Siku za karibuni kumekuwa na habari mbaya kwa baadhi ya watu na habari nzuri kwa baadhi ya wengine kuhusiana na ajira. Habari mbaya imekuwa ni ile ya kufukuzwa kazi kwa waajiriwa ambao hawakuwa na vyeti halisi. Habari nzuri imekuwa ni tangazo la serikali kuajiri watumishi wengi. Pia wapo madaktari ambao walikuwa wameomba kwenda kufanya kazi nchini Kenya, ambao serikali imeamua kuwaajiri mara moja.
Wengi walioumia sana na kufukuzwa kazi kwa vyeti feki ni watu wazima, ambao wameshakaa kazini muda mrefu na wengine walikuwa wanakaribia kabisa kustaafu. Wengi ambao wananufaika na ajira mpya ni vijana, ambao wamehitimu masomo yao kwa kipindi kirefu lakini hawakuwa na ajira.
Leo, mimi rafiki yako, nimekuandalia barua ya wazi kwako wewe kijana ambaye umepata ajira mpya, au siku za karibuni utapata ajira. Katika barua hii nitakushirikisha shimo moja kubwa ambalo limekuwa linameza waajiriwa wengi, na wanapokuja kustuka, muda unakuwa umeenda na hakuna mabadiliko wanaweza kufanya.
Nimekuwa nakutana na vijana wengi kabla na wakati wanapoanza ajira, wanakuwa na mipango mikubwa na mizuri. Wanakuambia hawatakaa kwenye ajira muda mrefu, wataanza biashara zao mapema ili wasitegemee ajira. Lakini imekuwa haichukui hata mwaka ndani ya ajira zao, hadithi zinabadilika.
SOMA; Kwa Nini Watu Wengi Wanashindwa Kuacha Ajira Hata Kama Ni Ngumu Kwao Na Haziwalipi.
Siku siyo nyingi nimekutana na kijana aliyekuwa amepata kazi mahali, na miezi sita imepita, kila mwezi anapokea mshahara mzuri kulingana na mahitaji yake na anapoanzia, lakini alikiri mbele yangu kwamba hajui fedha inaenda wapi. Alinieleza namna ambavyo kila akipokea mshahara matumizi yanavyokuwa makubwa, na yote ni ya msingi kabisa. Hapa niliona anaanza kuingia kwenye shimo ninalokwenda kuwashauri hapa leo. Kwa sababu hiyo ni miezi sita pekee, na bado hajawa na familia.
Tatizo kwenye elimu na malezi yetu.
Kusoma tumesoma sana, karibu miaka 20 ya maisha yetu tumeitumia darasani. Lakini elimu ya msingi kabisa kuhusu fedha, hatujapatiwa. Tulichofundishwa ni namna ya kutafuta fedha, kwa kufundishwa taaluma inayotupa kazi. Lakini zaidi ya hapo hakuna. Namna ya kudhibiti matumizi, namna ya kuweka akiba, namna ya kuwekeza ni elimu ambayo hatujaipata darasani.
Kama tumekosa elimu hii darasani, ingesaidia sana kama tungeipata kwenye familia na kwenye jamii. Lakini napo pia hatuipati. Hivyo tunapozipokea fedha zetu, hatuna wazo tunapaswa kufanya nini. Na hivyo tunajikuta tunazitumia kwa jambo lolote ambalo limejitokeza mbele yetu. Kitu kimoja kizuri kuhusu fedha ni kwamba, huwa haikosi matumizi, kama fedha ipo, itapata matumizi tu. Ndiyo maana mtu anaweza kukuambia hajui fedha yake inaenda wapi, siyo kwamba anakutania, anakuambia ukweli, kwa sababu hana mpango wowote anaouishi.
Shimo kubwa la kuepuka kwenye ajira.
Shimo kubwa sana ambalo nakusihi wewe rafiki yangu uepuke kuliingia, ni kutumia fedha kama unavyoipata.
Tujikumbushe mzunguko wa fedha wa mwajiriwa ndani ya mwezi mmoja. Mwisho wa mwezi, mwajiriwa anapokea mshahara wake. Japokuwa atawekewa benki, atakwenda kuutoa karibu wote na kuanza matumizi yake, ambayo anayaita muhimu, japo siyo yote.
Mpaka kufika tarehe 15 ya mwezi unaofuata, mwajiriwa huyu anakuwa ameshamaliza mshahara wake wote. Lakini maisha lazima yaendelee, na mshahara hautatoka mpaka tena mwisho wa mwezi. Hivyo anakopa, ili aweze kusukuma siku. Anapewa mkopo, labda wa vitu au wa fedha, lakini atalazimika kulipa kwa riba. Mwisho wa mwezi unafika, anapokea tena mshahara wake, anautoa, anaenda kulipa madeni, anabaki na kiasi kidogo, anakitumia tena, hakimfikishi mbali kinaisha, anarudi tena kukopa. Mzunguko unakuwa ni huu, mara 12 kwa mwaka na kwa miaka ya kutosha tu. Hapo bado hajapata wazo la kuwa na gari au nyumba na benki wakamwambia unakopesheka. Anakuwa na deni kubwa la benki, ambalo anakatwa kila mwezi, na bado ana madeni madogo madogo ya mitaani. Ah! Hapo bado hajawa na familia, watoto wakahitaji ada za shule na mahitaji mengine.
SOMA; Hizi Ndio Mbinu Anazutumia Mwajiri Wako Kuhakikisha Unaendelea Kuwa Mtumwa Wake.
Hili ni shimo ambalo limemeza ndoto za watu wengi mno. Ukimsikiliza mtu pale anapoanza kazi, na ukaja kukutana naye miaka mitano au kumi kwenye kazi, unaona namna gani alivyozika ndoto nyingi. Anakuwa hana namna tena, mambo yamemwelemea na analazimika kwenda kama mambo yanavyokwenda. Baadaye wengi wakishaona hawawezi kuondoka kwenye shimo, imani pekee inabaki kwamba wakistaafu na kupata mafao, ndipo wataanza kuishi ndoto zao. Huko nako kunakuwa na changamoto kubwa zaidi.
Kuepuka shimo hili rafiki yangu, huna budi kujijengea nidhamu ya fedha. Unahitaji kuwa makini sana na fedha zako, usiendeshe maisha kwa mazoea hata kidogo. Kwenye kila kipato unachopata, kuanzia mshahara wako wa kwanza kabisa, weka kiasi kidogo pembeni. Tena wewe ambaye ni mwajiriwa mpya, ningekushauri ufungue akaunti mpya ya benki, ukiacha ile unayotumia na ambayo mshahara utakuwa unaingia. Ukifungua kwenye benki moja, unaweza kuwaomba wawe wanakata kiasi fulani kila mwezi kwenye akaunti yako ya mshahara kwenda akaunti mpya uliyofungua. Hii itakusaidia kujenga nidhamu ya kuwa na akiba na kuweka sehemu ya kipato chako pembeni.
Wakati huo unajijengea nidhamu ya fedha, hakikisha pia unaendelea kutafiti biashara unazoweza kufanya ukiwa kwenye ajira yako, na hata uwekezaji ambao unaweza kufanya.
Ninachotaka hapa ni wewe usiwe unategemea kipato kimoja tu cha ajira. Kwa sababu sasa hivi kinaweza kuwa kinakutosha, lakini kumbuka mahitaji yanaongezeka, utakuwa na familia, utahitaji nyumba, utahitaji gari, yote hayo huwezi kuyahudumia na kipato cha mshahara pekee.
Jijengee nidhamu ya fedha, kwa kuhakikisha unaweka sehemu ya kipato chako pembeni na pia tafuta njia za kukuza zaidi kipato chako. Haya ndiyo muhimu sana napenda wewe rafiki yangu uongoke nayo kwenye barua hii ya leo.
MUHIMU ZAIDI nakushauri usome kitabu kinaitwa BIASHARA NDANI YA AJIRA, hakuna wakati sahihi kwako kuanza biashara kama ukiwa kwenye ajira. Hichi ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma. Kipate na ukisome, kitakupa mwanga sana juu ya biashara gani ufanye, upateje mtaji, utumieje muda wako vizuri na pia mifereji nane ya kipato unayopaswa kuwa nayo. Kupata kitabu hichi tuwasiliane kwa simu 0717396253.
Karibu sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.