Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Mwaka Mpya Mambo Mapya Ni Uongo, Epuka Kupoteza Mwaka Wako 2017.

$
0
0


Moja ya misingi ninayoifuata kwenye maisha yangu ya kila siku ni huu; kama kitu kinafanywa na kila mtu, basi siyo kitu sahihi kwa mtu makini kufanya. Unaweza usikubaliane nao, lakini umekuwa unaniwezesha kuepuka vitu ambavyo ni vya kupoteza muda, na kunisukuma kufanya makubwa na siyo mazoea pekee.
 

Vitu vinavyofanywa na kila mtu ni vitu rahisi, vitu ambavyo havina changamoto. Hii ni kwa sababu watu wengi ni wavivu, watu wengi hawapendi kujisumbua na watu wengi wanapenda njia rahisi na ya mkato. Lakini tangu kuanza kwa misingi ya dunia, hakuna jambo la thamani limewahi kuwa rahisi, limewahi kupatikana kwa njia ya mkato.

Tukiangalia historia ya dunia, wote ambao wameweza kufanya mambo makubwa, ni wale ambao walikataa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Katika mambo yote makubwa yaliyowahi kufanyika hapa duniani, ni watu wachache waliyaanzisha na kuyaamini, huku wengine wengi wakiwacheka na kuwashangaa, kwa nini wanahangaika na mambo magumu wakati maisha ni rahisi?

Tukiangalia vinaja waliogundua usafiri wa anga, walichekwa sana, watu waliwashangaa kwa nini wanahangaika na vitu vigumu wakati upo usafiri wa uhakika wa reli. Waliokuwa kwenye usafirishaji wa reli walijua huo ndiyo usafiri wa uhakika. Lakini vijana wale hawakukata tamaa licha ya kukosa kuungwa mkono, waliendelea na hatimaye leo tuna usafiri wa anga ambao umefanya usafiri kuwa rahisi mno.

Tuliangalia utengenezaji wa kompyuta binafsi (personal computer) miaka ya nyuma kila mtu alishawishika kwamba hakuna mtu atakayehitaji kompyuta nyumbani kwake. Kompyuta zitabaki kwenye taasisi kubwa za kisayansi na serikali. Walipotoka watu na kuanza harakati za kuhakikisha kila mtu anaweza kuwa na kompyuta nyumbani kwake, watu waliwashangaa, kwa sababu hawakuona uhitaji kwa kipindi hiko. Lakini sasa hivi karibu kila mtu ameshatumia kompyuta kwenye mazingira ambayo siyo ya kiofisi.

Yote haya nataka nikuoneshe namna gani kundi kubwa la watu limekuwa linapotea na kuwapoteza wengine.
Siku chache zijazo, kauli itakayotawala kila mahali itakuwa hii; MWAKA MPYA, MAMBO MAPYA. Leo bila ya kupepesa macho nataka nikuambie tu kwamba kauli hiyo ni ya uongo. Na kitu pekee kinaibeba kauli hiyo iendelee kuwepo kila mwanzoni mwa mwaka ni kwa sababu inawabembeleza wazembe wengi. Wale ambao hawapo tayari kukaa chini na kusuka mwaka wanaokwenda kuanza, wamekuwa wakijiambia mwaka mpya mambo mapya na kuridhika kwamba tayari mwaka mpya ni bora kwao.

Leo tutakwenda kuliangalia hili kwa undani ili tuweze kujua hatua sahihi kuchukua ili mwaka 2017 uwe bora sana kwetu.

Moja. Mwaka mpya siyo kitu kipya.

Mwaka mpya unapoanza, hakuna kitu kipya kabisa kinachotokea kwenye dunia. Jua litaendelea kuchomoza mashariki na kuzama magharibi. Majira ya mwaka yataendelea kujirudia kama ambavyo yamekuwa yanajirudia kila mwaka.

Mbili. Mwaka mpya ni kipimo cha muda wa maisha yetu.

Hivyo tunavyohesabu miaka, maana yake tunaangalia tulikotoka na wapi tunaenda. Tunatumia miaka kuangalia ni vitu gani tunafanya, ni hatua zipi tunapiga na tunatumiaje muda wetu.

Tatu. Upya wa mwaka ni mipango na matendo yako.

Hivyo basi, upya wa mwaka siyo ile namba inayosomeka, kwamba ilikuwa 2016 na sasa ni 2017. Bali upya wa mwaka ni ile mikakati yako mipya, yale matendo ya tofauti unayokwenda kufanya kwenye mwaka husika, ili kufanya makubwa zaidi.
Na hapa ndipo wengi wanaposhindwa, na kubaki na kauli mwaka mpya mambo mapya.

Changamoto za kauli mwaka mpya mambo mapya.

Kauli hii imekuwa haichochei matendo mapya kwa watu, hii ni kwa sababu watu wamekuwa hawaisemi kwa kumaanisha, bali wanaisema kwa sababu kila mtu anaisema. Hivyo watu wanaweza kufikiria mambo mapya ya kufanya kwenye mwaka husika, lakini haichukui siku nyingi, unawakuta wamerudi pale pale.

Kila mwanzo wa mwaka watu wamekuwa wanajiahidi vitu vingi mno, lakini mwezi wa kwanza hauishi, unakuta watu wanaendelea na maisha yao waliyoyazoea.

Nenda sehemu za kufanya mazoezi leo mwezi wa kumi na mbili, na utakuta zipo tupu kabisa. Ila nenda mwanzoni mwa mwezi wa kwanza na utakuta zimejaa kabisa. Nenda tena mwezi wa pili au watatu, na utakuta zipo tupu kabisa.

Tunawezaje kuboresha kauli hii ya mwaka mpya mambo mapya ili itunufaishe?

Kama nilivyosema awali, kama kitu kinafanywa na kila mtu, usikifanye, unapoteza muda wako. Hivyo basi, kwa namna yoyote ile usijiambie au kuwapigia kelele wengine kwamba mwaka mpya mambo mapya. Badala yake kaa chini na suka mikakati ya mwaka mpya 2017, chagua hatua za kwenda kuchukua 2017, na ongeza viwango vyako kwa mwaka 2017. Baada ya hapo anza kufanyia kazi, fanya haya sasa na wala usisubiri mpaka mkesha wa mwaka mpya, pale ndipo wengi wanapotea zaidi.

Usiwe mtu wa maneno na kelele, bali kuwa mtu wa kuchukua hatua. Na huhitaji kuanza na hatua kubwa kama ambazo wengi wamekuwa wanapanga halafu wanashindwa kutekeleza. Angalia ni yapi mazuri umefanya mwaka 2016 na yaboreshe zaidi. Angalia wapi ulikosea 2017 na usirudie makosa hayo.

Karibu kwenye semina ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA KUWEKA MALENGO.

Kama ilivyo kwenye kauli mwaka mpya mambo mapya, kuweka malengo ya mwaka mpya ni uongo mwingine ambao umekuwa unawapoteza wengi. Mwaka mpya 2017 tunakwenda kuanza mwaka kitofauti kabisa, hakuna kuweka malengo, badala yake tunatengeneza mfumo wa mafanikio kwenye maisha yetu. Uzuri wa mfumo ni kwamba ukishausuka basi wewe ni kuufuata tu. Hakuna tena kujiuliza sasa hapa nafanya nini, mfumo unaeleweka, wewe unaweka juhudi na kuvuna mafanikio.

Kama ungependa kushiriki semina hii ya kipekee kwa mwaka 2017, na uuanze mwaka 2017 kwa utofauti, bonyeza maandishi haya kupata maelekezo.

Kwa vyovyote vile rafiki yangu, nakusihi sana usifanye jambo lolote kwa mazoea, hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka. Fanya jambo ambalo umelitafakari na unajua ni muhimu kabisa kwako. Usifanye kitu kwa sababu tu kila mtu anafanya, au kwa sababu umekuwa unafanya. Fanya kitu ambacho kina maana kwako, na unaweza kuweka juhudi kupata matokeo makubwa zaidi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>