Habari za leo rafiki?
Kama ulilipia kujiunga na semina, na mpaka sasa haupo kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA, tuwasiliane mara moja kwa simu 0717396253, semina inaanza, usikose.
Karibu kwenye makala yetu ya leo ambapo mimi rafiki yako, nitakwenda kukushirikisha dakika 30 ambazo zitakuwa muhimu sana kwako kwa mwaka huu 2017.
Kwa taarifa tu, ambazo najua unazijua, lakini siyo mbaya kama nitarudia hapa, tumeshatafuna nusu ya kwanza ya mwaka 2017. Na sasa tumeanza nusu nyingine ya mwaka huu. Kama unakumbuka vizuri, siyo siku nyingi sana tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, tukijiambia mwaka 2017 utakuwa wa kipekee na wa tofauti sana. Hili ndiyo natumaini linaendelea kwako.
Mwaka ni kipimo cha muda ambacho kina miezi 12, wiki 52, siku 365 au 366. Ni kipindi kizuri cha kupima maisha yetu kwa kule tunapotoka na kule ambapo tunaenda. Lakini cha kushangaza sana ni kwamba wengi wamekuwa wanausahau mwaka, na kukumbuka mwaka mpya tu.
Ukitaka kuhakikisha hili wewe angalia tu mwanzo, jinsi ambavyo watu wengi wanakuwa na mikakati mikubwa na mizuri, ukiisikiliza unaona kabisa namna ambavyo maisha yao yanakwenda kuwa makubwa. Lakini rudi kwa watu hao hao mwezi mmoja baadaye, na waambie kile ambacho walisema wao, watakushangaa. Wengi wanakuwa wamesahau na wanaendelea na maisha yao, kama walivyozoea.
Hapo sasa ndipo mimi rafiki yako huwa sipapendi. Sipapendi kwa sababu ni njia ambayo wengi wanachagua kupoteza muda na maisha yao. Kwa sababu watu huwa wanaendesha maisha yao hivyo, wengine wakiona kesho ipi au miaka bado ipo, wanakuja kustuka umri umeenda, kazi imeisha au hawana tena nguvu za kufanya walichokuwa wanafanya kama mwanzo. Hapo ndipo maisha yanakuwa magumu sana, na kuanza kuangalia nani alaumiwe.
Ili kuzuia hilo rafiki, leo nataka utenge nusu saa ya muda wako. Muda mfupi sana kwenye mwaka wako mzima, lakini utakuwa na matokeo makubwa sana kwako.
Kwenye nusu saa hii kuwa kwenye eneo tulivu kabisa. Kaa mbali na watu wengine, kaa mbali na simu yako, tena izime kabisa. Kumbuka ni nusu saa tu, hivyo usiniambie kutatokea dharura, maana dharura ambayo haiwezi kusubiri nusu saa, hakuna chochote unaweza kufanya kuisaidia.
Hivyo tafuta mahali unaweza kujifungia kabisa, na wala watu wasijue kama upo. Kama huna eneo kama hilo basi nenda eneo tulivu, labda ufukwe wa bahari, au eneo la mapumziko, popote ambapo kwa nusu saa, hakuna atakayekusemesha.
Huu ni muda muhimu sana kwa sababu utakwenda kufanya mkutano na mtu muhimu mno kwenye maisha yako, mtu ambaye ni wewe mwenyewe. Hivyo heshimu sana mkutano huu na ufanye ukiwa na utulivu.
Tatizo la malengo.
Tatizo la kuweka malengo mwanzo wa mwaka ni kwamba, mara nyingi malengo yetu yanakuwa machafu. Machafu nikiwa na maana kwamba yanakuwa hatujayafikiria kwa kina. Tunayaweka kwa mhemko, kwa sababu kila mtu anaweka malengo basi tunaona na sisi ni lazima tuweke. Kibaya zaidi, tunakuwa tumeweka malengo kwa kubashiri, kitu ambacho hatuwezi kupatia kwa sababu hatujui nini kinatokea kesho. Nina hakika kama mwezi wa kwanza uliweka malengo, kuna mambo yameshatokea hapo katikati ambayo hukuyategemea kabisa kama yangetokea.
Sasa unalokwenda kufanya kwenye dakika hizi 30, litakwenda kuvunja kabisa changamoto hiyo ya malengo, ambayo huenda umeweka miaka na miaka lakini huoni ukipiga hatua.
Tengeneza maono ya maisha yako.
Dakika 30 unazotenga leo, ni za kutengeneza maono au ndoto kubwa ya maisha yako. Na kama tayari ulishaitengeneza, basi unaipitia na kuiboresha zaidi. Hili ni jambo muhimu sana sana sana, yaani maono yatakusukuma kuliko yale malengo ya kudakia, kwa sababu wengine wameweka malengo basi na wewe uweke.
Maono ya maisha yako ndiyo ramani ya maisha, ndiyo msingi wa maisha yako ya mafanikio. Maono ndiyo yanakusukuma ufanye nini au kukuzuia usifanye nini. Maono ya maisha yako ndiyo maisha yako halisi, bila maono, maisha hupotea.
Sasa maono hayaigwi, wala hayana kuomba msaada wa mtu kukuelekeza. Kwa kifupi hichi ni kitu kutoka ndani yako, ambacho tayari kipo, lakini wewe umekuwa unakificha, umekuwa unakididimiza ili kisikusumbue.
Nikupe mfano, umewahi kwenda dukani na mtoto, halafu akaanza kulilia kitu ambacho huwezi kukinunua? Halafu watu wanaanza kukuangalia, labda mtoto analilia pipi au biskuti, na wewe hukubeba fedha ya vitu hivyo. Unajisikiaje pale watu wanapokuangalia kwa jicho la ‘huyu naye anashindwa kumtuliza huyo mtoto kwa pipi!’. Unamwangaliaje yule mtoto anayelilia pipi? Bila shaka utaondoka naye haraka, utakazana kumzuia asilie au hata asione kile ambacho analilia.
Sasa hivyo ndiyo umekuwa unayafanyia maono ya maisha yako. Yapo ndani yako, yapo na wewe ukilala, yapo na wewe ukioga. Lakini yanapojitokea, unayarudisha na kuyadidimiza. Ukijiambia hilo haliwezekani, au maisha ni magumu, au una mambo mengi ya kufanya.
Na hapo ndipo wengi wanapopotelea, wakikazana kulainisha maisha, wanasahau ndoto kubwa za maisha yao, wanapokuja kustuka, muda umeenda na maisha wanaona kama hawajayaishi.
Hivyo basi rafiki, nusu saa unayoitenga leo, tengeneza vizuri maono ambayo tayari yapo ndani yako. Zile ndoto kubwa ambazo umekuwa unazifikiria tangu ukiwa mtoto. Na nikutahadharishe jambo moja hapa, ulipokuwa mtoto ulikuwa na akili sana, usijiambie huo ulikuwa utoto. Ulikuwa unaweza kufikiri vizuri bila ya kumwonea aibu yeyote. Tangu umeanza kuona aibu, hujawahi kuwa mkweli kwako. Ndiyo maana leo nimetaka ujipe nusu saa ya kuwa mwenyewe, kwa sababu najua ukifanya hili mbele ya wengine, aibu itakujia na hutalitekeleza, na utaendelea kusindikiza mwaka.
Katika nusu saa yako hii, hakikisha una kalamu na kijitabu chako cha kuandika mambo yako muhimu. Nilishakuambia lazima uwe na kijitabu chako, sasa kama mpaka sasa huna, sijui unayaendeshaje maisha yako.
Kwenye nusu saa hii, sahau kabisa kuhusu dunia. Nataka uwe mbinafsi kwa nusu saa tu.
Sahau kuhusu watoto wanaokutegemea, sahau kuhusu wazazi wagonjwa, sahau kuhusu mwenza anayekusumbua, sahau kuhusu mwajiri anayekutumikisha na sahau kuhusu wateja wasumbufu. Ni wewe na wewe tu, kwa ubinafsi wa hali ya juu.
Hapa sasa yaangalie maisha yako, maisha yaliyokamilika kwako yana nini. Kumbuka hakuna aibu hapa, hakuna kusema wengine watanichukuliaje. Wewe yaone maisha yaliyokamilika kwako yanafananaje, tengeneza picha hiyo kwenye akili yako. Na hapo unajumuisha kila eneo la maisha yako, kuanzia kazi au biashara ambayo ungekuwa unaifanya kama maisha yako yangekuwa kamili, mahusiano yako na wengine, mchango wako kwa wengine, maisha yako binafsi, kuanzia mavazi, malazi, nyumba, magari na kadhalika. Jipe ruhusa ya kupitia ndoto yako, ambayo ipo ndani yako. Kitakuja kisauti kinakuambia lakini hilo haliwezekani, achana nacho, wewe endelea kupitia picha yako hiyo.
Baada ya hapo, fikiria ni hatua gani unapaswa kuchukua kila siku ili kuweza kuyabadili na kuboresha maisha yako. Angalia hapo ulipo sasa, na ona ni kitu gani unaweza kufanya kila siku, kufikia maisha ya ndoto yako. Na mambo yapo mengi, kuweka juhudi kwenye kazi zako za kila siku, kujiwekea akiba, kuongeza kipato, kuboresha mahusiano yako na wengine, kujifunza kila siku.
Andika haya yote kwenye kijitabu chako, kuanzia ndoto yako na mipango yako unayoifanyia kazi kila siku.
Kama ulishafanya zoezi hili mwanzo wa mwaka, lirudie tena sasa. Na hili ni zoezi utakalofanya kila siku, ila hutatumia nusu saa kama sasa, badala yake utatumia dakika tano pekee.
Utakachofanya kila siku, ni kujipa angalau dakika tano, za kuipitia ile picha ya maisha ya ndoto yako, na kisha kuandika maono makubwa ya maisha yako. Baada ya hapo utaandika yale unayokwenda kufanyia kazi kwa siku husika. Utarudia hivyo kila siku, kila siku, bila ya kuacha.
Je nikifanya hivi mwaka huu 2017 nitapata kila ninachotaka?
Jibu ni hapana, lakini utakuwa na mabadiliko makubwa mno kwa namna unavyoyachukulia maisha yako. Kuanzia sasa, kazi yako hutaichukulia kama kazi tu, wala biashara yako hutaichukulia kama biashara pekee. Bali utaichukulia kama huduma uliyoitwa kuitoa hapa duniani. Utaona kila unachofanya namba ambavyo kinaathiri kila eneo la maisha yako. Utafanya maamuzi bora zaidi, kwa sababu una picha kubwa zaidi ya maisha yako.
Kubwa kabisa, ambalo unaweza leo usilielewe, ila kwa kufanya hivi utalielewa taratibu ni kwamba fursa zitaanza kujitokeza kila mahali na kukufuata. Wewe mwenyewe utashangaa namna unaanza kuona mambo ambayo ulikuwa huyaoni. Dunia itaanza kufunguka kwako, na kukupa njia bora za kupata unachotaka.
Fanya zoezi hili muhimu leo rafiki, halafu endelea kulifanya kila siku kwa dakika tano pekee. Nenda kafanyie kazi mipango ya siku, na kila fursa inayokuwa mbele yako, inayoendana na maisha ya ndoto yako, ifanyie kazi.
Kama nilivyosema, hii ni nusu saa muhimu sana kwenye maisha yako, lakini matokeo yake unaweza usiyaone haraka. Lakini endelea kufanyia kazi hili, na kwa hakika hutabaki hapo ulipo sasa.
Nakutakia kila la kheri kwenye ngwe hii ya pili ya mwaka 2017, uende ukafanye makubwa, yanayokufikisha kwenye maisha ya ndoto yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.