Mara nyingi huwa inatokea tunajikuta ni watu wenye shauku, nguvu na hamasa kubwa sana hasa pale tunapofanya mambo mapya katika maisha yetu. Kwa bahati mbaya kwa wengi wetu hamasa ile huzidi kupungua pole pole kwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele. Watu wengi huwa hawaelewi ni kwa nini hasa hamasa walikuwa nayo mwanzo inapungua siku hadi siku. Kutokana na kukosa hamasa huku mara nyingi kinachotokea ni uzalishaji au utendaji wa kile unachokifanya hupungua na wakati mwingine kukata tamaa kabisa hutokea na kushindwa kuendelea mbele.
Katika safari yako ya mafanikio uliyonayo hakuna kitu kibaya kama kukosa hamasa. Unapokosa hamasa sio tu itasababisha wewe kuwa na hisia mbaya lakini zaidi itakupelekea wewe kushindwa kutimiza mipango na malengo yako uliyojiwekea. Lakini, kitu muhimu ambacho mimi na wewe tunatakiwa tujiulize kwa nini huwa inatokea kwa wengi hamasa hii kupungua kwa siku chache mbeleni mara baada ya kuanza kufanya kitu kipya. Katika makala hii ninakwenda kukwambia sababu muhimu zinazokufanya wewe ukose hamasa mara kwa mara ili tatizo hili lisijirudie tena kwako.
SOMA: Jipe Changamoto MaraKwa Mara.
Sababu 7 Zinazokufanya Upoteze Hamasa Kwa Kile Unachokifanya.
1. Umekuwa una hofu sana ya kuogopa kushindwa.
![]()
2. Umekuwa una malengo ambayo siyo yako.
Kwa kumalizia, ili kuwa na hamasa mpaka mwisho wa mafanikio yako ni muhimu kujua kuna wakati uvumilivu unahitajika na zaidi kuamini kwa kile unachokifanya na kuacha kusikiliza maneno ya nje ambayo yanaweza yakakutisha tamaa na ukajikuta umekosa hamasa. Fuata njia ambayo unaamini itakufikisha kwenye mafanikio yako, acha kujiwekea malengo kwa kuiga utakwama na kumbuka pia mafanikio yanakuja kwa kuwa king’ang’azi wa ndoto zako, kila kitu kinawezekana chini ya jua.
Katika safari yako ya mafanikio uliyonayo hakuna kitu kibaya kama kukosa hamasa. Unapokosa hamasa sio tu itasababisha wewe kuwa na hisia mbaya lakini zaidi itakupelekea wewe kushindwa kutimiza mipango na malengo yako uliyojiwekea. Lakini, kitu muhimu ambacho mimi na wewe tunatakiwa tujiulize kwa nini huwa inatokea kwa wengi hamasa hii kupungua kwa siku chache mbeleni mara baada ya kuanza kufanya kitu kipya. Katika makala hii ninakwenda kukwambia sababu muhimu zinazokufanya wewe ukose hamasa mara kwa mara ili tatizo hili lisijirudie tena kwako.
SOMA: Jipe Changamoto MaraKwa Mara.
Sababu 7 Zinazokufanya Upoteze Hamasa Kwa Kile Unachokifanya.
1. Umekuwa una hofu sana ya kuogopa kushindwa.
Mara nyingi inapotekea ukawa una mashaka na hofu kubwa ya kuogopa kushindwa kwa kile unachokifanya, hiyo inaweza ikawa ni sababu kubwa ya kukupotezea hamasa uliyonayo na ukajikuta unashindwa kusonga mbele. Kwa mfano kama akili yako itakuwa inaogopa kushindwa, kitakachotokea kwako hutafanya kitu kitu cha kukuhamasisha zaidi, ila utahakikisha ufanye kila jambo litakalopelekea wewe usishindwe mwisho wa siku utajikuta hamasa uliyonayo inapungua polepole. Unapokuwa na hofu sana ni lazima upoteze hamasa.
SOMA: Hivi Ndivyo Unavyoweza Kumudu Kuondoa Hofu Zako Za Kesho, Zinazokusumbua Na Kukutesa.
2. Umekuwa una malengo ambayo siyo yako.
Unaweza ukajiuliza ni ‘kivipi nakuwa nina malengo ambayo siyo yangu’? Ni kweli, wala sijakosea kuna wakati unakuwa unakosa hamasa kwa sababu malengo uliyonayo yanakuwa siyo yako, unakuwa umebeba malengo ya watu wengine. Watu wengi bila kujijua huwa ni watu wakuweka malengo si kwa sababu malengo hayo yapo ndani mwao ni kwa sababu wameona wengine wanafanya hivyo. Unapokuwa unaweka malengo kwa kuiga mara nyingi kinachokutokea unapokutana na changamoto kidogo tu ni lazima upoteze mwelekeo na hamasa.
SOMA: Hiki Ndicho Kitu Kikubwa Kinachokuzuia Kwenye Mafanikio.3. Umekuwa una mitizamo mingi sana ambayo ni hasi.
Sababu kubwa inayokufanya ukose hamasa, ni wewe kuwa na mitazamo hasi sana kwa jambo unalolifanya. Unapokuwa na fikra kama siwezi kufanikiwa sana kwa sababu sina bahati, sina mtaji wa kutosha au siwezi kushindana na wengine kibiashara, tambua kabisa ni lazima hamasa uliyonayo itapungua tu. Kuwa na mitizamo chanya ni chachu kubwa sana kwa mafanikio yako. Unapojenga mitizamo chanya kwamba ni lazima nitafanikiwa hata kama mtaji wangu ni mdogo, uwe na uhakika ni lazima utakuwa na hamasa kubwa itakayokusaidia kufanikiwa.
SOMA: Hizi Ndizo Fikra Zinazokuzuia Kufikia Viwango Bora Vya Mafanikio. Sababu kubwa inayokufanya ukose hamasa, ni wewe kuwa na mitazamo hasi sana kwa jambo unalolifanya. Unapokuwa na fikra kama siwezi kufanikiwa sana kwa sababu sina bahati, sina mtaji wa kutosha au siwezi kushindana na wengine kibiashara, tambua kabisa ni lazima hamasa uliyonayo itapungua tu. Kuwa na mitizamo chanya ni chachu kubwa sana kwa mafanikio yako. Unapojenga mitizamo chanya kwamba ni lazima nitafanikiwa hata kama mtaji wangu ni mdogo, uwe na uhakika ni lazima utakuwa na hamasa kubwa itakayokusaidia kufanikiwa.
4. Umekuwa ukisikiliza sana maneno ya nje.
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayotaka katika maisha yako kuna wakati ni muhimu sana kwako kuishi wewe kama wewe na kuziba masikio kutokusikiliza kelele za nje ambazo zinaweza kukupoteza. Unaweza ukajikuta una mipango na malengo yako mazuri uliyojiwekea katika mradi wako na unasonga mbele vizuri, lakini kuna wakati kwa bahati mbaya au nzuri huwa inatokea watu wanaoanza kutoa ushauri kuhusiana na kile unachokifanya. Mara nyingi ushauri huu unapokuwa hasi inakuwa ni rahisi sana kwako kukosa hamasa ya kusonga mbele kutokana na maneno ya kukatisha tamaa.
SOMA: Hapana, Huwezi.Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayotaka katika maisha yako kuna wakati ni muhimu sana kwako kuishi wewe kama wewe na kuziba masikio kutokusikiliza kelele za nje ambazo zinaweza kukupoteza. Unaweza ukajikuta una mipango na malengo yako mazuri uliyojiwekea katika mradi wako na unasonga mbele vizuri, lakini kuna wakati kwa bahati mbaya au nzuri huwa inatokea watu wanaoanza kutoa ushauri kuhusiana na kile unachokifanya. Mara nyingi ushauri huu unapokuwa hasi inakuwa ni rahisi sana kwako kukosa hamasa ya kusonga mbele kutokana na maneno ya kukatisha tamaa.
5. Umekuwa ukikosa uvumilivu.
Kukosa uvumilivu wa kutosha kwa kile unachofanya, hii ni sababu mojawapo kubwa inayopelekea wewe ukose hamasa. Watu wengi ambao wamekuwa wakikosa uvumilivu katika maisha yao na kutaka mambo yaende kwa haraka kama wao wanavyotaka, mara nyingi nyingi wanapokutana na ugumu au changamoto kidogo huwa ni watu wa kukosa hamasa na mwisho kabisa hupelekea wao kukata tamaa kabisa. Kutokana na wao kutaka matokeo ya haraka, mambo yanapogoma kidogo huwa ni watu wakufikiri wamekosea njia na kujikuta wamekosa morali na hamasa.
SOMA: Vumilia Mateso Ya Muda Mfupi Ili Upate Furaha Idumuyo.Kukosa uvumilivu wa kutosha kwa kile unachofanya, hii ni sababu mojawapo kubwa inayopelekea wewe ukose hamasa. Watu wengi ambao wamekuwa wakikosa uvumilivu katika maisha yao na kutaka mambo yaende kwa haraka kama wao wanavyotaka, mara nyingi nyingi wanapokutana na ugumu au changamoto kidogo huwa ni watu wa kukosa hamasa na mwisho kabisa hupelekea wao kukata tamaa kabisa. Kutokana na wao kutaka matokeo ya haraka, mambo yanapogoma kidogo huwa ni watu wakufikiri wamekosea njia na kujikuta wamekosa morali na hamasa.
6. Umekuwa ukiishi na matarajio makubwa yasiyo sahihi.
Kuwa na imani na matarajio makubwa kwa kile unachokifanya ni kitu kizuri sana katika safari yako ya mafanikio. Lakini, matarajio hayo unayokuwa nayo yanapokuwa makubwa sana na hayaendani na uhalisia husababisha wewe ukose hamasa. Kwa mfano kuna watu ambao huamini kimakosa wanaweza wakawa matajiri kwa muda mfupi baada ya kuanza biashara tu. Pia wapo wanaomini wataanza kupata mshahara mkubwa mara tu waanzapo kazi, kitu ambacho sio kweli. Mambo yanapoenda kinyume na ulivyokuwa ukitarajia kwanza, utaona maisha magumu na utakosa hamasa.
SOMA: Jinsi Unavyoweza Kuendelea Kuwa Na Hamasa Kubwa Kila Siku.Kuwa na imani na matarajio makubwa kwa kile unachokifanya ni kitu kizuri sana katika safari yako ya mafanikio. Lakini, matarajio hayo unayokuwa nayo yanapokuwa makubwa sana na hayaendani na uhalisia husababisha wewe ukose hamasa. Kwa mfano kuna watu ambao huamini kimakosa wanaweza wakawa matajiri kwa muda mfupi baada ya kuanza biashara tu. Pia wapo wanaomini wataanza kupata mshahara mkubwa mara tu waanzapo kazi, kitu ambacho sio kweli. Mambo yanapoenda kinyume na ulivyokuwa ukitarajia kwanza, utaona maisha magumu na utakosa hamasa.
7. Umekuwa ukipoteza imani katika mipango yako.
Mara nyingi akili yako inakuwa inahamasa kubwa hasa pale unapoamini kuwa una uwezo mkubwa wa kufikia malengo na mipango yako uliyojiwekea. Unapokosa imani na kuwa na wasiwasi juu ya mipango yako uliyojiwekea hamasa ya kufanya mambo yako hupungua na mwisho wa siku usipokuwa makini utajikuta umeshakata tamaa. Unapokosa imani, kujitilia shaka wewe mwenyewe na kushindwa kujiamini kwa namna yoyote ile juu ya malengo yako uliyojiwekea uwe na uhakikia ni lazima utendaji wako utapungua na pia utakosa hamasa.
SOMA: Hii Ndiyo Imani Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kufanikiwa.Mara nyingi akili yako inakuwa inahamasa kubwa hasa pale unapoamini kuwa una uwezo mkubwa wa kufikia malengo na mipango yako uliyojiwekea. Unapokosa imani na kuwa na wasiwasi juu ya mipango yako uliyojiwekea hamasa ya kufanya mambo yako hupungua na mwisho wa siku usipokuwa makini utajikuta umeshakata tamaa. Unapokosa imani, kujitilia shaka wewe mwenyewe na kushindwa kujiamini kwa namna yoyote ile juu ya malengo yako uliyojiwekea uwe na uhakikia ni lazima utendaji wako utapungua na pia utakosa hamasa.
Kwa kumalizia, ili kuwa na hamasa mpaka mwisho wa mafanikio yako ni muhimu kujua kuna wakati uvumilivu unahitajika na zaidi kuamini kwa kile unachokifanya na kuacha kusikiliza maneno ya nje ambayo yanaweza yakakutisha tamaa na ukajikuta umekosa hamasa. Fuata njia ambayo unaamini itakufikisha kwenye mafanikio yako, acha kujiwekea malengo kwa kuiga utakwama na kumbuka pia mafanikio yanakuja kwa kuwa king’ang’azi wa ndoto zako, kila kitu kinawezekana chini ya jua.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio makubwa na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA kila siku kujifunza zaidi, mpaka maisha yako yaimarike.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila siku.
IMANI NGWANGWALU,
0713048035/ingwangwalu@gmail.com