Katika kitu kimoja ambacho tunaweza kuwa na uhakika nacho ni kwamba mabadiliko lazima yatokee. Hakuna kitu kitakachoendelea kubaki kama kilivyokuwa. Kila kitu kinabadilika na kwa bahati mbaya sana mabadiliko yanatokea kwa kasi kubwa.
Kwa bahati mbaya pia binadamu ni viumbe ambao hatupendi mabadiliko. Tunapenda kuendelea kufanya kile ambacho tumeozea kufanya na tuendelee kupata matokeo ambayo tumezoea kupata. Tunatamani mambo yaendelee kuwa kama yalivyo sasa ila hayawezekani. Kama tulivyoona japo mwanzo mabadiliko ni lazima yatokee na mbaya zaidi hayakusubiri wewe uwe tayari ndio yatokee.
Aina tatu za watu wanaozalishwa na mabadiliko.
Kulingana na utayari na maandalizi ya watu kuhusu mabadiliko, mabadiliko yoyote yanapotokea yanazalisha watu wa aina tatu.
Aina ya kwanza ni watu ambao wananufaika na mabadiliko yanayotokea. Hawa ni watu ambao walijua kwmaba mabadiliko yanakuja na hivyo kujiandaa vyema kwa ajili ya kupokea mabadiliko hayo. Hawa ni watu ambao ni viongozi katika kile wanachofanya na wanajua kila kitu kinachoendelea katika hiko wanachofanya, iwe ni kazi au biashara.
Sifa moja kubwa ya watu hawa ni kwmaba wanapenda sana kile ambacho wanafanya. Na pia kuna sifa nyingine za watu hawa ambazo utaweza kujifunza kwenye kitabu nitakachokushirikisha hapo chini.
Aina ya pili ya watu ni wale ambao wanaamshwa na mabadiliko. Watu hawa wanakuwa hawana habari kwamba kuna mabadiliko yanayokuja. Ila mabadiliko yanapotokea wanakiuwa tayari kubadilika. Kutegemea na muda waliobadilika, watu wa kundi hili wanaweza kunufaika na mabadiliko yanayotokea au la.
Sifa moja kubwa ya watu wa kundi hili ni kwmaba wanafanya kile wanachofanya kwa mazoea. Kama ni kazi wanafanya kile ambacho wameambiwa wafanye na hawakwendi hatua ya ziada. Kama ni biashara wanafanya kile ambacho wamezoea kufanya kila siku na hawaweki kingine chochote. Utajifunza sifa nyingine za kundi hili kwenye kitabu nitakachokushirikisha hapo chini.
Aina ya tatu ya watu ni wale ambao wanaachwa nyuma na mabadiliko. Hawa ni watu ambao wamegoma kabisa kubadilika. Watu hawa licha ya kuona mabadiliko bado wanaendele akung’ang’ania kile ambacho wamezoea kufanya kila siku kwenye maisha yao. Kama ni wafanyakazi wataendela kufanya kile ambacho walifanya miaka kumi iliyopita na kuendelea kupata majibu yale yale. Kama ni wafanyabiashara wataendelea kufanya biashara waliyokuwa wanafanya na kwa mtindo ule ule.
Sifa moja kubwa ya watu hawa wanakuwa ni watu wanaopenda sana kile wanachofanya kiasi kwmaba hawaoni kama wanawez akufanya kitu kingine. Pia wanaweza kuwa watu ambao hawapendi kile wanachofanya kiasi kwamba hawaoni umuhimu wa kufanya mabadiliko. Utajifunza sifa nyingine za kundi hili kwenye kitabu ambacho utakwend akukipata hivi punde.
Wewe upo kundi gani katika makundi haya matatu?
Kundi la kwanza wananufaika sana na mabadiliko, hawa ndio wanaopata faida kubwa na kuwaamsha wale ambao walikuwa hawajui nini kinaendelea. Kundi hili lina watu wachache.
Kundi la pili wanaweza kunufaika wa wasinufaike, hii inategemea ni muda gani ambapo wamechukua hatua. Wakichukua hatua mapema wananufaika na wakichelewa wanapotea. Kundi hili lina watu wengi sana na kuna uwezekano mkubwa upo hapa na kibaya zaidi unaweza kuwa kati ya wale ambao wanastuka wakati ambao hawawezi kunufaika tena na mabadiliko yaliyokwisha tokea.
Kundi la tatu wanaachwa nyuma na mabadiliko, kutokana na kugoma kwao wanajikuta kwenye wakati ambao kile wanachofanya hakina thamani tena na hivyo kupoteza kabisa. Kundi hili lina watu wachache pia na mara nyingi ni watu ambao umri wao umekwenda kiasi na wamefanya kitu hiko kwa miaka mingi. Kundi hili lina changamoto zake kubwa sana.
Unaweza usielewe vizuri upo kwenye kundi lipi, lakini utakapopata kitabu nitakachokushirikisha hapo chini utaelewa kw auwazi kabisa upo upande upi.
Je ungependa kuwa kwenye kundi la kwanza? Ungependa kuwa wa kwanza kuyanusa mabadiliko na kunufaika zaidi? Je umechoshwa na kauli kwmaba biashara fulani inalipa ila unapokwend akuifanya kila mtu anakuwa ameshaifanya? Nina jibu la maswali yako.
Kama unapenda kuwa wa kwanza kunusa mabadiliko, kama unapenda kunufaika zaidi na mabadiliko yanayotokea na kama unapenda kuwa wa kwanza kuingia kwenye biashara ambazo baadae zitalipa basi una kitu kimoja cha kufanya kabla siku ya leo haijaisha. Kitu hiko muhimu ni kusoma kitabu; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA. Katika kitabu hiki utajifunza mbinu nyingi sana za kukuweka kwenye kundi la kwanza ambalo ni watu wanaoyaona mabadiliko kabla hata hayajafika.
Jipatie kitabu hiki leo na uanze kujifunza mambo haya muhimu. Kitabu hiki kinapatikana kwa soft copy, yaani pdf na kinatumwa kwa email. Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano. Kukipata kitabu, tuma fedha tsh elfu tano kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu mara moja.
Kama upo makini na maisha yako, na kama unataka kufanikiwa basi unahitaji kukisoma kitabu hiki mapema sana kabla siku ya leo haijaisha. Hii ni kwa sababu wakati unasoma hapa mabadiliko yanaendele akutokea. Hivyo kama utasema nasubiri kesho, utakuta umeshapitwa tayari. Mambo yote ni leo, pata kitabu chako na uanze kujiandaa na mabadiliko ambayo ni lazima yatokee.
Nakutakia kila la kheri katika kutumia vizuri mabadiliko yanayoendelea kutokea.
TUPO PAMOJA.