Ukuaji wa intaneti na mitandao ya kijamii umekuwa fursa nzuri sana ya ukuaji wa kila aina ya biashara.
Ni rahisi sana sasa hivi kutangaza biashara na hata kuwafikia wateja wengi kupitia mitandao ya kijamii. Ni rahisi sana sasa hivi kuuza moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii. Na kwa ubora zaidi, unaweza kumiliki biashara moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii, na ukaokoa gharama za ofisi au eneo la biashara.
Lakini pamoja na fursa hii nzuri ya kufanya biashara kwenye mitandao ya kijamii, bado tatizo kubwa ni moja, watu wanashindwa kuuza kupitia mitandao hii. Watu wanajitahidi sana kutangaza biashara zao lakini wanashindwa kuwashawishi wateja mpaka wanunue. Na hii inatokana na kosa moja ambalo wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya kwenye mitandao hii wakati wanatafuta wateja.
Kupitia somo letu la MTAALAMU NETWORK, nimekuandalia somo ambalo litakuwezesha kujua makosa unayofanya kwenye kujaribu kuuza kwenye mitandao ya kijamii na hatua muhimu unazopaswa kuchukua. Ni muhimu uangalie somo hili la leo kwa sababu litakuwezesha kutangaza biashara yako kwa usahihi na wateja kuwa tayari kununua kwako.
Angalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya sasa. Angalia somo na fanyia kazi yale unayokwenda kujifunza. Unaweza pia kuangalia somo hili moja kwa moja hapo chini.
Tunaishi kwenye mapinduzi makubwa ya mtandao wa intaneti, hakikisha huachi nyuma na mapinduzi haya. Karibu sana nikushauri vizuri namna ya kunufaika na mtandao wa intaneti. Kwa mahitaji ya ushauri wa matumizi ya intaneti kwenye kukuza biashara yako, tuwasiliane kwa njia ya wasap namba 0717396253.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.