Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

ONGEA NA KOCHA; Kama Mimi Ningekuwa Wewe, Lazima Ningefanya Hivi Ili Niweze Kufanikiwa Zaidi.

$
0
0
Rafiki yangu,

Moja ya vitu ambavyo nashukuru kuvijua mapema kwenye maisha yangu, ni ukweli kwamba maisha ni kuchagua, unavyoishi, unachagua mwenyewe, iwe ni kwa kujua au kwa kutokujua. 

Unachagua mwenyewe pale unapojua nini unataka, na unajikuta umechagua bila ya kujua pale ambapo upo upo tu na kufuata ya wengine.
 

Nilipojua maisha yangu ni kile ninachochagua mwenyewe, basi nilichagua kuishi maisha ya mafanikio. Hivyo tu. Niliamua kama nachagua namna ya kuishi, basi nachagua kuishi namna bora itakayopelekea mimi kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yangu. Hivyo nikaweka ndoto na maono yangu na kila siku nayafanyia kazi.

Moja ya hitaji la msingi kabisa la maisha ya mafanikio ni kujifunza kila siku, na kuchukua hatua pia. Hivyo nimekuwa najifunza kila siku, na kuchukua hatua kwenye yale ambayo najifunza. Na pia nimewakaribisha wale wanaopenda kujifunza kila siku, tujifunze pamoja kupitia KISIMA CHA MAARIFA. Na kupitia KISIMA tumekuwa tunajifunza mengi kila siku, na kupiga hatua ndogo ndogo kuelekea kwenye mafanikio yetu.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Sasa leo rafiki yangu nakuandikia kwamba kama ningekuwa wewe, najua siwezi kuwa wewe, lakini kuna wakati naangalia watu ambao wanawasiliana na mimi kwa mambo mbalimbali, na kusema laiti huyu angefanya hivi, laiti angechukua hatua hata, angekuwa mbali zaidi kwa sasa.



Wakati naanza kazi hii ya kuandika, kushauri na kufundisha, watu wengi sana walipenda tuonane kwa ajili ya kuwashauri moja kwa moja. Na mimi nilifurahia sana jambo hilo, kwa sababu nilijua nawasaidia wengi, na moja ya falsafa zangu ni kwamba kadiri ninavyowasaidia wengi kupata kile wanachotaka, ndivyo na mimi napata kile ninachotaka. Hivyo nikawa nakutana na watu wengi, tunashauriana na nafarijika sana.

SOMA; Kitu Kimoja Unachohitaji Ili Kufanikiwa Kama Unaanzia Chini Kabisa.

Nilikuja kustushwa sana pale nilipokuwa narudi kuwafuatilia kujua ni hatua gani wamechukua, wengi unakuta wameshasahau hata tuliongelea nini. Wanakuwa na sababu nyingi kwa nini hawajachukua hatua. Na hapa ndipo nilipogundua kwamba kumbe sikuwa nasaidia chochote, badala yake nilikuwa napoteza muda ambao ningeweza kuwa naandaa makala nyingine nzuri kwa wengi zaidi. Hivyo niliachana na utaratibu ule mara moja, na kuweka gharama za kuonana kwa ajili ya ushauri, hapa sasa mtu anataka muonane kwa haraka sana, unamwambia sawa, ukimwambia zipo gharama anakuambia sawa nitakutafuta, na hutamsikia tena. Sasa hii inakuwa njia nzuri ya kuwachuja wale ambao wapo makini na wanajua nini wanataka, na wale ambao wamehemka tu na kile walichosoma na kupata mawazo ya haraka kwamba kama nikimtafuta huyu bwana tunaweza kuongea kitu.

Pamoja na hilo la kulipia gharama za ushauri, pia nimekuwa napenda mtu ninayemshauri tuendelee kuwa karibu, ili nijue anaendeleaje na hatua anazochukua. Watu ambao nipo nao karibu zaidi, ni wale waliopo KISIMA CHA MAARIFA, hawa ndiyo tunaowasiliana kila siku na kujifunza mambo mazuri kila siku.

Sasa hapa ndipo nataka kukuambia kama ningekuwa wewe ningefanya nini.

Kama mimi ningekuwa wewe rafiki yangu, ningejiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tunakuwa karibu, hivyo tunaweza kuwasiliana kwa jambo lolote ambalo unahitaji ushauri kutoka kwangu. Na kila siku unaendelea kujifunza mambo mazuri zaidi.

Lakini wengi wanapenda kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kama ingekuwa bure, siyo bure kujiunga, kuna gharama, na wengi wamekuwa wanapenda kujiunga lakini gharama hawaziwezi.

Na hapa pia nataka kukuambia kama ningekuwa wewe ningefanya nini.
Ada ya KISIMA ni tsh elfu 50 kwa mwaka, ukigawa hii kwa mwezi ni kama shilingi elfu nne. 

Sasa mimi ningesoma makala nyingi niwezavyo kwenye AMKA MTANZANIA, ambapo zipo makala nyingi na zote ni bure. Kila ninachosoma ningekifanyia kazi haraka sana, na ningeanza zoezi la kuweka akiba, kila siku naweka angalau elfu moja, nikishindwa basi mia tano, au nikishindwa kabisa, napambana kile mwezi niwe na elfu kumi, au kama kila kitu kimegoma kabisa, basi nahakikisha nimeweka elfu tano. Nafanya hivi kwa mwaka mmoja, situmii hiyo hata kidogo. Hapo nakuwa najijengea tabia ya kuweka akiba, ambayo ni muhimu sana kwenye maisha na wengi hawaiwezi, pia najijengea nidhamu ambayo ni msingi wa mafanikio na wengi hawana.

Baada ya mwaka mmoja, ningejiunga na KISIMA CHA MAARIFA, na kuhakikisha najifunza zaidi kila siku na kutoka pale ambapo nipo.

Huu ni ujanja tu ambao nimekupa. Kwa sababu kila siku napokea maombi mengi ya ushauri wa biashara na mambo mengine muhimu, na mimi siwezi kujibu yote kwa sababu najua mengi hayatafanyiwa kazi, na huenda tusiwasiliane tena na mtu huyo. Lakini anapokuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, tunawasiliana kwa urahisi.

Hivyo nimalize kwa kusema rafiki, kama unahitaji ushauri wowote kutoka kwangu, kwanza jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, hapo nitajua kweli upo makini na utafanyia kazi kile nitakachokuambia, pia nitaweza kukufuatilia kwa karibu.

Pia kujua zaidi kwa undani kuhusu huduma zote ninazotoa, angalia video hii kwa kubonyeza maandishi haya.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ada ya kujiunga, tsh 50,000/= kwa namba 0755953887 au 0717396253 kisha tuma ujumbe kwa njia ya wasap, namba 0717396253 ili upate maelekezo ya kujiunga.

Nakukaribisha sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>