Kati ya tabia ambayo kwa haraka haraka unaweza kuiona sio ya muhimu sana ila unatakiwa uwe nayo na kuitumia kila siku katika maisha yako ili upate mafanikio ni tabia ya kuamka asubuhi na mapema.
Ninaposema kuamka asubuhi na mapema, hapa ninamaanisha ni kule kuamka kati ya saa kumi kamili hadi saa kumi na moja kamili, hicho ndicho kitu ninacho maanisha. Mpaka hapo tupo pamoja.
Inawezekana unaanza kuwaza, khaaaa!, Imani na wewe sasa umezidi, muda wote huo naamka saa kumi au saa kumi na moja nakwenda wapi wakati usingizi ni mtamu sana hasa ule usingizi wa asubuhi?
Sikiliza rafiki yangu, leo nitakupa siri muhimu sana ambayo imejificha nyuma ya kuamka asubuhi na mapema. Nikiwa na maana kama utaendeleza utamaduni wa kuamka asubuhi na mapema ni rahisi kufanikiwa.
Hili linatokeaje na kuna umuhimu upi sasa ambao unauweza kupata wakati unaamka asubuhi na mapema? Tafadhari usitoke hapo ulipo fuatana nasi katika makala haya tujifunze pamoja.
1. Inakusaidia kujenga nidhamu karibu ya kila kitu.
Zoezi la kuamka asubuhi na mapema mara nyingi linakusaidia wewe kujenga nidhamu karibu ya kila eneo lililo muhimu katika maisha yako. Nidhamu hiyo ni lazima utakuwa nayo tu.
Kivipi hilo , linawezekana? Hili linatokea hivi, kama umeweza kumudu kuacha usingizi wa asubuhi na kuamua kuamka asubuhi na mapema basi tambua hata nidhamu zingine basi ni wazi unaweza kujenga.
2. Inakusaidia kujiona ni mshindi.
Unapoamka asubuhi na mapema pia inakusaidia sana kujioa ni mshindi katika maisha yako. Kile kitendo cha kuamka asubuhi na mapama tu kinakupa picha kwamba kama vile umeshinda kitu cha kwanza katika siku hiyo.
Hivyo, kwa sababu hiyo utajikuta hata maeneo mengine katika siku yote utakuwa unafay kwa ujasiri kwa sababu ulishashida mapema kabisa baada ya kuamka asubuhi na mapema.
3. Inakusaidia kuweka vipaumbele vyako mapema.
Pia unapoamka asubuhi na mapema inakusaidaia kuweza kuipangilia siku yako mapema kwa kujua lipi uanze nalo na lipi usianze nalo. Unakuwa una pcha kubwa sana ya jinsi siku yako itakavyokuwa tofauti ungechelewa kuamka.
Mara nyingi asubuhi panakuwa pametuia hivyo ratiba hata za nini ufanye siku hiyo inakuwa ni rahisi kuweza kuzitekeleza na kuweza kufika mbali kimafanikio.
Kwa ufupi, hizo ndizo faida ambazo unaweza ukazipata ikiwa utakuwa na tabia ya kuamka asubuhi na mapema kila siku katika maisha yako.
Lakini hata hivyo kuamka asubuhi na mapema hakuwezi kuja kwa bahati mbaya tu, ni lazima kwanza uzingatie baadhi ya vitu ili uweze kumudu zoezi hilo.
Kwaznza, hakikisha kila siku unalala mapema.
Pili, mbali na kulala mapema hakikisha umejiwekea muda maalumu pia wa kulala, usiwe unabadilika badilika sana.
Tatu, pia hakikisha unaweka alamu ya simu ili kwa siku za mwanzoni kabla hujazoea ikusaidie kukujengea nidhamu binafsi.
Tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Endelea kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA kila siku kwa ajili ya mafanikio yako.
Kwa makala nyingine nzuri endelea kujifunza pia kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,