Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri katika kutimiza majukumu yako ya kila siku. Mpendwa rafiki, endelea kutimiza majukumu yako na yapende majukumu yako kwani majukumu ni sehemu ya maisha yako ya kila siku huwezi kuyakwepa. Ukikwepa majukumu yako ni sawa na kukwepa maisha yako sasa kama wewe ni binadamu ambaye uko hai endelea kupambana na maisha bila kukata tamaa.
Mpendwa msomaji, hongera sana kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo basi, tunaalikwa sisi sote kuweza kutumia vizuri muda wetu. Na mafanikio yetu yote yanapatikana katika matumizi ya muda. Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kuweza kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja.
Mpendwa msomaji, katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja sehemu ya kuogopwa sana kwenye karni hii ya ishirini na moja (21). Kwa hiyo, ili uweze kujua ni sehemu gani hiyo ya kuogopwa katika karni ya ishirini na moja nakusihi sana rafiki tuweze kuambatana wote kwa pamoja mwanzo hadi mwisho wa somo letu la leo.
SOMA; Kama Unataka Mafanikio Makubwa Katika Maisha Yako, Acha Kuogopa Kufanya Mambo Haya.
Kuna kitu katika maisha yetu ambacho hakiwezi kukwepeka nacho ni mabadiliko. Mabadiliko ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku kwanza kabisa mabadiliko yalikuwepo, yatakuwepo, na yataendelea kuwepo. Hapo zamani tulikuwa katika zama za mawe, zikaja zama za chuma, zama za mapinduzi ya viwanda na kwa sasa tupo za taarifa. Kwa hiyo, tunaona ni jinsi gani dunia inavyobadilika kila siku.
Kumbe basi, bila mabadiliko yoyote yanayotokea hapa duniani hakuna maendeleo. Kama isingekuwa mabadiliko yaliyoweza kutokea wakati wa nyuma leo hii mimi na wewe tusingeweza kuwasiliana na kusoma makala hii unayoisoma hapa. Mpendwa msomaji, sasa turudi katika kiini cha somo letu la leo baada ya kupata muhtasari mfupi juu ya mabadiliko hapa duniani.
Mpendwa msomaji, sehemu ya kuogopwa sana kwenye karni ya ishirini na moja (21) ni kuogopa sehemu ambayo haina mabadiliko. Kwa kweli licha ya dunia kuwa na mabadiliko mengi yanayoendelea kutokea bado kuna watu wanaendelea kuishi katika mfumo wa zama za huko nyuma. Zipo sehemu nyingi za kuogopwa sana katika karni hii ya ishirini na moja (21) kwanza kabisa ni watu ambao ni sisi wenyewe. Waogope watu wanaokataa kwenda na mabadiliko yanayoendelea kutokea hapa duniani. Waogope watu wanaoendelea kuishi yale maisha ya karni iliyopita, zama zilizopita mpaka leo hii tupo karni ya ishirini na moja. Waogope watu ambao hawataki kubadilika kimaendeleo katika nyaza zote unazozijua wewe.
SOMA; Mambo 6 Unayalazimika Kuyaacha Mara Moja Ili Kufanikiwa.
Rafiki, ziogope taasisi zinazoendelea kuwepo ambazo hazina mabadiliko yoyote tangu ilipoanzishwa mpaka leo. Zipo taasisi ambazo zinaendelea kung’ang’ania ile mifumo ya zamani ya kutolea huduma badala ya kwenda na mabadiliko. Sehemu ambayo haina mabadiliko ni dalili tosha ya kuwa watu wa sehemu hiyo hawana mabadiliko yaani hawakui.
Mpendwa msomaji, ndio maana nakusihi sana kuogopa sehemu ambayo haina mabadiliko yoyote. Sehemu ambayo haibadiliki miaka yote hata maendeleo yake ni yanakuwa ni yale yale ya kawaida. Hakuna maboresho yoyote yanayotokea na watu wanaendelea kukaa na kuridhika na matokeo waliyokuwa nayo. Mtu au taasisi ambayo haitaki kwenda na mabadiliko ni wale watu au taasisi iliyochagua kubaki hapo hapo ilipo.
Mpendwa rafiki, kama una rafiki ambaye hataki kubadilika au habadiliki muogope sana, kama una mwenza ambaye habadiliki muogope, kama unafanya kazi katika taasisi ambayo haibadiliki basi iogope hiyo taasisi. Kuwa sehemu ambayo haitaki kubadilika au kuwa na watu ambao hawataki kubadilika ni mzigo mkubwa sana kwa mtu aliyechagua kuamka na kubadilika.
Hatua ya kuchukua leo, kama uko katika sehemu ambayo haitaki kubadilika ondoka na tafuta sehemu ambayo inataka kubadilika. Kama umeshindwa kuondoka basi, kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona sehemu hiyo husika. Kama umezungukwa na watu ambao hawataki kusikia kuhusu mabadiliko waogope, wakimbie na tafuta watu sahihi wanaoweza kuendana na ndoto yako. Kama unataka mabadiliko lazima uamue kuwa na watu walioamua kwenda na mabadiliko.
Kwa kuhitimisha, tunahitaji mabadiliko kila siku ili tuweze kuijenga dunia. Kuendelea kuwa na watu wachache ambao hawataki kusikia kuhusu mabadiliko ni kuendelea kujirudisha nyuma wewe mwenyewe. Kuwa na watu sahihi ambao wanaweza kukupa mwanga wa kule unakotaka kwenda.