Habari za leo rafiki yangu,
Kama upo hai, yaani kama unasoma hapa, nina kitu kimoja muhimu sana cha kukuambia. Unahitaji sana kuwa na blog. Ni hivyo tu rafiki, kuwa na blog na utaweza kuitumia kutengeneza jina lako, kujenga uwezo wako wa kufikiri, kuongeza sifa na wasifu wako na pia kutengeneza kipato.
Kwenye kipindi cha leo, nimekueleza kwa mifano namna gani blogu itakuwa na manufaa makubwa sana kwako. Iwe una biashara, umeajiriwa au ni mwanafunzi, blog itakunufaisha sana.
Kama ni mwajiriwa, unaweza kuitumia blog kuongeza sifa yako na kuwa na thamani zaidi kwa mwajiri wako wa sasa na hata wa baadaye. Kama unatafuta kazi, kwa kuwa na blog utakuwa na sifa ya ziada ambayo itakufanya uajiriwe ukilinganisha na wengine.
Kama unafanya biashara, blog yako itakuongezea wateja zaidi. Kwa sababu zama hizi kabla watu hawajafanya maamuzi wanauliza kwanza kwenye mtandao wa google. Unapokuwa na blog, google itawaleta kwenye blog yako wale wanaoulizia mambo yanayoendana na unayofanya wewe.
Kama wewe ni mwanafunzi, blog inaweza kukusaidia kujifunza na kuelewa zaidi. Kwani kupitia blog yako unaweza kuwafundisha wengine kile ambacho unajifunza, na kwa njia hii utaelewa vizuri zaidi na utajijengea sifa kubwa baadaye.
Kwa hali yoyote ile, blog inaweza kukusaidia kuboresha uwezo wako wa kufikiri, uwezo wako wa kujenga hoja na hata kuweza kuwashawishi wengine kupitia kile unachoandika.
Kwa kifupi nakuambia rafiki yangu, unahitaji blog. Zama hizi, kama huna blog ni sawa na haupo hapa duniani. Unahitaji blog mno. Angalia kipindi hichi cha leo kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.
Angalia kipindi hichi cha leo na jua umuhimu wa blog, kisha wasiliana na mimi kwa simu +255 717 396 253 nikupe blog nzuri unayoweza kuitumia kunufaika.
Karibu sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.