Habari rafiki?
Kila mtu kuna hatua fulani ambayo anataka kupiga kwenye maisha yake. Na wengi ni kuanzisha biashara au kukuza zile biashara ambazo tayari wanazo. Wengine ni kuondoka kwenye ajira ambazo wamekuwepo kwa muda mrefu bila ya kuona manufaa. Wengine ni kuanza vitu vya ndoto zao, kama kuandika vitabu, kuimba na sanaa nyingine.
Lakini kati ya kupanga na kuanza, huwa kuna ukinzani mkubwa sana. Huwa zinaibuka kila sababu ambazo zinaweza kuonekana ni sababu dhahiri kabisa zinazowazuia watu wasianze.
Sababu kubwa kwa wengi imekuwa ni kwamba hawapo tayari. Wengi wanajiona kuna kitu bado hawajakamilisha, na hivyo kusubiri mpaka wawe tayari. Ni hali hii ya kufikiri hawapo tayari ndiyo imewapoteza wengi. Na imewafanya baadhi ya watu kuahirisha maisha yao na kujikuta wanaendesha maisha ya mkumbo mpaka pale wanapoondoka hapa duniani.
Chukua mfano wa mtu ambaye anasema akimaliza masomo ataanza kuishi maisha ya ndoto yake. Anamaliza masomo ila kazi bado, anajiambia akipata kazi basi ataanza kuishi ndoto zake. Anapata kazi kweli, lakini anagundua hajajipanga na hivyo kujiambia akishajipanga atakuwa tayari kuanza. Katika kujipanga anaona au kuolewa, anajiambia sasa ana majukumu mapya, yakishakaa sawa ataanza. Kabla hajakaa sawa anapata watoto na majukumu ya kifamilia yanaongezeka. Hapa sasa anajiambia akishamaliza malezi ya watoto ataanza. Mpaka pale anamaliza malezi, muda unakuwa umeenda sana, na hivyo anajipa tumaini la mwisho, nikishastaafu nitaanza.
Je wewe upo kwenye hatua ipi ya sababu kati ya hizo hapo juu? Je kuna chochote unataka kufanya lakini umekuwa unaahirisha? Sasa mimi neno langu ni moja tu, ACHA MANENO WEKA KAZI.
Hakuna muda mzuri wa kuanza chochote zaidi ya sasa. Sasa una kila unachotaka ili kufika kule unakotaka. Na hata kama unaona kwa sasa huna, basi unapoanza kufanya na ukakomaa, dunia haina ujanja, itakupa tu kile unachotaka.
Angalia video ya somo la leo, ujue umuhimu wa kuanzia hapo ulipo sasa, na namna unavyoweza kuanza. Unaweza kuangalia kwa kubonyeza maandishi haya. Au pia unaweza kuangalia hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.
Kuangalia vipindi vyangu vingine zaidi bonyeza maandishi haya.
Kusikiliza vipindi vya sauti pia bonyeza maandishi haya.
Fanyia kazi haya unayojifunza ili maisha yako yaweze kuwa bora zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.