Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

KITABU; The Compound Effect(Jinsi Ya Kuboresha Maisha Yako Kidogo Kidogo)

$
0
0

Katika utaratibu wetu wa kushirikishana kitabu kila mwezi, mwezi huu wa tatu nawashirikisha kitabu THE COMPOUND EFFECT. Hiki ni kitabu ambacho kimeandikwa na Darren Hardy ambaye pia ni mhariri wa jarida kubwa la mafanikio(SUCCESS magazine).

compound effect

Katika kitabu hiki Darren ameeleza mbinu mbali mbali ambazo zitakuwezesha kuboresha maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.

Kama jina lilivyo, yaani compound effect, mwandishi anatukumbusha kwamba kitu chochote ambacho utakifanya kidogo kidogo kila siku baadae kinakuwa kikubwa sana.

SOMA; Hii Ndio Hatari Kubwa Ya Zama Hizi Tunazoishi..

Kwa mfano kama utaanza kula vyakula ambavyo sio vya afya kidogo kidogo kila siku, hutaona mabadiliko ndani ya mwaka mmoja, au hata miwili. Ila miaka mingi baadae utaanza kuona afya yako ikiwa mbovu na hatimaye kujikuta kwenye matatizo makubwa sana ya kiafya.

Vile vile kama utaanza kuweka akiba leo, kidogo kidogo na fedha hii ukaiweka mahali ambapo inaweza kukupatia riba ya asilimia 10 kwa mwaka, kwenye miaka ya mwanzo hutaona tofauti kubwa, ila miaka 20 au 30 baadae fedha hiyo itakuwa imeongezeka sana na kukupatia uhuru wa kifedha.

compound effect 2

Mwandishi anatuambia kwamba machaguo tunayofanya kila siku, yawe mazuri au mabaya yana madhara kwenye maisha yetu. Hata kama kitu unachofanya ni kidogo kiasi gani, kama utakifanya kila siku kinaendelea kujijenga na baadae kinakuwa na madhara sana, inaweza kuwa kukusaidia ufanikiwe au kukuzuia ufanikiwe.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Pia mwandishi amejadili sana kuhusu tabia na zinavyoweza kuathiri mafanikio yetu. Ameeleza jinsi tabia tunavyozijenga kwa mambo madogo madogo tunayofanya kila siku na baadae tabia hizi zinakomaa na hatuwezi tena kuondokana nazo. Yaani unajenga tabia halafu baadae tabia zinakujenga. Ameelezea njia za kuweza kuondokana na tabia yoyote mbaya, na kwa kuwa kuondokana na tabia mbaya ni kugumu, mwandishi ametoa mbinu nzuri ambazo kama ukizifuata basi unaweza kuachana na tabia yote ambayo inakurudisha nyuma. Hata kama ni ulevi uliopindukia.

Mwandishi pia amegusia jinsi ya kujenga tabia nzuri ambazo zitakuletea mafanikio makubwa sana baadae.

Katika sura nyingine mwandishi amezungumzia vishawishi mbalimbali ambavyo vinaturudisha nyuma licha ya kuwa na mipango mizuri ya kuboresha maisha yetu. Amezungumzia sana nafasi ya watu wanaokuzunguka katika kukurudisha nyuma na hata vyombo vya habari katika kukupa ahabari ambazo ni mbaya tu na wewe kuona dunia ni sehemu mbaya sana. Habari hizi unazosikia kila siku zina madhara makubwa sana kwako. Mwandishi ametoa ushauri mzuri sana ambao kama utaufuata utaondokana na vishawishi hivi vinavyokurudisha nyuma kila siku.

SOMA; UKURASA WA 71; Angalia Nyuma Kwa Lengo Moja Tu…

Mwishoni mwandishi amemalizia na kitu ambacho kitakuwezesha kufikia malengo na mipango yako haraka zaidi kuliko unavyofikiri. Mwandishi ametoa mbinu moja ambayo itakuwezesha kuwa mbele ya wengine wote wanaofanya kile unachofanya. Iwe ni kwenye kazi au biashara, hutakiwi kuikosa mbinu hii moja ambayo itakutoa popote ulipo na kukufikisha juu zaidi.

Nachoweza kukuambia ni soma kitabu hiki, kisome na fanyia kazi yale yaliyopendekezwa na maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa.

Tenga muda mchache na soma kitabu hiki, hakuna utakachopoteza, na utapata mengi sana ambayo hujawahi kufundishwa shuleni na hata wanaokuzunguka hawayafahamu.

Nakusihi tena soma kitabu hiki, hata kama utasoma kurasa tano tu kila siku, utaanza kuona kile kinachojadiliwa kwenye kitabu hiki kikitokea kwenye maisha yako.

Kupata kitabu THE COMPOUND EFFECT bonyeza hayo maandishi na utakipakua.

Nakutakia kila la kheri katika kuboresha maisha yako. Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambapo utajifunz amengi zaidi.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4322


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>