Najua unapoona NYEUSI NA NYEUPE unajua nini kinaenda kuendelea hapa. Najua unajua kwamba utakwenda kuupata ukweli kama ulivyo, hata kama hupendi kuusikia ukweli. Lakini hakuna namna, lazima tu uusikie, ili sasa uamue kama utaendelea kujidanganya na kubaki hapo ulipo, au utaufanyia kazi ukweli na kuweza kufika mbali zaidi.
Tatizo linapoanzia.
Waandishi na wahamasishaji wengi wamekuwa wanasisitiza jambo hili muhimu, ili kufikia mafanikio ya kifedha, unahitaji kuwa na biashara au njia nyingine za kukuingizia kipato. Huwezi kufikia uhuru wa kifedha kama umeajiriwa na mtu mwingine, haijalishi mshahara anakulipa mkubwa kiasi gani. Ni jambo ambalo haliwezi kutokea, unaweza kuwa na maisha mazuri, lakini uhuru wa kifedha, unakutaka kwenda mbele zaidi kuhusu kujitengenezea kipato.
Sasa watu wanapoambiwa hilo huwa wanakuja na sababu hii; lakini siyo wote tuwe na biashara na kujiajiri, na hata hivyo kila mtu asipotaka kuajiriwa kazi zitafanywa na nani?
Watu huwa wanakuja na sababu nyingi kwa nini wasijisukume zaidi ya pale walipo.
Na mimi nazielewa sana sababu zako rafiki, umebanwa, unaipenda kazi yako, inakupa kila ambacho unataka na maneno mengine mengi unayoweza kujiambia.
Lakini ukweli utabaki kama ulivyo, kama umechagua kuishi maisha ya umasikini, hiyo ni njia sahihi kabisa ya kufuata. Hujakosea njia kabisa. Lakini kama unataka kuwa na maisha yenye uhuru wa kifedha, hasa kwa baadaye, pale nguvu zinakuwa zimekuishia na huwezi kufanya tena kazi kama unavyofanya sasa, umepotea njia, kwa fikra hizo huwezi kufikia kile unataka.
Tatizo zaidi.
Waandishi na wahamasishaji wengi, wamekuwa hawauchekei umasikini kabisa.
Wamekuwa wakiwaambia watu waziwazi ya kwamba, umasikini ni mzigo, umasikini ni matatizo, umasikini ni kushusha utu wako, na mimi naongeza yangu mawili, umasikini ni dhambi, umasikini ni laana. Kitu ambacho unapaswa kukivunja, kukiangusha na kukitokomeza kabisa kwenye maisha yako, bila ya kujali itakuhitaji kufanya nini. Yaani kama kipo kipaumbele cha kwanza kufanyia kazi, hata kama itakuhitaji usilale kabisa, ni kuondokana na umasikini, hauna jambo lolote zuri zaidi ya kukudhalilisha.
Lakini wazembe utawasikia wakiutetea, watakuambia hatuwezi wote kuwa matajiri, kila mtu akiwa tajiri nani atamfanyia kazi mwenzake. Na wazembe waliokubuhu wataenda mbali zaidi na kukuambia hata vitabu vya dini vinasema kwamba masikini hawataisha katika nchi.
Na mimi nakubaliana nao kabisa, lakini najua bado ni wazembe, ambao hawataki kujisumbua, wanapeleka maisha kama yanavyoenda yenyewe.
Kwa nini uwe wewe, kwa nini usiwe wewe.
Pamoja na kwamba nakubaliana na hizo hali, kwamba lazima wawepo watu wa kuajiriwa, na kwama watu wote hawawezi kuwa matajiri, swali langu ni kwa nini uwe wewe na kwa nini usiwe wewe.
Kwa nini uwe wewe ndiye wa kuajiriwa miaka yako yote, kwa nini usiwe wewe wa kuwaajiri wengine. Ndiyo, namaanisha wewe. Kwa nini unataka kujificha kwenye kivuli cha uzembe? Kwa sababu kweli wazembe wataendelea kutumia sababu hiyo, na huenda wengine hawajui hata kama ni sababu, wanaona ni mfumo wao wa maisha. Lakini kwa nini wewe? Kwa nini? Hapo ndiyo mimi sikuelewi kabisa.
Ni kweli kabisa ya kwamba, watu wote hawawezi kuwa matajiri, na hata tukachukua fedha zote duniani kila mtu akagawiwa kiasi sawa, zitawaponyoka masikini na kurudi kwa matajiri. Ambacho sielewi kwa nini wewe umeamua kujiweka kundi hilo? Kwa nini?
Yaani kwa utashi wako kabisa, pamoja na unayojua, umekubali kabisa kwamba wewe utakuwa kwenye kundi la masikini? Kwamba hutaweza kuondoka kwenye umasikini?
Wakati unajua kabisa kwamba umechagua kuwa hapo, kwa mambo uliyofanya au kutokufanya?
Hapo ndipo mimi sikuelewi kabisa rafiki yangu, ndiyo maana nitakushangaa unaponiletea sababu hizo za hovyo.
Wewe kama rafiki yangu, sitegemei uwe na sababu za kizembe kiasi hicho katika kutetea mambo ya hovyo. Ninachotaka ni useme imetosha sasa, sitaki tena kuwa kwenye kundi la wazembe, nitachukua hatua kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu. Na nina uhakika hilo linawezekana.
Nimemaliza kwa leo rafiki, lengo langu lilikuwa ni kukukera, kukuondoa kwenye mawazo ya kizembe ambayo sehemu kubwa ya jamii inajiaminisha na kukufanya ufikiri tofauti zaidi, na siyo tu kufikiri, bali uchukue hatua sasa. Iwapo kazi hiyo nimeifanikisha basi chukua hatua, iwapo nimeshindwa kukushawishi kwa nini usiendelee na uzembe huo, basi unaweza kuendelea nao rafiki, kwa sababu uzuri wa maisha ni kwamba, kila mmoja wetu ana uwezo wa kuchagua anataka nini kwenye maisha yake, hakuna wa kulazimisha.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.