Habari za leo msomaji wa AMKA MTANZANIA, natumaini unaendelea vizuri na mipango yako ya kuboresha maisha yako. AMKA MTANZANIA iko nawe bega kwa bega kuhakikisha unafikia mafanikio unayostahili kwenye maisha yako.
Katika utaratibu wa kujisomea vitabu leo utapata kitabu kizuri sana cha kujisomea ambacho kitakupa mwanga wa kuelekea kwenye mafanikio.
Kitabu hiki kinaelezea siri 21 za mafanikio za mamilionea waliojitengeneza.
Tunaposema mamilionea waliojitengeneza inamaanisha watu walioanza chini kabisa bila ya kuwa na kitu chochote ila wakafanya kazi kwa juhudi na maarifa na hatimaye wakifikia kuwa mamilionea. Tunasema wamejitengeneza kwa sababu wanakuwa hawajapata msaada mkubwa mwanzoni, tofauti na wengine ambao walirithi mali za wazazi au kupata msaada wa aina nyingine.
Kama na wewe ni mmoja wa watu ambao huna msaada wa aina yoyote na maisha yako bado ni magumu sana nataka nikuambie leo kwamba yanaweza kubadilika na kuwa bora kama ukiamua. Nasema kama ukiamua kwa sababu bila ya kuamua hakuna kitakachobadilika.
Utakapoamua na kujifunza vile ambavyo waliofanikiwa wanavifanya bila shaka na wewe utafanikiwa. Mpaka sasa maisha yako ni magumu kwa sababu hujafanya juhudi kubwa ya kuyafanya yasiwe magumu.
Unafanya mambo ambayo watu wenye maisha magumu wanafanya ha hivyo unaendelea kuwa na maisha magumu.
Kitabu hiki, The 21 Success Secrets of Self Made Millionaires kilichoandikwa na Brian Tracy kimeeleza kwa kina sana mambo ishirini na moja ambayo kama ukianza kuyafanya sasa utapata mafaniko makubwa sana sio kifedha tu bali kwenye kila nyanja ya maisha yako.
Nakusihi usome kitabu hiki na uanze kutekeleza yale uliyojifunza kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Kwa kufanya hivi utaanza kuona mabadiliko makubwa.
Kitabu hiki ni kifupi sana na kimeandikwa kwa ligha rahisi sana ya kiingereza. Hivyo unaweza kukisoma ndani ya masaa mawili au matatu ukawa umekimalia. Kisome na ukishakimaliza kirudie tena na tena mpaka vile vitu viwe kwenye akili yako.
Kupata kitabu The 21 Success Secrets of Self Made Millionaires bonyeza hayo maandishi ya jina la kitabu na utakipakua(download).
Kumbuka kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kama bado hujafanya hivyo. Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kila siku utakuwa unapata makala nzuri ya kukuelimisha na kukuhamisisha wewe ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Pia utakuwa unapata uchambuzi wa vitabu hivi vizuri kwa lugha ya kiswahili. Yote haya yataanza mwezi wa nane na yakishaanza gharama za kujiunga na kisima cha maarifa zitaongezeka.
Chukua hatua ya kujiunga leo kwa kutuma fedha tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha utume email yako kwenye moja ya namba hizo na utaunganishwa na kisima cha maarifa.
Kumbuka kujifunza kila siku ndio hitaji la chini sana ili kufanikiwa(continuous learning is minimum requirement for success). Pata nafasi ya kujifunza kila siku kupitia KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kufikia mafanikio kwenye maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kuboresha maisha yako.
TUKO PAMOJA.
OMBI; TUMA MAKALA HII KWA MARAFIKI ZAKO KWA KUSHARE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA EMAIL ILI NAO WAPATE MAMBO HAYA MAZURI.