Quantcast
Channel: AMKA MTANZANIA
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live

Leo Ndiyo Siku Ya Mwisho Ya Kujiandikisha Kwenye Semina Ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO.

$
0
0


Habari za leo rafiki yangu?

Naomba kuchukua nafasi hii kwa mara ya mwisho kabisa kukukumbusha ya kwamba leo tarehe 02/01/2017 ndiyo siku ya mwisho ya kujiandikisha kwenye semina ya MWAKA 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO na kupata nafasi ya kuwa karibu na mimi kwa mwaka mzima wa 2017.
 

Kwa msisitizo naomba niseme hivi, LEO NI SIKU YA MWISHO KABISA KABISA KABISA...

Kwa nini nasema hivi?

Kwa sababu kila wakati ninapoandaa semina, natoa taarifa mapema kabisa na siku ya mwisho kujiunga inakuwa inajulikana. Na ile siku ya mwisho nawakumbusha watu kwamba leo ni mwisho. Lakini huwa wanakuja watu baadaye muda umeshapita na kuomba kujiunga, wakiwa na sababu mbalimbali. Tatizo linakuwa kwamba kwa mfumo tunaotumia kuendesha semina hizi huwezi kuingilia katikati, lazima uwe umejiandikisha kabla ya semina kuanza.

Ndiyo maana unaona nakukumbusha sana, kama bado una waza waza kujiunga au la, nakushauri chukua hatua leo hii, kwa sababu kuchelewa kwako kutakugharimu mno.

Hivyo fanya malipo ya kushiriki semina, pamoja na mafunzo ya mwaka mzima wa 2017 kwa kulipa ada ambayo ni tsh elfu 50 (50,000/=). Lipa ada kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 na ukishatuma malipo yako tuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako kamili kwenda namba 0717 396 253 (wasap tu).

Nikukumbushe tena rafiki, chukua hatua leo, ili mwaka huu 2017 tuweze kwenda pamoja.

Kama ndiyo kwa mara ya kwanza unapata taarifa hizi za semina leo na hujui nini kinaendelea, basi bonyeza hapa na soma maelezo ya semina na fanya malipo mara moja.

Nakusisitiza rafiki kwa sababu sipendi ukose nafasi hii, najua ni muhimu kwako, najua kuna kitu utakwenda kupata ambacho kitakuwezesha kuyabadili maisha yako. Na kama ambavyo nimekuwa nakuambia, iwapo hutapata thamani kwenye huduma yoyote unayolipia kwangu, basi jisikie huru kunieleza na bila ya kukuuliza swali lolote nitakurejeshea kiwango ulicholipia.

Hivyo huna chochote unachopoteza, tena kama wewe ni mjanja unaweza ukalipia ada, ukajifunza semina halafu mwisho ukadai fedha yako na kuondoka. Lakini sikushauri ufanye hivyo kwa sababu kile ulichosoma hakitakusaidia. Na pia nitajua na hivyo nitakuzuia kabisa kushiriki mafunzo mengine yoyote nitakayotoa.

Najitahidi kuweka thamani kubwa sana kwenye huduma yoyote ninayokupa wewe, najitahidi sana nihakikishe unatoka na kitu ambacho unaweza kufanyia kazi. Na kwa mwaka huu 2017 upo mwongozo kabisa wa kuyaendesha maisha ya kila siku, ambao tutaufanyia kazi kwa pamoja.

Karibu sana rafiki, usipitwe na nafasi hii ya kipekee. Nakusubiri kwa hamu ili kwa pamoja tuweze kufanya makubwa kwa mwaka huu 2017.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

ONGEA NA KOCHA; Uchawi Pekee Na Wa Uhakika Wa Mafanikio Ni Huu...

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?
Jana tarehe 02/01/2017 ilikuwa ndiyo siku ya mwisho ya kulipia ada ya kujiunga na semina ya 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO. Kama tayari ulishatuma ada na bado hujawekwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA wasap nitumie ujumbe wenye majina yako kamili kwenye namba 0717396253 kwa njia ya wasap. Pia jana kuna baadhi ya watu walipata changamoto wakati wa kulipia na kuambiwa muamala umefeli, kama ilikutokea hiyo tuwasiliane leo. Vinginevyo niwakaribishe sana wale wa semina na niwatakie wengine mwaka mwema na wenye mafanikio makubwa, tutaendelea kuwa pamoja kila siku kupitia AMKA MTANZANIA tukipeana maarifa muhimu kwa mafanikio yetu.

Leo nakwenda kukushirikisha kitu muhimu sana kwa mafanikio yako, huu ni uchawi muhimu ambao unapaswa kuwa nao ili uweze kufanikiwa. Kwa uchawi huu hakuna kitakachokuzuia wewe kufanikiwa. Kwa wale wanaoogopa na kuona labda nataka kukufundisha kuloga, hapana sifanyi hivyo, nataka nikupe mbinu ya kuweza kutumia vizuri akili yako kwa faida zako.

Nimepata wazo hili la uchawi baada ya msomaji mwenzetu mmoja kuniandikia akiniambia kwamba anafikiri yeye ana pepo maana kila akipata fedha ndiyo zinapigwa simu za ndugu wa karibu ambao wana matatizo mbalimbali, hivyo inabidi awasaidie na hivyo fedha anazokuwa amepata zinaisha. Ila anachoshangaa ni kwamba akiwa hana fedha simu nazo hazipigwi.

Nilimjibu kwamba huna pepo wala chochote, bali alichonacho ni nidhamu mbovu ya fedha na maisha kwa ujumla. Hivyo anachohitaji siyo kuondolewa pepo, bali kujijengea nidhamu nzuri ili kuweza kufika kule anakotaka kufika.

Hivyo uchawi ninaokwenda kukushirikisha leo rafiki yangu siyo mwingine bali ni NIDHAMU.

Nimekuwa nikiwasiliana na watu, nikiwashauri na kuwaongoza kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao kwa karibu miaka minne sasa, na kikubwa ambacho najifunza ni kwamba ukosefu wa nidhamu ni kikwazo kikubwa sana. Maarifa wengi wanayo, hamu ya mafanikio wengi wanayo, wanachopaswa kufanya wengi wanajua, ila tatizo ni nidhamu ya kuweza kufanya.

Watu wengi wanajua ya kwamba njia ya uhakika ya kupunguza uzito wa mwili ni kufanya mazoezi, mara kwa mara. Lakini mbona hawafanyi? Watu kwa makusudi wanachagua kutokufanya mazoezi, au wanachagua kula hovyo. Yote hii ni kwa sababu wanakosa nidhamu ya kufanya kile ambacho ni sahihi au nidhamu ya kutokufanya kile ambacho hawataki kufanya.

Kwenye mafanikio pia, wengi wanajua mafanikio yanahitaji kujituma, kujitoa, uvumilivu na muda. 

Lakini bado wengi hawafanyii hayo kazi. Tatizo kubwa hapo ni nidhamu.

Nidhamu ni muhimu sana kwenye mafanikio yako. Na nidhamu tunayozungumzia hapa siyo ya kunyenyekea na kusalimia, bali ule uwezo wa kufanya kile ambacho unapaswa kufanya, bila kuzuiliwa na sababu yoyote, na kutokufanya kile ambacho hutaki au hupaswi kufanya, bila ya kuruhusu sababu iingilie.

Sijui umenielewa vizuri rafiki, unapanga kile ambacho unahitaji kukifanya, halafu unaanza kukifanya, bila kuruhusu sababu ya aina yoyote ile ikuzuie wewe kufanya ulichopanga kufanya. 

Unapoanza kufanya yale yanayokupeleka kwenye mafanikio, sababu nyingi za kukurudisha nyuma zitajitokeza, unahitaji nidhamu ili kuweza kuendelea kufanya licha ya sababu zinazojitokeza.

Pia kama kuna kitu ambacho hutaki kufanya, hukifanyi. Hili pia linahitaji nidhamu kwa sababu kuna msukumo mkubwa wa kijamii ambao unaweza kukufanya ufanye yale ambayo hutaki kufanya kwa sababu tu kila mtu anafanya. Unahitaji nidhamu ya hali ya juu kuweza kushinda msukumo huu wa kijamii, kwa sababu ni rahisi kuona kwamba wewe ndiye unayekosea na kutamani kujiunga na kundi kubwa. Kwa mfano mara nyingi unajikuta unafanya yale mambo ambayo wanaokuzunguka wanayafanya, hata kama hujui kwa nini unayafanya, au hayana faida kwako.

Hivyo uchawi ambao kila mmoja wetu anapaswa kuwa nao ni nidhamu binafsi, nidhamu ya kuweza kujisimamia kwenye kile unachofanya, nidhamu ya kukuondoa kwenye sababu zinazokuzuia kufanikiwa.

Swali ni je unawezaje kujijengea nidhamu binafsi?

Hapa nako pia hakuna uchawi, bali unahitaji kujijengea tabia ya kufanya. Panga kile unachotaka, na anza kuchukua hatua hata kama ni ndogo sana. Chukua hatua kwa chochote unachotaka, usisubiri mpaka mambo yawe mazuri, mambo huwa hayawi mazuri hata siku moja, kila wakati kuna changamoto zake.

Usikubali sababu yoyote ikuzuie kuchukua hatua. Pale unapopanga kufanya kitu, mara moja zinakuja sababu za kwa nini huwezi kufanya kitu hicho, au unaona vitu vingine muhimu zaidi vya kufanya. usiruhusu hili likutokee, badala yake weka sababu pembeni na fanya. Fanya hata kwa hatua ndogo kabisa, kadiri unavyofanya ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kufanya.

Mwisho kabisa usifanye kitu ambacho hutaki kufanya. Katika kila kitu unachofanya kwenye maisha yako, kwanza jiulize kitu hicho kina msaada gani kwako au kwa wale wanaokuzunguka. 

Halafu jiulize je unataka kufanya kitu hicho? Je ni kitu chenye manufaa kwako na wale wanaokuzunguka? Kama jibu ni hapana, basi usikifanye, hakina faida kwako na kinakuzuia kufanya yale ya muhimu. Hapa panaweza kuwa pagumu kwa sababu utahitaji kuwaambia watu HAPANA, lakini jifunze kutumia neno hilo mara kwa mara, litakupa uhuru mkubwa sana.

Nidhamu ni muhimu mno, bila ya nidhamu huwezi kupiga hatua yoyote kwenye maisha yako.

Nikimalizia kwa kile alichoniandikia msomaji mwenzetu kwamba simu zinakuwa nyingi anapokuwa na fedha, lakini zikiisha simu haziji, ni kukosa nidhamu nzuri ya kifedha. Kwanza kabisa kwenye kila kipato unachopatwa, hupaswi kukitumia chote, asilimia kumi ya kipato unachopatwa unapaswa ujilipe wewe mwenyewe kwanza. Usiruhusu kiwango hicho kiwe na matumizi mengine yoyote, hii ni njia yako ya kununua uhuru wako, usikubali kuingilia kwa njia yoyote ile. Hivyo fanya matumizi yoyote utakayo na ile asilimia 90 ya kipato chako kinachobaki, ikiisha usijaribu hata kidogo kugusa ile asilimia 10. Kama ni watu watalala njaa basi na iwe hivyo, lakini usiguse sehemu ile ambayo umejilipa wewe mwenyewe kwanza. Na uzuri ni kwamba watu huwa wanapata njia mbadala, kama ambavyo kipindi huna fedha wana njia zao mbadala za kufanyia kazi matatizo yao.

Kujifunza zaidi kuhusu kujilipa wewe mwenyewe na ufanyie nini kile unachojilipa, soma hapa;  

Unawalipa Watu Wote Kasoro Huyu Mmoja wa Muhimu

Unahitaji nidhamu binafsi,

Unahitaji nidhamu ya fedha,

Unahitaji nidhamu ya muda,

Unahitaji nidhamu ya kufanya kile unachopaswa kufanya,

Unahitaji nidhamu ya kutokufanya kile ambacho hutaki kufanya.

Huu ndiyo uchawi wa mwaka 2017 ambao nimekukabidhi leo, ufanyie kazi kila siku, na hutabaki hapo ulipo sasa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

UCHAMBUZI WA KITABU; Sometimes You Win, Sometimes You Learn. (Somo Kubwa Unaloweza Kujifunza UCHAMBUZI Kupitia Makosa Yako).

$
0
0
Tunaishi kwenye dunia ambayo ni ya kushinda au kushindwa, kupata au kukosa, hali ambayo inayafanya maisha yetu labda yawe ya furaha sana kama tunashinda, au ya huzuni sana kama tunashindwa. Hivi sivyo maisha yanapaswa kwenda, kwa sababu jambo moja la uhakika ni kwamba, kila binadamu aliye hai, kuna namna atashindwa kwenye maisha. Yapo makosa ambayo atafanya na yatamkosesha kile ambacho anakitaka.
 

Hii ndiyo iliyopelekea mwandishi John Maxwell kuandika kitabu Sometimes You Win, Sometimes You Learn. Kauli ya kawaida iliyozoeleka na wengi ni kwamba sometimes you win, sometimes you lose, yaani mara nyingine unashinda, mara nyingine unashindwa. Lakini Maxwell anatuambia tuondoe neno kushindwa na tuweke neno KUJIFUNZA. Kwa sababu kama tunataka kunufaika na makosa tunayofanya, basi lazima tujifunze kupitia makosa hayo.

Karibu tujifunze kwa pamoja namna tunavyoweza kunufaika na makosa tunayofanya kwenye maisha yetu ya kila siku.

1. Mwisho wa kusoma siyo cheti au shahada (degree).

Umekuwa ni utamaduni wa wengi kufikiria kwamba kujifunza kunaisha pale wanapohitimu masomo yao ya shuleni. Ukweli ni kwamba unapohitimu ndiyo kujifunza kuhusu maisha kunaanza. Masomo ya shuleni yanakupa tu mwanga, lakini kujifunza halisi kupo kwenye maisha yako ya kila siku.

2. Kila mtu anashindwa, lazima na wewe utashindwa.

Ni kawaida yetu binadamu kufikiria kwamba maisha yanapaswa kuwa rahisi, sijui hata ni nani alitudanganya, kwa sababu ukiangalia mtiririko wa maisha yetu, kila kitu tumekuwa tunaanza kwa kushindwa. Angalia mtoto mdogo anapojifunza kutembea, anaanza kwa kuanguka. Lakini habaki pale alipoanguka, anaamka na kuendelea mbele.

Katika maisha yako ya kila siku, utashindwa na utafanya makosa. Hivyo usijisahaulishe wala usikubali kudanganywa kwamba maisha yako yatanyooka pekee, hata kama ungekuwa mtu gani.

3. Kushindwa ni darasa zuri mno kwako.

Unaweza kutumia kushindwa kama mwisho na kukata tamaa, au unaweza kutumia kushindwa kama hamasa ya wewe kusonga mbele zaidi. Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha, basi unachopaswa kufanya ni kujifunza kupitia kushindwa kwako, jifunze kupitia makosa yako. Kipi ulichofanya kimepelekea matokeo uliyopata.

Kushindwa halafu usijifunze chochote kutokana na kushindwa huko hapo ni kushindwa mara mbili. Usikubali kushindwa mara mbili, jifunze kwa kila kosa na kila unaposhindwa.

4. Tofauti ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

Inaanzia na namna wanavyoyachukulia makosa yao.
Mtu aliyefanikiwa anapokosea au anaposhindwa, anakubali mchango wake kwenye kushindwa kwake, anajifunza na kuchukua hatua. Wakati mwingine hawezi kurudia kosa kama lile au kushindwa kwa namna ile.

Ila sasa kwa wasiofanikiwa, hata mara moja hawezi kukubali amefanya makosa au ana mchango kwenye kushindwa kwake. Atakuja na kila sababu kwa nini ameshindwa, ila sababu hata moja haitamhusu yeye. Atakuambia kuhusu uchumi mbaya, kuhusu serikali mbovu, kuhusu wazazi waliomlea, kuhusu ndugu waliomtenga na hata kuhusu mke au mume ambaye amesababisha.

Usiwe mtu wa kutafuta sababu za kufunika kushindwa kwako, kubali mchango wako kwenye kushindwa, jifunze na songa mbele.

5. Kwa nini kushinda na kushindwa tunapokea tofauti?

Tunaposhinda tunachukulia kawaida, tunaona ni haki yetu kushinda, kwa sababu ndiyo tulichotegemea. Lakini tunaposhindwa tunaumia sana, hii ni kwa sababu tunakuwa na mategemeo makubwa ya kushinda. Tunakuwa tumewekeza hisia nyingi kwenye ushindi na tunapoukosa, tunaona kama hatustahili.

Anza kuchukulia ushindi kama ushindi, kama nafasi nzuri ambayo umeipata kwa kufanya mambo mazuri. Na pia chukulia kushindwa kama darasa la kujifunza namna bora kabisa ya kufanya mambo. Ukifanya hivi utanufaika kila mara, iwe umeshinda au umeshindwa.

6. Tengeneza mzunguko chanya kwenye maisha yako.

Tunaposhinda tunatengeneza mzunguko chanya, yaani unaposhinda kitu kimoja, unakuwa na hamasa ya kufanya kitu kingine na kingine na kingine tena. Yaani kama utaendelea kushinda basi unajikuta unafanya mengi.

Tatizo lipo kwenye kushindwa, maana hapa unatengeneza mzunguko hasi kwenye maisha yako. Unaposhindwa jambo moja, unaanza kujiona kama huwezi au hufai, hivyo unaogopa kuchukua hatua kwenye jambo jingine na hivyo kurudi nyuma zaidi.
Usikubali kushindwa kwenye jambo moja kulete mzunguko hasi kwenye maisha yako, jifunze kwa kila jambo na endelea kujaribu mengine zaidi.

7. Kujifunza kwenye kushindwa siyo kitu rahisi.

Ni kweli kujifunza kupitia kushindwa ni kitu chenye manufaa sana, lakini kwa nini wengi hawafanyi hivyo? Kwa sababu siyo rahisi. Siyo rahisi kujifunza wakati umeshindwa, kwa sababu kushindwa kunaumiza na kwa asili tunapoumizwa tunapenda kukaa na kupunguza yale machungu.
Kujifunza wakati wa kushindwa kunatutaka tuende tofauti na asili yetu. Kunatutaka tutabasamu wakati hatuna furaha, inahitaji nidhamu kuweza kufanya hivi. Jijengee nidhamu hii kwa kuanza na hatua ndogo ndogo na hatimaye utaweza kujifunza kwenye kila kushindwa unakopitia.
Mambo kumi na moja unayoweza kujifunza kupitia kushindwa;

8. UNYENYEKEVU; Hamasa ya kujifunza.

Huwezi kujifunza kupitia kushindwa kama huna unyenyekevu. Unyenyekevu ni hamasa kubwa ya kujifunza pale unaposhindwa. Kama unajiona wewe ni wa pekee sana, hustahili kushindwa, basi huwezi kujifunza kupitia kushindwa au makosa unayofanya.
Kuwa mnyenyekevu, jua unaweza kukosea, jua haupo juu ya wengine na jifunze kupitia makosa na kushindwa kwako.

9. UHALISIA; Msingi wa kujifunza.

Kitu kikubwa ambacho kushindwa kunatufundisha ni uhalisia. Kwa fikra za kawaida maisha ni marahisi sana. Watu watakudanganya mengi kuhusu maisha na mafanikio, fanya kazi hii utafanikiwa, fanya biashara hii utafanikiwa. Lakini unaposhindwa, ndiyo unakutana na uhalisia wa maisha ya kwamba kila mtu anaweza kushindwa. Na hapa ndipo kujifunza kunapoanzia.
Unaposhindwa, achana na zile hadithi za uongo ulizojazwa na uangalie uhalisia.

10. MAJUKUMU; Hatua ya kwanza ya kujifunza.

Watu wote ambao wanayachukua maisha yao kama jukumu lao, wanajifunza kupitia makosa wanayofanya na hata kushindwa wanakopitia. Tatizo lipo kwa wale ambao wanakimbia majukumu yao, wanaoona maisha yao yanatengenezwa au kubomolewa na watu wengine.
Kumbuka ya kwamba maisha yako ni jukumu lako, na hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya kujifunza kupitia makosa yako.

11. UBORESHAJI; Lengo la kujifunza.

Hakuna mtu ambaye ni mkamilifu, na hivyo kitu cha kwanza unachopaswa kujifunza kwenye kushindwa ni kujiboresha zaidi kila siku. Watu wengi wamekuwa wakiwaangalia watu waliofanikiwa na kufikiri wamefika pale mara moja. Ukweli ni kwamba hawakujikuta pale, bali wamekuwa wakipiga hatua ndogo ndogo kila siku mpaka wamefika unapowaona sasa.
Unaposhindwa, kumbuka hizo ni hatua za wewe kuelekea kwenye mafanikio, unachohitaji ni kuangalia njia ya kuwa bora zaidi leo zaidi ya jana, na kuwa bora zaidi kesho zaidi ya leo.

12. MATUMAINI; Msukumo wa kujifunza.

Bila ya matumaini, maisha hayana maana. Kwa sababu kama tulivyojifunza, utashindwa mara nyingi kwenye maisha yako, huenda kuliko hata utakavyoshinda. Unahitaji kuwa na matumaini kwamba pamoja na kushindwa unakopitia, mambo yatakuwa mazuri baadaye. Pamoja na giza kubwa unalopita wakati wa kushindwa, mwisho kutakuwa na mwangaza.
Matumaini yanakusukuma kuweza kupita wakati mgumu wa kushindwa.

13. KUFUNDISHIKA; Njia ya kujifunza.

Kushindwa na kukosea ni jambo moja, kujifunza kupitia kushindwa na makosa yako ni jambo jingine tofauti. Ni lazima uwe unafundishika ndiyo uweze kunufaika na makosa unayofanya. Kama hufundishiki, utaendelea kurudia makosa yale yale au kushindwa kwenye mambo yale yale.
Maisha ni darasa, wale walio tayari kuifunza, wana kila cha kujifunza. FUNDISHIKA.

14. CHANGAMOTO; Kichocheo cha kujifunza.

Unaposhindwa unakutana na changamoto mbalimbali, unakutana na shida na magumu ambayo kwa kuyavuka unafikia mafanikio makubwa zaidi.
Hivyo unaposhindwa, au unapofanya makosa, chukulia hicho kama kichocheo cha wewe kujifunza zaidi na kuweza kufika kule unapotaka kufika.

15. MATATIZO; Fursa ya kujifunza.

Siku zote yachukulie matatizo yako kama ni fursa kwako kujifunza, usichukulie kama kikwazo, kwa kufanya hivyo hutaweza kusonga mbele. Unapoyageuza matatizo kama fursa kwako kujifunza, unaona njia nyingi za kutoka hapo ulipo na kufika unakotaka kufika.

16. UZOEFU MBAYA; Mtazamo wa kujifunza.

Unaposhindwa, hakuna shaka ya kwamba unaisikia vibaya. Umejipanga vizuri na unategemea kupata matokeo mazuri halafu unashindwa. Au umefanya makosa ambayo hukutegemea kama ungeweza kuyafanya, kama kusahau kitu ambacho ni muhimu na inakugharimu. Lazima utajisikia vibaya sana, unakuwa ni uzoefu mbaya kwako.

Tumia uzoefu huu mbaya, kujisikia huko vibaya kama mtazamo wa wewe kujifunza. Kila unapopitia hali usiyoipenda kama hiyo ya kushindwa au kufanya makosa, kumbuka ni wakati wa kujifunza.

17. MABADILIKO; Gharama ya kujifunza.

Unaposhindwa au unapofanya makosa, unapojaribu kurudia kile kile ambacho umefanya, huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti ni kujidanganya. Ni lazima uwe tayari kubadilika kama unataka kunufaika na kushindwa au makosa unayofanya. Mabadiliko ni magumu na watu hawayapendi, lakini wewe lazima uwe tayari kulipa gharama hii, kama unataka kunufaika na kushindwa au makosa yako.

18. UKOMAVU; Thamani ya kujifunza.

Baada ya yote hayo ni kipi unaondoka nacho kwenye kushindwa? Unaondoka na ukomavu, unaondoka na uzoefu kwamba njia ipi ni sahihi kupita na ipi siyo sahihi kupita. Usije ukarudia yale yale uliyofanya na hatimaye kurudi kwenye makosa yale yale. Hakikisha kwa kila kosa unalofanya, kwa kila unaloshindwa, basi unaondoka na somo la maisha yako, la namna unavyoweza kuwa bora zaidi.

19. Mambo matatu ya ukweli unayopaswa kujua kuhusu maisha;

Moja; maisha ni magumu, usijidanganye kwa namna yoyote ile kwamba maisha yatakuwa rahisi kwako. Lazima upambane, utaanguka, utakosea na utashindwa. Lakini mwisho wa siku kama utaendelea kusonga mbele, utafanikiwa.

Mbili; maisha ni magumu kwa kila mtu. Kitu kingine ambacho watu wanajidanganya kuhusu maisha ni kuona kama wengine maisha kwao ni rahisi. Kila mtu kuna mambo anapambana nayo kwenye maisha yake, usione kwa nje ukafikiri mambo ni rahisi, ukipewa viatu vya wengine unaweza usiweze kuvivaa kabisa.

Tatu; maisha ni magumu zaidi kwa baadhi ya watu kuliko kwa wengine. Na hili ni jambo ambalo watu wanaamua kuchagua, yaani unachagua maisha yako yawe magumu zaidi kuliko ya wengine. 

Kama kuamua kutokujifunza kupitia makosa yako mwenyewe, na hivyo kuyarudia yale yale kila siku.

20. Aina tano za watu ambao maisha ni magumu zaidi kwao.
Maisha ni magumu sana kwa watu wa aina hii;

1. Maisha ni magumu sana kwa watu ambao wamegoma kujifunza na wameacha kukua kimaarifa.

2. Maisha ni magumu mno kwa wale ambao wanajaribu kuukimbia uhalisia, au kupingana na uhalisia wa maisha.

3. Maisha ni magumu sana kwa wale ambao hawafikiri kwa usahihi, wale ambao wanafanya mambo kwa mazoea na kwa kuiga, bila ya kufikiri kwa kina.

4. Maisha ni magumu sana kwa wale ambao wanachukua muda sana kufanya mabadiliko pale mambo yanapobadilika. Wale ambao wanaendelea kung’ang’ania njia za zamani ambazo hazifanyi tena kazi.

5. Maisha ni magumu mno kwa wale ambao hawazifanyii kazi changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha yao.

Usiwe katika kundi lolote la watu hao, usitake kuongeza ugumu wa maisha yako.

Ujumbe mkuu wa kitabu hiki ni mmoja; MAISHA NI KUSHINDA NA KUJIFUNZA. UKISHINDA FURAHIA NA JIFUNZE, UKISHINDWA JIFUNZE ZAIDI. USIKATE TAMAA PALE UNAPOSHINDWA, HUWEZI KUKWEPA KUSHINDWA KWENYE MAISHA YAKO, BALI UNAWEZA KUCHAGUA KUJIFUNZ AKUTOKANA NA KUSHINDWA NA HATA MAKOSA UNAYOFANYA.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Maneno Mawili (02) Yasiyokuwa Na Msaada Kwenye Maisha Yako.

$
0
0
Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? 

Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri kuishi maisha yeye maana hapa duniani. Maisha ya ubinafsi siyo maisha mazuri kuishi hapa duniani yaani unajifikiria wewe mwenyewe na siyo watu wengine. Leo ni siku ya kipekee sana kwetu tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai hivyo basi, tuitumie vizuri siku hii ya leo kwa kuzalisha mambo chanya na yenye tija kwenye maisha yetu.

Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Leo tutakwenda kujifunza maneno mawili yasiyokuwa na msaada kwenye maisha yako. Je ungependa kuyafahamu ni maneno gani hayo? Basi karibu rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja hivyo nakusihi sana uweze kusafiri na mimi mpaka mwisho wa makala hii na karibu tena tujifunze rafiki.

Inawezekana hapo ulipo umeshajilaumu sana kwenye maisha yako na kutumia haya maneno mawili hata kujilaani wewe mwenyewe na kujiona wewe siyo kitu kabisa hapa duniani. Wakati mwingine unaweza kujiona wewe ni mjinga wenzako wanaishi na wewe unachekesha tu hapa duniani kulingana na jinsi mambo yanavyokuendea.

Rafiki, maneno mawili ambayo hayawezi kuwa msaada kwenye maisha yako au yasiyoweza kubadilisha maisha yako kabisa ni LAITI NINGELIJUA. Laiti ningelijua yamekuwa ni maneno mawili yanayotumiwa na watu wengi sana katika maisha yao pale anapokuwa mambo yameenda tofauti na vile alivyotarajia.

Mpedwa msomaji, inawezekana mwingine anajilaumu na kujilaani laiti ningelijua bora ningeanza maisha yangu mapema kuliko kuendelea kula ujana ningeweza kuukomboa wakati hapa duniani na muda umeshaenda tena huwezi kupambana nao. Mwingine anajilaumu na kujilaani laiti ningelijua nisingelitegemea serikali na kuweka tumaini langu lote la maisha juu ya mikono ya serikali.

Aidha, utaendelea kujilaani na kujilaumu kwa kutumia maneno haya mawili laiti ningelijua na mwisho wake unakata tamaa kabisa ya maisha. Laiti ningelijua maana yake ni kwamba ulikuwa na tumaini la kitu Fulani halafu mambo yanakuja kwenda tofauti na ulivyotegemea. Ukichunguza kila idara ya maisha ya mtu lazima maneno haya mawili yamemgusa kwenye maisha yake.

Mpendwa msomaji, laiti ningelijua haiwezi kubadilisha maisha yako hata siku moja kwani huo ni wakati uliopita tena hauna nafasi tena kwenye maisha yako kwani wakati wenye nafasi katika maisha yako ni wakati wa sasa. Huwezi kubadilisha wakati wa jana kwani ulishapita bali unaweza kufanya kitu chochote sasa kwani ndio wakati wenye uhakika na wewe na wala siyo kesho wala baadaye.

Utaweza kujilaumu sana na kulalamika sana laiti ningelijua nisingefanya kitu Fulani, laiti ningelijua nisingelisoma masomo Fulani na mengine mengi yanayofanana na hayo. Kwanza kabisa laiti ningelijua ni dalili au ishara ya wazi kabisa inayodhihirisha kuwa mtu huyo anayesema hivyo ana dalili za ulalamikaji, kujilaani na kulaumu. Kwa mfano, Yuda Iskariyoti aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu aliweza kujilaumu na kujilaani yeye mwenyewe kwani alimsaliti Yesu na kushindwa hata kujisamehe yeye mwenyewe na hatimaye kupelekea kujinyonga.

Mpendwa msomaji, kuna kina Yuda wangapi katika maisha yetu wanafanya makosa hatimaye wanakuja kujilaumu, kulalamika, kujilaani na kushindwa hata kujisamehe yeye mwenyewe? 

Kama mtu anafanya makosa katika maisha yake kwa sababu ya laiti ningelijua halafu anashindwa kujisamehe hata yeye mwenyewe na kujipelekea hata kujinyonga na kuona hata hakuna maana hata ya kuishi hapa duniani je mtu huyo anaweza kumsamehe hata mwenzake aliyemkosea?

Mpendwa rafiki, katika maisha yako siku zote mambo hayawezi kwenda kama ulivyotarajia. 

Huwezi kuilazimisha dunia iende kama vile unavyotaka wewe iende. Hupaswi kujilaumu, kujilaani na kushindwa hata kujisamehe wenyewe kama tulivyoona mfano kupitia Yuda. Unapaswa kujiandaa tayari kisaikolojia kupata matokeo tofauti na vile unavyotarajia wewe.

Pia, unapaswa kuwa na mpango wa ziada katika maisha yako yaani Plan B. Kuna wengine tumaini lao lilikuwa ni kusoma na kumaliza hatimaye kupata ajira ndani ya serikali au nje ya serikali lakini kwa sasa mambo yamebadilika. Kama ungekuwa umejiandaa kwa mpango wa pili huwezi kuja kujilaumu kwa kusema laiti ningelijua. Hata ukisema laiti ningelijua haiwezi kubadilisha maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo, katika maisha yako chochote unachofanya jiandae kupata matokeo tofauti na unavyotarajia. Pili, ukiwa unaweka mipango yako hakikisha basi unakuwa na mpango wa ziada wa kuwa na plan B. na kama mambo yamekwenda ndivyo sivyo usilalamike chukua hatua bali chukua hatua chanya. Wengine wako mitaani wamekaa na kujilaumu bora hata wasingesoma kwa sababu wamesoma na kukosa ajira lakini kama ungejiandaa na bila kutegemea upande mmoja kwa sasa usingejilaumu.

Wewe bado ni bora kuliko mtu mwingine hapa duniani. Una kitu au hazina ndani yako ambacho bado hujaigundua. Una nafasi ya kuibadilisha duniani kama ukifikiria vya kutosha kwa kile ambacho unacho sasa.

Kwa kuhitimisha mpendwa msomaji, somo letu la leo limetualika kuwa katika maisha yetu maneno mawili laiti ningelijua hayawezi kabisa kubadilisha maisha yetu. Inatupasa kusahau yaliyopita na kuanza upya kabisa kwani katika maisha hakuna kufeli bali kuna kujifunza kutokana na makosa ya kila siku. Hupaswi kukata tamaa bali unapaswa kunyanyuka hapo ulipo uende ukaijaze dunia kwani bado ina njaa kubwa na mtu wa kuijaza ni mimi na wewe.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Vitabu 105 Tulivyosoma Kwenye Kundi La Kusoma Vitabu Kwa Mwaka 2016.

$
0
0

Rafiki,
Katikati ya mwaka 2014 nilipata maono (VISION) ya kusoma vitabu 500 ndani ya miaka mitano. Hakika haya yalikuwa maono makubwa ambayo sikuwahi kufikiri kama yanawezekana. Hivyo sikuanza kuyafanyia kazi mara moja, bali nilikaa chini nikifikiria inawezekanaje kufikia maono hayo makubwa. Mwenyewe nilipata wasiwasi kama itawezekana. Kwa wakati huo nilikuwa tayari nina miaka miwili ya usomaji wa vitabu, lakini sikuwa nimesoma vitabu vingi sana ndani ya miaka hiyo miwili.

Siku moja nikiwa na maongezi na rafiki yangu Daudi Mwakalinga nikamshirikisha hili, na akalipokea akawa chanya sana kwenye hili. Nikaona kumbe inawezekana. Basi nikakaa chini na kupiga mahesabu, vitabu 500 ndani ya miaka mitano vinaishaje? 

Nikagundua inabidi kusoma vitabu 100 kila mwaka, hivyo miaka mitano vitakuwa vitabu 500.

Nikaendelea na hesabu zangu, kama mwaka ninahitaji kusoma vitabu 100, je nitavigawaje hivyo vitabu 100. Nikaona kwa mwaka kuna wiki 52, hivyo kama nitasoma vitabu viwili kila siku, kwa mwaka vitakuwa vitabu 104, nikaona hapa sasa namba inahesabika. Vitabu viwili kila wiki, siyo mzigo mkubwa sana, angalau ni kitu kinachowezekana kufanyika.

Kufika Oktoba mwaka huo 2014 nilikuja na mpango wa kuanzisha kundi la kusoma vitabu, kwa sababu nilijua kama nataka kufikia lengo hili, basi ni vyema nikaenda na wale wanaoweza kwenda.

Kwa kuwa mimi huwa napenda kufanya mambo magumu yawe rahisi, nikasema inabidi kutengeneza kundi ambalo litakuwa na watu wanaopenda kusoma vitabu, na lisiongeze mzigo kwa mtu. Mfano ulazima wa kukutana mara kwa mara na mengine ambayo yangeweza kuzuia au kuleta changamoto kwenye usomaji wetu wa vitabu.

Hivyo nikaona njia rahisi ni kutumia teknolojia mpya zinazokuja kila siku. Hivyo nikaamua kuanzisha kundi kupitia mtandao wa TELEGRAM, wakati huo wasap ilikuwa bado hamwezi kutumiana vitabu, lakini telegram itafaa. Na nikaweka mpango kwamba tutakuwa na kundi la kusoma vitabu, ambapo shughuli pekee ni usomaji wa vitabu, na siku moja ya wiki kila mtu LAZIMA ashirikishe kile ambacho amesoma kwenye vitabu, na kwa kila kitabu ashirikishe mambo 20 aliyojifunza. Kushindwa kufanya hivyo zaidi ya wiki mbili mtu huyo anatolewa.

Basi baada ya kuona mpango huu ni mwema, ndipo nilipoandika na kutoa taarifa kwa watanzania wenzangu kupitia mtandao wa AMKA MTANZANIA. Nilijua taarifa hii ingepokelewa vizuri na kwa hamasa, lakini mambo yalikuwa tofauti. Wengi walisema haiwezekani, walipinga mno na kushangaa kabisa. lakini nashukuru kuna watu kama 50 kwa kipindi kile waliitikia wito na tukaanza kusoma vitabu.

Hapa ndipo TANZANIA VORACIOUS READERS() ilipozaliwa. Kundi la kusoma vitabu ambalo kila mtu anakaribishwa kujiunga bure kabisa, lakini asipotimiza wajibu wa kusoma vitabu na kushirikisha wengine yale aliyojifunza anaondolewa. Tangu kipindi hicho tumekuwa tunasoma vitabu viwili kila wiki na tumekuwa tunaongezeka na kupungua kulingana na watu kuweza kuendana na taratibu za kikundi.

Wapo watu walioondolewa kwenye kundi na kulalamika mno, na wakati utaratibu ulikuwa wazi kabisa kwamba usipotimiza mahitaji ya kundi la usomaji wa vitabu utaondolewa.

Ninachoweza kusema ni kwamba kwa zaidi ya miaka hii miwili ya kusoma vitabu kupitia kundi la TVR, nimejifunza mengi mno, nimekuwa nasoma vitabu vingine nje ya kundi lakini ndani ya kundi najifunza mengi zaidi.

Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana marafiki ambao tumekuwa kwenye kundi pamoja kwa kipindi hiki. Kwa kipekee niwashukuru viongozi wa kundi, Deo Kessy, Daudi Mwakalinga na Daudi Siwalaze. Wameweza kuendesha kundi vizuri kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, na tunazidi kupata na kushirikishana maarifa haya muhimu ya kuyaboresha maisha yetu zaidi.

Hapo chini nimeorodhesha vitabu 105 tulivyovisoma mwaka 2016 kwenye kundi letu hili. Unaweza kuvipitia na kujionea mwenyewe.

 Karibu uwe mwanachama wa kundi hili la kusoma vitabu.

Nawe pia unaweza kuwa mwanachama wa kundi hili la kusoma vitabu. Sifa pekee unazohitaji ni uweze kusoma Kiingereza, maana vitabu vingi ni vya Kiingereza, uwe tayari kusoma vitabu na kila Jumamosi jioni, kuanzia saa 12 jioni, uwe tayari kuwashirikisha wanakikundi mambo 20 uliyojifunza kutoka kwenye kila kitabu ulichosoma.

Kama unaona una sifa hizo na unapenda kweli kusoma vitabu, basi tuma ujumbe kwa njia ya TELEGRAM, telegram ni mtandao unaofanana na wasap, unaweza kuwa nao kwenye simu yako au hata kompyuta yako. Tuna ujumbe kwa mwenyekiti wa kundi hili, Bwana Deo Kessy, kwenye namba 0717 101 505. Mtumie ujumbe kwamba unapenda kujiunga na kundi la kusoma vitabu na umekubaliana na masharti ya kundi, kisha atakuweka kwenye kundi.

ANGALIZO KABLA HUJATUMA MAOMBO YAKO.

Hakikisha upo tayari kusoma vitabu, kwenye hili kundi hatuna biashara nyingine zaidi ya vitabu, na usipotimiza hilo unaondolewa, hakuna sababu sababu. Hivyo kama unaomba kujiunga, siku ukitolewa kwa sababu husomi vitabu na kuwashirikisha wengine, usianze kuleta malalamiko. Nasema hili kwa sababu watu wengi wakitolewa ndiyo wanakuja na malalamiko mengi.

Karibu sana rafiki kama upo tayari kuongeza maarifa zaidi. Lengo letu la kufika vitabu 500 tutalifikia bila shida, na tutakwenda zaidi na zaidi.

VITABU 105 TULIVYOSOMA KWENYE TVR MWAKA 2016.

1. 50 Great Lessons from  Life -            Tony O’Reilly


2. First things first -  Sheila Mulcahy et al

3. 10X Rule-The Only Difference Between Success and Failure - Grant Cardone

4. The DNA of relationships - Dr. Gary Smalley

5. The Master Of Destiny - James Alen

6. Are You Fully Charged - Tom Rath

7. A More Beautiful Question-Power of Inquiry to spark breakthrough Ideas         - Warren Berger

8. The Four Purposes of Life-Finding Meaning and Direction in a changing world  - Dan Millman

9. Why Motivating People  doesnt work - Susan Fowler

10. Critical Thinking - Halvey Segler

11. You Can Win - Shiv Khera

12. Simplicity Parenting - Kim John Payne and Lisa M. Ross

13. Innovation-Small book about Big ideas - Max McKeown

14. The Confidence Game- Maria Kannikova

15. Don’t Go Back To School - Kio Stark

16. In Good Times and Bad - Gary and Melisa Neuman

17. Young World Rising - Rob Salkowitz

18. The Book of Life - Krishnamurti Jiddu

19. How to become  Genius and Expert in any subject with Accelarated Learning - Harvey Segle

20. The Naked Millionaire - David Taylor

21. All Time Essentials for Entrepreneurs - Jonathan Yate

22. Managing Oneself - Peter Ferdinand Drucker

23. Handbook to higher Consciousness - Ken Keyes

24. Zen to Done-The Ultimate Simple Productivity System - Leo Babauta

25. The hard truth about Soft Skills - Peggy Klaus

26. My Philosophy for Successful Living - Jim Rohn

27. Difficult Conversation-How to discuss what matters most - Douglas Stone, Bruce Patton, Sheila Heen

28. Stunning Success - Robin Sharma

29. The Longevity Project - Dr Friedman

30. Ignore everybody and 39 other keys to Creativity - Hugh Macleod

31. SpeedWealth - T. Harv Eker

32. 7 Habits of Highly Effective People - Stephen Covey

33. The Creator's Code-The Six Essential Skills of an Extraordinary Entrepreneur - Amy Wilkinson

34. The Family First-Your Step by Step Plan of Creating a phenomenal Family - Dr. Phil McGraw

35. The essentials of Business Entiquette - Barbara Pachter

36. Strengthfinder 2.0 - Tom Rath

37. The 50th Law - 50 Cent na Robert Greene

38. Lean In - Sheryl Sandberg

39. Deep Work - Cal Newport

40. Emotional Intelligence Works - Michael Ravitz and Susan Schubert

41. Failing Forward - John C. Maxwell

42. Happier - Tal Ben Shahar

43. The leader who had no title - Robin Sharma.

44. Men are from Mars, Women are from Venus - by John Gray

45. Smart Leaders-Smarter Teams - Roger Schwarz

46. Delivering Happiness - Tony Hsieh

47. Poke the Box - Seth Godin

48. Getting Results the Agile way - J.D. Meier

49. Just Listen - Mark Goulston

50. How to turn thoughts into Things - Bo Sanchez

51. The Lost Sven Secrets of Success - Joe Vitale

52. The Wonder Weeks - Hetty Van De Rijt, Frans Plooij

53. You were born Rich - Bob Proctor

54. Sign-posts on the road to Success            - W.E Kenyon

55. Start with Why - Simon Sinek

56. The Way to Wealth - Benjamin Franklin

57. The Paradox of Choice-Why More is Less - Schwartz

58. Business at the Speed of Thought - Bill Gates

59. Tao Te Ching - Lao Tzu

60. 5 Love Languages of Children - Gary Chapman

61. Brain Storm: Tap into Your Creativity to Generate
Awesome Ideas and Remarkable Results  - Jason Rich

62. The Defining Decade-Why your twenties matters - Meg Jay, PhD

63. How To Manage Your Boss - Ros Jay

64. Coach Yourself To Win - G. Huttman

65. Think Like a Champion - Donald Trump

66. Smart Leadership - Jonathan Yudelowitz

67. Eight Lessons for a Happier Marriage - William Glasser and Carleen

68. Blue Ocean Strategy - Kim Chan

69. Notes from a Friend - Anthony Robbins

70. Generation iY-Our Last Chance to Save their future - Tel Elmore

71. Be Your Own Brand - David and Karl D. Speak

72. Being Married - Sharon Aris

73. Secrets of The Richest Man Who ever lived - Mike Mudock

74. Entrepreneurship 101 - Donald Trump

75. Selfish reasons to have more kids - Bryan Caplan

76. Prosperity on Purpose - Justine Herald

77. The Righteous Mind - Haidt

78. One Minute Manager - K. Blanchard

79. It's not about the money - Bob Proctor

80. Rules for  a knight - Ethan Hawke

81. The 21 Irrefutable Laws of Leadership - John C. Maxwell

82. The Most Successful Business in the World - Michael E. Gerber

83. Secrets of Self -Made Millionaires - Adam Khoo

84. Artificial Maturity-Helping Kids Meeting the Challenge of becoming Authentic 
Adults - Tim Elmore

85. From Poverty to Power - James Allen

86. Invisible Gorilla - Christopher Chabris

87. 10- Minutes Toughness - Jason Selk

88. The Road To Character - David Brooks

89. What Winners Do to Win - Nick Joy

90. Love is a Mix Tape -  Sheffield Rob

91. A Whole New Mind-WHY RIGHT BRAINERS WILL RULE THE FUTURE - Daniel H. Pink

92. Power of Thinking Without Thinking - Malcolm Gladwell

93. Alone Together - Sherry Turkle

94. Mountains beyond mountains - Trancy Kidder

95. The Total Money Make Over - Dave Ramsey

96. Mentored by a Millionaire - Steven Km Scrott.

97. Unleashing Power of Rubber bands - O.Nancy

98. Daring Greatly-How the Courage to Be Vulnerable Transpforms the Way we Live, Love, parent and Lead - Brene Brown

99. 7 Keys to 1000 Times More            - Mike Mudock

100. Winning - Jack and Suzy Welch

101. Flash Foresight-How to seed the Invisible and Do the Impossible - Daniel Burrus

102. I AM MALALA - The Girl Who Stood Up for Education and was Shot by the 
Taliban - Malala Yousafzai

103. Lead The Field - Earl Nightngale

104. Love Dare

105. Sometimes You Win Sometimes You Learn - John C. Maxwell
                       
Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA 
MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku.  

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na 
kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

USHAURI; Hatua Za Kuchukua Pale Watu Uliowakopesha Fedha Hawataki Kukulipa.

$
0
0
Habari za leo rafiki?

Karibu kwenye kipengele chetu cha ushauri wa changamoto mbalimbali ambazo zinatuzuia sisi kufikia mafanikio makubwa. Kupitia kipengele hiki unaniandikia changamoto inayokusumbua na mimi nakushauri hatua sahihi unazoweza kuchukua ili kuondokana na changamoto hizo.
 

Changamoto ni sehemu ya maisha yetu, hivyo hatupaswi kuzikimbia u kuziogopa, bali kujifunza kupitia changamoto hizo ili kuwa bora zaidi.

Leo tunakwenda kuangalia changamoto ya kuwakopesha watu fedha halafu wanashindwa kukulipa. Je unawezaje kuondokana na hali hii? Tutajifunza kupitia changamoto ya msomaji na rafiki yetu, kama alivyotuandikia.

SOMA;  USHAURI; Jinsi Ya Kuondoka Kwenye Madeni Mabaya.

Habari coach.
Changamoto yangu kubwa ni kuwa na huruma sana iliyopitiliza ambapo mtu akiwa na shida na kuja kwangu na kukopa pesa basi ni lazima nitampa hata kama nina hela ya mtu ili mradi tu ananiahidi kuwa atalipa. Hii imenipelekea kuwakopesha watu wengi zaidi ya milioni 10 kwa kiasi tofauti kwa kila anayekuja. Matokeo huu ni mwaka wa 3 sasa hizo pesa sijalipwa naishia kugombana na watu tu. Nisaidie kuondokana na tatizo hili. Kwani imefika mahali sasa mambo yangu yote hayaendi tena wengine wananiendea kwenye imani za kishirikina ili nisahau kuwadai. Pia ninapowadai napata sana taabu ya kuishia kwenye beef na mtu pamoja na familia zao. Clara F. N

Clara kwanza kabisa nikupe pole kwa changamoto hiyo unayopitia, ni hali ya kuumiza sana pale unapomwamini mtu na kutoa msaada halafu msaada wako unaishia kukuumiza wewe mwenyewe. 

Ni haki yako kabisa kupata fedha zako ambazo umewapa watu hao na inaumiza pale unaposhindwa kutimiza mipango yako mingine kutokana na watu kushindwa kutimiza walichoahidi.

Lakini pamoja na matatizo hayo ya watu, wewe mwenyewe umechangia kuingia kwenye matatizo hayo, na hivyo napenda tuanzie hapo, tuanze na wewe kwanza. Ili ujifunze na hili lisirudie tena kwako.

Kuhusu tabia yako ya kukopesha kwa urahisi.

Iko hivi, binadamu wanapenda kupata kitu kwa urahisi, hivyo kwa namna yoyote ile wamekuwa wakitafuta njia rahisi ya kutimiza mahitaji yao. Na wanapoipata njia hiyo wanawaambia na wengine pia, kama ulivyo msemo kizuri kula na wenzio.

SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Madeni Sugu Na Kufikia Uhuru Wa Kifedha Kwenye Maisha Yako.

Sasa hiki ndiyo watu wamekuwa wakifanya kwako, wanajua una udhaifu wa huruma, unaweza kumsikiliza mtu na ukamhurumia bila hata ya kuhoji wewe ukachukua hatua ya kumsaidia. Hivyo kesho atakuja tena na hadithi yenye huruma zaidi na wewe utasaidia. Na kibaya zaidi watawaambia wenzao pia na wao watakuja na hadithi zenye huruma na wewe utaishia kukubaliana nao na kuwakopesha.

Hivi ndivyo umetengeneza matatizo hayo ya kifedha mpaka kufikia kiwango hicho cha milioni 10.

Ukweli ni kwamba uliwakopesha watu fedha bila ya kujiridhisha iwapo wanazihitaji kweli, na kama wanazihitaji kweli basi hukujiridhisha kama wanaweza kuzilipa. Na hivyo kufanya kosa kwako na kwa wao pia. Kwa kifupi iko hivi, watu wanapenda fedha za kupata kiurahisi, hivyo wakiona mwanya huo wanautumia, hawataki kujali watakuja kuzilipaje. Hivyo kwa kuwa wewe ulikuwa unatoa kiurahisi, hata wale ambao walikuwa hawana uhitaji mkubwa sana na wao walishawishika kukukopa, na kama ni ndugu basi ulichochea zaidi.

Unafikiri kwa nini benki huwa haziwakopeshi watu kirahisi? Kwa sababu wanajua kusingekuwa na masharti kila mtu angekimbilia kuchukua mkopo, na wengi wa hao hawawezi kulipa mikopo hiyo kabisa.

Hivyo basi, hatua ya wewe kuchukua kwa sasa, ili kuepuka matatizo zaidi kwako, usikopeshe mtu kabisa. kwa vyovyote vile usikopeshe mtu, kama kuna mtu ana shida kweli na wewe unaona ana shida ya uhakika, ya kufa na kupona, basi msaidie. Hata kama yeye anataka kama mkopo, mpe kile kiasi ambacho hata kama hatakurudishia utakuwa umempa kama sehemu ya msaada wako kwake. Lakini kukopesha kwa ahadi ya kurejeshewa baadaye usifanye hivyo.

Yaani kataa kabisa na kama ni ndugu yako ndiyo unahitaji kuwa makini zaidi. Kama nilivyosema hapo juu, saidia pale unapoweza lakini usikopeshe. Utajikuta unazidi kutengeneza matatizo makubwa kwako na kuharibu mahusiano yako na wengine.

SOMA; Jinsi Ya Kuondoka Kwenye Madeni Mabaya.

Najua hili linaweza kuwa gumu kwako, kwa kuwa utahofia watu watakuona una roho mbaya, lakini fanya hivyo. Mtu anapokuja kutaka mkopo mweleze hata wewe una changamoto za kifedha. Hii itakupa wewe uhuru wa kuweza kutekeleza mipango yako ya kifedha. Kama ipo shida kubwa saidia kadiri ya uwezo wako.

Kuhusu fedha unazodai sasa.

Kwa wale ambao unawadai sasa, mtafute kila mmoja na kaa naye chini. Mwulize kuhusu deni lake kwako na mwulize ana mpango gani wa kukulipa. Msikilize kwa makini amepanga kukulipaje, kiasi gani na kwa muda gani. Na kama hana mpango kabisa wa kukulipa mwambie akuambie hivyo. Sasa mtu akishakupa huo mpango wake wa kukulipa, mwambie muandikishiane na mtafute shahidi wa kusimamia hilo. Na kama atashindwa kutimiza kile alichoahidi basi uwe na nafasi ya kuchukua hatua zaidi. Fanya hili kwa utulivu wa hali ya juu, usiwe na jazba au kuonesha kama unataka kumkomoa, bali ongea na kila unayemdai vizuri kutaka kupata mpango wake wa kukulipa.

Iwapo mtu ameonesha hana nia ya kukulipa tena basi wewe angalia mwenyewe hatua zipi unachukua. Kama ni mimi ningeachana naye, na kuendelea na maisha yangu. Najua kuachana naye inanipa mimi uhuru wa kufanya mambo yangu na siyo kusumbuana na mtu ambaye hana mpango wowote wa kulipa. Lakini pia atakuwa ameamua kuharibu kabisa mahusiano baina yetu. 

Hivyo chagua kama utaamua kuchukua hatua au kuachana na wale ambao hawana mpango wa kukulipa.

Kuhusu kufanyiwa ushirikina ili usahau kudai.

Hii siyo kweli rafiki, hakuna anayeweza kukufanyia wewe ushirikina ili usahau kumdai. Bali wanachokifanya watu ni kucheza na hisia zako ili uone aibu kuwadai au uwaonee huruma kuwadai. Hivyo kuwa makini, fanya kama nilivyokushauri hapo juu na fuatilia kadiri mtakavyokubaliana. Kama utasahau hapo ni wewe mwenyewe na siyo ushirikina wa mtu. 

Ingekuwa watu wana uwezo wa kutumia ushirikina kwa aina hiyo, wangeutumia kukopa kirahisi benki na kusahaulisha benki isiwadai. Lakini hilo halitokei kwenye benki kwa sababu benki zinaendeshwa na taratibu na siyo hisia.

Mwisho kabisa nikutake utue mzigo huo na kuweza kupiga hatua. Hata kama watu watakubaliana na wewe kukulipa, usiweke fedha hiyo ya deni kwenye mipango yako mingine. 

Unaweza kuamua kuchukulia kama umefanya biashara ukapata hasara. Hii itakupa wewe nafasi ya kuchukua hatua mpya kwenye maisha yako, ambapo utajua kipi sahihi kufanya. Na kumbuka, usikopeshe tena, saidia pale unapoweza, lakini usikopeshe. Na kwa upande wa ndugu kuwa makini zaidi, maana hawa wanajua udhaifu wako na kuweza kuutumia kwa manufaa yao.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Siri Ya Kudumu Katika Mahusiano Ya Ndoa.

$
0
0
Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa.  Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani.  Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa:

1. Mapenzi ya kweli. 

Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua.

2. Uvumilivu

Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha.  Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu.  Hii itawasaidia sana kuweza kutengeneza maelewano ndani ya nyumba.


 3. Hofu ya mungu.

Ndoa yeyote ile ambayo inataka kuwa imara ni lazima iwe na hofu ya Mungu ndani yake.  Kama mliapa ya kwamba mtaishi pamoja mpaka kifo kitakapo watenganisha, hivyo ili yote hayo yawe kweli ni lazima Mungu atawale katika ndoa yenu ili muweze kutimiza lile ambalo mlikuwa mmeliahidi mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na mashaidi wengine. 


 4. Uwezo wa kujishusha.

Hakuna kitu muhimu katika  mahusiano kama hiki. Kuwepo na uwezo wa kujishusha katika mahusiano kunafanya mahusiano hayo kuimarika. kwani ndoa    nyingi hufa kwa sababu ya kutokuwa na mtu mmoja ambaye anajishusha. Hata ugomvi wa wanandoa wengi hutokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu hicho. 

Hivyo ili uweze kudumu katika ndoa ni kazima uwe na uwezo kujishusha hasa pale unapokosea.  Pia katika suala la kujishusha ni lazima ujue matumizi ya samahani. Neno samahani lina thamani kubwa katika kuongeza upendo kwa mwenzi wako.

5.  Matumizi mazuri ya pesa.

Hili ni la muhimu kwa wanandoa. Kwa upande wa wanaume ili uweze kuwa bora, ni lazima uweze kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo kwa mkeo yatakuwa ni kero.  Na pia kwa mwanamke ili kumfurahisha mwanaume ni lazima awe na nidhamu ya fedha,  hapa nikiwa na maana ya kwamba fedha za matumizi ambazo unaachiwa au kutafuta mwenyewe ni lazima uweze kuzitumia katika mpangilio.

 6. Uchaguzi mzuri wa marafiki. 

Ukiwa katika ndoa ni lazima uwe na marafiki sahihi ambao mwezi wako watampendeza kitabia, kwani wapo baadhi ya marafiki wao kazi yao ni kuvunja ndoa za watu.  Watu hawa kazi yao ni kichwa maneno kutoka upande A kwenda upande B. 

Marafiki wa aina hii hawafai hata chembe. Hivyo ili kudumu katika mahusiano ya ndoa lazima ufanye uchaguzi sahihi wa marafiki. 

Mpaka kufikia hapo sina la ziada endelea kujifunza kupitia www.amka mtanzania.com kila siku.

Ndimi Afisa mipango Benson chonya


UCHAMBUZI WA KITABU; THE SLEEP REVOLUTION (Boresha Maisha Yako Kupitia Usingizi Wako)

$
0
0
Moja ya mahitaji muhimu sana kwenye maisha yetu ni kupata muda wa mwili na akili zetu kupumzika. Mwili unafanya kazi kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku, na unahitaji pia muda wa kupumzika ili kuweza kuendelea kufanya kazi zaidi kwa siku zinazofuata.
 

Lakini dunia ya sasa imebadilika mno, kumekuwa na mambo mengi ya kufanya kuliko muda tulionao wa kufanya mambo hayo. Na imekuwa ni tabia kwa watu kwamba pale wanapohitaji muda na hawana, basi ipo sehemu moja ya kuiba muda, na sehemu hiyo ni kwenye muda wa kulala, au muda wa usingizi.

Tunaishi kwenye zama ambazo usingizi unaonekana kama ni anasa, kulala ni sawa na kupoteza muda. Kutokana na kasi ya mabadiliko, watu wengi wamepunguza sana muda wa kulala. Licha tu ya mahitaji ya kazi, teknolojia nayo imeingilia sana nafasi yetu ya usingizi. Sasa hivi tunavyo vifaa (simu janja) ambavyo vinatuunganisha na dunia masaa 24 kwa siku. Tunaenda vitandani na vifaa hivi na tukiamka tunavyo. Imefika hatua mtu anachelewa kulala kwa sababu tu anafuatilia mambo yanayoendelea kupitia mtandao wa intaneti.

Mwandishi Arianna Huffington, mwanzilishi wa jarida la Huffington Post, alijifunza thamani na umuhimu wa usingizi kwenye maisha yetu kwa njia ngumu. Alijifunza baada ya kuanguka na kupoteza fahamu ghafla kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kupata muda wa kutosha wa kulala.

SOMA; Hatua Sita Za Kubadili Maisha Yako Na Kufikia Mafanikio Makubwa.

Baada ya tukio hili aliamua kufanya utafiti wa kutosha kwenye eneo la usingizi na ndipo akaandika kitabu hiki cha THE SLEEP REVOLUTION. Karibu nikushirikishe yale muhimu niliyojifunza kwenye kitabu hiki.

1. Kuna kiwango cha kuchoka ambapo mtu anakuwa hajui hata kama amechoka, sawa na kiwango cha ulevi ambapo mtu haelewi kama amelewa. Hivi ndivyo dunia ya sasa inavyokwenda, watu wengi wana uchovu na wamekusa muda wa kulala, na hivyo kupeleka siku zao kwa kujisukuma na kushindwa kufanya mambo makubwa.

2. Usingizi ni kitendo ambacho kimekuwa kinaheshimiwa toka enzi na enzi. Kwa sababu huu ndiyo wakati ambao watu waliweza kupumzika na kujiandaa na shughuli za siku inayofuata. Pia ndiyo wakati ambapo watu walipata kuja pamoja. Usingizi pia umekuwa ni wakati wa watu kuota na baadaye kutafsiri maana ya ndoto zao. Hivi ndivyo ilivyokuwa, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa.

3. Kwa dunia ya sasa, sehemu rahisi ya kuiba muda ni kwenye usingizi, kupunguza muda wa kulala, pale watu wanapotaka kufanya kazi zaidi, wanapunguza muda wa kulala, pale watu wanapotaka kusoma zaidi wanapunguza muda wa kulala. Hapa tunatengeneza deni ambalo lina madhara makubwa sana kwetu baadaye.

4. Ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya watu kwenye jamii zetu hatupati usingizi wa kutosha. Hasa kwa wafanyakazi, wafanyabiashara, wanafunzi na watu wengine ambao wana shughuli mbalimbali. Tumekuwa tunahitaji muda zaidi na sehemu pekee ya kupata muda huo ni kupunguza muda wa kulala, kitu ambacho kinapelekea kupunguza ufanisi wetu, umakini na kuharibu afya zetu.

5. Kwenye jamii nyingi limekuwa linaonekana ni jambo la kishujaa kwa wale ambao wanalala muda mfupi. Watu wamekuwa wakijisifia kabisa, mimi nalala masaa manne tu, au mimi naweza kukesha na mambo yangu yakaenda vizuri. Kwenye jamii nyingi, anayelala mapema anaonekana ni mvivu au hajui anachokitaka, hivyo watu wengi wamekuwa wanajichelewesha kulala huku hakuna la muhimu wanalofanya. Na hata kama wanafanya la muhimu, madhara ya usingizi wanayotengeneza ni makubwa sana.

6. Muda tunaolala siyo muda unaopotea. Ukiangalia kwa haraka unaweza kusema kwamba kulala ni kupoteza muda. Lakini wanasayansi kupitia tafiti wanatuonesha kwamba muda tunaolala kuna mambo mengi yanayoendelea kwenye mwili wetu kwa ajili ya kuufanya kuwa bora zaidi. Ukichukulia mwili kama mfano wa gari, wengi wameuwa wanafikiri kulala ni sawa na kuzima gari, kuna mpaka usemi kwamba kulala ni kuangusha gari. Lakini ukweli ni kwamba kulala ni sawa na gari ambayo imewashwa na kuwekwa gia ambayo ni neutral na hiyo lipo kwenye mngurumo muda wote.

7. Muda tunaolala ndiyo muda ambao mwili na akili zetu zinafanya usafi. Ni muda ambao mwili na akili vinajiandaa kwa ajili ya siku ambayo inafuata. Kama tukichukulia mwili kama betri, basi kulala ndiyo muda w akuchaji betri na unapofanya kazi ndiyo unaitumia betri. Mwisho wa siku betri inakuwa imeisha na inahitaji kuchajiwa tena. Sasa unapochelewa kulala au kukosa usingizi wa kutosha, ni sawa na betri uliyochaji halafu haikujaa, haiwezi kufanya kazi muda mrefu. Ndiyo maana utajikuta unaianza siku yako ukiwa umechoka. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kuchaji betri yako, yaani muda wa kutosha wa kupumzisha mwili na akili yako kupitia kulala.

SOMA; Kanuni Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako. (Hatua Nne Muhimu Za Kufuata).

8. Yafuatayo ni madhara ya kukosa usingizi wa kutosha;

i. Mwili kuwa na uchovu muda wote.

ii. Kupungua kwa kinga ya mwili na kupata magonjwa mara kwa mara.

iii. Kuongezeka kwa uzito wa mwili na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa kama kisukari na presha.

iv. Kupata msongo wa mawazo na baadaye sonona.

v. Kukosa umakini kwenye kazi na kufanya makosa ya wazi.

vi. Kukasirika haraka kwa mambo madogo.

vii. Kusinzia sehemu ambazo siyo sahihi.

viii. Kupata magonjwa ya akili na kupoteza kumbukumbu.

9. Kukaa masaa 24 bila ya kulala ni sawa na mtu mwenye kilevi cha asilimia 0.1 kwenye mwili wake. Hiki ni kiwango ambacho kisheria huruhusiwi kabisa kuendesha gari au chombo cha moto. Hii ni kwa sababu uwezo wako wa kufanya maamuzi unakuwa umeshuka mno kiasi cha kufanya makosa ya wazi wazi kabisa.

10. Baada ya usingizi kuwa tatizo la msingi kwa watu wengi, watu wameamua kutafuta njia ya mkato ya kutatua tatizo hili na hapa ndipo matumizi ya dawa za usingizi yalipoanza kushika kasi. 
Makampuni ya madawa, hasa kwa nchi zilizoendelea yamenufaika sana na kuwauzia watu dawa za usingizi. Lakini dawa hizi zimekuwa hazitibu tatizo la msingi, badala yake zinatuliza tu dalili za tatizo.

11. Njia nyingine ya mkato ambayo watu wamekuwa wanaitumia kuiba muda mwingi kwenye usingizi ni kutumia vinywaji ambavyo vinachangamsha, vinywaji kama kahawa, au vinywaji vya kuongeza nguvu yaani ENERGY DRINKS kama redbull. Hii ni njia ya kudanganya mwili kwamba haujachoka na hivyo kuendelea kuutumia, lakini gharama yake ni kubwa sana baadaye.

12. Mapinduzi ya viwanda ndiyo yalileta mvurugano mkubwa kwenye utaratibu wa kawaida wa kulala. Ni katika kipindi hiki ambapo wamiliki wa viwanda walipohitaji kupata uzalishaji zaidi kwa kutumia gharama ndogo na hivyo kuja na utaratibu wa kufanya kazi kwa shifti na kwa muda mrefu. Hapa ndipo wafanyakazi walipoanza kufanya kazi kwa zaidi ya masaa 12.

13. Mtazamo wa watu wengi ni kwamba kulala sana ni kupoteza muda. Mvumbuzi Thomas Edison wakati wa uzee wake alipoulizwa kuhusu mtazamo wake kwa maendeleo ya siku za baadaye alisema watu wa siku zijazo watatumia muda mfupi kitandani. Kiongozi wa kivita wa zamani wa ufaransa Napoleon alipoulizwa kuhusu muda wa kulala alijibu, masaa sita kwa mwanaume, saba kwa mwanamke na nane kwa mjinga. Kwa ushawishi wa aina hii kutoka kwa watu waliopita, si ajabu usingizi kuonekana ni kitu cha kupoteza muda.

14. Swali la msingi kabisa ni kwa nini tunalala? Ipi faida ya kulala? Kulala kuna faida nyingi sana kwenye mwili na afya zetu, kulala kunaupa mwili nafasi ya kupumzika, kujitengeneza upya na kuondoa sumu kwenye mwili na akili. Pia kulala kunaupa ubongo nafasi ya kukua. Kwa tafiti za kisayansi inaonesha kwamba ubongo wetu unaendelea kukua licha ya umri tulionao. Zamani iliaminika kwamba mtu akishakua basi ubongo unakoma kukua, lakini si kweli, ukuaji wa ubongo unaendelea kadiri tunavyoupa nafasi ya kukua.

15. Kuna hatua nne za kulala, kila hatua ina umuhimu mkubwa kwenye maisha yetu.
Hatua ya kwanza ni usingizi mwepesi, hili ni daraja kati ya kuwa macho na kuwa umelala. Huu ni ule wakati ambao haupo macho kabisa na pia haupo usingizini.
Hatua ya pili ni usingizi mzito kiasi, hapa macho yanaacha kucheza cheza, joto la mwili linapungua.

Hatua ya tatu ni usingizi mzito ambao una mawimbi ya delta. Huu ni usingizi mzito sana ni siyo rahisi kuamshwa kutoka kwenye usingizi huu. Na ikitokea umeamshwa kwenye hatua hii ya usingizi basi akili yako inakuwa haielewi nini kinaendelea.

SOMA; Viungo Vikuu Vitatu(3) Vya Furaha Ya Kudumu Kwenye Maisha.

Hatua ya nne ni usingizi unaojulikana kama REM SLEEP yaani RAPID EYE MOVEMENT, macho yanakuwa yanacheza cheza. Katika hatua hii ya usingizi ndipo tunapokuwa na ndoto. Mawimbi ya ubongo wakati huu yanakuwa ya kawaida, na ndoto tunazozipata kwenye usingizi huu tunazikumbuka vizuri.

16. Tafiti za kisayansi zinaonesha kwamba ukiipa akili yako jukumu la kufanyia kazi unapokwenda kulala, unaamka ukiwa na majibu au ukiwa na hatua za kuchukua. Hii inaonesha namna ambavyo usingizi ni muhimu kwa maisha yetu ya kawaida.

17. Kukosa usingizi kunahusishwa na kusambaa kwa kazi kwa baadhi ya kansa. Hii inatokana na kupungua kwa kinga ya mwili ambayo inapambana na mabadiliko yanayotokea kwenye mwili. Unapokosa muda wa kulala, kinga yako ya mwili inapungua.

18. Kukosa muda wa kulala pia kunahusishwa na ugumba kwa wanawake na wanaume pia. Kukosa muda wa kutosha wa kulala, kunasababisha uzalishwaji kidogo wa homoni ya testesterone ambayo ndiyo inazalisha mbegu za kiume. Pia kunasababisha kuharibika kwa mpangilio wa homoni mbalimbali za uzazi kwenye mwili wa mwanamke na hivyo kuwa vigumu kubeba ujauzito.

19. Ndoto ni moja ya sehemu muhimu ya usingizi wetu. Kuna maelezo mbalimbali kuhusu ndoto, yapo maelezo kwamba ndoto ni sauti iliyopo ndani yetu ambayo inajua kipi sahihi kufanya lakini huwa hatuipi nafasi na hivyo tunapopumzisha akili zetu sauti hii inapata nafasi. Yapo maelezo kwamba ndoto ni mrejesho wa mambo tuliyofanya kwenye siku yetu au mambo tunayohofia. Kwa vyovyote vile, ndoto zetu ni muhimu na hivyo tunapaswa kuziandika pale tunapoamka na kuona namna tunavyoweza kuzitumia.

20. Swali la msingi kabisa ni je ni muda gani sahihi wa kulala? Yaani muda sahihi kulala ni masaa mangapi? Kutokana na tafiti za kisayansi, muda wa kulala unatofautiana kwa makundi mbalimbali ya watu. Na hapa ni muda kutokana na makundi mbalimbali;

Watoto wachanga (miezi 0 mpaka 3) masaa 14 mpaka 17.

Watoto wa miezi 4 mpaka 11 masaa 12 mpaka 15

Watoto mwaka mmoja mpaka 2 masaa 11 mpaka 14

Watoto miaka 3 mpaka 5 masaa 10 mpaka 13

Watoto miaka 6 mpaka 13 masaa 9 mpaka 11

Watoto miaka 14 mpaka 17 masaa 8 mpaka 10.

Vijana miaka 18 mpaka 25 masaa 7 mpaka 9

Watu wazima miaka 26 mpaka 64 masaa 7 mpaka 9.

Wazee miaka 65 na kuendelea masaa 7 mpaka 8.

Kwa tafiti za kisayansi, huo ndiyo muda sahihi wa kulala ambao ukiweza kuupata unapata manufaa yote yanayotokana na usingizi na kuepuka matatizo yanayotokana na kukosa muda wa kulala.

Weka ratiba zako vizuri ili uweze kupata muda wa kutosha wa kulala, usingizi ni sehemu muhimu ya maisha yetu.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Hii Ndio Dayari Unayopaswa Kwenda Kuichoma Moto Leo Katika Maisha Yako.

$
0
0

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu unaendelea vizuri na maisha yako lakini pia unaendelea kugusa maisha ya watu wengine na siyo kuishi maisha ya kibinafsi ya kujifikiria wewe mwenyewe na familia yako. Leo ni zawadi ya kipekee sana katika maisha yetu hivyo ni vema na haki kuitumia zawadi hii vizuri kwa kuzalisha mambo chanya katika maisha yetu.
 

Mpendwa msomaji, kila siku unatakiwa kujitahidi kuanza siku yako katika hali ya mtazamo chanya. Hakikisha asubuhi yako umeianza kwa kuingiza kitu chanya na siyo kuanza kusikiliza habari ambazo zinakuletea mtazamo hasi wa siku. Kwa mfano, unafungulia habari katika radio asubuhi unasikia watu kumi wameuawa na bokoharamu je habari hiyo itakusaidia nini katika maisha yako? Kwa hiyo habari nyingi zimeandaliwa kimasilahi hususani katika magazeti zinawakosesha matumaini watu wengi na kuwaaminisha kuwa duniani si sehemu salama.

SOMA; Mambo Mawili (2) Ya Msingi Ya Kuzingatia Katika Msamaha Wa Kweli.

Rafiki, napenda kukushauri usianze siku yako kwa kusikiliza habari kwani hazitokupa utulivu wa akili na utashindwa kuanza siku yako kwa furaha na hamasa kubwa ya kwenda kufanya kazi. 

Basi, ndugu msomaji, nikualike tena katika makala yetu ya leo ambapo leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja dayari unayopaswa kwenda kuichoma moto leo katika maisha yako.

Mpendwa msomaji, huenda unajiuliza katika akili yako ni dayari gani basi unayopaswa kwenda kuichoma katika maisha yako? Ili kuweza kufahamu ni dayari gani unayopaswa kwenda kuchoma moto leo basi nakualika uweze kusafiri pamoja nami mpaka mwisho wa somo letu la leo ili uweze kuyafahamu yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Karibu sana rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la ndugu alichaguliwa kuongoza kikundi cha watu kumi na tano. Ndugu huyo alipochaguliwa kuongoza kikundi cha watu hao kumi na tano alikuja na sera zake juu ya kuliongoza kundi lake. Ndugu huyo baada ya kuwasilisha sera zake katika kikundi hicho wale wenzake kumi na nne walimpinga pamoja na kumcheka na kumkebehi kulingana na aina ya uongozi wa ndugu huyo.

Kila siku ndugu alikuwa akijaribu kuwasilisha mambo kwa wanakikundi wake lakini wanakikundi wenzake waliendelea kumpinga na kuchemka na kumpa kila aina ya kebehi unayoijua. Ndugu huyo baada ya kuona kila anapofanya jambo hakubaliki kwa wenzake aliamua kuchukua dayari au kijitabu kidogo ili aweze kuandika orodha ya machungu na maumizo ya moyo.

SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2

Ndugu aliendelea kuwaongoza hivyo hivyo kwa muda mrefu sasa huku akiendelea kuwaongoza wenzake aliendelea kuandika kila siku yale mambo mabaya anayotendewa na wenzake. Aliamua kuandika machukizo yote anayofanyiwa katika maisha. Hivyo dayari ya kuorodhesha maumizo iliendelea kujaa. Alikuwa anaandika na kuyasoma yale maumizo anayopatiwa na mwenzake kila siku.

Ndugu msomaji, yale maumivu aliyokuwa anayaandika na kuyasoma kila siku yaliendelea kugeuka kuwa mwiba na kumuumiza moyo wake. Majeraha ya nafsi yaliendelea kumtafuna kila siku huku akijua njia bora ya kumaliza matatizo ni kuendelea kuandika na kuyasoma kila siku.

Mpendwa msomaji, tunajifunza nini kupitia ndugu huyu? Tunajifunza kuwa katika maisha yetu hatupaswi kuandika orodha ya maumivu tunayofanyiwa na wengine katika maisha yetu. Ndugu huyu alisahau kabisa kuwa dawa ya kuondoa maumivu katika moyo ni kumfutia mtu deni kwa kumsamehe tu. Ndugu alishindwa kufikiria njia nzuri ya kuondokana na mateso moyoni ni kusamehe badala ya kuendelea kuorodhesha maumivu.

Siku moja ndugu alichukua dayari yake aliyokuwa akiandikia majeraha ya moyo wake akaanza kusoma mwanzo hadi mwisho. Baada ya kusoma aliweza kupata na maumivu na majeraha makubwa katika maisha yake aliamua kulia kwa uchungu na hatimaye alifanya maamuzi ya kuchoma daftari la kuandika kumbukumbu ya orodha ya maumivu.

SOMA; Hizi Ndizo Lugha Tano (5) Muhimu Za Kuonesha Upendo Kwenye Mahusiano Yetu.

Baada ya kulichoma daftari hilo alijihisi mtu mpya katika maisha yake na kujiona mtu wa furaha na amani katika maisha yake.

Kweli msamaha huleta uhuru wa ndani na kutambua amani ya ndani na kuonja huruma ya Mungu ndani ya maisha yetu. Ni watu wangapi katika maisha yetu wanaendelea kuteseka katika maisha yako kuandika maumivu katika mioyo yao na kushindwa kusamehe? Ni vema kuamua kuchoma dayari ya maumivu katika maisha yako na kuwa mtu mpya.

Hatua ya kuchukua leo, nenda leo kachome daftari la kumbukumbu ya orodha ya maumivu katika maisha yako. Kachome daftari na kuanza maisha mapya ya uhuru na amani ya moyo na siyo kuandika maumivu kama mfano wa ndugu hapo juu.

Kwa hiyo, msamaha ni dawa ya kufuta maumivu uliyoandika katika dayari ya moyo wako. 

Unaposamehe unakuwa unamfutia mtu deni na hivyo kubaki huru. Kumbuka upendo haukasiriki pale unapomsamehe mwenzako bali upendo huvumilia yote na wala hauandiki orodha ya maumivu moyoni. Kuendelea kuandika orodha ya maumizo katika dayari ni kujichagulia kuishi dunia ya kifungoni na siyo dunia ya uhuru.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

ONGEA NA KOCHA; Kama Bilionea Akiishiwa Anaweza Kufanya Hivi, Kwa Nini Wewe Usianzie Hapa Na Ukafanikiwa?

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?

Karibu kwenye maongezi yetu ya siku ya leo, ambapo mimi kocha wako napata nafasi ya kukushirikisha mambo muhimu kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora zaidi na unafanikiwa.
 

Leo nataka nikushirikishe habari moja niliyoisona na ikanisukuma sana kukushirikisha na wewe pia. Ni katika mahojiano ambapo Mjasiriamali Bilionea Mark Cuban aliulizwa swali kama akipoteza mali zake zote kwa pale alipo, je ataweza kurudi tena kwenye ubilionea?

Kabla sijakupa jibu lake ambalo lilinishangaza na kunifanya nikushikishe, naomba nikuambie kidogo kuhusu Mark Cuban na namna nilivyomfahamu.

SOMSA; Kama Unafikiri Huwezi Kuwa Bilionea Soma Hapa Na Uanze Kuelekea Kwenye Ubilionea.

Mark Cuban ni bilionea mjasiriamali wa nchini marekani. Amepata utajiri wake kutokana na shughuli za ujasiriamali, ambapo alianza na kampuni za mtandao wa intaneti baadaye akaweza kuuza kampuni zake na kuwa bilionea. Anawekeza kwenye makampuni mbalimbali na pia anamiliki timu ya mpira wa kikapu.

Nilimfahamu Mark Cuban kutokana na usomaji wangu wa vitabu, nilikutana na kitabu chake kinachoitwa How To Win At The Sport Of Business: If I Can Do It, You Can Do It.  

Kupitia kitabu hiki Cuban alitoa misingi 12 ya kila mjasiriamali kufuata kama anataka kufanikiwa. 

Unaweza kuzisoma sheria hizo kwenye makala hii; Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban. (bonyeza hayo maandishi kuisoma)

Sasa turudi kwenye jibu la swali aliloulizwa Cuban, iwapo anaweza kurudi kwenye ubilionea kama ikatokea amefilisika kabisa. Jibu lake lilikuwa na ndiyo na akasema hana wasiwasi kabisa kwamba atashindwa kuwa bilionea tena hata kama atapoteza kila kitu.

Alipoulizwa atawezaje kurudi kwenye ubilionea kama atapoteza kila kitu, na jibu lake ndiyo lilinishangaza ziadi.

SOMA; Orodha Mpya Ya Mabilionea; Mambo Kumi Ya Kuzingati Ili Na Wewe Uweze Kuingia Kwenye Orodha Hii Siku Za Baadae.

Alisema anajua uimara wake uko wapi, na hivyo atatafuta fursa mbili tu zitakazomrudisha kwenye ubilionea. Alisema atatafuta kazi ya kuwa mhudumu wa baa usiku na pia atatafuta kazi ya kuuza kwa kamisheni mchana. Hivyo mchana atakuwa anauza vitu kwa kamisheni na usiku atakuwa mhudumu wa baa. Anasema akifanya hivi kwa muda ataweza kutengeneza mtaji wa kumrudisha kwenye biashara na hatimaye kurudi kwenye utajiri.

Mark Cuban alijivunia ya kwamba anajua yupo vizuri kwenye mauzo, hivyo akipewa kitu chochote anaweza kukinadi na kumshawishi mtu akinunue. Kwa uimara huu alisema angetafuta bidhaa ambayo anaipenda na ina kamisheni kubwa, angepambana nayo mpaka aweze kupata akiba ya kumtosha kuanzisha biashara.

Najua unaweza kuwa unafikiria, ah anasema hivyo kwa sababu tayari ni bilionea, anaweza kusema chochote anachotaka. Ila nikuambie ya kwamba alianzia huko ndiyo akawa bilionea. 

Aliwahi kuwa mhudumu wa baa na wakati huo pia akiwa afisa mauzo wa kampuni ya kompyuta ambapo alipita nyumba kwa nyumba na ofisi kwa ofisi kuuza vifaa vya kompyuta.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hali Ya Kukosa Uthubutu Na Kuingia Kwenye Biashara Itakayokufikisha Kwenye Ubilionea.

Je unajifunza nini hapa rafiki yangu?

Sijakushirikisha tu habari hii ili ufurahie na kuhamasika, ila nimekushirikisha ili ujifunze na uchukue hatua mara moja kwenye maisha yako.

Na hii inaenda moja kwa moja kwa wale ambao wanasema wanataka kuanza biashara ila hawana mtaji. Badala ya kukaa na kusubiri mtaji, kwa nini usitafute shughuli yoyote unayoweza kufanya, hasa kuuza vitu kwa kamisheni na ukatengeneza mtaji wako hapo?

Hii pia inaenda moja kwa moja kwa wale wanaodharau kazi walizonazo sasa wakiona haziwafai na haziwezi kuwapeleka popote, kwa nini usianze kuitumia kazi hiyo kama njia ya wewe kutoka zaidi? Kwa nini usiweke juhudi kwa muda fulani na uweze kuondoka na kupiga hatua zaidi?

Mwisho kabisa napenda nikuambie rafiki yangu, acha kutafuta sababu za kujiridhisha na hali yoyote uliyonayo sasa. Acha kuwasingizia wazazi, ndugu na jamaa kwamba wamekutupa. Acha kupeleka lawama kwa serikali kwamba imeshindwa kukusaidia licha ya hilo kuwa jukumu la serikali. Ninachotaka kukuambia rafiki yangu, chukua hatua, waache wengine wajiridhishe watakavyo, ila wewe usicheze mchezo huo, chukua hatua na songa mbele.

Anzia chini kabisa, usiangalie wengine wanakuchukuliaje, usione watu watakuonaje na usomi wako, miaka ijayo watakuheshimu sana, na wengine watakuomba uwaajiri, kama tu hutafukia ndoto uliyonayo sasa. Nakusihi sana rafiki yangu, shika hatamu ya maisha yako kwenye mikono yako. Mwisho wa siku wewe ndiye unayeyaishi maisha yako, kama utataka kwa nje uonekane wa aina fulani lakini ndani ni wa tofauti, jua utajiumiza maisha yako yote.

Kila gumu unalopitia, litumie kama nafasi ya wewe kupiga hatua. Na popote ulipo sasa, hapo ndipo pa kuanzia. Kama serikali imekusomesha halafu sasa haikupi ajira, sawa, chukua hatua nyingine. Usiniambie umekaa unasubiri ajira miaka miwili na bado unaendelea kusubiri. Niambie kwamba unajipa miaka yako miwili ya kuchukua hatua hasa, bila ya kuangalia wengine wanasemaje, na nina uhakika utafika mbali sana. Kama umeweza kumudu miaka miwili bila ya ajira, utaweza kumudu mingine miwili ya kupambana kusimamisha maisha yako vizuri.

Kumbuka tupo pamoja kwenye safari hii rafiki, nipo hapa nilipo leo, nikikushirikisha maarifa haya, siyo kwa sababu serikali iliniambia hiyo ndiyo kazi yako, au kwa sababu wazazi, ndugu na jamaa waliniambia fanya hivyo, ila kwa sababu niliamua kushika hatamu ya maisha yangu, niliamua kupambana kuhakikisha maisha yangu yanasimama, na ninayaona matunda ya maamuzi haya kila siku. Ndiyo maana nina imani isiyo na shaka kabisa kwamba wewe rafiki yangu, iwapo utachukua hatua ya kushika hatamu ya maisha yako, hutabaki hapo ulipo sasa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

USHAURI; Jinsi Ya Kutumia Uwezo Wako Na Vipaji Vyako Kutengeneza Kipato.

$
0
0
Rafiki, karibu kwenye makala yetu ya leo ya ushauri wa changamoto mbalimbali ambazo zinatuzuia kufikia maisha ya mafanikio.

Leo tunakwenda kuangalia changamoto ya kutengeneza kipato kupitia uwezo na vipaji ambavyo tayari tunavyo au tunavyoweza kutengeneza.

Kabla hatujaingia ndani na kuona tunafanya nini, haya hapa ni maelezo ya msomaji mwenzetu aliyeomba ushauri kwenye hili;
Mimi nina kipaji cha kutype, nina speed kubwa sana na accuracy, ninafikiria kutafuta mashule mbalimbali ili niwe nawachapia mitihani yao. Changamoto kubwa ni namna nitakavyoweza kujitangaza ili nijulikane. Naomba ushauri wako tafadhali. Joyce M. M.
Joyce, hongera kwa kipaji hicho cha uchapaji ulicho nacho na pia vizuri sana kwa kufikiria namna gani unaweza kukitumia kutengeneza kipato ziadi. Kwa fikra hizi kama utachimba ndani zaidi utaona wazi hatua za kuchukua ili kuweza kutumia uwezo na vipaji vyako kutengeneza kipato.

Pamoja na kipaji hiki cha uchapaji ambacho unacho, bado hakikutoshelezi wewe kuweza kujitengenezea ajira itakayokupa kipato kizuri. Hii ni kwa sababu uwezo wa kuchapa pekee siyo kitu adimu sana. Kwani wachapaji wapo wengi.

SOMA; Jinsi Ya Kugundua Vipaji Vilivyopo Ndani Yako.

Unachopaswa kujua ni kwamba vitu adimu ndiyo vinavyopewa thamani kubwa. Kama kitu kinaweza kufanyika na watu wengi, basi hata thamani yake inakuwa ni ndogo. Hivyo uwezo wako wa kuchapa kwa kasi na kwa umakini, haukupi wewe kitu cha kujitofautisha na wengine wengi wanaoweza kufanya hivyo.

Hivyo ushauri mkubwa ninaokwenda kukupa leo ni kuongeza thamani yako kwa kuwa adimu zaidi. Na ili uwe adimu unahitaji kufanya vitu ambavyo haviwezi kufanywa na wengi.

Kwa kuwa tayari una uwezo wa kuchapa, sasa angalia vitu vingine unavyoweza kuviongezea kwenye uchapaji ili uwe adimu zaidi.

Kwa mfano unaweza kujifunza uandishi wa vitabu na makala na kuanza kuandika, kwa kuwa una kasi na umakini mkubwa, utaweza kuzalisha kazi nyingi zinazoweza kuwasaidia watu na wao wakawa tayari kukulipa.

Pia unaweza kujifunza uhariri na kuwasaidia watu kuhariri kazi zao na wakakulipa. Kwa kuwa una kasi na umakini, unaweza kupitia kazi kubwa za watu, kuzirekebisha na wao wakakulipa.

SOMA; Jinsi ya kugeuza kipaji chako kuwa biashara inayokuingizia kipato.

Pia unaweza kuwafundisha watu namna ya kuongeza kasi kwenye uchapaji. Ni namna gani wewe uliweza kuwa na kasi na umakini? Wapo wengi ambao wangependa kuweza kuchapa kwa kasi na umakini mkubwa na wapo tayari kulipia ili kufundishwa.

Pia unaweza kuwasaidia watu kuandika vitabu au makala. Wapo watu ambao wana mawazo mazuri ambayo yangefaa kuwa kitabu au makala nzuri lakini hawana muda na uwezo wa kubadili mawazo hayo kwenda kwenye maandishi. Wewe unaweza kuwasaidia hilo nakutengeneza kipato.

Kama tulivyoona hapo juu, zipo njia nyingi za kuongeza thamani kwenye uwezo wako wa kuchapa ili kuweza kutengeneza kipato kupitia uwezo na kipaji chako.

Sasa swali la msingi ni je unawezaje kuwafikia watu unaoweza kufanya nao kazi?

Jibu ni kwa kuwaonesha kazi zako ambazo tayari umeshafanya. Na hapa unahitaji kuwa na kazi ambazo tayari umeshawafanyia wengine na wapo tayari kutoa ushuhuda mzuri, au unahitaji kuwa na eneo lenye kazi zako kama vile blog.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Saa Hili moja Kufikia Mafanikio Makubwa.

Hivyo kitu cha kwanza kabisa nakushauri uanzishe blog yako na chagua mada utakayokuwa unaandikia. Katika maelezo ya blog yako eleza huduma ambazo utakuwa unatoa, ikiwepo ya uchapaji na uhariri wa vitabu na makala. Wakati huo unaendelea kujifunza na kuboresha ujuzi na vipaji vyako vingine ili baadaye uweze kutoa thamani kubwa zaidi.

Unaweza pia kuanza kwa kuwasaidia watu kazi zao bure kabisa na hapa ukaonesha uwezo ambao upo ndani yako. baada ya huduma hiyo ya bure, baadaye watakapohitaji ndiyo watalipia kulingana na gharama zako.

Kwa Joyce na marafiki wengine, kutegemea kipaji au uwezo mmoja pekee katika kutengeneza kipato, ili hali kitu hicho kila mtu anaweza kukifanya ni kujidanganya. Utakosa thamani kubwa ya kutoa kwa wengine na hivyo kushindwa kutengeneza kipato kizuri.

Ongeza zaidi ujuzi na jua zaidi vipaji vilivyopo ndani yako. kadiri unavyoweza kuleta pamoja vitu vidogo vidogo unavyoweza kufanya na vinavyoendana, ndivyo unavyoongeza thamani yako na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutengeneza kipato kupitia ujuzi na vipaji vyako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Hii Ndiyo Tafsiri Sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Ndoa.

$
0
0
Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  ni miongoni mwa kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata kuliko udhaniavyo.

Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi.

Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako.  Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwenzi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpenzi wako ni mtu wa karibu jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho huwa anakipendelea sana,

Baada ya kupata majibu anza kufanya uchunguzi mwingine ni kitu ambacho huwa anapenda kulizungumzia sana,  baada ya kupata majibu, majibu hayo yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na mwisho wa siku mnunue kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza. 

"Pia wakati mwingine maneno yangu sio sheria unaweza ukananunua zawadi ambayo kiukweli unahisi fika itampendeza mwezi wako"

Hayo ni baadhi ya mambo machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi wa zawadi ya kumpa mpenzi wako. Kwani zawadi ni ishara upendo imara. Pia imeshauriwa ya kwamba zawadi ni heri iwe ile ya kudumu kwani hii hukumbukwa daima. 

Pasipo kupoteza muda tuendelee kidogo kwa kuangalia japo kwa uchache umuhimu wa zawadi katika mahusiano ya ndoa.

1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli.

Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako,  mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako.  kwani zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana,   mtu ambaye anapendwa kweli .   hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka. 


 2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.

Usishangae huo ndio ukweli, kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi mpenzi wako basi anza kufanya hivyo mara moja.  Kwani zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako. 

3. Zawadi huacha kumbukumbu.

Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani?  Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo.  Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano. 

Na ili kuacha alama hiyo, kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia kabla sijaweka nukta nikumbushe pande zote mbili mvulana na msichana ana haki ya kutoa zawadi kwa mwezi wake. Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa zawadi kwa mwezi wako. 

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya

UCHAMBUZI WA KITABU; KEYS FOR LEADERSHIP (Mwongozo Wa Uongozi).

$
0
0


Katika maisha yetu ya kila siku, kuna vitu au watu ambao tunawaongoza. Mafanikio yetu katika jambo lolote tunalofanya, yanatokana na uwezo wetu mzuri wa kuongoza.
 

Kila mtu ni kiongozi wake yeye mwenyewe, na wengine wamepata nafasi ya kuwa viongozi wa familia zao, viongozi wa jamii zao, viongozi wa maeneo yao ya kuabudu na hata viongozi wa kitaifa.

Uongozi siyo kitu cha kuzaliwa nacho na wala siyo kitu cha kuzoea. Uongozi una misingi yake na miongozo yake. Marehemu Dr Myles Munroe, alikuwa mwandishi wa vitabu na katika kitabu cha KEYS TO LEADERSHIP anatushirikisha miongozo ya uongozi.
Karibu tujifunze kwa pamoja kupitia kitabu hiki kizuri.

1. Kila mtu ambaye ni mfuasi ana uongozi uliojificha ndani yake.

2. Sifa ya kila kiongozi ni kuwa na imani ya uongozi.

3. Viongozi bora wanatofautishwa na mtazamo wao chanya, kujijua wao wenyewe na kujiamini.

4. Kila mtu ana mbegu ya uongozi ndani yake, lakini wengi hawana ujasiri wa kuikuza mbegu hiyo.

5. Uongozi wa kweli ni zao la hamasa na siyo kulaghai na kudanganya.

6. Viongozi wa kweli hawatafuti kutawala bali wanasukumwa na mapenzi ya kufanya kile wanachofanya.

7. Jukumu ulilonalo ndiyo linaloamua eneo lako la uongozi.

8. Ujinga mkuu wa mtu ni juu yake binafsi. Kile unachoamini kuhusu wewe, ndiyo kinachotokea kwenye maisha yako. Hakuna mtu anayeweza kupata makubwa kuliko anachoamini.

9. Mawazo yako yanatengeneza imani yako, imani yako inatengeneza mtazamo wako, mtazamo wako unatawala mapokeo yako ya vitu na mapokeo yako yanatengeneza tabia zako.

10. Uongozi ni upendeleo wa uaminifu unaopewa na wafuasi.

11. Pesa zote duniani zinaweza kukufanya wewe tajiri, mamlaka yote duniani inaweza kukufanya ujione imara, lakini vitu hivi haviwezi kukufanya wewe kuwa kiongozi.

12. Hakuna kitu chenye nguvu kama mtazamo. Mtazamo wako ndiyo unatawala namna unavyochukulia mambo yanayokutokea. Mtazamo wako ndiyo wewe mwenyewe. Kama huwezi kutawala mtazamo wako, utakutawala wewe.

SOMA; Kiongozi Anazaliwa au Anatengenezwa? Jibu Hili Hapa.

13. Kinachowatofautisha wanaoshinda na wanaoshindwa ni mtazamo. Watu wengi wamezipoteza fursa nzuri kutokana na mtazamo waliokuwa nao.

14. Mtazamo ni zao la asili la kujithamini, kujiamini na kujikubali.

15. Hakuna mafunzo yoyote ya uongozi, usimamizi au madaraka yenye nguvu zaidi ya mtazamo.

16. Kila mmoja wetu ameumbwa kusimamia, kuongoza, kudhibiti na kutawala mazingira yanayomzunguka.

17. Wewe tayari ni kiongozi, iwe unatumia uongozi wako au la. Uwe ni masikini au tajiri, mweusi au mweupe, mdogo au mkubwa, mwanamke au mwanaume, una elimu au huna, uongozi upo ndani yako.

18. Kuanza kama mfuasi hakuondoi uwezo wako wa kuwa kiongozi.

19. Uongozi siyo kikundi cha watu wachache, ni kitu ambacho kipo kwa kila binadamu.

20. Ufunguo mkuu wa uongozi ni mtazamo, mtazamo unaanzia ndani ya mtu mwenyewe.

21. Watu wengi siyo viongozi leo kwa sababu walishajishawishi ua kwamba wao siyo viongozi.

22. Kwa sababu viongozi bora wanajijua wao wenyewe kwanza na kusudi la maisha yao, wanayatawala mazingira yao badala ya mazingira kuwatawala wao.

23. Viongozi wa kweli wanapambana kuvuka changamoto wanazokutana nazo na wanakuwa wabunifu kupitia magumu yao.

24. Uwezo mkubwa wa uongozo upo ndani yako unakusubiria wewe uutumie. Ulizaliwa kuongoza, lakini lazima kwanza uwe kiongozi.

25. Uongozi wa kweli unakupa jukumu la kuwapeleka wafuasi kule kusikojulikana na kuweza kuwatengenezea uhalisia mpya.

26. Uongozi ni uwezo wa kushawishi wengine kupitia hamasa inayochochewa na mapenzi na kutengenezwa na maono yanayoongozwa na kusudi.

27. Watu unaowahamasisha wanakuita wewe kiongozi pale wanaposukumwa kushiriki kwenye maono chanya unayowashirikisha, iwe ni maoni ya nchi, kampuni au chochote.

28. Kama hamasa ndiyo ufunguo sahihi wa ushawishi kwenye uongozi, basi kila kiongozi anapaswa kuwa mtu wa hamasa.

29. Uongozi wa kweli ni kupata imani, sababu, wazo au kusudi siyo tu la kuishi nalo, bali la kuwa tayari kufa nalo, lakini liwe la kuwanufaisha wengine.

30. Uongozi mkuu huwa unapatikana wakati wa migogoro binafsi, migogoro ya kiuchumi, migogoro ya kijamii, ya kiimani na hata ya kisiasa.

31. Japokuwa viongozi wana wafuasi, kuwa na wafuasi siyo hitaji kuu la wewe kuwa kiongozi. Mahitaji ya uongozi yanaweza kukutaka uwe tayari kusimama mwenyewe wakati wa mgogoro, kupingwa na hata kukataliwa.

32. Pale unapokuwa na kusudi na maono, yafanyie kazi hata kama ni wewe pekee unayeamini hivyo kwa wakati huo.

33. Viongozi bora wanaifunza uongozi kulitia viongozi wengine, lakini hawajaribu kuiga viongozi hao. Wanathamini kile kitu cha kipekee ambacho kipo ndani yao.

34. Uongozi wa kweli unaanza na wewe ni nani badala ya wewe unafanya nini. Ukishajua wewe ni nani na una nini, chochote utakachofanya, utakuwa kiongozi mzuri.

35. Huhitaji kitu cha ziada ili kuwa kiongozi, hivyo ulivyo, tayari uongozi upo ndani yako. Unachohitaji ni kuanza kutumia uongozi huo.

36. Usitafute ukuu, bali tafuta kuwahudumia wengine na kile kilichopo ndani yako, kwa uwezo wako na watu watakutafuta. Uongozi siyo kutafuta umaarufu, bali kutoa thamani kwa wengine.

SOMA; Ni Muhimu Sana Wewe Kuwa Kiongozi.

37. Njia ya mkato ya kufikia uongozi ni kuwahudumia wengine. Uongozi wa kweli siyo watu wangapi wanakuhudumia wewe, bali wewe unawahudumia watu wangapi. Kadiri unavyowahudumia wengi, ndivyo unavyotengeneza thamani kubwa na kuwa kiongozi mkubwa pia.

38. Kupenda fedha kiasi cha kutojali utu, thamani na ustawi wa wengine ni matumizi mabaya ya nguvu ya kupata utajiri.

39. Viongozi wa kweli ni waaminifu, hawadanganyi wala kulaghai ili kupata kile wanachotaka. Viongozi wa kweli ni wa kweli kwao wenyewe kwanza, halafu ni wa kweli kwa wengine.

40. Kitu muhimu sana kutafuta kwenye maisha ni ukweli.

41. Kutokujiamini na kutokujithamini hupelekea watu kuwadharau wengine na kuwa chanzo cha rushwa, ukandamizaji na hitaji la kuwatawala wengine.

42. Hakuna kitu hatari kama madaraka kuangukia kwenye mikono ya mtu anayejiona wa chini, atawakandamiza sana wengine.

43. Kama unajipenda wewe kweli, utatumia madaraka yako kuwasaidia wengine badala ya kuwaumiza. Vile unavyojiona wewe mwenyewe, ndivyo unavyomwona kila anayekuzunguka. Kama unajiona hufai, unaona kila mtu hafai.

44. Kiini cha uongozi ni kuwapa wengine thamani. Kwa maneno mengine unawapa kitu ambacho kinawafanya kuwa bora na kinawafanya wahusike nacho. Viongozi wa kweli wanawapa watu kitu cha kuamini, wanawapa sababu ya kuishi na kuyafanya maisha yao kuwa na thamani kwa wengine pia.

45. Huwezi kuwaongoza watu kwenda mahali ambapo wewe mwenyewe hujawahi kwenda.

46. Thamani unayoweka kwa wengine ni taswira ya thamani unayoweka kwako wewe mwenyewe.

47. Katika uongozi wako, unahitaji kufikia hatua ambayo unajua kwamba wewe ni wa muhimu. Viongozi wa kweli wanaamini wao ni wa muhimu na wanahitajika na kizazi chao na dunia kwa ujumla.

48. Kile anachoamini kiongozi, ndicho kinachotengeneza asili ya uongozi wake.

49. Uongozi wa kweli unatokea pale mtu anapotumia moto unaowaka ndani yake kuwasha moto ndani ya wengine pia.

50. Kile ambacho hatujui kuhusu sisi wenyewe, ndiyo kikwazo kwetu. Viongozi wanazuiwa na kiasi cha ujuzi wao kuhusu wao wenyewe na dunia kwa ujumla.

51. Unaweza kuigiza kama kiongozi, lakini huwezi kufikiri kama kiongozi kama kweli hujajikubali kuwa kiongozi.

52. Kuchochea imani ya uongozi ndani yako ni maamuzi na wewe pekee ndiye unayeweza kufanya maamuzi hayo.

53. Uongozi wa kweli hauwezi kuwepo kama hakuna kusudi. Kusudi ndiyo linatengeneza jukumu la maisha.

54. Ili uweze kuwa kiongozi ambaye ulizaliwa kuwa, unahitaji kujua kusudi la maisha yako na kuzalisha kile ambacho unapenda kufanya.

55. Viongozi hawafanyi tu kwa sababu wanafanya, bali wanafanya kwa sababu wanajua kwa nini wanafanya. Mapenzi yao yanawasukuma na kuwahamasisha.

56. Viongozi wa kweli hawana kazi/majukumu, bali wana zoezi la maisha yao yote.

57. Viongozi wapo tayari kuweka maisha hao yote kwenye kufikia kusudi la maisha yao.

58. Viongozi wa kweli hawahitaji hamasa kutoka nje ili kuchukua hatua, wana hamasa kutoka ndani yao wenyewe.

59. Uongozi ni sanaa na sayansi kwa wakati mmoja. Ni kitu ambacho tayari kipo ndani yako, lakini bado unahitaji kukiendeleza.

60. Uongozi wa kweli ni matumaini ya kesho na ndiyo unaotengeneza kufanikiwa au kushindwa kwa watu, jamii, taifa na hata dunia kwa ujumla.

61. Kazi kubwa ya kiongozi ni kujiendeleza yeye binafsi kila siku.

62. Viongozi wote wakubwa ni wanafunzi wa maisha, kwa maisha yao yote. Hawafiki mahali na kujiona tayari wanajua kila kitu.

63. Maono ndiyo chanzo cha nidhamu ya viongozi.

64. Viongozi wanajua, kitu cha kwanza kudhibiti ni wao wenyewe.

65. Viongozi wa kweli siyo wafungwa wa tamaduni zao.

66. Viongozi hawafuati njia, bali wanatengeneza njia. Viongozi wanakwenda kule ambapo wengine wanahofia kwenda.

67. Viongozi wa kweli wanajua kila mtu amezaliwa kujaza pengo fulani hapa duniani, wanathamini mchango wa kila mtu.

Je ungependa kuwa kiongozi bora kwenye maisha yako? Anza kwa kuendeleza uongozi ambao tayari upo ndani yako. Uongozi ni kujiamini na kuchukua hatua, anza sasa.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Hii Ndiyo Imani Chanya Unayopaswa Kumjengea Mtoto Katika Malezi.

$
0
0


Habari mpendwa rafiki na msomaji wa amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri katika shughuli zako za kila siku. Pole pia rafiki kwa changamoto unazokutana nazo katika maisha yako. Je huwa unazichukuliaje hizo changamoto unazokutana nazo? 


Umezichukulia kama ni laana au fursa? Kwa kila changamoto unayokumbana nayo hakikisha unajifunza kitu usipofanya hivyo utakua unaona mambo ni magumu.

Rafiki, kama ukizichukulia changamoto katika hali ya mtazamo chanya basi utakua uko sehemu sahihi lakini kama unachukulia changamoto unazokutana nazo kama vile ni mkosi au laana uko sehemu mbaya yakupasa ubadilishe mtazamo wako kwanza.

Mpendwa msomaji napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa hiyo nakusihi sana rafiki karibu tuweze kusafiri pamoja mpaka mwisho wa somo letu la leo.

SOMA; Huyu Ndiye Adui Namba Moja Kwenye Malezi Ya Watoto.

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja imani chanya unayopaswa kumjengea mtoto katika malezi. Karibu tujifunze ndugu msomaji. Ili tuweze kuwa na watoto bora katika jamii yetu yatupaswa kwanza tuweze kuwapatia malezi bora katika familia. Katika familia ndio msingi wa malezi ya mtoto unapoanzia hivyo kama mtoto amekosa kupewa malezi bora katika familia naye atakwenda kujenga jamii iliyo mbovu.

Wazazi ndio walimu wa kwanza katika malezi ya watu lakini siku hizi wasaidizi ndio wanageuka kuwa walimu wa kwanza katika malezi ya mtoto. Wazazi wanajisahau kwa kisingizio cha kuwa bize katika kutafuta mafanikio. Mafanikio yako unayoyatafuta yanaleta maana gani kama familia yako ni mbovu? Tunapaswa kurudi katika njia sahihi na kukumbuka wa wajibu mzazi ni upi. 

Kama mzazi ukishatambua kuwa wewe ndio mwalimu wa kwanza katika malezi ya watoto huwezi kujisahau kabisa na hata kukosa muda wa kuwaangalia watoto wako.

SOMA; Hii Ndio Faida Ya Kutumia Falsafa Ya Imani Ya Kidini Kwenye Malezi Bora Ya Watoto

Mpendwa msomaji, malengo mahususi ya somo letu la leo ni kufahamu imani chanya unayopaswa kumjengea mtoto katika malezi. Imani chanya unayopaswa kumjengea mtoto ni uwezo wa kujiamini na kumwambia kuwa anaweza kufanya kitu Fulani. Kuna baadhi ya wazazi wanakuwa wanawajengea watoto wao imani hasi ya kwamba wao hawawezi kufanya kitu Fulani. Imani hasi ya kumwambia mtoto kuwa huwezi kufanya kitu Fulani huwa inawaathiri sana kisaikolojia. Kama mzazi unatakiwa kumjengea mtoto imani chanya kuwa anaweza na siyo hawezi.

Rafiki, kuna watoto wengine wanaambiwa na wazazi wao, walimu au walezi wao kuwa hawana akili hivyo dhana hii inakuwa inajijenga kwa mtoto kuwa yeye hana akili na wenye akili ni watu wengine. hata mtoto kama anataka kuthubutu kufanya kitu Fulani anaogopa kufanya kulingana ana imani hasi aliyojengewa kuwa yeye hana akili na hawezi kufanya kitu. Tunaliona hili katika familia zetu ni jinsi gani watoto wanajengewa mitazamo hasi katika maisha yao.

Kuna wazazi, au walezi ambao wanakuwa wanawatishia watoto wao pale wanapokuwa wanajaribu kufanya jambo Fulani hivyo hii hali huwa inaua kipaji cha mtoto lakini pia hata ubunifu wa kufanya mambo mbalimbali katika maisha yake. Tunapaswa kuwajengea imani chanya kwa watoto kama vile wewe unaweza na siyo wewe huwezi badala ya kumwambia hawezi mwache ajaribu na mpongeze kwa kumpa moyo hata kama amekosea. Mtoto anapokuwa anajaribu jambo na mzazi unakosa kumpatia au kumjengea imani chanya juu ya kile anachofanya huwa inammaliza kabisa.

SOMA; Adhabu Saba (7) Zisizostahili Katika Malezi Ya Watoto.

Mpendwa mzazi na mlezi, unatakiwa kuchunga sana maneno unayomwambia mtoto wako kwani maneno hasi huwa yanaharibu watoto na kuwajengea imani hasi katika akili yao. Kuna siku moja nilishuhudia mtoto mmoja aliyesifiwa na mtu wa pembeni kuwa wewe ni mzuri lakini mtoto Yule aliweza kumjibu mtu Yule wa pembeni kuwa yeye si mzuri ni mbaya. Na mtu wa pembeni akamuuliza kwa nini unasema wewe ni mbaya? Mtoto akajibu kuwa mama yake huwa anamwambia kuwa yeye ni mbaya, yuko kama nyani.

Kwa kweli, mtoto Yule alikataa kabisa kuambiwa kuwa yeye ni mzuri na akaendelea kushikilia imani hasi aliyoambiwa na mama yake kuwa yeye yuko kama nyani hivyo ni mbaya. Watoto wanapata mateso makubwa ya akili ambayo athari yake ni kubwa kupita maelezo katika jamii yetu. Kama wazazi muda wa kuamka na kubadilika katika malezi ya watoto.

Hatua ya kuchukua leo, epuka kumjengea mtoto au watoto wako imani hasi inayompelekea kutokujiamini katika maisha yake. Anza leo kumwambia mtoto maneno chanya ya kumtia moyo na kumhamasisha katika kile anachofanya. Epuka maneno hasi yanayomharibu mtoto na kumjengea imani hasi na hatimaye kutokujiamini.

Mwisho, watoto wanahitaji malezi ya baba na mama kuliko malezi ya wasaidizi wa ndani. Hivyo basi, hatuwezi kuwajengea watoto msingi imara wa malezi kama mzazi unakosa muda wa kukaa na mtoto wako kumuuliza siku yake ilikwendaje ili kama kuna mambo ambayo haya kwenda vizuri akuelezee na wewe kama mzazi uweze kumtatulia mtoto wako. Kama mtoto anakosa mtu wa karibu wa kumwelezea matatizo yake, ambaye mtu sahihi ni wazazi ambao ni baba na mama au walezi. Kila mzazi awajibike katika kuhakikisha mtoto anapata malezi bora.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

ONGEA NA KOCHA; Mapenzi, Hasira, Kujitoa Na Kupambana, Neno Langu Kwa Wale Walionasa.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?

Mwaka 2017 unakwendaje kwako?

Unachukua hatua au bado unalalamika?

Kama unachukua hatua basi hongera sana, kwa sababu ni kuchukua hatua pekee ndipo kutakapokuletea matokeo ambayo unayataka. Kuchukua hatua kutakutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha mbele zaidi, hata kama ni padogo.
 

Kama bado unalalamika, unalalamikia serikali, unawalalamikia ndugu na jamaa, unamlalamikia mwajiri, basi nikupe pole kwa sababu umechagua njia ambayo haina majibu. Yaani umechagua kufanya kitu ambacho hakina uzalishaji, ni sawa na kusukuma ukuta kwa mikono, unaweza kutokwa jasho na kuchoka kabisa, lakini hakuna kazi ambayo unakuwa umefanya. Kwenye fizikia wanasema WORK DONE IS ZERO, yaani kama umesukuma kitu lakini hakijasogea, hujafanya kazi. Kifizikia kazi inapimwa kwa kiwango ambacho imesogea. Hivyo kulalamika, hata kama upo sahihi kabisa, hujafanya kazi yoyote, kwa sababu kulalamika ni kuongea tu, na maneno hayaleti mabadiliko hata siku moja, ni VITENDO.

Leo nataka kuandika vitu ambavyo sijaandika siku nyingi na ambavyo naona watu wengi wanavifanya kimakosa huku wakitegemea matokeo makubwa sana. Wengine wamekuwa wanashindwa kuanza kwa kujipa sababu lukuki, lakini ukweli ni kwamba hawana kile wanachopaswa kuwa nacho ili kupiga hatua.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria.

Watu wengi wamekuwa wanalalamika kwamba maisha ni magumu, fedha hakuna na mambo hayaendi, lakini ukweli ni kwamba wengi wamechagua yale maisha wanayoishi sasa, yaani watu wamechagua maisha ambayo ni magumu zaidi, wamechagua maisha ambayo hakuna fedha na wamechagua mambo kutokwenda. Hii ndiyo maana pekee ya malalamiko haya kwenye karne hii ya 21 ambapo kila mtu ana uhuru wa kufanya chochote anachotaka kufanya kama hakivunji sheria.

Lakini watu wengi wamekuwa hawachukui hatua, badala yake wanaendelea kukaa pale walipo, na kuendelea kufanya kile wanachofanya, huku wakiendelea kulalamika kwamba mambo hayaendi.

Albert Einstein amewahi kunukuliwa akisema kwamba ujinga ni kufanya jambo lile lile, kwa njia ile ile na kutegemea kupata matokeo tofauti. Sasa hapa ndipo ninapotaka na wewe ufikirie. 

Kwamba umekuwa unafanya mambo yale yale, mwaka nenda mwaka rudi. Unaenda kazini na kufanya kazi zako vile vile, unapokea mshahara ambao haukutoshi, unaenda kukopa na ukipokea mshahara mwingine unalipa madeni. Unaenda hivi miaka mitano, kumi mpaka sihirini, halafu ndani yako unafikiria kabisa kuna muujiza utakaotokea na kubadili mambo?

Unafanya biashara yako vile vile, huduma na bidhaa unazotoa ni zile zile, wateja ulionao ni wale wale na hakuna kipya kikubwa unachofanya, halafu unataka kutuaminisha kwamba mambo ni magumu kwako? Ndiyo tutaamini mambo ni magumu kwako, na tuna uhakika ni magumu kwa sababu umechagua na umeridhika na mambo hayo.

Kila kitu ambacho unafanya sasa, unafanya hivyo kwa sababu umechagua wewe mwenyewe, au umeridhika na kitu hicho, vinginevyo ungeshaondoka zamani sana. Naomba nirudie hili kwa msisitizo zaidi. UPO HAPO ULIPO, UKIFANYA HICHO UNACHOFANYA, KWA SABABU UMECHAGUA KUKIFANYA AU UMERIDHIKA NA MATOKEO AMBAYO UNAPATA. INGEKUWA HUJARIDHIKA UNGESHAFANYA KILA MBINU UTOKE HAPO ULIPO SASA.

Najua kuna ambao wamenasa, yaani wanataka kutoka lakini wanaona hawawezi kutoka, wamenasa. Kama vile ambavyo mtu yupo kwenye kazi ambayo haipendi na wala haimlipi vizuri lakini hawezi kuiacha kwa sababu ndiyo anaitegemea kuendesha familia yake. Naelewa vizuri sana kwamba kuna uwezekano umenasa, unatamani sana kutoka lakini ukiangalia nyuma huthubutu kufanya hivyo.

Leo nataka kuongea na wale ambao wamenasa, wale ambao wamechoka lakini hawaoni wanatokaje pale walipo. Wale ambao wanatamani sana kupiga hatua lakini hawaoni wapi waanzie. Na hata ndiyo ninayotaka kuwapa siku ya leo.

SOMA; Kama Una Tabia Sugu Inayokukera Iondoe Hivi.
MAPENZI.

Ni kitu gani unakipenda sana kwenye maisha yako, kitu gani unapenda sana kuhusu maisha yako na kitu gani ambacho unapenda kufuatilia na kitu gani ambacho unapenda kuongelea na kushirikisha wengine?

Kuna mwanamuziki siku za nyuma kidogo aliwahi kuimba wimbo unaitwa MAPENZI YANA RUN DUNIA, akimaanisha mapenzi ndiyo yanaendesha dunia. Na hii ni kweli kabisa, siyo tu kwa mapenzi kati ya wachumba au wenza, bali mapenzi kwa ujumla.

Wale wanaofanikiwa sana ni wale ambao wana mapenzi makubwa kwenye kile ambacho wanakifanya. Wale ambao hakuna namna unaweza kuwatoa kwenye kile wanachofanya, kwa sababu kimeshakuwa sehemu ya maisha yako.

Hivyo na wewe, tafuta kitu ambacho unakipenda sana, kitu ambacho upo tayari kukifanya na kukisimamia hata kama kila mtu anafanya tofauti au anakushangaa. Na anza kukifanya, wakati unaendelea kufanya kile unachofanya sasa, na hapo utapata ukombozi wako.

Mapenzi yana nguvu kubwa sana, angalia namna watu wanavyoweza kufanya mambo ya ajabu kabisa kwa ajili ya mapenzi, sasa wewe tumia nguvu hivyo vizuri ili uweze kutoka hapo ulipo sasa.

HASIRA.

Ni kitu gani ambacho kinakukasirisha sana kuhusu maisha yako na hata kwenye maisha yako. Ni kitu gani ambacho huwezi kukivumilia kabia, kila unapokiona hupati amani kabisa, yaani unatamani kufanya kitu ili kubadili ile hali inayokupa hasira?

Hapa ndipo ilipo nguvu nyingine ya kukuwezesha wewe kutoka hapo ulipo sasa. Iwe umeridhika tu au umenasa, kwa kupata hasira ambayo huwezi kuivumilia, itakusukuma kuchukua hatua kubwa.

Hasira tunayojadili hapa siyo ya kugombana na watu au kupiga watu, bali hasira ya kuchoka na namna maisha yanavyokwenda, hasira ya kutaka mambo yawe bora zaidi. Hasira ya kukufanya usiwe mzembe, uwe tayari kuchukua hatua hata kama wengine hawachukui hatua.

KUJITOA.

Ni kitu gani upo tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya hicho kwenye maisha yako. Ni wapi upo tayari kwenda hatua ya ziada, kufanya zaidi ya wengine na hata kuwasaidia watu zaidi? Ni eneo gani la maisha yako ambapo hijibanii, upo tayari kutoa zaidi, upo tayari kuwanufaisha watu zaidi?

Kiwango chako cha kujitoa ndiyo kinachokutofautisha na wengine na ndiyo kitakachokutoa hapo ulipo sasa.

SOMA; Kuanza Biashara Kwa Mtaji Kidogo, Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuikuza.

KUPAMBANA.

Mambo hayatakuwa rahisi, utasoma hapa, utapata hamasa na kusema yaani kuanzia leo nabadili maisha yangu kabisa, nitafanya haya muhimu kila siku. Lakini kesho utaamka ukiwa na mawazo ya changamoto zako nyingine na kuwa umesahau haya kabisa. Au utaanza kuyafanya na watu wanaanza kukushangaa, wengine wanakupinga, wengine wanakusema vibaya, wengine wanakukatisha tamaa.
Napenda nikuambie wazi kabisa, mambo hayatakuwa rahisi na hivyo utahitaji kupambana sana, yaani SANA. Utahitaji kupambana siyo kidogo. Kupambana na uzembe na uvivu wako mwenyewe, kupambana na wale wanaokuzunguka na kupambana na changamoto zinazotokana na kile unachofanya.

Hivyo ndivyo unavyoweza kutoka hapo ulipo nasa rafiki yangu. Hizo ndizo hatua zitakazokutoa hapo, zifanyie kazi na utoke, au achana nazo na uendelee kulalamika. Lakini kabla hujaendelea kulalamika, fanya tathmini tangu umeanza kulalamika, ni matokeo gani makubwa umewahi kuyapata kwenye maisha yako kutokana na kulalamika?

Usikubali kuwa mjinga, kwa kufanya mambo yale yale na kutegemea matokeo tofauti. Kuwa mwerevu na chukua hatua sasa. Na hatua za kuanza kuchukua kuanzia leo tayari nimeshakupa hapo. Kazi ni kwako tu rafiki yangu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Mzigo Wa Kuwasaidia Wengine Kifedha Na Njia Bora Zaidi Ya Kutoa Msaada Kwa Wengine.

$
0
0


Habari za leo rafiki?

Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku na ni kupitia changamoto ndipo tunapojifunza na kupiga hatua zaidi. Bila ya changamoto maisha yasingekuwa na raha ya kuishi, kwa sababu kila kitu kingekwenda vizuri na kusingekuwa na haja ya kufikiri zaidi na kupambana zaidi. Lakini pia changamoto nyingine zinatokana na sisi wenyewe kukosa maarifa sahihi ya kufanya mambo, hivyo tunapopata maarifa changamoto hizo zinatoweka kwa sababu tunakuwa tumepata uwezo wa kufanya maamuzi sahihi. 
 

Swala la kuwasaidia wengine moja kwa moja kifedha imekuwa ni changamoto kubwa kwa wengi. Imekuwa inawakwamisha wengi kupiga hatua kwa sababu kipato kidogo wanachopata kinakuwa kinategemewa na wengi. Na tatizo kubwa kwenye utegemezi wa aina hiyo ni kwamba watu wakishajua wanapata fedha sehemu fulani, basi mawazo yao yote yanapelekwa pale, hawafikirii tena njia nyingine za kutatua changamoto zao.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kufanya Pale Ndugu Zako Wanapokuona Wewe Ni Mbaya(Mchawi) Kwa Sababu Una Mafanikio.

Leo kupitia makala hii ya ushauri wa changamoto tunakwenda kuangalia namna ya kuondokana na changamoto hii ya mzigo wa kuwasaidia wengine na pia tutaangalia njia bora kabisa ya kuweza kuwasaidia watu wengine.

Kabla hatujaangalia nini cha kufanya, tupate maoni ya msomaji mwenzetu anayesumbuliwa na changamoto hii;

Ni kwamba kwa miezi minne nina uwezo wa kupata milioni moja ya Kitanzania lakini hainisaidii maana sioni umuhimu wake kwani nikiipata inaisha bila kujua ndani ya mwezi maana nina huruma sana na watu wanaoniomba pesa kwani wanajua napokea kiasi kikubwa cha pesa ndani ya muda huo na tendo hili hunilazimu niwasaidie na mwishowe najikuta sina pesa tena mpaka nisubiri miezi mingine minne tena na nikizipata mwendo ni uleule zinaisha tu wakati malengo yangu makubwa ni kufanya biashara kupitia hiyo pesa ili nipate pesa ya kutosha niweze kuwainua hawa wanaoniomba pesa lakini inashindikana TAFADHALI USHAURI. ANSIGARIUS K. M.

Rafiki, hivi ndivyo changamoto hii ya utegemezi inavyokuwa mzigo kwa wengi. Watu wanashindwa kupiga hatua kwenye maisha sababu ya utegemezi mkubwa kutoka kwa wengine. 

Lakini ipo njia ya kuweza kuondokana na hili na kuweza kutengeneza uhuru wa kifedha pamoja na kuwasaidia wengine vizuri zaidi. Hapa tutajadili njia hizo.

1. Saidia kulingana na uwezo wako.

Kusaidia ni kuzuri kwa sababu ni kweli wapo watu wenye uhitaji zaidi yetu sisi, lakini kusaidia mpaka wewe mwenyewe unabaki huna kitu siyo kitu kizuri, humsaidii yule unayefikiria unamsaidia na wewe mwenyewe unajiweka kwenye hali mbaya zaidi. Wape watu msaada kulingana na uwezo wako na hivyo ili kuhakikisha mambo yako yanakwenda vizuri, kuwa na kiwango maalumu cha kutoa msaada kwa wale wenye uhitaji. Na kila mwezi au wakati mwingine wa malipo kwako, msaada wako usizidi kiwango kile.

Kwa mfano unaweza kuchagua kwamba asilimia 10 ya kipato chako ndiyo utakayotoa msaada. Toa msaada wa kiasi hicho na kikishaisha usitoe tena, subiri mpaka kipato kingine. Kwa njia hii utaweza kutenga fedha kwa ajili ya mambo mengine muhimu kwenye maisha yako kama biashara na uwekezaji ili baadaye uweze kufikia uhuru wa kifedha.

SOMA; Jinsi Ya Kuepuka Dharura Zako Na Za Wengine Kuwa Kikwazo Cha Kufikia Malengo Yako.

mtu kujua una fedha au huna.

Kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanafanya ni kuruhusu kila mtu ajue kwamba sasa hivi ana fedha au la. Hujawahi kujiuliza kwa nini ukiwa na fedha watu wanakuja na shida kubwa na muhimu sana wewe kuwasaidia, lakini ukiwa huna fedha watu hao huwaoni?

Hii ni kwa sababu watu wakishajua una fedha, basi wanapata sababu kubwa ya kukueleza ili uwapatie fedha, ndivyo tabia za binadamu zilivyo.

Watu wengi wanapopata fedha tabia zao hubadilika kabisa. Ataanza kutoa ofa zisizo na msingi, ataanza kufanya manunuzi ambayo hayakuwa yamepangiliwa na hata mwonekano wake unabadilika. Na kwa wale ambao ni walevi, ndiyo kabisa dunia nzima itajua kwamba wana fedha. Watu hawa fedha zinapoisha kila mtu anajua kwa sababu wananyong’onyea, hawaonekani kabisa.

Kama ulishajenga utaratibu huu wa kimaisha, wa watu kujua kirahisi kwamba una fedha au huna, uvunje haraka. Vunja utaratibu huo ili watu waache kukutabiria na kupata fedha kutoka kwako kirahisi.

Hata kama umeajiriwa na watu wanajua mwisho wa mwezi unapokea mshahara, bado usikubali kuonekana mwisho wa mwezi una fedha. Endesha maisha yako kwa usawa kila siku na watu wasiweze kukutabiria kiurahisi kama una fedha ua la. Kwa njia hii utaepusha wale ambao hawana uhitaji sana ila wanatengeneza uhitaji pale wanapojua kwamba una fedha.

3. Ikumbuke njia bora kabisa ya kuwasaidia masikini.

Unaijua njia bora kabisa ya kuwasaidia masikini? Ni wewe kutokuwa masikini. Sasa unapowasaidia watu na wewe kubaki huna kitu, hujawasaidia chochote, kwa sababu na wewe unakuwa mmoja wao kwamba huna kitu. Mnapokuwa wote hamna kitu baadaye hakuna atakayeweza kumsaidia mwenzake. Kama ni ajira unayo, siku ikiisha wote mnakuwa wa kusaidiwa.

Hivyo wakati unawasaidia wengine fikiria sana hili, je kuwasaidia kwako wengine kunakuacha wewe ukiwa na shida zaidi ya wao? Kama jibu ni ndiyo kaa chini na ujipange upya.

4. Usiwape watu samaki, wafundishe namna ya kuvua samaki.

Ukimpa mtu samaki atamla halafu atarudi tena kwako akitaka samaki. Ukimfundisha mtu namna ya kuvua samaki utampa uhuru wa maisha yake na kuondoa utegemezi kwako. Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye msaada wa kifedha. Ukiwapa watu fedha watazitumia na zikiisha watarudi tena kwako, kwa sababu fedha siku zote huwa hazitoshi na matatizo ni mengi. Lakini kama utawafundisha watu hao namna ya kujitengenezea kipato chao wenyewe, utawatengenezea uhuru wa kifedha na wewe utakuwa huru pia.

SOMA; Kama Unajibebesha Mizigo Hii Katika Maisha Yako, Sahau Kuhusu Mafanikio.

Hivyo kwa kila mtu anayekutegemea, angalia ni kwa namna gani unaweza kumtengenezea njia ya kumwingizia kipato, hata kama ni kidogo sana. Faida nyingine ya kufanya hivi ni kumfanya mtu aone uchungu wa kutafuta fedha hivyo kuzitumia vizuri. Mtu anapopata fedha kirahisi, haoni uchungu wake na anazitumia kirahisi.

5. Kumbuka sheria kuu ya fedha kwako.

Kama utashindwa kufuata hayo manne niliyokushirikisha hapo juu, basi kila unapopata fedha kumbuka sheria kuu ya fedha kwako, ambayo ni JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA. Hata kama huwezi kabisa kuacha kuwasaidia wengine, kwa sababu hawajiwezi kabisa na wanakutegemea wewe moja kwa moja, basi kumbuka hili; JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA.

Kwa kila kipato chako tenga asilimia ambayo unajilipa, isipungue asilimia kumi. Na unapopokea kipato jilipe, ile inayobaki sasa unaweza kufanya chochote unachotaka, unaweza hata kuigawa yote, lakini, chonde chonde usiguse ile ambayo umejilipa wewe mwenyewe. Hii uliyojilipa siyo kwa ajili ya msaada au dharura, bali kwa ajili ya uwekezaji ili uweze kufikia uhuru wa kifedha hapo baadaye. Weka fedha hiyo kwenye mfumo ambao huwezi kuziumia hata kama una shida kiasi gani. Mfano kuweka kwenye akaunti maalumu au kuwekeza kwenye mifuko ambayo hutoi kwa urahisi kama ukiweka benki.

Anza kujilipa wewe mwenyewe kwanza kwa kila kipato, na inayobaki itumie kadiri unavyoona inafaa.

Fanyia kazi mambo haya matano muhimu tuliyojifunza kuhusu kutoa msaada kwa wengine kwa kuondokana na mzigo wa utegemezi na kuwawezesha watu kujitengenezea kipato chao wenyewe. Ni muhimu sana uzingatie haya ili na wewe mwenyewe uweze kufikia uhuru wa kifedha.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.

Hawa Ndio Maadui Makubwa Wa Mafanikio Yako Unaowabeba Sana.

$
0
0
Wengi kulingana na uzoefu tumezoea kuona maadui wengi wa mafanikio yetu walio nje yetu. Mara nyingi tunakuwa hatuko tayari kukubali kuwa rafiki na mtu ambaye kwa namna moja au nyingine tumetambua ya kwamba yeye ni kikwazo au adui wa mafanikio yetu, naamini hili unalijua vizuri. Kwa hilo huwa tupo tayari kumweka kando mtu huyo kwa sababu ni  chanzo cha kutufanya tushindwe kufanikiwa.

Hata hivyo pamoja na kuwa makini na wale tunaomini ndio maadui wa mafanikio yetu, tumekuwa tukisahau kwamba wapo baadhi  ya maadui wakubwa wa mafanikio ambao wako ndani yetu. Kwa bahati mbaya sana maadui hawa tumekuwa hatupo makini nao sana lakini ndio wamekuwa wakituzuia kufanikiwa kuliko hata wale maadui wa nje tunaowajua.

Je, unajua hawa ni maadui wapi ulionao wa mafanikio unawashikiria sana na wanakufanya ushindwe kufanikiwa?

1. Woga.

Kati ya kitu ambacho kinamsumbua sana binadamu ni pamoja na woga. Binadamu kwa kawaida kimaumbile ni mtu wa kuogopa mambo mengi sana ikiwemo hata woga wa mafanikio yake. Woga huu mara nyingi hupatikana kutokana na kujifunza, uzoefu au kusikia lakini ukija kuungalia hata kile kinachoogopwa kinakuwa sio halisi ama kwa lugha nyingine tunaweza kusema hakipo.

Inapofika mahali ukawa una woga mkubwa ndani yako suala la kufanikiwa katika maisha linakuwa ni gumu. Hiyo yote inakuwa ni kwa sababu hakuna hatua ambayo utaweza kuichukua zaidi ya wewe kuogopa na kujihisi hutaweza. Kwa hiyo kama unaendekeza woga, tambua huyo ni adui mkubwa sana aliye ndani yako ambaye anakuzuia kufanikiwa. Waangalie watu wengi waoga maisha yao huwa ni ya kushindwa sana karibu siku zote.


2. Wasiwasi.

Tukiachana na suala la woga pia adui mwingine ambaye binadamu anambeba ndani yake ni wasiwasi. Watu wengi wanakuwa ni watu wa kutilia wasiwasi au mashaka kwa mambo wanayoyafanya au wanayotaka kuyafanya. Utakuta mtu anataka kufanya kitu fulani lakini ndani yake kunakuwa kuna maswali mengi sana ndani yake anayojiuliza kama ‘hivi kweli hapa nitafanikiwa’ na je ikitokea nimeshindwa itakuwaje?’.

Kwa wasiwasi huu mwingi ambao wengi wanakuwa nao unakuwa unawafanya kushindwa kufanikiwa. Utakuta kweli mtu huyu amefanikiwa kuushinda woga na kujaribu kuchukua hatua. Lakini, kitendo cha kuthubutu huku ukiwa na wasiwasi mkubwa ndani yako wa ‘sijui nitafanikiwa au nitashindwa, huwafanya kushindwa moja kwa moja. Na hii huwa inatokea kwa sababu ya mawazo ya kina yanakuwa yanaamini kile unachokihofia ndicho unachokitaka mwisho wa siku unajikuta umeshindwa.

 3. Imani potofu.

Maisha yote ya mafanikio yanaongozwa na imani. Unaweza ukawa una mipango na malengo mazuri kabisa ya kukusaidia kufanikiwa, lakini kitu cha kujiuliza je una imani inayokusaidia kufikia mafanikio hayo? bila kuwa na imani sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio ni rahisi kushindwa. Watu wengi wanakuwa wanatafuta mafanikio lakini huku ndani mwao wakiwa na imani hasi, imani potofu ambazo zinawazuia kufanikiwa.

Kwa mfano utakuta mtu anatafuta mafanikio lakini wakati huo huo ndani yake anaamini watu wanaofanikiwa ni wezi, mafisadi au wanyonyaji kwa wengine. Kwa imani kama hizi kufanikiwa inakuwa ni ngumu kwa sababu ndani yako unakuwa na imani potofu inayokuzuia kufanikiwa huko. Ni lazima kujenga mtazamo chanya ambao utakupa mafanikio. Acha kuwaza hasi ama kujenga imani potofu utakwama kufikia mafanikio yako makubwa.


4. Maamuzi mabovu.

Kila mtu katika maisha yake ana maamuzi ya aina fulani ambayo anayatoa kila siku. Kwa maaumuzi hayohayo hupelekea maisha yako kuwa mabaya au mazuri. Kama ndani yako unabeba maamuzi mabaya kila wakati basi elewa una adui mkubwa anayekuzuia kufanikiwa. Kwani kwa kuwa na maamuzi hayo itasababisha maisha yako kuwa mabovu na ya ajabu sana.

Kwa mfano maisha yako yapo hivyo kwa sababu ya maamuzi ambayo ulishayafanya siku za nyuma. Kama ulifanya maamuzi mabovu ndivyo na maisha yako yalivyo sasa. Kuwa na maamuzi mabovu ni adui mkubwa sana aliye ndani yako ambapo usipokuwa makini anaharibu sana maisha yako pasipo wewe kujua. Kitu cha msingi kwako ni kuwa makini na kujifunza kuwa na maamuzi sahihi. Kinyume cha hapo utapotea.

5. Hamasa.

Ili ufanikiwe ni lazima uwe na hamasa kubwa sana ndani yako kila siku. Bila kuwa na hamasa hakuna mafanikio utakayoweza kuyafikia. Kwa bahati mbaya au nzuri hamasa huwa zinaanzia ndani mwetu. Kama ikitokea umekosa hamasa pole pole unakuwa umebeba adui wa kukuangusha bila kujijua. Kwa hiyo unahitaji kujijengea hamasa ili uweze kufikia mafanikio yako kwa kiasi kikbwa siku hadi siku.

Kwa vyovyote vile, ni lazima kupambana na maadui hao walio ndani yetu ili kufikia mafanikio makubwa. Chukua hatua mapema za kubadili maisha yako.

Nakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.com kila siku.
Ni wako rafiki,

Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,
E-mail;- dirayamafanikio@gmail.com


UCHAMBUZI WA KITABU; WHY WE WORK (Nadharia Ya Nini Kinawasukuma Watu Kufanya Kazi).

$
0
0


Nadharia ambayo imekuwa inatawala ulimwengu wa kazi na biashara ni kwamba watu wanafanya kazi ili walipwe. Kwamba kitu pekee kinachowasukuma watu kufanya kazi ni fedha. 


Nadharia hii imekuwa inatumika kuwalaghai watu wafanye kazi zaidi kwa kuwaongezea fedha, au kuwaadhibu wape wanaposhindwa kufanya kazi kwa kuwakata fedha.

Lakini tafiti nyingi zinaonesha kwamba kinachowasukuma watu kufanya kazi siyo fedha pekee. Japo fedha ni muhimu, lakini siyo kitu pekee kinachowasukuma watu kufanya kazi. Bali watu wanasukumwa zaidi na maana ambayo kazi wanayoifanya inawapa. Kwamba ni mchango gani wanatoa kupitia kazi hizo wanazofanya.

Mwanzilishi mkubwa wa nadharia kwamba watu wanafanya kazi kwa ajili ya fedha pekee ni mwandishi Adam Smith aliyeandika moja ya vitabu vilivyojenga misingi ya ubepari. Katika kitabu chake cha THE WEALTH OF NATIONS, Adam aliandika kwamba kwa asili watu ni wavivu na hawapendi kufanya kazi, hivyo ili kiwanda kiweze kuzalisha kwa wingi na kupata faida, lazima kigawe majukumu yake katika vipande vidogo vidogo sana ambavyo vinaweza kufanywa na yeyote bila hata ya ujuzi mkubwa, kisha kutafuta watu unaoweza kuwalipa kiasi kidogo na wakafanya kazi hiyo. Wakikataa tafuta wengine, maana huhitaji utaalamu mkubwa. Na alitumia mfano wa kiwanda cha kutengeneza pini, ambapo aligawa jukumu la kutengeneza pini katika hatua tano, ambapo kila hatua inahitaji mtu mmoja, hatua ya kwanza ni kukata waya, hatua ya pili kuunyoosha, hatua ya tatu kuweka ncha mbele, hatua ya nne kuweka kichwa cha pini na hatua ya tano kutoa pini iliyokamilika. Hapo unaweza kumwajiri mtu yeyote na akafanya kazi.

SOMA; Sababu Tatu(3) Zinazokuzui Kufanikiwa Kwenye Kazi Unayofanya.

Tatizo la nadharia ya Smith ni kuwachukulia watu kama mashine ambazo zinaweza kufanyishwa kazi muda wowote na kupata kile mtu anachotaka. Na hii imeondoa kabisa maana ya kazi kwa watu, kuwafanya watu kupata msongo wa mawazo kwa kufanya kazi ambazo hazina maana kwao.

Mwanasaikolojia na mwandishi Barry Schwartz kupitia kitabu chake hichi cha WHY WE WORK anatukumbusha msingi mkuu wa kazi kwetu, ambao ni kutengeneza maana kwetu sisi. Anatuonesha kupitia tafiti jinsi ambavyo kazi yenye maana kwa mtu ina faida kwake na kwa jamii kwa ujumla. Karibu tujifunze kwa pamoja kupitia uchambuzi wa kitabu hiki.

1. Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba kinachowasukuma kufanya kazi ni kupata fedha. Unaweza kufikiri hivi wakati una shida sana ya fedha, lakini unapozipata fedha ndipo unapoona bado kuna ombwe ndani yako. Kazi inahitaji kuwa na maana kwako zaidi ya fedha unazozipata. 

Kazi inahitaji kukuridhisha wewe kwanza, kuliko hata inavyokuingizia fedha.

2. Watu ambao wanaridhishwa na kazi zao, wanapoulizwa nini kinawaridhisha kwenye kazi zao, hawataji fedha. Kitu cha kwanza kwao ni ile maana ambayo kazi wanayofanya inaleta kwenye maisha yao, ule mchango ambao wanautoa kwa wengine.

SOMA; Mambo Saba(7) Yanayowafanya Wafanyakazi Wengi Kuwa Na Ufanisi Mdogo Kwenye Kazi Zao.

3. Watu ambao wanaridhishwa na kazi zao, wanajihusisha sana na kazi zao. Wanapokuwa wanafanya kazi zao, akili yao yote na moyo wao wote unakuwa kwenye kazi hiyo. Hakuna kingine kinakuwa muhimu kwao kama kazi yao wakati wanaifanya.

4. Kitu kingine kinachowasukuma watu kufanya kazi zao, na kuwafanya wazipende ni ile hali ya kuwa na maamuzi kwenye kazi zao. Pale wanapojua kwamba wao ndiyo wenye maamuzi kwenye kazi hizo, wanapojua wao ndiyo wanajisimamia wenyewe na wanaweza kufanya kile ambacho ni sahihi kwa namna wanavyotaka wao, wanavutiwa na kazi hizo.

5. Watu hawapendi kazi kwa sababu tu ni rahisi, tafiti zinaonesha wengi wanapenda kazi ambazo zinawapa changamoto, kazi ambazo zinawasukuma zaidi kila siku, kazi ambazo zinawafanya wajifunze zaidi na kazi ambazo zinawafanya kuwafikia watu wengi zaidi kila siku.

6. Pamoja na kwamba kinachowasukuma watu kufanya kazi siyo fedha, bado sehemu kubwa ya watu kwenye jamii wanafanya kazi ili walipwe. Watu wengi wanakwenda kazini kwa sababu wasipoenda watakosa fedha ya kuendesha maisha yao. Na hii inatokana na kufanikiwa kwa jamii kutuuzia nadharia ya uongo kwamba lengo kuu la kazi ni kupata fedha, hakuna zaidi ya hapo.

7. Utafiti uliofanya na shirika la Gallup unaonesha kwamba asilimia 63 ya watu hawaridhishwi na kazi zao, na ni asilimia 13 pekee ambao wanakiri kuridhishwa na kazi wanazozifanya. Hii inaonesha kwamba sehemu kubwa ya watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi na haziwaridhishi. Lakini wanaendelea kuzifanya kwa sababu jamii imewauzia nadharia ya uongo kwamba unafanya kazi ili ulipwe. Wanafanya na kulipwa kweli, lakini hawaridhiki na kazi zao.

SOMA; Kitu Kimoja Kinachowatofautisha Waliofanikiwa Na Walioshindwa, Na Jinsi Unavyoweza Kukitumia Kufikia Mafanikio Makubwa.

8. Watu wengi wamekuwa wanafikiri ya kwamba kuna baadhi ya kazi zinakuwa na maana na kuwaridhisha watu na nyingine haziwezi kuwa na maana. Na hapa kazi kama udaktari, uanasheria, ualimu na nyingine kama hizo zinaonekana kuwa na maana kwa wale wanaozifanya. Kazi nyingine kama za kufanya usafi au usaidizi mwingine zinaonekana ni sehemu tu ya kujipatia fedha, au ya kupita ili kupata kazi nzuri. Ukweli ni kwamba kila kazi inaweza kuwa na maana kwa mtu anayeifanya, maana haianzi na kazi yenyewe, badala yake maana inaanza na mtu mwenyewe.

9. Unaweza kutengeneza maana kwenye kazi unayofanya kwa kuangalia namna ambavyo watu wengine wananufaika na kazi unayoifanya. Kwa mfano kama kazi yako ni kufanya usafi ofisini, angalia namna ambavyo huduma yako ya usafi inaiwezesha ofisi kutoa huduma kwa watu wengine. Hebu fikiria kama ofisi ingekuwa chafu, watu wangekuja kupata huduma ambazo wanazipata pale? Kwa kuangalia eneo hili la kazi yako, utaona maana kubwa ya kazi hiyo kwako.

10. Kitu kingine kinachowatofautisha wanaoridhishwa na kazi zao na wale wasioridhishwa ni namna watu wanavyochukulia kazi hizo. Wale wasioridhishwa na kazi zao wanazichukulia kazi kama kazi tu, kitu ambacho wanafanya ili walipwe. Hakuna kingine wanachoona kwenye kazi hizo. Ila wale wanaoridhishwa na kazi zao wanazichukulia kazi zao kama WITO. Wanachokulia kama deni ambalo wanapaswa kulilipa hapa duniani, kwa njia hii wanatoa huduma bora na kupata matokeo bora pia.

11. Kuna faida nyingi pale mtu anapofanya kazi ambayo inamridhisha. Kwanza kabisa anaifanya kwa moyo mmoja na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa wengine. Pili inamridhisha yeye mwenyewe na hivyo kutokuwa na msongo wa mawazo unaosababishwa na changamoto za kazi. Tatu inamfanya mtu kupata kipato kikubwa zaidi. Yaani hapa ni kama kinyume, kinachomsukuma mtu kufanya kazi siyo fedha, lakini anajikuta anapata fedha zaidi kwa sababu anatoa huduma zaidi.

12. Wale wanaochukulia fedha kama sababu pekee ya watu kufanya kazi, pia wamekuwa wanatumia fedha kama zawadi au adhabu kwenye kazi. Pale mtu anapofanya vizuri anaongezewa fedha na akifanya vibaya anapunguziwa fedha. Kwa mawazo ya haraka haraka unaweza kuona zawadi ya fedha inawasukuma watu kufanya kazi zaidi, lakini tafiti zinaonesha zawadi ya fedha inapunguza morali ya watu kufanya kazi. Kama watu walifanya vizuri kwa sababu kazi inawaridhisha na wewe ukawapa fedha, wanaanza kuangalia kile walichofanya kama kitu cha kununuliwa na kusahau msukumo wao wa awali. Kidogo kidogo watu wanasahau msukumo halisi na kuangalia fedha pekee.

13. Hasara nyingine ya kutumia ongezeko la fedha kama zawadi kwa wale wanaofanya kazi vizuri, kunawafanya watu kutafuta njia zisizo sahihi za kuonekana wamefanya kazi ili walipwe zaidi. Inaacha kuwa kufanya kazi halisi na inakuwa kutafuta njia itakayoonesha kwamba mtu amefanya kazi. Na hapa ndipo uongo unapotawala sehemu za kazi.

14. Kuwepo kwa miongozo mingi ya namna mtu anavyopaswa kufanya kazi yake imekuwa chanzo cha wengi pia kutokuridhishwa na kazi zao. Pale ambapo mtu anasimamiwa sana, anakosa uhuru wa kufanya kazi yake kwa uwezo wake na anaishia kufanya kwa hofu.

15. Mawazo na mifumo ya kijamii ina nguvu kubwa ya kuwabadili watu. Hata kitu cha uongo, kinapokelewa kama ukweli pale ambapo watu wengi wanakikubali katika jamii. Na hivi ndivyo maeneo ya kazi yamekuwa yanawabadili wafanyakazi. Pale ambapo utamaduni wa kazi ni kuwaangalia wafanyakazi kama watu wako pale kwa ajili ya kupata fedha, na watu wanafanya kwa ajili ya kupata fedha pekee.

16. Mara nyingi watu wanatoa kile ambacho wanategemewa kutoa, wanafanya kile ambacho wanategemewa kufanywa. Na ndiyo maana watu wakitegemewa kufanya kazi zao kwa kujituma wanafanya hivyo, wakitegemewa kufanya ili wapate fedha, wanafanya hivyo pia.

17. Kile ambacho watu wanafanya kwenye kazi zao za kila siku, kinatokana na namna watu wengine wanavyofanya kwenye kazi zao hizo pia. Hii ndiyo maana wazo lolote ambalo linachukuliwa na wengi, linaonekana kama wazo zuri hata kama siyo wazo sahihi.

18. Wachumi wanafikiria ufanisi kwa kipimo cha fedha, kwamba kiasi kilichowekezwa kimezalisha kiasi gani. Na katika hesabu hizi, mfanyakazi anaonekana kama uwekezaji na siyo mchango muhimu kwenye uzalishaji. Kipimo sahihi ambacho kinaweza kuwajumuisha wafanyakazi pia ni kuangalia mtu amepata ubora kiasi gani, kwa kuangalia pia mchango wa wafanyakazi kwenye kile kilichofanyika.

19. Watu wengi ambao wanafanya kazi zao kwa sababu tu ya fedha, wanaweka juhudi sana mwanzoni na huenda wakafanikiwa kuzipata hizo fedha. Lakini baada ya kupata fedha, ndipo wanapoona kazi zao kama mzigo kwao, wanaanza kufanya mambo ambayo wengine wanashindwa kuwaelewa. Ni vyema kutengeneza maana ya kazi yako kwako kabla hujafika hatua ya kuichoka na kujikuta unaharibu kila ambacho ulishatengeneza.

20. Mengi ambayo umejifunza hapa yanaweza kuwa yanakushangaza, kwa sababu tangu unakua mpaka sasa, tangu unasoma mpaka unatafuta kazi au biashara ya kufanya, mawazo yako yote yalikuwa ni kuhusu kupata fedha. Lakini sasa unajifunza kitu cha tofauti, ambacho unaweza usijue ni namna gani ya kukitumia, sasa naomba nimalize kwa kukupa hatua muhimu za kuchukua;

1. Kwa kazi au biashara ambayo unafanya sasa, anza kutafuta maana yake kwako licha tu ya kupata fedha. Angalia ni watu gani wananufaika na kile unachofanya, angalia ni mchango gani unaotoa kwa wengine, utaanza kuona umuhimu wako kwa wengine.

2. Kazi au biashara yoyote unayoifanya, imiliki kama yako, hata kama umeajiriwa. Ona kila unachofanya kama kina nembo yako, hivyo kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.

3. Acha kuangalia fedha pekee kwenye kila unachofanya, acha kuhesabu fedha pekee kwenye kila unachogusa, angalia pia namna unavyogusa maisha ya wengine.

4. Unapoajiri watu, ajiri kwa uwezo wao na hamasa yao ya kufanya kazi. Na usiajiri tu kwa sababu wanataka fedha. Ajiri watu ambao wana mchango kwenye kile unachotaka wafanye.

5. Unapoajiri watu ambao wana uwezo na hamasa ya kufanya kazi, wape uhuru wa kufanya kazi zao kwa ubora wa hali ya juu. Pia usiwajengee utaratibu wa kupongezwa kwa fedha pale wanapofanya kazi nzuri. Angalia njia nyingine za kuwaonesha wana mchango na wanajaliwa kuliko tu fedha.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea MOBILE UNIVERSITY (www.mobileuniversity.ac.tz)

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

ONGEA NA KOCHA; Sehemu Sahihi Unayopaswa Kuwa Kama Una Kiu Ya Kweli Ya Mafanikio.

$
0
0
Habari za leo rafiki yangu?

Karibu sana kwenye mazungumzo yetu ya leo ambapo mimi na wewe tunakwenda kujadili mambo muhimu kuhusu maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Haya ndiyo matarajio ya kila mmoja wetu, na ndiyo yanayotusukuma kufanya kile ambacho tunakifanya. Japo mwisho wa siku, ni wachache wanaofikia matarajio hayo, na hii inatokana na wengi kukosa msingi sahihi wa kuyaendea maisha yao.

Kuna vitu vingi unaweza kuona wengine wanafanya na ukaona ni rahisi sana kufanya, lakini kila ukijaribu kufanya wewe unashindwa. 

Unapowaona wengine wanafurahia kufanya na wanafanya kama sehemu ya maisha yao, unajaribu wewe unashindwa, ndipo unapoweza kupata hisia kwamba huenda wale wanajua kitu ambacho wewe hujui. 

Na nikuambie tu kitu rafiki yangu, hisia zile ni za kweli, ni kweli kwamba wanajua vitu ambavyo wewe hujui, na wanajua misingi ya kuyaendea maisha yao. Wewe unaweza kuona wakifanya, ukajaribu na kushindwa kwa sababu huna msingi.

Leo hii nataka kuongea na wewe kama kweli maisha bora, yenye furaha na mafanikio ndiyo hitaji lako. Kama huna hitaji hilo unaweza usiendelee kusoma kwa sababu hutapata manufaa yoyote.

Ninachokwenda kukuambia leo ni sehemu sahihi ya wewe kuwepo, kama kweli unataka kuishi maisha ya mafanikio, na siyo tu mafanikio ya kawaida, bali yenye furaha kubwa.

SOMA; Maswali Manne (4) Yakujiuliza Ili Uweze Kuongeza Ustawi Wa Biashara Yako.

Kila siku huwa napokea email za aina hii;
“Nina mtaji wa shilingi laki nne, naomba unishauri nifanye biashara gani?”
“Nina watu wa kunisapoti kwa mtaji, lakini sijui biashara gani nikifanya itaniletea faida nzuri.”
“Nataka kuacha kazi na kujiajiri, nimekaa kwenye ajira miaka mingi sioni mbele, tafadhali nishauri njia bora za kufuata.”
“Sina kazi na sina mtaji, nyumbani uwezo ni mdogo, naomba unishauri nawezaje kutoka kimaisha?”

Hayo ni baadhi tu ya maombi ambayo napokea kila siku kutoka kwa wasomaji na marafiki wenzetu ambao wanakuwa wamekwama kwa namna moja au nyingine.

Naweza kuwapenda sana marafiki zangu hawa na kuwaandikia kipi wafanye, lakini nitakuwa sijawasaidia, kwa sababu tatizo lao si ni nini wafanye, bali tatizo lao ni kukosa msingi wa maisha ambao wanaweza kuufuata mpaka wakafanikiwa.

Tatizo siyo kukosa wazo la biashara, bali tatizo ni kukosa mfumo bora wa maisha na kibiashara utakaomwezesha mtu kuanzisha biashara inayomfaa yeye na itakayomletea faida kubwa.

Hivyo njia pekee ambayo naweza kuwasaidia marafiki zangu hawa, ni kuwakaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa ndani ya KISIMA, kila siku tunajifunza hatua bora za kuchukua ili kuimarisha aisha yetu ya mafanikio. Ndani ya KISIMA mafanikio siyo mali na fedha pekee, bali mafanikio ni kwenye maeneo matano muhimu ya maisha yetu.

Na hii ndiyo sababu nasema kama kweli una kiu ya maisha ya mafanikio, basi sehemu sahihi ya wewe kuwepo ni kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye KISIMA, unayajenga yale maisha yanayokufaa wewe. Kwenye KISIMA unakutana na watu mbalimbali, waliopo sehemu mbalimbali na wanaojua ni wapi wanakwenda na watafikaje pale.

Nitumie nafasi hii kukukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA kama bado hujawa mwanachama. Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kila siku ni kujifunza, kila siku ni kupiga hatua.

SOMA; Una Mtaji Lakini Hujui Ni Biashara Gani Ufanye? Soma Hapa Kujua.

Na misingi yetu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni hii. NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA. Kwenye kila jambo tunalofanya kwenye maisha yetu, misingi hiyo mitatu inatuongoza. Hii ni misingi muhimu sana kwa mafanikio yetu.

Mwaka huu 2017 tuna maneno matatu yanayotuongoza kwenye maisha yetu ya mafanikio. 

Maneno hayo ni KUTHUBUTU, USHINDI NA SHUKRANI. Ni maneno matatu rahisi kutamka lakini yana uzito mkubwa sana kwenye maisha yetu. Kwa kuzingatia maneno hayo matatu kila siku, na kutumia misingi mitatu ya maisha, chochote unachofanya, lazima utafanikiwa. 

Utaacha kuuliza nifanye nini ili kufanikiwa na utaanza kuchukua hatua kwa kila kinachokuzunguka.

Nawezaje kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA?

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA basi utaratibu wa kujiunga uko hivi; unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh elfu 50 (50,000/=) ada hii inaisha pale mwaka unapoisha , tangu siku uliyojiunga. Kwa ada hii kila siku utajifunza kupitia makala na shuhuda za wengine. Pia utapata mafunzo mbalimbali ya semina kwa njia ya mtandao. Na muhimu zaidi, inakuwa rahisi kwako kuwasiliana na mimi moja kwa moja, kwa changamoto yoyote unayokutana nayo.

Kujiunga, tuma ada yako tsh 50,000/= kwa TIGO PESA 0717 396 253 au MPESA 0755 953 887 Kisha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako na utaunganishwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Karibu sana rafiki, tusafiri pamoja kwenye safari hii ya mafanikio.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

USHAURI; Ndugu Zako Wanavyotumia Mafanikio Yako Kukuadhibu, Na Jinsi Ya Kuepuka Hilo.

$
0
0
Habari za leo rafiki?

Katibu kwenye makala yetu ya ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Kupitia makala hizi tunashirikishana hatua mbalimbali za kuchukua kwa changamoto tunazokutana nazo kwenye maisha yetu.

Leo tunakwenda kuangalia changamoto ya watu kutumia mafanikio yako kukuadhibu. Yaani iko hivi, pale inapotokea wewe umefanikiwa kuliko wale wanaokuzunguka, hasa ndugu zako, wao wanachukulia kwamba ni jukumu lako wewe kuwapa chochote unachotaka. Na kama usipowapa basi watasema unaringa au huwajali. Kwa kuwa wewe una mafanikio kidogo kuliko wao, wanachofikiria ni kwamba muda wowote unaweza kuwasaidia na hivyo ukiwaambia huwezi wanaona umekataa tu au una roho mbaya.

Hili limekuwa changamoto kwa wengi ambao wamepata nafasi nzuri kidogo na kuzungukwa na watu ambao hawajapata nafasi kama hizo. Kupitia makala hii ya leo tutajifunza hatua sahihi za kuchukua ili kuondokana na changamoto hii na kuweza kufurahia maisha na mafanikio yako, badala ya mafanikio kuwa mzigo kwako.

SOMA; Hatua Za Kuchukua Pale Watu Wako Wa Karibu Wanapokukatisha Tamaa.

Kabla hatujaangalia ni hatua zipi za kuchukua, tupate alivyotuandikia msomaji mwenzetu ambaye anakabiliwa na changamoto hii.

Asante kocha wangu kwa ushauri wako mwingi ambao naona unanifungua kila siku ninapo soma Makala zako, na semina ya siku kumi iliyopita naona imenisaidia sana japo bado napambana.

CHANGAMOTO ZANGU NI KAMA IFUATAVYO:

1 . Wiki iliyopita nilipata changamoto kubwa sana, katika familia yetu tuko saba mimi angalau ndio naonekana kama nina kipato kikubwa kuliko wote, lakini kila mtu ana shughuli zake. nilipokea ombi mmoja anataka 200,000, mwingine 500,000, na mwingine 200,000 hii ni familia moja wote mzazi na watoto wote wanataka pesa wakati watoto ni wafanyakazi na mama ni mfanyabiashara. nikapokea ombi lingine mwingine anaomba 200,000 amlipie ada mtoto baada ya ada yake kumkopea mwingine na mwingine anaomba nimpe kadi yangu ya kura ili apate dhamana wapi sijui. Bahati nzuri sikuwa na pesa yoyote mkononi hivyo sikuweza hata mmoja kumpatia na wote hapo nina wafanyakazi pia. changamoto moja ni kubwa sana katika hao mwenye kuomba kadi yangu ya kupigia kura huwa anapenda kuiga saini yangu kutumia katika vitu vyake na hivyo baada ya kumnyima kadi hakuna mawasiliano tena naye. Nifanye nini kwa huyu ambaye anatumia signature yangu kwenye mambo yake na alitamka yeye mwenyewe, naomba msaada. Je kwa mtindo huo wa wote wanataka niwakopee ningekuwa na pesa ningefanyaje?

2. Mimi ni mfanyakazi lakini ni mwenyeji wa Mbeya kwa sasa nimehamishiwa Mtwara. Changamoto yangu kubwa ni kuwa nina miaka mitano tu ya kazi kwa sasa, nilikuwa nimejipanga kuanzisha bustani kubwa katika shamba la ekari tatu nikitaka nijue matokeo yake kabla sijamaliza muda wangu wa kazi kama inalipa. Kutokana na uhamisho huu naona kabisha siwezi kufanya tena hiyo biashara kwa sababu nilitaka niandae visima katika shamba hilo maana ni sehemu ya maji, pia nizungushie wigo kuzuia watu ambao hawaogopi kuvuna mali ya wenzao. Nifanyeje ili niweze kufanikiwa? NI MIMI MWANAMAFANIKIO, MSAADA WAKO NI MAFANIKIO YANGU UWE NA SIKU NJEMA. Lesther M.

Ndugu Lesther,

Kwenye changamoto ya kwanza, kama ambavyo nimeeleza kwenye utangulizi wa makala hii ya leo, wanachokifanya ndugu zako ni kutaka kukuadhibu kwa mafanikio kidogo uliyonayo. Kwa sababu haiwezekani watu wote hao kutaka fedha kwako kwa wakati mmoja. Hata kama una fedha nyingi kiasi gani, bado huwezi kugawa nyingi kiasi hicho kwa wakati mmoja. Utashindwa kufanya mambo mengine muhimu kwenye maisha.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kufanya Pale Ndugu Zako Wanapokuona Wewe Ni Mbaya(Mchawi) Kwa Sababu Una Mafanikio.

Hata kama wewe ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko wengine wote, bado huwezi kugawa tu kama kila mtu anavyotaka mwenyewe, wewe pia una mahitaji yako muhimu kwa ajili ya kutengeneza uhuru wa kipato ambao utakunufaisha wewe na wengine pia.

Hivyo kama ambavyo tumejifunza kwenye makala zilizopita, ni muhimu uangalie njia bora zaidi ya kuwasaidia hao ndugu zako badala ya kuwapa fedha moja kwa moja. Angalia namna ambavyo unaweza kuwasaidia kutengeneza kipato zaidi ili waache kuwa tegemezi kwako moja kwa moja.

Na uzuri umesema kila mtu ana shughuli zake, basi unaweza kukaa chini na kila mtu na kumshauri njia bora za kuweka akiba na kukuza kipato kupitia shughuli wanazofanya. Kwa sababu unaweza kujikuta wewe unajinyima ili kufanya mambo makubwa, huku wenzako wanajiachia wakijua wakipata shida wewe upo na utawasaidia. Fuatilia hilo la kuwapa elimu zaidi ya namna wanaweza kutunza vipato vyao na kuongeza kipato zaidi.

SOMA; Kuwa Makini Na Fedha Zako, Ni Wewe Pekee Unayeweza Kuzilinda.

Kuhusu hilo la ndugu yako kutaka kitambulisho chako na kuiga sahihi yako ni jambo la ajabu sana nasikia kutoka kwako. Na kwa hili nazidi kupata picha kwamba ndugu zako hao wanatumia mafanikio yako kukuadhibu. Yaani wanachofanya ni wao kutaka chochote wanachotaka kwako na ukiwanyima basi unaringa au una roho mbaya kwa sababu umefanikiwa na hutaki wao wafanikiwe.

Sasa naomba nikuambie jambo moja, haijalishi watakuona una roho mbaya kiasi gani, haijalishi watakuona huwajali kiasi gani, kamwe usiruhusu mtu kutumia utambulisho wako kwa kitu chochote kile, hata kama ni kitu kizuri. Kama ana shida na utambulisho msaidie atengeneze utambulisho wake mwenyewe. Yaani kama ni kitambulisho hana, msaidie apate kitambulisho hata kama ni leseni ya udereva. Lakini kamwe usiruhusu mtu atumie kitambulisho chako kwa jambo lolote lile, hata kama unamwamini kiasi gani, kitambulisho ni chako wewe, lolote litakalotokea iwe ni kwa bahati mbaya, litakuhusu wewe moja kwa moja. Usikubali kabisa kuendekeza hilo, litakuja kukuingiza kwenye matatizo makubwa. Huyo ndugu yako anaweza kwenda kuomba mkopo mahali kwa jina lako, ukashangaa unakuja kukamatwa wewe ulipe mkopo.

Na kuhusu yeye kutumia sahihi yako, hilo nalo lifanyie kazi. Kwanza kaa naye chini yeye kumweleza ya kwamba aache kutumia sahihi yako, kwa sababu siyo vizuri na ni kosa kisheria. 

Kama ataamua kuendelea kutumia, basi chukua hatua zaidi, unaweza kulifikisha kwa wazee wa familia au ukoo na ukiona huko hupati msaada basi chukua hatua za kisheria. Wakati unafuatilia hilo hakikisha mtu huyo hapati picha zako kwa namna yoyote ile, maana anaweza kupata picha zako na kwenda kuchukua mkopo kwa jina lako au kufanya jambo jingine lolote ambalo litakuumiza wewe.

Kuhusu changamoto ya pili ya wewe kuhamishwa eneo la kazi na hivyo kushindwa kuendelea na mradi uliopanga kufanya mwanzo, huna namna inabidi uache mradi huo kwa sasa na kuangalia mradi mwingine unaoweza kufanya kwa lile eneo unalofanya kazi kwa sasa. Kwa sababu itakuwa vigumu sana kwako kuanzisha mradi mpya huku wewe ukiwa mbali na mradi huo. Kujaribu kufanya hivyo inaweza kukuingiza kwenye hasara kubwa.

Angalia kwa eneo ulilopo sasa, ni mradi gani unaweza kufanya, na anza kuufanya mapema kabla tena mabadiliko hayajatokea. Pia hilo lililotokea liwe msukumo kwako wa kuchukua hatua haraka ili kuondoka kwenye ajira. Kwa sababu ni jambo la kuumiza pale ambapo umeshaweka mipango ya maisha yako ya unataka uishi wapi na ufanye nini, na unalazimika kuacha yote hayo kwa sababu ya ajira.

Ile mipango yako ya mwanzo usiiue kabisa, bali isimamishe kwa sasa, tumia nafasi uliyopo sasa kuanza kitu kingine upya, kitakachowezekana kwa sasa, halafu baadaye ukishanunua uhuru wako, unaweza kurudi kwenye mipango yako ya awali. Usipoteze muda kufikiria mipango yako ya mwanzo, angalia sasa unaweza kuchukua hatua gani na chukua hatua hiyo.

Fanyia kazi haya ambayo tumeshauriana hapa, ili uweze kushika hatamu ya maisha yako na kufikia yale mafanikio ambayo unayaangalia.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE
Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kama ungependa kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwangu kuhusiana na changamoto yako bonyeza maandishi haya na utapata utaratibu wa kupata ushauri kutoka kwangu. Karibu sana rafiki tufanye kazi kwa pamoja.

Kupata vitabu vya mafanikio kwenye Kazi, Biashara Na Maisha kwa ujumla tembelea MOBILE UNIVERSITY, bonyeza hayo maandishi.
Viewing all 1010 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>