Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni imani yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri katika maisha yako. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani leo ni siku nyingine mpya, bora na ya kipekee sana katika maisha yetu. Wewe ndiyo una maamuzi ya kuamua leo iwe siku bora kwako au ya hovyo, una uwezo wa kuamua leo iwe siku yako ya furaha au ya kutokuwa na furaha kila kitu ni maamuzi na mtazamo wako kichwani.
Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii siku ya leo kuweza kukualika katika kipindi chetu cha leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Kwa hiyo, mpenzi msomaji wangu nakualika tusafiri pamoja mpaka pale tamati ya kipindi chetu cha leo. Kupitia somo letu la leo nitakwenda kukushirikisha watu muhimu waliopewa uwezo mkubwa na Mungu hapa duniani. Ili uweze kufahamu kwa undani kile nilichokuandalia mpendwa msomaji wangu nakusihi; karibu sana tusafiri pamoja hadi pale tamati ya kipindi chetu cha leo.
Miongoni mwa viumbe hai vilivyopewa uwezo mkubwa na Mungu hapa duniani basi watu hao ni wanawake. Mungu amempa mwanamke uwezo mkubwa sana katika maisha yake, amempa mamlaka makubwa ya kufanya mambo makubwa hapa duniani licha ya wanawake wengi kushindwa kutumia uwezo wao mkubwa ulioko ndani mwao. Mwanamke aliyeamua kutumia uwezo wake mkubwa aliopewa na Mungu anakwenda kuwa Baraka katika dunia yake na matunda yake yataonekana duniani.
SOMA; Hii Ndiyo Faida Ya Kupanda Mbegu Bora Kwa Wasaidizi Wako Wa Kazi Katika Familia Yako.
Mwanamke ni kiungo cha kuunganisha familia, katika familia mwanamke ndiyo kiungo cha kuunganisha familia, kuijenga familia na kuwa familia bora na imara endapo tu mwanamke akitumia uwezo na mamlaka kubwa ambayo Mungu amempa. Mwanamke aliyesimama katika familia yake anakuwa ni kichocheo cha maendeleo ndani na nje ya familia yake kwa kuweza kuwahamasisha wenzake kwa njia mbalimbali kama vile kupashana habari.
Ndugu msomaji, mwanamke ndiyo dunia, hakuna ubishi kuwa kila mmoja wetu amezaliwa na mwanamke na Mungu ndiye aliyepanga kila mtu atazaliwa kupitia familia na atazaliwa na mwanamke. Mwanamke ni kama nyumba ambayo mtu anazaliwa, anaishi, mpaka anakuwa na kuweza kujisimamia mwenyewe na miguu yake. Mwanamke ni tabibu katika familia kwani anaweza kutibu vitu vingi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na mambo yanaweza kwenda vizuri.
Rafiki, ni kweli kabisa mwanamke ana nafasi kubwa sana katika jamii yetu, na habari njema ni kwamba kama mwanamke akiweza kutumia rungu au uwezo mkubwa aliopewa na Mungu basi anaweza kuwa faida kwa jamii nzima na wala si hasara. Mwanamke ni upendo katika familia, familia ikiwa na mwanamke anayetumia uwezo wake vizuri katika hali chanya anakuwa upendo katika familia yake lakini siyo tu kuleta upendo bali pia huleta amani.
SOMA; Siri Ya kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa.
Mwanamke ni furaha, kuna msemo mmoja niliusoma katika kitabu kimoja ukisema kuwa kama mama hana furaha basi nyumba nzima haina furaha, msemo huu unadhihirisha kuwa mwanamke ambaye ndiye mama huleta furaha katika familia. Kama mama akiwa na furaha atawaalika na familia yake kuwa na furaha kama tulivyosema hapo juu kuwa mwanamke ni kiungo katika familia yaani kama ni timu ya miguu basi mwanamke ni kiungo mchezeshaji wa timu nzima inapokuwa uwanjani inacheza lazima atahakikisha inakuwa salama dhidi ya mashambulizi ya wapinzani.
Mpendwa msomaji, itakuwa ni litania ndefu kama tukiendelea na kuelezea sifa au nafasi ya mwanamke na uwezo mkubwa au mamlaka makubwa aliyopewa na Mungu. Sasa tuangalie upande wa pili wa uwezo wa mwanamke aliyopewa na Mungu kama akienda kinyume na uwezo wake.
Mpenzi msomaji wangu, unaweza kushangaa kwa nini leo Deo Kessy ameamua kumwelezea mwanamke kama somo, lakini hii yote ni kwa sababu tu ya uwezo mkubwa aliopewa na Mungu lakini pia kutoa mwanga kwa jamii. Licha ya mwanamke kupewa uwezo mkubwa lakini kama mwanamke akitumia vibaya uwezo wake basi anaweza kuwa mwiba katika jamii yake.
Mwanamke ana ushawishi mkubwa katika jamii lakini kama mwanamke akitumia vibaya uwezo wake anaweza kusambaratisha familia kwa kusambaza chuki kwa watoto, anaweza kuigawa familia, mwanamke anaweza kuibomoa familia kiimani na n.k. Kwa hiyo mwanamke akitumia vibaya rungu au uwezo aliopewa basi anaweza kugeuka kuwa mateso au mwiba kwa watu wengine katika familia au jamii.
Wanawake wengine wanatumia vibaya uwezo wao kwa kusambaza sumu kupitia ndimi zao, chuki zinaenda kuzaa roho za mauti miongoni mwa watu. Familia inaweza kukosa raha kwa mwanamke aliyekosa hekima na busara na wakati mwingine wanaweza kusambaratisha familia baina ya pande mbili. Siku ndimi zikitumika vizuri basi tunaweza kuokoa roho za watu, kwani ulimi ni mdogo lakini unaweza kuleta madhara makubwa katika jamii ni kama vile moto mdogo unaweza kusambaratisha msitu mzima vivyo hivyo kwa mwanamke anayetumia uwezo mkubwa au rungu alilopewa na Mungu vibaya kwenye maisha yake anaweza kuleta madhara makubwa.
Hatua ya kuchukua leo, Tumia uwezo au mamlaka makubwa uliyopewa kuleta Baraka duniani na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Kila mtu anaalikwa kutumia mamlaka yake vizuri sehemu yoyote aliyopo bila kujali cheo au wadhifa alionao.
Kwa hiyo, mwanamke akitumia uwezo wake vizuri anaweza kuwa nguvu ya ushawishi katika jamii yake, lakini mwanamke akitumia uwezo wake vibaya basi anaweza kugeuka kama moto mdogo unaoweza kuteketeza msitu mzima.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kujifunza kila siku. Asante sana.