Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Maana Halisi Ya Dhana Ya Kujilipa Wewe Mwenyewe Kwanza Kabla Hujafanya Matumizi Ya Fedha Zako.

$
0
0
Ushauri muhimu sana utakaoupata kwenye usimamizi wa fedha zako binafsi ni huu; JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA, KABLA HATA HUJAFANYA MATUMIZI. Ni ushauri wenye maajabu makubwa kwani ukiweza kufanya hivyo kwa nidhamu, bila ya kujali kipato chako ni kidogo kiasi gani, utaweza kuufikia utajiri.

Lakini changamoto kubwa ambayo nimekuwa naiona ni kwamba wengi hawaelewi vizuri dhana hii ya kujilipa wao wenyewe kwanza. Na hivyo wamekuwa wanakosa fursa hii nzuri ya kufikia utajiri kwa kuanza na kipato walichonacho.

Watu wengi wamekuwa wanafikiri kujilipa wao wenyewe ni kuweka akiba, na hivyo kujitahidi kuweka akiba, ambazo pia wanaziweka kwa njia ambayo siyo sawa. Hili linapelekea kutokuwa na akiba ya kuweka, au wakiwa na akiba basi haidumu muda mrefu. Watu wengi wamekuwa wanafanya matumizi yao, na kile kinachobaki ndiyo wanaweka akiba. Lakini kama wote tunavyojua, matumizi huwa hayaishi kama fedha bado ipo, na hivyo hushangaa mbona hawana akiba ya kuweka.

Suluhisho la hayo yote ni kuielewa vizuri dhana na jilipe wewe kwanza. Hapa unapopata fedha yoyote ile, kabla hujafikiria matumizi yoyote, unatoa sehemu ya kipato hicho na unakuwa umejilipa wewe mwenyewe. Baada ya hapo ndipo unaweza kuweka akiba na kufanya matumizi mengine.

Naomba uelewe vizuri hapo, unajilipa wewe mwenyewe kwanza, halafu ndipo unaweka akiba na kufanya matumizi. Ile unayojilipa wewe mwenyewe kwanza siyo fedha ya akiba, wala siyo fedha ya maendeleo, bali hii ni mbegu yako ya utajiri wa baadaye.

Angalia somo la leo ambapo nimekueleza hili kwa kina. Nimekueleza kwa mfano ni kiasi gani cha kipato chako ujilipe wewe mwenyewe. Na pia nimekupa mifano ya njia bora ya kulinda ile fedha ambayo unajilipa wewe kwanza, ili uweze kuwekeza na kupata kipato kikubwa kwa baadaye.

Muhimu sana nimekusisitizia kwamba fedha unayojilipa wewe mwenyewe kwanza haipo kwenye mipango yako ya maendeleo. Iwe ni kujenga nyumba au kununua gari, hivyo unapaswa kuvifanya, lakini siyo kutoka kwenye fedha unayojilipa wewe kwanza.

Angalia somo hili la leo, yapo mengi sana ya kujifunza na kama ukiyafanyia kazi, basi maisha yako ya kifedha yatakuwa bora. Bonyeza maandishi haya kuangalia somo hili muhimu. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Jifunze na muhimu zaidi fanyia kazi yale uliyojifunza. Na kama utapenda kujifunza zaidi basi nakukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tuwe karibu zaidi. Pia utajifunza mengi kuhusu fedha kwenye semina ya mwezi wa saba ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenye namba 0717396253. Karibu sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>