Mawasiliano ni moja ya misingi muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Na pia ni moja ya mahitaji muhimu kama tunataka kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote ambalo tunalifanya. Kumbuka ya kwamba chochote unachotaka kinatoka kwa watu wengine, hivyo jinsi unavyoweza kuwashawishi na wakakubaliana na wewe ndivyo itakuwezesha kupata unachotaka. Na ushawishi unaanzia kwenye mbinu bora za mawasiliano ambazo mtu anakuwa nazo.
Watu wengi wamekuwa wakiwasukuma wengine ili kupata kile wanachokitaka. Na wamekuwa wakifanya hivi kwa kubishana, kutisha, kudanganya na hata kulaghai ili wapate wanachotaka. Kwa njia hizi inakuwa vigumu zaidi kwa watu kuwa tayari kutoa kile ambacho wengine wanakitaka. Ni kutokana na changamoto hii Daktari na Mwanasaikolojia Mark Goulston alipokuja na kitabu ambacho kina mbinu bora za ushawishi ambazo zinamwezesha mtu kupata kile anachokitaka kutoka kwa mtu yeyote. Daktari Mark anatumia taaluma yake na uzoefu wake kwenye kazi ya ushauri katika kutushirikisha mambo haya muhimu ya kuzingatia kwenye mawasiliano yetu.
Karibu tujifunze kwa pamoja;
1. Kila mtu ana mahitaji yake, matamanio yake na pia ajenda zake. Kila mtu ana siri yake ambayo anaificha, ambayo hataki wengine waijue. Na pia kila mtu yupo bize, ana msongo wa mawazo, na hana muda wa kumtosha kufanya kila anachotaka kufanya. Ili kuweza kwenda na hayo yote yanayoendelea kwenye maisha yake, mtu anajitengenezea ukuta ambao bila ya kujua hayo huwezi kumshawishi kwa jambo lolote. Kabla hujataka mtu afanye au akupe chochote unachotaka, anza kwanza kuvunja ukuta huu ambao kila mtu amejijengea.
2. Ushawishi unaenda kwa mzunguko ambao una hatua tano muhimu. Yaani kabla mtu hajashawishika kufanya chochote unachomwambia, anapitia hatua hizi tano ambazo unatakiwa kuzijua na kujua jinsi ya kumpitisha mtu kwenye kila hatua;
Hatua ya kwanza ni kumtoa mtu kwenye kukataa mpaka kuwa tayari kusikiliza. Wakati wowote mtu yupo kwenye hali ya kukataa, unahitaji kuwa na mbinu ya kumfanya akusikilize.
Hatua ya pili ni kumtoa kwenye kusikiliza mpaka kukufikiria. Hapa mtu anakuwa amesikiliza kile ulichomwambia, na kuna mbinu bora za kumwambia na akaanza kufikiria kwamba anaweza kufanya au anaweza kuwa tayari.
Hatua ya tatu ni kumtoa kwenye kufikiria mpaka kuwa tayari kufanya. Baada ya mtu kufikiria kwamba anaweza kufanya anashawishika zaidi na kuwa tayari kufanya.
Hatua ya nne ni kumtoa kwenye kuwa tayari kufanya mpaka kufanya. Hapa ndipo mtu anapofanya kile ambacho unataka afanye au anakupa kile ambacho ulitaka akupe.
Hatua ya tano ni kumtoa kwenye kufanya mpaka kufurahia kufanya na kuendelea kufanya. Kufanya siyo mwisho wa mzunguko huu, bali mtu anahitaji kufurahia kwamba amefanya na kuendelea kufanya kadiri inavyohitajika.
Huu ndio mzunguko wa ushawishi ambao unatakiwa kuujua na jinsi ya kuutumia kwa watu mbalimbali. Utajifunza hayo kwenye kitabu hiki.
3. Ili uweze kuwa na ushawishi kwa wengine unahitaji kuujua vizuri ubongo wa binadamu. Ubongo wa binadamu umegawanyika kwenye sehemu kuu tatu ambazo zinatofautiana kwa miaka ambayo zimekuwepo.
Sehemu ya kwanza ni ubongo wa chini ambao una tabia kama za mjusi. Hii ni ile sehemu ya ubongo ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha unaishi (kwa kiingereza survival). Ubongo huu kazi yake ni kuhakikisha umepata chakula na unaweza kujikinga na hatari. Ubongo huu huwa unachukua hatua haraka bila hata ya kufikiri kwa kina. Kwa mfano kama umewahi kuwa kwneye hatari kama kukimbizwa na mnyama kama mbwa utakua umeona unapata nguvu nyingi hata za kuruka ukuta ambao kwa kawaida huwezi kuuruka, hii ndiyo kazi ya ubongo huu. Kwa kiingereza wanasema FIGHT-OR-FRIGHT.
Sehemu ya pili ni ubongo wa kati, ambao una tabia za mnyama. Hii ni sehemu ya ubongo ambayo imebeba hisia zote za mtu. Hisia za upendo, furaha, huzuni, hasira, maombolezo, wivu na hata raha zipo kwenye sehemu hii ya ubongo. Sehemu hii ya ubongo ndiyo inatusukuma kufanya vitu vinavyotupa hisia nzuri na kutuepusha na vitu vinavyoleta hisia mbaya.
Sehemu ya tatu ni ubongo wa juu ambao una tabia za utu. Huu ndio ubongo ambao unatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine wote. Huu ndiyo ubongo ambao unafikiri kwa kina kwenye kila jambo tunalofanya au linalotokea. Huu ndio ubongo ambao unatunza kumbukumbu. Ubongo huu unakusanya taarifa kutoka kwenye sehemu nyingine za ubongo na kufanya maamuzi sahihi.
4. kwa bahati mbaya sana, watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi kwa kuongozwa na ubongo wa chini na ubongo wa kati. Ni mara chache sana watu wanaweza kuutumia ubongo wa juu vizuri na kufanya maamuzi bora. Maamuzi mengi yanayofanywa na ubongo wa chini na wa kati ni maamuzi ambayo yana faida ya muda mfupi lakini kwa muda mrefu yana hasara kwao. Mfano ni mtu ambaye anabaka, hapa anauridhisha ubongo wa kati ambao utapata raha, lakini angetumia ubongo wa juu angeona siyo kitu sahihi kwake kufanya.
5. Ili uweze kumshawishi mtu yeyote, hakikisha unaongea naye akiwa kwenye ubongo wa juu. Kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu, hakuna kitu unachoweza kumwambia akakusikia na kukuelewa. Haijalishi utatumia mbinu bora kiasi gani, kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu, unapoteza muda wako.
Hii ndiyo maana ni vigumu sana kumshauri mtu ambaye ana hasira, au aa furaha au yupo katikati ya hisia kali za mapenzi. Kuweza kumshawishi mtu mtoe kwanza kwenye ubongo wa kati na wa chini na mpeleke kwenye ubongo wa juu ambapo anaweza kufikiri sawasawa.
SOMA; KITABU; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.
6. Adui wa kwanza wa wewe kuwashawishi wengine ni wewe mwenyewe. Ili uweze kuwashawishi wengine ni lazima wewe ushawishike kwanza. Ni lazima wewe ukubaliane na kile unachotaka wengine wafanye au wakupe. Ni lazima uweze kujidhibiti mwenyewe ili kuweza kuwashawishi wengine kuchukua hatua ambayo unajua ni muhimu kwao.
7. Ondoa chujio ambalo tayari unalo. Kila mmoja wetu ana chujio ambalo anatumia kuwachuja wengine kwa kadiri wanavyoonekana au walivyowazoea. Hivyo tunawapanga watu kwenye makundi kwa kufikiri tunawajua sana. Ili kuweza kuwa na ushawishi kwa wengine kwanza ondoa chujio hili na mwendee kila mtu bila ya kumhukumu, kuwa tayari kujifunza zaidi kutoka kwake. Usimweke mtu kwenye upande wowote, badala yake msikilize yeye kama yeye na hapa utaona njia bora za kuweza kumshawishi.
8. Kila kitu ambacho mtu anafanya, kuna sababu inayomsukuma kufanya. Hakuna mtu anayefanya kitu kwa ajali au kwa bahati mbaya pekee. Hivyo unapokutana na tatizo au changamoto kutoka kwa wengine, jua kuna kitu kimewasukuma kufanya walichofanya. Ili uweze kuwashawishi watu, jua ni kitu gani kinawasukuma wafanye kile ambacho wanafanya sasa na ni jinsi gani unaweza kuwafanya kuacha wanachofanya sasa na wafanye kile ambacho unawashawishi wafanye.
9. Mfanye mtu ajisikie ameeleweka. Ni lazima umwelewe mtu kabla hujataka kumshawishi afanye chochote unachotaka afanye. Jaribu kuvaa viatu vyake na mweleze wazi ya kwamba unaelewa kwa nini yupo pale alipo sasa. Na hata kama anafanya kitu ambacho anakosea, mwelewe kwamba kuna kitu kinasababisha yeye afanye hivyo. Usione kwamba yeye hayupo sahihi na kumweleza hivyo, ukienda kwa njia hiyo atakachofanya ni kujitetea na hutaweza kumshawishi kwa njia yoyote ile. Mwelewe mtu na atafunguka kwako.
10. Kama unataka wengine wajali kuhusu wewe, anza kujali kuhusu wao kwanza. Moja ya njia muhimu za kuweza kuwashawishi watu ni kuwafanya wavutiwe na wewe, wajali kuhusu wewe na hivyo wawe tayari kufanya kile ambacho unawaambia wafanye. Lakini hii haitakuja kwa wewe kukazana watu wavutiwe na wewe na wajali kuhusu wewe. Badala yake inakuja pale unapoanza kujali kuhusu wengine, na unapovutiwa na wengine.
Hivyo unapokutana na watu, usitumie nafasi hiyo kujisifia zaidi wewe, badala yake tumia nafasi hiyo kutaka kuwajua zaidi. Jua ni mambo gani wanafanya, changamoto gani wanapitia, yapi wameweza kukamilisha. Kadiri unavyojali kuhusu wao wanaanza kufunguka kwako na watakuwa tayari kufanya kile unachotaka wafanye.
11. Wafanye wengine wajione ni wa thamani. Hii ni mbinu muhimu sana unayotakiwa kuwa nayo kama unataka kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani. Hakuna kitu ambacho mtu anapenda kama kuona amethaminiwa. Hii ndiyo maana watu wanapenda kuitwa mheshimiwa, bosi, mtaalamu, bingwa, na majina mengine yanayoonesha sifa za watu. Mfanye mtu aone ana mchango mkubwa kwenye kile anachofanya na kile unachotaka afanye ataweka mchango mkubwa pia. Kuwafanya watu wa thamani ni zawadi kubwa sana unayoweza kuwapa.
12. Epuka kueleweka tofauti na unavyotaka ueleweke. Katika harakati zako za kuwashawishi wengine, unaweza kuwa unatoa picha ya kinyume kabisa na kile ulichokuwa unataka kutoa wewe. Kwa mfano unataka watu wakuone wewe ni mwenye husara lakini kwao unaonekana ni mpumbavu. Au unataka wakuone ni mwaminifu ila wao wanakuona ni tapeli. Hali hii huwa inatokana na mtu kutokujiandaa vizuri na kutosikiliza wale ambao anataka kuwashawishi. Unahitaji kuwafuatilia kwa makini watu na kuona wanapokeaje kile ambacho unawapatia.
13. Kuna vitu vitatu ambavyo vinawasukuma watu kuchukua hatua, ukiweza kuvitumia vizuri vitu hivi utaweza kuwashawishi watu iwe ni kwenye kazi, biashara na hata kwenye familia.
Kitu cha kwanza ni mapenzi, hamu au shauku. Watu wapo tayari kufanya kile ambacho wanapenda kufanya na wana shauku kubwa ya kukifanya. Hivyo angalia ni kitu gani watu wanapenda na kitumie katika ushawishi wako.
SOMA; Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.
Kitu cha pili ni hamasa. Watu wanapokuwa na hamasa wanakuwa tayari kuchukua hatua kwenye jambo lolote ambalo wanalipenda. Wafanye watu wahamasike kwenye kile ambacho unataka wafanye.
Kitu cha tatu ni fahari, watu wanaona ufahari pale wanapoona wamekuwa na mchango kwenye jambo fulani. Watu wanapoona kile walichofanya kina mchango kwa wengine wanafarijika sana.
Tumia vitu hivi vitatu kwa pamoja na utaweza kuwashawishi watu kuchukua hatua.
14. Uaminifu ni muhimu sana katika kuwashawishi wengine. Huwezi kuwashawishi watu kama hawakuamini na watu hawawezi kukuamini kama husemi ukweli na kutekeleza kile unachoahidi. Usiwe na haraka kwenye ushawishi wako, badala yake jenga mahusiano yenye uaminifu, kadiri watu wanavyokuamini, kutokana na matendo yako na siyo maneno tu, ndivyo wanavyokuwa tayari kukubaliana na wewe.
EPUKA WATU HAWA WA AINA TANO.
Japokuwa lengo la kitabu hiki ni kukupa mbinu za kuweza kuwashawishi watu, kuweza kuwafanya wakubaliane na wewe, kuna watu ambao hawashawishiki na wala hawawezi kukubaliana na wewe kwa lolote. Hawa ni watu ambao ni sumu kali na njia pekee kwako ni kuwaepuka haraka sana. Watu hawa wanajiangalia wao wenyewe sana na hivyo hawawezi kuwa tayari kufanya kitu ambacho kitawanufaisha wengine. Watu hawa wanaongozwa zaidi na ubongo wa chini na wa kati. Watu hao wa aina tano ni kama ifuatavyo;
15. AINA YA KWANZA; Watu ambao ni wahitaji na wategemezi kwako moja kwa moja (needy people). Hawa ni watu wazima, wenye nguvu zao na akili zao lakini wanakuchagua wewe ndiyo ubebe matatizo yao. Wanakuambia wazi kabisa bila ya wewe wao hawawezi kuishi na hivyo wanakutegemea kwa kila kitu. Hata maamuzi madogo ambayo wangeweza kufanya wenyewe hawafanyi mpaka wakusubiri wewe.
Kama ingekuwa hivi tu wala isingekuwa shida, ila tatizo kubwa la watu hawa ni kwamba wanapenda kulalamika na watakulalamikia kwa kila kitu. Hata uwasaidie kiasi gani, ukikosea kidogo watakulalamikia kwamba umeharibu siku yao au maisha yao. Watataka wewe uache kila unachofanya ushughulikie matatizo yao na ukishindwa kufanya hivi watakulaumu kwamba huwajali.
Hawa ni watu ambao dakika moja watakuambia wewe ndiyo msaada mkubwa kao, na dakika inayofuata watakuambia wewe ndiyo umeharibu maisha yao.
Suluhisho; wakimbie haraka sana watu hawa, kaa nao mbali maana huwezi kuwasaidia kwa lolote. Haijalishi ni ndugu, rafiki au mtu gani, kama amekuwa na tabia hii na ukamweleza lakini habadiliki, kimbia haraka sana.
16. AINA YA PILI; Watu ambao ni waonevu (bullies). Katika maisha yako utakutana na watu ambao ni waonevu, na watakuonea sana. Hawa ni watu ambao wanataka wewe ufanye kile ambacho wanataka wao iwe unataka au hutaki. Hawajali kuhusu wewe wanachojali ni wao wenyewe. Na hawa watakuja wengi kuanzia ndugu, wenza, waajiri na hata washirika kwenye biashara.
Watu ambao ni waonevu wana tabia moja, huwa wanaenda kwa wale watu ambao wanaonekana ni wanyonge. Hivyo njia ya kuwaepuka hawa ni kukataa kuwa mnyonge. Usikubaliane kabisa na kile ambacho watu wanakulazimisha kufanya, hata kama ni mtu gani. Na waambie wazi kwamba hukubaliani na hilo na wakiona wewe ni mgumu watahamia kwa wengine. Kama ni mwajiri anakuwa mwonevu kwako, tafuta kazi nyingine.
17. AINA YA TATU; Watu ambao ni wapokeaji na wachukuaji tu(TAKERS). Hawa ni watu ambao wanajiangalia wao wenyewe tu, kila mara wanakuja kwako na shida ambayo wanataka uwasaidie na wanalalamika sana. Lakini siku wewe una shida ukiwaendea wana kila sababu ya kwa nini hawawezi kukusaidia. Watu hawa wanaona kama wao ndio wanastahili zaidi ya wengine. Watu hawa ni hatari sana kwako kwani wanaweza kuharibu mipango yako na ratiba zako kwa jinsi wanavyokuja na shida zao.
Njia ya kuondokana na watu hawa ni kuwa na kitu ambacho unataka wakufanyie. Pale anapokuja na kitu unataka umsaidie, mwambie sawa nitafanya hivyo ila na mimi nilikuwa naomba unisaidie hiki, (mwambie kitu ambacho unajua kabisa kipo ndani ya uwezo wake), atakimbia na hutamwona tena.
18. AINA YA NNE; Watu ambao wanajijali na kujisifia wao tu (NARCISSISTS). Hawa ni watu ambao wanafikiri duniani wao pekee ndiyo muhimu. Watu hawa huzungumzia zaidi mafanikio yao na kuona wengine kama hawajui wanachokifanya. Watu hawa ukiongea nao wanataka watawale mazungumzo kila unachowaambia wanakuonesha ni jinsi gani wao ni bora kuliko wewe. Watu hawa hawana shida na wewe ila pia hawajali chochote kuhusu wewe. Wanajiangalia wao tu. Waepuke watu hawa kwa kukaa nao mbali, kwa sababu hakuna namna unayoweza kuwashawishi, kwa sababu hawataki kusikia chochote kuhusu wewe, wanataka uwasikilize wao tu na kuwasifia.
SOMA; USHAURI; Biashara Unazoweza Kuanza Kwa Mtaji Wa Tsh Laki Mbili Na Kuweza Kufanikiwa.
19. AINA YA TANO; Watu ambao wana matatizo ya kisaikolojia, au ugonjwa wa akili (PSYCHOPATH). Hawa ni watu ambao hawana hisia zozote zile, wanachoangalia wao ni kile ambacho wanakitaka tu. Hawajui kama wanaumiza wengine na wala hawajali kama wanachotaka kitakuwa kibaya kwa wengine. Kwa tabia hizi watu hawa huwa na mafanikio makubwa kifedha na kikazi au kibiashara lakini kimaisha wanashindwa kwenda vizuri na wengine. Unapokutana na watu wa aina hii kimbia haraka sana, usitake hata kujadiliana nao, maana wanapokuangalia hawaoni kingine bali ni jinsi gani watanufaika kupitia wewe hata kama wewe utaumia.
Waepuke watu hao wa ina tano na hakikisha wewe mwenyewe haupo katika moja ya aina hizo tano za watu. Kwa sababu badala ya kuwashawishi watu utakuwa unawafukuza kabisa.
20. Katika mipango yako ya kuwashawishi wengine kuwa makini sana usivuke mstari na kuwa mnyonyaji na mkandamizaji. Kuna tofauti ndogo sana kati ya ushawishi na ukandamizaji. Ushawishi ni pale ambapo unawawezesha watu kuchukua hatua au kufanya kitu ambacho kina manufaa kwao. Ukandamizaji ni pale ambapo unawawezesha watu kufanya kitu ambacho kina manufaa kwako ila kwao hakina manufaa au kinawaumiza kabisa. Kuna watu ambao wanaweza kutumia maneno yao vizuri na kuwakandamiza wengine, usiingie kwneye kundi hili.
Ni imani yangu kwamba umejifunza njia za kuongeza ushawishi wako kwa wengine na pia umejua yapi ya kuepuka.
Kama unavyojua, mambo haya yatakusaidia kama utayafanyia kazi. Hivyo yafanyie kazi.
Kwa kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili tembelea MOBILE UNIVERSITY, www.mobileuniversity.ac.tz Vitabu ni hazina, kila siku jifunze na fanyia kazi yale unayojifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz