Habari za leo rafiki yangu?
Ni imani yangu kwamba unaendelea vyema na unaweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.
Swali langu kwako leo rafiki ni hili; je jana ulipata zawadi ya kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO? Kitabu hichi kilitoka jana tarehe 01/06/2017 na kwa siku hiyo ya jana nilitoa zawadi kwako rafiki yangu kukipata kwa shilingi 4,000/= badala ya bei yake ya shilingi 5,000/=. Kama tayari umeshakipata basi unaweza kuishia hapa, usiendelee kusoma. Kama bado hujakipata kitabu hichi basi endelea kusoma, kuna nafasi nyingine nzuri kwako, ila hii inaisha leo tarehe 02/06/2017.
Wapo marafiki ambao wameniandikia usiku kwamba hawakuweza kulipia jana na hivyo kukosa nafasi hii. Ni marafiki wengi ambao wamekuwa wakipata huduma zangu nyingine nzuri na tumekuwa pamoja muda mrefu. Hivyo nikawaambia walipie leo ili waweze kupata kitabu hichi kizuri sana. Hivyo na wewe rafiki yangu, nakupa nafasi hii, kama bado hujalipia kitabu kwa bei ya zawadi basi lipia leo terehe 02/06/2017. Hii ni nafasi ya mwisho kabisa ya kulipia kitabu hichi kizuri kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh 4,000/= baada ya hapo kitaendelea kupatikana kwa bei yake ya shilingi 5,000/=.
Kwa wale ambao tumekuwa pamoja muda mrefu, mnajua vizuri sana kuhusu gharama za huduma mbalimbali ambazo huwa ninatoa. Huwa bei ni ile ile, haipungui wakati wowote ule, labda kwa kupanda lakini siyo kwa kupungua. Lakini wakati huu nimeanza kutoa kama zawadi kwa marafiki zangu, kwa sababu nimesikitishwa sana na namna watu wanavyotapeliwa mchana kweupe kabisa.
Unaona watu wakiwa wanahangaika na fursa wanazoambiwa zinawalipa mamilioni kwa siku, wanakazana kweli lakini mwisho wa siku wanapoteza muda walioweka, fedha zao na hata heshima zao, pale wanapowashawishi wengine kuingia halafu ikagundulika siyo.
Nimesikitishwa sana na namna watu wakishaambiwa kuhusu fedha wanasahau kila kitu. Mtu mmoja aliniuliza kuhusu biashara fulani ya mtandao, nikamwambia kaa nayo mbali, siyo biashara halali. Akaniambia mbona kuna watu nawajua wamepata fedha! Hapo ndipo niliposhangaa. Watu wanaiba na wanapata fedha, je na wewe unataka uibe? Usahihi haupimwi kwa kiasi cha fedha mtu anapata, bali kwa misingi ambayo inafuatwa.
Hivyo rafiki yangu, nimesema imetosha, usitake tena kudanganywa wala kutapeliwa. Usitake tena watu watumie matatizo yako ya kifedha au kukosa kazi kuwa mtaji wa wao kukutapeli wewe. Sasa ni wakati sahihi wa kufanya maamuzi bora inapokuja kwenye biashara ya mtandao.
Pia hata kama hufanyi biashara ya mtandao, ipo siri kubwa ya mafanikio ya biashara yako kwa kutumia mtandao wa wateja wako.
Ngoja nikupe mfano ili tuelewane vizuri, una shida ya kupata bidhaa fulani muhimu kwako. Na zipo kampuni mbili zinauza bidhaa hii, kampuni A na kampuni B. Wakati unaulizia, kila kampuni inajinadi ndiyo bora kabisa, ukiangalia matangazo yao, kila mmoja anasema ni bora na atakusaidia, unashindwa kujua uchague kampuni ipi. Sasa wakati bado unafikiria hilo, unakutana na mimi rafiki yako ambaye tunaaminiana, kabla hata hujaniuliza chochote naanza kukuambia namna nimetumia bidhaa ya kampuni B na imenisaidia sana. Je wewe utaenda kununua bidhaa ya kampuni ipi? Lazima utanunua B kwa sababu, umesikia kutoka kwangu mimi mtu ambaye unaniamini.
Sasa kila mfanyabiashara, anapaswa kutumia nguvu hii ya mtandao, kwa kuwatumia wateja alionao sasa, kuwafikia wateja wengi zaidi. Kwa kujifunza biashara ya mtandao kupitia kitabu hichi cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO, utaweza kuona namna gani uboreshe biashara yako zaidi.
Nimalize kwa kusema rafiki yangu, hii ni nafasi ya mwisho kabisa ya kupata zawadi hii ya kitabu kwa bei ya punguzo. Ninachokushauri ni ukipate leo hii, uweze kukisoma na kufanyia kazi.
UNAPATAJE KITABU HICHI?
Kitabu ni nakala tete, yaani softcopy (pdf) hivyo unaweza kusomea kwenye simu yako, tablet au kompyuta kama unavyosoma hapa.
Kitabu kinatumwa kwa email, hivyo popote ulipo unaweza kutumiwa kitabu hichi, huhitaji hata kuondoka hapo ulipo sasa hivi.
Gharama ya kitabu ni ndogo, ukilinganisha na maarifa utakayopata. Ni shilingi elfu tano (5,000/=).
Lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, na napenda sana upate kitabu hichi mapema, nakupa zawadi ya kitabu hichi kwa shilingi elfu nne (4,000/=). Zawadi hii ni kwa siku moja tu, leo tarehe 02/06/2017. Baada ya hapo bei yake ni shilingi elfu tano.
Malipo yanafanyika kupitia namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, TIGO PESA 0717 396 253, AIRTEL MONEY tuma moja kwa moja kwenye tigo pesa. Majina yanayotokea ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha, tuma email yako kwa njia ya mesej kwenda namba 0717 396 253 pamoja na jina la kitabu na utatumiwa kitabu mara moja.
Rafiki, nikusisitize sana, pata kitabu hichi. Naona kila siku namna watu wanafanya maamuzi yasiyo sahihi na yanawagharimu. Huenda ulishafanya hivyo au bado. Sasa wekeza kiasi hicho kidogo upate maarifa sahihi, ambayo yatakuepusha kupotezewa muda, fedha na hata heshima yako.
Pata kitabu hichi leo hii tarehe 02/06/2017 kwa bei ya punguzo ili uweze kukisoma.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani.
MUHIMU; Lipa tsh 4,000/= leo upate kitabu. Baada ya leo hutapata tena nafasi hii ya kipekee kupata kitabu hichi kwa bei ya punguzo. CHUKUA HATUA SASA.