Kuendesha biashara ni changamoto kubwa sana. Hakuna jambo lolote unalofanya una uhakika nalo kwa siku zijazo. Kinachokupa faida leo kesho kinaweza kisiwepo kabisa kama biashara. Hii ndio sababu kubwa unahitaji kujitoa sana kama kweli unataka kufanikiwa kupitia biashara.
Kuna aina moja ya biashara ambayo ina changamoto kubwa ziadi kuliko hata biashara za kawaida. Aina hii ya biashara tunaita BIAHSARA ZA FAMILIA. Hizi ni biashara ambazo zinaendeshwa kifamilia. Ni rahisi kuanzisha kama ndani ya familia kuna mwenye uwezo wa kufanya hivyo, ila zina changamoto zake za ziada ukiacha tu zile changamoto za kawaida za biashara.
Kwa uzoefu wangu kupitia wafanyabiashara ambao nimewashauri, kwenye biashara za familia kuna changamoto kubwa sana. Hasa kama anayewezesha biashara kuendelea kuwepo ni mwajiriwa, basi biashara ni vigumu kuendelea. Kwa mfano pale mwajiriwa huyu anapohitaji fedha, huondoa kwenye biashara na akipata mshahara anarejesha fedha ile. Iwe atarejesha au hatarejesha, kuondoa tu fedha kwenye biashara ambazo sio kwa lengo la biashara ni kuizuia biashara kuweza kujiendesha yenyewe.
Karibu kwenye kipengele chetu hiki cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia malengo yetu na mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Kupitia kipengele hiki utapata mbinu za uhakika za kufanyia kazi changamoto unayopitia na hivyo kuweza kuwa na maisha bora na kufikia kile unachotaka.
Leo kwenye kipengele hiki tutaangalia changamoto ya biashara za familia na ni hatua gani za kuchukua ili uweze kuondokana na changamoto ya aina hii. Kabla hatujaangalia kwa undani zaidi, tusome maoni aliyotuandikia msomaji mwenzetu;
Pole sana kwa changamoto hii unayopitia kwa miradi yako kufa kwa sababu ya mwenza wako. Uzuri ni kwamba changamoto hii unaweza kuifanyia kazi na baadae ukaweza kuendesha biashara zako vizuri.
Kama tulivyoona pale juu, biashara zinazoendeshwa kifamilia zina changamoto nyingi sana. Kwanza nidhamu kwenye biashara hii inakuwa ni ndogo na mwingiliano unakuwa mkubwa. Hivyo watu wote ambao mnaendesha biashara za familia mnahitaji kuwa makini sana kama kweli mnataka kukuza biashara hiyo.
Kwa Edah na wengine ambao mnaendesha biashara za familia, haya hapa ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kuwa na mafanikio kupitia biashara za aina hii.
1. Kaeni chini kwa pamoja kuweka malengo na mipango ya biashara.
Watu wote kwenye familia mnaohusika na biashara hiyo ya familia kaeni chini kwa pamoja ili kuweka malengo na mipango ya biashara. Amueni kwa pamoja mnataka kuiona biashara yenu ikifika wapi miaka miwili, mitano na hata kumi ijayo. Bila ya malengo makubwa ambayo mnayafanyia kazi ni rahisi mtu kufanya jambo ambalo litarudisha biashara nyuma.
Baada ya kuwa na malengo haya ya muda mrefu, wekeni mipango ya muda mrefu na muda mfupi. Wekeni mipango mizuri ambayo itawezesha biashara kujiendesha kwa faida ili iweze kukua zaidi. Mkishaweka mipango hii kubalianeni kwamba kila mtu ataheshimu na kufuata malengo na mipango ile. Na inapotokea mtu anataka kukiuka mnakumbushana.
2. Tofautisheni biashara na maisha yenu.
Changamoto nyingi za biashara za familia zinatokana na kushindwa kutofautisha maisha ya familia na biashara. Kama nyumbani hakuna hela ya kula, basi ni rahisi kuchukua kwenye biashara, kwa sababu mnaona yote ni yale yale tu, na baadaye itarudishwa.
Sasa iwe fedha itarudishwa au haitarudishwa, bado biashara itaathirika. Tofautisheni biashara na maisha yenu. Hakikisheni mnaweza kuendelea na maisha bila ya kuingilia biashara. Biashara ichukuliwe kama kitu ambacho kinajitegemea na kama mnahitaji kuondoa fedha basi iondolewe sehemu ya faida tu na sio mpaka mtaji.
SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.
3. Akili yenu isiwe kwenye biashara.
Akili zetu binadamu ni kitu cha kushangaza sana. Tukishajua suluhisho la tatizo letu ni kitu fulani, basi huwa hatufikiri tena mbadala. Kwa mfano kama mna biashara na mkipata tatizo la fedha mnachukua fedha kwenye biashara, tatizo lolote linaopotokea hamtafikiria sehemu nyingine ya kupata fedha, bali kwenye biashara.
Sasa wekeni utaratibu wa kufikiria kama biashara isingekuwepo mngefanya nini? Mwenzako anaposema tuchukue fedha kwenye biashara kutatua hili, muulize kama biashara isingekuwepo, tungechukua hatua gani? Kaeni chini mfikiri kwa kina, msipende kukimbilia njia rahisi, na kama mtaondoa biashara kwenye fikra zenu, mtapata njia nzuri ya kutatua changamoto ya fedha mliyonayo.
4. Jengeni nidhamu kubwa kwenye biashara yenu.
Nidhamu ni muhimu sana kwenye biashara, hasa ya familia. Kama mtalala njaa laleni tu, lakini msichezee fedha za biashara. Najua itakuwia vigumu kuelewa hapa lakini ndio jambo sahihi unatakiwa kufanya. Chukulieni biashara ile kama kitu ambacho hakihusiki kabisa katika kutoa hela bila ya utaratibu. Na fanyeni kuwa marufuku kuchukua fedha ambayo ni sehemu ya mtaji.
Kama mtu hafi, basi fedha ya biashara isiguswe. Kama utaendekeza huruma za kutoa fedha kwenye biashara kwa matatizo kidogo, basi jua biashara itakufa na hata ukianza nyingine itakufa pia.
SOMA; Kama Una Tabia Hizi 30 Tayari Wewe Ni Mjasiriamali, Chukua Hatua.
5. Kama yote yatashindikana, kopa fedha kwa mwenza wako na ufanye biashara mwenyewe.
Sitakudanganya kwamba yote tuliyojadili hapo juu yatafanya kazi vizuri. Nimewahi kushauri biashara moja ya familia, na mwanaume alikubali kufanya yale yote tuliyokubaliana pale, lakini kila nilipokuwa nafuatilia hakuna hata moja ambalo alitekeleza. Hivyo najua ni ngumu sana hasa pale inapokuwa mama ndio anaendesha biashara na baba ndio amewezesha.
Hivyo kama utajaribu hizo njia hapo juu na ikashindikana, yaani ukaanza biashara nyingine kwa mipangilio hiyo na bado ikafa kwa sababu za kifamilia, badili mpango. Badala ya kufanya biashara ya kifamilia, ongea na mwenza wako, mweleweshe kwamba mmekuwa mnaanza biashara na zote zinaishia kufwa, na sababu za kufa ni mwingiliano wa kifamilia (anaweza kubisha na kukuambia wewe ndio umeua, jiandae kwa hilo), hivyo mwombe akukopeshe fedha na uendeshe biashara wewe kama wewe na utakuwa unamlipa fedha aliyokukopesha. Katika mpango huu mpya wewe ndio unakuwa msimamizi mkuu wa biashara na unahakikisha unaiendesha kwa taratibu zote ambazo zitaiwezesha kufikia mafanikio.
Kikubwa hapa unahitaji kuonesha hamu yako kubwa ya kufanikiwa kwenye biashara na hivyo kuhitaji uhuru wa kuendesha biashara isiyoingiliwa na mambo ya kifamilia. Fanya mambo yote haya kwa maelewano na sio kwa ugomvi. Kwa sababu ukifanya kwa ugomvi itakuwia vigumu kuendesha biashara kama biashara hiyo inaleta msuguano mkubwa ndani ya familia.
Naamini kama kweli utatumia busara na mbinu hizi tulizoshirikishana hapa, utapata mahali pa kuanzia.
Nikutakie kila la kheri katika kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa.
Kwa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu bonyeza hapa kupata taratibu za ushauri.
TUPO PAMOJA
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.
Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

![]() |
MAFANIKIO YA BIASHARA YA FAMILIA NI WOTE KUWA KITU KIMOJA. |

Mume wangu ndiye anachangia mimi kushindwa kufikia malengo. Kila tukianzisha biashara anachukua pesa za biashara kwa lengo la kurudisha kila Mara na harudishi mradi unakufa. Yeye ni mtumishi, nifanye nini ili niweze fikia malengo, mimi sina kazi nategemea hiyo miradi tunapoianzisha naomba ushauri nifanyeje ili niweze fikia malengo YANGU. Edah M.Habari Edah,