Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

USHAURI; Mambo Ya Kufanya Pale Matumizi Yanapokuwa Makubwa Kuliko Mapato.

$
0
0

Hesabu zote za fedha binafsi zinaishia kwenye mambo mawili makuu; mapato na matumizi. Mapato yanajumuisha vyanzo vyote vya fedha ulivyonavyo na matumizi yanajumuisha kila kitu ambacho kinategemea au kutumia fedha zako.

100_7560 ED1

Ili kufikia uhuru wa kifedha na kuweza kuwa tajiri ni muhimu sana kipato chako kikazidi matumizi. Kwa bahati mbaya mambo hayako hivi kwa watanzania walio wengi. Watanzania wengi matumizi yao ni makubwa kuliko mapato na hapa ndiko matatizo yote ya fedha yanapoanzia.

Leo tutashauriana mambo muhimu ya kufanya ili kuondoka kwenye shimo hili la matumizi makubwa kuliko mapato. Kabla hatujaingia kwenye mambo hayo tuone kile ambacho msomaji mwenzetu ametuandikia.

Changamoto inayonikabili ni kujikuta nina mzigo wa madeni kila kukicha. Matumizi yangu ya lazima ni makubwa kuliko kipato changu cha mwezi. Mfano: Nina duka la spea za pikipiki ambalo huniingizia kati ya Tsh 50,000 hadi 100,000 kwa mwezi na ninafanya kazi ya kujitolea kwenye taasisi moja ambako hupata pia kati ya Tsh 50,000 hadi 100,000. Matumizi: Chakula (nyumbani) 150,000/ na (kazini) 60,000/,Nauli 24,000/, Ada ya mtoto 60,000/, Viburudisho(mtoto) 15,000/, Utilities 40,000/, House Girl 30,000/, Other charges 50,000/. Je, nifanyeje kukabiliana na hali hii?

Kuna mambo mengi sana unaweza kuyafanya kukabiliana na hali hii.  Hapa tutajadili mambo matatu ya muhimu kuanza nayo ili kuweza kuondokana na tatizo hili la matumizi kuzidi mapato na hatimaye kufikia uhuru wa kifedha.

1. Yajue mapato yako yote na matumizi yako yote.

Ni muhimu sana kujua ni kiasi gani unapata na ni kiasi gani unatumia. Mwenzetu hapa ameshatuambia kipato anachopata na pia ametupa baadhi ya matumizi. Ila matumizi aliyotupa hayajakamilika, na ili kuyakamilisha fanya hivi; Tafuta kijitabu maalumu ambapo utaandika mambo haya. Katika kitabu hiki andika matumizi yako yote ya kwenye maisha yako ya kawaida. Usiyaandike kama ulivyotuandikia hapa, bali andika kila fedha unayoitumia na unaitumia wapi. Kwa mfano kwenye other charges ni vyema ukaandika fedha hiyo inakwenda wapi kwa uhakika zaidi.

Sehemu nyingine kwenye kijitabu hiki andika matumizi na gharama zote za kuendesha biashara yako. Andika gharama zote unazotumia kwenye biashara.

Baada ya kuandika haya angalia ni vitu gani kwenye orodha ya matumizi yako unaweza kuviondoa, kuvipunguza aua kutafuta mbadala kwa gharama ndogo. Kwa vyovyote vile kuna baadhi ya matumizi ambayo unaweza kuyapunguza na maisha yako yakaendelea kuwa vizuri. Jua ni matumizi yapi na anza kuyafanyia kazi.

2. Ongeza kipato chako.

Baada ya kufanya hatua hiyo hapo juu sasa unakwenda hatua nyingine muhimu ambayo ni kuongeza kipato chako. Hapa ndipo unapohitajika kufungua macho na kuona fursa zaidi zinazopatikana maeneo unayoishi, kazi unayofanya au biashara unayofanya ambazo unaweza kutumia kuongeza kipato chako.

TAHADHARI; Usifanye hatua hii kama hujafanya hatua ya kwanza hapo juu kwa sababu hali yako itazidi kuwa mbaya kama utaongeza kipato bila kudhibiti matumizi yako.

Kwa mfano kwa ndugu yetu hapa tayari ana biashara ya duka la spea za pikipiki na ametuambia anapata shilingi elfu hamsini mpaka laki moja kwa mwezi. Hapo ni sawa na wastani wa shilingi elfu mbili mpaka tatu kwa siku. Sijajua ukubwa wa duka hilo au mtaji uliowekeza ila nina uhakika kipato unachopata kwenye biashara hii ni kidogo sana. Nakushauri uanze kulifanyia hili kazi na uone ni jinsi gani unaweza kuongeza faida kwenye biashara yako napia ni jinsi gani unaweza kupunguza gharama za biashara hiyo.

Inawezekana huna usimamizi wa kutosha kwenye biashara yako(soma; Jinsi Unavyoweza Kufanya Biashara Yenye Mafanikio Ukiwa Bado Umeajiriwa.), inawezekana unatumia gharama nyingi ambazo sio muhimu na pia inawezekana hufanyi mbinu zozote kukuza biashara hii. Yote hayo yanaweza kuwa yanakurudisha nyuma ila kwa kuwa hujataka kuyajua unaendelea na maisha magumu.

3. Usikope kwa ajili ya matumizi.

Matumizi yanapokuwa makubwa zaidi ya mapato kitu cha kwanza unachokimbilia kufanya ni kukopa ili uweze kukamilisha matumizi yako. Hili ndio kosa kubwa sana ambalo linakuingiza kwenye mbio za panya. Unapoanza kukopa kwa ajili ya matumizi inakuwia vigumu sana kuondoka kwenye mikopo hii kwa sababu hujatatua tatizo la msingi, hivyo unapopata mkopo unaupeleka kule kule kwenye matumizi ambayo hujaweza kuyadhibiti.

Unapokuwa na matumizi makubwa zaidia ya mapato kwanza kabisa fanya hatua ya kwanza na ya pili hapo juu kisha USIKOPE. Fanya chochote utakachofanya, lala njaa, uza unachomiliki au vinginevyo ila USIKOPE kwa ajili ya matumizi.

Watu wengi wanapoanza kuchukua mikopo kwa ajili ya matumizi wanajikuta wanatumia muda mwingi wa maisha yao kuchukua na kulipa mikopo hivyo kushindwa kufikia uhuru wa kifedha na kufurahia maisha yao.

Hesabu za fedha ni rahisi sana kwenye mipango ila inapokuja kwenye uhalisia ni ngumu sana. Na hii inatokana na tabia mbaya tulizojengewa kuhusu matumizi ya fedha. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA mwezi huu wa saba na wa nane tunajadili jinsi ya kujenga tabia ya kuwa na matumizi mazuri ya fedha ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo ili uweze kupata elimu hii ambayo italeta mapinduzi ya kifikra kwenye maisha yako. Kujiunga tuma tsh elfu kumi kwenye mamba 0717396253/0755953887 na kisha tuma email yako ya gmail na utaunganishwa kwenye KISIMA. Wahi nafasi hii ya kipekee.

Nakutakia kila la kheri katika harakati zako za kufikia uhuru wa kifedha.

TUKO PAMOJA.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.

kitabu-kava-tangazo432

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>