Na; Charles Nazi
Siri moja wapo ya utajiri ni kuanzisha na kumiliki biashara yako. Hakuna mtu anayeweza kutajirika kwa kuajiriwa na mtu mwingine.
Napenda kuongelea namna ya kubadili kitu unachokipendana kuwa biashara. Kwa mfano mtu anayependa kuandika (mwandishi) anaweza kuwa mtunzi wa vitabu, anaweza kumiliki magazeti, vyombo vya habari kama vile rediona televisheni. Hatua ya kwanza kufanya ni kukagua kipaji chako au kile kitu unachokipenda. Endeleza kipaji chako kwa kuchukua mafunzo kwenye fani ya kitu unachokipenda ili uwe mahiri. Chagua eneo la kuandika kwani hata katika uandishi kuna uandishi wa mambo mengi, mfano; uandishi wa makala, hadithi, tamthilia, habari nk. Kwa wale wanaopenda kusoma hadithi watamkumbuka James Hadley Chase ambaye alikuwa anaandika hadithi za kusisimua ni mfano wa mtu aliyefanikiwa kwenye uandishi na ameuza mamilioni ya vitabu. Faida ya kufanya biashara ambayo unaipenda ni kwamba, biashara inageuka kuwa kama mchezo, hata kama kuna changamoto huwezi kukata tama haraka.
SOMA; Jinsi Ya Kugundua Vipaji Vilivyopo Ndani Yako.
Hivyo unachotakiwa ni kuendelea kufanya unachokipenda mambo ya pesa yatakufuata. Hapo juu nilitoa mfano wa mwandishi, lakini unaweza kuwa msanii, mwimbaji,mwanariadha, mcheza mpira wa miguu, mchekeshaji nk. Mbinu za mafanikio ni zile zile. Hatua za mafanikio ni kuanza kuwa na malengo ya kuwa mtu aliyefanikiwa kwa kutumia kipaji chako. Uwe na ndoto ya kuwa milionea kumiliki sh. Bilioni 1.7 Tafuta kipaji au kitu unachokipenda ili ukibadili kuwa biashara. Unapaswa kukiendeleza kipaji chako kwa kupata mafunzo katika fani inayofanana na kipaji chako ili uwe mahiri. Panua biashara kwa kufanya unachopenda kwa mapana zaidi kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa utafanikiwa.
Jee umeshawahi kujiuliza una kipaji gani? Kama hujui jaribu kutumia njia hii. Muulize ndugu,mke,mume, rafiki au jamaa yako wa karibu ajaribu kukuelezea jinsi anavyokufahamu kwamba unapenda nini au una kipaji gani. Kama utashindwa kupata jibu unaweza kumtafuta mwandishi wa makala hii ili aweze kukusaidia kuvumbua kipaji chako.
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;http://tinyurl.com/mshauriwabiashara au Piga simu namba 0784394701
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.