Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Nilitaka Kushiriki Semina Ila Nimechelewa Kujiunga. Ufanyeje Ili Hili Lisikutokee.

$
0
0
Semina zote ambazo huwa tunazitoa kwa njia ya mtandao, taarifa huwa zinaanza kutolewa angalau wiki mbili kabla ya semina kuanza. Na taarifa hutolewa mara kwa mara kupitia njia mbalimbali ikiwepo makala na hata ujumbe unaotumwa kwenye email.
Lakini katika semina zote ambazo tumeshatoa huwa kuna watu wanajitokeza baada ya mafunzo kuanza na kusema kwamba walichelewa kupata taarifa na hivyo hawakujiunga kwa wakati. Huwa wanaomba kuingia pale ilipo na kutumiwa mafunzo mengine ya nyuma.
Mwanzo tulikuwa tunakubali hilo, lakini kwa semina za hivi karibuni na hii inayokuja siku chache zijazo jambo hilo halitawezekana.
Yaani kama utashindwa kujiunga sasa, ambapo kujiunga mwisho ni tarehe 02/10/2015 ijumaa ijayo, ndio utakuwa umekosa mafunzo haya mazuri kwenye maisha yako. Hutaweza tena kujiunga baada ya hapo.
 
Kwa nini usiweze kujiunga?
Hatukatazi kujiunga kwa sababu tunataka kukukomoa, bali kwa sababu tunataka kukusaidia.
Kuna kitu kikubwa sana ambacho unakipata kwa kufuatilia mafunzo haya tunayotoa kwa hatua. Unapata nafasi ya kupata sehemu ya mafunzo, kutafakari na hata kuuliza swali. Pia unakuwa na jukumu la kufanya kila siku ambayo unapokea mafunzo haya. Hii inakusaidia sana kuondoka na kitu ambacho kitabadili maisha yako.
Lakini unapopata mafunzo haya yote kwa mkupuo, yaani mara moja, utakuwa unakazana kusoma uyamalize, hivyo ni vigumu kufanya kila jukumu ambalo lipo kwenye kila somo.
Mafunzo haya tunayotoa kwa njia ya mtandao tungeweza kuyaweka kama kitabu na tukakupatia, lakini kusoma kama kitabu huwezi kupata faida kubwa unayoipata kwa kuyapokea kidogo kidogo, kufanyia kazi mazoezi unayopewa, kuuliza maswali na kujibiwa na pia kuwa na mijadala kuhusiana na kile unachojifunza.
Kwa sababu hii kubwa, kama utashindwa kujiandikisha wakati huu ambapo bado unayo nafasi ya kujiandikisha, hatutakupokea tena. Hivyo chukua hatua sasa, BONYEZA MAANDISHI HAYA SASA HIVI NA UWEKE TAARIFA ZAKO.
Na wala sio fedha.
Katika mafunzo kama haya tuliyotoa mara ya mwisho, ilikuwa kuhusu MAFANIKIO KWENYE BIASHARA, mtu mmoja aliyechelewa, baada ya kumjibu kwamba hataweza kujiunga kwa sababu amechelewa alitoa jibu kali sana. Alisema kwani mimi si ninawalipa fedha yenu, nyie nitumieni hayo mafunzo na nitajua mwenyewe.
Nilimwambia, na ninakuambia wewe pia, kikubwa hapa sio fedha. Kitu cha mbele hapa sio fedha, bali mafunzo haya yakusaidie wewe. Ukitoa fedha leo, ukachukua mafunzo, usiyasome kwa sababu yamekuwa mengi kwako na hivyo uone kwamba mafunzo haya hayana msaada kwako. Baadae yakija mafunzo mengine utasemaje? Utaona mafunzo haya huwa hayana msaada wowote kwangu, na hivyo hutojiunga tena. Hatutaki hali hii itokee.
Lengo kubwa ni wewe upate maarifa ambayo yatafanya maisha yako kuwa bora ili uweze kuona kweli kwamba gharama uliyotoa imerudisha matunda.
Pia gharama unayolipia mafunzo haya kwa sasa sio gharama halisi. Ni gharama ndogo ukilinganisha na mafunzo unayopokea. Gharama hizi zitakuja kuongezeka baadae na kwa kuwa wewe ndio utakuwa mshiriki wa mafunzo ya baadae, inabidi mafunzo haya ya sasa yakusaidie ili baadae uweze kumudu gharama halisi zitakazokuwa zinatozwa kwenye mafunzo hayo.
Chukua hatua sasa.
Kama kweli unataka kupata mafunzo haya, kama unataka kupata maarifa ambayo yatakufanya uishi maisha ya kujiamini, ufanye biashara kwa viwango vingine na upeleke kazi yako kwenye viwango vya juu sana, usikose semina hii.
Kama hukupata maelezo kamili ya semina hii, yako hapa chini;
MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
Hii ni semina kwa njia ya mtandao ambayo itakukumbusha kitu muhimu sana kwenye maisha yako. Kwamba wewe ni mshindi na una kila unachohitaji kushinda. Kinachokuzuia mpaka sasa ni kukosa maarifa sahihi na kuzungukwa na jamii ambayo inakulazimisha kwamba huwezi tena kushinda.
Huu ni uongo wa hali ya juu sana na umekufanya uishi maisha ambayo sio stahili kwako. Kupitia semina hii utaweka ahadi yako na nafsi yako ambayo itakuwezesha kushinda.
Nini kipya kwenye semina hii, si yale ambayo tunajifunza kila siku?
Semina hii ina mambo mengi sana mapya. Pamoja na haya unayojifunza kila siku, hapa kuna mbinu za tofauti za kuhakikisha kwamba unaishi ule ushindi uliopo ndani yako.
Kitu kikubwa sana ambacho hujawahi kupata kwenye semina nyingine ni kwamba mimi sitakufundisha, bali utakuwa unajipa ahadi wewe mwenyewe. Jinsi masomo ya semina hii yalivyoandaliwa ni kwamba utakuwa unajiambia ni kipi ambacho unafanya. Sio mimi nakwambia WEWE NI MSHINDI, bali wewe unajiambia mwenyewe MIMI NI MSHINDI. Na masomo yote kwenye semina hii yamekaa kwa muundo huo.
Kwa hiyo hii inakuwa ni ahadi ya kweli na nafsi yako, unajiambia mimi ni mshindi, hii ina nguvu zana kuliko kuambiwa wewe ni mshindi
MUUNDO WA SEMINA HII;
Semina hii itaendeshwa kwa mwezi mmoja, mwezi huu wa kumi.
Semina itaanza jumatatu ya tarehe 05/10/2015 na kumalizika ijumaa ya tarehe 30/10/2015.
Semina hii itakuwa na mafunzo 20 ambapo somo moja litatumwa kila siku kwa siku tano za wiki. Siku za mwisho wa wiki zitakuwa za kuuliza na kujibu maswali.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, email, kundi la wasap na kutumiwa ujumbe mfupi.
Kwa kujiunga na semina hii;
Kila siku ya semina utatumiwa email yenye mafunzo ya semina ikiwa na hatua za kuchukua pia.
Utapata nafasi ya kuwepo kwenye kundi la wasap, ambapo utaweza kusoma masomo haya kwenye simu yako na pia kupata nafasi ya kushiriki mijadala inayoendana na hiki tunachojifunza.
Kila siku asubuhi utapata ujumbe mfupi kwenye simu yako ya mkononi ukikupa mbinu za ushindi na kukumbusha kwamba wewe ni mshindi.
Utaweza kuwasiliana nami, na hata kuuliza maswali na kujibiwa wakati wowote wa kipindi hiki cha semina.
Yafuatayo ni masomo yaliyopo kwenye semina hii;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.
Masomo haya 20 yameandaliwa vizuri sana kiasi kwamba kadiri unavyokwenda unaendelea kuvunja minyororo yote ambayo inakuzuia kufikia mafanikio. Kumbuka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako yanaanza na wewe mwenyewe, na ndio maana mafunzo haya yameandaliwa ili kukuwezesha wewe mwenyewe kubadilika, kujiahidi kwamba utashinda na baadae utashinda kweli.
CHETI CHA AHADI.
Ili kuongeza na kuweka msisitizo zaidi kwenye ahadi hii, baada ya mafunzo haya tutaandaa vyeti maalumu vya wewe kujiahidi mambo haya muhimu. Utaweka sahihi kwenye cheti hiko na kukiweka mahali ambapo kila siku unaweza kukiona na kujikumbusha kwamba wewe ni mshindi na ni mambo gani unafanya kama mshindi.
Yaani nakuhakikishia, kama utajiunga na mafunzo haya, na kuyafanyia kazi, na ukapata cheti hiki ambacho kitakuwa kinakukumbusha kila siku, hakuna kitu chochote, narudia tena, HAKUNA KITU CHOCHOTE kinachoweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
GHARAMA ZA SEMINA HII.
Kwa yote haya mazuri upo tayari kulipia kiasi gani cha fedha?
Hakuna thamani unayoweza kuweka kwenye mafunzo haya, yana thamani kubwa sana ambayo huwezi kuitathmini kwa viwango vya fedha. Lakini kwa sababu wewe ni rafiki yangu, na lengo langu ni kukuona wewe unafanikiwa, utachangia mchango mdogo wa kuhakikisha semina hii inaweza kuendeshwa.
Na mchango huo utakuwa tsh elfu 30(30,000/=) kwa mafunzo ya semina. Kwa wale watakaotaka kupata vyeti vya kumbukumbu ya ahadi yao wataongeza gharama kidogo za kupata cheti kile, tutajuzana baadae.
Hii ni gharama ndogo sana ambayo huwezi kuipata kwa mafunzo kama haya ambayo utayapata.
KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA.
Ili uweze kushiriki mafunzo haya, unahitaji kujiunga kwa kujaza taarifa zako na kisha kulipia ada ya mafunzo.
Kujiunga na kulipia kumefunguliwa leo tarehe 18/09/2015 na mwisho wa kujiunga na kulipia itakuwa tarehe 02/10/2015. Baada ya hapo hutakuwa tena na nafasi ya kujiunga.
Ili kuhakikisha washiriki wanapata mafunzo bora, nafasi za ushiriki huwa zinakuwa chache. Hivyo ni vyema ukachukua hatua haraka.
Kujaza taarifa zako
bonyeza maandishi haya na malipo fanya kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253.
Chukua hatua haraka kabla nafasi hii ya kipekee haijakupita.
Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ambayo ninaamini bila ya kusita kwamba yatabadili maisha yako. Nimejitoa kuweka kila ninachojua kwenye mafunzo haya ili yawe msaada mkubwa sana kwenye maisha yako, usijaribu kabisa kuyakosa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
P.S Kama bado hujajaza fomu ya kujiunga bonyeza maandishi haya sasa na ujiunge na mafunzo haya mazuri.
N;B Kumbuka imebaki wiki moja tu ya kujiunga na mafunzo haya, BONYEZA HAPA kujaza fomu sasa ili usikose mafunzo haya muhimu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1010

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>