Habari za leo rafiki,
Karibu kwenye makala zetu za ushauri wa changamoto mbalimbali ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio tunayotaka kwenye maisha yetu. Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, hivyo njia bora siyo kuzikimbia, bali kuzitatua na kuweza kusonga mbele. Kwa sababu jambo moja kuhusu changamoto ni kwamba, usipoitatua, itaendelea kukufuata popote utakapoenda.
Kwenye ushauri wa leo tutakwenda kuangalia kuhusu kuacha masomo (chuo) na kwenda kufanya biashara. Je ni uamuzi sahihi, hasa pale hali ya wewe kuendeleana masomo inakuwa ngumu? Karibu kwenye makala ya leo tukaangalie kwa undani.
Lakini kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyeomba ushauri juu ya hili;
Mimi ni mwanafunzi wa chuo lakini napenda sana biashara na nasoma kwa shida sana natamani hata kuacha chuo nifanye biashara naomba ushauri. Arnold S. T.
Arnold, pole sana kwa changamoto hiyo unayopitia ya kusoma kwa shida. Na pia hongera kwa kuwa na mapenzi ya kufanya biashara, na hivyo kupata mawazo ya kuachana na masomo na kwenda kufanya biashara. Lakini mimi sikushauri uache chuo na kwenda kufanya biashara.
Najua huenda umewahi kusoma mahali kwamba wafanyabiashara wakubwa duniani waliacha chuo na kwenda kufanya biashara. Huenda una mifano ya Bill Gates na Mark Zuckerberg ambao waliacha chuo na kuingia kwenye biashara, na leo hii ni mabilionea wakubwa. Hizi ni hadithi nzuri sana ambazo tunapewa kila siku na kushawishika kwamba, kuendelea kusoma ni kupoteza muda na badala yake tuachane na shule na kuingia kwenye biashara.
SOMA; Biashara Ambazo Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Anaweza Kufanya Bila Kuathiri Masomo Yake.
Hayo yanaweza kuwa mawazo mazuri kwa juu juu, lakini leo nikusaidie kuchimba ndani kidogo ambapo utaona ambacho umekuwa huoneshwi. Tukianza na marekani penyewe, ambapo ndipo mifano hii ni mingi sana, asilimia 80 ya biashara zote zinazoanzishwa, hufa ndani ya miaka mitano, yaani hapo zinakufa kabisa, hazisikiki tena. Nakatika zile zinazopona, asilimia 80 tena zinaufa kwa miaka mingine mitano. Hii ina maana biashara 100 zikianzishwa leo, miaka kumi baadaye zitakuwa zimebaki biashara nne pekee. Sijui unaelewa vizuri hapo, yaani biashara 96 kati ya 100 zitakuwa zimepotea kabisa ndani ya miaka 10. Sasa unaweza kuona namna gani mazingira ya biashara siyo rahisi kama wengi wanavyofikiri. Simaanishi kwamba ukiendelea kusoma utapunguza hatari hii.
Kitu cha pili, angalia watu hawa waliacha vyuo, walikuwa wanasoma vyuo gani? Ukiangalia waliacha vyuo ambavyo kupata nafasi ya kudahiliwa tu lazima uwe na uwezo wa kipekee sana. Chuo kama Havard ambapo ndipo wengi wanaotumiwa kwenye mifano wameacha, kuna watu wanakesha usiku na mchana wapate nafasi ya kusoma pale lakini wanakosa.
Kwa hiyo hii inaonesha watu hawa tayari kuna kitu kikubwa walichokuwa nacho kabla hata ya kupata nafasi kwenye vyuo hivyo. Hapa pia simaanishi uwezo wako ni mdogo, bali mazingira hayaendani.
Kitu cha tatu na cha mwisho nitakachokuonesha leo, japo vipo vingi, ni kosa moja kubwa
katika kufikiri linaloendana na hadithi hizi. Kwenye saikolojia kuna kitu kinaitwa SURVIVORSHIP BIAS. Na hii ni kwamba wale wanaopona au kufanikiwa, ndiyo wanaohadithia au wanaoandikwa sana. Yaani ipo hivi, wakati Bill Gates au Mark wanaanzisha biashara zao, wapo watu wengi mno ambao nao walikuwa wanaanzisha biashara zao. Lakini wao husikii hadithi zao sasa hivi, kwa sababu wameshapotea kabisa kwenye ulimwengu wa biashara. Hivyo tunasikia na kusoma kuhusu washindi pekee, wale wanaoshindwa hatuwasikii, kwa sababu hakuna mtu ana muda nao.
Je ufanye nini?
Nimekuambia usiache chuo na kwenda kufanya biashara, hivyo ushauri wangu kwako ni huu, fanya vyote kwa pamoja. Ndiyo, endelea na masomo na huku ukifanya biashara yako kwa pembeni. Najua hili ni gumu, hasa ukizingatia kwa sasa unasoma kwa shida, lakini huna namna, itakubidi ufanye hivyo. Kwa sababu nakuhakikishia, hata ukiacha chuo na kwenda kufanya biashara, bado mambo hayatakuwa rahisi kama unavyofikiri sasa.
Swali ni je utawezaje kufanya vyote kwa pamoja, utapata wapi muda, utapata wapi mtaji? Na haya ndiyo maswali muhimu ya kujiuliza ili uweze kuanza vizuri.
Kwanza kabisa unahitaji kujipanga vizuri, lazima uache kujichukulia kama wanafunzi wengi wa vyuo. Wewe una kesi tofauti, hivyo lazima ujipange kitofauti kabisa. Na hili linaanzia kwa namna unavyotumia muda wako na hata unapopanga ratiba zako binafsi na ratiba za chuo.
Hivyo hapa kaa chini na panga muda wako. Uzuri chuoni ratiba ya wiki nzima utakuwa unaijua, unajua unapaswa kuwa wapi kwa wakati gani. Na pia mitihani unajua ni wakati gani na unapaswa kuwa umesoma nini na nini ili kuweza kufaulu. Hapo sasa unapangilia ule muda wako mwingine uliobaki. Wakati wanafunzi wenzako wanaenda kupumzika, kutembea, disco, kuangalia mpira na starehe nyingine, wewe weka muda wako huo kwenye biashara utakayokuwa umeanzisha. Wakati wenzako wanafanya mambo ya nje ya shule, wewe fanya yale ya biashara yako. Ila usiache kuhudhuria vipindi na wala usiache kujiandaa kwa ajili ya mitihani na kazi nyingine za kitaaluma.
SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Waalimu Wa Sanaa Na Kada Nyingine Zilizokosa Kipaumbele Kwenye Ajira Za Serikali. ( Kama Umesoma Na Huna Ajira, Pia Soma Hapa.)
Pili ufanye biashara gani? Najua hapa pia utachukulia kama sababu, lakini biashara zipo nyingi za kuanza kufanya. Kama huna mtaji kabisa, au mtaji wako ni kidogo, nakushauri jiunge na biashara ya mtandao (NETWORK MARKETING) na jifunze biashara hii kwa undani, kisha weka juhudi zako zote katika kuifanya. Zipo kampuni unaweza kuanza na mtaji kidogo mno, jiunge nazo na weka juhudi kubwa sana kuhakikisha unatengeneza mtandao mkubwa. Hii ni biashara ambayo inaweza kukupa mtaji wa kuingia kwenye biashara nyingine.
Kama una mtaji kidogo pia unaweza kuanza biashara ya kutoa mahitaji kwa wanafunzi wenzako hapo chuoni. Biashara ya vitu vidogo vidogo kama nguo, vocha na hata vifaa vya simu na kompyuta, unaweza kuanza nayo na kuikuza vizuri.
Unaweza pia kuanza kufanya biashara kwa kutumia mtandao wa intaneti. Hapo unatumia blogu na mitandao ya kijamii kufanya biashara kwa kusambaza bidhaa au huduma zako mwenyewe, au kutangaza biashara za wengine. Vipo vitu vingi unaweza kufanya kwa kuanzia hapo ulipo. Muhimu ni uache kufikiria huwezi na kujiuliza wapi unapoweza kuanzia.
Endelea na masomo yako na anza biashara. Maisha yatakuwa magumu zaidi, lakini utakuwa na matumaini ya kuelekea kwenye urahisi. Utalazimika kusahau starehe, utalazimika kukosa usingizi, utaonekana mshamba na huendi na wakati, hasa pale wanafunzi wenzako wanapokwenda kwenye mambo ya kijamii, wewe vumilia hayo, weka juhudi na miaka michache baada ya kumaliza chuo, huenda ukawaajiri wanaokucheka leo.
Nimefika mwisho lakini nilisahau kukuambia kwa nini nakuambia uendelee na chuo. Japo unajua labda huwezi kupata ajira, au huna mpango wa kuajiriwa. Zipo sababu nyingi lakini nakupa chache muhimu. Kwanza kabisa muda unaokimbia chuo ni muda mfupi, labda ni miaka mitatu au mitano. Pili pamoja na kupenda biashara, bado unahitaji kuwa na kitu ambacho unaweza kufanya, unahitaji kuwa na utaalamu au taaluma fulani, ambayo hata hapo baadaye unaweza kuigeuza kwa biashara. Na kingine cha mwisho, unahitaji kujijengea nidhamu, shuleni au chuoni ni sehemu nzuri ya kujifunza nidhamu, hasa ya kufanya mambo kwa wakati.
Hivyo, kwa vyovyote vile, kama umeshaanza chuo, kazana umalize, usiishie njiani. Chochote ambacho unajiambia unaacha chuo ukakifanye, anza kukifanya ukiwa chuoni. Utaona namna unavyowezekana kama kweli umejitoa kufanya.
Vitabu vya rejea.
Kwa kumaliza kabisa nakupa vitabu viwili vya rejea uvisome, ili uweze kufanyia kazi haya uliyojifunza leo;
Kitabu cha kwanza ni JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, kwenye kitabu hichi utajifunza kuanzisha blog yako na kuitumia kuingiza kipato. Gharama ya kitabu hichi ni tsh elfu 10.
Kitabu cha pili ni PATA MASAA MAWILI YA ZIADA, kwenye kitabu hichi utajifunza jinsi ya kupata masaa mawili na hata zaidi ya hayo kwa kupangilia vizuri siku yako. Hivyo utaweza kupata muda wa kufanya masomo au kazi na kuendelea kufanya biashara. Gharama ya kitabu hichi ni tsh elfu 5.
Kupata vitabu hivi, tuma fedha kwa namba 0755953887 au 0717396253 kisha tuma email yako kwenye moja ya namba hizo na utatumiwa kitabu kwenye email yako.
Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog