Habari rafiki?
Ninayo furaha kubwa kukujulisha ya kwamba, kitabu kipya IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING) kipo tayari. Hichi ni kitabu kizuri ambacho kitakupa uelewa halisi wa biashara ya mtandao. Hapa utakwenda kujifunza misingi ya biashara hii, mfumo mzima wa biashara na namna ya kuifanya vizuri ili kufanikiwa.
Kabla sijakueleza kuhusu kitabu hicho nikupe hadithi moja muhimu sana kuhusu biashara hizi imewahi kutokea kuhusu biashara hii ya mtandao. Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa nashawishiwa kujiunga na biashara ya mtandao, lakini kutokana na taarifa nilizokuwa nimepata kwa watu, niliona ni biashara isiyofaa. Na hivyo sikujisumbua nayo. Baadaye nikaona wapo watu wanaifanya kwa muda mrefu, nikasema lazima kutakuwa na kitu watu wengi hawakijui. Nikaingia google na kutafuta vitabu vilivyoeleza vizuri biashara hii. Nilisoma kitabu kimoja na baadaye nikakutana na mtu akanishauri nisome kitabu cha Robert Kiyosaki kinachoitwa THE BUSINESS OF 21ST CENTURY. Nilikisoma kitabu hicho, na kwa hakika niliuelewa vyema mfumo huu wa biashara. Nikachagua biashara ya kujiunga nayo na kuifanya.
Baadaye kutokana na muda wangu kubana, kwa kuwa sikuendelea kuikuza biashara ya mtandao, badala yake niliweka nguvu zangu nyingi kwenye biashara nyingine na uandishi. Sasa kila mara zinapokuja biashara mpya hapa Tanzania, watu wengi wamekuwa wananitafuta, wakiamini kwa mtandao mkubwa nilionao, nitanufaika sana. Sasa mwaka 2014 ilikuja biashara moja inaitwa TelexFree, ilikuja kwa mgongo huu wa network marketing na nilitafutwa na wengi, wengi wakiniambia hii ni dili nzuri ya mjini hupaswi kuikosa. Nikasema wacha nihudhurie mafunzo yao. Nikahudhuria na nikaifuatilia kwa kina, kwa vigezo ambavyo nimekushirikisha kwenye kitabu hichi. Nikaona kampuni ile haifai. Nikawaambia watu ninaofahamiana nao kuhusu kampuni hiyo kukosa sifa.
Lakini kama unavyojua, watu wakishapewa mahesabu ya mamilioni, akili zinahama kabisa. Wengi hawakunisikiliza. Haikuchukua muda serikali ilifungia biashara ile, kwa sababu zile nilizoeleza watu wasijiunge. Sema hii haikuchukua muda sana, kama ingeenda miezi sita zaidi, madhara yake yangekuwa makubwa kuliko ya DECI, akama unaikumbuka DECI.
Sasa kila siku marafiki zangu wamekuwa wananiomba ushauri juu ya kampuni mpya zinazokuja kila siku. Zipo kampuni mpya karibu kila siku zinakuja, zinazojinadi kwa kutumia njia hii ya mtandao. Lakini ukizichunguza kwa ndani, unaona kabisa siyo biashara halali za mtandao, bali ni utapeli au kama unavyojulikana kama mchezo wa upatu.
Baada ya kuona habari za kampuni hizi zisizo sahihi zinazidi kuwa nyingi, nimeamua kukaa chini na kuandika kitabu hichi cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO.Katika kitabu hichi nimeichambua kwa kina biashara hii kiasi cha kukuwezesha wewe kufanya maamuzi sahihi kuhusu biashara hii. Ukisoma kitabu hichi, hutakuja kutapeliwa au kudanganywa tena, utakuwa unawaangalia wengine wakidanganyana na mamilioni ya uongo, lakini wewe utachukua maamuzi sahihi.
Na kama tayari upo kwenye biashara ya mtandao, utajifunza njia bora za kujenga timu yako ili kuweza kufanikiwa kupitia biashara hii. Utajifunza namna ya kupata watu sahihi badala ya kupata watu wanaojiunga na kuacha haraka.
Kwenye kitabu hichi utajifunza msingi wa biashara kwa ujumla na kuhusu kutafuta masoko ya biashara. Hii ni kwa kila mtu na siyo tu kwa biashara ya mtandao.
Utajifunza kwa kina maana ya biashara ya mtandao, na nimekupa mifano ya jinsi ambavyo hapo ulipo sasa unafanya biashara ya mtandao lakini hulipwi. Nimekueleza kwa kina mifumo ya malipo. ipo mifumo mikuu minne ya malipo. unapaswa kuijua yote, faida na changamoto zake na mambo ya kuzingatia kwa kila mfumo. Hapa utaona kwa picha kabisa.
Nimekushirikisha kwa kina mambo KUMI ya kuzingatia ili kuweza kuikuza biashara ya mtandao. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa na kusema biashara hii haifai.
Nimekupa faida KUMI za biashara hii ya mtandao, wengi wamekuwa wanafikiria fedha tu, ndiyo fedha ni moja wapo, lakini unajua faida nyingine TISA! Nimezieleza kwa kina ndani ya kitabu hichi.
Kwa kuwa kampuni zinazofanya biashara hii ni nyingi, kuchagua ni changamoto. Kwenye kitabu hichi, nimekupa vigezo KUMI vya kuzingatia ili uweze kuchagua kampuni itakayokufaa kufanya nayo biashara hii.
Mwisho kabisa, na ambapo ni muhimu zaidi, nimekupa maarifa ya kuitambua biashara halali na mchezo wa upatu. Hapa nimekupa mambo KUMI muhimu ya kuangalia ili kujua kama biashara ni halali au la. Nakuambia utakaposoma namba moja pekee, utaona namna biashara nyingi unazoambiwa ni za mtandao siyo bali ni utapeli.
Ninachokuambia rafiki yangu, soma kitabu hichi.
Huenda unasema kwamba wewe hufanyi biashara ya mtandao, wala huna mpango wa kuifanya, kwa sababu una biashara nyingine. Sasa nakuambia wewe ndiyo muhimu mno kukisoma. Kwa sababu ndani ya mtandao kuna siri kubwa sana ya kukuza biashara yoyote ile. Kwa kusoma kitabu hichi, wewe mwenye biashara, unaweza kuona njia ya kutumia mtandao wa wateja wako ulionao sasa kuwafikia wateja wengi zaidi.
Nasema rafiki yangu, soma kitabu hichi, na utaondoka na maarifa sahihi kuhusu biashara ya mtandao na hata kuweza kukuza biashara yoyote unayofanya kwa kutumia mtandao wa wateja wako.
UNAPATAJE KITABU HICHI?
Kitabu ni nakala tete, yaani softcopy (pdf) hivyo unaweza kusomea kwenye simu yako, tablet au kompyuta kama unavyosoma hapa.
Kitabu kinatumwa kwa email, hivyo popote ulipo unaweza kutumiwa kitabu hichi, huhitaji hata kuondoka hapo ulipo sasa hivi.
Gharama ya kitabu ni ndogo, ukilinganisha na maarifa utakayopata. Ni shilingi elfu tano (5,000/=).
Lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, na napenda sana upate kitabu hichi mapema, nakupa zawadi ya kitabu hichi kwa shilingi elfu nne (4,000/=). Zawadi hii ni kwa siku moja tu, leo tarehe 01/06/2017. Baada ya hapo bei yake ni shilingi elfu tano.
Malipo yanafanyika kupitia namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, TIGO PESA 0717 396 253, AIRTEL MONEY tuma moja kwa moja kwenye tigo pesa. Majina yanayotokea ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha, tuma email yako kwa njia ya mesej kwenda namba 0717 396 253 pamoja na jina la kitabu na utatumiwa kitabu mara moja.
Rafiki, nikusisitize sana, pata kitabu hichi. Naona kila siku namna watu wanafanya maamuzi yasiyo sahihi na yanawagharimu. Huenda ulishafanya hivyo au bado. Sasa wekeza kiasi hicho kidogo upate maarifa sahihi, ambayo yatakuepusha kupotezewa muda, fedha na hata heshima yako.
Pata kitabu hichi leo hii tarehe 01/06/2017 kwa bei ya punguzo ili uweze kukisoma.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani.