu kile unachokifanya bila shuruti ya kusukumwa na mtu. Kuna watu wengine wameshazoea kufanya kazi kwa kusimamiwa na mtu ndio afanye kitu Fulani.

4. Kujitoa kwa moyo. Kujitoa kwa moyo ni kufanya kazi unayoipenda kwa moyo. Na mtu yoyote anayejitoa bila kujibakiza kwenye jambo lolote lile huwa anafanikiwa kwenye maisha yake. Jinsi unavyojitoa kwa moyo ndio kinakuwa kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio. Anza kuwasha moto wa huu wa kuchochea kile unachofanya kwenye maisha yako. Kama unafanya kazi kwa shingo upande ni ngumu kupata mafanikio kwenye kile unachofanya yaani unafanya tu ili mradi umalize au ili mradi liende.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; PROSPERITY ON PURPOSE (Mwongozo wa kuishi maisha ya mafanikio makubwa).

5. Kutoahirisha mambo. Kama unavyojua watu wengi wanakumbana na changamoto ya kuahirisha mambo katika maisha yao. Kuahirisha mambo ni mwizi wa muda wa watu wengi ni wangapi kila siku wanapanga kufanya jambo Fulani lakini wanaishia njiani kwa kuahirisha. Kutoahirisha mambo ni kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio kwenye jambo lolote lile katika maisha yako. Ukipanga kitu Fulani hakikisha unakifanya kwa moyo na wakati bila kuweka sababu yoyote ile.

SOMA; Kama Unafikiri Mafanikio Yako Hivi Tu, Tayari Umeshapotea.

6. Kutosikiliza wengine wanasema nini. Ukianza kusikiliza wengine wanasema nini utashangaa unazima kichocheo cha kuwasha moto wa mafanikio kwenye maisha yako. Unatakiwa kuwa kiziwi kabisa kutowasikiliza watu kwa sababu wataanza kukukatisha tamaa kama ukiwapa nafasi ya kuwasiliza ndio mwanzo wa kukatishwa tamaa. Wewe sikiliza sauti yako ya ndani kwani ndio inaona kule unakotaka kwenda na siyo mtu mwingine. Hakuna mtu anayekujua wewe zaidi ya wewe mwenyewe. Jisikilize uendelee kuchochea moto wa mafanikio mpaka unafika pale unapotaka kufika.

7. Kutokuwa mtu wa sababu. Kuna watu kazi yao ni kulalamika na kutafuta sababu kila siku ya maisha yao. Akitaka afanye kitu Fulani lazima aanze kutanguliza sababu kwanza. Ukiwa ni mtu wa sababu rafiki sahau kuhusu mafanikio kwenye maisha yako kwani sababu ndio zinazaa vitu kama uvivu, wivu, majungu, umbea, kulaumu na kulalamika. Hivyo acha kuwa mtu wa sababu na washa moto wa mafanikio.

Kwa kuhitimisha, dunia imejaa kelele nyingi sana hivyo ni vema kuangalia kile kitu unachopenda wewe kufanya na siyo kusikiliza watu. Hakuna kichocheo chochote kinachoweza kutokea kwenye maisha yako kama vile radi au ajali lazima uamue kuwa navyo. Habari njema ni kwamba uamuzi ni bure wala huhitaji uwe na mtaji ndio uanze.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Wasifu Wa Watakaofundisha Kwenye Semina Ya MILIONI YA ZIADA Na Mada Nzuri Watakazofundisha.

$
0
0
Habari za leo rafiki?
Nachukua nafasi hii kukukumbusha ya kwamba imebaki siku moja pekee ili kujipatia tiketi yako ya kushiriki semina ya MILIONI YA ZIADA. Mwisho w akupata tiketi za semina hii ni kesho tarehe 28/10/2016, hivyo kama bado hujapata tiketi yako, chukua hatua leo ili usikose nafasi hii ya kipekee.
Kwenye makala hii ya leo nakuletea wasifu wa watakaofundisha kwenye semina hii, pamoja na mada watakazofundisha kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA. Jisomee mwenyewe sifa za watu hawa wanne, na uone kama kuna kitu kikubwa unaweza kujifunza kutokana na ujuzi na uzoefu wa watu hawa kwenye biashara mbalimbali wanazofanya.


Kabla hatujaingia kwenye wasifu wa walimu wa semina ya milioni ya ziada, naomba nijibu maswali mawili muhimu ambayo sikuyajibu kwenye makala ya jana. Jana nilitoa makala yenye maswali na majibu kuhusu semina, lakini kuna haya mawili nimeona ni muhimu ila sikuwa nimeyajibu, naomba niyajibu hapo chini ili kuweka mambo sawa.

Swali; Ahsante coach ni sahihi kama nitalipia siku ile  ya semina (mlangoni)
Hapana, kusubiri ulipe mlangoni utaikosa nafasi. Kuna maandalizi muhimu yanapaswa kufanywa kabla ya siku ya semina, mfao vifaa vya kia mshiriki wa semina kuandikia, pia maandalizi ya chakula. Hivyo tunahitaji kuwa na idadi kamili ili kufanya maandalizi mazuri. Ndiyo maana mwisho wa kufanya malipo ya semina ni ijumaa tarehe 28/10/2016. Chukua hatua sasa ya kulipia tiketi yako ili usikose nafasi hii nzuri.

Swali; Habari kaka Amani, nikushukuru kwa jitihada zako za kutuelimisha, nina swali moja kuhusiana na semina hii, hakuna uwezekano wa kupata audio ya semina hio kwa watu walioko mikoani pengine kwa gharama ileile ya 35? 
Hapana, uwezekano wa kuandaa audio haupo, kama nilivyoelekeza kwenye maswali na majibu yaliyopita, kuandaa hizi audio au video na kuzisambaza ni kazi nyingine inayohitaji muda wa kutosha, kitu ambacho kwa sasa hatutaweza kufanya. Tutaandaa webinar, maelekezo muhimu kuhusu webinar hii tutayatoa baadaye.

Karibu kwenye wasifu wa walimu watakaofundisha kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA.

Wasifu wa Faithvictory Kivea
Ni mfanyabiashara wa kusindika vyakula, matunda na mboga mboga kwa muda mrefu.  Pia Mrs Kivea hufundisha na kushauri wafanyabiashara wenye mtaji mdogo kuwawezesha wakuze mitaji yao. Kingine ni kuwa anajihusisha na kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo maeneo ya Kibamba, Dar Es Salaam. Amekuwa akifanya hivi kwa mafanikio makubwa.
Mrs Kivea, atafundisha mada zinazohusu kugeuza mtaji mdogo na kuwa mtaji mkubwa. Timu yetu inaamini kwa kiasi kikubwa utamfurahia na kujifunza vitu muhimu sana kuelekea kujitengenezea angalau milioni ya ziada kila mwezi. Karibu ujifunze kutoka kwake.

Wasifu wa Michael Mwakilasa.
Yeye ni mfanyabiashara aliyebobea katika uzalishaji wa mafuta ya diseli kutumia mabaki ya mafuta migahawani na mahotelini. Mr Mwakilasa ni Mtanzania wa kwanza kabisa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha diseli.
Mr Mwakilasa, ameishi nchini Marekani kwa zaidi miaka 23, kwa hiyo, Mbali na uzoefu na utaalamu wa kuzalisha mafuta ya Diseli, Mr Mwakilasa ana uzoefu mkubwa wa biashara kwa kufanya kazi katika mashirika makubwa nchini Marekani na Canada.
Mr Mwakilasa atazungumzia mambo muhimu ya uanzishaji viwanda vidogo. Atachangia uzoefu wake na pia kuwapa mbinu kwa wale wafanyabiashara wadogo wanaotaka kuanzisha viwanda vidogo. Pia atatoa mbinu mbali mbali ambazo zitakusaidia kukupeleka kwenye lengo lako la kutengeneza angalau Milioni Moja ya Ziada kwa Mwezi.

Wasifu wa Makirita Amani.
Makirita Amani ni mwandishi, mshauri na mjasiriamali. Ni mwanzilishi na mwendeshaji wa mitandao ya AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA, mitandao ambayo inatoa elimu, maarifa na hamasa ya kujitambua na mtu kuchukua hatua juu ya maisha yake mwenyewe.
Makirita ni mkurugenzi wa kampuni ya uwekezaji inayoitwa KICHAMATA INVESTMENT COMPANY, kampuni inayowekeza kwenye kilimo biashara. Kampuni hii ina wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali Tanzania.
Makirita ni mwandishi wa kitabu, BIASHARA NDANI YA AJIRA, Jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Amekuwa akitoa ushauri na kufundisha kuhusu biashara, utambuzi binafsi na mafanikio.
Kwenye semina hii Makirita atafundisha jinsi ya kuanza biashara kutokea sifuri hata kama huna mtaji. Atafundisha mambo muhimu ya kuzingatia pale unapoanza biashara yako ili uweze kuikuza na kukuletea mafanikio.
Pia Makirita atakushirikisha hatua sita muhimu za kufuata ili uweze kuanza biashara na kufikia faida ya zaidi ya milioni moja kila mwezi.
Usikose nafasi hii ya kujifunza jinsi unavyoweza kuanza biashara yako ukiwa hapo ulipo sasa.

Wasifu wa Felix Maganjila
Ni mmoja wa washauri na walimu wenye uzoefu wa muda mrefu katika biashara za ndogo na za kati hapa Afrika Mashariki. Yeye anamiliki blogu ya www.napendabiashara.co.tz na pia ni mmiliki wa mfumo kabambe  wa kumsaidia mfanyabiashara kuongeza mauzo bila kuwekeza pesa nyingi. Mfumo huu unapatikana www.makeyoursalesgrow.com
Kabla ya kuanza kutoa ushauri na mafunzo kwa wafanyabiashara, yeye mwenyewe pia amefanya biashara mbalimbali hapa Tanzania. Pia amefanya biashara wakati akiishi Nairobi, Kenya kabla hajarudi Tanzania moja kwa moja.
Katika uzoefu wake wa miaka 20 wa kushauri na kufundisha, ameshaweza kuwasaidia wafanyabiashara wengi kupata mafanikio.
Mfano, aliweza kuisaidia kampuni Fulani kukuza mauzo kutoka Tshs Milioni 200 kwa mwezi hadi milioni 800 katika kipindi kisichozidi miezi 6. Pia aliweza kusaidia kampuni nyingine kuongeza mauzo kutoka Tshs milioni 8 kwa mwezi hadi Milioni 30 kwa Mwezi ndani ya mwezi 3.
Kwa kampuni ndogo, aliweza kumsaidia mfanyabiashara kukuza mtaji kutoka Tshs 300,000 hadi milioni 5 ndani ya miezi 5
Katika semina hii Maganjila atakufundisha yafuatayo yatakayokusaidia kukuza pato lake:
·        Kanuni kuu ya kukuza mtaji wako hata kama ni mdogo
·        Utajifunza mbinu ya kuweka akiba ambayo haifundishwi mahali popote.
·        Mfumo bora kabisa duniani wa kutumia, kutunza na kusimamia pesa zako. Hii ni siri ambayo watu wengi waliofanikiwa hawataki uijue kwani wanaogopa na wewe kutajirika.
·        Hatua sita za kufuata zitakazokuza kipato chako na kukuacha unashangaa kwa nini hujaijua siri kwa muda mrefu. Kufahamu siri hii, itakufanya uwe tofauti sana kimapato.
·        Mambo 9 ya kufanya kuweza kuongeza pato lako haraka na kwa kiasi kikubwa
Pata tiketi yako sasa uweze kugundua siri za kukubadilisha maisha yako.

Imabeki siku moja pekee kupata tiketi yako, kesho ndiyo siku ya mwisho kwako kupata tiketi ya kushiriki semina ya MILIONI YA ZIADA. Kupata tiketi yako leo, ili uweze kupata maarifa haya mazuri kutoka kwa walimu hawa wanne, chukua hatua sasa.
Kupata  tiketi tuma ada ya kushiriki semina tsh 35,000/= kwenda namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na sehemu ulipo ili uweze kuandaliwa na kuletewa tiketi.

Chukua hatua sasa rafiki, hii ni nafasi ambayo hupaswi kuikosa kabisa kwenye maisha yako.
Karibu sana kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz


MUHIMU SANA; Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuipata fursa ya kutengeneza MILIONI YA ZIADA kwa kuanzia hapo ulipo.

$
0
0
Habari rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, ni siku nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho umechagua kufanya. Tumia muda wa leo vizuri rafiki yangu.
Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha ya kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kabisa kuipata fursa ya kutengeneza MILIONI YA ZIADA kula mwezi kwa kuanzia hapo ulipo sasa.

Leo ndiyo siku ya mwisho kulipia tiketi yako ya semina hii ili ujihakikishie nafasi ya kushiriki semina hii, na tuweze kufanya maandalizi bora kwako ili itakapofika siku ya semina, uweze kuondoka na kitu bora kabisa.

Kwa uzoefu wangu, kupitia semina mbalimbali ambazo nimekuwa natoa, watu wengi huwa wanakuja baada ya siku ya mwisho, wakiwa na sababu nyingi kwamba hawakuona tangazo la siku ya mwisho. Kwa bahati mbaya sana wamekuwa wanakosa nafasi hizo. Hivyo napenda nikusihi wewe rafiki yangu, chukua hatua sasa, ukisema utafanya baadaye utasahau, halafu ukisahau utakuja kukuta nafasi zimeshakwisha na hivyo kukosa fursa hii nzuri na ya kipekee sana kwako kupata maarifa sahihi.

Chukua hatua sasa kuhakikisha unashiriki semina ya milioni ya ziada, usikose semina hii nzuri na ya kipekee.
Nilianza kukupa taarifa za semina hii tangu mwanzoni mwa mwezi wa nane, hivyo kwa miezi miwili iliyopita nimekuwa nakukumbusha kuhusu semina hii. Leo tumefika kileleni kabisa, leo ndiyo siku ya mwisho ya kupata tiketi yako ya kushiriki kwenye semina hii.

Kwa kukumbusha tu, kama ndiyo unazipata taarifa hizi kwa mara ya kwanza;

Semina ya MILIONI YA ZIADA, ni semina inayotoa maarifa ya jinsi ya kuongeza kipato chako kwa zaidi ya milioni kila mwezi, kwa kuanzia hapo ulipo sasa. Ni semina muhimu kwa wale wanaotaka kuanzisha biashara, na wale ambao tayari wana biashara na wanataka kuzikuza. Semina hii ni mahususi kwa waajiriwa na wasioajiriwa na kwa wafanyabiashara wadogo na wafanyabiashara wa kati.

Kama umekuwa unapanga kuanza biashara lakini kila siku unajikuta huwezi kufanya hivyo, badala yake unakuwa na sababu kwa nini huwezi kuanza, au kama una biashara lakini imedumaa, kila mwaka iko hapo hapo, njoo kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA, na walimu wanne, wenye ujuzi na uzoefu mbalimbali watakushirikisha hatua za kutoka hapo ulipo sasa.
Hii ni semina ambayo mtu yeyote mwenye kiu ya kuongeza kipato chake, hapaswi kuikosa. Inafanyika mara moja pekee kwa mwaka. Ni muhimu sana uchukue hatua leo.

Kwa kifupi kabisa hizi ni taarifa muhimu kuhusu semina;

Taarifa Kuhusu Semina ya MILIONI YA ZAIDI
Tarehe: Itafanyika tarehe 30-Octoba-2016
Mahali: Ubungo Plaza, Blue Pearl Hotel
Ada: Ni Tshs 35,000 tu kwa mtu.
Muda: Saa 3.45 asubuhi mpaka saa 10 jioni
Malipo: Lipa kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887.

Nihitimishe kwa kusisitiza hili rafiki yangu, kama utashindwa kuchukua hatua leo, utakuwa umeamua wewe mwenyewe kukosa maarifa haya ya kukuwezesha kutoka hapo ulipo sasa. Mwisho wa kulipia tiketi za semina hii ni leo ijumaa tarehe 28/10/2016, na semina ni jumapili tarehe 30/10/2016. Baada ya leo tunahitaji kufanya maandalizi ya vifaa vya kuandikia, chakula na maandalizi mengine ili utakapofika jumapili upate huduma bora kabisa.

Fanya malipo sasa kwa kutuma tsh 35,000/= kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na mahali ulipo ili uweze kuletewa tiketi yako.

Karibu sana rafiki kwenye semina hii ya MILIONI YA ZIADA, usifanye makosa na kuikosa semina hii.

Nakukaribisha sana, tuwe pamoja na walimu wengine watatu, tukikushirikisha maarifa bora yatakayokutoa hapo ulipo.
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz


Taarifa Muhimu Kwa Waliolipia Semina Ya Milioni Ya Ziada Na Nafasi Ya Mwisho Kabisa Kwa Ambao Hawajalipia.

$
0
0
Habari rafiki?

Leo napenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa fupi kuhusu semina ya MILIONI YA ZIADA, itakayofanyika kesho jumapili tarehe 30/10/2016 pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.
Mwisho wa kulipia ili kupata tiketi za semina hii ilikuwa jana ijumaa, tarehe 28/10/2016, ili leo jumamosi tuweze kufanya maandalizi yote muhimu kwa ajili ya semina hii.

Kwa wale ambao tayari wameshalipia, kuna ambao tumeweza kuwafikishia tiketi walipo, wengine bado hawajapata tiketi zao. Kwa wale ambao hawajapewa tiketi zao, tunza ujumbe wako uliopokea baada ya kutuma malipo ya semina, kisha asubuhi siku ya semina utaonesha ujumbe huo kisha utapewa tiketi yako.


Nafasi ya mwisho kabisa kama hujapata tiketi.
Mpaka jana usiku kuna watu walikuwa wakituma ujumbe kuomba kama nafasi za kupata tiketi bado zipo. Wengine wamekuwa wakisema hawakupata taarifa mapema au hawakuwa wamepata fedha ya kushiriki semina hii.

Ili tusiwaache wenzetu nyumba, ambao wanaweza kunufaika sana na semina hii, tunatoa nafasi ya mwisho kabisa leo jumamosi tarehe 29/10/2016. Kama utaweza kufanya malipo kabla ya saa sita kamili mchana leo jumamosi, fanya hivyo ili uweze kushiriki semina hii.
Hii ni nafasi ya mwisho kabisa kwako rafiki yangu, kama kweli hutaki kupitwa na semina hii, basi chukua hatua kabla ya saa sita kamili mchana. Baada ya hapo tutahitaji kufanya maandalizi kwa ajili ya washiriki.

Kwa kifupi kabisa hizi ni taarifa muhimu kuhusu semina;
Taarifa Kuhusu Semina ya MILIONI YA ZAIDI
Tarehe: Itafanyika tarehe 30-Octoba-2016
Mahali: Ubungo Plaza, Blue Pearl Hotel
Ada: Ni Tshs 35,000 tu kwa mtu.
Muda: Saa 3.45 asubuhi mpaka saa 10 jioni
Malipo: Lipa kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887.

Nihitimishe kwa kusisitiza hili rafiki yangu, kama utashindwa kuchukua hatua leo, utakuwa umeamua wewe mwenyewe kukosa maarifa haya ya kukuwezesha kutoka hapo ulipo sasa. Muda ulioongezwa ni kwa leo jumamosi mpaka saa sita kamili mchana, chukua hatua sasa hivi unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii nzuri ya kujifunza.

Fanya malipo sasa kwa kutuma tsh 35,000/= kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na tunza ujumbe wako ili uweze kupewa tiketi yako siku ya semina.
Karibu sana rafiki kwenye semina hii ya MILIONI YA ZIADA, usifanye makosa na kuikosa semina hii.

Nakukaribisha sana, tuwe pamoja na walimu wengine watatu, tukikushirikisha maarifa bora yatakayokutoa hapo ulipo.
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz


Asante Sana Rafiki Na Karibu Kwenye Semina Ya MILIONI YA ZIADA LEO.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Ni imani yangu kwamba uko vizuri na unaendelea kuweka juhudi kubwa ili kuyafanya maisha yako kuwa bora kama ambavyo umepanga kwenye malengo yako. Hongera sana kwa hatua hii muhimu rafiki yangu.


Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe rafiki yangu kwa kuendelea kuwa nami mpaka sasa. Nakushukuru kwa kuendelea kufuatilia maarifa ambayo nimekuwa natoa kila siku. pia nikushukuru kwa kuwa mvumilivu kwa kipindi cha wiki hii ambapo nilikutumia makala na email nyingi zinazohusiana na semina. Nashukuru uliendelea kusoma na kujibu hata pale ambapo ulijua huenda hutoweza kufika. Nakushukuru kwa hilo rafiki.
Kuanzia wiki ijayo tutarudi kwenye utaratibu wetu wa kawaida wa kupokea makala na email tatu kila wiki.

Leo hatutakuwa na makala au email ya falsafa, badala yake tutaendelea kuzipata wiki ijayo.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye semina ya MILIONI YA ZIADA, inayofanyika leo pale BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO PLAZA. Semina inaanza saa tatu na nusu asubuhi mpaka saa kumi na nusu jioni.

Kama tayari umeshalipia semina fika mapema na tiketi yako kama umeshapewa, kama bado fika na ujumbe maalumu wa semina uliotumiwa, kisha utakuta orodha ya majina na utapewa tiketi yako na kuweza kuingia kwenye semina.

MUHIMU KWA WALE AMBAO HAWAKULIPIA TIKETI.
Kama hukuweza kulipia tiketi mapema, ipo nafasi ya kuweza kushiriki semina hii ya leo. Zimebaki nafasi chache na hivyo unaweza kuja na kulipia pale pale ukumbini. Cha kufanya wahi mapema saa tatu asubuhi,  ukiwa na fedha yako kamili, tsh 35,000/= utalipa moja kwa moja na kupata tiketi ya kushiriki semina hii.

Tutakuwepo walimu wa nne na wana mafanikio wengi tukishirikishana maarifa muhimu ya kuweza kukutoa hapo ulipo sasa na kufika mbali zaidi.

Karibuni sana marafiki zangu, leo tutaonana na kujifunza ana kwa ana, hatua kwa hatua, litakuwa tukio kubwa na la kipekee kwenye maisha yetu. Usikubali kulikosa.

Kwa kifupi kabisa hizi ni taarifa muhimu kuhusu semina;
Taarifa Kuhusu Semina ya MILIONI YA ZAIDI
Tarehe: Itafanyika tarehe 30-Octoba-2016
Mahali: Ubungo Plaza, Blue Pearl Hotel
Ada: Ni Tshs 35,000 tu kwa mtu.
Muda: Saa 3.45 asubuhi mpaka saa 10 jioni
Malipo: Fika BLUE PEARL HOTEL, UBUNGO PLAZA ukiwa na fedha kamili tsh 35,000/= na utalipia na kupata tiketi yako mlangoni.

Nihitimishe kwa kusisitiza hili rafiki yangu, kama utashindwa kuchukua hatua leo, utakuwa umeamua wewe mwenyewe kukosa maarifa haya ya kukuwezesha kutoka hapo ulipo sasa.

Karibu sana rafiki kwenye semina hii ya MILIONI YA ZIADA, usifanye makosa na kuikosa semina hii.
Nakukaribisha sana, tuwe pamoja na walimu wengine watatu, tukikushirikisha maarifa bora yatakayokutoa hapo ulipo.
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz


Shukrani Za Dhati Kwa Washiriki Wa Semina Ya Milioni Ya Ziada Na Taarifa Za Upatikanaji Wa Vitabu.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Ni imani yangu kwamba uko vizuri kabisa na unaendelea kufanyia kazi yale ambayo umekuwa unajifunza kila siku ili maisha yako yawe bora zaidi. Kumbuka jukumu la kuyafanya maisha yako kuwa bora ni lako mwenyewe, hakuna mtu mwingine mwenye muda wa kufanya hilo zaidi yako wewe mwenyewe. Hivyo chagua kuchukua jukumu hili mapema ili uweze kuwa na maisha bora kama utakavyo.

Leo napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa marafiki wote ambao jana walihudhuria semina ya MILIONI YA ZIADA iliyofanyika BLUE PEARL HOTEL, ubungo plaza. Imekuwa ni semina nzuri na ya kipekee ambapo washiriki wote wamekiri kutoka na vitu ambavyo watakwenda kuvifanyia kazi ili kuboresha maisha yao kwa kuanzia na eneo la kipato.

Natumia nafasi hii kuwashukuru sana marafiki wote ambao walihudhuria semina ile. Wapo marafiki ambao walisafiri kutoka mikoa mbalimbali, Mwanza, Shinganya, Mtwara, Mbeya, Iringa na Tanga. Tunathamini sana kujitoa kwenu kwa muda na kwa fedha ili kuweza kupata maarifa ambayo yatafanya maisha kuwa bora zaidi.
Kitu kimoja ambacho nimekuwa najifunza kupitia mafunzo mbalimbali ninayotoa ni kwamba wapo watu ambao kwa namna yoyote ile, lazima watafanikiwa. Kwa sababu ni watu ambao wapo tayari kujitoa na kuwekeza katika mafanikio yao. Kwa sababu kama ulikuwa hujui, unahitaji kuwekeza muda, nguvu na hata fedha ili ufanikiwe.

Tunashukuru sana kwa kujitoa kwenu na tunawaahidi tutaendelea kuwa pamoja, tukipeana maarifa bora zaidi kila siku ili maisha yetu yaweze kuwa bora.
Hapa ninaweka baadhi ya picha tulizopiga kwenye semina yetu ya jana.

WAWEZESHAJI WOTE WANNE WA SEMINA.

NIKIWA NA BAADHI YA WASHIRIKI WA SEMINA AMBAO PIA NI WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA

MWEZESHAJI FELIX MAGANJILA AKITOA SOMO

BAADHI YA WASHIRIKI WA SEMINA, WAKIFUATILIA SOMO


NIKITOA SOMO
MUDA MCHACHE KABLA YA SEMINA KUANZA.


TAARIFA YA UPATIKANAJI WA KITABU BIASHARA NDANI YA AJIRA.
Kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA kinaendekea kupatikana nchi nzima. Kwa sasa tumepata mawakala kwa baadhi ya mikoa, lakini unaweza kukipata popote pale ulipo tanzania kwa kusafirishiwa kuja ulipo.
Kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA kinakupa mbinu za kuanza biashara ukiwa bado umeajiriwa. Pia kinakupa mbinu za kutumia muda wako vizuri, mawazo ya biashara, na mifereji nane ya kipato unayopaswa kuwa nayo. Ni kitabu ambacho kinamfaa kila anayetaka kuanzisha biashara au kukuza biashara yake.
Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=) na kwa waliopo mikoani unaongeza tsh elfu tano (5,000/=) kama nauli ya kutumiwa ulipo. 

Kupata kitabu hiki kama upo dar tuma fedha tsh elfu kumi kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu ili uweze kupatiwa kitabu chako.
Kama upo mkoani, tuma tsh elfu 15 kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na mahali ulipo, pia unaweza kupendekeza kitumwe kwa basi gani.

MAWAKALA WA MIKOANI.

Mpaka sasa tunao mawakala watatu ambapo unaweza kupata kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
1.     MWANZA.
Kwa wakazi wa Mwanza na maeneo ya karibu, kitabu kinapatikana kwa Bwana Mwita Wairoma, anapatikana Nyegezi Mwanza, namba zake za simu ni 0764558848/0719756365/0789461348/0622558848
2.     KYELA, MBEYA.
Kwa wakazi wa Mbeya na maeneo ya karibu, kitabu kinapatikana kwa Bwana Atupele Mwang’onda, anapatikana Kyela Mbeya, simu zake ni 0629777265/0759051543
3.     ZANZIBAR.
Kwa wakazi wa Zanzibar kitabu kinapatikana kwa Bwana Juma Hussein, namba zake za simu ni 0714312924/0776465551
Usikose kitabu hiki rafiki yangu.

Kama ungependa kuwa wakala wa kitabu hiki, tuwasiliane kwa namba 0717 396 253. Karibu sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Njia 7 Za Kujenga Tabia Bora Za Kudumu.

$
0
0
Msingi mkubwa wa mafanikio yoyote yale unajengwa na tabia. Hiyo ikiwa na maana kwamba tabia ndizo zinatusaida kujenga mafanikio ya aina fulani.
Hivyo kwa mantiki hiyo, ni muhimu kujenga tabia bora za kudumu ili kuweza kufanikiwa. Je, tunawezaje kujenga tabia bora za kudumu?
1. Jiwekee malengo.
Ili  kufanikiwa kujijengea tabia ya kudumu unayoitaka, ni muhimu sana kujiwekea malengo ya tabia hiyo unayoitaka. Ni lazima ujue kipi ufanye na kipi usifanye ili kujihakikishia kwamba utamudu kuijenga  tabia hiyo.
Kwa mfano, kama unataka kuwa msomaji mzuri wa vitabu, ni muhimu kujijengea utaratibu wa kusoma kila siku hata kama ni kurasa mbili. Chochote  unachotaka kiwe katika tabia yako ya kudumu, kiwekee malengo.

2. Tafuta msaada zaidi.
Badala ya kukata tamaa ni muhimu kutafuta msaada kwa wale ambao wamefanikisha tabia kama hiyo unayoitafuta. Acha kujishaua sana, waulize siri ya mafanikio yao.
Watu hawa ambao utajifunza tabia mpya unayotaka kuijenga watakusaidia kukuweka kwenye mstari wa kufanikiwwa. Na watu hawa wanaweza wakawa ni marafiki au jamaa zako za karibu sana.
3. Badili tabia zako hatua kwa hatua.
Kama tabia unazotaka kuzibadili ni nyingi na unahamasa kubwa ya kujenga tabia ya kudumu, badili tabia hizo hatua kwa hatua. Acha kutaka kubadili tabia hizo mara moja, utakwama.
Kama ni unataka kusoma kitabu, acha kusoma kurasa nyingi sana kwa siku moja. Kama ni kufanya mazoezi, acha kufanya mazoezi hayo kwa nguvu sana siku moja. Jifunze kubadili kila kitu hatua kwa hatua na utafanikiwa.
4. Ondoa mawazo hasi.
Wakati upo kwenye harakati za kubadili tabia zako, amini utaweza kumudu kufanikiwa. Ondoa mawazo na kila mazingira ambayo yatakufanya ufikiri kwamba huwezi kubadilika.
Kila kitu kinawezekna kwako ikiwa utakuwa chanya. Chukua hatua kila siku chanya, zinazoendana na kile unachokitaka. Kwa kufanya hivyo, utafanikiwa kufikia uwezo wako wa kubadilisha tabia hiyo
5. Tambua vizuizi.
Ni muhimu pia kutambua vizuizi ambavyo vinaweza kukuzuia wakati unabadili tabia zako. Ukishajua vizuizi hivyo inakuwa ni rahisi kuvuka na kuweza kufanikiwa.
Tambua kwamba bila kujua vizuizi hivyo, utashidwa kujenga tabia ya kudumu. Hiyo inakuwa hivyo ni kwa sababu utakuwa unashindwa kujua ni njia ipi sahihi utumie ili kukabiliana na vizuizi hivyo. 
6. Chukua hatua kila siku.
Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuimba, imba kila siku. Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuweka akiba, weka akiba hiyo kila unapopata pesa. Chukua hatua za kila tabia unayoitaka kila wakati.
Kwa kadri utakavyozidi kuchukua hatua kila siku, utajenga misuri mikubwa itakayoweza kukusaidia hatimaye kuweza kufanikiwa kutengeneza tabia yako mpya  unayoihitaji.  
7. Tafuta namna ya kujipa zawadi.
Pia unaweza ukajijengea mikakati ya kujipa zawadi fulani ikiwa utafanikiwa kujenga tabia ya kudumu. Hii ni mbinu ya kisaikolojia ambayo unakuwa kama unaidanganya akili yako ili ikisaidie kutengeza tabia unayoitaka.
kwa kuhitimisha, hayo ndiyo mambo ya msingi yanaweza kukusaidia kuweza kujenga tabia ya kudumu katika maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio, tembelea piaDIRA YA MAFANIKIO kila siku kuweza kujifunza na kuelimika zaidi.
Tunakutakia kila la kheri,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,



Hatua Muhimu Za Kukusaidia Uanze Uwekezaji Wa Ardhi Na Majengo Hata Kama Una Kipato Kidogo

$
0
0
Namshukuru Mungu kwa siku hii ya leo, nimeamka salama nikiwa na afya njema ambayo imenipa hamasa ya kuendelea kufanya kazi kama siku zote. Hata wasomaji wa Amka Mtanzania naamini mungu anaendelea kuwabariki na kupata kile mnachostahili kwa wakati. “Kwa umoja wetu tunasema asante msanifu wa sayari na maumbile yetu hakuna msanifu bora Zaidi yako” Mbali na kuandika mara kwa mara kuhusu uwekezaji wa ardhi na majengo, leo ningependa kuzungumza na watu wenye ndoto ya uwekezaji ingawa kipato chao ni kidogo, Nimeona watu wakilalamika kwamba uwekezaji huu wa ardhi na majengo haiwezekani kwa watu kama wao bali inawezekana kwa wengine tu walionacho zaidi. Inashangaza kuona Watu wengi wameweka juhudi kutafuta uwekezaji ambao ni rahisi kufanya na itakayowaletea mafanikio ya haraka. 


Ukweli ni kwamba hakuna aina ya uwekezaji ambao ni wa muda mfupi kufanya na kuwa tajiri kwa utimilifu. Uwekezaji wa ardhi na majengo una changamoto zake hata kama una kipato kikubwa kiasi gani, muhimu ni maarifa na hamasa ndiyo itakayokupa ushindi. Hivyo kigezo cha kuwa na kipato kidogo hakipaswi kuwa kikwazo cha kusonga mbele, bali hamasa ya uwekezaji unaotaka kufanya. Hivyo basi leo nimekuletea mambo muhimu ya kuzingatia ili ufike pale unapotarajia kufika pasipo kujali au kuhofia kushindwa kwa sababu ya kipato chako kuwa duni. 

Naamini leo hii utaianza safari yako ya mafanikio pasipo hofu ya kushindwa hata kama itachukua muda mrefu kiasi gani maadamu mwisho wa safari iwe ya furaha na yenye tija kwako na kwa jamii iliyokuzunguka.

1. NIDHAMU YA FEDHA
Ukweli ni kwamba watu wengi wamekuwa na malengo na matarajio makubwa sana juu ya maisha yao kiasi kwamba licha ya kupata mshahara na ujira mdogo tofauti na malengo yao bado wanafanya bidii mno katika shughuli nyingi wanazozifanya, wengine hulazimika kufanya shughuli zaidi ya moja kukuza uchumi wao ili angalau waweze kuendesha maisha yao na kukidhi mahitaji yao na wanaowategemea. Lakini idadi kubwa ya watu tuna matumizi makubwa Zaidi ya kipato chetu, wakati mwingine tunazidiwa na matumizi yasiyo na ulazima, tunalazimika ili twende sambamba na walimwengu wengine. Ndugu na rafiki yangu fahamu kwamba kila mtu anaishi kwa ndoto zake, unachopaswa wewe ni kuwa na nidhamu ya kile unachokipata na kupangilia matumizi. Nidhamu pekee ndiyo itakayo kufanya ufikie malengo yako kwa wakati, nidhamu pekee ndiyo itakayokufanya uweke akiba kwa ajili ya uwekezaji ndani ya muda muafaka. Mara zote huwaambia marafiki zangu kuwa usipojitahidi kuweka akiba sasa, upo uwezekano mkubwa wa kuangamizwa na umaskini siku zijazo. Kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo gharama za maisha zinavyozidi kupanda kutokana na ushindani wa maisha kuongezeka huku fursa zikiwa ni chache. Muda sahihi wa kufanya maamuzi na kuanza kuweka akiba ni sasa, tathmini malengo yako na jiulize maswali muhimu, je unahitaji kiasi gani cha fedha na muda ili kufikia hitaji la uwekezaji wako. Huna sababu ya kuzeeka huku ukiwa na msongo wa mawazo, huna sababu yoyote ya kufa maskini ikiwa leo hii una nguvu na uwezo wa kufanya lolote upendalo. Timiza ndoto zako inawezekana.

SOMA; Mambo Matatu Ya Kuzingatia Kabla Ya Kufanya Uwekezaji Wa Majengo Ili Uepuke “Bomoabomoa”

2. MAARIFA YA UWEKEZAJI
Maarifa ni silaha namba moja ya mafanikio yako katika uwekezaji, maarifa ni ngao yako dhidi ya umaskini na karaha zote za maisha. Haijalishi una kiwango gani cha elimu, maarifa ya uwekezaji wa majengo ni muhimu sana. Ni lazima upate maarifa ya jambo husika kabla ya kuanza kulifanyia kazi, pasipo maarifa sahihi ya uwekezaji wako ni rahisi sana kukwama, maarifa ya uwekezaji wa ardhi na majengo ni muhimu sana ili uweze kutembea na kufikia malengo pasipo kukata tamaa, watu wengi wamekata tamaa kwa kutokuwa na uhakika wa kufanikiwa kwa jambo walifanyalo, matokeo ya kushindwa huumiza moyo na hata wakati mwingine mwili hudhoofu. Mara zote huwashauri marafiki zangu kuwa kabla ya kuanza safari zao za uwekezaji ni vema wapate mwalimu wa kuwafundisha na hata kuwaongoza. Rafiki yangu mpendwa jitahidi sana kila siku kuongeza ujuzi na maarifa kuhusu uwekezaji wako na biashara uifanyayo ili kuongeza ufanisi na kupunguza uwezekano mkubwa wa kushindwa. Kitu cha muhimu kukumbuka ni kwamba, katika maisha ya sasa ni vigumu sana kufanikiwa ukiwa mwenyewe pasipo kuwa na watu wanaokuzunguka kukujenga na kukuongoza kimawazo katika kufikia malengo yako.

SOMA; Epuka Migogoro Ya Ardhi Isiyo Na Ulazima Ili Uyafikie Mafanikio Yako Kwa Uhakika

3. TOA HUDUMA ZINAZOGUSA JAMII
Watu wote waliofanikiwa sana ni wale waliogusa maisha ya watu wengi. Dunia ya leo ukitaka kupata chochote unachotaka unahitaji kuwasaidia watu wengi kupata vile wanavyotaka. Nikiwa na maana kwamba kile unachokifanya lazima kiwe kinagusa maisha ya watu wengine. Unapaswa kujiuliza unawafikia watu kiasi gani kwa huduma unayotoa, je unapata marejeo ya huduma unayotoa, je uwekezaji unaofanya unakidhi na kufurahiwa na wote wanaofikiwa au kuipata huduma zako. Kama unachokifanya hakigusi maisha ya wengine ni wazi kuwa unapaswa ubadili mtazamo wako wa hicho unachokifanya. Kwa kugusa maisha ya watu wengine ndipo na wao wanapotoa fedha zao ili uendelee kuwagusa kupitia uwekezaji wako. Kama unachokifanya kinaleta furaha kwenye maisha ya wengine hawataacha kutoa fedha zao mfukoni kukupatia ili uwape huduma zaidi. Wakati mwingine maisha ni Zaidi ya fedha bali utu na haiba yako kwa wengine ni njia yako ya mafanikio. Ni ukweli usiopingika kwamba unahitaji watu wengi sana ili ufanikiwe. Chochote kile unachokifanya kwenye dunia hii ili ufikie mafanikio makubwa unahitaji watu wengi zaidi. Wewe uliyejenga nyumba ya makazi hakikisha wakazi wako wanafurahia mazingira yako, uliyejenga karakana hakikisha miundombinu inakidhi watumiaji wako. Na wewe mwenye ndoto ya kuwa na mgahawa wa kisasa, saluni ya kisasa, shule ya kisasa, gereji ya kisasa, maduka ya kisasa na makazi ya mifugo ya kisasa usife moyo bali anza safari yako kwa nguvu zote. Watu wengi wa sasa wapo tayari kugharamia mahali ambapo wanapata kilicho bora.

SOMA; Mambo Muhimu Unayopaswa Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Greenhouse.

4. HAMASA YA UWEKEZAJI
Hakuna mafanikio pasipo changamoto, hakuna ushindi pasipo mapambano na hakuna furaha pasipo amani. Kama utambuavyo kuwa tupo hapa tulipo kutokana na matokeo ya mawazo yetu. Fikra na Mawazo yetu ndiyo yanayoakisi namna tulivyo na tutakavyokuwa. Watu wote waliofanikiwa wana siri nzito nyuma yao, karibu wote watakwambia ni msukumo mkubwa walionao wa kupambana na umaskini na kufikia ndoto zao. Safari zao za mafanikio zilijaa changamoto na vihoja vya kusikitisha lakini hamasa ndio silaha yao kuu iliyowafanya wasigeuke nyuma na hata kufikia utimilifu wao. Kwa watu walio na kipato kidogo wanahitaji hamasa Zaidi ili wafikie ndoto zao katika uwekezaji wa ardhi na majengo. Hii ni kutokana na kuhitaji muda mwingi Zaidi tofauti na wale wenye kipato cha kati na kuendelea ili kufikia viwango vya kisanifu. Hatua ya kwanza ni kuwa na eneo, huwezi kujenga kwa wakati huo weka mazingira kwa ajili ya matumizi mengine ambayo ni ya muda mfupi huku ukijipanga, leo hii wapo watu wengi wanaotafuta maeneo ya wazi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Hamasa ina ushawishi mkubwa sana katika maisha yetu, hamasa ndiyo inayosababisha kufanyika kwa maamuzi yenye ujasiri wa ushindi. Rafiki yangu nakusihi sana jitahidi kujifunza na mara zote kuwa tayari kupokea mawazo mapya. Pale unapofikiria na kujiona kwamba unajua kila kitu, ndiyo unakuwa mwisho wako wa kukua na kufanikiwa. Ili kufanikiwa kwenye maisha ya uwekezaji ni muhimu uwe tayari kujifunza kila siku ili uhamasike zaidi.
Tuendelee kuwa pamoja kupitia AMKA MTANZANIAtufike kwenye kilele cha mafanikio, pia endelea kufuatilia makala zijazo ili ujifunze zaidi.
Mwandishi wa makala hii ni mwanataaluma na mshauri wa ujenzi.
Anapatikana kwa: Simu: +255 685 729 888
Baruapepe: kimbenickas@yahoo.com
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>