Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Ifahamu Faida Ya Kwenda Moja Kwa Moja Kwenye Lengo Kusudiwa.

$
0
0
Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni imani yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri na kama hauko vizuri pole sana rafiki. 


Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo katika maisha yako na itumie vizuri leo kwani leo ndiyo maisha yako. Kila unapoamka asubuhi hakikisha unaitumia vizuri asubuhi yako kabla ya dunia haijaamka, asubuhi ndiyo pa kupata ushindi wa kwanza kabisa katika siku yako.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kuweza kukualika tena katika kipindi chetu cha leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia. Kwa namna ya pekee kabisa, nakukaribisha ili uweze kuambatana nami mpaka pale tamati ya kipindi chetu cha leo. Kupitia makala ya leo ninakwenda kukushirikisha faida ya kwenda moja kwa moja kwenye shabaha au lengo kusudiwa.

Kwanza kabisa, napenda kukusimulia simulizi fupi ambayo kuna ndugu mmoja aliweza kunishirikisha. Ndugu mmoja alikuwa anaishi katika kijiji chenye changamoto ya maji hivyo ili aweze kupata inamlazimu kwenda kutafuta maji sehemu ya mbali kwa kutumia usafiri wa punda. Ndugu huyo aliamua kwenda kwa mzee mmoja aliyeko karibu na kijiji chake ambaye anaweza kumsaidia punda kama chombo cha usafiri ili kimrahisishie kwenda kutafuta maji.

Rafiki, ndugu alifanikiwa kufika mpaka kwa mzee huyo ambaye ndiye anatoa msaada wa punda kwa ajili ya kwenda kuchotea maji. Baada ya kufika kwa mzee, yule ndugu alimsalimia mzee yule na kuendelea kupiga stori nyingine na kushindwa kuelezea kile kilichompeleka pale yaani lengo alilokusudia. Katika maongezi yao ya muda mrefu kidogo aliweza kujitokeza kijana mwingine kwa yule mzee.

Mpenzi msomaji, yule kijana mgeni alipofika kwa yule mzee wa punda aliweza kumsalimia mzee na kumwambia shida yake iliyompeleka pale bila ya kupindisha pindisha maelezo. Akamwambia mzee nimekuja na shida yangu ni punda, yule mzee akamjibu sawa na punda umepata nenda kawachukue ukafanye shughuli yake.

Baada ya yule kijana kuondoka, yule ndugu wa mwanzo akamwambia mzee na mimi nilikuwa nahitaji punda kwa ajili ya kwenda kuchotea maji. Yule mzee akamjibu muda wote umekuja hapa unazunguka kumbe una shida ya punda umeshindwa kusema mpaka amekuja mtu mwingine nimempatia.

Ndugu msomaji, nini tunaweza kujifunza kupitia simulizi hii ya huyu ndugu aliyekuwa anahitaji punda kwa ajili ya kwenda kuchotea maji? Kwanza kabisa, punda ni mnyama ambaye huwa anatumika na watu wengi wanaoishi maeneo ya kijijini kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kulima, kubeba mizigo kama vile kuchota maji nakadhalika. Mara nyingi watu wengi wanakosa fursa mbalimbali kwa sababu ya kushindwa kueleza shida yao iliyowapelekea kama vile ilivyomkuta ndugu yetu aliyekuwa anahitaji punda.

Hapa tunajifunza kuwa unapoenda kwa mtu na una shida fulani basi kumbuka lengo ulilokusudia, lengo lililokupeleka pale. Unaweza ukaanza na salamu na baada ya salamu nenda moja kwa moja kwenye lengo au pointi yako, yaani “go direct to the point” huna haja ya kuzunguka mbuyu na kuwa na maelezo mengi. Unapozunguka mbuyu unakuwa unajikosesha fursa mwenyewe hivyo unatakiwa kuelezea kwanza shida yako, halafu hapo baadaye ndiyo unaweza kuendelea na hadithi nyingine.

Epuka ngoja ngoja kwani hata waswahili wanasema kuwa ngoja ngoja ya umiza matumbo na chelewa chelewa utamkuta mwana si wako. Watu wengi ngoja ngoja huwa inawaponza sana katika maeneo mengi, unaenda sehemu una shida ya kazi unazunguka zunguka anakuja mtu anayoosha maelezo anapatiwa kazi na kumuacha yule ambaye anazunguka zunguka. Watu hawana muda wa kusoma wewe unahitaji kitu gani badala yake unatakiwa kwenda moja kwa moja kwenye lengo lako. Bora useme lengo lako uwe huru kabisa kama ni kupata au kukosa.

Mpenzi msomaji, wengi wanakaa na maumivu waliyosababishiwa na watu wao wa karibu lakini wanashindwa kuwaambia ukweli na wanaishia kulalamika bila kuchukua hatua. 

Wengi wanaishia kujilaumu na kujiona wajinga pale wanapoingia katika kasumba kama ilivyomkuta ndugu yetu aliyekosa punda. Wengine inawakuta hata pale wanapoamua kutafuta wachumba ambao wanatarajia kufunga nao ndoa wanashindwa kuwaeleza mapema watu wao ambao walifikiri ndiyo wangewaoa hatimaye watu ambao wanajua kunyoosha maelezo wanafanikiwa kupata kile walichokusudia.

Hatua ya kuchukua leo, kama una shida na mtu nenda moja kwa moja na eleza shida yako mapema kuliko kuzunguka zunguka. Watu hawana muda wa kukaa na kukusikiliza huku wakikuchunguza unahitaji nini, watu sio malaika na wana mambo mengi ya kufanya hivyo ni vema ukamwambia mtu lengo lako mapema ili kujihakikishia ushindi halafu baadaye endelea na hadithi nyingine.

Kwa kuhitimisha, unapokuwa na shida na kwenda sehemu fulani kwa msaada wa kupatiwa huduma ni vema ukaeleza shida yako mapema ili upate uhakika wa huduma uliyoifuata ipo au hakuna. Kwenda moja kwa moja kwenye lengo huwa inaokoa muda kwa wahusika wote wawili, hivyo basi nakualika rafiki kutumia mbinu hii katika Nyanja mbalimbali katika maisha yako.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>