Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele chetu cha ushauri wa changamoto ambazo zinakuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Hakuna maisha ambayo hayana changamoto na hivyo unapopata mawazo mbadala inakusaidia sana kujua ni kipi cha tofauti kufanya. Na huu ndio umekuwa msingi wa makala za kipengele hiki ambazo zimekuwa zinakujia kila jumatatu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Kupitia kipengele hiki wewe msomaji unajaza fomu kwa kueleza kwa kifupi changamoto inayokusumbua kisha tunaijadili na kukushirikisha baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kuondokana na changamoto hiyo au kuifanya isiwe kikwazo kwako kufikia mafanikio makubwa.
Watu wengi wamekuwa wakiandika changamoto zao na kupatiwa majibu, wengine wengi wamekuwa wakirudia changamoto ambazo tulishazipatia majibu. Lakini pia kuna watu wengine ambao wanahitaji msaada zaidi wa ushauri na mwongozo ili kuweza kuvuka changamoto na kufikia mafanikio makubwa.
Kwa kuhitaji mwongozo huu wa ziada watu wamekuwa wakinitafuta mara kwa mara kwa njia ya simu au wakitaka tuonane. Ni watu wengi sana ambao wamekuwa wakitaka tuonane na muda wangu ni mfupi kuweza kuonana na kila mtu. Na hata ningejitahidi kuweza kuonana na kila mtu au kumjibu tatizo lake moja kwa moja, bado wengi hawafanyii kazi yale ambayo utawashauri. Hivyo tunakuwa tumepoteza muda ambao ni wa thamani sana kwa kila mmoja wetu.
Ili kutatua changamoto hii ya watu kutaka tuonane na muda kuwa changamoto kuna taratibu ambazo AMKA CONSULTANTS tunazitumia kwa ajili ya kutoa ushauri na mwongozo.
Kwanza kabisa kuna utaratibu wa ushauri peke yake. Hapa ni pale ambapo wewe unataka ushauri tu na sio kuendelea kufuatiliwa kwa kile ambacho unafanya. Ili kupata ushauri mzuri na wa kina tunahitaji kuwa na mazungumzo marefu kidogo. Katika mazungumzo hayo tutaijadili changamoto unayoipitia kwa kina na tutakuja na mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na changamoto hiyo. Mazungumzo haya tunaweza kufanya ana kwa ana, ambayo ni ngumu kidogo kutokana na upatikanaji, au tunaweza kufanya kwa njia ya simu ambayo ni rahisi tukishapanga muda.
Ukishampatia mtu maelezo kama hayo anafurahi sana na kukuambia nipo tayari tupange muda. Ila unapomwambia kuna gharama, wengi hushangaa na kupotea. Ndio kuna gharama kidogo ambazo utahitaji kuchangia kwenye huduma hiyo ya mazungumzo ya ushauri. Gharama hiyo inabadilika kadiri siku zinavyokwenda, hivyo nikiandika hapa leo, na wewe ukasoma makala hii mwaka mmoja ujao unaweza kukukuta gharama zimeshabadilika. Ninachotaka ujue ni kwamba kuna gharama utakazohitaji kuchangia kama utahitaji ushauri wa kina zaidi kuhusiana na changamoto unayopitia.
Aina ya pili ya msaada wa changamoto unaoweza kupata AMKA CONSULTANTS ni kupata mwongozo kwa kile unachofanya (coaching), hapa tunakwenda hatua kwa hatua na kila unachofanya tunakuwa pamoja. Tunajadili kila baada ya muda fulani kwamba tumetoka wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi na vitu gani muhimu kufanya. Njia hii ya coaching itakulazimisha wewe kufanya hata kama una uvivu kiasi gani. Ni njia nzuri sana ya kuweza kufanya kitu ambacho umekuwa unapenda kufanya ila unashindwa kufanya. Pia ni nzuri sana kwenye kuweza kubadili tabia ambazo zimekuwa zinakurudisha nyuma. Hii nayo pia ina gharama zake na ni kubwa kidogo ukilinganisha na muda utakaokuwa unafuatiliwa. Gharama hizi pia zinabadilika kadiri muda unavyokwenda. Ila kwa sasa gharama ni hizi hapa; BONYEZA MAANDISHI HAYA KUJUA.
Lengo kubwa la makala hii ya leo ni kukujulisha wewe msomaji kwamba kitu kizuri kinahitaji gharama. Watanzania hatuna utamaduni wa kulipia ushauri kwa sababu tunaamini ni rahisi sana kupata ushauri. Ndio maana watu wengi ukiwaambia wanahitaji kuchangia gharama huishia kushangaa.
Watanzania tumezoea kuchukua ushauri maarufu ambao kila mtu anaweza kukuambia, hata mtoto wa darasa la tano. Hatujazoea ushauri wa kina ambao unaendana na wewe kulingana na changamoto unazopitia na hali uliyo nayo.
Vipi kama ndio naanza na sina fedha ya kulipia ushauri?
Juma lililopita alinipigia simu dada mmoja akitaka tuonane kwa haraka kwani ana shida ambayo anahitaji ushauri. Nikamwambia karibu, ila kuna gharama za ushauri unahitaji kuchangia. Akaniambia mimi ndio nimemaliza chuo sina kipato chochote, huna njia ya kutusaidia sisi ambao bado? Nikamwambia njia ipo nzuri sana ya kumsaidia kila mtu. Nilimwambia nenda kwenye AMKA MTANZANIA, kuna makala karibu elfu moja, soma zile makala kumi ambazo zimesomwa sana na utaondoka na kitu ambacho unaweza kuanza kukifanyia kazi, kifanyie kazi kitu hiko na utakapoanza kuona mabadiliko nitafute, hapo unaweza kupata ushauri mzuri.
Hii ni kweli kwa kila msomaji. Kama huna fedha za kuweza kulipia ushauri kuna makala nyingi sana kwenye AMKA MTANZANIA ambapo tumeshajadili karibu kila changamoto unayopitia wewe, iwe ni biashara, kazi, na hata maisha ya kawaida. Unachohitaji wewe ni kuwa na muda wa kupitia makala hizi na kuwa tayari kuanza kufanyia kazi yale ambayo unajifunza.
Hii itakuwa njia rahisi sana kwako kwa sababu hata utakapopata ushauri utajua uutumieje na uutumie wapi. Kwa mfano unaweza kuanza na makala kama hii; USHAURI; Jinsi Ya Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara, kama changamoto yako ni kuanza biashara.
Au ukasoma makala hii; USHAURI; Biashara Nzuri, Inayolipa Na Unayoweza Kuifanya,kama hujui ni biashara gani ufanye.
Pia kama unaanzia chini kabisa, yaani unaanzia na sifuri basi soma makala hii; Kitu Kimoja Unachohitaji Ili Kufanikiwa Kama Unaanzia Chini Kabisa, na utapata mambo mengi ya kufanya.
Makala zipo nyingi sana rafiki, soma na hii pia; USHAURI; Jinsi Ya Kutoka Kimaisha Kwa Kuanza Na Mshahara Mdogo, hapa pia utapata mbinu bora kabisa za kuanza maisha kwa kipato kidogo.
Kwa kifupi ni kwamba vitu vingi unavyohitaji kujua tayari vipo kwenye AMKA MTANZANIA, visome na fanyia kazi. Kama utahitaji ushauri wa ziada jiandae kulipia gharama kidogo ili uweze kupata ushauri utakaokuwa bora sana kwako,
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako;
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.
Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

![]() |
UNAPOJIKUTA KWENYE HALI KAMA HII, UNAHITAJI USHAURI MAKINI NA SIO WA MTAANI. |