Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Kitu Ambacho Kitakuonyesha Kama Unafanikiwa Au Hufanikiwi Kwa Kitu Unachokifanya.

$
0
0
Kila mtu anatamani sana kuona akifanikiwa kwa lile jambo ambalo analifanya. Hakuna hata mmoja ambaye hatamani iwe hivyo katika maisha yake. Mafanikio yakuwa ya lazima sana kwa kila mmoja wetu.
Pamoja na nia hiyo njema bado hujikuta watu wengi wakiwa katika safari hii ya mafanikio wakiwa kama ni watu wakubahatisha bahatisha, hawajui kwamba watafanikiwa au la.
Kutokana na hil wengi hujikuta wakijiendea tu. Wanakuwa ni watu ambao kama wanasafiri, lakini hawajui kama safari yao itafika mwisho au la, inakuwa ilimrasdi tu wanaenda.
Sasa kwenye mafanikio, unatakiwa kiukweli ujue kama unafanikiwa au la. Hili sio suala la bahati au la kujiuliza sana nitajuaje kwamba hiki ninachokifanya kinakwenda kunipa mafanikio au hapana.
Kama unataka kujua hili, nitakuapa jibu, hii ni rahisi sana, kwa kawaida huwa kipo kitu kimoja tu ambacho kinakucfanya ugundue kwamba unafanikiwa kwenye jambo unalolifanya au hutaweza kufanikiwa tena.

Kitu pekee ambacho kitakufanya ujue jambo unalolifanya litafanikiwa kwa kiasi kikubwa au hapana ni hamasa uliyonayo kwa hicho unachokifanya. Angalia, hamasa uliyonayo ipo kwa kiasi gani.
Hamasa uliyonayo ndiyo inayopima unataka kufanikiwa kwa kiasi kipi? Kama hamasa yako ni kubwa uwe na uhakika hutakubali kushindwa maana hapo utatumia njia zote mpaka kuweza kufanikiwa.
Kama ni kujifunza, utajifunza, kama ni kuweka juhudi utaweka kila aina ya juhudi mpaka uone unafanikiwa. Sasa unapoanza tu kukosa hamasa elewa kabisa kushindwa kunaanza kujitokeza  kwa hicho unachokifanya.
Hata mwandishi Napoleon Hill katika kitabu chake cha ‘Think and Grow rich’aliwahi kuandika kwamba hamasa ni mwanzo wa mafanikio yote. Akiwa na maana hakuna mafanikio bila ya wewe kuwa na hamasa.
Ila usipate tabu na kuelewa juu ya hili, kwa mfano hapo ulipo ujiulize una malengo gani ambayo umejiwekea? Je, unayo hamasa kubwa ya kuona unafanikiwa. Ukiona una hamasa kidogo, jiandae kushindwa.
Kwa kawaida hamasa inachofanya kwako ni kuweza kukusukuma uweze kwenda mbele zaidi na kufanya tena na tena mpaka kuhakikisha unafanikiwa. Hamasa inakuwa kichocheo cha mafanikio yako.
Kila wakati unapoona hamasa huna hebu jipange upya na kuhakikisha unaipata na unaitumia kama daraja la mafanikio la kuweza kufanikiwa kwako kwa kila kitu ambacho unakifanya.
Najua unataka kujiuliza kwamba ina maana mtu akiwa ana hamasa na mafanikio ndiyo kesha yapata? HAPANA. Hamasa ni kitu cha kwanza katika safari ya mafanikio kinachokupa msukomo wa kufanikiwa na tena vitu vingine vinafuata.
Ila bila kuwa na hamasa hivyo vyote vitu vingine ni kazi bure. Kwa mfano tunaona huwezi kufanikiwa bila kuwa na nidhamu binafsi, sasa nidhamu binafsi haiwezi kufanya kazi kama tayari umekosa hamasa.
Kwa vyovyote vile iwavyo unalazimika kwanza kuhamasika ili uweze kujenga mafanikio yako makubwa. Hapa ndipo ilipo siri ya kujenga mafanikio makubwa. hutakiwi kukwepa katika hili hata kidogo, ni lazima uanze na kuhamasika.
Unataka kujua kitu hicho kinakupa mafanikio au hakikupi mafanikio, rafiki yangu, chunguza hamasa uliyonayo kila wakati na kufanya mabadiliko mapema sana kama hamasa  yako iko chini.
Fanyia kazi hilo na chukua hatua kubwa ya kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
Kwa makala nyingine za maisha na mafanikio, tembelea pia dirayamafanikio.blogspt.com kupata maarifa bora ya kubadilisha maisha yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
dirayamafanikio.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles