Kama huna taarifa ni kwamba, moja ya biashara zilizokuwa na kasi kubwa ya kusambaa sana, ikijificha kwenye biashara ya mtandao, iliyojulikana kama D9 club, imetumbuliwa na serikali. Serikali kupitia BENKI KUU na MAMLAKA YA MASOKO YA FEDHA, imepiga marufuku biashara hii kwa kuendeshwa kinyume na sheria na kuwa na mfumo wa upatu, ambapo watu wanaweka fedha na kuishia kuzipoteza, wao au wale wanaoshawishiwa kuingia.
Hili lilikuwa wazi, kwamba biashara hii isingechukua muda. Ilikuwa wazi kabisa ni upatu, na ilichelewa kufungiwa, kwa sababu kama nilivyoeleza kwenye kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO, mamlaka za kiserikali huwa zinachelewa sana kuchukua hatua.
Sasa hiyo siyo habari kubwa, kwa sababu imeshafungiwa, habari kubwa, na ambayo nataka nikutahadharishe nayo wewe rafiki yangu ni hii; KUNA BIASHARA NYINGINE MBILI ZITAFUNGIWA, KWA SABABU NAZO ZINAJINADI KAMA BIASHARA ZA MTANDAO, ILA NDANI YAKE KUNA UPATU. Nakueleza hilo rafiki yangu, na kinachofanya hizi hazijafungiwa haraka ni kile kilichofanya D9 ichelewe kufungiwa. Bado madhara yake hayajaonekana wazi, ila yanakuja.
Ninachotaka ni wewe rafiki yangu uepuke kujihusisha na biashara hizi ambazo zitakuja kufungiwa. hii itakusaidia kutopoteza fedha, lakini pia kulinda heshima yako. Hakuna kitu kinaharibu heshima kama umekazana kufanya kazi zako kwa uaminifu, halafu wakaja watu wakakushawishi ujiunge na biashara, ukashawishika na kujiunga, na wewe ukashawishi watu waliokuwa wanakuheshimu, kwa heshima yako wakajiunga, halafu ikagundulika siyo biashara halali. Unaharibu sana jina lako.
Hichi ndiyo kilinisukuma mimi kuandika kitabu IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING) baada ya kuona watu wanadanganywa mno kuhusiana na biashara hii na kuingizwa kwenye upatu. Kwenye kitabu hichi nimeeleza misingi yote ua biashara ya mtandao, mfumo wa malipo, jinsi ya kuchagua kampuni, na muhimu zaidi, jinsi ya kutambua kama biashara ni halali au ni mchezo wa upatu.
Kwenye sura hiyo ya uhalali, nimekushirikisha mambo kumi muhimu ya kuangalia, na iwapo ungeyaangalia mapema, D9 ungeiogopa kama ukoma, kabla hata serikali haijaifungia.
Sasa leo sitaki kusema mengi hapa rafiki, ninachosema ni hichi, kama ulishapata kitabu, kisome mpaka mwisho, ili usiingie kwenye utapeli mwingine unaoendelea sasa.
Na kama hujapata kitabu hichi, nina habari njema sana kwako leo.
Siku kilipotoka kitabu hichi, nilikupa zawadi wewe rafiki yangu, kukipata kwa bei ya punguzo, kwa shilingi elfu 4, badala ya elfu 5. Marafiki wengi walitumia nafasi hii na kupata kitabu. Ila wapo ambao hawakuitumia nafasi ile.
Na kwa kuwa mimi nakupenda sana wewe rafiki yangu, na ninaumia sana kuona unapoteza fedha na heshima yako kwa mambo yasiyo halali, nakupa tena kitabu hichi leo kwa bei ya punguzo, ya shilingi elfu 4 pekee.
Ninachosema rafiki yangu ni hichi, leo tarehe 16/06/2017 nakupa zawadi ya kitabu IJUE BIASHARA YA MTANDAO, kwa bei ya shilingi 4,000/= hili ni punguzo kutoka bei yake halisi ya shilingi 5,000/=
Ninachokuambia rafiki yangu, soma kitabu hichi.
Huenda unasema kwamba wewe hufanyi biashara ya mtandao, wala huna mpango wa kuifanya, kwa sababu una biashara nyingine. Sasa nakuambia wewe ndiyo muhimu mno kukisoma. Kwa sababu ndani ya mtandao kuna siri kubwa sana ya kukuza biashara yoyote ile. Kwa kusoma kitabu hichi, wewe mwenye biashara, unaweza kuona njia ya kutumia mtandao wa wateja wako ulionao sasa kuwafikia wateja wengi zaidi.
Nasema rafiki yangu, soma kitabu hichi, na utaondoka na maarifa sahihi kuhusu biashara ya mtandao na hata kuweza kukuza biashara yoyote unayofanya kwa kutumia mtandao wa wateja wako.
UNAPATAJE KITABU HICHI?
Kitabu ni nakala tete, yaani softcopy (pdf) hivyo unaweza kusomea kwenye simu yako, tablet au kompyuta kama unavyosoma hapa.
Kitabu kinatumwa kwa email, hivyo popote ulipo unaweza kutumiwa kitabu hichi, huhitaji hata kuondoka hapo ulipo sasa hivi.
Gharama ya kitabu ni ndogo, ukilinganisha na maarifa utakayopata. Ni shilingi elfu tano (5,000/=).
Lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, na napenda sana upate kitabu hichi mapema, nakupa zawadi ya kitabu hichi kwa shilingi elfu nne (4,000/=). Zawadi hii ni kwa siku moja tu, leo tarehe 16/06/2017. Baada ya hapo bei yake ni shilingi elfu tano.
Malipo yanafanyika kupitia namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, TIGO PESA 0717 396 253, AIRTEL MONEY tuma moja kwa moja kwenye tigo pesa. Majina yanayotokea ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha, tuma email yako kwa njia ya mesej kwenda namba 0717 396 253 pamoja na jina la kitabu na utatumiwa kitabu mara moja.
Rafiki, nikusisitize sana, pata kitabu hichi. Naona kila siku namna watu wanafanya maamuzi yasiyo sahihi na yanawagharimu. Huenda ulishafanya hivyo au bado. Sasa wekeza kiasi hicho kidogo upate maarifa sahihi, ambayo yatakuepusha kupotezewa muda, fedha na hata heshima yako. Tumeona watu wamefanya makosa kwenye D9, na watu wanaendelea kufanya makosa sasa kwenye biashara nyingine, ambazo pia zitafungwa, sitaki wewe uwe mmoja wao. Nunua kitabu hichi leo na kisome.
Pata kitabu hichi leo hii tarehe 16/06/2017 kwa bei ya punguzo ili uweze kukisoma.
NENO LA MWISHO KWAKO RAFIKI YANGU.
Zipo biashara mbili, ambazo zitafungiwa kama ilivyofungiwa D9, ni jambo la muda. Huenda umeshajiunga, au huenda wapo watu wanakushawishi sasa ujiunge. Ninachokuambia ni hichi, soma kwanza kitabu IJUE BIASHARA YA MTANDAO, ndani yake utapata maarifa sahihi ya kujua kama biashara ni halali au la. Kwa wale waliosoma awali, D9 ilikuwa na sifa zote 10 za kuwa mchezo wa upatu. Sasa ukisoma sifa hizo 10, utaona biashara nyingine pia zinazoelekea kwenye D9.
Pata kitabu hichi leo kwa bei ya punguzo, tsh 4,000/=. Chukua hatua leo rafiki, hutajutia baadaye.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani.