Habari za leo rafiki?
Kama umekuwa unasoma makala zangu kwa muda, na hata kuangalia video ninazotengeneza, utakuwa umesoma au kusikia nikisema hili mara nyingi, kwamba tunaishi kwenye zama mpya, zama ambazo kila mtu anapaswa kuutumia mtandao wa intaneti kwenye shughuli zake za kila siku.
Nimekuwa naandika kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti, na nimetoa kitabu ambacho kinawaelekeza watu jinsi ya kuanzisha blog zao wenyewe na kuweza kuzigeuza kuwa sehemu ya kujitengenezea kipato.
Nimekuwa pia naona watu wengi wanaanzisha blog lakini hawafiki mbali. Wanaanza kwa lengo la kuzitumia kutengeneza kipato, lakini hawachukui muda kabla ya kuachana na blog hizo. Kipato walichokuwa wanategemea hawakipati na kukata tamaa kabisa.
Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu sana wa mambo yote yanayohusu intaneti, hasa eneo la kutengeneza biashara na kitu kimoja ambacho nimejifunza na naona wengi wanakikwepa ni msingi muhimu sana wa kuweza kutumia mtandao wa intaneti vizuri.
Upo msingi mmoja muhimu sana, ambao mtu yeyote anayetaka kutumia mtandao wa intaneti kwa manufaa, iwe ni kutengeneza kipato au kuutumia kukuza biashara au kazi yake, anapaswa kuujua na kuusimamia. Msingi huu ndiyo unaowatenganisha wanaofanikiwa kwenye mtandao wa intaneti na wale ambao wanashindwa.
Kwenye kipindi cha leo cha VIDEO nimekueleza msingi huu muhimu na jinsi unavyoweza kuujenga kwenye biashara zako za mtandao wa intaneti.
Nakusihi sana rafiki yangu uangalie kipindi hichi, kwa sababu utajifunza vitu ambavyo nimejifunza kwa uzoefu, kwa makosa niliyokuwa nafanya mimi, na makosa ambayo naona wengi wanayafanya na yanawagharimu.
Kama una blog angalia kipindi hichi, kama pia huna blog angalia kwa sababu kuna mengi unayakosa kama bado hujaanza kutumia mtandao wa intaneti kibiashara.
Angalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kukiangalia moja kwa moja hapo chini kwa kubonyeza.
Kwa uhitaji wa ushauri wa karibu kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao, kuhusu kuanzisha blog yako na kuweza kuikuza, wasiliana na mimi kwa njia ya wasap 0717396253.
Pia unaweza kujipatia kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, maelekezo ya kukipata yapo kwenye picha hapo chini.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.