Mkono. Jifunze Hapa Namna Ya Kuanzia Chini Kabisa.
Habari za leo rafiki yangu?
Karibu kwenye makala ya leo ya ushauri wa changamoto ambazo zinatuzuia kufanikiwa. Leo tutakwenda kuangalia changamoto ya kukosa pa kuanzia na tabia ya wengi kusubiri kupata wafadhili ndiyo waweze kuanza. Hili limekuwa tatizo kubwa kwa vijana wengi, na linatokana na kile ambacho tumeaminishwa kama taifa kwamba sisi wenyewe hatuwezi, mpaka aje mtu kututoa hapa tulipo. Ndiyo maana hata bajeti yetu kama taifa, sehemu kubwa tunategemea misaada ya wafadhili. Hili ni hatari na kama mtu unayetaka kufanikiwa, hupaswi kabisa kusubiri wafadhili ndiyo uchukue hatua.
Kabla hatujaangalia ni hatua zipi za kuchukua, kwanza tusome ujumbe wa msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuomba ushauri kwenye hili;
Changamoto inayonikumba ni Mtaji, je kuna wafadhili wanaotoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali? Maximilian M. N.
Kama ambavyo ameandika mwenzetu Mazimilian, mtaji ni changamoto kwa wengi. Lakini tatizo zaidi linakuja pale mtu anapokuwa na njia moja tu ya kuondokana na changamoto hiyo.
Ambayo wengi hufikiria kupata msaada wa wafadhili, au kusaidiwa na ndugu zao.
Tumekuwa tunaona malalamiko ya wengi kwenda kwa wazazi, ndugu, na hata serikali, pale wanapokosa watu wa kuwawezesha kupata mtaji wa kuanza.
Japokuwa inaweza kuonekana ni sahihi kabisa mtu kulalamikia kukosa mtaji wa kuanza, na kulalamika pale ambapo watu hawamsaidii, mimi napenda kukuambia kama kweli unataka kutoka hapo ulipo, usisubiri upewe mtaji na yeyote. Usisubiri wafadhili waje kukukuta hapo ulipokaa na kukupa mtaji, usisubiri wazazi au ndugu ndiyo wakupe mtaji wa kutoka hapo.
Bali unachohitaji wewe ni kuanza, angalia popote unapoweza kuanzia kwa sasa na anza.
Anza hata kwa hatua ndogo sana, anza hata kwa kujitolea sehemu kusaidia kazi, anza hata kwa bidhaa moja na kuipitisha nyumba kwa nyumba, fanya chochote cha kuanza, na hii itakuwezesha kutoka hapo ulipo.
S0MA; Usianzishe NGO Anzisha Kampuni.(Usianzishe Msaada Anzisha Biashara)
Napenda nikuambie kwamba hakuna mtu yeyote atakayekuja kukutoa hapo ulipo kama wewe mwenyewe hutaonesha juhudi za kujinasua hapo ulipo. Haijalishi una uwezo mkubwa kiasi gani, haijalishi una wazo zuri kiasi gani, kama umekaa na unasubiri watu waje kukutoa hapo, umechagua kubaki nyuma.
Nimekuwa nasisitiza sana mtu achukue hatua badala ya kusubiri kwa sababu wanaosubiri ni wengi. Na wale waliosaidia wanaosubiri na wakaishia kupoteza msaada walipewa ni wengi.
Hivyo hata wafadhili wa sasa, hawafadhili tena maneno matupu. Badala yake wanataka kuona huyo mtu anayetaka kusaidiwa ameshapiga hatua gani yeye mwenyewe. Kukiwa na watu wawili, wote wanahitaji msaada, mmoja amekaa nyumbani na kusubiri, mwingine ameanza kitu kidogo na anapambana nacho kila siku. Mfadhili atakuwa tayari kumsaidia yule anayefanya kitu kuliko aliyekaa na kusubiri. Kwa sababu aliyefanya kitu anaonesha kweli ana hasira, ila aliyekaa na kusubiri, bado ana namna ya kuwa na maisha, la sivyo angeshapata hasira na kutoka kupambana.
Sasa basi unaanzia wapi?
Na hapa ndipo wengi huuliza swali, kwamba waanzie wapi? Kama vile kuna siri fulani iliyofichwa ambayo ni wao tu hawajaijua. Mimi majibu yangu mara zote yamekuwa hayana maajabu yoyote, kwani unapopaswa kuanzia ni pale ulipo sasa. Kwa sababu utawezaje kuanzia sehemu ambayo haupo sasa? Angalia hapo ulipo sasa, angalia ulichonacho ndani yako, angalia mazingira yanayokuzunguka kisha amua ni hatua ipi unaweza kuichukua mara moja, na ichukue.
Mifano michache ya wapi unaweza kuanzia;
1. Tafuta mahali na jitolee.
Kama wewe umesoma ila kazi ndiyo hujapata, angalia mazingira yanayokuzunguka, angalia kipi unaweza kufanya, kisha omba mahali ambapo unaweza kujitolea kufanya kazi unayoweza kufanya. Wewe omba tu kujitolea, wala usitegemee kupewa chochote, na wakikupa nafasi, fanya kazi iliyo bora sana.
Njia bora ya kupata nafasi kama hii, ni kuangalia taasisi, kampuni au biashara yoyote, ichunguze kwa undani, angalia wapi wanapata shida kubwa, angalia namna gani unaweza kuwasaidia kuondokana na shida hiyo, kisha omba wakupe nafasi ya kuwasaidia shida yao hiyo.
Eneo moja ambalo kila kampuni au biashara inateseka ni kwenye kuuza kile wanachotengeneza, iwe ni bidhaa au huduma. Kuwafikia wateja wengi ni changamoto kubwa. Nenda na mpango wako wa kuongeza wateja na mauzo zaidi na hutakosa kazi ya kufanya.
2. Uza chochote.
Sehemu moja ambayo kila mtu anaweza kuanzia na akapiga hatua kwenye maisha yake, ni kutafuta chochote ambacho anaweza kukiuza, halafu akakiuza. Tafuta kitu chochote ambacho unaweza kuuza, kwa hapo ulipo na kiuze kama ‘kichaa’. Yaani pita kila kwa anayehitaji na mshawishi kununua, usikubali yeyote akurudishe nyuma. Inaweza kuwa bidhaa au huduma yoyote, na inaweza kuwa yako au ya mwingine.
Kwa mfano unaweza kuchagua nguo chache na kuziuza, au ukachagua vitabu vichache na kuviuza. Au ukaenda kwenye biashara yoyote, ukaomba upewe nafasi ya kuuza bidhaa zao, hata kama ni kuzunguka nyumba kwa nyumba. Hizi ni kazi ambazo zipo wazi kabisa lakini wengi hujifanya hawawezi kuzifanya, zinawadhalilisha. Sasa nikuulize kipi kinakudhalilisha, kutembea na mabeseni nyumba kwa nyumba, ukakazana kuuza 10 kwa siku ukapewa elfu
10 au kukaa nyumbani huna cha kufanya na kuomba watu wakupe hata fedha ya kununua vocha?
Chagua kitu chochote na kiuze hasa. Kuuza ni njia ya uhakika ya kutengeneza kipato kwa kutumia nguvu zako na ujuzi wako.
SOMA; Kuanzisha Asasi Zisizo Za Kiserikali(NGO) Kama Njia Ya Kutengeneza Kipato.
3. Jiunge na biashara ya mtandao ambayo mtaji wa kuanzia ni kidogo.
Zipo biashara nyingi za mtandao (network marketing) ambazo unaweza kujiunga kwa mtaji kidogo kabisa, na wakati mwingine bure. Ukatumia bidhaa zao na kuziuza pia, huku ukitengeneza mtandao na kunufaika. Hapa unahitaji kuwa na tahadhari, kwa sababu zipo biashara nyingi zimeibuka siku hizi wakisema ni za mtandao, lakini siyo kweli. Ni vyema kuanza na biashara zinazoeleweka, ambazo zina bidhaa au huduma ambayo kweli inauzwa na watu wanaihitaji na kuilipia.
4. Anzisha blog kwenye eneo lolote unalopenda kufuatilia na andika kama mashine.
Kama kuna kitu chochote ambacho wewe unakijua na wengine hawakijui, au kuna kitu unapenda kukifuatilia sana, anzisha blog, halafu andika kama mashine. Yaania andika kila siku ukitoa taarifa na maarifa ambayo yatawasaidia wengine kufanya maamuzi sahihi na kupiga hatua. Andika makala hata tano kwa siku, kama hakuna unachofanya sasa. Tumia mitandao ya kijamii kusambaza maarifa yako na kuwafikia wengi zaidi. Baada ya hapo unaweza kuuza maarifa na taarifa zaidi kwa wale wanaotaka zaidi kutoka kwako. Hapa unaweza kujitengeneza kama mtaalamu wa kitu fulani, ukajenga hadhira yako na ukatengeneza kipato bora kabisa kwako.
5. Ungana na wengine na fanyeni kitu pamoja.
Wakati wewe unasema huna mtaji wa kuanza, wapo wengine ambao wana mtaji lakini hawajui wafanye nini, au wana mtaji ila hawana muda wa kuanzisha na kusimamia biashara.
Hapa unaweza kuwafikiria watu 100 unaowajua moja kwa moja, mfikirie kila mtu kuna kipi ambacho anaweza kuwa anataka kufanya lakini hana muda wa kukifanya. Wakati mwingine omba kukutana nao na fanya nao maongezi. Rudi na ukae chini, tengeneza kitu ambacho mnaweza kufanya pamoja. Nenda tena kwao na pendekezo lako, halafu angalieni mnaweza kuanzia wapi. Katika watu 100 utakaoongea nao, hutakosa 10 ambao watakusikiliza kweli, na katika hao 10 mmoja au wawili watakuambia tujaribu. Ni ujasiri wako na uwezo wako wa kufikiri tofauti utakaokusaidia kwenye hali kama hiyo.
Kwa vyovyote vile rafiki, ninachokushauri ni amka hapo ulipo na anza kufanya kitu, fanya chochote na watu watakuona. Anza kufanya na wafuate watu ukiwa na kitu unafanya, waambie wakusaidie zaidi na wengi watakuwa tayari kufanya hivyo.
Kama utahitaji ushauri zaidi kuhusu biashara gani ya mtandao uingie, au kama unataka kuanzisha blog, au kama kuna kitu unataka kuanza lakini hujui uanzie wapi, wasiliana na mimi moja kwa moja wasap namba 0717396253, ujumbe uwe kwa njia ya wasap tu, usitume ujumbe wa kawaida wala usipige simu. Karibu.
Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog