Ni wakati mzuri ambao tunakutana tena kwa ajili ya kushauriana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji wa ardhi na majengo. Leo nitazungumzia kwa kina namna ya kuilinda nyumba yako dhidi ya athari zitokanazo na mchwa. Nimelazimika kuandika Makala hii baada ya kumtembelea rafiki yangu ambaye aliniomba nifike kwenye eneo lake la ujenzi. Tulizungumza mengi lakini rafiki huyu alifanya kosa ambalo wakati ujao litamgharimu sana yeye pamoja na watumiaji wengine. Rafiki huyu alipuuzia umuhimu wa kuilinda nyumba yake dhidi ya mchwa. Yamkini wapo marafiki wengine ambao nao wapo kwenye hatari hii ya kuharibiwa nyumba zao ambazo walitumia fedha nyingi kuhakikisha kuwa wanafikia lengo na kutimiza ndoto zao.
1. MCHWA NI NINI?
Mchwa ni kati ya jamii ya wadudu wanaojumuisha aina nyingi tofauti, Lakini wengi wao ni mchwa waharibifu kwa kilimo, mwitu na nyumba. Mchwa hupatikana katika sehemu kame na zile zisizotumika kwa ukamilifu. Kuna jamii tofauti za mchwa zinazopatikana chini ya ardhi, kwenye sehemu za mwituni katika miti iliyozeeka au yenye shina la shimo, na baadhi ya maeneo mchwa hujenga kalibu nakshi (vichuguu).
Aina ya mchwa wasumbufu ni wale wanaoshambulia na kuharibu vitu vyote vyenye asili ya mimea kama vile milango, madirisha, makabati, vitanda, meza, viti, vitabu, karatasi maboksi na mbao za paa. Mchwa ni hatari sana kwenye uwekezaji wa majengo, husababisha nyufa kwenye msingi wa nyumba, kuta na sakafuni hata kama hawatachomoza juu ya ardhi. Madhara ya mchwa ni kutitia na kubomoka kwa nyumba.
2. MBINU ZA KUZUIA MCHWA KWENYE NYUMBA
Kabla ya kuzuia mchwa, sharti yafahamu makundi ya dawa ambayo ni asilia na kemikali.
Kwenye sayansi ya uhandisi ujenzi, umuhimu wa kupambana na mchwa huzingatiwa sana kutokana na madhara yake kwenye majengo. Wahandisi ujenzi hupambana na mchwa kabla na baada ya ujenzi.
I. MBINU ZA KUPAMBANA NA MCHWA KABLA NA WAKATI WA UJENZI
Mbinu hii hutumika kwenye eneo ambalo nyumba mpya itajengwa, hili ni eneo ambalo mimea hai na mfu imetawala kabla ya kujengwa nyumba kwa mara ya kwanza. Mbinu hii ina hatua tatu muhimu za kuzuia mchwa wasishambulie nyumba itakayojengwa kwenye eneo hilo.
v Kusafisha eneo kabla ya ujenzi; hatua hii unapaswa kufyeka na kung’oa miti, nyasi na mizizi yote kwenye eneo lako la ujenzi. Mchwa huvutiwa na mimea dhaifu na iliyokufa,
Ni vema ukachimba angalau sentimita 20 kwenda chini kwenye eneo lote la ujenzi na kuondoa udongo wote ambao kwa kiasi kikubwa huwa una miti, majani, nyasi na mizizi iliyokufa. Kwa kufyeka na kuondoa udongo huo wa juu utakuwa umeondoa vyanzo vya chakula cha mchwa kwenye eneo lako. Na endapo utagundua kuwa kuna kichuguu kwenye eneo lako hakikisha una ki bomoa na kumuua malkia wa mchwa na kuweka dawa kali sana ya kuuwa mchwa.
v Kuweka kinga kwenye eneo la ujenzi; hatua hii hutumika kuiwekea nyumba kinga dhidi ya mchwa. Baada ya kuchimba msingi unapaswa umwagie dawa msingi wote kabla ya kuanza ujenzi. Pia baada ya kujenga msingi wa nyumba yote ni vema ukaweka dawa eneo lote la sakafu ya ndani baada ya kumwaga kifusi, na mwisho hakikisha unaweka dawa eneo lote la nje kuzunguka nyumba yako hasa pembezoni mwa ukuta wa msingi wa nyumba. Kwa kufanya hivi utakuwa umeikinga nyumba yako dhidi ya mchwa hata kama watakuwa wanazaliana na kuweka makazi jirani na eneo lako la ujenzi.
v Kuweka vikwazo wakati wa ujenzi; hatua hii inajumuisha mbinu mbalimbali za ujenzi za kuilinda nyumba dhidi ya mchwa kutokana na aina ya ujenzi na malighafi zinazotumika. Mhandisi ujenzi hulazimika kutoweka mazingira rafiki ya kuharibiwa kwa malighafi zozote ambazo zipo hatarini dhidi ya mchwa waharibifu. Kwenye hatua hii atatumia mbao zilizopikwa na dawa dhidi ya mchwa, atatumia malighafi za chuma, vioo na aluminiam kwa milango, madirisha makabati na yote yanayofanana na hayo. Pia atamwaga zege (jamvi) kwenye sakafu ya nyumba yote kabla ya kusakafia sakafu, kwa ufupi atahakikisha malighafi zote zenye asili ya mimea zinakuwa salama au kutumia malighafi mbadala.
II. MBINU ZA KUPAMBANA NA MCHWA BAADA YA UJENZI
Mbinu hii hutumika kwenye nyumba ambayo imekamilika baada ya ujenzi na ipo tayari kwa matumizi au imeshaanza kutumika kwa muda mrefu. Kwa nyumba ambayo haijaanza kutumika mmiliki huweka dawa nyumba yote kuikinga isishambuliwe na wadudu waharibifu wakiwemo mchwa. Pia kwa nyumba ambayo inatumika lakini imegundulika ina wadudu waharibifu wakiwemo mchwa, mmiliki au mtumiaji wa nyumba atalazimika kusafisha nyumba hiyo na kuweka dawa nyumba yote kuuwa na kuikinga dhidi ya wadudu waharibifu wakiwemo mchwa. Hatua hii si salama sana na si rafiki wa mazingira kutokana na kadhia na kuhatarisha afya ya viumbe wengine akiwemo binadamu. Mbinu hii humlazimu mtumiaji au mmiliki wa nyumba kuweka utaratibu na mazoea ya kuweka dawa kila baada ya muda fulani kupita.
3. TAHADHARI DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA
Kwenye ujenzi huwa nasisitiza sana umuhimu wa kutumia wataalamu ili kufikia lengo lako kwa uhakika na usalama zaidi. Leo pia nakukumbusha kuwa kabla ya kutumia dawa hizi za kuilinda nyumba yako dhidi ya mchwa ni vema ukapata ushauri wa mtaalamu wa ujenzi au kilimo na mifugo. Kuna aina nyingi za dawa zinazotumika kwa sasa na bado nyingine zinaendelea kubuniwa kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia ya utengenezaji wa madawa. Tumia dawa kwa kuzingatia maelekezo ya mtaalamu au mzalishaji wa dawa hizo. Dawa hazifanani kwenye mbinu za matumizi hivyo usiige tu kutoka kwa wengine, madhara yake huwa ni makubwa.
Kabla ya kuweka dawa kwenye nyumba ambayo umeshaanza kuitumia ni vema ukazingatia yafuatayo;
Hakikisha mifereji imekuwa safi, hakuna bomba linalovujisha maji na kausha maeneo yote yenye unyevunyevu. Weka dawa kwenye maeneo yote ambayo unafikiri ni njia au makazi ya mchwa, weka hata maeneo yote ambayo unahisi ni chanzo hata kama hakutakuwa na mchwa utakao waona.
Ng’oa na ondoa mbao zote ambazo zimeharibiwa sana na mchwa na uweke mbadala kwa usalama wa watumiaji. Pia usiruhusu mbao zozote zigusane na udongo wowote au unyevunyevu kwa muda mrefu. Hakikisha unaziba matundu yote kwenye sakafu na kuta, pia epuka kufukia miti ardhini maana hukaribisha mchwa.
Dawa nyingi za mchwa hazipaswi kuwekwa ikiwa watakuwepo watoto, wajawazito au mama anayenyonyesha. Hakikisha hakuna matumizi yoyote kwenye nyumba wakati na baada ya kuweka dawa, mtaalamu atakushauri muda wa kurudi kwenye nyumba kutokana na nguvu na tabia za dawa.
Ni vema ukakumbuka kuondoa viumbe wengine kama vile kuku, ng’ombe, ndege, samaki na wanyama wote wafugwao ili wasidhurike, maana viumbe hufa endapo watakula chochote mahali palipowekwa dawa.
Ushauri wangu kwako rafiki, ni vema ukaweka kinga dhidi ya mchwa kabla na wakati wa ujenzi na ikishindikana kabla hujaingia au kuhamia kwenye nyumba ili kuepuka kadhia na madhara kwa watumiaji wa nyumba wakati wa kuweka dawa. Ni vema ukatumia dawa zenye nguvu zaidi angalau idumu zaidi ya miaka 7 ili kupunguza kadhia za kuweka mara kwa mara. Wewe ambae umenunua kiwanja au umenunua nyumba, umuhimu wa kuweka kinga dhidi ya mchwa upo palepale. Hapa Tanzania wamejitokeza wataalamu wengi na kampuni nyingi ambazo zinatoa huduma hizi, changamoto kubwa ni wengi kutofahamu umuhimu wa jambo hili. Ni vema tukaweka utaratibu wa kuweka dawa dhidi ya wadudu waharibifu wakiwemo mchwa ili uwekezaji wa majengo uwe salama wakati wote. Na endapo utapata tatizo lolote la kiafya kutokana na dawa ni muhimu ukapata ushauri wa wataalamu wa afya kwa haraka zaidi.
Tuendelee kuwa pamoja kupitia AMKA MTANZANIA tufike kwenye kilele cha mafanikio, pia endelea kufuatilia makala zijazo ili ujifunze zaidi.
Mwandishi wa makala hii ni mwanataaluma wa ujenzi.
Anapatikana kwa: Simu: +255 685 729 888
Baruapepe: kimbenickas@yahoo.com