Ipo siku utaangalia nyuma na kiitazama siku hii ya leo na utajishangaa sana, kwa nini hukuchukua hatua mapema na ukakubali kujazwa na hofu zisizo na msingi.
Ipo siku utaangalia nyuma na kiitazama siku hii ya leo, nakujishangaa tena sana kwa nini ulipoteza muda kwa mambo ya hovyo yasiyoeleweka.
Ipo siku utaangalia nyuma na kiitazama siku hii ya leo, na kustaajabu kwa nini hukuweka nidhamu binafsi kwa mambo ambayo yangekuwa msaada kwako leo sana.
Ipo siku utaangalia nyuma na kuitazama siku hii ya leo na kushangaa kwa nini ulikuwa unafanya mambo yako kwa kulipua badala ya kuweka nguvu za uzingativu pamoja.
Kile ambacho hukifanyi leo, miaka kumi ijayo upo uwezekano mkubwa sana wewe kujuta na kujilaumu kwa nini hukufanya.
Kuna mambo au fursa unaweza ukawa unazichukulia sana poa leo, lakini fursa hizo zikikupita, ipo siku utakumbuka nyakati hiza za leo za taarifa.
Fursa ipi leo ambayo ni muhimu kwako na unaona inaweza kukusaidia? Kama fursa hiyo unayo leo, hebu ifanye ili baadae yasiwe majuto kwako.
Maisha yenye thamani, yanakuja kwa kujengwa siku hadi siku, na sio maisha ya bahati nasibu, jenga maisha yako leo kuepuka majuto yasiyo na maana kesho.
Leo ni siku nzuri ya kujenga maisha yako ya kesho kuliko siku yoyote ile, usiipoteze siku hii ya leo kwa kufanya upuuzi na kujikuta ukijuta kwa kesho.
Pamoja na kwamba huwezi kujua kesho yako iko vipi, lakini unayo kila sababu ya kufanya kila siku yako kuwa bora sana.
Ukiweka mikakati ya kufanya siku yako kuwa bora kila siku na ukaamua usipoteze kitu chochote, miaka kumi ijayo utakuwa ni mtu mwingine kabisa katika maisha yako.
Nini unachongoja sasa kuweza kuchukua hatua na kufanya maisha yako kuwa bora kabisa? usingoje ikafika siku ikaifanya leo ikawa siku ya majuto kwako.
Kumbuka leo ni siku bora ambayo yenye kila fursa ya kukupa mafanikio yako makubwa. Itumie vyema siku ya leo kwa manufaa yako ya kesho.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Tovuti; www.amkamtanzania.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Barua pepe; dirayamafanikio@gmail.com